Tuesday, 14 March 2023

MWANAUME AUAWA AKIJARIBU KUMUOKOA JAMAA ALIYEKUWA ANAPIGWA NA MKE


Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 24 ameaga dunia baada ya kujeruhiwa katika vita vya wanandoa wawili eneo la Rachuonyo Kasikazini katika kaunti ya Homa Bay nchini Kenya.

Dan Ouma anaripotiwa kujaribu kuwatenganisha wanandoa wawili waliokuwa wakipigana lakini badala yake akapigwa na kifaa kichwani butu katika vita hivyo. 

Akithibitisha kisa hicho, Chifu wa kata ya Kanyaluo Magharibi Elius Ombim amesema kuwa mwanaume mmoja kutoka kijiji ca Seme Kaloo alikuwa akipigwa na mke wake na watoto kufuatia mzozo wa nyumbani.

Hili lilisababisha majirani - akiwemo Ouma - kuingilia kati lakini akawa ndiye aliyebeba msalaba wa vita hivyo.

Alipigwa kwa kifaa butu kichwani na kukimbizwa hadi Hospitali ya Kadienge kabla ya kuhamishiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kaunti ya Homa Bay akiwa hali mahututi.

 Kwa bahati mbaya, aliaga dunia katika hospitali hiuo akipokea matibabu na mwili wake kuhamishiwa katika makafani ya Homa Bay.

Chanzo - Tuko News
Share:

KAMATI YA SIASA CCM IMESELA YATISHWA HALI MBAYA YA VYOO SHULE YA NYIKA...YATOA MAAGIZO

Kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi Kata ya Imesela ikitembelea ujenzi wa mradi wa choo shule ya msingi Nyika.
Kajala Jeremia Katibu Mwenezi na itikadi kata ya Imesela akizungumza kwenye ziara ya kamati ya Chama Cha mapinduzi.
OFisi ya serikali ya kijiji chaMwamanyuda kata ya Imesela iliyojengwa na sungusungu,nguvu za wananchi na mfuko wa serikali.
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Nyika akitoa taarifa mbele ya kamati ya chama.
Diwani wa kata ya Imesela Seth Msangwa akizungumza katika mwendelezo wa ziara ya siasa ya kamati ya chama cha Mapinduzi.


Na Halima Khoya,Shinyanga.


Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Imesela halmashauri ya Shinyanga imeutaka uongozi wa shule ya Msingi Nyika kufanya kikao na uongozi wa serikali ya kijiji ili kuitisha mkutano wa hadhara na wananchi kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa choo cha walimu pamoja na wanafunzi.


Maagizo hayo yametolewa Machi 10,2023 kwenye mwendelezo wa ziara ya Kamati ya Siasa ya Cha Mapinduzi (CCM) kata ya Imesela baada ya kutembelea mradi unaoendelea katika shule hiyo na kukuta ujenzi wa umesimama.


Diwani wa Kata ya Imesela Seth Msangwa amesema ujenzi wa choo cha walimu umetumia muda mrefu kukamilika kutokana na changamoto tofauti ikiwa ni pamoja na ushirikiano mdogo wa wananchi na uongozi wa kijiji ambapo amewataka kuitisha kikao kwa ajili ya kuchangia ujenzi huo ili kuweka mazingira salama kwa walimu na wanafunzi.


Msangwa amesema katika ujenzi wa choo cha walimu atachangia saruji, kuleta mtu wa kufyatua matofali na mchanga na kwamba miongoni mwa changamoto walizozikuta watazichukua na kuzipeleka kwenye uongozi wa juu huku changamoto zingine amewataka wananchi na uongozi wa kijiji kukaa kikao kujadili uwiano uliopo kati ya vyoo vya wanafunzi na idadi ya wanafunzi wanaotumia vyoo hivyo ambavyo havina kiwango.


"Kipindi naomba nafasi katika eneo hili niliahidi kutoa ushirikiano kwa wananchi wote lakini kama nyie msipokuwa na ushirikiano tutafikiaje malengo, Kaeni chini muijenge Nyika yenu, hali ya vyoo vya wanafunzi ni mbaya na wala sitaki kupaona,kaeni na wananchi mchangie ili hata serikali iwe na wepesi kutia mkono wake baada ya nyie kuanza",amesema Msangwa.


Kwa upande wake Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Kata ya Imesela,Richald Nyanda amesema katika shule hiyo kuna uhaba wa matundu ya vyoo kutokana naa idadi ya wanafunzi iliyopo na kwamba hali iliyopo kwenye matundu hayo ni mbaya hali inayohatarisha afya kwa waafunzi.


"Taarifa uliyotupa na uhalisia uliopo Nyika hatuna vyoo hata wewe ukienda saivi unaweza ukaogopa kuingia, watoto wetu wana hali mbaya, kufikia tarehe 25 kuwe na kamati mpya ya kijiji, matundu yanayohitajika ni 21 na yaliyopo ni 6 alafu tumekaaa tu hakuna utaratibu wa kujenga mengine,bada ya kikao hicho itisha serikali ya kijiji ili kushughulika na hili",amesema Nyanda.


Awali akitoa taarifa ya shule Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Nyika,Marco Sylivester amesema kuwa Shule hiyo ina matundu ya vyoo 6 na uhitaji wa matundu ya vyoo 21 pia ina uhaba wa matundu ya vyoo vya walimu mawili na kwamba inafanya taratibu za kujenga vyoo hivyo ambavyo vimefikia kwenye msingi.


"Shule ya Msingi Nyika ina wanafunzi 512 na walimu 8, shule ina madarasa 8 mahitaji 21,mahitaji ya matundu ya vyoo vya walimu ni 02 yaliyopo ni 0, shule ina jumla ya wanafunzi 83 kwa miaka miwili waliofanya mtihani ni 82 waliofaulu 46,waliofeli 37 ambayo ni sawa na asilimia 57%,Tutafanyia kazi maagizo yote tuliyopewa",amesema Sylivester.
Share:

Monday, 13 March 2023

Wimbo Mpya : NYANDA MALIGANYA - ITETEMA

 

Share:

WANAFUNZI WA KIKE 96 WA SHULE ZA SEKONDARI KUPATIWA MAFUNZO YA TEHAMA DIT

Naibu Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam Taaluma (DIT), Utafiti na Ushauri wa Kitaalam Prof.Ezekiel Masige Amri akifungua Mafunzo ya Siku Tano (5) ya TEHAMA kwa wanafunzi 96 wa kike wa kidato cha tatu shule za Sekondari nchini ambapo yanafanyika katika Ukumbi wa DIT kuanzia leo Jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi wa Kituo cha Umahili wa Tehama DIT, Dkt.Petro Pesha akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa Mafunzo ya Siku Tano (5) ya TEHAMA kwa wanafunzi 96 wa kike wa kidato cha tatu shule za Sekondari nchini ambapo yanafanyika katika Ukumbi wa DIT kuanzia leo Jijini Dar es Salaam. Bw.Alexius Revocatus Kagunze kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa Mafunzo ya Siku Tano (5) ya TEHAMA kwa wanafunzi 96 wa kike wa kidato cha tatu shule za Sekondari nchini ambapo yanafanyika katika Ukumbi wa DIT kuanzia leo Jijini Dar es Salaam. Mwakilishi wa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Bw.Abraham Mangesho akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa Mafunzo ya Siku Tano (5) ya TEHAMA kwa wanafunzi 96 wa kike wa kidato cha tatu shule za Sekondari nchini ambapo yanafanyika katika Ukumbi wa DIT kuanzia leo Jijini Dar es Salaam. Badhi ya wanafunzi wa Kidato cha tatu Shule za Sekondari nchini wakiwa katika ufunguzi wa Mafunzo ya Siku Tano ya TEHAMA kwa wanafunzi 96 wa kike, Mafunzo ambayo yanafanyika katika Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) Jijini Dar es Salaam.

**********************

NA MWANDISHI WETU

TAASISI ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) imefungua Mafunzo ya Siku Tano (5) ya TEHAMA kwa wanafunzi 96 wa kike wa kidato cha tatu shule za Sekondari nchini ambapo yanafanyika katika Ukumbi wa DIT kuanzia leo Jijini Dar es Salaam.

Mafunzo hayo yaliyofadhiliwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) yamefunguliwa na Naibu Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam Taaluma (DIT), Utafiti na Ushauri wa Kitaalam Prof.Ezekiel Masige Amri kwa niaba ya Mkuu wa Taasisi hiyo.

Akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Mafunzo hayo leo Machi 13,2023, Prof.Amri amepongeza juhudi kubwa iliyofanyika katika kuhakikisha mafunzo yanatolewa kwa mabinti wa shule za sekondari yatakwenda vizuri na kupata mrejesho mzuri kutoka kwa wahusika wa mafunzo hayo.

Prof.Amri ameushukuru mfuko wa Mawasiliano kwa Wote UCSAF pamoja na Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kuona umuhimu wa TEHAMA kwa vijana hasa jinsia ya kike kwa kuwa vijana wa kike siyo wengi kwani wanaogopa masomo ya sayansi hivyo mafunzo haya yatakuwa chachu ambayo itasaidia kuleta uwiano sawa na ule wa vijana wa kiume.

Aidha amewaeleza wanafunzi umuhimu wa TEHAMA kwa kipindi hiki ya kwamba "Katika dunia ya sasa hakuna jambo linaloleta mapinduzi ya haraka kama TEHAMA na sasa hivi tupo kwenye Mapinduzi ya nne ya viwanda hii inapelekea mahitaji makubwa ya Teknolojia".

.." niwaambie tu kuwa mawasiliano mengi sasa hivi yanatumia Tehama, kadhalika viwanda vinahitaji mifumo inayojiendesha yenyewe ikisaidiwa na Tehama kwa hiyo wataalam katika sekta hii wanahitajika hivyo hii ni fursa ya pekee kwenu" amesema Prof.Amri

Sambamba na hilo Prof. Amri ameeleza kuwa nchi yetu inatambua umuhimu wa kuandaa wataalam wa Tehama katika nyanja mbalimbali na ndiyo sababu kubwa ya Ofisi ya Rais TAMISEM kwa kushirikiana na UCSAF wameweza kushirikiana na Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) katika kuhakikisha wanawapatieni ninyi mafunzo yatakayowasaidia ili muwe chachu kwa vijana wengine wa kike.

Kwa upande wake Bw.Alexius Revocatus Kagunze kutoka Ofisi ya Rais TAMISEM amewasisitiza wanafunzi kutumia fursa hii vizuri kwani dunia ya sasa bila Tehama itakuwa vigumu kushindana ndani na nje ya nchi.

Alexius amesema "Niwaombe vijana wote mliopata nafasi ya kufika DIT kwa ajili ya mafunzo kuwa makini katika kusikiliza na kuuliza maswali, niwaambie tu kuwa dunia ya sasa ni ya Teknolojia na hiyo ndio itakayotusaidia ili tuweze kushindana kimataifa na dunia nzima na bila hiyo sisi kama nchi tutabaki nyuma na kutegemea wataalam kutoka nje ya nchi sisi kama Serikali tunaahidi kuwa tupo nyuma yenu kama walezi na wazazi kuhakikisha mnapata mafunzo yatakayowapatia ninyi utalaam".

Akizungumza kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Abraham Mangesho amesema kuwa mfuko unajitahidi kufadhili mafunzo haya ya Tehama ili kujenga uelewa kwa wasichana na kuwapa hamasa ili waone kuwa wao pia wanaweza kusoma masomo ya Sayansi au Tehama kwani jinsia hii inaonekana kubaki nyuma hivyo kupitia mafunzo haya ya siku tano tunaamini chachu itakayojengwa ndani yao italeta uthubutu wa kusoma Tehama ili waweze kuwa wataalam.
Share:

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YAELEKEZA LUGHA ZA KIINGEREZA NA KISWAHILI KUTUMIKA WAKATI WA UTUNGAJI WA SHERIA .

Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro akiwasilisha taarifa inayohusu Muundo na Majukumu ya Wizara pamoja na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria Tarehe 12 Machi, 2023.

Sehemu ya wanakamati wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria pamoja na menejimenti ya Wizara ya Katiba na Sheria na Viongozi wa Taasisi za wizara hiyo wakifuatilia taarifa ya Mhe. Waziri Ndumbaro.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Mary Makondo (Mbele kushoto) akiandika maelekezo yaliyokuwa yakitolewa na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria.

Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakifuatia mazungumzo wakati wa kikao cha Wizara ya Katiba na Sheria na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria.

********************

Na George Mwakyembe & Lusajo Mwakabuku – WKS.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imeielekeza Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kutumia lugha zote mbili wakati wa utungaji wa Sheria na kanuni yaani Kiingereza na Kiswahili ili kuepusha kazi hiyo kufanywa mara mbili kunakopelekea kuongezeka kwa gharama rasilimali fedha na muda pale Sheria husika inapotakiwa kutafsiriwa baada ya kupitishwa.

Maelekezo hayo yametolewa na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria walipokuwa wakipokea taarifa inayohusu Muundo na Majukumu ya Wizara pamoja na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Katiba na Sheria iliyowasilishwa na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro, 12 Machi, 2023.

Akiwasilisha taarifa mbele ya Kamati hiyo, Waziri Ndumbaro akiwa ameambatana na Menejimenti ya Wizara pamoja na Wakuu wa Taasisi zote zilicho chini ya Wizara ya Katiba na Sheria amesema Wizara ya Katiba na Sheria imekuwa na mchango mkubwa katika kuhakikisha inasimamia ipasavyo suala la haki na usawa jambo linalopelekea wawekezaji kuvutiwa kuwekeza nchini.

"Wizara ya Katiba na Sheria ni Wizara inayochangia kwa kiasi kikubwa katika kuvutia wawekezaji kwa kuimarisha Haki na Usawa, wawekezaji hawawezi kuja kuwekeza nchini kama hakuna Haki na Usawa”. Alisema Mhe. Ndumbaro.

Akichangia kwenye kikao hicho Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mh. Jaji Dkt Eliezer Feleshi amesema jukumu kubwa lilopo Sasa ni kuendelea kutafsiri Sheria zote 446 pamoja na Sheria ndogo 29,172 na tayari Wizara ilishajipanga na wanaendelea na kazi hiyo, maelezo haya yalipelekea wajumbe kutaka utungaji wa Sheria hizo ufanyike katika lugha ya Kiingereza na Kiswahili ili kuepusha kazi ya kutafsiri baada ya mswada wa Sheria kupitishwa.

Pamoja na jukumu hilo Jaji Dkt Feleshi amesema ofisi yake pia ina jukumu la kusimamia majadiliano ya migogoro mbalimbali iliyopo Mahakamani ili migogoro hiyo iijadiliwe nje ya Mahakama kama Kauli Mbiu ya Wiki ya Sheria iliyofanyika February mwaka huu iliyoelekeza umuhimu wa utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi katika kukuza uchumi endelevu.

Naye Mtendaji Mkuu wa Mahakama Prof, Elisante Ole Gabriel ameishukuru Wizara kwa Ushirikiano wanaowapa na kusema sasa wamejipanga kuboresha Mahakama za Kata nchi mzima kuhakisha kuwa zinakuwa na miundo mbinu bora na ya kisasa.

Katika hatua nyingine, Kamati imeelekeza kuendelea kukiimarisha Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto kwani ni moja kati ya vyuo vinavyoipa sifa nchi katika ukanda wa Afrika Mashariki kwa kuwa Chuo bora chenye kuendeleza watumishi wa Mahakama. Kamati vile vile imeelekeza Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ambacho ni chombo cha Kikatiba chenye jukumu la kuhakikisha linalinda haki za binadamu hususani masuala ya makundi maalumu ya wanawake na watoto kutekeleza majukumu yake ipasavyo hasa matukio mbalimbali ya ukiukwaji wa haki za binadamu na watu yanapojitokeza badala ya kukaa kimya.

Baada ya wasilisho na maelekezo ya kamati, Mhe. Dkt. Ndumbaro alisema kuwa Wizara yake imepokea maelekezo yote na akaiomba kamati kuwa utakapofika wakati wa kuwasilisha Bajeti ya Wizara na Taasisi zake mbele ya Bunge, kamati iiunge mkono ili bajeti itayoombwa iweze kupitishwa na hivyo kuiwezesha Wizara na Taasisi zake kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Share:

Picha : VIKAO VYA KAMATI ZA BUNGE LA AFRIKA VIKIENDELEA LEO MACHI 13,2023


Makamu wa Rais wa Tatu wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament - PAP), Mhe. Lucia Doss Passos akizungumza leo Jumatatu Machi 13,2023 kwenye kikao cha Kamati ya jinsia, familia, vijana na watu wenye ulemavu ya Bunge la Afrika. Kamati za Bunge la Afrika vinafanyika Midrand Afrika Kusini kuanzia Machi 6 hadi 17,2023 ambapo wajumbe wa kamati hizo wanajadili masuala mbalimbali kuhusu Bara la Afrika. 

Miongoni mwa kamati zilizofanya vikao vyao leo asubuhi ni Kamati ya Jinsia, Familia, Vijana na Watu wenye Ulemavu na Kamati ya Uchukuzi, Viwanda, Mawasiliano, Nishati, Sayansi na Teknolojia.

 Tazama matukio katika picha hapa chini. Picha na Kadama Malunde
Kikao cha Kamati ya Jinsia, Familia, Vijana na Watu wenye Ulemavu ya PAP kikiendelea
Kikao cha Kamati ya Jinsia, Familia, Vijana na Watu wenye Ulemavu ya PAP kikiendelea
Kikao cha Kamati ya Jinsia, Familia, Vijana na Watu wenye Ulemavu ya PAP kikiendelea
Kikao cha Kamati ya Jinsia, Familia, Vijana na Watu wenye Ulemavu ya PAP kikiendelea
Kikao cha Kamati ya Jinsia, Familia, Vijana na Watu wenye Ulemavu ya PAP kikiendelea
Kikao cha Kamati ya Jinsia, Familia, Vijana na Watu wenye Ulemavu ya PAP kikiendelea
Kikao cha Kamati ya Jinsia, Familia, Vijana na Watu wenye Ulemavu ya PAP kikiendelea
Kikao cha Kamati ya Jinsia, Familia, Vijana na Watu wenye Ulemavu ya PAP kikiendelea
Kikao cha Kamati ya Jinsia, Familia, Vijana na Watu wenye Ulemavu ya PAP kikiendelea
Kikao cha Kamati ya Uchukuzi, Viwanda, Mawasiliano, Nishati, Sayansi na Teknolojia ya PAP kikiendelea
Kikao cha Kamati ya Uchukuzi, Viwanda, Mawasiliano, Nishati, Sayansi na Teknolojia ya PAP kikiendelea
Kikao cha Kamati ya Uchukuzi, Viwanda, Mawasiliano, Nishati, Sayansi na Teknolojia ya PAP kikiendelea
Kikao cha Kamati ya Uchukuzi, Viwanda, Mawasiliano, Nishati, Sayansi na Teknolojia ya PAP kikiendelea
Kikao cha Kamati ya Uchukuzi, Viwanda, Mawasiliano, Nishati, Sayansi na Teknolojia ya PAP kikiendelea
Kikao cha Kamati ya Uchukuzi, Viwanda, Mawasiliano, Nishati, Sayansi na Teknolojia ya PAP kikiendelea

Kikao cha Kamati ya Uchukuzi, Viwanda, Mawasiliano, Nishati, Sayansi na Teknolojia ya PAP kikiendelea
Kikao cha Kamati ya Uchukuzi, Viwanda, Mawasiliano, Nishati, Sayansi na Teknolojia ya PAP kikiendelea leo Jumatatu Machi 13,2023.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog Midrand Afrika Kusini.


Share:

NIMEMFUMANIA MUME WANGU NA RAFIKI YANGU TENA KATIKA KITANDA CHANGU!

Share:

JIPATIE MGAO WA TSH 3M MERIDIANBET UKIJISAJILI NA KUCHEZA


Ofa za Meridianbet hazijawahi kuwa ndogo, ni promosheni juu ya Promosheni, mtaji mdogo sana wa kuanzia Tsh 5,000/= unashinda mgao wa bonasi ya TZS 3,000,000 kutoka hapa nyumba ya Odds kubwa na kasino ya mtandaoni yenye sloti rahisi kushinda kama Aviator, poker na Roulette. Ni hivi kwa salio dogo kabisa la kianzio cha Tsh 5,000/= unaweza kushinda mpaka Tsh 3M.

 

Jisajili, weka pesa katika akaunti yako na cheza moja ya sloti bomba kutoka kasino ya mtandaoni ya Meridianbet, uwe mmoja ya washindi wa mgao wa bonasi wa TZS 3,000,000 kwaajili ya kucheza michezo mbalimbali katika tovuti yetu. Odds kubwa za soka unazipata Meridianbet Kasino ya mtandaoni, sloti, Poker, Aviator na Roulette- Chagua Tukupe.

 

Jisajili kwenye APP au tovuti ya www.meridianbet.co.tz kuanzia tarehe 08.03.2023 mpaka tarehe 31.03.2023, na uweke angalau TZS 5,000 na soka na michezo ya kasino ya mtandaoni ujiwekee nafasi ya kushinda bonasi ya pesa ya TZS 1,000,000. Beti na Meridianbet mechi za ligi zote, odds ni kubwa sana, usikose pia Kasino ya mtandaoni ya Meridianbet yenye michezo rahisi ya sloti kama Poker, Aviator, Roulette.

 

Unavyoweka pesa zaidi, kubashiri kwa odds kubwa na kuzungusha – nafasi ya kushinda moja ya zawadi zetu inaongezeka. Ukiwa na meridianbet unaweza kubashiri mubashara, tembelea maduka ya meridianbet uweze kucheza michezo ya sloti na kasino ya mtandaoni.

 

Zawadi zitatolewa kama ifuatavyo:

Nafasi ya 1 – TZS 1,000,000 Bonasi ya pesa

Nafasi ya 2 – TZS 500,000 Bonasi ya pesa

Nafasi ya 3 – TZS 300,000 Bonasi ya pesa

Nafasi ya 4 – TZS 200,000 Bonasi ya pesa

Nafasi ya 5 mpaka 24 – TZS 50,000 Bonasi ya pesa

 

Vigezo na Masharti:

 

·       Promosheni itadumu kuanzia tarehe 08.03.2023 mpaka tarehe 31.03.2023 saa 5:59 usiku

·       Washindi watatangazwa tarehe 01.04.2023

·       Kwa kujisajili na www.meridianbet.co.tz wateja watakuwa wamekubaliana na vigezo na masharti ya promosheni.

·       Ofa hii ni kwa ajili ya mchezaji mmoja au IP adress mmoja pekee.

·       Meridianbet wakali wa kasino ya mtandaoni wana haki ya kutotoa zawadi, kusitisha au kubadili sheria za promosheni wakati wowote.

 

 



Share:

Sunday, 12 March 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU MACHI 13,2023





























Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger