Monday, 6 March 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE MACHI 7,2023

























Share:

BEKI WA MTIBWA SUGAR IDDY MOBY AFARIKI DUNIA


Beki wa Mtibwa Sugar, Iddy Moby Mfaume amefariki dunia jana mchana katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, jijini Dodoma.


Kwa mujibu wa daktari wa Hospitali ya Kampuni ya Mtibwa Sugar, Khalid Sabuni, Mobby alipata tatizo la kiafya jana (Machi 4, 2023) mkoani Morogoro wakati akiwa katika mazoezi binafsi ya barabarani (roadwork) kuelekea mchezo wao wa #ASFC dhidi ya KMC.


“….akiwa anaelekea uwanjani, alianza kupata tatizo la kuumwa kichwa, kisha alisikia kizunguzungu na kutaka kuanguka lakini alipiga magoti”, amesema Dkt. Sabuni wakati akithibitisha kifo hicho.


Dkt. Sabuni amesema, Mobby alipelekwa katika hospitali hiyo ya kampuni, na kisha hospitali ya Bwagala kwa ajili ya matibabu zaidi lakini ilipofika usiku hali ilikuwa mbaya na hivyo kupewa rufaa kwenda Hospitali ya Benjamin Mkapa, jijini Dodoma ambako umauti umemfika.

“…..alifika Dodoma usiku lakini kufikia mchana wa leo akawa amefariki”, amehitimisha Dkt. Sabuni.

Iddy alisajiliwa Mtibwa Sugar msimu huu akitokea Ruvu Shooting lakini aliwahi pia kuzichezea timu za Geita Gold, Polisi Tanzania, na Mwadui FC kwa nyakati tofauti na pia aliwahi kuitwa katika kikosi cha timu ya taifa ‘Taifa Stars’.
Share:

WANAWAKE NACTVET WATOA MSAADA KWA WAFUNGWA GEREZA LA SEGEREA


Na. Mwandishi wetu

Wafanyakazi wanawake wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET), wametembelea gereza la Segerea, jijini Dar es Salaam, kutoa msaada wa taulo za kike (pads) kwa wanawake wafungwa na mahabusu katika gereza hilo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yanatakayofikia kilele chake tarehe 8 Machi.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo tarehe 6 Machi, 2023, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake NACTVET, Bi. Deborah Ngalemwa, amesema wanawake hao wameguswa kuwakumbuka wanawake wenzao wenye uhitaji kwa kutoa msaada. “Tunaamini kabisa kuwa wanawake wafungwa na mahabusu wa gereza hili ni binadamu ambao mifumo ya miili yao ni ya kawaida na wana haki ya kujihifadhi katika mazingira safi kimwili, hivyo tukaona kwa mwaka huu tuanze nao, lakini pia tuwe sehemu ya hamasa kwa watu wengine kusaidia makundi yenye uhitaji,” amesema Ngalemwa.

Aidha, Bi. Deborah ametoa wito kwa wanawake na watu mbalimbali kwenye jamii kuweka utaratibu wa kutenga kiasi kwenye kile wanachopata ili kusaidia jamii inayowazunguka hususan watu kwenye makundi mahsusi kama yatima, wajane na watoto wa mtaani, ili nao wajione wanathaminiwa kama watu wengine. Amewaomba wanawake walio gerezani watambue kwamba mahali walipo ni sehemu ya mafunzo ya muda ya kuboresha shughuli zao za kila siku.

Kwa upande wa uongozi wa gereza wametoa shukrani na pongezi kwa wanawake wa NACTVET kwa msaada huo kwani uhitaji ni mkubwa na kuwataka waendelee kusaidia makundi mengine yenye uhitaji bila kuwasahau Wafungwa wanaume ambao wamekuwa wanakumbukwa mara chache sana.
Share:

MCHECHU AKABIDHIWA RASMI OFISI YA HAZINA, AANZA MAJUKUMU YAKE

Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu ameanza rasmi majukumu yake baada ya kukabidhiwa ofisi na mtangulizi wake, Mgonya Benedicto jana katika Ofisi ya Msajili wa Hazina, Dar es Salaam. Mchechu ameteuliwa kushika wadhifa huo hivi karibuni na Mheshimiwa Rais Samia Saluhu Hassan. Kabla ya uteuzi huo, alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika na Nyumba la Taifa (NHC).
Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Ofisi ya Msajili wa Hazina jana mara baada ya kukabidhiwa rasmi ofisi.
Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu akizungumza na Menejimenti ya Ofisi ya Msajili wa Hazina jana baada ya kukabidhiwa rasmi ofisi na mtangulizi wake, Mgonya Benedicto.


(Picha na Ofisi ya Msajili wa Hazina)



Share:

NEMC KUHAMASISHA UTUNZAJI WA MAZINGIRA KUPITIA SHULE ZA MSINGI, SEKONDARI




Mkurugenzi Mkuu NEMC Dk. Samwel Gwamaka akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dodoma Katika ukumbi wa habari Maelezo.

Mkurugenzi Mkuu NEMC Dk. Samwel Gwamaka akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dodoma Katika ukumbi wa habari Maelezo.



Na Dotto Kwilasa, Malunde1 Blog-DODOMA.

Baraza la Taifa na Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)limepanga kuanzisha klabu za utunzaji wa mazingira kuanzia  ngazi ya shule za msingi na sekondari ili kuwajengea watoto  msingi mzuri wa namna ya kutunza na kuhifadhi mazingira katika maeneo yao.

Hayo yamebainishwa Leo March 3,2023 jijini hapa na Mkurugenzi Mkuu NEMC Dk.Samweli Gwamaka wakati akizungumza na wandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa majukumu wa baraza hilo  katika kipindi cha serikali ya awamu ya sita.

Amesema NEMC inaanzisha klabu za mazingira na kuzilea  kwa sababu watoto  wakianza kufundishwa wakiwa katika umri mdogo ni rahisi zaidi kuelewa umuhimu wakutunza mazingira na faida zake kijamii,kiuchumi na kiafya.


“Sasa tunajikita  kuelimisha na kukikamata kizazi cha watoto wadogo kuanzisha shule za msingi na sekondari ili wachukulie suala la utunzaji wa mazingira ni jukumu lao la kila siku katika mwenendo mzima wa maisha yao.Tunaamini watakapo kuwa wakubwa tabia itakuwa imejengeka ,”amesema .

Amesema Serikali ya Awamu ya Sita imeboresha usafi wa mazingira  ikiwa ni pamoja na kuhamasisha usafi wa kila jumamosi na  elimu kwa wananchi kupitia vyombo vya habari ambapo jitihada hizo zimesaidia kutokomeza ugonjwa wa kipindupindu ambao haujasikika nchini kwa miaka saba mfulululizo ikilinganishwa na miaka  ya nyuma  ikifika kipindi cha mvua lazima wapatikane wagonjwa,”alisema.

Pamoja na hayo Dk.Gwamaka ameeleza kuwa NEMC imeendelea kupokea na kushughulikia malalamiko taklibani 369 ya uchafuzi na uharibifu wa mazingira kutoka kwa wananchi ikiwemo kuvuja kwa mafuta kutoka kwenye bomba,kuchoma taka hatarishi chini ya kiwango,uchafuzi wa vyanzo vya maji,utiririshaji wa maji taka na uchafuzi wa hewa kutokana na shughuli za viwanda.

Malalamiko mengine wanayoyapokea ni kelele za mziki,kushamiri kwa gereji bubu maeneo ya makazi ya watu,kushamiri kwa vituo vya mafuta katikati ya makazi ya watu,matumizi ya mifuko ya plastiki, na kutoa elimu sahihi na suluhisho kuhusu jambo husika.

“Tumeendelea kufanya ukaguzi katika maeneo taklibani 2133 ya uwekezaji na mazingira yakiwemo maeneo ya mafuta na gesi, matanuru ya kuchomea takahatarishi,maeneo ya machimbo ya makaa yam awe,  pamoja na maeneo ya miradi mikubwa lengo ni kujiridhisha na uzingatiaji wa matakwa ya sheria ya mazingira ya mwaka 2004.

Ameeleza kuwa NEMC imepata mafanikio makubwa ndani ya serikali hii ya awamu ya sita ikiwemo kutokomeza mifuko  ya plastiki ambayo ilikuwa ni kikwazo chini ya uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hasaan na Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU MACHI 6,2023

















Share:

Sunday, 5 March 2023

GGML YAAHIDI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI, YACHANGIA 40% MAPATO YA DHAHABU


Makamu Rais wa Kampuni mama ya GGML, AngloGold Ashati – anayeshughulikia miradi endelevu Ghana na Tanzania, Simon Shayo akielezea mchango wa GGML katika mdahalo wa miaka miwili ya Serikali ya awamu ya sita madarakani chini ya Rais Samia Suluhu Hassan. Mdahalo huo umefanyika juzi mjini Geita.
*****


NA MWANDISHI WETU
KAMPUNI ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imeeleza kuridhishwa na juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan kuvutia wawekezaji na kuboresha sekta ya madini na kuifanya kampuni hiyo kuendelea kukua kila mwaka.


