Friday, 24 February 2023

BANDARI YA DAR ES SALAAM YAIAKIKISHIA NEMC KUENDELEA KUPUNGUZA UCHAFUZI WA MAZINGIRA KWENYE BAHARI

Mkurugenzi Mkuu wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Mrisho Mrisho akizungumza na Bodi na Menejimenti ya NEMC mara baada ya NEMC kutemebelea eneo la upanuzi wa Bandari ya Jijini Dar es Salaam kuona utekelezaji wa masharti ya cheti cha mazingira pamoja na kuhakikisha maeneo yale ambayo udongo unaochimbwa kwenye maeneo hayo na sehemu inapokwenda kuhifadhiwa pawe ni sehemu salama pasiweze kuathiri mazingira katika maeneo hayo.

Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt. Samuel Gwamaka (katikati) akiwa na Mwenyekiti wa Bodi NEMC, Prof.Mhandisi Esnat Chaggu ( wa kwanza kulia) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Mrisho Mrisho wakitembelea eneo la upanuzi wa Bandari ya Jijini Dar es Salaam kuona utekelezaji wa masharti ya cheti cha mazingira pamoja na kuhakikisha maeneo yale ambayo udongo unaochimbwa kwenye maeneo hayo na sehemu inapokwenda kuhifadhiwa pawe ni sehemu salama pasiweze kuathiri mazingira katika maeneo hayo.Mkurugenzi Mkuu wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Mrisho Mrisho akizungumza na Bodi na Menejimenti ya NEMC mara baada ya NEMC kutemebelea eneo la upanuzi wa Bandari ya Jijini Dar es Salaam kuona utekelezaji wa masharti ya cheti cha mazingira pamoja na kuhakikisha maeneo yale ambayo udongo unaochimbwa kwenye maeneo hayo na sehemu inapokwenda kuhifadhiwa pawe ni sehemu salama pasiweze kuathiri mazingira katika maeneo hayo.

Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt. Samuel Gwamaka akizungumza mara baada ya Bodi na Menejimenti ya NEMC kutembelea eneo la upanuzi wa Bandari ya Jijini Dar es Salaam kuona utekelezaji wa masharti ya cheti cha mazingira pamoja na kuhakikisha maeneo yale ambayo udongo unaochimbwa kwenye maeneo hayo na sehemu inapokwenda kuhifadhiwa pawe ni sehemu salama pasiweze kuathiri mazingira katika maeneo hayo. Mwenyekiti wa Bodi NEMC, Prof.Mhandisi Esnat Chaggu akizungumza mara baada ya Bodi na Menejimenti ya NEMC kutembelea eneo la upanuzi wa Bandari ya Jijini Dar es Salaam kuona utekelezaji wa masharti ya cheti cha mazingira pamoja na kuhakikisha maeneo yale ambayo udongo unaochimbwa kwenye maeneo hayo na sehemu inapokwenda kuhifadhiwa pawe ni sehemu salama pasiweze kuathiri mazingira katika maeneo hayo.

Bodi na Menejimenti ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wakipata picha ya pamoja na Manahodha wa Meli inayotumika kuchimba mchanga katika upanuzi wa bandari ya Dar es Salaam mara baada ya kutembelea katika eneo la upanuzi wa Bandari ya Jijini Dar es Salaam kuona utekelezaji wa masharti ya cheti cha mazingira pamoja na kuhakikisha maeneo yale ambayo udongo unaochimbwa kwenye maeneo hayo na sehemu inapokwenda kuhifadhiwa pawe ni sehemu salama pasiweze kuathiri mazingira katika maeneo hayo

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

*************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limepanga kukutana na waagizaji wa mafuta nje ya nchi na wanaopokea mafuta hayo kwenye matenki bandarini kujadili ni jinsi gani wanaweza kuboresha miundombinu ambayo imekuwa sehemu ya uchafuzi wa mazingira kwenye bahari.

Ameyasema hayo jana Februari 23,2023 Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt. Samuel Gwamaka wakati Bodi na Menejimenti ya Baraza la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kutembelea katika eneo la upanuzi wa Bandari ya Jijini Dar es Salaam kuona utekelezaji wa masharti ya cheti cha mazingira pamoja na kuhakikisha maeneo yale ambayo udongo unaochimbwa kwenye maeneo hayo na sehemu inapokwenda kuhifadhiwa pawe ni sehemu salama pasiweze kuathiri mazingira katika maeneo hayo.

Akizungumza na Waaandishi wa habari Dkt.Gwamaka amaesema kuna changamoto ambazo wamezipokea kutoka uongozi wa bandari, katika changamoto hizo sehemu kubwa ni changamoto zinazohusiana na upokeaji wa mafuta ikiwa ni pamoja na mambo yanayopokea mafuta kuchakaa kutokana na kutumika kwa muda mrefu zaidi ambayo yanamilikiwa na watu binafsi.

"Mara nyingi tumekuwa tukiwasiliana na wawekezaji wengi katika eneo hili ambapo unakuta mafuta yanatapakaa baharini kwasababu kubwa ni ubovu wa miundombinu ya mabomba ya kupokea mafuta kwenye meli hivyo tukikaa nao tutazungumza kuona ni namna gani wanaweza kuboresha miundombinu hii kusiweze kuleta athari zozote za kimazingira". Amesema Dkt.Gwamaka

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw.Mrisho Mrisho amesema wamekuwa wakifanya shughuli zao bila uchafuzi wa kimazingira, hivyo wamepokea ushauri kutoka NEMC hasa kwenye masuala mazima ya miradi , kuhakkikisha wanaangalia sula zima la utuzunzaji wamazingira.

"Wakati wote wa ufanyaji wa hii miradi tumefanya kazi na NEMC kwa ukaribu na kila wakati tunawafuata na kuwaambia kile tunachoendela nacho

Pamoja na hayo amewapongeza NEMC kwa kutoa ushirikiano wa kutosha kwenye kuhakikisha miradi ambayo inatekelezwa na bandari inaenda sambamba na kuhakikisha utunzaji wa mazingira hivyo wapo tayari kuendelea kupokea ushauri wowote wanaopewa wenye lengo la kuhifadhi mazingira.

Nae Mkurugenzi wa Mazingira kutoka Ofiisi ya Makamu wa Rais Dkt. Andrew Komba amesema miradi mingi ambayo wameiona kwenye bandari hiyo kwa namna moja ama nyingine ina muingiliano mkubwa na sekta zingine hivyo wanashauri Mamlaka ya Bandari ikafanye Tathiminni ya Kimkakati ya Mazingira ili sekta zote zinazoonekana zinashabiana na shughuli zinazoendelea bandarini ziweze kushirikishwa ili tuone kwa namna gani kwa pamoja tunaweza kwenda mbele.
Share:

Video Mpya : NG'WANA SAMAKA -BOSI KALEWA

Share:

BIBI YANGU KANIPA MBINU YA KUMFUNGA MUME ASITOKE NJE YA NDOA!

Watu wengi husema kuwa ndoa ni ngumu na hii ni kutokana na wanaume wengi kutokuwa waaminifu katika ndoa zao kwani baada ya kipindi fulani huanza kutafuta wanawake wengine wa nje kwa madai ya kubadilisha ladha maana huwezi kula chakula kile kile kila siku.

Naitwa Queen, nimekuwa kwenye ndoa kwa miaka mitano sasa, hakika naweza kusema mimi ni miongoni mwa wanawake ambao wamefaidi matunda ya ndoa vilivyo, sijawahi kukumbana na kadhia yoyote ile.

Hata hivyo, kuna baadhi ya wanawake nao wamekuwa na tabia hiyo tena kwa sana ila wamekuwa wakifanya kwa siri kubwa kiasi ni vigumu kwa waume zao kuwabaini kwa wepesi.

Kipindi naolewa Bibi yangu aliniambia kuwa mimi ndio mwenye wajibu wa kuilinda ndoa yangu kuliko mtu yeyote yule, nina wajibu kuliko hata mume wangu mwenyewe. Nilimuuliza Mama kivipi?, ndipo akaniambia mume anahitaji kuchungwa kama mtoto mdogo maana huko nje vishawishi ni vingi.

Basi nilikaa nikitafakari ushauri wa Bibi yangu ambaye ameishi na mume wake ambaye ni Babu yangu kwa miaka zaidi ya 50 kwenye ndoa, niliona ni ushauri wa maana sana kwangu.

Nilirejea kwa Bibi na kumuuliza ni njia zipi naweza kuilinda ndoa yangu, ndipo akaniambia kuwa mwanaume kwa kawaida anahitaji kufungwa kwa dawa za mitishamba ambazo zinatolewa na waganga ambao ni waaminifu na wabobezi wa kazi hiyo.

Nilimuuliza Bibi sasa anawezaje kumpata mtu mwaminifu wa kunifanyia hivyo?, ndipo akanitajia jina la Dr. Kiwanga na kuniambia amewaunganisha watu wengi naye na kila mmoja amekuwa akija kwake na kumueleza kuwa Dr. Kiwanga amekuwa msaada mkubwa kwao.

Bibi alichukua simu yake na kunitajia namba ya Dr. Kiwanga ambayo ni, niliisevu kwenye simu yangu na kesho yake niliamua kumpigia, alipokea nilimuuleza shida yangu ni kwamba nahitaji kumfunga mume wangu asichepuke kamwe!.

Nakumbuka Dr. Kiwanga alinisikiliza, aliniambia baada ya siku tatu dawa itaanza kufanya kazi na kuanzia hapo hakuna hata siku mmoja mume wangu atachepuka katika ndoa yetu. Na kweli kwa kipindi hiki cha miaka mitano sijawahi kusikia mume wangu ana mwanamke mwingine nje ingawa majirani zangu wamekuwa wakisema waume zao wametekwa na michepuko kabisa.

Kumbuka Dr. Kiwanga anatibu maradhi kama kifua kikuu, kisukari, msukomo wa damu, kifafa na magonjwa mengineyo, pia anasuluhisha shida za kifamilia kama kutokouwa na uwezo wa kupata mtoto, kutopata mchumba wako wa maisha, shida za ndoa, kuwa na bahati katika maisha haswa katika michezo ya kamari na mengineyo.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na Dr. Kiwanga kwa namba +254769404965, barua pepe kiwangadoctors@gmail.com au tembelea tovuti yake ambayo ni www.kiwangadoctors.com kwa mengi zaidi.

Mwisho.
Share:

Thursday, 23 February 2023

MBUNIFU WA MAVAZI NCHINI KASIKANA AJA NA JUKWAA LA KUTANGAZA WABUNIFU MIKOA YA KANDA YA ZIWA

Mbunifu wa mitindo ya mavazi Kutoka Mkoani Geita, Bertha Joseph Komba(KASIKANA) anatarajia kuzindua Jukwaa la Golden Fashion Festival  ambalo linalengo la kuibua vipaji mbali mbali vya wabunifu pamoja na kuhimiza jamii kuipa thamani biashara ya ubunifu  kwani bado jamii kubwa hapa nchini imekuwa ikipuuzia kazi mitindo hasa ushonaji kwa kuona kazi hiyo aina manufaa makubwa.

Akizungumza na waandishi wa mbunifu wa mavazi Bertha Komba almaarufu Kasikana Collectione amesema ameamua kuja na jukwaa la Golden Fashion Festival kwa lengo la kuibua na kutangaza vipaji vya wabunifu kutoka Mikoa ya Kanda ya ziwa ikiwa ni pamoja na kuipa thamani kazi ya  ubunifu ambayo kwa kiasi kikubwa imekuwa ikikosa sapoti kutokana na kuonekana  ni kazi ya maslahi kidogo.

“Tuna imani kupitia jukwaa hili tutaiomba Serikali kuitazama kwa jicho la kipekee Sanaa ya ushonaji na ubunifu kwa waweze kuiongezea thamani hasa katika matumizi yam ashine za kisasa ,lakini pia iweze kuboresha vyuo vya ufundi na kujenga viwanda vya ushonaji ambavyo vitasaidia vijana wengi Kupata ajira”, ameeleza Kasikana.

Kasikana ameongeza kuwa  ni vyema kwa Watanzania wakapenda vitu vinavyotengenezwa Nchini ikiwa ni pamoja na kuwatumia wabunifu mbali mbali nguo au vitu ambavyo wanaviitaji na kwamba matarajio ya jukwaa hilo ni kuwafikia wabunifu waliopo Kwenye Wilaya  tano zilizopo Mkoani Geita pamoja na ambao wapo vijijini ambao bado awajapata nafasi ya Kutangaza vitu ambavyo wanabuni.

“Hivyo natangaza rasmi kwamba natarajia Kutambulisha jukwaa hili na kuzindua ifikapo tarehe 3/3/2023  kwenye ukumbi wa Otonde Plaza ndani ya uzinduzi natarajia kuonesha ubunifu wangu na kuwatambulisha baadhi ya wanamitindo ambao watakuwa wamevaa mavazi yaliyobuniwa”, amesema Kasikana.

“Pia  kutakuwa na mavazi ambayo yatauzwa hapo hapo. mara bada ya uzinduzi na utambulisho wa jukwaa hili tutaanza mchakato wa maandalizi ya Tamasha kubwa la mitindo ambalo tunatarajia kulifanya mwezi wa12 mwaka huu”, amesema Kasikana.

Share:

POLISI WAZUNGUMZIA AJALI BASI LA MWENDOKASI, MAENDELEO YA MTEMBEA KWA MIGUU ALIYEGONGWA

MTU mmoja aliyetajwa kwa jina moja la Ismail ambaye aligongwa na Gari la Mwendokasi wakati anatembea kwa miguu kandokando ya Barabara ya Morogoro na Jamhuri, imeelezwa kuwa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Jeshi la Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, ACP. Murilo J. Murilo imeeleza kuwa baada ya kutokea ajali hiyo iliyohusisha Gari mali ya Kampuni ya UDART (Mwendokasi) na Gari ndogo aina ya Toyota Avanza mali ya Rwanda Air, ajali hiyo ilisababisha majeruhi madogo kwa baadhi ya abiria.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa majeruhi wanne wamelazwa katika Hospitali hiyo ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi wakiwemo, Dereva wa Gari ndogo (Toyota Avanza), Jumbe Mohamed (38) na Shukuru Omari (32), Saidi Hasani (43) wote ni abiria gari hiyo ndogo pamoja na mtu huyo ambaye alikuwa anatembea kwa miguu (Ismail).

Hata hivyo, kwa mujibu wa taarifa hiyo Uchunguzi wa awali wa Jeshi la Polisi umebaini kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe na kutojali kwa alama za barabarani kwa Dereva wa gari ndogo aliyekuwa anatoka Mnazi mmoja kuelekea mzunguko wa DTV kutochukua tahadhari wakati anakatisha barabara kubwa ya Morogoro.

Aidha, Jeshi la Polisi limeendelea kutoa wito kwa Madereva kufuata na kuzingatia Sheria na alama za barabarani kila wakati ili kuepusha ajali ambazo zinaweza kuepukika.

Ajali hiyo iliyotokea jana Jumatano (Februari 22, 2023) majira ya saa 6:10 katika makutano hayo ya barabara ya Morogoro na Jamhuri, Kisutu, jijini Dar es salaam ikihusisha Gari namba T122 DGW Aina ya Dragon mali ya Kampuni ya UDART (Mwendokasi) na Gari ndogo aina ya Toyota Avanza, mali ya Rwanda Air.

Chanzo- Michuzi TV
Share:

MAAFISA TEHAMA, MAENDELEO YA JAMII WA HALMASHAURI WAPEWA MAFUNZO YA KANZIDATA YA TAIFA YA WANAWAKE NA UONGOZI TANZANIA

Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi akizungunza kwenye kikao kazi cha Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri mbalimbali nchini kuhusu  Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu wameendesha Kikao na Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri mbalimbali nchini kuhusu  Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania.

Kanzidata ya Wanawake na Uongozi Tanzania ni mfumo rasmi wa kuhifadhi data mtandaoni ulioanzishwa ili kurekodi kuhifadhi na kusambaza wasifu wa wataalamu wanawake wa Kitanzania walioko ndani na nje ya nchi.

Akifungua kikao hicho, kilichofanyika leo Alhamisi Februari 23,2023 Mjini Morogoro, Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Christopher Mushi  ameishukuru TGNP kwa kushirikiana Wizara kutengeneza mfumo huo ulioundwa na vijana wa Kitanzania ambao utasaidia katika upatikanaji wa taarifa za wanawake ili kuhifadhi na kusambaza wasifu wa wataalamu wanawake wa Kitanzania.
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Christopher Mushi.
 
Amesema kuanzishwa kwa mfumo huo ni sehemu ya utekelezaji wa vipaumbele  vitano vya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu ikiwemo kuwezesha ushiriki wa wanawake katika nafasi za uongozi na ngazi za maamuzi.

“Lengo la kikao kazi hiki kuwajengea uelewa maafisa maendeleo ya jamii na maafisa TEHAMA kuhusu  Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania ambapo kuufahamu vizuri mfumo huu itakuwa rahisi walengwa (wanawake) kujisajili kwenye mfumo. Naomba mkirudi kwenye maeneo yenu ya kazi mkawahamasishe wanawake wenye taaluma na ujuzi wajiunge”,amesema Mushi.

“Maafisa maendeleo ya jamii na TEHAMA tuna wajibu wa kuhamasisha jamii kuhusu mfumo huu, walengwa wajue umuhimu wa Kanzidata hii lakini pia wajisajili na mwisho wa siku ndiyo tutakuwa tunafanya mahubiri kwa vitendo kwamba tunawezesha wanawake kushiriki katika uongozi na ngazi za maamuzi”,ameongeza.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Bi. Lilian Liundi amesema Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania imeanzishwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu kwa kushirikiana na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa ufadhili wa Wadau wa Maendeleo kutoka Ubalozi wa Sweden na Norway kupitia shirika la Norwegian Agency for Development Cooperation  (Norad).

“Uzinduzi Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania ulifanyika Machi 8,2022 wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Kitaifa yaliyofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha. Mfumo huu wa pekee wa kuweka wasifu wa wanawake wa Tanzania walioajiriwa katika sekta binafsi au serikali waliopo ndani nan je nchi umetengenezwa na vijana Wataalamu wa TEHAMA wa hapa Tanzania. Hii ni nyenzo kubwa  kwa ukombozi na kuleta usawa wa kijinsia”,amesema Liundi.
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi 

“Kanzidata ya Wanawake na Uongozi Tanzania itarahisisha taarifa za ajira katika sekta ya Umma na sekta binafsi. Mfumo huu utawezesha Serikali pamoja na waajiri wa ndani na nje ya nchi kama vile taasisi za kuajiri na kuteua, kutafuta na kupata wanawake wa Kitanzania wenye ujuzi, weledi na ubobezi katika taaluma mbalimbali kwa ajili ya mitandao ya kitaalamu na kuchaguliwa katika nafasi zilizo wazi katika nyanja na sekta zote. Naomba wanawake mtumie mfumo huu”,ameeleza Liundi.

Amewaomba Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa TEHAMA kutangaza mfumo huo wa pekee wa kuweka taarifa za wanawake wa Tanzania ili kuwafikia wanawake wengi zaidi huku akiahidi kuwa TGNP itazitambua Halmashauri zilizofanya vizuri kusajili wanawake wengi wakati wa Tamasha la Jinsia mwezi Septemba mwaka huu 2023.

“Nina imani kubwa kabisa kazi ambayo tumeijia hapa itasonga mbele katika kuendeleza masuala ya usawa wa kijinsia ambalo ni suala la maendeleo, wanawake ambao ni zaidi ya asilimia 50 ya wananchi wa Tanzania   pamoja na makundi mengine huwezi kuwaacha nyuma katika mchakato wa maendeleo na ndiyo maana tuko hapa, twende wote kwa pamoja. Kikao hiki cha leo ni katika harakati za kuendeleza juhudi za kwamba wanawake wanashiriki katika nafasi za uongozi na maamuzi na sote tunafahamu serikali ya awamu ya sita  ilisema bayana kwamba itaendeleza  juhudi za awamu zilizopita kuhakikisha kwamba wanawake na makundi mengine wanashiriki katika nafasi za maamuzi kwa vigezo vinavyotakiwa",amesema Liundi.

"Na kwa mantiki hiyo ndiyo maana tuna juhudi za kutengeneza Kanzidata hii kwa lengo la kuhifadhi kumbukumbu kuhusu wasifu wa wanawake wenye taaluma na ujuzi mbalimbali, nani amebobea kwenye nini, nani anachipukia kwenye nini na yuko wapi ili itakapofikia wanatafutwa kwa ajili ya kufanya kazi kwa manufaa ya nchi hii ya Tanzania hata nje ya Tanzania wajulikane kwa urahisi. Naomba wanawake wajiunge katika Mfumo huu kwa anuani ya https://twl.jamii.go.tz kwani pia mtandao huu utakuwa unatoa fursa mbalimbali zinazotokea katika sekta binafsi au serikalini”,ameongeza Liundi.

Nao Washiriki wa kikao hicho wameahidi kwenda kuhamasisha wanawake kujisajili katika mfumo huo kwa kukutana na makundi mbalimbali ya wanawake.
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Christopher Mushi akizungumza leo Februari 23,2023 Mjini Morogoro wakati akifungua kikao kazi cha Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri mbalimbali nchini kuhusu  Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania kilichoandaliwa na TGNP kwa kushirikiana na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu. Picha na Kadama Malunde 
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Christopher Mushi akizungumza wakati akifungua kikao kazi cha Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri mbalimbali nchini kuhusu  Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania 
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Christopher Mushi akizungumza wakati akifungua kikao kazi cha Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri mbalimbali nchini kuhusu  Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi akizungunza kwenye kikao kazi cha Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri mbalimbali nchini kuhusu  Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi akizungunza kwenye kikao kazi cha Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri mbalimbali nchini kuhusu  Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi akizungunza kwenye kikao kazi cha Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri mbalimbali nchini kuhusu  Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania.
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi akizungunza kwenye kikao kazi cha Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri mbalimbali nchini kuhusu  Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi akizungunza kwenye kikao kazi cha Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri mbalimbali nchini kuhusu  Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi akizungunza kwenye kikao kazi cha Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri mbalimbali nchini kuhusu  Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi akizungunza kwenye kikao kazi cha Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri mbalimbali nchini kuhusu  Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi akizungunza kwenye kikao kazi cha Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri mbalimbali nchini kuhusu  Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania
Afisa TEHAMA kutoka TGNP, Antweny Sawe akielezea jinsi ya kutumia mfumo wa Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania

Afisa Maendeleo ya Jamii Mwandamizi kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, John Mapunda akiongoza majadiliano ya kuandaa mpango kazi wa kila wilaya kuhusu utekelezaji wa Kanzidata ya Taifa ya wanawake na uongozi Tanzania

Kikao kazi cha Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri mbalimbali nchini kuhusu  Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania kikiendelea
Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri wakiwa ukumbini.

Maafisa Maendeleo ya Jamii wakipiga picha ya kumbukumbu
Maafisa Maendeleo ya Jamii wakipiga picha ya kumbukumbu
Maafisa TEHAMA wakipiga picha ya kumbukumbu
Maafisa TEHAMA wakipiga picha ya kumbukumbu.

Picha na Kadama Malunde - Morogoro
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive

Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger