Wednesday, 29 March 2023

WAZIRI MABULA AWATAKA WAKURUGENZI KULINDA NA KUSIMAMIA UVAMIZI WA MAENEO YA WAZI


WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk.Angeline Mabula,akizungumza wakati akifungua Mkutano wa nane wa mwaka wa Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipango Miji ulioanza leo Machi 29 hadi 30,2023 jijini Dodoma.


WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk.Angeline Mabula,akisisitiza jambo wa washiriki wa Mkutano wa nane wa mwaka wa Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipango Miji ulioanza leo Machi 29 hadi 30,2023 jijini Dodoma.


KATIBU Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhandisi Anthony Sanga ,akizungumza wakati wa Mkutano wa nane wa mwaka wa Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipango Miji ulioanza leo Machi 29 hadi 30,2023 jijini Dodoma.


MKUU wa Mkoa wa Dodoma Bi.Rosemary Senyamule,akitoa salama za Mkoa wake ka washiriki wa Mkutano wa nane wa mwaka wa Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipango Miji ulioanza leo Machi 29 hadi 30,2023 jijini Dodoma.


Rais wa Chama Cha Wataalam wa Mipangomiji Tanzania, Dk.Juma Matindana,akizungumza wakati wa Mkutano wa nane wa mwaka wa Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipango Miji ulioanza leo Machi 29 hadi 30,2023 jijini Dodoma.


MWENYEKITI wa Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipango Miji Prof.John Lupala,akielezea lengo la Mkutano wa nane wa mwaka wa Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipango Miji ulioanza leo Machi 29 hadi 30,2023 jijini Dodoma.


MSAJILI wa Bodi ya Usajili wa Watalaam wa Mipangomiji, Lucas Mwaisaka,akitoa taarifa ya Mkutano wa nane wa mwaka wa Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipango Miji ulioanza leo Machi 29 hadi 30,2023 jijini Dodoma.


SEHEMU ya Washiriki wakisikiliza hotuba ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk.Angeline Mabula (hayupo pichani) wakati akifungua Mkutano wa nane wa mwaka wa Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipango Miji ulioanza leo Machi 29 hadi 30,2023 jijini Dodoma.


MAKAMU Mwenyekiti wa Bodi Bi.Immakulata Senje,akitoa neno la shukrani kwa niaba ya washiriki mara baada ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk.Angeline Mabula,(hayupo pichani) kufungua Mkutano wa nane wa mwaka wa Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipango Miji ulioanza leo Machi 29 hadi 30,2023 jijini Dodoma.


WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk.Angeline Mabula,akitoa tuzo kwa mshiriki mmoja aliyefanya vizuri mara baada ya kufungua Mkutano wa nane wa mwaka wa Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipango Miji ulioanza leo Machi 29 hadi 30,2023 jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna-DODOMA

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk.Angeline Mabula ,amewaagiza Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za mitaa kupima, kulinda na kusimamia maeneo yote ya umma na maeneo ya wazi ili kuondokana na mwenendo mbaya unaoendelea kukithiri wa kuvamia maeneo hayo.

Agizo hilo amelitoa leo Machi 29,2023 jijini Dodoma wakati akifungua Mkutano wa nane wa mwaka wa Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipango Miji.

Dk.Mabula amesema Wakurugenzi hao wanapaswa kulinda maeneo hayo ili kuondokana na mwenendo mbaya unaoendelea kukithiri wa kuvamia maeneo hayo.

“Umejitokeza utaratibu mbaya na usiovumilika, wa kuvamia maeneo ya wazi, maeneo ya umma pamoja na maeneo hatarishi na kuyabadilisha kuwa ya matumizi mengine, hasa makazi, maeneo hatari kimazingira pamoja na maeneo ya wazi, yakiwemo maeneo maalum kwa matumizi ya baadaye yanapaswa kupimwa, kumilikishwa na kulindwa dhidi ya wavamizi,”amesema Dk.Mabula

Amesema kuwa ili tuwe na mijini nadhifu na iliyopangwa vyema katika nchi yetu hakuna budi kuanza kusimamia upangaji wa miji midogo na vitovu vya vijiji.

"Takwimu za Sensa ya Watu na Makazi 2022 inaonyesha kuwa miji inakuwa kwa asilimia 4.8 na taarifa tulizonazo tuna jumla ya miji midogo inayochipukia 4310 nchini ambayo isiposimamiwa ipasavyo itakuwa miji holela ya baadae," Amesema

Na kuongeza"Kwa kutambua umuhimu wa miji hiyo na uwepo wa kasi ndogo ya upangaji wa vijiji nchini, Wizara imeandaa mwongozo wa upangaji na ujenzi wa nyumba bora vijijini ili kuwezesha jamii yetu kuanza kupanga maeneo yao kuanzia vijijini," amesema waziri Mabula

Aidha ametoa maelekezo kwa Bodi ya Usajili wataalam wa Mipangomiji na wanataaluma wote kuweka mkazo Zaidi katika namna ya kuzuia miji yetu midogo na vijiji kuwa makazi holela yabaadae kwa kusimamia na kuelimisha jamii matumizi ya mwongozo wa upangaji na ujenzi wa nyumba bora vijijini.

Hata hivyo amesema Pia Serikali itaendelea na jukumu lake la kuimarisha mahusiano ya kitaasisi ili kuimarisha maendeleo ya miji pamoja na kupata fedha kwa ajili ya kupanga na kusimamia miji.

''Naelekeza kuwa gharama za kuweza kumudu kupanga, kupima na kumilikisha maeneo yote nchini ni kubwa,Ninaelekeza Mamlaka za Upangaji nchini kutenga fedha kutokana na mapato ya ndani ya kila mwaka, kwa ajili ya kazi ya kupanga,kupima, kumilikisha,kuendeleza na kusimamia miji katika maeneo yao.''amesisitiza Waziri Mabula

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhandisi Anthony Sanga,amesema kuwa sasa ni wakati wa kujikita kwenye TEHAMA ili kurahisisha wananchi kupata huduma kwa haraka na kuondokana na migogoro ya ardhi.

Awali, Msajili wa Bodi ya Usajili wa Watalaam wa Mipangomiji, Lucas Mwaisaka, amesema kuwa watalaam wa mipangomiji 508 wamesajiliwa huku kati yao 36 wamefutiwa usajili kwa kukiuka maadili ya taaluma hiyo.
Share:

PROF. MBARAWA- LIPENI KODI KWA WAKATI

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa akisisitiza jambo kwa Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam, wakati alipozindua nyumba za makazi za watumishi wa umma zilizopo Magomeni Kota na Canadian Village
Msasani Peninsula -Masaki jijini Dar es Salaam.

Naibu Katibu Mkuu Ujenzi, Bw. Ludovick Nduhiye akizungumza na Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam (hawapo pichani), wakati wa uzinduzi wa nyumba
za makazi za watumishi wa umma zilizopo Magomeni Kota na Canadian Village Msasani Peninsula -Masaki jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya Watumishi wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani) wakati alipozindua nyumba za makazi za watumishi wa umma zilizopo
Magomeni Kota na Canadian Village Msasani Peninsula -Masaki jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa akifurahia jambo na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Arch. Daud Kondoro mara ya kuzindua nyumba za makazi za watumishi wa umma zilizopo
Magomeni Kota na Canadian Village Msasani Peninsula -Masaki jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Arch. Daud Kondoro kuhusu ujenzi wa nyumba za makazi za watumishi wa umma zilizopo
Magomeni Kota na Kanadiani Village Msasani Peninsula -Masaki jijini Dar es Salaam, kabla ya Waziri huyo kuzindua nyumba hizo.


Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali na Taasisi za Ujenzi akikata utepe kuashiria uzinduzi wa wa nyumba za makazi za watumishi wa umma zilizopo Magomeni Kota na
Canadian Village Msasani Peninsula -Masaki jijini Dar es Salaam, kabla ya Waziri huyo kuzindua nyumba hizo.


Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa akitoa malekezo kwa Viongozi wa Wizara na Taasisi kabla ya kuzindua ujenzi wa nyumba za makazi za watumishi wa umma zilizopo Magomeni Kota na Canadian Village Msasani
Peninsula -Masaki jijini Dar es Salaam, kabla ya Waziri huyo kuzindua nyumba hizo.


Muonekano wa jengo la nyumba za Watumishi wa Umma ambalo limejengwa katika eneo la Magomeni Kota jijini Dar es Saalaam.

…………………………………..


Serikali itaendelea kuuwezesha Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kujenga nyumba za kisasa kwa ajili ya watumishi wa Umma na za kibishara ili kukabiliana na ongezeko la mahitaji ya nyumba yanayoongezeka siku kwa siku
nchini.

Akifungua Majengo kwa ajili ya makazi kwa watumishi wa Umma katika eneo la Magomeni Kota na Canadian Village Msasani Peninsula Masaki jijini Dar es Salaam Waziri wa Ujenzi na Uchkuzi Profesa Makame Mbarawa amesema nia ya Serikali ni kuhakikisha watumishi wake wanaishi katika makazi yaliyo bora na hivyo kuleta tija na ufanisi katika kazi za Umma.

“Lengo kuu la Serikali ni kuhakikisha watumishi wanapata makazi salama na ya kisasa yanayoendana na sayansi na teknolojia., hivyo TBA hakikisheni wapangaji wote watakaopata nafasi ya kuishi kwenye nyumba hizi wanalipa kodi kwa wakati’ amesema Waziri Prof. Mbarawa.

Prof. Mbarawa amesema Serikali inatambua umuhimu wa makazi bora kwa wananchi wake ambapo mahitaji ya nyumba bora yanakadiriwa kuwa zaidi ya nyumba milioni tatu kwa nchi nzima hivyo Serikali itaendeelea kujenga nyumba za ghorofa zitakazoweza kuhudumia watumishi wengi katika eneo dogo.

Waziri Prof Mbarawa amewtaka TBA kuhakikisha watakaopanga kwenye nyumba hizo wanazitunza kwa kuzingatia kanuni za usafi na matumizi bora ya nyumba ili zidumu kwa muda mrefu.

“Watakaoshindwa kulipa kodi kwa wakati watoeni muweke wengine tunataka nyumba hizi ziweze kukusanya fedha na fedha hizo hizo zitumike kujenga nyumba nyingine nyingi zaidi’ amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa.

Naibu Katibu Mkuu wa Ujenzi, Bw. Ludovick Nduhiye amesema Wizara itaiwezsha TBA kwa kuipa fedha ili kutimiza malengo ya Serikali .

Kwa upande Wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miudombinu, Mhe Selemani Kakoso ameipongeza Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwa namna inavyofanya kazi kwa ubora na ubunifu na kuitaka Wizara kuiwezesha TBA kukusanya madeni wanayodai watumishi mbalimbali ili kujiimarisha kiuchumi na kujenga miradi mingine.

“Mfumo mpya mliuoanzisha sasa wa kukusanya kodi ambao utamuwezesha mwenye nyumba kulipa kodi kwa wakati utasaidia kupata makusanyo kwa wakati na hivyo kutimiza malengo hivyo uendelezeni’ amesisitiza Mhe.
Kakoso. 

Mtendaji Mkuu wa TBA, Arch. Daud Kondoro amesema ujenzi wa nyumba za kisasa katika maeneo ya Magomeni kota na Canadian village jijijini Dar es Salaam ni mwendelezo wa Wakala huo kujenga nyumba za watumishi katika maeneo mbalimbali nchini ambapo miradi kama hiyo inaendelea katika eneo la Nzuguni-Dodoma, Mtwara, Shinyanga, Kilimanjaro na Kagera lengo likiwa kukabiliana na upungufu wa nyumba bora kwa watumishi wa umma.

Zaidi ya Shilingi bilioni kumi zimetumika katika ujenzi wa miradi miwili ya Magomeni Kota na Canadian Village na nyumba hizo zina uwezo wa kuhudumia familia 28 kwa wakati mmoja.
Share:

GGML, STAMICO WASAINI MKATABA WA SH BILIONI 55.2 KUCHORONGA MIAMBA


Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML), Elder Damon (kushoto) akisaini mkataba kati ya kampuni hiyo na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) wenye thamani ya Sh bilioni 55.2 kwa lengo la kuendeleza shughuli za uchorongaji miamba kwenye migodi ya kampuni hiyo. Kulia na Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, Dk. Venance Mwasse.


Na Mwandishi wetu

KAMPUNI ya Geita Gold Mining Limited (GGML) na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), imesaini mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya Sh bilioni 55.2 kwa lengo la kulipatia shirika hilo kandarasi ya kuchoronga miamba ndani ya mgodi wa GGML.


Akizungumza katika hafla fupi ya kutia saini makubaliano hayo jana mjini Geita, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Elder Damon alisema kuwa tangu kuanzishwa kwa kanuni za ushirikishaji wazawa kwenye shughuli za uchimbaji madini mwaka 2018, idadi ya wafanyabiashara watanzania waliofanikiwa kushinda kandarasi mbalimbali ndani ya mgodi huo, imeongezeka.


"Nia yetu imekuwa kusaidia jamii kwa kuwapa ujuzi ili kuwawezesha kushindana kikamilifu. STAMICO imekuwa ikitoa huduma za uchorongaji miamba ndani ya GGML, kusaidia programu za uchimbaji wa wazi tangu Septemba 2020.


“STAMICO imetoa huduma za uchorongaji miamba kwa viwango vya juu kwa kuzingatia usalama na ufanisi katika sekta ya uchimbaji madini kulingana na malengo ya sekta hii. Makubaliano haya na STAMICO yanaonyesha uungaji mkono unaoendelea katika ukuzaji wa ujuzi na utaalamu kuhusu uchorongaji miamba na utafiti wa madini nchini,” alisema Damon.


Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, Dk. Venance Mwasse aliipongeza GGML kwa imani waliyoionesha kwao tangu walipoanza kufanya kazi mwaka 2020.


“Tunapenda kuwahakikishia GGML na Serikali kuwa kazi yetu itatekelezwa kwa ubora na viwango vya juu,” alisema Dkt. Mwasse.

Mgeni rasmi aliyehudhuria hafla ya utiaji saini, Waziri wa Madini, Dk. Doto Biteko alisema kuwa hali ya STAMICO imebadilika na kuwa bora zaidi tangu mkataba wao wa awali na Geita Gold Mining Limited ulipoanza.


“Tangu 2020 STAMICO iliposaini mkataba wake wa kwanza na GGML, mambo yameboreshwa ndani ya Shirika. STAMICO imefanya vizuri sana kwa kuzingatia ubora na ufanisi wa kazi jambo ambalo wengi wetu tunajivunia.

“STAMICO imeiwakilisha vizuri nchi yetu ndiyo maana wawekezaji wengi kama GGML bado wana imani ya kufanya nao kazi,” alisema Dkt. Biteko.

Aidha, Dkt. Biteko alizitaka kampuni nyingine za ndani kunufaika na zabuni za nje kila zinapotangazwa kwa sababu kanuni za sheria hiyo ya madini ya mwaka 2017 zinatoa nafasi kwa watanzania kuchangamkia fursa zinazojitokeza kwenye sekta ya madini.

Share:

TBS YAADHIMISHA SIKU YA VIWANGO BARANI AFRIKA



WAFANYABIASHARA wadogo na wa kati wanakabiliwa na changamoto kadhaa,zikiwemo mitaji midogo, teknolojia duni, elimu ndogo ya masuala ya ujasiriamali, elimu ndogo kuhusiana masuala ya ubora na usalama na pia kukosekana kwa masoko ya uhakika ambapo kwa kiasi kikubwa huwadumaza. 

Ameyasema hayo jana Machi 28,2023 Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mhe.Beno Malisa kwa niaba ya mkuu wa Mkoa wa Mbeya katika Maadhimisho ya Siku ya Viwango Afrika, yaliyofanyika katika ukumbi wa Beaco, Jijini Mbeya. 

Amesema kuwa ni ukweli usiopingika kwamba wajasiriamali wadogo na wa kati wanapokuwa katika mazingira ya changamoto mbalimbali hawawezi kuchangia ipasavyo katika maendeleo, kutokomeza umaskini na kukuza viwanda na uchumi wa Taifa kwa ujumla. 

"Ni wazi kuwa wakiendelezwa na kuondolewa changamoto zinazowakabili watachangia kwa kiasi kikubwa katika mipango ya Taifa ya kuondoa umaskini, kujenga ustawi wa jamii na kukuza uchumi". Amesema 

Pamoja na hayo amesema wajasiriamali wadogo na wa kati hawawezi kufikia malengo yao iwapo watapuuza masuala ya ubora na usalama katika uzalishaji wao. 

Amesema kwa mujibu wa takwimu za Chama cha Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Wakulima Tanzania (TCCIA), asilimia 95 ya biashara zinazofanyika nchini ni biashara za wajasiriamali wadogo na wa kati, ambazo huchangia takriban asilimia 35 ya Pato la Taifa (GDP) na kuzalisha hadi asilimia 40 ya ajira. 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uandaaji Viwango (TBS), Bw.David Ndibalema amesema mbali na mafunzo na elimu ambayo hutolewa mara kwa mara kwa wajasiriamali wadogo, wa kati na umma kwa ujumla, Serikali hutenga fedha kila mwaka kwa ajili ya kuhudumia wajasiriamali wadogo na wa kati pale wanapoomba kuthibitisha ubora wa bidhaa zao. 

"Anachotakiwa kuwa nacho mjasiriamali huyu mdogo ni leseni ya biashara na barua ya utambulisho kutoka Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) ambapo TBS hupokea barua hiyo na kuendelea na taratibu zingine za uthibitishaji ubora". Amesema 

Amesema tangu kuanza kwa utaratibu huo, tumefanikiwa kuthibitisha ubora wa bidhaa za wajasiriamali 1,515 nchini kote na wengine wengi wako katika hatua mbalimbali za michakato ya kupata leseni ya kutumia alama ya ubora.
Share:

Tuesday, 28 March 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO MACHI 29,2023















Share:

RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI MUDA HUU

Share:

TANZANIA NA MAREKANI KUIMARISHA UHUSIANO WA KIBIASHARA NA UWEKEZAJI


Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji,akizungumza na Balozi wa Marekani nchini Mhe. Michael Battle ,mazungumzo yaliyofanyika katika Ofisi ndogo ya Wizara, jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji,akiwa katika picha na Balozi wa Marekani nchini Mhe. Michael Battle mara baada ya kumaliza ,mazungumzo yaliyofanyika katika Ofisi ndogo ya Wizara, jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji,akiagana na Balozi wa Marekani nchini Mhe. Michael Battle mara baada ya kufanyika mazungumzo yaliyofanyika katika Ofisi ndogo ya Wizara, jijini Dar es Salaam.

Na.Mwandishi Wetu- DAR ES SALAAM

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) Tanzania itaendelea kuimarisha uhusiano wa kibiashara na uwekezaji baina yake na Marekani na inawakaribisha wawekezaji kutoka nchini humo kuja kuwekeza na kushirikiana na watanzania katika ufanyaji biashara katika sekta mbalimbali nchini.

Dkt. Kijaji ameyasema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo kuhusu kuendeleza uhusiano wa kibiashara na uwekezaji baina ya nchi hizo na Balozi wa Marekani nchini Mhe. Michael Battle Machi 27, 2023 katika Ofisi ndogo ya Wizara, jijini Dar es Salaam.

Aidha, Waziri Kijaji ameiomba Marekani kuongeza muda wa Mkataba wa Mpango wa Ukuzaji fursa za Kiuchumi Afrika (AGOA) uliotiwa saini mwaka 2000 na awamu inayotarajiwa kuisha ni kati ya 2015 na 2025.

Akifafanua zaidi, Dkt. Kijaji amesema Mpango huo wa AGOA unalenga kutoa fursa ya upendeleo kwa nchi zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara kupeleka bidhaa zaidi ya 6,500 bila kulipa ushuru wa forodha nchini Marekani

Dkt. Kijaji pia ameainisha kuwa Tanzania ni moja ya nchi inayonufaika na fursa ya Mpango wa AGOA ambapo Sekta ya Nguo na Mavazi inachangia mauzo kwa asilimia 95. Kutoka katika Viwanda vikubwa vya Mazava Fabrics and Production E.A L, na Tanzania Tooku Garments Co., Ltd . Bidhaa zingine zinazochangia asilimia 5 ni bidhaa za Mikono, Uchakataji bidhaa za kilimo (Agro-processing) na Ngozi.

Naye Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mhe. Michael Battle amesema Marekani itaimarisha uhusiano wa kibiashara na uwekezaji na Tanzania hususani katika sekta mbalimbali ikiwemo viwanda na kufanya biashara na benki za kitanzania ili kirahisisha upatikanaji wa mitaji kwa wafanyabiashara wa Tanzania.
Share:

TANZANIA NA FINLAND ZAKUBALIANA KUENDELEZA SEKTA YA MISITU NA NYUKI NCHINI.


Na John Mapepele

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa leo Machi 28, 2023 amefanya kikao na ujumbe wa Serikali ya Finland ulioongozwa na Balozi wa Finland hapa nchini, Mhe. Thereza Zitting na kukubaliana uendelezaji na uwekezaji mkubwa kwenye Sekta ya misitu na nyuki hapa nchini.

Mazungumzo hayo yamefanyika ofisini kwake ambapo pande zote mbili zimekubaliana kupitia mikataba ya awali iliyoingiwa na Serikali ya pande zote mbili ili kuiboresha ikizingatiwa kuwa nchi hizi zimekuwa na mahusiano mazuri kwa takribani miaka 40.

Aidha, katika kikao hicho ambacho kilihudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Hassan Abbasi na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu nchini ( TFS), Prof. Dos Antos Silayo

Amesema Serikali ya Finland imeonyesha nia ya dhati katika uhifadhi wa misitu na kuongeza thamani ya mazao ya misitu na nyuki ili yaweze kuwa katika kiwango cha kimataifa.

Mhe. Mchengerwa amewakaribisha wawekezaji kutoka Finland kuja kuwekeza huku akisisitiza kuwa Tanzania ina maeneo mengi yanayoweza kuwekezwa ambapo Mhe. Balozi Zitting amemhakikishia Mhe waziri kuwaletea wawekezaji hao.

Pia amesema Serikali ya Finland imekuwa ikitoa msaada mkubwa wa mafunzo kwa wananchi kwenye sekta ya Misitu huku akitolea mfano wa Chuo kilichopo Mafinga mkoani Iringa.

Aidha, Mhe. Mchengerwa amesema Serikali ya Finland katika awamu hii imekubali kuisaidia Tanzania vifaa katika kukabiliana na majanga kwenye Maeneo ya misitu yaliyohifadhiwa kama moto na ujangili.
Share:

KASINO YA MTANDAONI MERIDIANBET| FURAHIA USHINDI

 Jisajili Meridianbet na ushinde mizunguko 50 ya bure kucheza michezo ya kasino. Kujisajili bonyeza hapa https://a.meridianbet.co.tz/c/GLd6O8

Sloti ya Crazy Time

Hayawi hayawi sasa yamekuwa. Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet kwa kushirikiana na watengenezaji mahiri wa michezo ya kasino za mitandaoni - Evolution Gaming, wanakuletea mchezo wa kijanja uitwao Crazy Time.

Crazy Time ni mchezo wa kipekee kutoka studio za Evolution Gaming. Mchezo huu umejengwa na dhamira ya kukamilisha ndoto ambazo hudakwa na kinasa ndoto (Dream Catcher). Usisubiri kusimuliwa kwasababu, mchezo huu utakupa furaha maradufu katika kila mzunguko.

Sloti ya Crazy Time una bonasi 4 za kukata na shoka. Unaweza kurudishiwa dau lako hadi mara 25000 bila kusahau chaguo la RNG yaani (Random Number Generation) pamoja na Gurudumu la Bahati (Wheel of fortune) litakalokupa fursa ya kushinda zawadi nyingine nyingi zaidi. Chizika leo na Meridianbet na ushinde kwa kupitia http://www.meridianbet.co.tz

Jinsi ya Kucheza Crazy Time

 

Ni rahisi sana kucheza sloti ya Crazy Time ndani ya Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet. Mchezo huu huchezwa kwenye Gurudumu la bahati ambalo lina sehemu 54, kila sehemu inakuwa na ongezeko la dau kwa namna tofauti tofauti.

Unachotakiwa kukifanya kwenye mchezo huu wa kusisimua wa Crazy Time, ni kubashiri wapi gurudumu hili litasimama, kisha, weka dau lako hapo. Tumia uwanja namba 1, 2, 3, 5, 10 kwenye mchezo mkuu au tumia uwanja wa bashiri za bonasi. Maeneo ya kushinda bonasi zinazohusiana na michezo ni Cash Hunt, Pachinko, Coin Flip pamoja na Crazy Time.

Cash Hunt ni mkusanyiko wa picha ambazo zinahusisha skrini kubwa yenye mazidisho 108 yasiyo na mpangilo maalumu. Coin Flip ni mchezo unaohusisha uchaguaji wa “Kichwa au mwenge” ambapo shilingi yenye rangi mbili - Nyekundu na Bluu, itakupa fursa ya kuchagua upande gani shilingi hiyo inaangukia huku kwenye skirini kubwa pakioneshwa thamani hiyo.

Pachinko ni mchezo wa bonasi ambao unahusisha ukuta wa mazidisho ya thamani ya dau lako. Ina aina 16 za mazidisho ambayo hayo yote yapo kwa ajili ya kukupa faida. Na, ya mwisho ni Crazy Time yenyewe, mchezo huu wa bonasi unamuhitaji mchezaji kufungua mlango mwekundu na kuingia kwenye ulimwengu wa kufikirika wa kuchizika.

Kwenye ulimwengu huo, utakutana na zawadi kede kede ikiwemo pesa za papo hapo. Crazy Time ina sehemu 64, pindi Gurudumu linapozungushwa unatakiwa kuboyeza kitufe chekundu ili kilisimamishe. Kikubwa zaidi, unaweza kujishindia hadi mara 25000 ya dau uliloliweka kupitia bonasi ya Crazy Time.  Chizika na kasino ya mtandaoni ya Merianbet na ushinde!!

 

Meridianbet, Nyumba yenye Odds Bora na Bonasi Kubwa!


Share:

MICHEZO YA MEI MOSI KUTIMUA VUMBI MOROGORO



Michezo Inayo wakutanisha wafanyakazi kutoka katika mashirikisho ya Micghezo ya Wafanyakazi wa Wizara, Mikoa, Idara zinazojitegemea na Wakala wa Serikali SHIMIWI), Wafanyakazi wa Mashirika ya Umma na Makampuni Binafisi (SHIMMUTA), Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (SHIMISEMITA) na Wafanyakazi wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama (BAMMATA) maarufu MEI MOSI mwaka huu itafanyika Mjini Morogoro kuanzia tarehe 16 hadi 30 Aprili, 2023 ambako pia kilele cha Sherehe za wafanyakazi KiTaifa zitakakofanyika.


Michezo itakayoshindaniwa ni Mpira wa Miguu, Netiboli, Riadha, Kuvutana kwa Kamba, Karata, Bao, “Draft”, Baiskeli na Mpira wa Wavu (Volleyball), katika Viwanja vya Jamhuri, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Mazimbu, Shule ya Sekondari Morogoro, Kiwanda cha Tumbaku, Magadu na Chuo cha Ujenzi.


Hadi sasa Timu zilizo onyesha nia ambazo zipo katika maandalizi ya kushiriki ni ofisi ya Rais Ikulu, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi), Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, wizara ya Mambo ya nje, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Ofisi ya Rais TAMISEMI, Wizara ya Ulinzi na JKT, Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Wizara ya Fedha, Wizara ya Kilimo, Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Wizara ya Maliasili na Benki ya CRDB.


Tunaziomba timu zinazojiandaa kushiriki zithibitishe kwa maandishi kwa kutaja aina ya Michezo watakayoshiriki ili kamati iweze kupanga ratiba na kufanya maandalizi muhimu kama Viwanja na waamuzi kulingana na idadi ya timu.


Aidha, tunasisitiza timu zote kufika katika kituo cha mashindano (Morogoro) ifikapo tarehe 14 Aprili, 2023. Timu itakayopangwa katika ratiba endapo itachelewa kufika na kukuta Mchezo/Michezo yake imepita itahesabika kuwa amepoteza Mchezo/Michezo hiyo kwa mujibu wa kanuni za mashindano.


Tunawatakia maandalizi mema pia tunawakaribisha Mjini Morogoro.
“Mshikamano Daima”
Share:

Monday, 27 March 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE MACHI 28,2023



















Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger