Friday, 3 March 2023

WEADO WAENDESHA KAMPENI YA CHANJO YA UVIKO-19, KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA KIJIJI CHA ILOBASHI WILAYANI SHNYANGA


Wananchi wa kijiji cha Ilobashi Kata ya Masengwa wilayani Shinyanga wakiwa kwenye Kampeni ya uhamasa ya Chanjo ya UVIKO-19, pamoja na kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia zikiwamo mimba na ndoa za utotoni kutoka Shirika la WEADO.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

SHIRIKA la Women Elderly Advocacy And Development Organization (WEADO) limeendesha Kampeni ya kuhamasisha wananchi hasa makundi ya Wanawake, Vijana na Wazee kuchanja Chanjo ya UVIKO-19 katika kijiji cha Ilobashi Kata ya Masengwa wilayani Shinyanga.

Zoezi hilo la Hamasa ya Kampeni ya Chanjo ya UVIKO-19, imefanyika leo Machi 3, 2023 na kutolewa na wataalamu wa Afya na viongozi wa Kata ya Masengwa, kwa ufadhili wa Shirika la watoto Duniani UNICEF kupitia Mdau kiongozi Help Age Tanzania.

Elimu hiyo ya Hamasa ya Chanjo ya UVIKO-19 imeendana pia na Kampeni ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia likiwamo tatizo la mimba na ndoa za utotoni, kwa ufadhili wa Shirika la Foundation For Civil Society.

Mganga kutoka Zahanati ya Ilobashi Dk. Victor Thomas, akitoa elimu ya Chanjo ya UVIKO-19 kwa wananchi wa Kijiji cha Ilobashi, amewasihi wajitokeze kwa wingi kuchanja ikiwa Chanjo ni salama na adhina madhara yoyote, na kupuuza upotoshaji ambao umekuwa ukienezwa dhidi ya Chanjo hiyo.

Amesema tangu Chanjo ya UVIKO-19 ianze kutolewa hapa nchini hakuna mtu yoyote ambaye amelalamika kupata madhara ya kiafya, na kuwasihi wananchi wajitokeze kupata Chanjo ili wapate Kinga ambayo itawalinda siku wakipata maambukizi ya virusi vya Corona wasipate madhara makubwa.

“Wananchi Chanjo ya UVIKO-19 ni salama na haina madhara yoyote na inatolewa bure hakuna malipo, jitokezeni kuchanja ili muwe salama siku mkipata maambukizi ya virusi vya Corona,”amesema Dk. Thomas.

Naye Katibu wa Baraza la Wazee mkoani Shinyanga Anderson Lyimo ambaye pia ni Katibu wa Baraza la Wazee Taifa, amewataka Wazee kujitokeza kwa wingi kupata Chanjo ya UVIKO-19, na kupuuza upotoshaji sababu wao kinga zao zimeshashuka ili wajilinde na ugonjwa wa Virusi vya Corona pale watakapopata maambukizi.

Kwa upande wake Ofisa Maendeleo Kata ya Masengwa wilayani Shinyanga Atupokile Maseta, akizungumzia masuala ya kupinga ukatili, amewataka wananchi wapaze sauti pale wanapokuwa wakifanyiwa vitendo vya ukatili, na siyo kunyamaza kimya, pamoja na kutoa ushirikiano mahakamani ili watuhumiwa wafungwe jela na kuacha kumaliza kesi kimya kimya ili kutokomeza tatizo hilo.

Aidha, Shirika la WEADO linatekeleza Mradi wa Kampeni ya kuhamasisha Chanjo ya UVIKO-19 kwa wananchi hasa makundi ya Wazee, Vijana na Wanawake, pamoja na kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia zikiwamo mimba na ndoa za utotoni wilayani Shinyanga.

Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Shinyanga Lidya Kwesigabo akitoa elimu ya hamasa ya Chanjo ya UVIKO-19, pamoja na kupinga vitendo vya ukatili zikiwamo mimba na ndoa za utotoni kwa Wananchi wa Kijiji cha Ilobashi Kata ya Masengwa wilayani Shinyanga.

Afisa Maendeleo ya jamii Kata ya Masengwa wilayani Shinyanga Atupokile Maseta akitoa elimu ya hamasa ya Chanjo ya UVIKO-19, pamoja na kupinga vitendo vya ukatili zikiwamo mimba na ndoa za utotoni kwa Wananchi wa Kijiji cha Ilobashi.

Mganga wa Zahanati ya Ilobashi wilayani Shinyanga Dk. Victor Thomasi akitoa elimu ya hamasa ya Chanjo ya UVIKO-19 kwa wananchi wa Kijiji cha Ilobashi Kata ya Masengwa wilayani Shinyanga.

Katibu wa Baraza la Wazee mkoani Shinyanga Anderson Lyimo akitoa elimu ya hamasa ya Chanjo ya UVIKO-19, pamoja na kupinga vitendo vya ukatili kwa wananchi wa Kijiji cha Ilobashi Kata ya Masengwa wilayani Shinyanga.


Mwezeshaji wa masuala ya kupinga vitendo vya ukatili katika Kijiji cha Ilobashi Kata ya Masengwa wiayani Shinyanga Mary Lutinya akitoa elimu ya kupinga vitendo vya ukatili ndani ya jamii zikiwamo mimba na ndoa za utotoni.

Wananchi wa Kijiji cha Ilobashi Kata ya Masengwa wilayani Shinyanga wakiwa kwenye elimu ya hamasa ya kuchanja Chanjo ya UVIKO-19, pamoja na kupinga vitendo ya ukatili wa kijinsia zikiwamo mimba na ndoa za utotoni.

Elimu ya hamasa ya Chanjo ya UVIKO-19 ikiendelea pamoja na kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia zikiwamo mimba na ndoa za utotoni.

Elimu ya hamasa ya Chanjo ya UVIKO-19 ikiendelea pamoja na kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia zikiwamo mimba na ndoa za utotoni.

Elimu ya hamasa ya Chanjo ya UVIKO-19 ikiendelea pamoja na kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia zikiwamo mimba na ndoa za utotoni.

Elimu ya hamasa ya Chanjo ya UVIKO-19 ikiendelea pamoja na kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia zikiwamo mimba na ndoa za utotoni.

Elimu ya hamasa ya Chanjo ya UVIKO-19 ikiendelea pamoja na kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia zikiwamo mimba na ndoa za utotoni.

Elimu ya hamasa ya Chanjo ya UVIKO-19 ikiendelea pamoja na kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia zikiwamo mimba na ndoa za utotoni.

Elimu ya hamasa ya Chanjo ya UVIKO-19 ikiendelea pamoja na kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia zikiwamo mimba na ndoa za utotoni.
Elimu ya hamasa ya Chanjo ya UVIKO-19 ikiendelea pamoja na kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia zikiwamo mimba na ndoa za utotoni.

Elimu ya hamasa ya Chanjo ya UVIKO-19 ikiendelea pamoja na kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia zikiwamo mimba na ndoa za utotoni.

Elimu ya hamasa ya Chanjo ya UVIKO-19 ikiendelea pamoja na kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia zikiwamo mimba na ndoa za utotoni.

Elimu ya hamasa ya Chanjo ya UVIKO-19 ikiendelea pamoja na kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia zikiwamo mimba na ndoa za utotoni.

Elimu ya hamasa ya Chanjo ya UVIKO-19 ikiendelea pamoja na kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia zikiwamo mimba na ndoa za utotoni.

Elimu ya hamasa ya Chanjo ya UVIKO-19 ikiendelea pamoja na kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia zikiwamo mimba na ndoa za utotoni.

Elimu ya hamasa ya Chanjo ya UVIKO-19 ikiendelea pamoja na kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia zikiwamo mimba na ndoa za utotoni.

Elimu ya hamasa ya Chanjo ya UVIKO-19 ikiendelea pamoja na kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia zikiwamo mimba na ndoa za utotoni.

Elimu ya hamasa ya Chanjo ya UVIKO-19 ikiendelea pamoja na kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia zikiwamo mimba na ndoa za utotoni.

Mganga wa Zahanti ya Ilobashi Dk. Victor Thomasi (kulia) akichanja Chanjo ya UVIKO-19 kwa wananchi ambao wamehamasika na kupata Chanjo kwenye Kampeni hiyo ya Shirika la WEADO.

Mganga wa Zahanati ya Ilobashi Dk. Victor Thomasi (kulia) akichanja Chanjo ya UVIKO-19 kwa wananchi ambao wamehamasika na kupata Chanjo kwenye Kampeni hiyo ya Shirika la WEADO.

Mganga wa Zahanati ya Ilobashi Dk. Victor Thomasi (kulia) akichanja Chanjo ya UVIKO-19 kwa wananchi ambao wamehamasika na kupata Chanjo kwenye Kampeni hiyo ya Shirika la WEADO.

Hamasa wakitoa burudani kwenye kampeni ya Chanjo ya UVIKO-19, pamoja na kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia zikiwamo mimba na ndoa za utotoni katika Kijiji cha Ilobashi Kata ya Masengwa wilayani Shinyanga.
Share:

NEMC KUHAMASISHA UTUNZAJI WA MAZINGIRA KUPITIA SHULE ZA MSINGI, SEKONDARI




Mkurugenzi Mkuu NEMC Dk. Samwel Gwamaka akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dodoma Katika ukumbi wa habari Maelezo.

Mkurugenzi Mkuu NEMC Dk. Samwel Gwamaka akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dodoma Katika ukumbi wa habari Maelezo.



Na Dotto Kwilasa, Malunde1 Blog-DODOMA.

Baraza la Taifa na Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)limepanga kuanzisha klabu za utunzaji wa mazingira kuanzia  ngazi ya shule za msingi na sekondari ili kuwajengea watoto  msingi mzuri wa namna ya kutunza na kuhifadhi mazingira katika maeneo yao.

Hayo yamebainishwa Leo March 3,2023 jijini hapa na Mkurugenzi Mkuu NEMC Dk.Samweli Gwamaka wakati akizungumza na wandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa majukumu wa baraza hilo  katika kipindi cha serikali ya awamu ya sita.

Amesema NEMC inaanzisha klabu za mazingira na kuzilea  kwa sababu watoto  wakianza kufundishwa wakiwa katika umri mdogo ni rahisi zaidi kuelewa umuhimu wakutunza mazingira na faida zake kijamii,kiuchumi na kiafya.


“Sasa tunajikita  kuelimisha na kukikamata kizazi cha watoto wadogo kuanzisha shule za msingi na sekondari ili wachukulie suala la utunzaji wa mazingira ni jukumu lao la kila siku katika mwenendo mzima wa maisha yao.Tunaamini watakapo kuwa wakubwa tabia itakuwa imejengeka ,”amesema .

Amesema Serikali ya Awamu ya Sita imeboresha usafi wa mazingira  ikiwa ni pamoja na kuhamasisha usafi wa kila jumamosi na  elimu kwa wananchi kupitia vyombo vya habari ambapo jitihada hizo zimesaidia kutokomeza ugonjwa wa kipindupindu ambao haujasikika nchini kwa miaka saba mfulululizo ikilinganishwa na miaka  ya nyuma  ikifika kipindi cha mvua lazima wapatikane wagonjwa,”alisema.

Pamoja na hayo Dk.Gwamaka ameeleza kuwa NEMC imeendelea kupokea na kushughulikia malalamiko taklibani 369 ya uchafuzi na uharibifu wa mazingira kutoka kwa wananchi ikiwemo kuvuja kwa mafuta kutoka kwenye bomba,kuchoma taka hatarishi chini ya kiwango,uchafuzi wa vyanzo vya maji,utiririshaji wa maji taka na uchafuzi wa hewa kutokana na shughuli za viwanda.

Malalamiko mengine wanayoyapokea ni kelele za mziki,kushamiri kwa gereji bubu maeneo ya makazi ya watu,kushamiri kwa vituo vya mafuta katikati ya makazi ya watu,matumizi ya mifuko ya plastiki, na kutoa elimu sahihi na suluhisho kuhusu jambo husika.

“Tumeendelea kufanya ukaguzi katika maeneo taklibani 2133 ya uwekezaji na mazingira yakiwemo maeneo ya mafuta na gesi, matanuru ya kuchomea takahatarishi,maeneo ya machimbo ya makaa yam awe,  pamoja na maeneo ya miradi mikubwa lengo ni kujiridhisha na uzingatiaji wa matakwa ya sheria ya mazingira ya mwaka 2004.

Ameeleza kuwa NEMC imepata mafanikio makubwa ndani ya serikali hii ya awamu ya sita ikiwemo kutokomeza mifuko  ya plastiki ambayo ilikuwa ni kikwazo chini ya uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hasaan na Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango.
Share:

TEA KWA KUSHIRIKIANA NA TAHA YAFIKISHA KILIMO CHA BUSTANI KWA VIJANA 400

Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Elimu Tanzania Bi. Bahati Geuzye (Kulia) akisisitiza jambo alipokutana na Afisa Mtendaji Mkuu wa TAHA Bi. Jacqueline Mkindi (wa pili kushoto) ofisini kwake Jijini Arusha. Kulia kwake ni Mratibu wa Mafunzo wa TAHA Bi. Loveness Adolf na kushoto ni Meneja miradi kutoka TEA Bw. Masozi Nyirenda
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania Bi. Bahati Geuzye akiwa ameongozana na Bw. Lugano Ipyana mnufaika wa mafunzo ya Kuendeleza Ujuzi wakielekea kwenye mashamba anayolima mnufaika huyo kukagua. Wengine ni Masozi Nyirenda Meneja Miradi –TEA (Kushoto) na Simon Mlay Msaidizi Mkuu wa Mkurugenzi – TAHA (Kulia)

Bahati Geuzye, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) akiangalia matunda aina ya Karela (Bitter Gourd) yanayolimwa na mnufaika wa Mafunzo ya Ujuzi Lugano Ipyana, aliyepata mafunzo hayo kupitia Taasisi ya TAHA ya Jijini Arusha

Mnufaika wa Mafunzo ya Kuendeleza Ujuzi Irene Mollel akimuelezea Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania Bahati Geuzye jinsi alivyonufaika na mafunzo hayo yaliyotolewa na Taasisi ya TAHA Jijini Arusha. Kushoto ni Masozi Nyirenda, Meneja Miradi kutoka TEA

Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Elimu Tanzania Bahati Geuzye (wa tatu kulia) pamoja na wataalam wa kilimo kutoka TAHA wakikagua mmea wa nyanya kwenye shamba la mnufaika wa Mafunzo ya Ujuzi Jijini Arusha.

Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Elimu Tanzania Bahati Geuzye (wa pili kulia) kwenye picha ya pamoja na mnufaika wa Mafunzo ya Ujuzi na wataalam wa kilimo kutoka TAHA Jijini Arusha.

**********************

Na Mwandishi Wetu

Matokeo ya Sensa ya watu na Makazi iliyofanyika mwaka 2022 nchini Tanzania yalibainisha kuwa, asilimia 34.5 ya watanzania wote ni vijana ambao ndio nguvu kazi ya Taifa. Serikali imeendelea na jitihada mbalimbali za kuhakikisha vijana wanahusishwa kikamilifu katika miradi na programu za maendeleo kupitia mafunzo ya ujuzi na Ufundi stadi ili kupunguza tatizo la ajira kwa vijana katika ngazi zote.

Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) katika kuunga mkono jitihada hizo za Serikali, ilitoa ruzuku kwa ajili ya Mafunzo ya Kuendeleza Ujuzi katika sekta ya Kilimo kupitia Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (SDF), kwa Taasisi inayojihusisha na Kilimo-Biashara cha Bustani na Mbogamboga (TAHA) mwaka 2021 kwa lengo la kunufaisha vijana 400 kwa kuwajengea uwezo kuhusu kilimo cha bustani (horticulture).

Kupitia ruzuku hiyo ya Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (SDF), jumla ya vijana 437 wamenufaika na mafunzo hayo ambayo yalifanyika katika maeneo mbalimbali ya Jijini Arusha yakitolewa na Taasisi ya TAHA na hadi sasa asilimia 90 ya vijana hao ni wakulima wakubwa wa mbogamboga na matunda wanaofurahia soko la ndani na nje ya Tanzania.

Gilliad Daniel Kiongozi wa Uzalishaji (Production Lead) kutoka TAHA anasema, ruzuku waliyopewa kupitia Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (SDF) imeleta mabadiliko chanya ndani ya Taasisi yao kupitia programu ya kuendesha mafunzo ya kuwajengea vijana uwezo katika Kilimo cha Bustani baada ya muitikio kuwa mkubwa tofauti na walivyotarajia.

‘‘Makubaliano ya mradi yalikuwa ni kuwafikia vijana 400 hadi unakamilika kwa maana ya kutoa mafunzo ila tulishangaa vijana walivyochangamkia fursa hiyo, mwisho tukafundisha 37 zaidi na hivyo kuwa na idadi ya wanufaika 437, alisema Gilliad’’

Aidha, TEA ilitoa ruzuku kwa Taasisi ya TAHA kupitia Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (SDF) kwa lengo la kufadhili mafunzo ya ujuzi kwa vijana katika Sekta ya Kilimo kama moja ya sekta za kipaombele ikizingatia kuwa, sekta hii ina mchango mkubwa katika uchumi wa Tanzania. Takwimu na machapisho mbalimbali yamekuwa yakionyesha kuwa asilimia 90 ya ardhi ya Tanzania hulimwa na wakulima wadogo na sekta ya kilimo inatoa ajira kwa asilimia 65.5 na inachangia asilimia 29.1 ya pato la Taifa, asilimia 30 ya soko la nje na asilimia 65 ya malighafi za viwandani

Hivi karibuni, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bi. Bahati Geuzye alifanya ziara ya kikazi Jijini Arusha mwanzoni mwa wiki kwa lengo la kukutana na uongozi wa TAHA lakini pia kuwatembelea baadhi ya wanufaika wa mafunzo hayo ya ujuzi kuona maendeleo yao baada ya kujengewa uwezo kupitia ruzuku ya Mfuko wa SDF

Katika ziara hiyo, Geuzye alifurahia kuona wanufaika wanaendeleza kilimo kwa kutumia utaalam walioupata chini ya TAHA lakini pia alifarijika kusikia kwamba kwao soko siyo changamoto tena maana mafunzo waliyopatiwa yanawasaidia kuzalisha bidhaa zenye ubora kulingana na mahitaji ya soko.

‘‘Nafarijika sana kuona hamkurudi nyuma baada ya mafunzo maana vijana wengi hawapendi kazi za kilimo kutokana na changamoto mbalimbali. Ni wakati muafaka sasa vijana wengine wajifunze kuthubutu na kutokukata tamaa kupitia kwenu mliofanikiwa katika sekta hii, alisema Geuzye’’

Geuzye aliongeza kwamba, Serikali inatambua mchango wa vijana katika kukuza uchumi wa nchi lakini pia mchango wa sekta ya kilimo katika kukuza pato la Taifa. Ndiyo maana vijana wanahamasishwa kuwekeza kwenye sekta hii, kupitia fursa mbalimbali zinazotolewa na Serikali, wadau na Sekta binafsi kwani kilimo ni muhimili wa maendeleo kwa nchi yetu.

Lugano Ipyana mmoja wa wanufaika alithibitisha hayo kwanza kwa kuishukuru Serikali kwa kuwathamini vijana kisha akasema, yeye alisoma hadi ngazi ya stashahada na kufanikiwa kufanya kazi na makampuni mbalimbali ya watu binafsi ila hakuridhika na kipato alichokuwa akipata kazini kwake hivyo aliamua kutafuta kitu kingine cha ziada cha kumuongezea kipato.

Ipyana anafafanua kwamba, mwaka 2021 alisikia tangazo la kuwezesha vijana kuwajengea uwezo kufanya kilimo cha bustani lililotolewa na TAHA na bila kusita alituma maombi akafanikiwa kuchaguliwa. Mafunzo yalikuwa ya muda mfupi na walijikita zaidi kwenye mafunzo kwa vitendo kitu ambacho kilimjengea uwezo wa kujiamini katika kile alichokuwa anakifanya.

Anafafanua kwamba, wakati wa mafunzo alikuwa na shamba lenye ukubwa wa ekari moja na ndilo alilolitumia kama shamba la majaribio kwa kulima nyanya na pilipili hoho. Wataalam wa kilimo cha bustani kutoka TAHA walimfungia miundombinu ya umwagiliaji na wakamuwezesha pembejeo zikiwemo mbegu na madawa na baadae wakamuunganisha na masoko kwa ajili ya kuuza mazao yake.

‘‘Kwa sasa nina zaidi ya ekari 5 ambazo ninaweza kulima aina 5 za mazao kwa wakati mmoja. Pia nashukuru nilikuwa natamani sana kuzalisha bidhaa kwa ajili ya soko la nje na nimefanikiwa, mara ya kwanza nililima maharage (French Beans) nikapata tani 2 ambazo niliuza takribani milioni 16, alisema Ipyana’’.

Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (SDF) unaoratibiwa na TEA umeleta mabadiliko chanya kwa vijana kupitia mafunzo ya elimu ya ufundi na stadi za kazi. Takribani vijana 35,000,000 wamenufaika na mafunzo hayo katika sekta sita za kipaombele. Sekta hizo ni utalii na huduma za ukarimu, nishati, kilimo biashara, ujenzi, uchukukuzi na TEHAMA.

Share:

MWAKILISHI WA JIMBO LA MTAMBWE HABIB ALI MOHAMED AFARIKI DUNIA


Habib Ali Mohamed.

MWAKILISHI wa Jimbo la Mtambwe, visiwani Zanzibar, kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Habib Ali Mohamed, amefariki dunia, wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Saiffe, jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Habari, Uenezi, Mawasiliano na Umma ACT-Wazalendo, Salim Biman, Mohamed amefariki dunia alfajiri ya leo tarehe 3 Machi 2023.

“Chama cha ACT-Wazalendo kinatuma salamu za pole Kwa Spika wa Baraza la Wawakilishi, wananchi wa Mtambwe, ndugu, jamaa na marafiki wote wa marehemu Mohamed, kwa kuondokewa na kiongozi wetu, mwanafamilia na mpendwa wetu,” imesema taarifa ya Bimani.

Kupitia taarifa hiyo, Bimani amesema ratiba ya mazishi itatolewa baadae baada ya chama hicho kushauriana na famili ya marehemu Mohamed.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA MACHI 3,2023




Magazeti ya leo Ijumaa March 3 2023



Share:

UNAWEZA KUPATA KAZI KWA URAHISI KUPITIA MTU HUYU!

Share:

Thursday, 2 March 2023

WAZIRI MABULA ASHIRIKI MSIBA WA MKE WA MZEE PHILEMON PARSHUKU OLASITI ARUSHA

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akisalimiana na familia ya marehemu Bi. Naserian Parshuku alipokwenda kutoa pole kwa mume wa marehemu Philemon Parshuku eneo la Kimindorosi Olisiti Arusha tarehe 1 Machi 2023.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akisaini kitabu cha maombolezo cha marehemu Bi. Naserian Parshuku alipokwenda kutoa pole kwa mume wa marehemu Philemon Parshuku eneo la Kimindorosi Olisiti Arusha tarehe 1 Machi 2023.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akimpa pole mzee Philemon Parshuku eneo la Kimindorosi Olisiti jijini Arusha kufuatia kufiwa na mkewe Bi. Naserian Parshuku. waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na waombolezaji wakati wa msiba wa mke wa mzee Philemon Parshuku eneo la Kimindorosi Olisiti jijini Arusha.

Sehemu ya waombolezaji wakiwa katika msiba wa marehemu Bi Naserian Parshuku eneo la Kimindorosi Olisiti jijini Arusha.

Mzee Philemon Parshuku aliyefiwa na mkewe akiwa na waombolezaji wengine eneo la Kimindorosi Olisiti jijini Arusha.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiwa katika picha na wajumbe wa chama cha mapinduzi. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger