Thursday, 23 February 2023

MAAFISA TEHAMA, MAENDELEO YA JAMII WA HALMASHAURI WAPEWA MAFUNZO YA KANZIDATA YA TAIFA YA WANAWAKE NA UONGOZI TANZANIA

Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi akizungunza kwenye kikao kazi cha Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri mbalimbali nchini kuhusu  Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu wameendesha Kikao na Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri mbalimbali nchini kuhusu  Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania.

Kanzidata ya Wanawake na Uongozi Tanzania ni mfumo rasmi wa kuhifadhi data mtandaoni ulioanzishwa ili kurekodi kuhifadhi na kusambaza wasifu wa wataalamu wanawake wa Kitanzania walioko ndani na nje ya nchi.


Akifungua kikao hicho, kilichofanyika leo Alhamisi Februari 23,2023 Mjini Morogoro, Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Christopher Mushi  ameishukuru TGNP kwa kushirikiana Wizara kutengeneza mfumo huo ulioundwa na vijana wa Kitanzania ambao utasaidia katika upatikanaji wa taarifa za wanawake ili kuhifadhi na kusambaza wasifu wa wataalamu wanawake wa Kitanzania.
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Christopher Mushi.
 
Amesema kuanzishwa kwa mfumo huo ni sehemu ya utekelezaji wa vipaumbele  vitano vya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu ikiwemo kuwezesha ushiriki wa wanawake katika nafasi za uongozi na ngazi za maamuzi.

 
“Lengo la kikao kazi hiki kuwajengea uelewa maafisa maendeleo ya jamii na maafisa TEHAMA kuhusu  Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania ambapo kuufahamu vizuri mfumo huu itakuwa rahisi walengwa (wanawake) kujisajili kwenye mfumo. Naomba mkirudi kwenye maeneo yenu ya kazi mkawahamasishe wanawake wenye taaluma na ujuzi wajiunge”,amesema Mushi.

“Maafisa maendeleo ya jamii na TEHAMA tuna wajibu wa kuhamasisha jamii kuhusu mfumo huu, walengwa wajue umuhimu wa Kanzidata hii lakini pia wajisajili na mwisho wa siku ndiyo tutakuwa tunafanya mahubiri kwa vitendo kwamba tunawezesha wanawake kushiriki katika uongozi na ngazi za maamuzi”,ameongeza.


Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Bi. Lilian Liundi amesema Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania imeanzishwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu kwa kushirikiana na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa ufadhili wa Wadau wa Maendeleo kutoka Ubalozi wa Sweden na Norway kupitia shirika la Norwegian Agency for Development Cooperation  (Norad).


“Uzinduzi Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania ulifanyika Machi 8,2022 wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Kitaifa yaliyofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha. Mfumo huu wa pekee wa kuweka wasifu wa wanawake wa Tanzania walioajiriwa katika sekta binafsi au serikali waliopo ndani nan je nchi umetengenezwa na vijana Wataalamu wa TEHAMA wa hapa Tanzania. Hii ni nyenzo kubwa  kwa ukombozi na kuleta usawa wa kijinsia”,amesema Liundi.
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi 

“Kanzidata ya Wanawake na Uongozi Tanzania itarahisisha taarifa za ajira katika sekta ya Umma na sekta binafsi. Mfumo huu utawezesha Serikali pamoja na waajiri wa ndani na nje ya nchi kama vile taasisi za kuajiri na kuteua, kutafuta na kupata wanawake wa Kitanzania wenye ujuzi, weledi na ubobezi katika taaluma mbalimbali kwa ajili ya mitandao ya kitaalamu na kuchaguliwa katika nafasi zilizo wazi katika nyanja na sekta zote. Naomba wanawake mtumie mfumo huu”,ameeleza Liundi.


Amewaomba Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa TEHAMA kutangaza mfumo huo wa pekee wa kuweka taarifa za wanawake wa Tanzania ili kuwafikia wanawake wengi zaidi huku akiahidi kuwa TGNP itazitambua Halmashauri zilizofanya vizuri kusajili wanawake wengi wakati wa Tamasha la Jinsia mwezi Septemba mwaka huu 2023.


“Nina imani kubwa kabisa kazi ambayo tumeijia hapa itasonga mbele katika kuendeleza masuala ya usawa wa kijinsia ambalo ni suala la maendeleo, wanawake ambao ni zaidi ya asilimia 50 ya wananchi wa Tanzania   pamoja na makundi mengine huwezi kuwaacha nyuma katika mchakato wa maendeleo na ndiyo maana tuko hapa, twende wote kwa pamoja. Kikao hiki cha leo ni katika harakati za kuendeleza juhudi za kwamba wanawake wanashiriki katika nafasi za uongozi na maamuzi na sote tunafahamu serikali ya awamu ya sita  ilisema bayana kwamba itaendeleza  juhudi za awamu zilizopita kuhakikisha kwamba wanawake na makundi mengine wanashiriki katika nafasi za maamuzi kwa vigezo vinavyotakiwa",amesema Liundi.


"Na kwa mantiki hiyo ndiyo maana tuna juhudi za kutengeneza Kanzidata hii kwa lengo la kuhifadhi kumbukumbu kuhusu wasifu wa wanawake wenye taaluma na ujuzi mbalimbali, nani amebobea kwenye nini, nani anachipukia kwenye nini na yuko wapi ili itakapofikia wanatafutwa kwa ajili ya kufanya kazi kwa manufaa ya nchi hii ya Tanzania hata nje ya Tanzania wajulikane kwa urahisi. Naomba wanawake wajiunge katika Mfumo huu kwa anuani ya https://twl.jamii.go.tz kwani pia mtandao huu utakuwa unatoa fursa mbalimbali zinazotokea katika sekta binafsi au serikalini”,ameongeza Liundi.

Nao Washiriki wa kikao hicho wameahidi kwenda kuhamasisha wanawake kujisajili katika mfumo huo kwa kukutana na makundi mbalimbali ya wanawake.
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Christopher Mushi akizungumza leo Februari 23,2023 Mjini Morogoro wakati akifungua kikao kazi cha Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri mbalimbali nchini kuhusu  Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania kilichoandaliwa na TGNP kwa kushirikiana na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu. Picha na Kadama Malunde 
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Christopher Mushi akizungumza wakati akifungua kikao kazi cha Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri mbalimbali nchini kuhusu  Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania 
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Christopher Mushi akizungumza wakati akifungua kikao kazi cha Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri mbalimbali nchini kuhusu  Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi akizungunza kwenye kikao kazi cha Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri mbalimbali nchini kuhusu  Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi akizungunza kwenye kikao kazi cha Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri mbalimbali nchini kuhusu  Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi akizungunza kwenye kikao kazi cha Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri mbalimbali nchini kuhusu  Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania.
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi akizungunza kwenye kikao kazi cha Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri mbalimbali nchini kuhusu  Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi akizungunza kwenye kikao kazi cha Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri mbalimbali nchini kuhusu  Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi akizungunza kwenye kikao kazi cha Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri mbalimbali nchini kuhusu  Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi akizungunza kwenye kikao kazi cha Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri mbalimbali nchini kuhusu  Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi akizungunza kwenye kikao kazi cha Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri mbalimbali nchini kuhusu  Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania
Afisa TEHAMA kutoka TGNP, Antweny Sawe akielezea jinsi ya kutumia mfumo wa Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania
Afisa TEHAMA kutoka TGNP, Antweny Sawe akielezea jinsi ya kutumia mfumo wa Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania
Afisa TEHAMA kutoka TGNP, Antweny Sawe akielezea jinsi ya kutumia mfumo wa Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania
Afisa TEHAMA kutoka TGNP, Antweny Sawe akielezea jinsi ya kutumia mfumo wa Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania

Afisa Maendeleo ya Jamii Mwandamizi kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, John Mapunda akiongoza majadiliano ya kuandaa mpango kazi wa kila wilaya kuhusu utekelezaji wa Kanzidata ya Taifa ya wanawake na uongozi Tanzania
Afisa Maendeleo ya Jamii Mwandamizi kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, John Mapunda akiongoza majadiliano ya kuandaa mpango kazi wa kila wilaya kuhusu utekelezaji wa Kanzidata ya Taifa ya wanawake na uongozi Tanzania
Afisa Maendeleo ya Jamii Mwandamizi kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, John Mapunda akiongoza majadiliano ya kuandaa mpango kazi wa kila wilaya kuhusu utekelezaji wa Kanzidata ya Taifa ya wanawake na uongozi Tanzania
Kikao kazi cha Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri mbalimbali nchini kuhusu  Kanzidata ya Taifa ya Wanawake na Uongozi Tanzania kikiendelea
Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri wakiwa ukumbini.
Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri wakiwa ukumbini.
Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri wakiwa ukumbini.
Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri wakiwa ukumbini.
Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri wakiwa ukumbini.
Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri wakiwa ukumbini.
Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri wakiwa ukumbini.
Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri wakiwa ukumbini.
Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri wakiwa ukumbini.
Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri wakiwa ukumbini.
Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri wakiwa ukumbini.
Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri wakiwa ukumbini.
Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri wakiwa ukumbini.
Maafisa Maendeleo ya Jamii wakipiga picha ya kumbukumbu
Maafisa Maendeleo ya Jamii wakipiga picha ya kumbukumbu
Maafisa TEHAMA wakipiga picha ya kumbukumbu
Maafisa TEHAMA wakipiga picha ya kumbukumbu.

Picha na Kadama Malunde - Morogoro
Share:

DKT. JINGU AHIMIZA UBUNIFU, UWAJIBIKAJI,UADILIFU KWA WATUMISHI WA TUME MAHALA PA KAZI



Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt John Antony Jingu akizungumza wakati wa ufunguzi wa Baraza la Wafanyakazi la Tume ya Taifa ya Uchaguzi lililokutana leo Februari 23,2023 jijini Dodoma. Dkt Jingu amehimiza ubunifu, Uadilifu, uwajibikaji miongoni mwa watumishi na ushiriki wa michezo kwa ajili ya kuwajengea afya watumishi mahala pa kazi.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt John Antony Jingu akizungumza wakati wa ufunguzi wa Baraza la Wafanyakazi la Tume ya Taifa ya Uchaguzi lililokutana leo Februari 23,2023 jijini Dodoma. Dkt Jingu amehimiza ubunifu, Uadilifu, uwajibikaji miongoni mwa watumishi na ushiriki wa michezo kwaajili ya kuwajengea afya watumishi mahala pa kazi.
Wajumbe wa baraza la Wafanyakazi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt John Antony Jingu wakati akifungua baraza hilo.
Wajumbe wa baraza la Wafanyakazi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt John Antony Jingu wakati akifungua baraza hilo.
Kaimu Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi, Nassoro Shemzigwa (kushoto) akiongoza baraza hilo. Kulia ni Katibu wa Baraza hilo, Livini Avith.
Wajumbe wa baraza la Wafanyakazi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakimsikiliza wakifuatilia.Menejimenti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt John Antony Jingu
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni Rasmi, Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt John Antony Jingu.
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi, Manejiment na Secretarieti wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni Rasmi, Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt John Antony Jingu.
Share:

MWANAFUNZI AMUUA KWA KISU MWALIMU WAKE


Mwanafunzi wa shule ya upili nchini Ufaransa amemuua kwa kumchoma kisu mwalimu mmoja raia wa Uhispaniaa katika shule moja katika mji wa Saint-Jean-de-Luz nchini Ufaransa.

Msemaji wa serikali ya Ufaransa Olivier Véran amethibitisha shambulio hilo la Jumatano ya leo na kusema mhusika ana umri wa miaka 16.

Polisi wamefika katika shule ya Saint-Thomas d'Aquin na mwendesha mashtaka wa eneo hilo, ambapo mwanafunzi huyo alikamatwa. Vyombo vya habari nchini Ufaransa vinasema kwamba mshambuliaji huyo aliingia darasani wakati mwalimu huyo wa Uhispania akitoa darasani na kumshambulia kwa kisu.

Mwalimu huyo anayekadiriwa kuwa na na umri wa miaka 50 alifariki kutokana na mshtuko wa moyo baada ya huduma za dharura kuwasili shuleni hapo, vyombo vya habari nchini humo vimeripoti.

Inasemekana mshambuliaji huyo alifunga mlango wa darasa na kumdunga kisu mwalimu huyo kifuani mwake.



Waziri wa Elimu wa Ufaransa, Pap Ndiaye ameelekea mara moja shuleni hapo.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI FEBRUARI 23,2023







             

       

Share:

NABII MWASHA:NINAIONA NEEMA KUPITIA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN MWAKA HUU


*********************

NA MWANDISHI WETU

MTUME na Nabii Shile Mwasha (Nabii wa Rufaa) wa Huduma ya Ufunuo wa Kristo na Kanisa la Miujiza lililopo Bunju Kilimani jijini Dar es Salaam amesema kuwa,mwaka huu anaiona Tanzania mpya chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan huku akisisitiza umuhimu wa maombi kwake na Taifa.

Ameyasema hayo leo Februari 22, 2023 wakati akitangaza mwaka wa Bwana uliokubalika katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es Salaam.

"Jambo kubwa ambalo nimekuja nalo leo ni kutangaza mwaka wa Bwana uliokubalika, watu wengi hawajui jina la huu mwaka, lakini Mungu ameniambia niwaambie kuwa, mwaka huu unaitwa mwaka wa moto, kwamba mwaka 2023 ni mwaka wa moto.

"Kwa hiyo kuna maelekezo ambayo Roho mtakatifu amenipa mimi kama Nabii wa Rufaa, unajua manabii wapo wengi, lakini neema ambayo nimepewa mimi Nabii wa Rufaa, kama kuna hospitali ipo ya Rufaa, kama kuna Mahakama ipo ya Rufaa na hata kama kuna manabii wapo wa rufaa,sasa mimi kipengele Mungu alichonipa ni kutangaza mwaka wa Bwana.

"Mwaka ambao mimi ninatangaza katika ulimwengu wa Roho ndiyo ambao una declare-demarcation ambao ni wa rufaa.

"Kwa mwaka huu ambacho ninasema ni kwamba kuna kitu ambacho ninakiona katika ulimwengu wa roho, ninaona Tanzania mpya sana, lakini tunatakiwa kumuombea Mama Samia (Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa sababu ipo neema juu yake, lakini pia tuombe kwa ajili ya watoto wa viongozi na familia mbalimbali maana ninaona wanachanua sana na wakistawi sana na ninaona mafanikio sana kupitia Serikali ya Tanzania na ninaona mafanikio pia kupitia Serikali hii ya CCM.

"Kwa hiyo tumuombee Mama Samia, na pia tumpongeza sana kwa ajili ya kusaidia na kuongeza kwa sababu pia nilitabiri kuhusu mwezi wa Ephata, kwamba utakuwa ni mwezi wa kufunguliwa, na nimpongeza sana Mama Samia kwa kuongeza Boom la Wanafunzi, hongera sana Mama. Hilo ni jambo kubwa sana ambalo amefanya, na ninaona neema kwake mbele, na tuendelee kuomba kwa sababu ipo vita na tutaendelea kuomba na kukemea.

"Kama nilivyosema huu ni mwaka wa moto, na watu wanatakiwa kuingia kwenye moto kwa sababu mwaka wa moto ni mwaka wa majanga, kwa hiyo huu mwaka kwa muda wa miezi minne utakuwa na majanga ya kufuatana, kwa hiyo inawezekana hata kesho ikawa kuna janga.

"Cha msingi ni kwamba upo katika moto wa roho mtakatifu, kwa sababu ambacho kitakusaidia kuokoka katika majanga ni ile moto ya roho mtakatifu. Kama haupo kwenye moto wa roho mtakatifu haya majanga hautayaweza, ndiyo maana kwa mwaka huu jambo pekee ambalo ninawaambia Watanzania wamgeukie Mungu,maana yake Mungu ndiye atawaokoa na huu moto na pia ninaiambia Dunia imgeukie Mungu,na ndiyo maana Mussa alipoona moto alisema,nitageuka ndani ya maono haya.

"Lengo la haya majanga yote ni nini, Mungu anaongea na Dunia, Mungu anaongea na Uturuki,Mungu anaongea na nchi kwamba zimgeukie yeye, zianze kumwangalia yeye ndiyo haya majanga yataisha.Kwa hiyo lengo la Mungu ni watu waokolewe.Lakini haya majanga mwisho wake ni mwezi wa nne, na nimeona katika ulimwengu wa roho kuwa mwezi wa tatu majanga yatakuwa mengi sana,"amefafanua Nabii Mwasha.

Pia amesema, Mungu amemwambia aiombee Jumuiya ya Afrika Mashariki kwani, alimuona mmoja wa marais wa jumuiya hiyo akipunga mkono.

"Katika ulimwengu wa roho nilimuona mmoja wa marais wa Afrika Mashariki akipunga mkono, sitamtaja kwa sasa.Lakini pia roho wa Mungu ameniambia tuombe sana, na tuendelee kuiombea nchi yetu, kwa hiyo mwaka 2023 ni mwaka ambao tunapaswa kukaa katika moto wa roho mtakatifu.Pia katika mwaka huu nimepewa majina mapya 12 ya miezi yaliyobeba unabii wa hatima ya miezi 12,"amefafanua Nabii Mwasha.
Share:

Wednesday, 22 February 2023

MAJID AUAWA AKIKABA WANAWAKE USIKU WA MANANE TINDE

Picha haihusiani na habari hapa chini




Na Halima Khoya - Malunde 1 blog

Mwanaume mmoja anayefahamika kwa jina la Majid Mohamed,mwenye umri wa miaka 36 Mkazi wa Tinde ameuawa kwa kushambuliwa na wananchi waliojichukulia sheria mkononi kwa tuhuma za kuwadanganya kuwa yeye ni wakala wa mabasi kisha kuwavamia na kuwaibia mali zao.


Akieleza juu ya tukio hilo Diwani wa Kata ya Tinde,Jafari Makwaya amesema tukio hilo limetokea Februari 21 2023 Majira ya saa nane usiku katika kitongoji cha Jomu Kata ya Tinde Mkoani Shinyanga, ambapo mwanaume huyo alikuwa amewavamia wanawake wawili kwa lengo la kuwaibia lakini mlinzi wa malori barabarani na madereva malori walifanikiwa kuwaokoa wanawake hao.


"Alipigwa akiwa kwenye shughuli za kuwavamia watu lakini dereva wa Lori na mlinzi wa malori walishuhudia tukio zima ambapo walienda kutoa msaada kwa wanawake wale kisha wakamvizia Majid Mohamed akiwa anakimbia kisha kumpiga na kitu chenye ncha kali na kumtupia kwenye mfereji wa barabarani", amesema Makwaya.



"Alikuwa anawadanganya watu kuwa ni wakala wa mabasi na ni mzawa wa Tinde na amewahi kufungwa kifungo cha maisha kwa kosa la ubakaji na wizi wa madawa ya hospitali na baada ya kutoka gerezani alianza kutishia maisha watu waliofuatilia kesi ,kuna idadi kubwa ya vijana ambao hawana kazi katika kata hii hivyo niombe kwa vyombo vya ulinzi na usalama kushughulika na vijana wanaowadanganya watu na kuwaibia kwa kimvuli cha uwakala", ameongeza.


Inaelezwa kuwa kijana huyo anayedaiwa kuwa kibaka maarufu amekuwa tishio katika eneo la Tinde kutokana na vitendo vyake huku wananchi wakidai amekuwa akikingiwa kifua hivyo kutofungwa jela.
Share:

MUME WANGU AKIENDA NJE KAZI HAIWEZI, ILA KWANGU MAMBO NI MOTO

Naitwa Mama Sofia, nimeolewa ni na watoto wanne na mume wangu wa ndoa, Jamal, tulifunga ndoa miaka miwili iliyopita, tuliishi kwa upendo na amani ndani ya nyumba bila kadhia yoyote ndani ya nyumba yetu hadi pale tulipojaliwa kupata mtoto mmoja.

Ukweli majirani walivutiwa sana na jinsi ambavyo tulikuwa tukiishi pamoja, nguzo pekee iliyotuongoza maisha ni uaminifu ndani ya ndoa, hakuna ubishi kwamba uaminifu ukikosekana kati ya wawili basi mambo huanza kuharibika.

Licha ya mapenzi moto moto niliyokuwa nampa mume wangu na ambayo yeye alikuwa akinionyesha, bado ndoa yetu kuna kipindi ilipitia kipindi kigumu hadi nikafikiria siku moja niondoke nirudi kwa wazazi wangu.

Hiyo ilikuwa ni baada ya mimi kujifungua, mume wangu ghafla alibadilika na akaanza kurejea nyumbani akiwa amechelewa sana tofauti na ilivyokuwa hapo awali ambapo alikuwa anakuja nyumbani mapema.

Nakumbuka kila nilipojaribu kumuuliza alipokuwa hakuwa na majibu yenye kueleweka zaidi ya kusema yeye ni Baba mwenye nyumba, hivyo sio hekima kumuuliza kila jambo afanyalo.

Basi niliamua kumchunguza taratibu kupitia simu yake ya mkononi, nilikuwa nasoma SMS zake na kuangalia ni kina nani hasa amekuwa akiwasiliana nao mara kwa mara, hadi mwisho wa siku nilikuja kumpata mwanamke ambaye alikuwa ndiye mchepuko wake uliyokuwa unamchelewesha kurudi nyumbani.

Niliamua kumpigia simu Dr. Kiwanga na kumuomba anisaidie kumfunga mume wangu, huyu Dr. Kiwanga ndiye alinisaidia kumpata mtoto wangu baada ya kukaa kwenye ndoa kwa zaidi ya mwaka mmoja bila kubeba ujauzito.

Nashukuru Dr. Kiwanga ambaye nimekuwa nikimwamini kwa kazi zake, aliniambia ndani ya siku tatu mambo yatakuwa sawa, nilimshukuru kwa usaidizi wake wa kuamua kuinusuru ndoa yangu ili isivunjike jambo ambalo likuwa likiwapata wengi kipindi hiki.

Baada ya siku mbili mume wangu alirejea kazi akiwa na maua aliyoniletea kama zawadi, nakumbuka aliwahi kufanya hivyo kipindi anataka kunichumbia. Hadi nilishangaa kwanini ameamua kufanya hivyo, nilimuuliza lengo lake ni lipi hasa?.

Mume wangu alinijibu kuwa amefanya hivyo ili kuniomba msamaha kwa kuisaliti ndoa yetu hadi kupata matatizo huko nje, nilimuhoji umepata tatizo gani?. Akiwa analia, aliniambia alipoenda kwa mchepuko wake alishindwa kabisa kufanya kazi aliyotakiwa kufanya kama wanaume na haelewi sababu ila akirejea kwangu anajihisi kazi kuimudu bila tatizo.

Kumbuka kuwa Dr. Kiwanga ana uwezo wa kuwezesha kuwa mtu wa bahati maishani, ana uwezo wa kukukinga na adui zako wanaokutakia mabaya kwa wakati wowote ule kwa muda wa siku tatu utaona matokeo yake utayaona.

Kwa mengi zaidi wasiliana nao kupitia barua pepe kiwangadoctors@gmail.com au kwenye wavuti www.kiwangadoctors.com au waweza kuwasiliana nao kupitia namba ya simu +254 769404965.

Mwisho.
Share:

AFARIKI BAADA YA KUANGUKA KWENYE MWAMBA AKIFANYA MAOMBI

Mwanaume anayesemekana kuwa na umri wa miaka 20, amefariki dunia baada ya kuanguka kutoka kwa mwamba wa Kit Mikayi eneo la Seme,kaunti ya Kisumu Kenya.

Mwanamume alifariki baada ya kuanguka kutoka kwa mwamba wa Kit Mikayi eneo la Seme, kaunti ya Kisumu. 

Katika tukio hilo la Jumapili, Februari 19, mwendo wa saa nane asubuhi, marehemu alikuwa ameandamana pamoja na waumini wengine juu ya mwamba huo kuomba.

 Lakini mambo yaligeuka baada ya mwanaume huyo kuteleza kutoka kwenye mwamba huo, ambao hutumika kama mahali pa maombi na kuanguka hadi kufariki, msimamizi wa eneo la Othany, Absalom Oyoo alithibitisha. 

"Hakuna kitambulisho cha kumtambua marehemu ni nani na uchunguzi unaendelea," alisema Oyoo, kama alivyonukuliwa na Capital.

 Msimamizi huyo alisema uchunguzi umeanzishwa ili kubaini namna marehemu alivyoanguka. Alitoa wito kwa serikali ya kaunti ya Kisumu kulizungushia uzio kwenye mwamba huo ili kuzuia watu kuingia na kutoka bila kujulikana.

 "Ingekuwa rahisi kuwafuatilia watu waliokuwa na marehemu kama walikuwa wametia sahihi kitabu cha wageni,” alisema.

 Shughuli zozote za maombi katika mwamba huo zimesitishwa ili kukamilika kwa uchunguzi wa tukio hilo. 

Mwili wa marehemu ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Rufaa na Mafunzo ya Jaramogi Oginga Odinga ukisubiri kufanyiwa uchunguzi wa maiti ili kubaini chanzo cha kifo chake. 

CHANZO-TUKO NEWS

Share:

TENGENI MAENEO YA UWEKEZAJI – WAZIRI MABULA

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza katika kikao kazi cha kujadili na kuweka mikakati ya kukwamua changamoto za sekta ya ardhi katika mkoa wa Morogoro kilichofanyika tarehe 22 Februari 2023 mkoani humo. Baadhi ya Wakuu wa wilaya za mkoa wa Morogoro wakiwa katika kikao kazi cha kujadili na kuweka mikakati ya kukwamua changamoto za sekta ya ardhi katika mkoa wa Morogoro kilichofanyika tarehe 22 Februari 2023 mkoani humo. Mkuu wa mkoa wa Morogoro Fatma Mwasa akizungumza katika kikao kazi cha kujadili na kuweka mikakati ya kukwamua changamoto za sekta ya ardhi katika mkoa wa Morogoro kilichofanyika tarehe 22 Februari 2023 mkoani humo. Mkuu wa wilaya ya Morogoro Mjini Rebecca Nsemwa akizungumza wakati wa kikao kazi cha kujadili na kuweka mikakati ya kukwamua changamoto za sekta ya ardhi katika mkoa wa Morogoro kilichofanyika tarehe 22 Februari 2023 mkoani humo. Sehemu ya washiriki wa kikao kazi cha kujadili na kuweka mikakati ya kukwamua changamoto za sekta ya ardhi katika mkoa wa Morogoro kilichofanyika tarehe 22 Februari 2023 mkoani humo.

Mkurugenzi Msaidizi Urasimishaji Makazi holela Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Nicholaus Mwakasege akiwasilisha mada ya mpango wa urasimishaji katika mkoa wa Morogoro wakati wa kikao kazi cha kujadili na kuweka mikakati ya kukwamua changamoto za sekta ya ardhi katika mkoa wa Morogoro kilichofanyika tarehe 22 Februari 2023 mkoani humo. (PICHA NA WIZARA YA ARDHI NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI)

********************

Na Munir Shemweta, WANMM MOROGORO

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amezitaka halmashauri nchini kuhakikisha zinatenga maeneo ya uwekezaji ili kurahisisha wawekezaji wanaokuja nchini kuwekeza kwenye sekta mbalimbali bila usumbufu.

Dkt Mabula ametoa kauli hiyo tarehe 22 Februari 2023 wakati wa kikao kazi cha kujadili na kuweka mikakati ya kukwamua changamoto za sekta ya ardhi katika mkoa wa Morogoro kilichofanyika mkoani humo.

Waziri Mabula amesema, Mhe Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameifungua nchi kwa kukaribisha wawekezaji ambapo alieleza kuwa tayari wawekezaji wameanza kuja kwa wingi na kushindana kwenye sekta mbalimbali kama vile kilimo, viwanda , madini na ujenzi wa nyumba.

Kwa mujibu wa Dkt Mabula, Rais Samia alielekeza kila halmashauri nchini kutenga maeneo ya uwekezaji hivyo ni jukumu la kila halmashauri kuhakikisha maeneo ya uwekezaji yanaandaliwa na kutengwa sambamba na kuwekewa mkakati utakaofanya maeneo hayo kuwa tayari kwa uwekezaji.

Akitolea mfano maeneo ya vijijini, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alisema kama vijijini maeneo yametengwa kwa ajili ya uwekezaji basi mamlaka husika zihakikishe taratibu zote za kuhaulisha ardhi ikamilike na kusubiri wawekezaji na kuacha kusubiri muekezaji aje ndiyo waanze kuhangaika kuhangaika.

‘’Tunahitaji kuwa na ardhi tayari akitokea muwekezaji akija wa kilimo tunamuambia nenda kilosa, au nenda malinyi akifika anakuta ardhi iko tayari na asifike akaanza kugombana na wananchi.

Ametoa rai kwa halmashauri nchini kuwa ‘pro active’ kwa kutenga maeneo mapema na kwenda kuyamiliki na kubainisha kuwa kama ni halmashauri ya wilaya au kijiji au mwananchi mmoja mmoja mwenye ardhi yake ambaye halmashauri inamtambua basi eneo hilo liwe limetengwa mapema.

Amesema halmashauri zikifanya hivyo au kutekeleza hayo basi azma ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhakikisha nchi inasonga mbele katika masuala ya uwekezaji na kuondoa changamoto katika uwekezaji itakuwa imesaidia sana.

Aidha, Dkt Mabula alisema ni jukumu la viongozi wote kuanzia ngazi wilaya halmashauri hadi vijiji kuhakikisha wanasimamia na kutatua changamoto zote za migogoro ya ardhi katika maeneo yao na kubainisha kuwa mgogoro wa mpaka na mpaka siyo wa waziri kwenda kuutatua na unapaswa kutatuliwa katika ngazi husika.

Akigeukia suala la urasimishaji makazi holela Dkt Mabula alisema zoezi hilo siyo program ya kudumu na ilianzishwa kwa lengo la kukabiliana na maeneo ambayo yalikuwa yameendelezwa bila kufuata taratibu za mipango miji. Programu ya urasimishaji makazi holela mwisho ni mwaka huu wa 2023.

Waziri Mabula amezielekeza mamlaka za upangaji nchini kuongeza nguvu ya kurasimisha mitaa yote iliyosalia na kuimarisha mikakati ya kuzuia ongezeko la makazi holela nchini ili kudhibiti ukuaji miji kiholela.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger