Monday, 27 March 2023
Sunday, 26 March 2023
SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI YAAGIZWA KUCHUNGUZWA BAADHI YA VIONGOZI WANAOJIHUSISHA NA VITENDO VYA MGONGANO WA MASLAHI




MWANAMKE AFARIKI AKIHONDOMOLA URODA NA MPENZI WAKE KICHAKANI
VIONGOZI WA DINI WATAKIWA KUWAHIMIZA WAUMINI KUHESHIMU IMANI ZA WENGINE
Na Mwandishi wetu,Dar Es Salaam.
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana amesema ni jukumu la viongozi wa dini kuwaunganisha Watanzania, kudumisha amani, umoja na mshikamano.
Pia, ametaka Viongozi hao kuendeleza utamaduni wa kuheshimu imani ya kila mmoja kwa kutazama mambo mazuri na sio changamoto chache zinazojitokeza.
Kinana ameyasema hayo leo Machi 26, 2023 wakati akizungumza katika hafla ya mashindano ya kuhifadhi na kusoma Kuraani tukufu yaliyoandaliwa na Taasisi ya Aswhabu al-Kahfi Islamic Centre, yaliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
“Hivi sasa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, ameweka mkazo kwenye maridhiano na tuna taasisi ya maridhiano na amani mbayo imeunganisha dini na madhehebu mbalimbali nchini, lengo ni kudumisha umoja, mshikamano na amani katika taifa letu.
“Mimi ningependa kuwasihi viongozi wa dini, kila madhehebu, kila dini ni muhimu tushikame,msitafute mapungufu ya kila mmoja, mtafute mema ya kila mmoja ili tuweze kushikamana,” amesema.
Kinana pia amewasihi Watanzania kuzingatia na kutanguliza mambo mazuri ya kila mmoja Ili kuondoa uwezekano wa kuibua migogoro isiyo na tija kwa ustawi wa taifa.
Awali akimkaribisha Kinana, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Selemani Jafo, amesema amani na maadili yanasisitizwa mahali popoote kwani hata Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025 imetaja ajenda ya amani na maadili.
"Kila mtanzania ana nafasi ya kukemea tabia zisizofaa kwenye jamii,tuishi Kwa kuzingatia miiko yetu na hii itasaidia kuishi kwenye hali ya utulivu na amani,"amesisitiza Waziri Jafo.
WIZARA YA AFYA YAWATOA HOFU WANANCHI MAAMBUKIZI MAPYA YA MARBURG
Na. WAF - Ziara Mkoani Kagera, Bukoba.
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amefanya ziara ya kutembelea katika Kijiji cha Ntoma Wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera kwa lengo la kujionea hali inavyoendelea baada ya kutangazwa kutokea kwa mlipuko wa ugonjwa wa Marburg Mkoani humo.
Katika Ziara hiyo, Waziri Ummy ameambatana na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dkt. Zabron Yoti pamoja na Mwakilishi wa Shirika la UNICEF Bi. Shalini Bahuguna.
Aidha, Waziri Ummy amesema kwa sasa hali ni salama na kuwataka Wananchi wa kijiji hicho na watanzania kwa ujumla kuondoa hofu kwa kuwa Serikali inawajali Wananchi wake.
“Niwatoe hofu Watanzania tuendelee kufanya kazi zetu lakini tuzingatie maelekezo ya Serikali ya kujikinga na ugonjwa huu kwa kuepuka kushikana mikono hususan kipindi hiki lakini pia tujitahidi kunawa mikono mara kwa mara kwa maji tiririka na sabuni.” amesema Waziri Ummy
Hata hivyo, Waziri Ummy amesema kuwa Serikali chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea na juhudi za kuhakikisha ugonjwa huo unamalizika na hautatokea tena katika maeneo hayo.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Kanyangele Bw. Hamim Hassan ameishukuru Serikali kwa kufanya juhudi kubwa ambapo hadi sasa hakuna mgonjwa yeyote aliyeongezeka kwa kuthibitika kuwa na ugonjwa huo.
“Hatua za Serikali kupitia Wizara ya Afya zilizochukuliwa za kuwaweka sehemu maalumu waliokuwa karibu na wagonjwa imesaidia sana kutoendeleza maambukizi kwingine na hali ni shwari kwa sasa.” amesema Bw. Hassan
MERIDIANBET KASINO YA MTANDAONI YAJA NA SLOTI YA WANYAMA

Sloti ya Forest Rock
Sloti ya Forest Rock ina muundo wa kizamani wenye kolamu 5 na mistari 15 ya ushindi. Kama kawaida ukiichagua kasino ya mtandaoni ya Meridianbet basi umechagua ushindi.
Sloti hii pendwa ya Forest Rock ina alama mbalimbali za wanyama pori wenye kukuletea faida kama vile Sungura alievaa headphone, Paka mwitu mpiga gitaa na Dubu ambaye anasimama kama meneja, Simba ni bonge la msanii na Tembo akiwa kama mpiga ngoma mkubwa. Sio hivyo tu, alama za Karata nazo zipo. Unasubiri nini kujiunga na familia ya washindi ya Meridianbet? Jiunge leo na ushinde.
Jinsi ya Kucheza Sloti ya Forest Rock
Ni rahisi sana kucheza sloti ya Forest Rock, unachotakiwa kukifanya ni kuhakikisha unapata alama tatu zenye kufanana ili ushinde. Kubwa zaidi ya yote ni pale utakapo pata alama tatu zenye nembo ya mchezo wa Forest Rock ambayo itakulipa hadi mara 20 ya dau uliloliweka. Sio hayo tu, Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet inakupa fursa ya kupata hadi mizunguko 20 ya bure.
Ukipata Jokeri tatu kwenye sloti hii utapewa mizunguko mingine zaidi. Sloti hii ya Forest Rock ina chaguo la kubashiri (Gambling option) ambalo linakupa fursa ya kuchagua kati ya kadi mbili ambazo ni Nyekundu na Nyeusi, uchague ipi itaanguka mezani na itakupa mara mbili ya faida uliyoipata. Cheza Kasino ya mtandaoni ya Meridianbet upate bonasi kibao.
Saturday, 25 March 2023
MERIDIANBET YAZINDUA DUKA JIPYA FIRE
Mabingwa wa michezo ya kubahatisha Meridianbet baada ya kusubiri kwa hamu duka jipya hatimaye leo hii mtaa wa Fire jijini Dar es salaam kunameremeta kwani limezinduliwa duka kwa ajili ya kubashiri michezo mbalimbali huku ODDS KUBWA kama mvua zikimwagika kila siku kazi inabaki kwako tu kuweka dau na kubashiri.
Duka hili litawawezesha wakazi wa Fire na wengine wapita njia kubashiri wakichagua machaguo zaidi ya 1000 wanayotaka.
Hii si mara ya kwanza Meridianbet wanazindua duka ni kawaida yao kwani mpaka sasa wana maduka mengi sana kwaajili ya kubetia katika maeneo mbalimbali jijini Dar es salaam kila mtaa ni wao tu rangi nyekundu ipo kila mahali na sasa wana Jackpot kubwa kabisa.
Beti na Meridianbet mechi za ligi zote, odds ni kubwa sana, usikose pia Kasino ya mtandaoni ya Meridianbet yenye michezo rahisi ya sloti kama Poker, Aviator, Roulette.
Baada ya uzinduzi wa duka hilo mitaa ya Fire, Bwana Twaha Ibrahim ambaye ni mkuu wa kitengo cha Maudhui Meridianbet kwanza alisema kuwa; “Duka hili ambalo tumezindua ni la nne kwa mwezi huu, na hakika natumaini mmefurahi sisi kuwaletea duka hili kwaajili ya kuwarahisishia kwenye shughuli zenu za kubetia”
Twaha hakuishia hapo aliwashukuru watu wote ambao walihudhuria kwenye uzinduzi huo na kuwaambia kuwa hawajakosea kuchagua Meridianbet kwenye kubashiri kwani Meridianbet hutoa kile ambacho wanakitaka na pia ODDS KUBWA zipo hapa.
Pia tembelea tovuti ya Meridianbet meridianbet.co.tz kuona ongezeko la odds kubwa na machaguo kibao.
Meridianbet pia wana kile ambacho unakipenda ambapo michezo ya kasino ya matandaoni hapa ndipo mahali pake kuna sloti za kijanja na michezo rahisi kushinda kama Aviator, Poker na Roulette, jiunge Meridianbet uwe moja ya washindi wa kila siku. Pia unaweza kubashiri mubashara mechi hizo.
FALSAFA YA MONTESSORI YATUMIKA KUWANOA WALIMU KAGERA
TGNP YAWAKUTANISHA WANAUME KUJADILI MASUALA YA NAFASI YA WANAUME KATIKA KUENDELEZA USAWA WA KIJINSIA

Meneja wa Fedha TGNP Bw.Altho Mwangoa akifungua Kilinge salama maalumu cha wanaume kugusia masuala ya Nafasi ya wanaume katika kuendeleza usawa wa kijinsia kilichofanyika leo Machi 25,2023 kwenye ukumbi wa Lost Beach Jijini Dar es Salaam.
Mwezeshaji Adv.Pasiense Mlowe akizungumza katika Kilinge salama maalumu cha wanaume kugusia masuala ya Nafasi ya wanaume katika kuendeleza usawa wa kijinsia kilichofanyika leo Machi 25,2023 kwenye ukumbi wa Lost Beach Jijini Dar es Salaam.
Mwezeshaji Dkt.Kitanta Simwanza akizungumza katika Kilinge salama maalumu cha wanaume kugusia masuala ya Nafasi ya wanaume katika kuendeleza usawa wa kijinsia kilichofanyika leo Machi 25,2023 kwenye ukumbi wa Lost Beach Jijini Dar es Salaam.

.jpeg)
















.png)


















