Monday, 17 April 2023

MSEVENI AKAMATWA TUHUMA ZA KUMBAKA MTOTO WAKE AKIMLEWESHA KWA POMBE NA CHIPSI


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa Aprili 7,2023. 

Na Salvatory Ntandu - Kahama 

Mkazi wa mtaa wa Nyasubi wilayani Kahama mkoani Shinyanga Mseveni Mchele (35-40) anashikiliwa na jeshi la Polisi kwa tuhuma ya kumbaka mtoto wake wa kufikia mwenye umri wa miaka 12 Mwanafunzi darasa la saba shule ya Msingi Nyasubi.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi amethibitisha kukamatwa kwa Mseveni na kudai kuwa Jeshi la Polisi wanaendelea na upelelezi wakikamilisha atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.

Alisema kuwa kitendo alichokifanya Mchele ni kiyume na maadili ya Kitanzania kwani haiwezekani baba kumbaka mwanae hata kama hajamzaa,na kuwataka wazazi na walezi kutokengeuka na badala yake watimize wajibu wao katika Malezi bora ya Watoto.

“Katika hili jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga hatutakuwa na mhali kwa mtuhumiwa kwani kitendo alichonya sio cha kiungwana haiwezekani baba kubaka mwanae tutahakikisha hatua kali za kisheria zinachukuliwa kwake ili iwefundisho kwa watu wengine,’alisema Magomi.

Naye Afisa ustawi wa jamii Manispaa ya Kahama Abrahaman Nuru alisema kuwa baada ya Mseveni kukamatwa walilazimika kumpeleka hospitali mwanafunzi huyo kwa ajili ya vipimo ambapo daktari alibainisha kuingiliwa.

“Mseveni baada ya maafisa Ustawi kumkamata alikiri kutenda kosa hilo kwa madai kuwa ulevi ndio umemsababishia kufanya kosa jambo lililosababisha kumpeleka kituo cha polisi Kahama kwa taratibu za kisheria,”alisema Nuru.

Kwa upande wake Mhanga wa tukio hilo ambaye jina lake limehifadhiwa alikiri kubakwa na baba yake wa kambo kwani alikuwa anamletea Chipsi na Kimiminika cheupe chenye asili ya Kilevi ambacho alikuwa anamlazimisha kunywa kwa madai kuwa ni dawa ya kutibu ugonjwa wa UTI.

“Wiki mbili zimepita baada ya Mama yangu kusafiri kwenda mkoani Morogoro kwenye matibabu baba amekuwa akinipa vimiminika hivyo na kujikuta nimelewa na nipo chumbani kwake nikiwa nimevuliwa nguo,”alisema Mhanga wa ukatili.

Hata hivyo Mama mkubwa wa Mhanga wa ukatili huo ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema kuwa taarifa za kubakwa kwa binti huyo zilitolewa na majirani zake baada ya kusikia kelele usiku za mwanae kufanyiwa ukatili huo na baba yake wa kambo ndipo walipotoa taarifa kwa ustawi wa jamii Kahama.

“Kwa sasa nimemchukua mwanangu wakati tunamsubiraia mama yake atoke kwenye matibabu mkoani Morogoro,kitendo alichokifanya baba yake wa kambo hakifai na tunaiomba serikali ichukue hatua kali za kisheria ili iwe fundisho kwa wazazi wanaowafanyia ukatili watoto wao,”alisema Mama mkubwa mhanga wa ukatili.
Share:

TANROADS KUPITIA WAKANDARASI WAZAWA, YAKAMILISHA UJENZI WA BARABARA KWA KIWANGO CHA LAMI RUDEWA-KILOSA (KM 24)


Na Mwandishi Wetu, Morogoro 

Mradi wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami Dumila-Kilosa-Mikumi sehemu ya LUDEWA-KILOSA yenye urefu wa kilometa 24 umefikia asilimia 90 ambapo mradi huo unatarajiwa kukamilika Julai, mwaka huu.

Kazi iliyobakia ni ujenzi wa madaraja matatu huku ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami ikiwa imekamilika na kuendelea kutumika.

Hayo yamesemwa Aprili 16, 2023 na Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Morogoro Mhandisi Mussa Kaswahili akitembelea miradi ya Ludewa-Kilosa na daraja la Kiyegeya lililopo wilayani Gairo ambapo amesema barabara hiyo ni sehemu ya barabara ya mkoa huo ambayo inaanzia Dumila hadi Mikumi.

Mhandisi Kaswahili ameongeza kuwa, hapo awali watumiaji wa barabara hiyo walikuwa wanatumia muda mrefu barabarani hadi kufika wakitokea Dumila kwenda Rudewa au Kilosa kutokana na ubovu wa barabara iliyokuwepo.

"Hapo awali kabla ya ujenzi wa barabara ya Dumila hadi Kilosa, ilikuwa kutoka Dumila hadi Ludewa ilikuwa ni masaa matatu lakini kwa sasa ni takribani dakika 40 tu unakuwa umefika" alisema Mhandisi Kaswahili.

Mhandisi Kaswahili ameendelea kwa kusema kuwa, mradi wa Ludewa-Kilosa ulibuniwa ili kuwajengea uwezo wakandarasi wazawa katika kuongeza ushiriki wako kwenye miradi ya ujenzi wa miundombinu.


"Mradi wa Ludewa-Kilosa ulibuniwa ili kuwajengea uwezo wakandarasi wazawa, katika mradi kuna wakandarasi 7 walioungana na kuunda Umoja Kilosa JV lengo ni kutumia wakandarasi wazawa badala ya kutumia wakandarasi wa kigeni hapo baadaye" alisisitiza Mhandisi Kaswahili

Wakiongea kwa nyakati tofauti, Meneja wa mradi LUDEWA-KILOSA kutoka kampuni ya ushauri ya Pidael JV Consulting Engineers Mhandisi Protas Mwasyoke na msimamizi wa mradi upande mkandarasi, Mhandisi Leons Msoka wamesema kwa mwenendo wa kazi za ujenzi zinavyoendelea na kwa kazi ikiyobakia ya ujenzi wa madaraja matatu, kazi hiyo itakamilika kwa wakati mwezi Julai, mwaka huu.

Akiwa katika daraja jipya la Kiyegeya wilayani Gairo, Mhandisi Kaswahili emeeleza kuwa, daraja hilo limejengwa kwa viwango na teknolojka ya kisasa na kumaliza kabisa changamoto iliyokuwa ikitokea hapo zamani hususan nyakati za mvua na hata kupelekaa daraja la zamani kubomoka na kuathiri shughuli za usafiri na usafirishaji.

Kufuatia hatua hiyo, serikali iliiingia katika mpango wa dharura na kutenga fedha haraka kwa ajili ili kujenga daraja jipya la Kiyegeya chini ya usimamizi wa Kitengo cha wahandisi washauri wa TANROADS Mkoa wa kwa kushirikiana na TANROADS makao makuu.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa daraja la kisasa la Kiyegeya Mhandisi Kaswahili amesema,

"Ujenzi wa daraja la Kiyegeya limegharimu kiasi cha shilingi bilioni 6.9 ambao mradi wa ujenzi wa daraja hilo ulikamilika Februari 28, 22022 na linatumika kwa asilimia 100 na kuongeza kuwa

"Nipende kuishukuru serikali ya awamu sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutenga na kuleta fedha ili miradi ya kimkakati ikiwemo mradi huu (ujenzi wa daraja la Kiyegea) iweze kutekelezwa na kufungua shughuli za uchumi za nchi na kwa mwananchi mmoja mmoja"

Mkoa wa Morogoro una madaraja takriban 2,029 huku mtandao wa barabara ukiwa takriban kilometa 2070. Serikali inaendelea kutenga fedha ili kuhakikisha barabara hizo zinahudumiwa ili kuweza kuhakikisha kwamba zinapitika muda wote na majira yote ya mwaka.
Share:

KANISA LA MLIMA WA MOTO WAENDELEZA MAONO YA HAYATI DK. RWAKATARE UAMSHO WA NDOA

Bishop Rose Mgeta akizungumza kwenye kongamano la uamsho wa ndoa lililoandaliwa na Kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni A jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Wagenimbalimbali wakijipatia chakula kwenye kongamano la uamsho wa ndoa lililoandaliwa na Kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni A jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki
Mchungaji aliyejipatia umaarufu kwenye mitandao ya kijamii, Richard Hananja akifuatilia mambo kwenye kongamano la uamsho wa ndoa lililoandaliwa na Kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni A jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki
Dk. Rose Rwakatare ambaye ni mtoto wa Mwanzilishi wa Kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni A jijini Dar es Salaam akifuatilia mambo kwenye kongamano la uamsho wa ndoa lililoandaliwa na Kanisa la Mlima wa Moto.
Washiriki mbalimbali wakifuatilia mambo kwenye kongamano la uamsho wa ndoa lililoandaliwa na Kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni A jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Askofu Danstan Maboya akifanya maombi kwenye kongamano la uamsho wa ndoa lililoandaliwa na Kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni A jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Wageni waalikwa wakifuatilia kwenye kongamano la uamsho wa ndoa lililoandaliwa na Kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni A jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki


*****************

Na Mwandishi Wetu

ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Mlima wa Moto, Mikocheni jijini Dar es Salaam, Bishop Rose Mgeta amesema Kanisa hilo litaendelea kutekeleza maono ya Mwanzilishi wa Kanisa hilo, Hayati Askofu Dk Getrude Rwakatare kutimiza maono yake kama kuendeleza makongamano ya uamsho wa ndoa kila mwaka.

Hayati Dk. Getrude Rwakatare alianzisha kongamano la uamsho wa ndoa mwaka 2000 kwa lengo la kuhakikisha anaokoa ndoa nyingi baada ya kuona ndoa nyingi zikiingia kwenye mogogoro na kusababisha watoto wengi kuachwa mitaani.

Kongamano hilo lilifanyika mwishoni mwa wiki na Maaskofu waliohudhuria hafla hiyo ni Rose Mgeta wa Mlima wa moto, Dastan Maboya, Richard Hananja, Daniel Mgogo,

Askofu Rose alisema kupitia tukio la uamsho wa ndoa, ndoa nyingi zimepona kutokana na shuduma mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na watu waliokuwa wanahudhuria makongamano hayo.

Alisema hata watoto wa hayati Getrude Rwakatare wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha ndoto za mwanzilishi wa Kanisa hilo zinatimizwa.

Mtoto wa Hayati Dr Getrude Rwakatare, Dk. Rose Rwakatare, ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, alisema kongamano la uamsho wa ndoa ilianzishwa mwaka 2,000 kupitia maono ya mwanzilishi wa Kanisa la Mlima wa Moto, Hayati Getrude Rwakatare.

Alisema kutokana na huduma kubwa ambayo Mungu alimkirimia kuhudumia waumini wa Kanisa na katika huduma zote Mungu alizomwitia katika ndoa alitilia mkazo watu kupendana na kuheshimiana na ndipo akaanzisha uamsho wa ndoa.

“Askofu Rwakatare alipenda wanandoa waishi kwa upendo ili ndoa ziweze kudumu na kuwa bora na zilizojaa amani na utulivu kwani hapo ndipo afya ya akili inapokuwepo na kuwa na familia bora,” alisema

Dk. Rose alisema kwa kushirikiana na wazee wa Kanisa hilo na askofu wa kanisa hilo, Askofu Rose Mgeta wamefanikisha kuendeleza tukio la uamsho wa ndoa kwa miaka yote na kwamba wamekusanyika kufanya uamsho wa ndoa ili ziweze kupata uamsho na ndoa ziweze kupona na kuwapa amani ya moyo wana ndoa.

“Kuwa na ndoa yenye masilikilizano inawezekana, Biblia inasema utaacha wazazi wako utaambanana na mwenzako na mtakuwa mwili mmoja sasa mwanaume asimame kwenye nafasi yake na mwanamke naye asimame kwenye nafasi yake kama mama na hapo mtayashinda majaribu yote,” alisma

“Jambo hili linasaidia kuwakumbusha wanandoa kuhusu mambo ambayo yako kinyume na mila na desturi za kitanzania kama mambo ya kuiga yanayoleta mmomonyoko wa maadili kwenye taifa, mfano ukatili wa majumbani unaosabaaisha vifo, kila kukicha unasikia huyu kampiga risasi mwenzake, huku kamchinja mwenzake haya hayakubaliki,” alisema

Aidha, Dk. Rose alisema wimbi jipya linaitesa dunia ni ndoa za jinsia moja na yeye kama Mwenyekiti wa Wazazi Mkoa wa Morogoro amekuwa mstari wa mbele kupinga vitendo hivyo kwani havitaleta mustakabali mwema kwa taifa la Tanzania.

“Tumuunge mkono Rais wetu Samia Suluhu Hassan, hili ni pepo ambalo tunapaswa kulikemea kwa nguvu zetu zote, tunapaswa kusali kwa bidii ili liondoke, kama majanga mengine ambayo tulipiga magoti yakaondoka hili nalo kwanini tusiombe likaondoka, wazazi tusimame kwa umoja wetu kupinga jambo hili, “ alisema

Kwa upande wake, Askofu Daniel Mgogo alisema amekuwa akitoa mafundisho mbalimbali ya ndoa kwenye mitandao ya kijamii lakini kwa muda wa miezi sita hakuandika chochote kwani alikwua nchini Marekani.

“Kumbe yale mafundisho yangu mnayapenda kwasababu nimekuta watu wengi wameniandikia kwenye mitandao yangu ya kijamii kwamba mbona hatuyaoni, lakini kwenye uamsho wa ndoa sitapiga nondo,” alisema

“Katika viumbe ambavyo vinahitaji ustadi wa hali ya juu kukaa navyo ni binadamu, kukaaa na kiumbe kinaitwa binadamu ni kazi kubwa sana hata wachungaji kuchunga watu wanaitwa binadamu mwaka mzima ni kazi kubwa sana na inabidi ukifikisha mwaka upate muda wa kupumzika maana ni kazi kubwa,” alisema
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU APRILI 17,2023


Magazetini leo Jumatatu April 17 2023






Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger