Mazishi ya Mwandishi wa Habari Mwandamizi, Richard Makore aliyekuwa Mhariri wa gazeti la Nipashe Kanda ya Ziwa yamefanyika nyumbani kwake Kijiji cha Remong'orori Wilaya ya Serengeti mkoani Mara, Ijumaa Machi 10, 2023.
Makore aliyezaliwa mwaka 1978 alifariki Jumanne Machi 07, 2023 katika ajali ya basi la Sheraton iliyotokea katika eneo la Kasamwa mkoani Geita likitokea jijini Mwanza na kusababisha jumla ya vifo 10 na majeruhi kadhaa.
Mauti yalimkuta Makore akiwa safarini akielekea kwenye majukumu ya kikazi mkoani Geita.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG





























Kamati Kuu ya Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) kikiongozwa na Mwenyekiti wao Hashim Rungwe wakimsikiliza Mwezeshaji kutoka TGNP, Bw.Deogratius Temba (hayupo pichani) wakati akiwasilisha rasimu ya Sera ya Jinsia ya Chama cha CHAUMMA leo Machi 11, 2023 katika ofisi za Chama hicho Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) Hashim Rungwe akipendekez jambo mara baada ya Mwezeshaji kutoka TGNP, Bw.Deogratius Temba (hayupo pichani) kuwasilisha rasimu ya Sera ya Jinsia ya Chama cha CHAUMMA leo Machi 11, 2023 katika ofisi za Chama hicho Jijini Dar es Salaam.
Kamati Kuu ya Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) kikiongozwa na Mwenyekiti wao Hashim Rungwe wakipata picha ya pamoja na Mwezeshaji kutoka TGNP, Bw.Deogratius Temba mara baada ya kumisikiliza akiwasilisha rasimu ya Sera ya Jinsia ya chama hicho leo Machi 11, 2023 katika ofisi za CHAUMMA Jijini Dar es Salaam.
Kamati Kuu ya Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) kikiongozwa na Mwenyekiti wao Hashim Rungwe wakipata picha ya pamoja baada ya kusikiliza uwasilishwaji wa rasimu ya Sera ya Jinsia ya Chama hicho kutoka kwa Mwezeshaji wa TGNP, Bw.Deogratius Temba mara baada ya kumisikiliza akiwasilisha rasimu ya Sera ya Jinsia ya chama hicho leo Machi 11, 2023 katika ofisi za CHAUMMA Jijini Dar es Salaam.