Friday, 17 February 2023

KIWANDA CHA VIJANA WALIOKOPA MAMILIONI YA FEDHA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SHINYANGA CHATEKETEA MOTO

 Kiwanda cha kutengeneza Magodoro chateketea Moto


Mwenyekiti wa kikundi cha vijana cha kutengeneza Magodoro Ally John akionyesha namna Kiwanda chao kilivyoteketea na Moto.
Mwenyekiti wa kikundi cha vijana cha kutengeneza Magodoro Ally John akionyesha namna Kiwanda chao kilivyoteketea na Moto.

Mwenyekiti wa kikundi cha vijana cha kutengeneza Magodoro Ally John akionyesha namna Kiwanda chao kilivyoteketea na Moto.

*****
KIWANDA cha kutengeneza Magodoro cha vijana wajasiriamali ambacho kipo Mtaa wa Viwandani Manispaa ya Shinyanga kimeteketea na moto.

Vijana hao wajasiriamali ni wanufaika wa mikopo fedha za mapato ya ndani ya halmashauri asilimia 10, ambazo hutolewa kwa wanawake na vijana asilimia nne na watu wenye ulemavu asilimia mbili.

Mwenyekiti wa kikundi hicho cha vijana cha kutengeneza Magodoro Ally John, akizungumza jana Kiwandani hapo, amesema Kiwanda chao kimeungua moto Februari 5 mwaka huu majira ya saa 8 usiku na kuteketeza kila kitu.

“Thamani ya mali zote ambazo zimeteketea kwenye Kiwanda chetu cha kutengeneza Magodoro ni Sh. Milioni 93 na tulikuwa na Oda ya Magodoro 282 ambayo ilikuwa kesho yake tuyapeleke Mwanza na Tabora na tulikuwa na Pikipiki mpya ndani ya kiwanda, vitu vyote vimeteketea hakuna ambacho kimeokolewa,”amesema John.

Aidha, amesema kikundi chao kinawezeshwa na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa kupewa mikopo, kwamba walianza kupewa mwaka 2017 kiasi cha fedha Sh. Milioni 15 wakarejesha fedha zote, na mwaka wa fedha (2020/2021) wakapewa tena Sh.milioni 40 na walikuwa wamerejesha Sh.milioni 10 na sasa Kiwanda kimewaka Moto.

Amesema kikundi chao kina vijana 10 na sasa hawana ajira na hawajui hatimaye yao, sababu bado wanadeni la kurejesha mkopo wa halmashauri kiasi cha fedha Sh.milioni 30 na Kiwanda ndiyo kimeteketea moto, na kuiomba halmashauri ione namna ya kuwanyanyua tena.

Naye Ofisa Maendeleo ya Jamii halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga John Tesha, amesema.....

SOMA HAPA ZAIDI CHANZO NIPASHE.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARI 17,2023

 













Share:

Thursday, 16 February 2023

MILANGO YA BIASHARA IMEFUNGUKA SOKO LA NCHI ZA AFRIKA - ALLY GUGU


Naibu Katibu Mkuu wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Ndg. Ally Gugu (Uwekezaji) akifungua Warsha ya kujadili fursa zilizopo katika soko la Biashara la Nchi za Africa katika ukumbi wa Hotel ya Sheratoni tarehe 15 Februari, 2023
Washiriki mbalimbali wa warsha ya kujadili fursa zilizopo katika soko la Biashara la Nchi za Africa katika ukumbi wa Hotel ya Sheratoni tarehe 15 Februari, 2023.
Naibu Katibu Mkuu wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Ndg. Ally Gugu (Uwekezaji) katika na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania Ndg. Gielead Teri katika ufunguzi wa Warsha ya kujadili fursa zilizopo katika soko la Biashara la Nchi za Africa katika ukumbi wa Hotel ya Sheratoni tarehe 15 Februari, 2023.
***

Serikali inaandaa mkakati maalum kwa ajili ya utekelezaji wa mpango wa kutuongoza na kuchanganua vipaumbele katika kuratibu na kushiriki soko huru barani Afrika.


Hayo yamesemwa na Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na biashara Ndg. Ally Gugu, wakati akifungua warsha ya kujadili fursa zilizopo katika soko la biashara la nchi za Africa katika ukumbi wa Hoteli ya Sheratoni tarehe 15 Februari, 2023


“Serikali imelenga kutoa elimu na ufafanuzi zaidi kwa Sekta binafsi na wafanyabiashara ili kupanua uelewa wa bidhaa na huduma ambazo zinahitajika zaidi katika soko la nchi za Afrika”,amesema Gugu.


Ndg. Gugu amesisitiza uhamasishaji na utekelezaji wa ajenda ya Afrika tunayoitaka ambapo biashara ni moja ya ajenda kuu


“Soko hili ni la watu bilioni 1.2 ambapo jana Nchi ya Comorro imeweza kuridhia ushiriki wake katika soko huru barani Afrika”. Ameongeza Gugu


Benki ya Maendeleo ya Afrika na AfriExim zimejitokeza katika kusaidia washiriki mbalimbali watakaopenda kupata huduma za kifedha ili kuwezeshwa kushiriki katika biashara kwenye soko huru barani Afrika.


Tanzania chini ya usimamizi wa Rais wa awamu ya sita Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kusimamia itifaki za kushirikisha wanawake na vijana katika soko hilo na tayari mkutano mkubwa wa kushirikisha vijana na wanawake ulifanyika Septemba 2022 ambapo Rais Samia Suluhu Hassan aliongoza viongozi mbalimbali katika mkutano huo.
Share:

TEMESA, MKANDARASI AFRICAN MARINE AND GENERAL ENGINEERING COMPANY WASAINI MKATABA WA UKARABATI MV.MAGOGONI

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) Lazaro N. Kilahala (aliyevaa suti) akisaini mkataba wa ukarabati wa kivuko cha MV. MAGOGONI pamoja na mkandarasi African Marine and General Engineering Company Ltd. inayotoka Mombasa nchini Kenya huku akishuhudiwa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Prof. Makame Mbarawa pamoja na viongozi mbalimbali akiwemo, Mhe. Mussa Azan Zungu (Mb), Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika hafla ya utiaji saini iliyofanyika leo eneo la Magogoni Kigamboni jijini Dar es Salaam. Gharama ya kukarabati kivuko hicho ni shilingi bilioni 7.5.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) Lazaro N. Kilahala kulia pamoja na mkandarasi kutoka kampuni ya African Marine and General Engineering Company Ltd. inayotoka Mombasa nchini Kenya wakionyesha mikataba yao waliyosaini leo mbele ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Prof. Makame Mbarawa ya ukarabati wa kivuko cha MV. MAGOGONI ambao unagharimu shilingi bilioni 7.5.

PICHA ZOTE NA ALFRED MGWENO (TEMESA)

*****************************

Na. Alfred S. Mgweno (TEMESA)

Serikali kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) leo imesaini mkataba wa ukarabati wa kivuko cha MV. MAGOGONI wenye thamani ya shilingi Bilioni 7.5. Mkataba huo umesainiwa leo katika eneo la kivuko cha Magogoni Kigamboni jijini Dar es Salaam kati ya Mtendaji Mkuu wa Wakala huo Lazaro N. Kilahala na mkandarasi African Marine and General Engineering Company Ltd. inayotoka Mombasa nchini Kenya na kushuhudiwa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Prof. Makame Mbarawa pamoja na viongozi mbalimbali akiwemo, Mhe. Mussa Azan Zungu (Mb), Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wabunge, Wakuu wa Wilaya pamoja na viongozi mbalimbali wa Taasisi nchini.

Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Prof. Makame Mbarawa amesema ukarabati wa Kivuko cha MV. MAGOGONI ni juhudi na mikakati ya Serikali katika kuboresha miundombinu mbalimbali ya usafirishaji nchini na kuongeza kuwa ukarabati huo utakapokamilika utaharakisha na kurahisisha shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii kwa wananchi waishio katika Wilaya ya Kigamboni, Ilala na maeneo mengine

’’Madhumuni ya ukarabati wa kivuko hiki ni kuhakikisha huduma inayotolewa na kivuko hiki ni salama kwa watumiaji na hivyo kuwaondolea wananchi kero ya usafiri inayotokana na kuchakaa kwa kivuko hiki. Kivuko hiki kilijengwa mwaka 2008 na kina uwezo wa kubeba Tani 500 yaani abiria 2000 na magari madogo 60 na ni kiunganishi muhimu kati ya maeneo ya Wilaya ya Kigamboni na Wilaya ya Ilala.’’ Amesema Profesa Mbarawa na kuongeza kuwa wakati umefika sasa wa kivuko hicho kufanyiwa ukarabati mkubwa.

’’Wakati kivuko hiki kinafanyiwa ukarabati kutakuwa na changamoto ya usafiri, kwahiyo niwaombe sana wakazi wa Dar es Dalaam hasa maeneo haya watumie kwa wingi Daraja la Nyerere ili kupunguza msongamano katika kivuko hiki, amesema Profesa Mbarawa na kuongeza kuwa wakati wa kutoa tenda Serikali inaangalia mambo mawili makubwa, ’’Jambo la kwanza tunaangalia bei, nani ni mwenye gharama za chini, kama alivosema Mtendaji Mkuu TEMESA, mkandarasi ambaye alikuwa na bei ya chini ilikuwa ni bilioni 7.5, aliyemfuatia wa pili alikuwa na bilioni 10, tofauti ya bilioni 2.5, kama hii ni pesa yako wewe utampatia nani mkataba wa kazi hiyo? Nawaachieni mjibu,’’ alimaliza Profesa Mbarawa.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mussa Azan Zungu akizungumza katika hafla hiyo amewaomba wananchi wa maeneo hayo kuvumilia changamoto ya kukosekana kwa kivuko hicho wakati kitakapokuwa kwenye matengenezo kwa kuwa matengenezo hayo yanalenga kuleta huduma bora na kivuko hicho kuwa salama kwa ajili ya kutumiwa na wananchi hao.

Naye Mbunge wa Kigamboni Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza katika hafla hiyo ametoa rai kwa Serikali kutoa fursa kwa sekta binafsi kuruhusiwa kuanza kutoa huduma ya kivuko katika eneo hilo.

Aidha, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA), Lazaro N. Kilahala akisoma taarifa fupi ya mradi huo amesema mkandarasi African Marine and General Engineering Company Ltd. Ataanza rasmi ukarabati wa kivuko hicho mara baadaa ya kulipwa malipo ya awali na anatarajiwa kukamilisha kazi hiyo ndani ya miezi sita.

’’Kivuko cha MV. MAGOGONI ni Tegemeo kubwa kwa wananchi wa Kigamboni kutokana na uwezo wake wa kubebea abiria na magari mengi kwa wakati mmoja hivyo ukarabati huu utawezesha kivuko hiki kutoa huduma ya uhakika na tija kwa wana Kigamboni.’’ Amesema Mtendaji Mkuu na kuongeza kuwa kazi ya ukarabati wa kivuko hicho itahusisha kazi za chuma, kuondoa mabati yaliyochakaa ya muundo wa chini na wa juu, ujenzi wa milango mipya ya kushushia na kupakia abiria, ukarabati wa chumba cha kuongozea kivuko, ufungaji wa injini mpya nne aina ya Caterpillar pamoja na gia boksi zake, matengenezo makubwa ya pampu jeti, marekebisho makubwa ya mfumo mzima wa umeme na elektroniki wa kivuko, kufungwa kangavuke (majenereta) mapya mawili, matengenezo ya mfumo wa tahadhari ya moto, kufunga kamera za CCTV, kuweka vifaa vya kisasa vya kuongozea kivuko, vifaa vya tahadhari na vya uokozi, pamoja na kupaka rangi kivuko chote.


Mtendaji Mkuu alimaliza kwa kuishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwa kukubali kuanza kwa utekelezaji wa mradi huo na miradi mingine na kuahidi kufanya kazi kwa weledi na jitihada kubwa ili kufikia malengo na matarajio ya Serikali na wananchi kwa ujumla.
Share:

TAKUKURU SHINYANGA : HAKUNA DOSARI UJENZI WA MADARASA, BARABARA KUNA DOSARI





Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga,Donisian Kessy

Na Halima Khoya,Shinyanga.

TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga katika kipindi cha robo pili ya mwaka wa fedha 2022/2022(Oktoba-Disemba,2022)  imeeleza jinsi ilivyojikita kwenye ufuatiliaji wa fedha za miradi kwa kutembelea ujenzi wa madarasa kwa shule zote za sekondari zilizopatiwa fedha na Serikali ili kuhakikisha fedha zilizoelekezwa katika miradi hiyo zinatumika kama ilivyokusudiwa,inakamilika kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.


Akizungumza na vyombo vya habari leo Februari 16,2023 Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga,Donisian Kessy amesema jumla ya Shilingi Bil 6.6 (6,640,000,000/)= zimeletwa kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 332,ikiwa ni utekelezaji wa mradi wa Kitaifa wa ujenzi wa madarasa 8,000 ya shule za sekondari ya mwaka 2022 ambapo ujenzi huo ulitakiwa kukamilika Desemba 30 2022.


Kessy amesema TAKUKURU ilifanya ufuatiliaji wa ujenzi wa madarasa 158 yenye thamani ya Shilingi Bil.3.3 (3,160,000,000/=) na haijabaini dosari mpaka sasa ambapo ufuatiliaji bado unaendelea.


Aidha TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga imefanikiwa kufuatilia Miradi ya maendeleo katika sekta za afya na barabara ambapo jumla ya Miradi ya maendeleo 10 imetekelezwa yenye thamani ya shilingi bil 3.6 (3,607,250/=) na dosari ndogo ndogo zilibainika.


“Mradi wa barabara ya mjini-Old Shinyanga inayotekelezwa chini ya usimamizi wa TANROADS,wenye thamani ya sh.700,010,000/= tulibaini kuwa kifusi cha subgrade layer G15 na sub base Course G25 (stabilized with cement) kimelipwa kwa urefu wa 1,080m badala ya 1,000m na kufanya mkandarasi kulipwa pesa ya ziada ya sh.12,240,000/= kwa kazi ambazo hazijafanyika,hali ya barabara ya mchepuo (diversion Road) siyo nzuri na inaathiri watumiaji”amesema Kessy.


“Ofisi ilifanya mawasiliano na meneja wa mradi TANROAD ambapo alitolea ufafanuzi kuwa wakati wa malipo walijulisha kazi ya barabara za mchepuo (access road/fider road) ambazo mkandarasi atazifanya mwishoni mwa mradi na kuahidi kuzingatia ushauri na kwa sasa barabara imerekebishwa na inapitika”ameongeza.


Kwa kipindi husika ofisi imefanya kazi za uchambuzi wa mfumo katika halmashauri (2) na Manispaa (1),(Ushetu,kahama na manispaa ya Shinyanga),ilifanyika warsha 3 na wadau husika kujadiliana mikakati ya namna ya rushwa iliyobainika na kuwekeana mikakati ya kutekeleza ili kumaliza mianya hiyo.


“Uwepo wa changamoto ya kamati ya kukusanya ushuru kwa kutumia risiti za mikono badala ya POS, changamoto ya mikataba iliyoingia manispaa juu ya uzoaji wa taka kutojulikana kwa kamati za soko,kuwepo kwa changamoto za masoko kutojua ni kiasi gani bajeti ya manispaa kinachorudi katika kuboresha miundombinu ya masoko na huduma nyinginezo katika utendaji wa masoko”amesema.


Takukuru imeweka hatua zitakazo chukuliwa kutatua adha hizo ambapo ukusanyaji wa fedha na michango yote itafanywe na kamati au watendaji wa Manispaa na ukaguzi maalumu wa mfumo wa upangishaji wa vibanda pamoja na kamati za elimu zipewe elimu juu ya usimamiaji wa uendeshaji wa masokona wahasibu wa mapato wapewe elimu.


“TAKUKURU inaendelea kutoa elimu kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa serikali,kuhakikisha miradi yote inakamilika kwa ubora,kama mtaona kuna vitendo vyovyote vinavyoonesha ubadhilifu vitoe taarifa”ameongeza.
Share:

Wednesday, 15 February 2023

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI FEBRUARI 16,2023








Share:

VIJIJI 11 WILAYANI KISHAPU HAVINA SHULE ZA MSINGI


Madiwani wilayani Kishapu wakiwa kwenye kikao cha Baraza.

Madiwani wilayani Kishapu wakiwa kwenye kikao cha Baraza.

Madiwani wilayani Kishapu wakiwa kwenye kikao cha Baraza.

Na Sumai Salum, KISHAPU

Vijiji 11 Kati ya 125 wilayani Kishapu mkoani Shinyanga havina shule za msingi hali iliyoelezwa kuwa sababu ya kushuka kwa kuwango cha ufaulu shule za msingi kutoka asilimia 69%(2022) hadi 64% (2023).

Vijiji hivyo ni                  Butungwa,Igumangobo,Igaga"A",Bulekela,Mwampalo,Ng'wanholo,Lwagalalo,Ikonda "A",Ng'wagalankulu,Malwilo na Nhendegese.

Akiwasilisha taarifa ya elimu na kujibu hoja ya elimu kwenye kikao cha Baraza la Madiwani robo ya pili leo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Afisa elimu awali na Msingi Bw. Angasilini Obeid Kweka, amesema kuwa kwa kila vijiji ambavyo havina shule za msingi Serikali ya kijiji isimamie upatikanaji wa madarasa manne na matundu ya vyoo nane.

Kweka amesema kuwa Mpango Shirikishi jamii huu umekuja na Hoja ya uhitaji wa madarasa 800 kwa wilaya nzima kutokana na muitikio wa uandikishaji wanafunzi kuongezeka ambapo kwa darasa la awali wamesajili 94% na darasa la kwanza wamesajili asilimia 104% mpaka leo na bado wanaendelea na zoezi hilo hivyo uhitaji utaongezeka zaidi.

"Baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya na sababu sio walimu kama wengi wadhaniavyo bali watoto wetu wanatembea umbali mrefu jambo ambapo sio rahisi mtoto kuvumilia anatembea zaidi ya kilometa 10 kwa siku lazima achoke na wakati mwingine asiende shule kama akikosa masomo kwa siku kadhaa ni lazima atafeli tu na wakati wa mvua pia Barbara zetu sio rafiki hawafiki mashuleni", amesema Kweka.

Mbali na hayo wakijibu hoja hiyo Diwani wa Kata ya Songwa Mhe. Abdul Ngoromole amesema wako tayari kusimamia suala hilo kwani umuhimu wa elimu wananunua hivyo ofisi ya mkuu wa wilaya na mkurugenzi waharakishe utoaji maelekezo kwa viongozi wa vijiji na kata ili kufikia Desemba 2023 wawe wamekamilisha huku akishauri fedha za kunufaisha jamii zinazozunguka mgodi zielekezwe pia kwenye ujenzi wa madarasa.


Katika hatua nyingine Diwani wa Kata ya Bunambiyu Mh. Mpemba Juma amesema pia kunahitajika kusimamia uundwaji wa bodi za shule kwani inasaidia kutatua changamoto zinazopelekea kushuka kwa ufaulu na usimamiaji wa Sheria ikilinganishwa na tukio la mwanafunzi kupata ujauzito na mwalimu mkuu Sekondari Bunambiyu kutoshirikisha mapema viongozi wa Kata hadi halmashauri wala jeshi la polisi.

"Mhe Mwenyekiti walimu hawa wanatakiwa wapunguziwe majukumu kwa mfano shule ya msingi Muguda ufaulu ni mbaya na hata shule ya msingi Beledi Mwalimu Mkuu wake ni Kaimu Mtendaji si rahisi akasimamia suala la ufaulu kabisa la sivyo ashushwe cheo", Mhe. Luhende Sana Diwani Kata ya Lagana.
Share:

EX WANGU ANATAKA MTOTO WAKE TATIZO MWANAJESHI NDIYE ALIYELEA MIMBA!

 

Jina langu Judi, miaka kama minne iliyopita nilikutana na kijana mmoja anayetokea familia ya kitajiri, tulipendana sana na tulifanya kila kitu, baada ya muda nilibeba ujauzito wake.

Katika ujana wangu nilijikuta nipo njia panda ambayo hadi leo naweza sema imeniweka kwenye mazingira magumu ila imenipa funzo kuwa tiba za asili ni muhimu kwa sisi wa Afrika na dunia kwa ujumla.

Basi kwa bahati mbaya, kumbe mwenzangu alikuwa na matatizo tangu kuzaliwa bila mimi kujua na hakuwahi kuniambia, sina hakika ni matatizo gani, ila alikuwa hawezi kujaza mtu mimba.

Hivyo nilipomwambia nina ujauzito wake, alikataa kabisa mimba, mimi nilidhani labda uoga tu ila aliendelea kunisisitiza nimtafute mwenye mimba na sio yake.

Nilishangaa sana, nikikumbuka mbona mimi sio mchepukaji kabisa na sijawa kutembea na mwanaume mwingine zaidi yake na sina kumbukumbu ya kufanya usaliti? imekuaje?

Siwezi kusahau, alinipiga sana yaani akinishtumu kuwa mimi ni msaliti na nimtafute mwenye mimba, wakati sielewi mwelekeo wa maisha, alitokea kijana Mwanajeshi, ukweli alitokea kunipenda na alinitolea mpaka posa nyumbani kwetu hivyo nikawa nasubiria tu ndoa.

Siku moja uliingia ugeni mzito pale nyumbani walituweka mtu kati na wazee wao wakisisitiza mimba sio yao na nimtaje mwenye mimba, walisisitiza kuwa mtoto wao ana matatizo na hawezi kumpa mtu mimba hivyo nipambane hali yangu na nisimjue tena.

Acha tu, niliumia sana, mbaya zaidi nilikuwa na uhakika kuwa ni yake na hakuna mtu anayenielewa, sitakaa kusahau nilijifungua kwa tabu kidogo sababu ya stress japo Mjeda alisema atalea mtoto na hana shida.

Cha ajabu kujifungua mtoto amefanana sana yule kaka, tena kafanana na baba yake kila kitu, sasa ndugu wakaajua yule ni mtoto wao, hivyo wakataka kumgharamia matuzo kila kitu.

Yule mpenzi wangu alikuja nyumbani pekee yake na kunieleza kweli alikuwa na tatizo hilo na alienda Hospitali mbalimbali bila kupona, ila aliamua kutumia dawa za mitishamba kwa siri kutoka kwa Dr. Kiwanga bila kuwaambia ndugu zake. Na sasa ameamini kweli dawa za Dr. Kiwanga zinafanya kazi vizuri.

Nimekwa njia panda maana anataka turudiane na kwao wana maisha mazuri sana, lakini mwanajeshi kashanitolea na posa na ninaogopa kumwaacha. Je, nifanye nini?.

Kumbuka Dr. Kiwanga anatibu maradhi kama kifua kikuu, kisukari, msukomo wa damu, kifafa na magonjwa mengineyo, pia anasuluhisha shida za kifamilia kama kutokouwa na uwezo wa kupata mtoto, kutopata mchumba wako wa maisha, shida za ndoa, kuwa na bahati katika maisha haswa katika michezo ya kamari na mengineyo.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na Dr. Kiwanga kwa namba +254769404965, barua pepe kiwangadoctors@gmail.com au tembelea tovuti yake ambayo ni www.kiwangadoctors.com kwa mengi zaidi.

Mwisho.




Share:

Wimbo Mpya : KISIMA - HANIFA

Share:

GGML YAGAWA TANI 23 MBEGU ZA ALIZETI KWA WAKULIMA GEITA


Mkuu wa Wilaya ya Geita, Kanali Boniphace Maghembe(katikati) akimkabidhi mbegu mkulima wa Alizeti Mhanda Juma(wa tatu kushoto) msaada uliotolewa na kampuni ya Geita Gold Mining Limited.Akishuhudia tukio hilo ni Meneja mwandamizi wa GGML anayeshughulikia mahusiano BW Gilbert Mworia(wa tatu kulia)


NA MWANDISHI WETU, GEITA

KAMPUNI ya Geita Gold Mining Limited. (GGML) imesambaza tani 23 za alizeti katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Halmashauri ya Mji wa Geita kwa lengo la kuleta mabadiliko katika sekta ya kilimo na jamii ya wakulima zaidi ya 5,875 wanaozunguka mgodi huo.


Katika msaada huo Halmashauri ya Wilaya ya Geita imepata tani 13.8 na Halmashauri ya Mji wa Geita imegawiwa tani 9.1 ikiwa ni mwendelezo wa mpango wa kampuni hiyo tangu mwaka 2015 ambapo imekuwa ikiwasaidia wakulima ambao asilimia kubwa walitegema kutumia mashamba yao kulima zaidi mahindi, mihogo, karanga na malisho ya mifugo.


Mabadiliko ya tetemeko la ardhi katika mazao yanayolimwa kufuatia programu maalum ya kuwajengea uwezo ikiwa ni sehemu ya mipango ya Mgodi ya Mazingira ya Kijamii na Kiutawala (ESG) katika eneo hilo ili kutoa elimu na mbinu bora kwa wakulima wadogo, ilisababisha kuanzishwa kwa kilimo cha alizeti kwa msaada wa kitaalamu. na Taasisi ya Kilimo ya Cholima, shirika la utafiti wa kilimo linalojishughulisha na GGML.


Akizungumza katika hafla ya kukabidhi mbegu za hizo za alizeti kwa wakulima wa Kijiji cha Kasota katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Meneja mwandamizi wa GGML anayeshughulikia mahusiano, Gilbert Mworia alisema kuwa Kampuni hiyo imetumia Sh milioni 108 kununua alizeti ili kuwanufaisha wakulima 5,875 kutoka Halmashauri zote za Mji na Wilaya ya Geita.


Alisema msaada huo unatokana na programu maalum ya kuwajengea wakulima uwezo ikiwa ni sehemu ya mipango ya Mgodi huo wa Mazingira ya Kijamii na Kiutawala (ESG) ili kutoa elimu na mbinu bora kwa wakulima wadogo.


Alisema kupitia mpango huo kulianzishwa kilimo cha alizeti kwa msaada wa kitaalamu kutoka Taasisi ya Kilimo ya Cholima, shirika la utafiti wa kilimo linalojishughulisha na GGML.


"GGML inatamani kunufaisha jamii iliyowakaribisha kwa kuanzisha miradi endelevu ambayo itadumua hata baada ya shughuli za uchimbaji madini kuisha. Tunayofuraha kusambaza mbegu hizi wakati wa mvua kwa sababu huu ndio wakati mwafaka kwa wakulima kuanza kukuza mbegu zao,” alisema.


Naye Mkuu wa Wilaya ya Geita, Kanali Boniphace Maghembe aliipongeza GGML kwa msaada huo na kuwataka wakulima wa Geita kutumia kikamilifu msaada huo katika kipindi hiki cha mvua.


“Wilaya ya Geita ina watu milioni 1.4, na asilimia kubwa ya watu hawa wanategemea kilimo. Tuna jukumu kubwa sana la kuwahimiza wakulima wetu kutumia mbinu za kisasa za kilimo kwa sababu kinaweza kubadilisha uchumi wetu kwa urahisi. Hali ya hewa ya eneo hili inaruhusu wakulima kulima mara mbili kwa mwaka, jambo ambalo linaweza kuongeza mavuno yao," DC alisema akiwakumbusha wakulima kuwa kilimo ndio uti wa mgongo wa uchumi wa nchi.


Aidha, mmoja wa wakulima wa alizeti katika Kijiji hicho cha Kasota, Saa Kumi Makungu ambaye pia Mwenyekiti wa chama cha ushirika cha NYABUSAKAMA alifurahi kupokea msaada huo na kusema utaboresha mavuno yao kwa kiasi kikubwa.


Akitoa kihistoria fupi ya kilimo kijijini hapo, Makungu alifichua kuwa zao la alizeti lilikuwa bado halijaanzishwa Kasota hadi mwaka 2015 ulipoanzishwa mpango wa pamoja wa kujenga uwezo kati ya GGML na Taasisi ya Kilimo ya Cholima.


Saa kumi alieleza kuwa aina za mbegu zinatambulika na Wakala wa Mbegu za Kilimo, zimeleta matokeo mazuri, kwa kuzalisha kati ya lita 12 na 18 za mafuta ya alizeti kwa kilo 100 za alizeti.


“Kwa kuwa mahitaji ya mafuta ya kula yakikua kwa kasi ni dhahiri mustakabali wa wakulima hawa wanaoungwa mkono na GGML ni mzuri sasa,” alisema.


Kampuni ya AngloGold Ashanti – Geita Gold Mining Limited GGML imesaidia NYABUSAKAMA kupata mashine mbili za kiwanda cha kuzalisha mafuta zenye uwezo wa kusindika mbegu za alizeti kwa kasi kubwa.


Mashine moja husindika mmea wa alizeti ili kupata mbegu na mashine ya pili husindika mbegu ili kupata mafuta ya alizeti kama zao la mwisho mchakato ambao huchukua dakika 25 kwa kilo 600 za mbegu za alizeti.

Share:

Tuesday, 14 February 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO FEBRUARI 15,2023











Share:

Wimbo Mpya : KISIMA - CHACHA

Share:

TCDC YAWAKARIBISHA WADAU SEKTA YA USHIRIKA KUJADILI NA KUWEKA MKAKATI WA KUIMARISHA SEKTA YA USHIRIKA NCHINI

 

Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC) kwa kushirikiana na Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania (TFC) wameandaa mkutano maalum wa wadau wa sekta ya ushirika unaotarajiwa kufanyika Februari 27, 2023, katika ukumbi wa mikutano wa Makao Makuu ya Benki ya CRDB.


Taarifa hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC), Abdumajid Nsekela katika mkutano na waandishi wahabari uliofanyika Makao Makuu ya Benki ya CRDB, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa TCDC, TFC, pamoja na wadau wengine wa sekta ya ushirika.

Nsekela amesema mkutano huo unalenga kuwaleta pamoja wadau wa sekta ya ushirika ili kujadili maendeleo ya ushirika na kuweka mkakati wa kuimarisha sekta ya ushirika nchini. Nsekela alitoa rai kwa wadau wote wa sekta ya ushirika kuitikia wito wa kushiriki mkutano huo kwani mawazo yao ni muhimu katika kuboresha mfumo wa ushirika.
“TCDC imedhamiria kuuboresha mfumo wa ushirika kuwa wa kibiashara na wa kisasa zaidi ili kuongeza ushiriki wa wananchi katika sekta mbalimbali, na kuongeza mchango wa sekta hii katika kupambana na umasikini, pamoja na kukuza uchumi wa nchi,” alibainisha Nsekela.

Aliongezea kuwa Kamisheni inaweka nguvu katika uanzishwaji wa mfumo wa kidijitali kuongeza ufanisi kwa Vyama vya Ushirika, kuimarisha Taasisi zinazohusika na usimamizi, kutoa elimu juu ya dhana ya ushirika ili kuongeza ushiriki wa sekta mbalimbali zaidi ya kilimo, na kuharakisha mchakato wa uanzishwaji wa Benki ya Taifa ya Ushirika.

“…pamoja na hayo katika mkutano huu tutakwenda pia kujadili Mifumo ya Masoko; usimamizi na matumizi ya mali za vyama, vyama kujiendesha kibiashara, mitaji kwenye vyama vya ushirika; Taswira ya Ushirika kwenye jamii. Maazimio yatakayofikiwa kupitia Mkutano huo yatapaswa kutekelezwa ipasavyo na kila mdau,” alisisitiza.

Nsekela ambaye amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa TCDC miezi michache iliyopita ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini Mhe. Rais Dkt. Samia Saluhu Hassan kwa miongozo na jitihada kubwa zinazofanyikwa kuimarisha ushirika, na kuahidi kushirikiana kwa karibu na Wizara ya Kilimo katika kufanikisha malengo waliyojiwekea.

Kwa upande wake Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mkurugenzi Mtendaji wa TCDC, Dkt. Benson Ndiege alisema katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na uboreshaji mkubwa wa sekta ya ushirika ambapo kumepelekea kuongezeka kwa wigo wa ushirika kwenye sekta mbalimbali, kuongezeka kwa mitaji katika vyama, na kuimarika kwa ukusanyaji wa mapato ya Serikali hususan kwatika sekta ya kilimo ambapo tozo za mazao 12 zinakusanywa kupitia ushirika.

Kwa mwaka 2021/2022 Serikali ilipokea jumla ya Shilingi 15,144,077,319.16 zikiwa ni fedha za ushuru unaotokana na zao la korosho uliolipwa na vyama vya TANECU, MAMCU, RUNALI, LINDI MWAMBAO, TAMCU na CORECU. Vilevile, jumla ya Shilingi 1,041,957,051.00 zimepokelewa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kama ushuru kutoka katika Vyama vya Ushirika vya KDCU na KCU kupitia zao la kahawa.
“Katika kipindi cha mwaka 2015 hadi 2022 tumeshuhudia wananchama wa ushirika wakiongezeka kutoka milioni 2.4 hadi milioni 7, lakini pia kumekuwa na uwezeshaji mkubwa wa masoko kupitia mfumo wa ushirika, bila kusahau ongezeko la viwanda vya ushirika ambavyo vimekuwa vikisaidia kuongeza thamani kwa upande wa mazao,” aliongezea.

Dkt. Ndiege alisema pamoja na mafanikio hayo bado kazi kubwa inahitajika kufanyika ili kuufanya ushirika kuwa na tija zaidi katika maendeleo ya wananchi mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla. Hivyo basi, aliwataka wadau wote wanaohusika na sekta ya ushrika kuhudhuria mkutano huo utakaofanyika Februari 27, 2023.

Baadhi ya wadau wanaotarajiwa kushiriki mkutano huo ni pamoja na Vyama Vikuu vya Ushirika, Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO), na Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU).


Share:

RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI MUDA HUU


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger