Thursday, 9 February 2023

WADAU SHINYANGA WAFANYA KIKAO CHA TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA MKATABA WA LISHE, CHANJO NA BIMA YA AFYA KWA WOTE...RC NAWANDA ATOA MAAGIZO MAZITO


Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yahaya Nawanda akizungumza wakati wa Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote  kilichohudhuriwa na wadau mbalimbali wa afya. Picha na Kadama Malunde
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yahaya Nawanda akizungumza wakati wa Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote  kilichohudhuriwa na wadau mbalimbali wa afya.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yahaya Nawanda ameagiza kila Halmashauri ya wilaya Mkoani Shinyanga kuhakikisha inafikia asilimia 100 ya chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi kwa wasichana wa umri wa miaka 14 (HPV) dozi ya kwanza (HPV 1) ifikapo Machi 15,2023 na asilimia 100 kwa HPV dozi ya pili ifikapo Septemba 2023.

Dkt. Nawanda ametoa agizo hilo leo Alhamisi Februari 9,2023 wakati wa Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa afya.

Lengo la Kikao hicho ni kufanya tathmini ya utekelezaji wa Mkataba wa Lishe kwa kipindi cha Mwezi Julai hadi Desemba 2022 uliosainiwa baina ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na Wakuu wa Mikoa yote ya Tanzania bara Septemba 30,2022.
Wadau wakiwa ukumbini.

Licha ya kuwapongeza watoa huduma kwa kufikia asilimia 100 ya utoaji wa chanjo ya UVIKO – 19 , Polio na chanjo ya kuzuia donda koo, Dkt. Nawanda amesema Chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi kwa wasichana wa umri wa miaka 14 (HPV) na Chanjo ya Surua si ya kuridhisha hivyo kuagiza Halmashauri kuchukua hatua kufikia malengo yaliyokusudiwa.


“Naelekeza kila halmashauri ihakikishe inafikia asilimia 100 ya chanjo ya HPV dozi ya kwanza (HPV 1) ifikapo Machi 15,2023 na asilimia 100 kwa HPV dozi ya pili ifikapo Septemba 2023. Pia kila halmashauri ihakikishe Chanjo ya Surua Rubella dozi ya pili iwe imefikia kiwango cha asilimia 100 ifikapo Septemba 15,2023”,amesema Dkt. Nawanda.

Akizungumzia kuhusu Utoajia Huduma za Lishe, Nawanda amesema Mkoa wa Shinyanga unaendelea kutekeleza afua za lishe ambapo umetekeleza kwa ufanisi mkubwa kwa baadhi ya viashiria vilivyo kwenye mkataba wa Lishe. Lakini takwimu zinaonyesha viashiria vya utoaji wa fedha zilizopangwa kutekeleza shughuli za lishe, utoaji wa huduma za chakula kwa wanafunzi shuleni, upimaji madini joto kwenye chumvi bado hauridhishi.


“Halmashauri zilizotoa fedha kwa kiasi kidogo zaidi ni Manispaa ya Shinyanga (34.66%), Msalala (43.89%), na Ushetu (48.46%), hivyo nawaelekeza Wakurugenzi kuhakikisha fedha zilizopangwa kutekeleza afua za lishe zinatolewa zote kabla ya Juni 30,2023. Pia Halmashauri za Kishapu na Ushetu kuhakikisha vitendanishi vya kupimia uwepo wa madini joto (Lodine test kit) kwenye chumvi vinakuwepo na upimaji ufanyike”,amesema Dkt. Nawanda.
Wakurugenzi wa Halmashauri na wadau wa afya wakiwa ukumbini.

Pia amewataka Maafisa Elimu (Msingi na Sekondari) na Wakuu wa Shule washirikiane na kamati za shule kuhakikisha chakula kinatolewa kwa wanafunzi kulingana na mwongozo wa lishe shuleni.


Kuhusu Bima ya Afya kwa Wote, Dkt. Nawanda amesema bima hiyo itasaidia kutatua changamoto za huduma ya afya hivyo kuwataka viongozi wa ngazi mbalimbali kuhakikisha wanahamasisha wananchi kupata huduma ya bima ya afya kwa wote pindi Mswada utakapopitishwa Bungeni.


Katika hatua nyingine amewataka Wakuu wa wilaya na Wakurugenzi kushirikiana na watoa huduma za afya ili kuhakikisha huduma za afya zinatolewa kwa ubora unaostahili huku akiwataka pia Wakuu hao wa Wilaya kuhamasisha wananchi kupata Vyeti vya kuzaliwa ndani ya siku 90 baada ya kuzaliwa ambavyo vinatolewa bure.
“Vyeti vya kuzaliwa vitolewe ndani ya siku 90 na iwe ajenda kwenye vikao vya Baraza la Madiwani. Hamasisheni wananchi wanapata vyeti vya kuzaliwa kwa haraka ili watoto wawe na vyeti ili kuepuka safari za kwenda kwa Wakuu wa wilaya kufuatilia vyeti vya kuzaliwa. Tuachane na tabia ya kufuatilia vyeti vya kuzaliwa watoto wakiwa na umri wa miaka 16”,amesema Mkuu huyo wa Mkoa.

Katika kikao hicho cha tathmini, wadau wamejadiliana kwa kina sababu za baadhi ya viashiria kutotekelezwa kama ilivyotarajiwa na kuweka mikakati thabiti ya kuongeza kasi ya utekelezaji wa kuinia hali ya lishe mkoani Shinyanga. Kuwasilisha kadi alama ya utekelezaji wa mkataba wa Lishe kwa kipindi cha miezi 6 (Julai- Desemba 2022), kutoa taarifa ya hali ya utekelezaji wa huduma za chanjo ikiwemo UVIKO-19 na kutoa elimu ya Bima ya Afya kwa wote.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yahaya Nawanda akizungumza wakati wa Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote  kilichohudhuriwa na wadau mbalimbali wa afya.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yahaya Nawanda akizungumza leo Alhamisi Februari 9,2023 wakati wa Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote  kilichohudhuriwa na wadau mbalimbali wa afya
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yahaya Nawanda akizungumza wakati wa Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote  kilichohudhuriwa na wadau mbalimbali wa afya.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yahaya Nawanda akizungumza wakati wa Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote  kilichohudhuriwa na wadau mbalimbali wa afya.
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Prof. Siza Tumbo akizungumza kwenye Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile akizungumza kwenye Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhee. Eliaas Ramadhani Masumbuko akizungumza kwenye Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza kwenye Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita akizungumza kwenye Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote
Wadau wa afya wakiwa kwenye Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mkude na Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita (kulia) wakisoma nyaraka kwenye Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote
Wadau wa afya wakiwa kwenye Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote

Wadau wa afya wakiwa kwenye Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote
Wadau wa afya wakiwa kwenye Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote
Mratibu wa Chanjo Mkoa wa Shinyanga, Timoth Sosoma akitoa taarifa ya hali ya utekelezaji wa huduma za chanjo ikiwemo UVIKO-19  kwenye Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote
Afisa Lishe Mkoa wa Shinyanga, Yusuph Hamis akiwasilisha kadi alama ya utekelezaji wa mkataba wa Lishe kwa kipindi cha miezi 6 (Julai- Desemba 2022) kwenye Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote
Meneja wa Bima  ya Afya (NHIF) Mkoa wa Shinyanga Isack Katenda akitoa elimu ya Bima ya Afya kwa wote kwenye Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Girl Effect, Khalila Mbowe akielezea shughuli wanazofanya mkoani Shinyanga kwenye Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Girl Effect, Khalila Mbowe akielezea shughuli wanazofanya mkoani Shinyanga kwenye Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Girl Effect, Khalila Mbowe akielezea shughuli wanazofanya mkoani Shinyanga kwenye Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote
Kaimu Meneja Mradi wa ACHIEVE Shinyanga unaotekelezwa na Shirika la NELICO kwa kushirikiana na Shirika la PACT, Fortunatus Richard akizungumza kwenye Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote
Wadau wa afya wakiwa kwenye Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote

Wadau wa afya wakiwa kwenye Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote
Wadau wa afya wakiwa kwenye Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote
Wadau wa afya wakiwa kwenye Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote
Wadau wa afya wakiwa kwenye Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote
Wadau wa afya wakiwa kwenye Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote
Wadau wa afya wakiwa kwenye Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote
Wadau wa afya wakiwa kwenye Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote
Wadau kutoka Shirika la Girl Effect wakiwa kwenye Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote
Wadau wa afya wakiwa kwenye Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote
Wadau wa afya wakiwa kwenye Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote
Wadau wa afya wakiwa kwenye Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote
Wadau wa afya wakiwa kwenye Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote
Wadau wa afya wakiwa kwenye Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote

Wadau wa afya wakiwa kwenye Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yahaya Nawanda (kulia) akiwakabidhi cheti viongozi wa wilaya ya Kahama kutokana na kuibuka Washindi wa pili wa kwenye Mashindano ya usafi wa afya na mazingira kwa Hospitali za Wilaya nchini Tanzania. Aliyevaa kilemba ni Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yahaya Nawanda (kulia) akiwakabidhi cheti viongozi wa wilaya ya Shinyanga kutokana na kuibuka Washindi wa kwanza wa afya ya usafi na mazingira kwa Manispaa nchini Tanzania. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Jomaary Satura akifuatiwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Elias Ramadhan Masumbuko na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Johari Samizi.
Wadau wa afya wakiwa kwenye Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote

Wadau wa afya wakiwa kwenye Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote
Share:

UTEUZI: RAIS SAMIA AMTEUA MHANDISI MUSA NYAMSINGWA KUWA MWENYEKITI WA BODI SIDO

Share:

UTEUZI: EPHRAIM BALOZI MAFURU ATEULIWA KUWA MTENDAJI MKUU AICC

Share:

UOKOAJI WAENDELEA TETEMEKO LA ARDHI UTURUKI, IDADI YA VIFO YAFIKIA ZAIDI YA 12,000



Idadi ya vifo kutoka nchi zote mbili ilitarajiwa kuongezeka kwani mamia ya majengo yaliyoporomoka katika miji mingi yamekuwa makaburi ya watu waliokuwa wamelala wakati tetemeko hilo lilipotokea.

Katika mji wa Uturuki wa Antakya, makumi ya maiti, baadhi zikiwa zimefunikwa kwa blanketi na shuka na nyingine zikiwa kwenye mifuko ya miili, zilipangwa chini nje ya hospitali.


Melek, 64, aliomboleza ukosefu wa timu za uokoaji. "Tulinusurika na tetemeko la ardhi, lakini tutakufa hapa kutokana na njaa au baridi."

Wengi katika eneo la maafa walikuwa wamelala ndani ya magari yao au mitaani chini ya blanketi kwenye baridi kali, wakihofia kurejea kwenye majengo yaliyotikiswa na tetemeko hilo la kipimo cha 7.8 - ambalo lilikuwa baya zaidi nchini Uturuki tangu 1999 - na kwa tetemeko kubwa la pili saa chache baadaye.

Idadi ya vifo iliyothibitishwa iliongezeka hadi 9,057 nchini Uturuki siku ya Jumatano, na nchini Syria ilipanda hadi angalau 2,950, kulingana na serikali na huduma ya uokoaji inayofanya kazi katika eneo linaloshikiliwa na waasi kaskazini magharibi.

Maafisa wa Uturuki wanasema kuwa takriban watu milioni 13.5 waliathirika katika eneo linalochukua takriban kilomita 450 kutoka Adana magharibi hadi Diyarbakir mashariki. Nchini Syria, watu waliuawa hadi kusini kama Hama, kilomita 250 kutoka kitovu cha tetemeko.

Baadhi ya waliofariki Uturuki walikuwa wakimbizi kutoka vita vya Syria. Mifuko ya miili yao ilifika mpakani kwa teksi, magari ya kubebea mizigo na kurundikana juu ya malori ya gorofa ili kupelekwa sehemu za mwisho za kupumzika katika nchi yao.

Zaidi ya watu 298,000 wamekosa makazi na makazi 180 ya waliokimbia makazi yao yamefunguliwa, vyombo vya habari vya serikali ya Syria viliripoti, vikirejea maeneo yaliyo chini ya udhibiti wa serikali, na ambayo hayashikiliwi na mirengo ya upinzani.

Nchini Syria, juhudi za kutoa misaada zinatatizwa na mzozo ambao umegawanya taifa hilo na kuharibu miundombinu yake.

Uwasilishaji wa msaada wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa kupitia Uturuki kwa mamilioni ya watu kaskazini-magharibi mwa Syria unaweza kuanza tena Alhamisi baada ya operesheni ya muda mrefu kusitishwa na tetemeko hilo, maafisa wa Umoja wa Mataifa walisema

.Katika mji wa Aleppo nchini Syria, wafanyakazi katika hospitali ya Al-Razi walimhudumia mtu aliyejeruhiwa ambaye alisema zaidi ya jamaa kumi na wawili akiwemo mama yake na babake waliuawa wakati jengo walilokuwamo lilipoporomoka.

Chanzo - BBC SWAHILI
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI FEBRUARI 9,2023












Share:

Wednesday, 8 February 2023

WAHANDISI GGML WAFANYA ZIARA YA MAFUNZO DARAJA LA KIGONGO–BUSISI


Mhandisi Abdukarim Majuto kutoka kundi la Makampuni ya Ushauri wa mradi wa ujenzi wa daraja hilo la Kigongo – Busisi, akitoa maelezo ya mradi huo kwa Wahandisi na watalaam mbalimbali kutoka GGML.


Na Mwandishi wetu -

KUNDI la wahandisi 40 kutoka kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) wametembelea daraja la Kigongo-Busisi linalounganisha mikoa ya Mwanza na Geita kwa lengo la kujifunza na kubadilishana uzoefu kuhusu mambo mapya kuhusu sayansi, teknolojia na uvumbuzi unaotumika sasa dunia kwenye sekta ya ujenzi.


Ziara hiyo ambayo ni sehemu ya mipango ya Kampuni ya GGML kuendeleza wafanyakazi wake kupitia ziara mbalimbali za kimafunzo kwenye miradi mikubwa ya kihandisi, imefanyika mwishoni mwa wiki.


Akitoa maelezo kwa wahandishi hao kutoka GGML, Mhandisi Abdukarim Majuto kutoka kundi la Makampuni ya Ushauri wa mradi wa ujenzi wa daraja hilo la Kigongo – Busisi alisema mradi huo umetumia teknolojia ya hali ya juu inayotumiwa na wahandisi duniani kote.


Alisema teknolojia inayotumika katika ujenzi wa miradi mikubwa chini ya maji ni moja ya kivutio cha kutembelea eneo la Daraja la Kigongo Busisi.


“Daraja lina urefu wa kilometa 3.2 katika Ghuba ya Mwanza na kuunganisha Kigongo mkoani Mwanza na Busisi mkoani Geita, ni moja ya maeneo ya kuvutia zaidi nchini,” alisema.


Ziara hiyo iliyohudhuriwa na vikundi vya mafundi wakiwemo wahandisi wa mitambo, umeme na viwanda, wasimamizi wa miradi, mafundi mekanika na wakuchomelea vyuma.


Aidha, Meneja wa Miundombinu wa GGML, Eliakim Kagimbo, alifichua kuwa Kampuni inapenda kutumia daraja hilo kama jukwaa la kujifunzia ili kupata maarifa ya kina juu ya vipengele vya kiufundi vya mradi mzima.


“Tunafuraha kuona daraja hili linajengwa karibu na tunakofanyia shughuli zetu. Kama unavyojua, GGML imetekeleza miradi kadhaa ya uhandisi kwa miaka mingi na daraja hili linatoa fursa kwetu kuboresha ujuzi wetu,” alisema.


Kwa upande wake msimamizi wa ujenzi wa TANROAD katika daraja hilo Mhandisi William Sanga, alikaribisha ziara hiyo ya mafunzo na kubainisha kuwa kukamilika kwa daraja hilo ni suala muhimu katika utekelezaji wa programu ya maendeleo ya nchi.


“Daraja la Kigongo–Busisi litakuwa kiungo muhimu kati ya Mwanza na mikoa ya jirani pamoja na nchi jirani. Kwa hivyo lina uwezo wa kuchochea ukuaji wa uchumi katika eneo hilo. Daraja hili litapunguza kiasi kikubwa cha foleni katika njia hii na pia kuboresha usalama wa watumiaji katika kivuko cha ziwa hili," alisema.


Tangu kuanzishwa kwake, GGML imekuwa ikifanya kazi kwa karibu na mamlaka za serikali za mitaa kusaidia miradi kadhaa ya jamii katika mkoa wa Geita kupitia Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi pamoja na programu za kitaifa.
Mhandisi Abdukarim Majuto kutoka kundi la Makampuni ya Ushauri wa mradi wa ujenzi wa daraja hilo la Kigongo – Busisi, akitoa maelezo ya mradi huo kwa Wahandisi na watalaam mbalimbali kutoka GGML.
Share:

DC MAKILAGI  AIPONGEZA EWURA KWA UTENDAJI WAKE


Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mhe.Amina Makilagi,akizungumza wakati akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.Adam Malima kilichofanyika leo Februari 8,2023 jijini Mwanza.


KATIBU Mkuu TUGHE Taifa Mhandisi Amani Msuya akiwasilisha salamu za TUGHE Taifa katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kilichofanyika leo Februari 8,2023 jijini Mwanza.


Mwenyekiti wa TUGHE ,Tawi la EWURA Mhandisi Victor Labaa akitoa neno la shukrani wakati wa kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kilichofanyika leo Februari 8,2023 jijini Mwanza.



Wajumbe wa Baraza wakifatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kilichofanyika leo Februari 8,2023 jijini Mwanza.


Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mhe.Amina Makilagi,akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe mara baada ya kufungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.Adam Malima kilichofanyika leo Februari 8,2023 jijini Mwanza.

...................................

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mhe. Amina Makilagi ameipongeza Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kwa utendaji wenye ufanisi.

Mhe. Makilagi, ametoa pongezi hizo wakati akifungua kikao cha tano cha Baraza la Wafanyakazi wa EWURA, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.Adam Malima, leo tarehe 8. 02.2023, jijini Mwanza.

“Ninaipongeza EWURA, kwa kazi kubwa ya udhibiti ambayo mmeendelea kuifanya, tumeona hasa kwenye bei za mafuta, kupunguza uchakachuaji, jinsi mnavyosimamia uagizaji mafuta kwa pamoja na mnavyopanga bei za maji,tunawashukuru sana kwa kuikomboa jamii, mmepunguza changamoto nyingi” alisema Mhe. Makilagi.

Mha. Poline Msuya, aliyemuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt. James Andilile katika kikao hicho, amesema Baraza la Wafanyakazi ni nyenzo muhimu katika utendaji wa taasisi, kwani ni njia mujarab ya ushirikishwaji wa wafanyakazi katika uamuzi wa masuala yanayowahusu kwenye utendaji wao wa kila siku.

Kwa upande wake, Katibu wa TUGHE Taifa, Mha. Amani Msuya, ametumia fursa hiyo kuipongeza EWURA kwa kuendelea kujali maslahi ya wafanyakazi wake na kusisistiza kwamba, upimaji utendaji wa wafanyakazi unapaswa kuwa wa wazi na usawa ili kuondoa malalamiko mahali pa kazi.

Aidha, Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la EWURA, Mha. Victor Labaa, amesema Baraza litaendelea kushirikiana na menejimenti katika kuimarisha ufanisi wa utendaji kwa mustakabali wa EWURA na Taifa ujumla.
Share:

NIMEPATA KISONONO KATIKA MADANGURO!


Kwa hakika tamaa za ujana ni mbaya sana, na yeyote anayejaribu kukidhi tamaa zake za ujana kwa pupa ni lazima utapata tabu sana kama ambavyo zilinikuta na mimi miaka ya nyuma.

Jina langu ni Seif kutokea jijini Nairobi nchini Kenya, miaka miwili iliyopita baada ya kupata kazi yenye mshahara mzuri, nilijikuta nikiwa na tamaa kubwa sana ya ngono.

Kila mwanamke mzuri ambaye alipita mbele yangu, basi mara moja ningetamani kushiri naye kitendo hilo, hali hiyo ilipelekea siku moja kwenda kwenye madanguro kutafuta mwanamke wa kufanya naye ngono.

Siwezi kusema uongo, huku nilikutana na wanawake wengi wazuri hadi kushindwa nichague yupi na niache yupi, ila mwisho wa siku nilichagua mmoja na kufanikiwa kushiriki naye ngono.

Basi huo ukawa ndio mtindo wangu wa kila mara, isingeweza kupita siku mbili bila kwenda kununua mwanamke huko, kibaya zaidi nilikuwa nashiriki ngono bila kitumia kinga.

Mtindo wangu huo mpya wa maisha, ulikuja kunigharimu vibaya sana baada ya kuja kuugua ugonjwa ulionisumbua sana ambao ni kisonono, katika maisha yangu sijawahi kuumwa kama wakati huo.

Nilitumia dawa za aina mbalimbali bila kupona hadi nikahisi ugonjwa ule huwenda nilitupiwa kwa njia za kishirikina maana sijawahi kuumwa halafu nikatumia dawa nikaacha kupona, hii ndio ilikuwa mara ya kwanza.

Baada ya kusumbuka sana, kuna siku niliona tangazo sehemu fulani kuwa AfricanDoctors wanatibu magonjwa mbalimbali ikiwemo kisonono, ndipo nikaamua kuwasiliana nao na kuwaomba dawa yao.

Hazikupita siku nyingi waliweza kunitumia dawa yangu na mara moja niliweza kuitumia, nashukuru polepole nilianza kujisikia nafuhu katika mwili wangu na sasa nimepona kabisa.

Wakati huo ambapo mwili wangu na afya imerejea katika hali yake ya kawaida, nimeacha kabisa kwenda kwenye madanguro kununua wanawake, sasa najipanga nioe mwanamke wangu wa maisha.

Wasiliana na AfricanDoctors kwa namba +254719153099

Mwisho.
Share:

FANYA HIVI UWE NA NGUVU YA USHAWISHI AU KIONGOZI, MWANASIASA MZURI!

Hakuna kitu kizuri katika maisha au jamii kama kuwa na nguvu ya ushawishi, hiki ni kitu ambacho kila mtu anapenda kuwa nacho ingawa wanasiasa mara nyingi ndio huwa ukitamani ili waweze kufanya siasi zao kwa wepesi zaidi.

Singependa kutaja jina langu ila mimi ni miongoni mwa viongozi au wanasiasa wenye ushawishi kubwa katika eneo la Meru nchini Kenya, wananchi na jamii yangu wanapenda kile ambacho nafanya na hata kuzungumza.

Hata hivyo, miaka ya nyuma hali haikuwa hivyo, kama ungekuwa ni mkutano wa kisiasa, basi kila ambapo ningependa jukaani watu wangeweza kuondoka, ilishawahi kunitokea hiyo mara kadhaa.

Ukweli ni kwamba hakuna mtu angevutiwa na vile ambavyo ningezungumza, na hiyo ni ishara tosha sikuwa na nguvu ya ushawishi katika macho yao na masikio yao.

Jamaa yangu mmoja ambaye alishuhudia watu wakiondoka katika mkutano mmoja wa kisiasa baada ya mimi kupewa nafasi ya kuzungumza, alinijia na kuniambia lazima nikubali kushughuli hali hiyo kwa ghrama yoyote kama ni kweli nina nia ya kuja kuwa kiongozi hapo baadaye.

Ndipo tulipoanza kutafuta tiba ya hilo na mwisho wa siku tukaweza kuwapata AfricanDoctors ambao kwa hakika naweza kusema wanasiasa wengi wamekuwa wakikimbilia kwao kwa ajili ya kupata huduma zao.

Basi mimi na yule jamaa yangu tulisafiri hadi kwao na kuwaeleza shida zetu ambazo tunataka utatuzi wao, ndipo walipoketi na kutufanyia kazi husika, niliwaeleza kuwa mimi nataka kuwa kiongozi mwenye nguvu ya ushawishi hapa Kenya.

Na kweli nadhubutu kusema ndivyo hasa ilivyokuja kuwa, ushawishi wangu ni mkubwa sana, ni kiongozi maarufu na anayependwa ndani ya jamii, asante AfricanDoctors kwa huduma yenu.

Wasiliana na AfricanDoctors kwa namba +254719153099.

Mwisho.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger