Saturday, 11 March 2023
Friday, 10 March 2023
BRELA YATOA UFADHILI KWA WANAFUNZI 5 WANAOSOMA ‘MASTERS’ YA MILIKI UBUNIFU

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), imetoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi watano ambao wanasoma Shahada ya Uzamili katika fani ya Miliki Ubunifu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Ameongeza kuwa kwa kushirikiana Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wamefanikisha kuwepo kwa mafunzo hayo ya Miliki Bunifu ambayo kwa kiasi kikubwa yataongeza uelewa na kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
“Ndugu Waandishi wa Habari tumetoa ufadhili huu kwa kuzingatia jinsia na makundi maalum na kwa awamu hii tumefadhili wanafunzi watano na kiasi cha Shilingi Milioni Kumi na Sita Laki Tano na Elfu Hamsini (16,550,000/=) Kimetolewa”, amesema Bw. Nyaisa.
Amewataja wanafunzi hao waliopata ufadhili kuwa ni pamoja na Bi. Grace Ezekiel Mwaikono kutoka Mahakama Kuu, Bw. Stanslaus Aidan Kigosi kutoka BRELA, Bw. Addo November Mwasongwe kutoka Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bw. Eric Maximillian Mlasani kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Bi. Merciana Nehemiah Ntabaye kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Vilevile, ametaja lengo la ufadhili kwa wanafunzi hao kuwa ni kupanua wigo wa utaalamu katika nyanja ya Miliki Ubunifu kwakuwa eneo hilo muhimu halina wataalamu wengi hapa nchini, kuongeza ufahamu kuhusu Miliki Ubunifu kwa maendeleo chanya ya Taifa la Tanzania kutokana na umuhimu wake katika maendeleo endelevu ya kiuchumi na kijamii.
Ameongeza kuwa ufadhili huo utahamasisha wanufaika kutambua faida zinazopatikana kutokana na elimu kuhusu Miliki Ubunifu na jinsi ya kuitumia katika kuendeleza na kukuza Ubunifu nchini, kuweka mkazo mahsusi katika muunganisho wa sheria na sera za Miliki Ubunifu katika muktadha wa mienendo iliyopo ya kiuchumi na kijamii inayopatikana barani Afrika.
Kwa upande wake Dkt. Sosthenes Materu, ambaye ni Amidi wa Shule Kuu ya Sheria, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, amewashukuru BRELA kwa ufadhili huo sambamba na jitihada za Taasisi hiyo katika kuendeleza Miliki Ubunifu kwa ajili ya kuchochea maendeleo.
Mwailishi wa wanufaika wa ufadhili wa BRELA ambaye ametoka katika kundi la watu wenye mahitaji maalumu Bw. Erick Maximillian Mlasani, ameishukuru BRELA kwa ufadhili huo na kuahidi baada ya kuhitimu watakuwa miongoni mwa wataalamu watakaojitoa kwa jamii ili elimu ya Miliki Ubunifu ifike mbali zaidi.


PINDA ATAKA UWAJIBIKAJI WA PAMOJA KUONGEZA MADUHULI YA SERIKALI
Naibu Waziri Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Geofrey Pinda akiongea na Makamishna wa Wasaidizi wa Ardhi Nchini mapema leo Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Eng. Anthony Sanga akiteta na jambo na Makamishna wa Wasaidizi wa Ardhi Nchini mapema leo Jijini Dodoma.
Makamishna Wasaidizi wa Ardhi Nchini wakifuatilia jambo leo Jijini Dodoma katika Kikao Kazi kilichowakutanisha pamoja ili kujadili namna bora ya ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia pango la Ardhi.
Naibu Waziri Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Geofrey Pinda akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa Wizara pamoja na Makamishna Wasaidizi wa Ardhi mara baada ya kufunga kikao kazi na viongozi hao Jijini Dodoma.TUCTA: UWEKEZAJI KATIKA USALAMA NA AFYA UNALIPA




VIDEO NA NYIMBO ZA HOVYO MARUFUKU KWENYE MABASI YA SHULE

AUABC : PAP PLAYS A PROMINENT ROLE IN COMBATING CORRUPTION
SHOTI YA UMEME YAUA MWANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA NYUMBA IKIUNGUA SHINYANGA
Thursday, 9 March 2023
KAMATI YA SIASA YA CCM IMESELA YATAKA WATOTO WALE CHAKULA SHULENI
Na Halima Khoya,Shinyanga.
BARRICK NORTH MARA YAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE KWA KUWATAKA WANAWAKE KUCHANGAMKIA FURSA ZILIZOPO KATIKA SEKTA YA MADINI
Meneja wa Barrick nchini Tanzania, Dk. Melkiory Ngido,akishiriki kukata keki wakati wa hafla ya wanawake wa mgodi huo kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani.
Meneja wa Barrick nchini Tanzania, Dk.Melkiory Ngido, akiongea na Wafanyakazi Wanawake wa mgodi wa North Mara wakati wa kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani.
Wafanyakazi Wanawake wa Barrick North Mara, wakiwa katika picha ya pamoja na Meneja wa Barrick nchini Tanzania, Dk.Melkiory Ngido( katikati) na Meneja Mkuu wa mgodi huo,Apolinary Lyambiko wakati wa hafla ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika mgodini hapo.Meneja Mkuu wa Barrick Tanzania, Dk. Melkiory Ngido ,amewataka Wanawake kijiamini na kuchangamkia fursa mbalimbali zilizopo katika sekta ya uchimbaji wa madini.
DART WANAWAKE WAIPIGA JEKI HOSPITALI YA MBAGALA KWENYE MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI.
Mwenyekiti wa Wanawake wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) Mwanamvua Stambuli akizungumza mara baada ya Kukabidhi msaada Hospitali ya Mbagala Rangi Tatu ikiwa ni maadhimishi ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo hufanyika Machi 8 ya Kila mwaka.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mbagala Rangi Tatu Ally Makori akizungumza mara baada ya Kukabidhiwa msaada kutoka DART ikiwa ni maadhimishi ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo hufanyika Machi 8 ya Kila mwaka.
Mwenyekiti wa Wanawake DART Mwanamvua Stambuli akikabidhi moja ya Msaada kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya ikiwa ni maadhimishi ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo hufanyika Machi 8 ya Kila mwaka.

Baadhi ya picha mbalimbali ya Wanawake wa DART katika Hospitali ya Mbagala Rangi Tatu walipokwenda kutoa msaada kwenye maadhimisho ya Siku Wanawake Duniani ambayo huadhimishwa kila machi 8 ya Kila Mwaka.
**************
Na Mwandishi Wetu
Wanawake wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) Elimu ya Biashara (CBE) katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani wametoa msaada wa vitu mbalimbali Hospitali ya Mbagala Rangi Tatu kwa kuonyesha upendo kwa wananchi katika kujali afya zao.
Akizungumza wakati wa Kukabidhi msaada huo Mwenyekiti wa Wanawake wa DART Mwanamvua Stambuli amesema kuwa msaada huo ni kutokana na kutambua umhimu wananchi wa Mbagala kwani siku za usoni watakuwa wateja wa kutumia huduma za usafiri wa mabasi yao.
Amesema wanawake wa DART wameguswa kipekee na kujitoa kwa wanawake wanaojifungulia hapo kupata msaada wa mahitaji mbalimbali.
Msaada wa DART unamegharimu shilingi milioni Nane kwa kununua mashuka 40 , Baiskeli ya kubebea waginojwa , Sabunj ya vipande, sabuni ya unga , Dawa ya Mswaki, pamoja na mashine mbalimbali
Aidha amesema katika msaada waliotoa utasaidia kutatua baadhi ya changamoto kwani kama wanawake wametambua ni mahitaji wanawake ikiwemo mashuka kwa ajili ya hospitali hiyo.
Mwenyekiti huyo amesema licha ya kutoa msaada huo kwani itakuwa ndio mwendelezo kutokana na kutambua mahitaji ya hospitali hiyo.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mbagala Rangi Tatu Ally Makori ameshukuru msaada huo na kutaka baadhi ya Taasisi kuiga mfano mzuri kwa DART.
Amesema hospitali hiyo wanawake wanaojifungua katika hospitali hiyo kwa siku ni kati 30 hadi 40 hivyo msaada huo ni mkubwa kutokana na mahitaji ya wanawake hao.
Mmoja ya Mwanamke aliyejifungua katika Hospitali Asha Hamis amesema msaada huo kwao ni mkubwa kwani maadhimisho hayo yamegusa wanawake tulifika katika hospitali hiyo.
WAFANYAKAZI WANAWAKE GGML WATOA MSAADA WA VIFAA TIBA KATIKA HALMASHAURI YA GEITA
KIKUNDI cha wafanyakazi wa kike wanaofanya kazi katika kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML ladies) wanaofanya kazi mjini Geita, wametoa msaada wa vifaa tiba mbalimbali kwa ajili ya kuwasaidia kina mama wajawazito na wazazi wanaojifungua katika hospitali ya Nzela na kituo cha Afya Kasota zilizopo katika halmashauri ya Wilaya Geita.
Akizungumzia msaada huo uliotolewa jana Mjini Geita, Makamu mwenyekiti wa kikundi hicho, Lina Sitta alisema wanawake wanaofanya kazi GGML wameguswa na changamoto za uhaba wa vifaa tiba katika vituo vya afya katika vijiji vinavyowazunguka.
“Tumeona kwa sasa tuanze na vijiji vya Kasota na Nzela ambavyo vipo karibu zaidi na mgodi wa GGML na tumekuwa tukiona changamoto ya akina mama kukosa sabuni,taulo za mama waliojifungua na nepi za watoto.Msaada huu tumeutoa maalum kuadhimisha siku ya wanawake duniani," alisema.
Mganga Msaidizi wa kituo cha afya Kasota, Stanley Victor amewashukuru GGML ladies kwa kutoa msaada huo lakini pia kwa GGML kusaidia ujenzi wa maabara, nyumba ya mtumishi na jengo la baba na mtoto kituoni hapo.
“Mmeitendea haki siku ya wanawake duniani mwaka huu.Wagonjwa wengi waliopo hapa wamefarijika sana kutokana na msaada huu,”alisema.
Kauli mbiu ya siku ya wanawake duniani mwaka huu ni Ubunifu na mabadiliko ya teknolojia: chachu katika kuleta usawa wa kijinsia.


