Pia imeahidi kuendelea kushirikiana na serikali kuhakikisha lengo la mchango wa sekta ya madini kufikia asilimia 10 ya pato ghafi la Taifa linafikiwa mwaka 2025 licha ya kwamba sasa limefikia asilimia 9.2


Kauli hiyo imetolewa jana na Makamu Rais wa Kampuni mama ya GGML, AngloGold Ashati – anayeshughulikia miradi endelevu Ghana na Tanzania, Simon Shayo wakati akizungumza kwa niaba ya wadau wa sekta ya madini katika madahalo wa miaka miwili ya Rais Samia madarakani.


Shayo alitolea mfano kuwa ripoti za karibuni kutoka Taasisi ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali za Madini, Mafuta, na Gesi Asilia (TEITI) zinaonesha GGML inachangia kati ya asilimia 30 na 40 ya mapato yote au dhahabu yote inayouzwa kwa sekta ya madini Tanzania.


“Kwetu hiyo ni faraja na hapa Geita tunaamini kwa kushirikiana na serikali ya mkoa na halmashauri yetu na wilaya zetu tunaweza kuufanya mgodi wetu ukazalisha zaidi na wakati wote mgodi uendelee kuzalisha zaidi ya wakia 500,000 kwa mwaka,” alisema.


Aidha, alisema wanaamini sekta madini inaweza kuvuka malengo yaliyowekwa na Serikali iwapo wawekezaji pamoja na wachimbaji wadogo wataendelea kujengewa mazingira bora ya uwekezaji.


“Tunaendelea kuiomba serikali chini ya uongozi wa Rais Samia kuendelea kutuwekea mazingira mazuri, tunaahidi kuongeza tija kwenye migodi yetu na sisi AngloGold Ashanti kupitia mgodi wetu wa GGML tunaamini wakati wote tutaendelea kuwa sehemu kubwa ya mafanikio hayo ya sekta ya madini,’ alisema.


Alisema uwepo wa GGML Tanzania, unajitafsiri si tu kwenye uchimbaji wa dhahabu na ulipaji wa kodi lakini kwenye uwekezaji kwenye jamii.


“Tunu yetu kubwa ni kwamba jamii ionekane kunufaika kwa sisi kuwepo hapa, tumejitahidi kwa uwezo wetu tangu tumeanza uchimbaji mjini Geita mwaka 2000 lakini tangu tumeanza kuingia makubaliano na halmashauri zetu kwa maana utekelezaji wa mpango wa CSR.


“Uwajibikaji wetu kwa jamii kupitia mpango ambao unasainiwa kwa pamoja tangu mwaka 2017, tumewekeza kila mwaka kati ya Sh bilioni 9.2. hadi 9.5 na mwaka huu tunaamini tutapata fursa ya kuunganisha mipango miwili ya mwaka 2022 na 2023 ambapo kwa wilaya ya Geita peke yake tutawekeza kiasi cha Sh bilioni 18.4,” alisema.


Alisema uwajibikaji wa GGML kwa jamii, unajitafsiri katika elimu, afya na kipato.


Aidha, alitoa ombi kwa Serikali kuendelea kuhakikisha wanachokifanya kwa jamii kinaongeza tija kusaidia serikali kupiga hatua zaidi kwenye huduma za jamii kwa wananchi wanaozunguka mgodi kunufaika.


Akizungumza katika mdahalo huo, Mkuu wa mkoa wa Geita, Martin Shigela alisema mkoa huo ndio namba moja kwa uzalishaji wa madini ya dhahabu kwani asilimia 60 ya mapato ya Taifa inatoka kwenye madini.


Alisema kwa miaka miwili iliyopita, wachimbaji wadogo na wakati wamezalisha kilo 13,000 sawa na tani 13.5 wakati migodi mikubwa kama GGML imezalisha kilo 35,000 sawa na tani 35.


“Mchango wetu katika kipindi cha miaka miwili unaonesha kuwa ardhi ya mkoa huu ina thamani ya Sh trilioni tano ambayo ni sawa na robo ya bajeti ya Taifa,’ alisema.


Alisema kwa kipindi cha miaka miwili, zaidi ya Sh bilioni 400 zimekusanywa kama mapato katika migodi inayochimba dhahabu Geita.


“Ukiangalia miaka ya nyuma hata asilimia 50 ya fedha ilikuwa haijafikiwa. Rais wetu amejenga mazingira uwekezaji, ametangaza nchi kimataifa na wawekezaji wanaweza kuja bila kuwa na hofu wala wasiwasi wowote,” alisema.
Share:

KAMPUNI YA ORYX GAS, TULIA ACKSON WAUNGANA KUWEZESHA WANAWAKE KUELEKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI


******************

Na Mwandishi Wetu

KATIKA kuelekea siku ya wanawake duniani mkoani Mbeya,Kampuni ya Oryx Gas kwa kushirikiana na Mfuko wa Tulia leo wameandaa tamasha kubwa ambapo Oryx Gas wameshindanisha vikundi 50 vya wanawake wanaojishughulisha na biashara za vyakula kupika vyakula mbalimbali vya kiasili na washindi wa kila kikundi wataondoka na zawadi ya majiko ya gesi na pesa jumla ya shilingi milioni tano.

Hatua ya kuandaa mashindano hayo ya vyakula kwa wanawake wanaojihusisha na biashara ya vyakula ni mojawapo ya jitihada kampuni hiyo inafanya katika kuelimisha Watanzania kutumia nishati safi ya kupikia kama mbadala wa kuni na mkaa.

Akizingumza mkoani Mbeya kuelekea Siku ya Mwanamke Dunia ambapo wameamua kuandaa mashindano hayo ya mapishi yaliyofanyika Machi 4,2023 , Meneja Masoko wa Kampuni ya Oryx Peter Ndomba ameelezea kwamba kumekuwepo na madhara makubwa ya kiafya,mazingira na kuichumi kutokana na jamii kutumia kuni na mkaa katika kupikia.

Hivyo amesema moja ya jitihada wanazofanya ni kuungana na Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia ili kuondokana na madhara na kuishi maisha bora.

"Tunaamini jitihada ambazo tumekuwa tunazifanya pia ni katika kutekeleza nia ya Rais Samia kuwa ifikapo mwaka 2030 angependa kuona zaidi ya asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia.Hivyo kwetu sisi tumeamua kuyabeba maono ya Rais na Serikali yake Kwa vitendo.

"Kwani tumekuwa tukitoa elimu kuhamasisha matumizi ya nishati ya gesi katika kupikia na tumekuwa tukigawa bure mitungi na majiko ya gesi kwa wananchi wa mikoa mbalimbali na leo tuko kwenye mashindano haya kwa lengo lile la kuendelea kuhimiza matumizi ya nishati safi katika kupikia,"amesema Ndomba.

Kuhusu ujumbe wao Kampuni hiyo kwa umma, Ndomba amesema wanawaomba wananchi walinde sana afya kwa kuepuka matumizi ya nishati chafu huku akifafanua katika kutoa hamasa mbalimbali wameanza kuona mabadiliko hasa kwa yale maeneo yaliyoathilika na ukataji miti.

"Hivyo basi tunazidi kuhamasisha wengi watumie gesi na ukweli ni kwamba Oryx Gas tunajivunia sana kukubalika na pia kuaminika na jamii na hii imetuwezesha kufikisha huduma sahihi ya gesi kila katika kila kijij cha Tanzania Bara na Zanzibar."
Share:

MCHENGERWA AANZA KWA KASI




*********************

👉 AONGOZA VIKAO VYA MABORESHO NA TAASISI ZAKE KWA ZAIDI YA MASAA 10

Na John Mapepele

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mohamed Mchengerwa leo Machi 5, 2023 ameongoza vikao vya maboresho na Watendaji na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya wizara hiyo kwa zaidi ya masaa kumi kujadili na kufanya mapitio mbalimbali ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa maelekezo ya viongozi wakuu wa nchi kwa lengo la kuimarisha uhifadhi wa raslimali kwa faida ya vizazi vya sasa na baadaye.

Katika vikao hivyo vilivyofanyika jijini Arusha, Mhe. Mchengerwa ameambatana na Naibu wake Mhe. Mary Masanja, Katibu Mkuu, Dkt. Hassan Abbasi, na Naibu Katibu Mkuu, Anderson Mutatembwa ambao pia wamepata fursa ya kushiriki kikamilifu katika kupitishwa kwenye sheria, kanuni na masuala mbalimbali yanayohusu uhifadhi na usimamizi wa rasilimali kwenye taasisi hizo.

“ Tumefanya mapitio na Watendaji wa wizara hii hasa Wakuu wa Taasisi ambazo zipo chini ya wizara hii na kufanya mapitio ya kina kabisa kwa siku nzima ya leo ambapo tumeona namna taasisi hizo zilivyoanzishwa na mwelekeo wa wizara na tunakotaka kuelekea na misingi ya utekelezaji wa maelekezo ya viongozi lengo likiwa pia kujenga matumaini kwa wananchi wetu” amefafanua Mhe. Mchengerwa mara baada ya kumaliza vikao hivyo.

Aidha, amesema katika vikao hivyo pia wameweza kujadili kwa kina sheria, kanuni na utekelezaji wa kazi za kila siku kwa kuzingatia kuwa kumekuwa na mabadiliko kwenye taasisi nyingi hususani baada ya kubadili mifumo ya kiraia na kufuata ile ya kijeshi katika usimamizi wa raslimali ambapo amesisitiza kuwa kumekuwa na mapungufu kadhaa ya kufanyiwa kazi na ameshaagiza kufanyiwa kazi mara moja.

“Kumekuwa na mapungufu makubwa sana ya kisheria , lakini pia kumekuwa na mapungufu mengi kwenye kanuni ambayo yanahitaji maboresho makubwa, kwa hiyo tunapaswa kufanya marekebisho ya haraka ili tuweze kufanya kazi ya uhifadhi wa raslimali kwa ufanisi zaidi, tayari tumeshapeana muda wa kufanya marekebisho haya mara moja, yale yanayonihusu mimi moja kwa moja nitayakamilisha haraka kwa wakati” ameongeza Mhe. Mchengerwa

Aidha, amesema katika vikao hivyo wameweza kukumbushana maelekezo mbalimbali yaliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ikiwa ni pamoja na viongozi wa taasisi kuhakikisha kuwa wanatoka na kwenda kufanya vikao mbalimbali na wananchi wanaozunguka maeneo husika ili kutoa uelewa wa kuhifadhi raslimali.

Amewataka kuwa karibu na jamii na kujenga umoja na mshikamano na kuwashirikisha wananchi katika mipango ya kulinda mifumo anuai ya ikolojia katika uhifadhi wa raslimali hali ambayo amesema kama itaboreshwa itasaidia sana kwa kuwa baadhi ya changamoto zinazojitokeza ni kwa sababu taasisi hazipo jirani na wananchi wanaowazunguka.
Share:

ALIYENG'ANG'ANIA MAPENZI AMUUA MWENZAKE



Neema Cheyo mkazi wa tarafa ya Bukene wilayani Nzega mkoani Tabora, amepoteza maisha baada ya mzazi mwenzake kumkata na kitu chenye ncha kali kinachodhaniwa kuwa ni panga katika maeneo mbalimbali ya mwili wake.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Richard Abwao amesema kuwa chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa mapenzi kwani mwanaume huyo alikuwa anang'ang'ania kuendelea na mahusiano hao licha ya wao kuachana.


"Tukio hilo limetokea Februari 21, 2023, majira ya saa 2:00 usiku ambapo baada ya kujeruhiwa na mzazi mwenzake alikimbizwa hospitali ya Nzega ambapo hali yake ilikuwa mbaya na alipoteza maisha, chanzo ni wivu wa mapenzi, Neema alikuwa hataki kurudiana na mwanaume wake wa zamani na alimpa laki nne ili mahusiano yavunjike lakini mwanaume huyo hakuridhika," amesema Kamanda Abwao.


Aidha Kamanda Abwao amesema kwamba mwanaume aliyehusika na mauaji hayo amekamatwa na atafikishwa mahakamani.
Share:

UNESCO, TIE YAWANOA WALIMU WATARAJIWA


*********************

UNESCO kupitia mradi wake wa O3 na O3 Plus kwa kushirikiana na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) yawanoa walimu watarajiwa waliopo Kwenye chuo kishiriki cha elimu Dar es salaam (DUCE) juu ya ufundishaji wa stadi za maisha, VVU, Afya ya Uzazi, ukatili wa kijinsia na kuhusiana Kwa heshima.

Wanafunzi 200 waliopo Kwenye masomo ya ualimu DUCE, wamepata fursa ya kufundishwa jinsi ya kutumia mfumo wa tehama wa Taasisi ya Elimu Tanzania wenye miongozo ya jinsi ya kufundisha wanafunzi kuhusu masuala ya stadi za maisha, VVU, Afya ya Uzazi, ukatili wa kijinsia na kuhusiana Kwa heshima Kwa kuzingatia umri na maadili.

UNESCO Kwa kupitia mradi wa O3 Plus inafanya kazi na vyuo vikuu na Vyuo Vya kati 16 Tanzania bara na Visiwani.

UNESCO inaunga mkono na kusaidia juhudi za serikali ili kuhakikisha elimu ya kina ya stadi za maisha inayozingatia afya ya uzazi, VVU/UKIMWI na unyanyasaji wa kijinsia inawafikia vijana wote kwa kuzingatia umri, maadili na tamaduni za kitanzania.. Kwa kusaidiana na TET UNESCO imesaidia kuweka miongozo ya kufundishia mada hizo mtandaoni.
Share:

OSHA KUENDELEA KUWACHUKULIA HATUA WANAOKIUKA KANUNI MAHALA PA KAZI


Mtendaji Mkuu wa OSHA Khadija Mwenda akizungumza na Waandishi wa habari leo Jijini Dodoma Katika ukumbi wa habari Maelezo kuhusu utekelezaji wa majukumu yake.

****


Na Dotto Kwilasa,DODOMA

WAKALA wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) umeyatoza faini maeneo ya kazi ambayo hayakuzingatia sheria na kanuni ikiwa ni pamoja na kuyachukulia hatua mbali mbali za kisheria zikiwemo kupewa hati ya maboresho ambapo  maeneo ya kazi 1,588 yalipewa hati hizo huku 105 yalitozwa faini.

Mtendaji Mkuu wa OSHA Khadija Mwenda amesema hayo leo March 4,2023 Jijini Dodoma wakati akizungumza na wandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa majukumu yake katika kipindi cha miaka miwili ya Serikali ya awamu ya sita na kwamba hatua hiyo imeboresha usalama na afya kwa lengo la kuzuia ajali, magonjwa na vifo vitokanavyo na kazi.

Amesema, katika kuimarika kwa shughuli za usimamizi wa usalama na afya mahali pa kazi OSHA imefanikiwa kuongeza idadi ya maeneo ya kazi yaliyosajiliwa kutoka 4,336 hadi 11,953 ongezeko hilo ni sawa asimilia 276.

"Idadi ya kaguzi zilizofanyika zimeongezeka kutoka kaguzi 104,203 hadi kufikia Kaguzi 322,241 sawa na asilimia 132,kumekuwa na ongezeko la asilimia 175 ya wafanyakazi waliopata mafunzo ya Usalama na afya mahali pa kazi kutoka wafanyakazi 32,670 hadi kufikia wafanyakazi 43,318;

Mafunzo hayo yanajumuisha mafunzo ya usimamizi wa masuala ya usalama na afya mahali pa kazi na uundwaji wa kamati za usalama na afya ,mafunzo ya kufanya kazi za mazingira ya juu  mafunzo ya huduma ya kwanza, mafunzo ya usalama na afya katika sekta ya mafuta na gesi na katika sekta ya ujenzi na majenzi na mafunzo ya usalama wa mitambo," amesema.

Mkurugenzi huyo pia amesema OSHA imeongeza kasi  upimaji afya za wafanyakazi kwa asilimia 320 kutoka wafanyakazi 363,820 hadi kufikia  milioni 1.1 na kwamba ongozeko hilo ni tafsiri kwamba hali ya usalama na afya  katika maeneo ya kazi inazidi kuimarika.

"Kuhusu kupungua kwa ajali na magonjwa yatokanayo na kazi Khadija OSHA ilichunguza  ajali mbali mbali zinazotokea katika sehemu za kazi kwa lengo la kubaini vyanzo vya ajali hizo ili kushauri namna bora ya kuzuia ajali kutokea tena;

Vile vile kutokana na hatua mbalimbali zilizochukuliwa  ajali zilizoripotiwa zilipungua kwa asilia 13.2 kutoka ajali 2,138 kupungua hadi kufika 1,855,"amefafanua.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger