Tuesday, 14 February 2023
TCDC YAWAKARIBISHA WADAU SEKTA YA USHIRIKA KUJADILI NA KUWEKA MKAKATI WA KUIMARISHA SEKTA YA USHIRIKA NCHINI
RC NAWANDA AONGOZA KIKAO CHA RCC, AKASILISHWA WANAFUNZI 2344 WA KIDATO CHA KWANZA AMBAO BADO HAWAJARIPOTI SHULE
Na Marco Maduhu, SHINYANGA
KAIMU Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk. Yahaya Nawanda, ameongoza kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa (RCC) na kueleza kutoridhishwa na hatua ambayo inaendelea ya kuripoti shule kwa wanafunzi ambao wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza.
Kikao hicho kimefanyika leo Februari 14, 2023 katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, Chama na Wabunge.
Nawanda ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, amesema bado hajaridhishwa na kasi ya wanafunzi kuripoti shule ambao wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu, na kuwaagiza Wakuu wa wilaya, Wakurugenzi, Maofisa elimu na watendaji wote wa Serikali hadi kufikia Jumatano ijayo wanafunzi 2344 ambao hado wajaripoti shule, wote wawe shuleni.
“Kikao kilichopita nilikuta asilimia 60 tu ya wanafunzi ambao wameripoti shule kuanza kidato cha kwanza ni katoa maagizo sasa imefikia asilimia 93 bado asilimia 7 hivyo hadi kufikia wiki ijayo nataka nipate taarifa hakuna mwanafunzi ambaye hajaripoti shule awe na sare asiwe na sare wote wawe shuleni,”amesema Dk. Nawanda.
“Kama zoezi hili limewashinda Wakuu wangu wa wilaya niambieni niingie mwenyewe mitaani kusaka watoto wote ambao bado hawajaripoti shule, lakini najua hili haliwezi kuwashinda na imani hadi kufikia wiki ijayo nitapewa taarifa wanafunzi wote 2344 ambao walisalia kuripoti shule watakuwa shuleni,”ameongeza.
Akizungumzia suala la kilimo amewataka viongozi kuhimiza wananchi kuhifadhi chakula ambacho watafanikiwa kuvuna, pamoja na Maofisa Ugani kutoa elimu kwa wakulima kuzitumia mvua chache ambazo bado zipo kwa kulima mazao yanayostahimili ukame.
Amegusia pia suala la kampeni ya upandaji miti na kutoa wito kwa wananchi waendelee kupanda miti kwa wingi ili kuifanya Shinyanga iwe ya kijani pamoja na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Aidha, Nawanda katika kikao hicho amewataka pia viongozi wa we wabunifu katika utendaji wao kazi, pamoja na kuwa na utamaduni wa kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi ikiwamo na Migogoro ya Ardhi.
Pia amemuahidi Rais Samia pamoja na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa, kuwa ataendelea kuzisimamia vizuri fedha za miradi za maendeleo ambao zimekuwa zikitolewa na Rais na kutekeleza madhumuni yaliyokusudiwa na kujengwa kwa kiwango kikubwa.
Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa, Awali akizungumza kwenye kikao hicho, amempongeza Rais Samia kwa kutoa fedha nyingi mkoani humo na kutekelezwa miradi mbalimbali ya maendeleo, huku akiwataka viongozi kuwa fedha ambazo zinaendelea kuletwa wazisimamie vizuri na siyo kuzichezea.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye ulemavu akizungumza kwenye kikao hicho amepongeza mapinduzi makubwa ya maendeleo ambayo yamefanywa na Rais Samia katika Mkoa wa Shinyanga.
Katika kikao hicho zimewasilishwa taarifa mbalimbali pamoja na kujadiliwa zikiwamo Sekta ya Elimu, Afya, Maji, Kilimo, Umeme , Madini na Taarifa ya Benki kuu na Sensa.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk. Yahaya Nawanda akizungumza kwenye kikao cha RCC.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akizungumza kwenye kikao cha RCC.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye ulemavu, akizungumza kwenye kikao cha RCC.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akizungumza kwenye kikao cha RCC.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Prof Siza Tumbo akizungumza kwenye kikao cha RCC.
Wabunge wa Shinyanga wakiwa kwenye kikao cha RCC.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye ulemavu akiwa kwenye kikao cha RCC.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha RCC Mkoa wa Shinyanga.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha RCC Mkoa wa Shinyanga.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha RCC Mkoa wa Shinyanga.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha RCC Mkoa wa Shinyanga.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha RCC Mkoa wa Shinyanga.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha RCC Mkoa wa Shinyanga.
Kikao cha RCC kikiendelea.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha RCC Mkoa wa Shinyanga.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha RCC Mkoa wa Shinyanga.
Kikao cha RRC kikiendelea.
Mbunge wa Vitimaalum Christina Mzava akiwa kwenye kikao cha RCC.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha RCC Mkoa wa Shinyanga.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha RCC Mkoa wa Shinyanga.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha RCC Mkoa wa Shinyanga.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha RCC Mkoa wa Shinyanga.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha RCC Mkoa wa Shinyanga.
Kikao cha RCC kikiendelea.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha RCC Mkoa wa Shinyanga.
Kikao cha RCC kikiendelea.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha RCC Mkoa wa Shinyanga.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha RCC Mkoa wa Shinyanga.
HIVI NDIYO VITABU 16 VILIVYOFUTWA VISITUMIKE SHULENI
RAIS SAMIA ATANGAZA KUNUNUA KILA BAO LA SIMBA, YANGA
Monday, 13 February 2023
ASKOFU MABUSHI AONYA UCHUMBA KWA WANAFUNZI
Na Estomine Henry - Shinyanga
Askofu wa Makanisa ya IEAGT Tanzania David Mabushi ameonya wanafunzi kuwa na tabia ya mahusiano ya uchumba wakiwa bado wanasoma.
Akizungumza katika Ibada ya Jumapili Februari, 12 2023 Askofu aliwataka wazazi na walezi kuwakanya watoto kuhusu hali ya mahusiano ya uchumba wakiwa katika masomo.
Mabushi amesema,wanafunzi wengi wanashindwa kutimiza ndoto zao kwa kuanza mahusiano ya uchumba wakiwa kidato cha kwanza hadi cha tano huko shuleni kwa kudanganyana na kujikuta wanapata madhara kutoka kwa wenzao na watu nje ya shule.
Pia Mabushi alisema ,wanafunzi wengi wamebakwa,mimba za utotoni na kupata maradhi mbalimbali yaliyokwamisha kuendelea na masomo kutokana na mahusiano ya uchumba huko shuleni.
" Ndoto zenu hazitatimia nyie wanafunzi kwa tabia ya kuwa na mahusiano ya uchumba kabla ya umri sahihi, huu ni uongo wa shetani kuwadanganya ili kuharibu ndoto zenu",alisema Mabushi.
Aidha Mabushi, alikazia wazazi na walezi kuwa makini na tamthilia mbalimbali kwa kuwa ni mbegu ya kupanda fikra za mahusiano kwa watoto kabla ya umri wao.
"Najua hata wazazi na walezi ,mnapenda hizi tamthilia ila zina mtego mkubwa kwa watoto wenu,Ni vema kuchuja na kuweka msingi kipindi cha wao kutazama ,la sivyo tutaendelea kupata mabaya kwa hawa watoto maana si wote wana uwezo wa kupambanua uhalisia wa maisha ya kweli kwao", alisema Mabushi.
Kwa upande wazazi,Joshu Loibulu alisema, "Tunahitaji umakini kwa watoto na mengi machafu wanajufunza wao kwa wao ,sisi kama wazazi ni kuwa nao karibu kuwapa maadili mema."
Naye,Grace Kali alisema,Nyumba za ibada ni jukwaa jema kwa kutunza watoto kwa dunia ya sasa ili wawe na maadili mema na kuwa na hofu ya Mungu.
JINSI UNAVYOWEZA KUTAJIRIKA KUPITIA MICHEZO YA BAHATI NASIBU
Watu wengi duniani kote wamekuwa wakicheza michezo ya Bahati Nasibu lakini ukweli ni kwamba ni idadi ndogo sana ya watu ambao huibuka na ushindi wa mamilioni ya fedha.
Wengi hujikuta wakiondoka mikono mitupu tu licha ya kutia juhudi na kuwa na matumaini makubwa kuwa wataibuka washindi na kushiriki mara nyingi kama ambavyo wangepewa maelekezo.
Mimi pia nilikuwa nikishiriki mchezo mmoja maarufu wa Bahati Nasibu katika Radio kwa miaka mingi bila ushindi, ilikuwa ni utaratibu wa kutuma kiasi kidogo cha fedha ili kujitengenezea uwezekano wa kuja kushinda fedha nyingi siku mbeleni.
Wenye mchezo huo walikuwa wakisisitiza kuwa yule ambaye anacheza mara nyingi ndiye anaibuka mshindi wa mamilioni ya fedha na zawadi nyingine kama gari, nyumba na viwanja.
Hata hivyo, licha ya kujaribu mara nyingi, kila mara mshindi angetangazwa mwingine tofauti na mimi hadi nikawa najisikia vibaya, nilikuwa natamani sana na mimi siku moja nishinde fedha, nyumba au gari.
Siku moja nilipata habari mahali kuwa Dr. Kiwanga amekuwa akiwasaidia watu kushinda michezo ya Bahati Nasibu maishani mwao, wengi wametajirika mara ya kupata huduma kutoka kwake.
Nilichukua hatua ya kufanya mawasiliano naye mara moja niweze kujaribu bahati maishani mwangu, niliongea naye kwa kina na kumueleza shida yangu na mara moja aliweza kunifanyia dawa.
Basi niliendelea kushiriki kucheza michezo ya Bahati Nasibu mara nyingi zaidi nikiwa na matumaini ya ushindi, nashukuru haikupita hata wiki mbili, nilipigiwa simu kuwa nimeshinda nyumba na fedha.
Tangu wakati huo ukawa ndio mwanzo wa mimi kuagana na umasikini, kwa sasa naishi katika nyumba yangu na familia yangu tena furaha ajabu sana. Kiukweli namshukuru sana Dr. Kiwanga kwa tiba yake ya uhakika kabisa.
Kumbuka Dr. Kiwanga ana uwezo wa kuwezesha kuwa mtu wa bahati maishani, ana uwezo wa kukukinga kutokana na adui zako wanaokutakia mabaya kwa wakati wowote ule kwa muda wa siku tatu utaona matokeo yake.
Kwa mengi zaidi wasiliana naye kupitia barua pepe kiwangadoctors@gmail.com ama kwenye wavuti www.kiwangadoctors.com au waweza kuwasiliana naye kupitia nambari ya simu +254 769404965.