Saturday, 11 February 2023

PROGRAMU YA 'TAKUKURU-Rafiki' YATAMBULISHWA HALMASHAURI YA SHINYANGA




Na Halima Khoya, Malunde 1 blog
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Mkoa wa Shinyanga imetambulisha Programu ya “TAKUKURU-Rafiki” kwa Madiwani na wataalamu wa halmashauri  ya wilaya ya Shinyanga ili kuongeza ushiriki wa kila mwananchi na wadau katika kutokomeza tatizo la rushwa katika utoaji wa huduma kwa jamii na utekelezaji wa miradi ya maendeleo.


Akitambulisha programu hiyo kwenye kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika Februari 10 2023 Kata ya Iselamagazi Halmashauri ya Wilaya ya shinyanga, Afisa wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga Helga Mfuruki amesema programu hiyo inaakisi maana ya neno “Rafiki”kwa kubeba dhana ya kuwa karibu na ushirikiano na wananchi na wadau.

Amesema Programu hiyo  itatekelezwa kwa kuwa na vikao ngazi ya kata ili kutambua kero zilizopo kwenye utoaji au upokeaji wa huduma mbalimbali.


“Baada ya kutatua kero hizo zilizoachwa pasipo kutatuliwa au kupatiwa ufumbuzi zinaweza kusababisha kutokea kwa vitendo vya rushwa, washiriki wa vikao hivyo wakiwamo wananchi,viongozi wa kisiasa, watendaji wa Serikali na Wazabuni watashirikiana kutatua kero hizo au kuweka mikakati jinsi ya kuzitatua kwa pamoja”, ameeleza Mfuruki.


Mfuruki amesema programu ya “TAKUKURU-Rafiki” itachangia kukuza ustawi wa utawala bora kwa kuzuia vitendo vya rushwa visitokee katika utoaji wa huduma kwa umma au utekelezaji wa miradi ya maendeleo sambamba na kuokoa fedha za umma kwa kujengwa au kutekelezwa miradi bora, endelevu na inayokidhi thamani ya fedha iliyotumika.


Ameongeza kuwa TAKUKURU-Rafiki itasaidia kuongeza uzingatiaji wa misingi ya utawala bora, ushirikiano wa kila mwananchi na wadau katika mapambano dhidi ya Rushwa na kuaminika kwa serikali kwa wananchi inayowahudumia.


“TAKUKURU imekuwa karibu nawe mwananchi na mdau ili katika namna rafiki tushirikiane kuzuia vitendo vya rushwa visitokee katika utoaji wa huduma kwa umma na utekelezaji wa miradi ya maendeleo kupitia program hii ya “TAKUKURU-Rafiki” usikae mbali,tushirikiane ili kwa pamoja tuijenge Tanzania",amesema.

Madiwani wakiwa ukumbini
Madiwani wakiwa ukumbini
Madiwani wakiwa ukumbini
Madiwani wakiwa ukumbini
Madiwani wakiwa ukumbini
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI FEBRUARI 11,2023




Share:

Friday, 10 February 2023

KIHENZILE ASHINDA UWENYEKITI WA KAMATI YA BUNGE YA VIWANDA, BIASHARA, KILIMO NA MIFUGO KWA MARA NYINGINE TENA


*****************

MBUNGE wa Mufindi Kusini David Kihenzile ameshinda kwa kishindo kwa mara ya pili kuongoza Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo Kihenzile ameibuka kidedea baada ya kupata kura 14 sawa na asilimia 88 na kumbwaga mpinzani wake Dk Christina Ishengoma aliyepata kura 2 sawa na asilimia 12.

Kufuatia ushindi huo, Kihenzile ataongoza tena kamati hiyo kwa awamu ya pili ambayo itamalizika Julai 2025 Bunge litakapovunjwa, kujiandaa na uchaguzi mkuu wa nchi.

Awamu ya kwanza alishinda Novemba 2020 na kuiongoza kamati hiyo kwa kipindi cha miaka miwili na nusu kabla ya kumaliza muda wake jana Januari 9, 2023.

Akizungumza mara baada ya matokeo hayo, Kihenzile amesema “nawashukuru Waheshimiwa Wabunge wenzangu kwa kuendelea kuniamini na kunichagua tena kuiongoza kamati hii ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo, naamini tutaendelea kushirikiana katika kutekeleza majukumu ya kamati yaliyo mbele yetu.”

Aidha, katika uchaguzi huo, nafasi ya Makamu Mwenyekiti ameshinda Mbunge wa Wanawake kupitia Mkoa wa Dodoma, Mariam Ditopile aliyepata kura 9 sawa na asilimia 56 akimshinda Samwel Hayuma aliyepata kura nne na Isac Francis aliyepata kura tatu.
Share:

KATIBU MKUU JOWUTA AMTEMBELEA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MSAJILI WA VYAMA VYA WAFANYAKAZI NA WAAJIRI

Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Vyombo vya Habari Tanzania (JOWUTA), Selemani Msuya akizungumza jambo na Msajili wa Vyama vya Wafanyakazi na Waajiri, Pendo Berege baada ya kumtembelea ofisini kwake jijini Dodoma

Share:

TBS YAWATAKA WAANDAJI WA VYAKULA KUZINGATIA USALAMA WA CHAKULA


NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limewataka Waandaji wa vyakula katika maeneo mbalimbali nchini pamoja na wananchi kwa ujumla kuhakikisha usalama wa chakula wanachokiandaa ili kuweza kumlinda mlaji au walaji wa chakula hicho.

Akizungumza leo Februari 10,2023 Jijini Dar es Salaam, Kaimu Meneja Kitengo cha Tathmini ya Vihatarishi vya Chakula Dkt. Ashura Kilewela amesema kuna umuhimu mkubwa wa kuzingatia usalama wa chakula kwani usalama wa chakula ni jukumu la kila mmoja wetu .

Dkt.Ashura ameongelea juu ya kutenganisha chakula kibichi na chakula kilichoiva ili vimelea katika chakula kibichi visiweze kuingia katika chakula kilichoiva na kuweza kumletea madhara mlaji au walaji wa chakula hicho.

Amesema katika kuhakikisha chakula kinakuwa salama kuna ulazima wa kutumia maji na malighafi salama kwani katika uandaaji wa chakula usipotumia malighafi salama uwezekano wa kuhamisha ule uchafuzi ni mkubwa.

"Mfano umeandaa nyama ambayo imetokana na mfugo ambao umetumia madawa yasiyo salama au kuna mabaki ya dawa za mifugo katika nyama ile hauna namna wewe muandaaji wa chakula kutoa yale mabaki ya dawa katika chakula kwahiyo ni msingi muhimu kuzingatia utumiaji wa malighafi iliyosalama". Amesema Dkt.Kilewela.

Pamoja na hayo amesema wanashirikiana na Wizara pamoja na Taasisi mbalimbali kutoa elimu na kuhakikisha wakulima mashambani wanaelewa athari za matumizi ya dawa kwenye chakula na kuhakikisha chakula wanachokizalisha ni salama .

Share:

WATUMISHI HOUSING YAVUKA LENGO UKUSANYAJI MAPATO





Na Dotto Kwilasa, DODOMA.

MKURUGENZI Mtendaji wa Taasisi ya Watumishi Housing Investment (WHI), Dokta Fred Msemwa amesema kupitia Mfuko wa Faida fund ambao unatumia mfumo wa malipo ya Serikali wamevuka lengo la kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 12.9 huku matarajio yao yakiwa ni kukusanya bilioni 7.8 ikiwa ni ndani ya miezi miwili tangu kuanzishwa kwake.


Hayo ameyasema jijini Dodoma wakati alipokuwa akieleza utekelezaji wa majukumu ya mfuko huo ambapo alisema kuwa wamefanikiwa kuwanufaisha watanzania kuongeza kipato kupitia uwekezaji wa pamoja katika Faida Fund.


Amesema kuwa makusanyo hayo ya Mfuko ni katika kipindi cha Novemba mwaka jana na mpaka kufikia Februari 9 walikuwa na bil.14, na kusema kuwa fedha hizo wameziwekeza katika masoko ya fedha ikiwemo mabenki na Serikali ambapo watanzania zaidi ya 4000 wamejiunga.


"Kwa sasa Watanzania 80000 ndio wanaoshiriki katika uwekezaji wa pamoja wa soko la fedha, hivyo nawashauri watanzania kujitokeza kujiunga na mfuko huu ambao utawawezesha kufikia malengo, kujiletea maendeleo na kujikwamua kiuchumi”, amesema.


Akizungumzia uendeshaji wa Mfuko huo, Mkurugenzi huyo amesema kuwa Faida Fund unafanya kazi kwa njia ya kuuza vipande, ambapo bei ya kipande ilikuwa sh 100, mpaka sasa thamani ya kipande imefikia sh 101.1, hivyo thamani ya vipande imeendelea kukua.


“ Watumishi Houseng ndio wanaonunua vipande kutoka kwa wawekezaji ambao ni wanachama wa Mfuko huo watakaokuwa na uhitaji wa kuuza vipande vyao ili wapate Fedha”, amesema.


Dk. Msemwa ametaja faida ya kuwekeza kwenye Mfuko huo kuwa ni pamoja na kuwa na uwezo wa kuwekeza katika masomo ya Fedha bila kulazimika kufuata mlolongo mrefu ikiwemo kwenda kwa madalali, uwekezaji hufanyika kwa njia simu hivyo kuokoa muda na kuwa na usalama wa fedha na kupata unafuu na kuwekeza bila tozo huku uwekezaji wako ukitambulika kwa kasi kubwa.


Amesema uwekezaji unaweza ukautumia kama dhamana pale utakapohitaji mkopo wa Benki ili kujiongeza zaidi kiuchumi na Mfuko wa faida fund ni endelevu na unalengwa sekta zote.
Share:

RC NAWANDA AKABIDHI PIKIPIKI KWA MAAFISA UGANI MKOA WA SHINYANGA...."MSITUMIE KWA ANASA, ZIKASAIDIE WAKULIMA"




Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yahaya Nawanda amekabidhi pikipiki 224 zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maafisa ugani kilimo mkoa wa Shinyanga.

Hafla fupi ya ugawaji wa pikipiki kwa maafisa ugani imefanyika leo Ijumaa Februari 10,2023 katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na kuhudhuriwa na viongozi na maafisa ugani kutoka wilaya za Kishapu, Shinyanga na Kahama.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Yahaya Nawanda ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu amesema jumla ya pikipiki zilizotolewa mkoa wa Shinyanga ni 224 ambapo Wilaya ya Kahama inapata pikipiki 100, Shinyanga 82 na Kishapu 39.
“Pikipiki hizi ni kutoka kwa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan. Nendeni mkazitunze zidumu ili kufikia malengo ya 10/30 ambapo tunataka kilimo kichangie asilimia 10 ya mapato ya nchi ifikapo mwaka 2030. Msizigeuze za kufanyia anasa wala kufanyia biashara ya bodaboda bali kazitumieni kuleta tija kwa wananchi/wakulima. Tunataka mzitumie kusaidia wananchi na si vinginevyo”,amesema Dkt. Nawanda.

“Pikipiki hizi ni mali ya Serikali, hizi ni fedha za umma na Mhe. Rais Samia ameleta pikipiki hizi ili tuongeze tija katika kilimo, tufanye kilimo biashara. Tunataka tuone tija ya pikipiki hizi, hatuwezi kufikia ajenda ya 10/30 kwa kupiga maneno tu hivyo tunataka vitendo zaidi ili kuwasaidia wakulima”,ameongeza Dkt. Nawanda.

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Mhe. Anord Makombe akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mabala Mlolwa ameipongeza serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa dhamira kubwa inayoonesha katika kuleta mageuzi makubwa kwenye sekta ya kilimo ikiwemo kuongeza bajeti katika sekta ya Kilimo huku akieleza kuwa Serikali itakeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa vitendo.

Kwa upande, Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mkude na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi wameahidi kusimamia matumizi yaliyokusudiwa ya pikipiki hizo huku wakiwasisitiza maafisa ugani kuepuka kubadilisha matumizi ya pikipiki hizo.

Nao baadhi ya maafisa ugani wameishukuru serikali kwa kuwapatia vitendea kazi hivyo wakisema vitawasaidia kuwafikia wakulima wengi zaidi ili kuhakikisha kilimo kinakuwa na tija.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yahaya Nawanda akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi pikipiki 224 kwa maafisa ugani mkoa wa Shinyanga leo Ijumaa Februari 10,2023. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yahaya Nawanda akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi pikipiki 224 kwa maafisa ugani mkoa wa Shinyanga
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yahaya Nawanda akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi pikipiki 224 kwa maafisa ugani mkoa wa Shinyanga
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yahaya Nawanda akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi pikipiki 224 kwa maafisa ugani mkoa wa Shinyanga
Muonekano wa sehemu ya pikipiki 224 zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maafisa ugani mkoa wa Shinyanga.
Muonekano wa sehemu ya pikipiki 224 zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maafisa ugani mkoa wa Shinyanga.
Muonekano wa sehemu ya pikipiki 224 zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maafisa ugani mkoa wa Shinyanga.
Muonekano wa sehemu ya pikipiki 224 zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maafisa ugani mkoa wa Shinyanga.
Muonekano wa sehemu ya pikipiki 224 zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maafisa ugani mkoa wa Shinyanga.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yahaya Nawanda akikata utepe wakati wa hafla ya kukabidhi pikipiki 224 kwa maafisa ugani mkoa wa Shinyanga
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yahaya Nawanda akikata utepe wakati wa hafla ya kukabidhi pikipiki 224 kwa maafisa ugani mkoa wa Shinyanga
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yahaya Nawanda akikata utepe wakati wa hafla ya kukabidhi pikipiki 224 kwa maafisa ugani mkoa wa Shinyanga
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yahaya Nawanda akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mkude (kushoto) pikipiki kwa maafisa ugani wilayani Kishapu
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yahaya Nawanda akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi pikipiki kwa maafisa ugani wilayani Shinyanga.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yahaya Nawanda akifuatiwa na Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mkude  (katikati) na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko wakijaribishia pikipiki zilizotolewa kwa maafisa ugani
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yahaya Nawanda (katikati) , Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mkude  (wa pili kushoto) ,Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko (kushoto), Mwenyekiti wa CCM Shinyanga Mjini, Mhe. Anord Makombe na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi wakiwa wamepanda kwenye pikipiki zilizotolewa kwa maafisa ugani
Maafisa ugani na wadau wakiwa kwenye hafla ya kukabidhi pikipiki kwa maafisa ugani mkoa wa Shinyanga
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Prof. Siza Tumbo akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi pikipiki 224 kwa maafisa ugani mkoa wa Shinyanga
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Mhe. Anord Makombe akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi pikipiki 224 kwa maafisa ugani mkoa wa Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mkude akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi pikipiki 224 kwa maafisa ugani mkoa wa Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi pikipiki 224 kwa maafisa ugani mkoa wa Shinyanga 
Share:

Thursday, 9 February 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARI 10, 2023



Magazeti ya Tanzania leo Ijumaa Februari 10,2023















Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger