Monday, 17 April 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU APRILI 17,2023


Magazetini leo Jumatatu April 17 2023






Share:

Sunday, 16 April 2023

WAZIRI MKUU ATAKA VIONGOZI WA DINI KUSIMAMIA HAKI NA KUTUNZA AMANI

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza kwa niaba ya Waziri Mkuu Kasim Majaliwa wakati wa ibada ya Harambee ya ujenzi wa shule ya Kanisa la Kiinjili la Kikutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki Ziwa Victoria-Mwanza iliyofanyika kanisani hapo mkoani Mwanza tarehe 16 April 2023
Sehemu ya waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKT) Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria- Mwanza wakiwa katika ibada ya Harambee ya ujenzi wa shule ya Kanisa la KKKT Dayosisi ya Mashariki Ziwa Victoria-Mwanza iliyofanyika katika Kanisa hilo Ilemela mkoani Mwanza tarehe 16 April 2023.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akipokea zawadi ya picha kwa niaba ya Waziri Mkuu Kasim Majaliwa wakati wa ibada ya Harambee ya ujenzi wa shule ya Kanisa la Kiinjili la Kikutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki Ziwa Victoria-Mwanza iliyofanyika kanisani hapo wilayani Ilemema mkoani Mwanza tarehe 16 April 2023.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Mashariki ya Ziwa Victoria- Mwanza Andrew Petro Gulle akizumgumza katika ibada ya Harambee ya ujenzi wa shule ya Kanisa la KKKT Dayosisi ya Mashariki Ziwa Victoria-Mwanza iliyofanyika katika Kanisa hilo katika manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza tarehe 16 April 2023.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiwaongoza waumini katika Harambee ya kuchangia ujenzi wa shule ya Kanisa la Kiinjili la Kikutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki Ziwa Victoria-Mwanza iliyofanyika kanisani hapo mkoani Mwanza tarehe 16 April 2023.
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Karagwe mkoani Kagera Askofu Dkt Benson Bagonza akizungumza mara baada ya kuchangia Harambee ya ujenzi wa shule ya Kanisa la KKKT Dayosisi ya Mashariki Ziwa Victoria- Mwamza tarehe 16 April 2023.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akionesha saa iliyotolewa na Waziri Mkuu Kasim Majaliwa kwa ajili ya kunadiwa ambapo saa hiyo ilinunuliwa kwa shilingi milioni 2.625 wakati wa Harambee ya ujenzi wa shule ya Kanisa la KKKT Dayosisi ya Mashariki Ziwa Victoria- Mwanza tarehe 16 April 2023.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiwa na viongozi wengine wakitoka katika ibada ya Harambee ya ujenzi wa shule ya Kanisa la KKKT Dayosisi ya Mashariki Ziwa Victoria- Mwanza tarehe 16 April 2023.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Mashariki ya Ziwa Victoria- Mwanza Andrew Petro Gulle akihitimisha Harambee ya ujenzi wa shule ya Kanisa la KKKT Dayosisi ya Mashariki Ziwa Victoria-Mwanza iliyofanyika katika Kanisa hilo katika manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza tarehe 16 April 2023.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiwa katika picha ya pamoja na kamati ya ujenzi wa shule wakati wa ibada ya Harambee ya ujenzi wa shule ya Kanisa la KKKT Dayosisi ya Mashariki Ziwa Victoria- Mwanza tarehe 16 April 2023. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)

******************


Na Munir Shemweta, WANMM MWANZA

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kasim Majaliwa amewataka viongozi wa dini nchini kuhakikisha wasimamia haki na kuienzi na kusimamia amani kwa manufaa ya wananchi wa sasa na vizazi vijavyo.


"Niwasihi sana ninyi viongozi wetu wa dini kutukumbusha mara kwa mara sisi, waumini na watu wote kuhusu umuhimu wa kusimamia haki na kudumisha amani na kuiombea nchi yetu na viongozi wake" alisema Majaliwa.


Majaliwa alisema hayo leo tarehe 16 April 2023 katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula wakati wa Ibada ya Harambee ya Ujenzi wa shule ya Kanisa la Kiinjili la Kikutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki Ziwa Victoria-Mwanza iliyofanyika katika Kanisa la KKKT Imani wilayani Ilemela mkoani Mwanza.


kupitia harambee hiyo ya ujenzi wa shule ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki ya Ziwa Victoria-Mwanza Kanisa hilo limefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi 119,563,000 zikiwemo fedha taslimu, ahadi na vifaa.


Kupitia hotuba yake Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewataka viongozi wa dini nchini kutochoka kufundisha na kulea vijana katika maadili mema na kuthamini kufanya kazi halali.


" Katika nyakati hizi ni ukweli ulio wazi kuwa kuna mmomonyoko mkubwa wa maadili katika jamii yeru, vitendo viouvu na mambo yasiyopendeza mwenyezi Mungu yanazidi kuongezeka mambo ambayo siku za nyuma yalikuwa nadra sana kutokea au kusikia lakini sasa yanakuwa habari za kila siku na wakati mwingine huonekana eti ya kawaida" alisema majialiwa kupitia hotuba yake.


Kwa mujibu wa Waziri Mkuu, kushuka kwa maadili ni jambo lenye athari mbaya kwa jamii na taifa kwa ujumla hivyo kunachangia sana na kurudisha nyuma juhudi za kujiletea maendeleo na kuifanya kazi ya kuondoa umasikini kuwa ngumu.


Amesema, anaamini kwa dhati kuwa viongozi wa serikali, dini na vyama vya siasa wakishika mafundisho ya dini na kuwa na hofu ya mungu maovu mengi yatapungua na nchi kuoongozwa vizuri.


" Naendelea kuwaomba kwa niaba ya serikali, viongozi wa dini zetu zote tusaidiane kukea taifa letu kimaadili na tuweke mkazo zaidi kwa vijana kwa sababu kwanza wao ndiyo wahanga wakuu wa maovu yanayotendeka lakini pia wao ni taifa la leo na viongozi wa kesho" alisema


Kupitia hotuba yake hiyo, Majaliwa alisisitizia pia suala la elimu na kueleza kuwa elimu ni muhimu kwa maendeleo ya taifa lolote na kutaka viongozi wa dini kusaidia kuzungumza na wazazi na kuwaslimisha kuhusu umuhimu wa kusomesha watoto.


Amelipongeza Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki ya Ziwa Victoria -Mwanza na waumini kwa ujumla kwa kujitoa kwa hali na mali kwa kufanya kazi ya Mungu kwa kuhakikisha jengo linakamilikia hasa ikizingatiwa fedha zote ni michango ya waumini na kubainisha kuwa, kitendo kilichofanyika ni chema na kinaleta baraka zote.


Awali Askofu Mkuu wa KKKT Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria- Mwanza Andrew Petro Gulle alisema ujenzi wa shule ya kanisa hilo unakadiriwa kuwa na gharama ya Shilingi 2,350,000,000 ambapo amesema mpaka sasa kiasi cha 430,000,000 kimetumika kujenga boma la madarasa kumi na boma la jingo la utawala.


Katika harambee hiyo ya ujenzi wa shule Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alichangia shilingi milioni 5 ili kutumika kukamilisha kazi ya ujenzi wa shule huku Dkt Mabula kuchangia milioni 2 katika ujenzi huo.

Share:

UJENZI WA BARABARA YA MIKUMI - IFAKARA WAFIKIA 78%, MIRADI MINGINE MITANO KUJENGWA MOROGORO





Wakati ujenzi wa barabara ya Mikumi hadi Ifakara kwa kiwango cha Lami ukifikia asilimia 78, miradi mingine mitano ya barabara inatarajiwa kujengwa mkoani Morogoro.


Akizungumza na waandishi, Meneja wa Wakala wa Barabara (Tanroads) mkoa wa Morogoro, Alinanuswe Kyamba amesema ujenzi wa barabara hiyo unaohusisha pia ujenzi daraja la Ruaha Mkuu unatarajiwa kukamilika Oktoba mwaka huu.


"Hadi kufikia Aprili 2023, utekelezaji wa mradi kwa ujumla ulikuwa umefikia asilimia 78, kwa sasa Mkandarasi amekamilisha km 43 za lami na kazi zingine zinaendelea kwa hatua nzuri. Madaraja yote yameshakamilika kwa asilimia 83 na daraja la Ruaha mkuu bado kitako cha juu kukamilika," amesema.


Amesema kukamilika kwa daraja la Ruaha Mkuu kutafanya magari mawili kupita kwa wakati mmoja tofauti zamani.


Amesema wa mradi huo ulianza mwaka 2018 lakini changamoto mbalimbali ikiwemo mvua umetajwa kuwa sababu ya kuchelewa kukamilika kwa mradi huo.


"Pia Mlipuko wa homa ya Mapafu (COVID -19) ilichangia kuwapo kwa ucheleweshwaji wa uangizaji wabaadhi ya vitendea kazi kwa ajili ya mradi.

Mbali na barabara hiyo pia mkoa wa Morogoro unakwenda kutekeleza miradi mingine mitano ambayo itakwenda kuunganisha wilaya zote kwa kiwango cha lami na kuinua uchumiwa Wananchi wa maeneo hayo.


Kwa mujibu wa Kyanda miradi yote imekwishatangazwa zabuni na iko katika hatua za mwisho ili kuweza kusaini mikataba


Miradi hiyo ni ule wa barabara ya Ubena Zomozi – Ngerengere (Kizuka Army Camp) yenye urefu wa 11.6km, Mradi wa ujenzi wa barabara ya Ifakara – Kihansi – Mlimba – Taweta – Madeke, Sehemu ya Ifakara – Mbingu, km 62.5.


"Pia kuna Mradi wa ujenzi wa barabara ya Ifakara – Kihansi – Mlimba – Taweta – Madeke, Sehemu ya Mbingu – Chita JKT, yenye urefu wa Km 37.5.


Mradi mwingine alioutaja ni ule wa wa barabara ya Bigwa – Kisaki (sehemu ya Bigwa –Mvuha, km 78, Pamoja na Madaraja ya Ruvu na Mvuha.


"Mradi wa mwisho utakuwa ni wa ujenzi wa barabara ya Ifakara – Lupiro – Mahenge / Lupiro – Malinyi – Kilosa kwa Mpepo – Londo – Lumecha na Malinyi JCT – Malinyi, km 422.54.
Share:

MWONEKANO MPYA NGORONGORO WAVUTIA





•Uoto wa asili, ikolojia vyaanza kurudi kwa kasi katika maeneo yaliyohamwa na wakazi •Matumaini yazidi kuwa makubwa,

•Wadau watoa Ushauri

Baada ya baadhi ya wakazi wa maeneo ya Ngorongoro kuhamia Msomera Mkoani Tanga, Ikolojia na uoto wa asili vimenza kuejea kwa katika maeneo waliyobomoa makazi yao jambo linaloonyesha tija kubwa ya zoezi la Uhamaji Kwa hiyari

Wanahabari na wadau wa Kituo cha wanahabari watetezi wa Rasilimali na Taarifa (Mecira) Veronica Mheta na Dixon Busagaga walijionea mabadiliko makubwa tena ya muda mfupi walipotembelea kwenye baadhi ya zilipokuwa ambazo wamiliki wake waliamua kuhama Kwa hiyari kuhamia Msomera na kwengineko, maeneo hayo ni kwa aliyekuwa Mbunge wa Ngorongoro,Saning'o ole Telele na kwa Foible Lukumay wakazi wa kata ya Enduleni wilayani Ngorongoro na kwengineko katika eneo hilo .

"Kwa macho yangu nilijionea namna eneo hili lilivyokuwa limeathirika. Lakini Leo ninafurahi kuona ikolojia na uoto wa asili vimeanza kurejea kwa kasi kubwa sana" Amenukuliwa Mheta

"Nimeambiwa kuwa hapa pataota hata miti iliyokuweko awali na ikakatwa na wakazi waliokuwa wakiushi Ili kujenga Nyumba na maboma ya mifugo, Kwa kweli kuna tija kubwa sana kwenye zoezi la Uhamaji wa hiyari". Aliongeza Busagaga Miongoni mwa Sababu zilizopelekea wadau wa mazingira na watetezi wa haki za binaadamu kupaza sauti na kuitaka Serikali kutafuta utaratibu mpya wa kufanya Ngorongoro kuwa sehemu Salama kwa ajili ya Wanyama, Mifugo na binaadamu ni pamoja na;-

1.ONGEZEKO KUBWA LA WATU ambapo awali kulikuwa na Watu wasiozidi 8000 lakini sasa hivi wapo zaidi ya watu 120,000

2. ONGEZEKO KUBWA LA MIFUGO ambapo awali ilikuwa chini ya 50,000 lakini sasa hivi imevuka 1.1m

3. Miripuko ya magonjwa Kutokana na kuingiliana kulikopitiliza baina ya wanadamu, Wanyama na mifugo

4. Umasikini uliopitiliza ambapo ni asilimia 3 pekee ndio wanamiliki asilimia 80 ya mifugo yote 1.1m na hivyo kuwafanya wananchi *MANAMBA*

5. Kutokujua kusoma na kuandika ambapo zaidi ya asilimia 63 ya Wananchi wa Ngorongoro *HAWAJUI KUSOMA NA KUANDIKA*

6. Ongezeko kubwa sana la makazi(Nyumba) zisizoruhusiwa kisheria kujengwa hifadhini sambamba na ufungaji wa mitambo, umeme wa sola, nakadharika hivyo kuifanya Serikali kuchukua hatua ya kuruhusu zoezi la Uhamaji wa hiyari kutoka hifadhini humo kwenda Msomera kwa atakayependa na kokote kule atakayetaka mtu anayehama yeye pamoja na mali zake zote ikiwemo mifugo.
Share:

Saturday, 15 April 2023

Video : MBIO ZA BAISKELI NA JESHI LA JADI SUNGUSUNGU WAKITOA BURUDANI KAMPENI YA KATAA UHALIFU, TOA TAARIFA

 

Tazama Video Mbio za Baiskeli na Jeshi la Jadi Sungu wakitoa burudani kwenye Bonanza la Michezo lililoongozwa na Kampeni ya Kataa Uhalifu Toa Taarifa Shinyanga Bila Uhalifu Inawezekana’ katika kata ya Chibe Manispaa ya Shinyanga.

Tazama Mbio za Baiskeli

Tazama Burudani ya Jeshi la Jadi Sungusungu








Share:

BENKI YA CRDB YASHIRIKI KAMPENI YA KATAA UHALIFU TOA TAARIFA..."USIKAE NA PESA NDANI INACHOCHEA UHALIFU, NJOO BENKI"


Meneja Biashara wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Mwanahamisi Iddi akizungumza wakati wa Bonanza la Michezo lililoongozwa na Kampeni ya Kataa Uhalifu Toa Taarifa Shinyanga Bila Uhalifu Inawezekana’ katika kata ya Chibe Manispaa ya Shinyanga.


Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Benki ya CRDB imeshiriki Bonanza la Michezo lililoongozwa na Kampeni ya Kataa Uhalifu Toa Taarifa Shinyanga Bila Uhalifu Inawezekana’ katika kata ya Chibe Manispaa ya Shinyanga huku ikihamasisha wananchi kuacha tabia ya kuhifadhi pesa ndani ya nyumba kwani vitendo hivyo vinachochea uhalifu.

Kampeni hiyo iliyoandaliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kwa Uratibu wa Amos John maarufu MC Mzungu Mweusi imefanyika leo Jumamosi Aprili 15,2023 katika kata ya Chibe kupitia Bonanza la Michezo lililohudhuriwa na mamia ya wananchi ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi.


Meneja Biashara wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Mwanahamisi Iddi amesema Benki ya CRDB inapiga vita masuala ya uhalifu hivyo kuwaomba wananchi kuacha tabia ya kuhifadhi fedha majumbani kwani hicho ni kichocheo cha uhalifu.


"Usikae na pesa ndani ya nyumba kwani kuweka fedha ndani kunachochea uhalifu. Weka pesa zako Benki ili pesa zako ziwe salama lakini pia uwe salama. Njooni Benki ya CRDB mfungue akaunti ili pesa zenu ziwe salama lakini pia tunao mawakala kila mahali. 

CRDB tupo kidijitali zaidi na  tumeongeza wigo kwa wananchi kufanya malipo yao kwa urahisi kupitia SimBanking, SimAccount, Internet banking na CRDB Wakala. karibuni sana",amesema Mwanahamisi.

Meneja Biashara wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Mwanahamisi Iddi akizungumza wakati wa Bonanza la Michezo lililoongozwa na Kampeni ya Kataa Uhalifu Toa Taarifa Shinyanga Bila Uhalifu Inawezekana’ katika kata ya Chibe Manispaa ya Shinyanga.
Meneja Biashara wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Mwanahamisi Iddi akizungumza wakati wa Bonanza la Michezo lililoongozwa na Kampeni ya Kataa Uhalifu Toa Taarifa Shinyanga Bila Uhalifu Inawezekana’ katika kata ya Chibe Manispaa ya Shinyanga.
Bonanza la michezo likiendelea

Mbio za baiskeli zikiendelea kwenye Bonanza la Michezo likiongozwa na Kampeni ya Kataa Uhalifu Toa Taarifa Shinyanga Bila Uhalifu Inawezekana

Bonanza linaendelea
Mshindi Mbio za baiskeli kundi la wanawake Temineta Charles

Soma pia : 


Tazama Mbio za Baiskeli
Tazama Burudani ya Jeshi la Jadi Sungusungu
Share:

UCHUMI WA TANZANIA WAPAA MIAKA MIWILI YA RAIS SAMIA - IMF


* Pato la Taifa lafikia Sh. trilioni 200 kwa mwaka 2023 kutoka Sh. trilioni 163 ya mwaka 2021

* Uchumi wa Tanzania sasa ni mkubwa kuliko baadhi ya nchi za Ulaya na ni wa 6 kwa ukubwa kwa nchi zote za Kusini mwa Jangwa la Sahara

* IMF yabashiri Pato la Taifa la Tanzania kufikia karibu Sh. trilioni 300 ndani ya miaka mitano ijayo
 

TAKWIMU mpya za Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) zinaonesha kuwa Pato la Taifa la Tanzania kwa bei ya sasa limeongezeka hadi kufikia Dola za Marekani Bilioni 85.42 (Shilingi trilioni 200) kwa mwaka huu wa 2023, ikiwa ni ishara kuwa sera za uchumi za Rais Samia Suluhu Hassan zinaleta mageuzi makubwa nchini.

Ongezeko hilo la Pato la Taifa ni kutoka Dola za Marekani Bilioni 69.9 (Shilingi trilioni 163.5) kwa mwaka 2021, wakati ambapo Rais Samia alipoingia madarakani.

Takwimu hizo za IMF zinaonesha kuwa Pato la Taifa la Tanzania huenda likaongezeka zaidi hadi kufikia Dola za Marekani Bilioni 136.09 (Sh. trilioni 276) ifikapo mwaka 2028.

Tangu alipoingia madarakani Machi 2021, Rais Samia ametekeleza sera rafiki kwa sekta binafsi, ambayo imeongeza kasi ya uwekezaji, biashara na ukuaji wa uchumi nchini.

Kwa mujibu wa takwimu hizo mpya za IMF, Pato la Taifa la Tanzania kwa mwaka 2023 ni kubwa kuliko nchi kadhaa ndogo za Ulaya, ikiwemo Croatia ($78.8 billion), Lithuania ($78.3 billion), Serbia ($73.9 billion) and Slovenia ($68.1 billion).

Kwa upande wa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara, Tanzania ni nchi ya 6 kwa ukubwa wa Pato la Taifa.

Kwa mujibu wa takwimu za IMF, nchi kumi zinazoongoza kwa ukubwa wa Pato la Taifa Kusini mwa Jangwa la Sahara ni hizi zifuatazo:

1. Nigeria $506.6 billion 🇳🇬

2. South Africa $399 billion 🇿🇦

3. Ethiopia $156 billion 🇪🇹

4. Kenya $118.1 billion 🇰🇪

5. Angola $117.8 billion 🇦🇴

6. Tanzania $85.4 billion 🇹🇿

7. Còte d'Ivore $77 billion 🇨🇮 

8. DRC $69.4 billion 🇨🇩

9. Ghana $66.6 billion 🇬🇭

10. Uganda $49.7 billion 🇺🇬

(MWISHO)
Share:

NIDHAMU, KUJITUMA SABABU WANAFUNZI WENGI KUFANYA VIZURI KWENYE MITIHANI.

Mgeni Rasmi katika mahafali ya 13 shule ya Sekondari Isimila iliyopo Mkoani Iringa Bw. Masozi Nyirenda (wa pili kutoka kulia) akiingia ukumbini na msafara wa wahitimu. Kulia ni Mkuu wa Shule Bw. Frank Mahenge na kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shule Dkt. Nasra Habib.
Mgeni Rasmi Masozi Nyirenda (kulia) na Mkuu wa shule Frank Mahenge (kushoto) wakifurahia burudani kutoka kwa wahitimu (hawapo kwenye picha) katika sherehe za mahafali ya 13 ya kidato cha sita shule ya Sekondari Isimila iliyopo mkoani Iringa.
Mgeni Rasmi Masozi Nyirenda (katikati) akipokea nakala ya risala kutoka kwa wahitimu wakati wa mahafali ya 13 ya kidato cha sita shule ya Sekondari Isimila mkoani Iringa. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya shule Dkt. Nasra Habib na kushoto ni Mkuu wa Shule Frank Mahenge.
Wahitimu wakidato cha Sita wakisoma risala mbele ya Mgeni Rasmi (hayupo pichani) katika sherehe za mahafali ya 13 ya kidato cha sita shule ya sekondari Isimila mkoani Iringa.
Mkuu wa Shule Bw. Frank Mahenge akielezea historia ya shule wakati wa mahafali ya 13 ya kidato cha sita shule ya Sekondari Isimila Mkoani Iringa. Waliokaa ni Mgeni Rasmi Masozi Nyirenda na Mwenyekiti wa Bodi ya Shule Dkt. Nasra Habib.
Mgeni Rasmi Bw. Masozi Nyirenda akisisitiza jambo katika sherehe za mahafali ya 13 ya kidato cha sita shule ya Sekondari Isimila Mkoani Iringa. Waliokaa ni Mkuu wa shule Frank Mahenge na mdau wa shule Dkt. Ave Maria Semakafu.
Mgeni Rasmi Masozi Nyirenda akitoa vyeti kwa wahitimu wa kidato cha sita Shule ya Sekondari Isimila mkoani Iringa katika mahafali ya 13 shuleni hapo.

*************************

Na MWANDISHI WETU.

WANAFUNZI wengi wanaomaliza masomo yao ya Sekondari na kufanya vizuri sababu imetajwa kuwa ni bidii ya kujituma katika kufikia ndoto zao lakini pia nidhamu ya kujali muda na kusimamia malengo waliyojiwekea kwenye masomo yao.

Hayo yametajwa katika sherehe za mahafali ya 13 ya kidato cha sita Shule ya Sekondari Isimila mkoani Iringa wakati wa hafla iliyofanyika jana shuleni hapo ambapo mgeni rasmi alikuwa Meneja Miradi kutoka Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bw. Masozi Nyirenda akimuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo.

Awali akielezea historia ya shule hiyo Mkuu wa shule Bw. Frank Mahenge alisema, shule ina wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha sita na jumla ya wanafunzi 1,178 wasichana wakiwa ni 835 na wavulana 343 huku kidato cha tano na sita wakiwa ni wasichana pekee.

Amesema, shule hiyo imekuwa ikifanya vizuri kwenye mitihani ya mwisho ya Taifa na kwamba kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo 2020 - 2022 shule imekuwa ikifaulisha kwa asilimia 100 daraja la kwanza hadi la tatu hivyo kuwafanya wanafunzi wengi kutamani kusoma katika shule hiyo.

"Shule yetu inafanya vizuri kwenye matokeo ya mwisho hivyo kuvutia wanafunzi kuomba nafasi za kujiunga na hii imepelekea tuwe na upungufu wa miundombinu ya kujifunzia na kufundishia kama vile mashine ya kurudufu, maktaba kwa ajili ya kujisomea, jengo la utawala, nyumba za walimu pamoja na bwalo, alisema Mahenge’’

Nao wahitimu wa kidato cha Sita katika risala yao walisema, wanajivunia kuwa sehemu ya familia ya shule ya sekondari Isimila kutokana na misingi, mikakati na malengo ya shule hiyo ambayo inawawezesha kufanya vizuri na kuifanya shule hiyo kuwa bora.

Mgeni Rasmi katika mahafali hayo Bw. Masozi Nyirenda Meneja Miradi kutoka TEA alisema, inafurahisha kuona kuwa shule ya Sekondari Isimila ni miongoni mwa shule zinazofanya vizuri ambapo matokeo ya miaka mitatu yameonesha hakuna aliyepata ufaulu wa daraja sifuri. Nidhamu na bidii ya masomo imesaidia wanafunzi kufanya vizuri katika mitihani yao ya mwisho.

“Nimefurahishwa kuona namna uongozi wa shule hii unavyoendelea kuweka mikakati ya kuhakikisha wanafunzi wake wanaendelea kupata matokeo mazuri. Miongoni mwa mikakati hiyo ni pamoja na kuongeza vyumba vya madarasa vinne, Ofisi mbili lakini pia kushirikiana na Mkurugenzi wa Halmashauri kutengeneza madawati 130, amesema Nyirenda”

Nyirenda alisema, Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) ilianzishwa kwa lengo la kuratibu uendeshaji wa Mfuko wa Elimu wa Taifa ambao unalenga kusaidia jitihada za Serikali za kuongeza upatikanaji wa Elimu bora na kwa usawa hapa nchini. Kupitia Mfuko huo wa Elimu wa Taifa, ufadhili wa miradi ya Elimu yenye thamani ya Bilioni 1.1 katika Mkoa wa Iringa umetolewa katika kipindi cha miaka mitano kuanzia 2015/2016 hadi 2022/2023

Aidha, aliushauri uongozi wa shule kuwasilisha maombi ya ufadhili kwenye Ofisi za Mamlaka kwa ajili ya upungufu wa miundombinu ili maombi hayo yaweze kufikiriwa kadri ya upatikanaji wa fedha, lakini pia kutumia michango ya wadau wa Elimu ndani ya Halmashauri kwani inaweza kusaidia kupunguza changamoto hizo.

Aliwapongeza wahitimu wote wa kidato cha sita kwa hatua waliyofikia na kuwakumbusha kuwa, mafanikio hayaji pasipo maandalizi hivyo anaamini wamejiandaa vya kutosha na wako tayari kwa mitihani yao ya mwisho ili waweze kuendelea na ngazi nyingine ya Elimu baada ya kuhitimu.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger