Tuesday, 31 January 2023

EWURA YARIDHISHWA KUWASA KUPELEKA MAJI YA ZAWADI YA USHINDI SHULE ZA SEKONDARI KAHAMA


Meneja wa EWURA Kanda ya Ziwa, George Mhina (kushoto) na wanafunzi wa shule ya Sekondari Kabela Gold wakifungua maji kupitia mradi wa maji uliotekelezwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Kahama (KUWASA) kwa ufadhili wa EWURA.

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imeridhishwa na utekelezaji wa mradi wa kusogeza maji safi katika shule za Sekondari Kabela Gold, Mwime, Bugisha na Kituo cha watoto wenye mahitaji maalum cha Mama Kalembe uliotekelezwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Kahama (KUWASA).

Akizungumza leo Jumanne Januari 31,2023 wakati akikagua na kuona utekelezaji wa mradi huo wa maji, Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Ziwa George Mhina amesema EWURA inaipongeza na kuishukuru KUWASA kupeleka huduma ya maji safi katika shule hizo.

Mhina amesema Mradi huo unatokana na KUWASA kuwa Mamlaka ya Pili Kitaifa kwa ngazi ya Mamlaka za Maji Safi na Usafi wa mazingira za mikoa kwa kutoa huduma bora ya maji safi mwaka 2022 ambapo EWURA iliipongeza na kuipatia KUWASA zawadi ya shilingi Milioni 15 kwa lengo la kurudisha zawadi hiyo kwa jamii kwa kuwapatia huduma ya maji safi.


“EWURA tumekuja kuthibitisha kama kweli KUWASA wamepeleka maji kwenye maeneo tuliyokubaliana na kama kweli huduma ya maji inapatikana. Mradi huu unaotokana fedha za ufadhili wa EWURA ni matokeo ya ushindi wa KUWASA kushika nafasi ya pili kitaifa kwa kutoa huduma bora ya maji safi. Tukakubaliana zawadi hii irudishwe kwa jamii, maji yapelekwe katika shule tatu na kituo kimoja cha watoto wenye mahitaji maalum katika Manispaa ya Kahama”,ameeleza Mhina.


Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira wa KUWASA, Mhandisi Magige Marwa amesema utekelezaji wa mradi huo ulianza Juni 2022 na kukamilika Septemba 2022 na unaendelea kutoa huduma huku wanufaika wakiwa zaidi ya 2000.

"EWURA ilitupa zawadi ya shilingi Milioni 15 ambapo nasi EWURA tuliongeza shilingi Milioni 5.3 kwa ajili ya kusogeza huduma ya maji safi kwenye shule hizo tatu na kituo cha watoto wenye mahitaji maalum. Tunashukuru tumekamilisha mradi na huduma ya maji inaendelea kutolewa. Tunaomba walinde miundombinu hii ya jamii", amesema Mhandisi Marwa.

“Tayari wanafunzi, walimu wameanza kupata huduma ya maji safi na salama. KUWASA inatoa wito kwa wananchi ambako mabomba ya maji yamepita waombe huduma ya maji ili kuondokana na adha ya kufuata maji umbali mrefu”, ameongeza Mhandisi Marwa.


Mkuu wa Shule ya Sekondari Bugisha, Musa Mpena na Mwalimu Mshauri Nasaha na Miradi shule ya Sekondari Kabela Gold Bi. Magreth Sikujua wameishukuru EWURA na KUWASA kwa kuwasogezea huduma ya maji safi ambayo wanayatumia kwa shughuli mbalimbali ikiwemo, kunywa,umwagiliaji miti na usafi shuleni.

Nao baadhi ya wanafunzi wa shule hizo, Abubakar Sadick, Rebeca Gwanchele, Fatuma Nyakalugu na Japhet Mwinula wamesema sasa wameondokana na adha ya kutumia muda mrefu kutafuta maji ambayo wala hayakuwa salama, mahudhurio ya wanafunzi darasani yameongeza na wameboresha usafi wa mwili na mazingira shuleni.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Kabela Gold wakifungua maji. Kushoto ni Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Ziwa  George Mhina. 
Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Ziwa George Mhina akielezea kuhusu mradi wa maji uliotekelezwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Kahama (KUWASA) kwa ufadhili wa EWURA
Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Ziwa George Mhina akielezea kuhusu mradi wa maji uliotekelezwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Kahama (KUWASA) kwa ufadhili wa EWURA
Mkurugenzi wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira wa KUWASA, Mhandisi Magige Marwa akielezea kuhusu mradi wa maji uliotekelezwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Kahama (KUWASA) kwa ufadhili wa EWURA
Mkurugenzi wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira wa KUWASA, Mhandisi Magige Marwa akielezea kuhusu mradi wa maji uliotekelezwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Kahama (KUWASA) kwa ufadhili wa EWURA
Mwalimu Mshauri Nasaha na Miradi shule ya Sekondari Kabela Gold Bi. Magreth Sikujua akiishukuru EWURA na KUWASA kwa  kupeleka huduma ya maji safi katika shule ya Sekondari Kabela Gold.
Mwanafunzi wa kidato cha nne , Abubakar Sadick akiishukuru EWURA na KUWASA kwa  kupeleka huduma ya maji safi katika shule ya Sekondari Kabela Gold.
Mwanafunzi wa kidato cha nne , Rebeca Gwanchele akiishukuru EWURA na KUWASA kwa  kupeleka huduma ya maji safi katika shule ya Sekondari Kabela Gold.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Bugisha katika Manispaa ya Kahama wakifungua maji kupitia mradi wa maji uliotekelezwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Kahama (KUWASA) kwa ufadhili wa EWURA.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Bugisha katika Manispaa ya Kahama wakifungua maji kupitia mradi wa maji uliotekelezwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Kahama (KUWASA) kwa ufadhili wa EWURA.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Bugisha katika Manispaa ya Kahama wakifungua maji kupitia mradi wa maji uliotekelezwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Kahama (KUWASA) kwa ufadhili wa EWURA.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Bugisha, Musa Mpena akiishukuru EWURA na KUWASA kupeleka huduma ya maji katika shule hiyo.
Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Ziwa George Mhina akizungumza katika shule ya Sekondari Bugisha katika Manispaa ya Kahama.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


 
Share:

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI YANG'ARA WIKI YA SHERIA DODOMA


Waziri wa Katiba na Sheria, Mh Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) akipokea machqpisho mbalimbali kutoka kwa Afisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Rehema Nyagawa wakati alipotembelea banda la Tume Leo Januari 26,2023 katika maonesho ya wiki ya sheria kitaifa inayoendelea katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.
Waziri wa Katiba na Sheria, Mh Dkt.Damas Ndumbaro (Mb) akipokea machqpisho mbalimbali kutoka kwa Afisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, akipatiwa eklimu ya mpiga kura wakati alipotembelea banda la Tume Leo Januari 26,2023 katika maonesho ya wiki ya sheria kitaifa inayoendelea katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma
Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Prof. Elisante Ole Gabriel akizungumza jambo leo Januari 23,2023 wakati alipotembelea banda la Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika maonesho ya wiki ya sheria kitaifa inayoendelea katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.
Jaji Mfawadhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Baraza la Ushindani Mhe. Salma Mussa Maghimbi tarehe 27 January, 2023 ametembelea Banda la Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwenye Maonesho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea kwenye viwanja vya Nyerere Square jijini Dodom.
Jaji Mfawadhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Baraza la Ushindani Mhe. Salma Mussa Maghimbi tarehe 27 January, 2023 ametembelea Banda la Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwenye Maonesho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea kwenye viwanja vya Nyerere Square jijini Dodom.
Jaji Mfawadhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Baraza la Ushindani Mhe. Salma Mussa Maghimbi akipatiwa machapisho mbalimbali ya Tume.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mh.Rosemary Staki Senyamule akipokea machapisho mbalimbali ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kutoka kwa Afisa Mwandamizi wa Tume, Titus Mwanzalila (kushoto) wakati kiongozi huyo alipotembelea Banda la Tume, Januari 26,2023 katika maonesho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Sylvester Anthony Mwakitalu ametembelea banda la Tume ya Taifa ya Uchaguzi na kupatiwa Elimu ya Mpiga Kura katika Maonesho ya Wiki ya Sheria Januari 25,2023. Maonesho ya Wiki ya Sheria yanaendelea katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Sylvester Anthony Mwakitalu ametembelea banda la Tume ya Taifa ya Uchaguzi na kupatiwa Elimu ya Mpiga Kura katika Maonesho ya Wiki ya Sheria, Januari 25,2023. Maonesho ya Wiki ya Sheria yanaendelea katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Viziwi Tanzania Makao Makuu Dodoma Mchungaji Frank Sarungi tarehe 27 Januari 2023, ametembelea Banda la Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwenye Maonesho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea katika Viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma.

Afisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bi. Rehema Nyagawa akizungumza Katibu wa Wanawake Chama cha Viziwi Tanzania Mkoa wa Dodoma Bi Amina Issah wakati alipotembelea banda la Tume kwenye maonesho ya Wiki ya Sheria Tanzania yanayoendelea katika viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma.
Watu wenye ulemavu wafurahishwa na kuwepo kwa wakalimani wa lugha ya alama inayotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwenye Banda la maonesho la Tume katika maoneolsho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpigakura, Bi. Giviness Aswile alipotembelea banda la Tume

Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Emmanuel Kawishe akizungumza na wadau alipotembelea banda la Tume

Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Leonard Tumua akiwa katika banda la Tume
Mkaguzi Mkuu wa ndani wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Amos Akim akiwa katika Banda la Tume.

Share:

KATAMBI:SERIKALI IMEANZA KUFANYIA KAZI MABORESHO YA MISHAHARA VYUO VIKUU

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi,akijibu maswali ya nyongeza bungen leo Januari 31,2023 jijini Dodoma yaliyoulizwa na Mbunge wa Viti maalum, Mhe. Dkt.Thea Ntara.

..................................

Na Mwandishi Wetu, Dodoma SERIKALI imeanza kufanyia kazi suala la maboresho ya mishahara kwenye vyuo vikuu kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi, ameyasema hayo leo bungeni alipokuwa akijibu maswali ya nyongeza Mbunge wa Viti maalum, Mhe. Dkt.Thea Ntara ambaye ameuliza mchakato wa mkataba namba 189 umefikia wapi ili kuboresha mishahara ya wafanyakazi wa majumbani na pia amehoji kuboresha mishahara kwa wakuu wa vyuo vikuu.

Akijibu maswali hayo, Mhe.Katambi amesema suala hilo la maboresho la mishahara linaangalia viwango kulingana na hali ya kiuchumi na uhalisia wa kidunia wa sasa. Aidha, amesema Serikali ilishaanza kuufanyia kazi mkataba wa kimataifa namba 189 ikiwa ni maelekezo ya Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Amesema mkataba huo kuna vipengele bado vinaendelea kufanyiwa kazi ambavyo vipo vinavyoendana na hali ya uchumi na uhalisia wa kimazingira na kitamaduni.

“Serikali inaendelea kuzichukua hizo hatua zote kwa haraka na naimani katika kipindi cha mwaka huu wa fedha hayo yote tutakuwa tumeweza kuyaangalia hasa kuhusu haki na stahiki za mikataba ya wafanyakazi wa ndani,”amesema.

Mhe.Katambi amesema serikali kupitia Kamishna wa Kazi inaangalia ili kuona namna ya kutengeneza viwango vinavyoendana na nchi za kuangalia maslahi kwenye kundi hilo. Awali, katika swali la msingi, Mbunge huyo amehoji lini Serikali itatangaza kima cha chini cha mshahara kwa Wafanyakazi wa serikali na mashirika binafsi.

Mhe.Katambi akijibu swali hilo, amesema kima cha chini cha mshahara kwa sekta ya umma kilitangazwa Mei 13, 2022 na utekelezaji wake umeanza Julai mosi mwaka 2022 na kwa sekta binafsi kima hicho kilitangazwa Novemba 25, 2022 baada ya Bodi ya Kima cha Chini cha Mishahara kukamilisha utafiti na kutoa mapendekezo ya viwango kwa sekta hiyo ambayo yaliridhiwa na Baraza la Ushauri kuhusu Kazi, Uchumi na Jamii (LESCO) na utekelezaji wake ulianza rasmi Januari mosi, 2023.
Share:

ENEO LA KITARAKA KUTUMIKA KIMKAKATI KUZALISHA MIFUGO KIBIASHARA


*****************************

Na Mbaraka Kambona, Singida

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega (Mb) amesema kuwa Serikali imedhamiria kulitumia eneo la kupumzishia mifugo la Kitaraka lililopo wilayani Manyoni, Singida liweze kutumiwa na vijana watakao hitimu mafunzo katika vituo atamizi kwa ajili ya kufanya shughuli za uzalishaji wa mifugo kibiashara ili kukuza uchumi wao na Taifa kwa ujumla.

Mhe. Ulega alibainisha hayo wakati wa kikao baina yake na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe. Peter Serukamba (kushoto) alipokutana nae katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, mkoani Singida Januari 30, 2023.

Wakati wa mazungumzo yao, Mhe. Ulega alimueleza Mkuu wa Mkoa huyo kuwa lengo la ziara yake ni kujadiliana nae kuhusu dhamira ya Serikali ya kutaka kulitumia eneo la kitaraka kwa ajili ya kufanya shughuli za uzalishaji wa mifugo ili kuwawezesha vijana kujipatia ajira lakini pia kuzalisha malighafi ya uhakika kwa ajili ya viwanda vya nyama na kuifanya sekta ya mifugo kuchangia ipasavyo katika pato la taifa na la mtu mmoja mmoja.

Alisema kuwa kupitia programu ya vituo atamizi iliyoanzishwa na serikali kwa ajili ya kuwafundisha vijana ufugaji wa kisasa, Serikali imetenga jumla ya Shilingi Bilioni 19 kwa ajili ya kuwawezesha vijana kufuga kibiashara kwa ajili ya kuuza ndani na nje ya nchi.

“Progaramu hii ya vituo atamizi ni ya miaka 3(2022/23-2024/25) na hizi bilioni 19 zinatolewa na wadau mbalimbali ambapo serikali inatoa bilioni 6.3, na bilioni 12.6 zitachangiwa na wadau wengine kutoka sekta binafsi”,alisema Ulega

Aliongeza kwa kusema kuwa mpango huo wa kutumia eneo la Kitaraka unatarajiwa kuzalisha robota 500,000 za malisho ya mifugo na kunenepesha ng’ombe 8000 kwa wakati mmoja.

Aidha, alifafanua kuwa eneo hilo la Kitaraka limekaa kimkakati kwa ajili ya unenepeshaji wa mifugo kwasababu ndani ya eneo hilo kuna kituo cha treni ya mwendokasi (SGR) hivyo itarahisisha usafirishaji wa malighafi kutoka hapo kwenda maeneo mengine ya soko. Aidha, Naibu Waziri alimuomba Mkuu wa Mkoa, uongozi wa halmashauri, na wananchi wa Singida kwa ujumla kuhakikisha wanatoa ushirikiano wa dhati katika kufanikisha adhma ya serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kukuza ajira kwa vijana kupitia sekta ya mifugo.

“Serikali ya Mhe Rais, Dkt. Samia imejielekeza ipasavyo ktk kutumia fursa za sekta za Mifugo,uvuvi na kilimo katika kuajiri Vijana na kuongeza uzalishaji nchini hivyo naomba mtoe ushirikiano wa kutosha ili adhma hii iweze kutimia kama ilivyokusudiwa”, alifafanua Mhe. Ulega
Share:

MFANYABIASHARA AFARIKI AKIMUNG'UNYA URODA NA MREMBO GESTI


Mfanyabiashara mwenye umri wa miaka 25, amepatikana amefariki dunia katika chumba cha hoteli alichokuwa amekodisha kumumunya urojo na mpenziwe.

Ali Musstafa anaripotiwa kuanguka na kukata roho katika Hoteli ya Avenue Lodge mjini Arua, Uganda kutokana na kushindwa kupumua alikokuwa akirusha roho na mpenzi wake.

 “Mwathiriwa alianguka na kufia chumbani. Mpenziwe alienda na kuwajulisha wasimamizi wa hoteli ambao mara moja walitoa taarifa kwa polisi wa Arua. Eneo la tukio lilikaguliwa na kuhifadhiwa vizuri," ilisoma ripoti ya polisi.

Polisi katika Wilaya ya Arua eneo la Nile Magharibi walisema hawakupata dalili zozote za sumu, dawa za kulevya au athari zingine za mwili kutoka eneo la tukio.

"Hakuna chembechembe za matumizi mabaya ya dawa za kulevya, sumu au athari zingine za mwili zilizopatikana katika eneo la tukio.

 Mwili huo ulipelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Arua na kuchunguzwa,” msemaji wa polisi, SCP Fred Enanga alisema Jumatatu, kama alivyonukuliwa na Daily Monitor.

Enanga anaamini kuwa mfanyabiashara huyo kutoka OZU, wadi ya Kenya katika Wilaya ya Arua alifariki dunia mwendo wa saa tatu usiku. 

Mwili wa marehemu baadaye ulichukuliwa kutoka chumba cha hoteli na kupelekwa kufanyiwa uchunguzi wa maiti.

 "Kifo wakati wa kujamiana kinaweza kutokea kwa sababu kadhaa, ambazo ni pamoja na mkazo wa mwili kutokana na shughuli hiyo au kwa sababu ya hali isiyo ya kawaida ," aliongeza.
Share:

MTOTO WANGU ALIVYOTOWEKA KWA NJIA ZA KISHIRIKINA



Jina langu ni Mama Samweli kutokea nchini Kenya, miaka kama mitatu iliyopita nilipitia changamoto kubwa sana kifamilia, hii ni baada ya mtoto wangu mmoja kupotea katika mazingira ya kutatanisha.

Ilikuwa ni jioni ya kawaida akiwa anacheza eneo la karibu ya nyumba yetu pamoja na watoto wa majirani zangu, huu ulikuwa ni utamaduni wao wa siku zote kukutanika katika eneo hilo na kucheza.

Hata hivyo, ilipofikia muda wa kurudi nyumbani sikuweza kumuona, ndipo nikajaribu kupaza sauti na kuita lakini hakuweza kuitika, nilianza kupita nyumba za majirani kuuliza kama yupo huko lakini sikumona.

Watoto waliokuwa wanacheza naye, tulipowauliza walisema kuwa tulipomaliza kusema walimuona akirejea nyumbani kama ilivyo kawaida, daima siwezi kusahau siku hiyo jinsi ambavyo nilichanganyikiwa.

Basi tulienda kuripoti kisa hicho Polisi na wao mara moja wakaanza kumsaka alipo, nilikuwa na matumaini kuwa Polisi wanaweza kusaidia kupatikana kwa mwanangu maana wao ni wajuzi wa kazi hiyo.

Hata hivyo, haikuwa hivyo, siku zilienda hadi mwezi kumalizika, hapo nikawa nasema kama mwanangu atapatikana, basi anaweza kupatikana akiwa amekufa. Mashaka yalikuwa ni makubwa sana kwangu.

Jirani yangu mmoja aliniambia kuwaAfricanDoctors wanaweza kusaidia kupatikana kwa mtoto wangu, basi nilichukua jukumu la kuwasiliana nao na kuwaeleza shida hiyo.

Siku chache baaada ya wao kunifanyia tiba yao, mtoto wangu alirejea mwenywe nyumbani akiwa mzima wa afya, tulipomuuliza ni wapi hasa katokea, alisema Bibi mmoja alimchukua na kwenda kuishi kwake lakini hasa hamkumbuki na hakumbuki kwake.

Hapo ndipo nikaelewa kuwa mtoto wangu alichukuliwa kwa njia za kushirikina, na kama sio AfricanDoctors basi ingekuwa ni ngumu kwa Polisi kuja kuweza kumpata.

Wasiliana na AfricanDoctors kwa namba +254719153099.

Share:

Monday, 30 January 2023

WAWILI BABATI WAHUKUMIWA MIAKA 20 JELA KWA UHUJUMU UCHUMI



Na John Walter-Babati

Watu wawili wakazi wa Kijiji Endagile kata ya Mamire wilaya ya Babati mkoani Manyara, John Lulu na Zebedayo Safari, wamehukumiwa kifungo Cha miaka 20 jela kwa kosa la kukutwa na meno mawili ya tembo.


Hukumu hiyo imetolewa leo Jumatatu Januari 30,2023 na Mheshimiwa Hakimu Victor Kimario katika mahakama ya wilaya ya Babati baada ya ushahidi ulitolewa na Mashahidi nane Mahakamani hapo kuthibitisha pasi na shaka.


Imeelezwa Mahakamani hapo kuwa Meno hayo yanayodaiwa kuwa ni sawa na idadi ya tembo mmoja aliyeuwawa ambaye thamani yake ni shilingi milioni 35.1, walikutwa nayo walipokamatwa na askari wa wanyamapori katika kijiji cha Bulkeri 23,10,2022 wakiwa kwenye pikipiki.


Upande wa waendesha mashtaka wa Jamhuri Rusticus Mahundi na Abood Komanya waliieleza Mahakama kwamba kwa kuwa watu hao walimuua Mnyama tembo ambaye ni kivutio kikubwa kwa watalii kuja nchini na Mheshimiwa Rais wa Dr. Samia Suhulu Hassan alifanya jitihada kuutangaza utalii kwa Filamu ya royal Tour na pamoja na kuwa hawana rekodi zozote za nyuma za watuhumiwa hao, aliiomba mahakama iwapatie adhabu Kali ili iwe fundisho kwa wengine.


Katika utetezi wake Mshtakiwa wa kwanza John Lulu aliiomba mahakama impunguzie adhabu kwani ana Watoto wawili wanaosoma Sekondari, dada yake mlemavu,mama yake mzee wote wanamtegemea.


Mshtakiwa wa pili Zebedayo Safari aliiomba mahakama impunguzie adhabu kwa kuwa kwenye familia yeye ndo tegemezi.
Share:

UWT SHINYANGA WAADHIMISHA MIAKA 46 YA CCM, WAKEMEA UKATILI DHIDI YA WATOTO

Mjumbe wa Baraza Kuu kutoka UWT Taifa Helen Bugoye akizungumza kwenye maadhimisho ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi CCM.

Na Sumai Salum, KISHAPU

UMOJA wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi CCM (UWT) Mkoa wa Shinyanga, umeadhimisha miaka 46 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi CCM, huku wakilaani kuendelea kwa matukio ya ukatili dhidi ya watoto ikiwamo ubakaji na ulawiti.

Maadhimisho hayo yamefanyika leo Januari 30, 2023 katika viwanja vya Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi CCM wilayani Kishapu.

Akizungumza mgeni Rasmi kwenye maadhimisho hayo, Mjumbe wa Baraza Kuu kutoka UWT Taifa Heleni Bugoye, amelaani matukio ya ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto wadogo, huku akiwataka wazazi kujenga tabia ya kulinda usalama wa watoto wao ili wasifanyiwe vitendo vya ukatili wa kijinsia.

“Wazazi tujenge tabia ya kuwasikiliza watoto wetu, pamoja na kuwaogesha wale wenye umri mdogo ili kuwakagua kuona kama hua wanafanyiwa vitendo vya ubakaji, ukimshika sehemu za siri na kuona anarudi nyuma tambua kuna shida,”amesema Bugoye.

Naye Mwenyekiti wa UWT wilayani Kishapu Rahel Madundo amewataka wazazi wawapeleke shule watoto wao, ili wasome na kutimiza ndoto zao na kuja kuwa tegemeo la familia na taifa, na wasipofanya hivyo ni kuwafanyia ukatili, na Serikali haitasika kuwachukulia hatua.

Aidha, katika sherehe hizo za miaka 46 ya kuzaliwa kwa CCM, Umoja huo wa wanawake UWT, pia umeadhimisha kwa kupanda Miti katika Hospitali ya Jakaya Kikwete wilayani Kishapu, pamoja na kutoa zawadi kwa wagonjwa katika Hospitali hiyo zikiwamo sabuni za kufulia, biskuti na Juice.

Nao Baadhi ya Wagonjwa akiwamo Zaituni Rashid amewashukuru wanawake hao wa UWT kwa kuwapatia msaada zawadi hizo, huku wakipongeza huduma za matibabu ambazo wanapewa katika Hospitali hiyo.


Naye Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Jakaya Kikwete wilayani Kishapu Dk. Mohamed Mkumbwa, amempongeza Rais Samia kwa kuendelea kutoa fedha na kuboresha huduma za matibabu katika Hospitali hiyo.
Maadhimisho ya miaka 46 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi CCM yakiendelea.


Share:

UWT SHINYANGA WAADHIMISHA MIAKA 46 YA CCM KISHAPU, WAWAJULIA HALI VIJANA WALIOSHAMBULIWA NA FISI



Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Taifa, Helen Bugoye (kulia) akimjulia hali mmoja wa wakazi wa Kishapu waliojeruhiwa kwa kushambuliwa na fisi ambapo sasa wanaendelea kupata matibabu katika Hospitali ya  Jakaya Mrisho Kikwete ya Wilaya ya Kishapu. UWT Mkoa wa Shinyanga wametembelea hospitali hiyo na kutoa zawadi mbalimbali kwa wagonjwa ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Miaka 46 ya kuzaliwa kwa CCM
Na Halima Khoya - Shinyanga

Jumuiya ya Umoja wa Umoja wa Wanawake Mkoa wa Shinyanga imeadhimisha miaka 46 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Kishapu kwa kupanda miti, kutembelea na kuwapa zawadi wagonjwa waliolazwa katika Hospitali ya  Jakaya Mrisho Kikwete ya Wilaya ya Kishapu.

UWT wakiongozwa na Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Taifa, Helen Bugoye
pia wamewajulia hali watu wanne wa familia moja wakazi wa Kijiji cha Mwalata Mkoani Shinyanga waliojeruhiwa kwa kushambuliwa na fisi sehemu mbalimbali za miili yao.


Tukio hilo la kushambuliwa na fisi limetokea Januari 30,2023 majira ya saa 7 usiku katika kijiji cha Mwalata Kata ya Ndololeji Halmashauri ya wilaya Kishapu Mkoani humo.


Akieleza juu ya tukio hilo, mama mzazi wa majeruhi wawili (Jishansa Kija mwenye miaka 18 na Lazaro Emmanuel anayesoma darasa la 5), Bi. Mbuko Jishanga amesema kuwa majira ya saa saba usiku alisikia kelele nje ya nyumba yake ndipo alipotoka na kumkuta mwanae Jishansa akiwa amejeruhiwa usoni pamoja na Emmanuel akiwa amejeruhiwa kichwani.


Jishanga amesema kuwa mara baada ya kukuta hali hiyo alimuagiza panga Mkwilima wake Malambi Mayara,ambaye baada ya kumjeruhi fisi huyo kichwani alimrukia kijana huyo ambapo aling'ata shingoni na kufanikiwa kumuua akiwa ameng'ang'ania kwenye mwili wa Mkwilima huyo.


"Majira ya saa 7 usiku nilisikia kelele nje,nilipotoka niliwakuta wanangu wakiwa wamejeruhiwa na fisi ikabidi nimuagize mtoto panga nikawa namvizia  fisi huyo atoke nje na alipotoka tu alikutana na panga la kichwa akaanguka,alipoamka tena nikamkata mara ya pili huku nikiwa napiga kelele,watu walijaa wakanisaidia kumuua vizuri pamoja na kuwaleta watoto hospitali", amesema Jishanga.


Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Wilaya Kishapu,Dr Mohamed Mkumbwa, amesema majira ya saa 10 alfajiri tarehe 30,2023 amepokea wanaume 4 wakiwa wamejeruhiwa maeneo mbalimbali ya miili yao ambao walipatiwa huduma za kimatibabu na kufikia sasa hivi hali zao ni nzuri.


Akizungumza baada ya kutembelea Hospitali ya  Jakaya Mrisho Kikwete ya Wilaya ya Kishapu, Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Taifa, Helen Bugoye ameeleza kusikitishwa na tukio hilo huku akiwataka wakazi wa Kishapu kushirikiana na Mamlaka zinazohusika kudhibiti wanyama wakali kuwawinda  wanyama hao.

"Wanawake tunaweza,kwani mzazi mwenzetu amewapambania watoto wake ambao walikuwa wamevamiwa na fisi, inatakiwa mamlaka ya maliasili wafike kwenye kijiji hiki ili kuwawinda wanyama hatarishi", amesema Bugoye.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger