Sunday, 29 January 2023

MAKONGONGORO NYERERE AZINDUA ZOEZI LA UPANDAJI MITI MANYARA

Na John Walter-Manyara
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Makongoro Nyerere amezindua zoezi la upandaji miti mkoani hapa huku akiagiza kila Mwananchi kuhakikisha anapanda mti na kuutunza katika eneo lake.

Amewataka wakuu wa wilaya, wakurugenzi pamoja na wakuu wa idara za mazingira kila mmoja kuhakikisha miti inapandwa kama muongozo unavyoelekeza.


Nyerere ameyasema hayo leo Januari 27,2023 wakati akizindua zoezi la upandaji wa miti katika kitongoji cha Sumbi, kijiji cha Nakwa kata ya Bagara Halmashauri ya mji wa Babati.

Mkuu wa mkoa amesema kuwa mkoa huo utaendelea kusimamia vyema Jitihada za Serikali katika kutunza mazingira na kuweka msisitizo wa uhifadhi wa mazingira kwa wnanchi wote ili kuendelea kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.


Pia ameeleza kuwa Serikali mkoani humo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeendelea kuhamasisha upandaji miti kwa kupanda katika maeneo ya ofisi za Umma kama shule, hospitali, vituo vya afya na zahanati.


Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais na Ofisi ya Rais, TAMISEMI imeendelea kuratibu utekelezaji wa kampeni ya kitaifa ya upandaji na utunzaji wa miti inayotekelezwa nchini ambapo kila Halmashauri inapaswa kupanda miti milioni 1.5 kila mwaka.


Kauli mbiu ya mwaka huu inasema 'Mazingira yetu, Tanzania Yetu, Nitaipenda daima" kauli hiyo inatabananisha kuwa uzuri wa nchi ni sambamba na kupanda miti na kutunza mazingira kwa ujumla.
Share:

KIKWETE AIPONGEZA WIZARA YA UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO KWA KUKUZA SANAA.


Na John Mapepele

Rais mstaafu wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho ameipongeza Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo kutokana kufanya vizuri kwenye Sanaa ya Muziki na Sanaa ya Filamu hapa nchini.

Mhe. Kikwete amesema haya wakati akitoa hotuba yake usiku wa kuamkia leo Januari 29, 2023 kwenye ukumbi wa Mlimani City kwenye uzinduzi wa album ya the Kid you know ya msanii maarufu nchini Mario.

Amefafanua kuwa ili Sanaa iweze kukua hapa nchini inategemea mahitaji ya Serikali ambapo ametoa wito kwa Serikali kuendelea kulea sanaa

Amepongeza Wizara kwa kufanikisha kuwa na mdundo ambao utalitambulisha Taifa la Tanzania duniani.

Pia amepongeza kwa Serikali kuanzisha Mfuko wa Utamaduni na Sanaa na kuanza kutoa mikopo isiyo na riba na kuomba kuwa na mkakati madhubuti ambao utasaidia sanaa kwenye kwenye ngazi za kimataifa.

Tukio hili limehudhuriwa na mamia ya wapenzi wa muziki huku wasanii mbalimbali wa nyimbo za kizazi kipya wakimsindikiza Marioo katika uzinduzi wa album hiyo.

Pia Katibu Mkuu wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi na viongozi wengine pamoja na wadau mbalimbali wa muziki wamejitokeza
Share:

Saturday, 28 January 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JANUARI 29,2023















Share:

Friday, 27 January 2023

PERFOMANCE WOMAN, THEATRE ARTS FEMINISTS WAKUTANA NA WAZAZI NA WANAFUNZI SHULE YA MSINGI KILIMANI...WABAINI WATOTO KUCHOMWA MOTO


Wanaharakati wa kutetea haki za wanawake na watoto kutoka Shirika lisilo la Kiserikali Perfomance Woman kwa kushirikiana na Shirika la Theatre Arts Feminists wametoa elimu ya ukatili wa kijinsia kwa wazazi na wanafunzi wa shule ya msingi Kilimani jijini Dar es salaam.


Wanaharakati hao (Mkurugenzi wa Shirika la Theatre Arts Feminists, Aluwa Mkilindi na Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali Perfomance Woman, Rose Mwasubila) wamesema mara baada ya kuzungumza na wanafunzi na wazazi wamebaini kuwepo kwa vitendo vya unyanyasaji wa watoto kuchomwa moto na walezi wao ambapo mmoja amechomwa moto na mama mzazi huku mwingine akichomwa na mke wa shangazi yake.


Wamesema vitendo hivyo vinasababishwa watoto kukosa ujasiri wa kuelezea changamoto za ukatili kutokana na kukosa urafiki na walezi wao au watu wao wa karibu.


“Tumetoa elimu kwa wanafunzi 600 ambapo wasichana ni 298 na wavulana ni 302 lakini pia tumetoa elimu kwa wazazi 45, tumewafundisha namna nzuri ya kuwalea watoto na kuwa marafiki zao ili iwe rahisi kubaini ukatili wanaofanyiwa pamoja na kuwafundisha wazazi namna na mbinu za kuwaadhibu watoto badala ya kuwaunguza na moto”,wamesema.
Mkurugenzi wa Shirika la Theatre Arts Feminists, Aluwa Mkilindi akitoa elimu ya kukomesha ukatili wa kijinsia
Mkurugenzi wa Shirika la Theatre Arts Feminists, Aluwa Mkilindi akitoa elimu ya kukomesha ukatili wa kijinsia
Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali Perfomance Woman, Rose Mwasubila akitoa elimu ya kukomesha ukatili wa kijinsia
Mkurugenzi wa Shirika la Theatre Arts Feminists, Aluwa Mkilindi akitoa elimu ya kukomesha ukatili wa kijinsia
Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali Perfomance Woman, Rose Mwasubila akitoa elimu ya kukomesha ukatili wa kijinsia
Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali Perfomance Woman, Rose Mwasubila akitoa elimu ya kukomesha ukatili wa kijinsia
Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali Perfomance Woman, Rose Mwasubila akitoa elimu ya kukomesha ukatili wa kijinsia
Mkurugenzi wa Shirika la Theatre Arts Feminists, Aluwa Mkilindi akitoa elimu ya kukomesha ukatili wa kijinsia
Mkurugenzi wa Shirika la Theatre Arts Feminists, Aluwa Mkilindi akitoa elimu ya kukomesha ukatili wa kijinsia
Mkurugenzi wa Shirika la Theatre Arts Feminists, Aluwa Mkilindi akitoa elimu ya kukomesha ukatili wa kijinsia
Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali Perfomance Woman, Rose Mwasubila akitoa elimu ya kukomesha ukatili wa kijinsia
Mkurugenzi wa Shirika la Theatre Arts Feminists, Aluwa Mkilindi akitoa elimu ya kukomesha ukatili wa kijinsia
Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali Perfomance Woman, Rose Mwasubila akitoa elimu ya kukomesha ukatili wa kijinsia
Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali Perfomance Woman, Rose Mwasubila akitoa elimu ya kukomesha ukatili wa kijinsia
Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali Perfomance Woman, Rose Mwasubila akitoa elimu ya kukomesha ukatili wa kijinsia
Share:

REA NA WADAU WAKUBALIANA KUUNGANISHA NGUVU USIMAMIZI MIRADI YA UMEME VIJIJINI


Mjumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Oswald Urassa akizungumza wakati wa kikao cha Wadau wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mkoa wa Lindi, kilichoketi kujadili namna bora ya utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini mkoani humo, Januri 27, 2023 katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa. Kushoto kwake ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Lindi ambaye ni Katibu Tawala wa Mkoa huo, Ngusa Samike pamoja na wa kwanza kulia ni Mbunge wa Kilwa Kusini, Ally Kasinge.

Mjumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Oswald Urassa akizungumza wakati wa kikao cha Wadau wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mkoa wa Lindi, kilichoketi kujadili namna bora ya utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini mkoani humo, Januri 27, 2023 katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.


Mjumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Oswald Urassa akizungumza wakati wa kikao cha Wadau wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mkoa wa Lindi, kilichoketi Januri 27, 2023 katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kujadili namna bora ya utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini. Wengine pichani kutoka kushoto ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Thomas Mbaga, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Lindi ambaye ni Katibu Tawala Ngusa Samike na Mkuugenzi wa TANESCO Kanda ya Kusini Mhandisi Felician Makota.


Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Lindi ambaye ni Katibu Tawala Ngusa Samike akizungumza wakati wa kikao cha Wadau wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mkoa wa Lindi, kilichoketi Januri 27, 2023 kujadili namna bora ya utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini. Kushoto ni Mjumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini, Oswald Urassa na kulia ni Mbunge wa Kilwa Kusini, Ally Kasinge.


Mbunge wa Kilwa Kusini, Ally Kasinge akizungumza wakati wa kikao cha Wadau wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mkoa wa Lindi, kilichoketi Januri 27, 2023 kujadili namna bora ya utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini. Kushoto kwake ni Mkuugenzi wa TANESCO Kanda ya Kusini Mhandisi Felician Makota.


Mbunge wa Kilwa Kusini, Ally Kasinge akizungumza wakati wa kikao cha Wadau wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mkoa wa Lindi, kilichoketi Januri 27, 2023 kujadili namna bora ya utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini. Wengine pichani kutoka kushoto ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Thomas Mbaga, Mjumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini, Oswald Urassa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Lindi ambaye ni Katibu Tawala Ngusa Samike.


Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Thomas Mbaga akizungumza wakati wa kikao cha Wadau wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mkoa wa Lindi, kilichoketi Januri 27, 2023 katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kujadili namna bora ya utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini mkoani humo.


Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Mtama, Shaibu Mchinga akichangia maoni yake wakati wa kikao cha Wadau wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mkoa wa Lindi, kilichoketi Januri 27, 2023 katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kujadili namna bora ya utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini mkoani humo.


Wataalam kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Jensen Mahavile (wa kwanza kulia) na Mhandisi Daniel Mwandupe (wa pili-kulia) wakiwa katika kikao cha Wadau wa REA Mkoa wa Lindi, kilichoketi Januri 27, 2023 katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kujadili namna bora ya utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini mkoani humo.


Baadhi ya Makatibu wa Wabunge wa Mkoa wa Lindi (mstari wa mbele), wakiwa katika kikao cha Wadau wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mkoa wa Lindi, kilichoketi Januri 27, 2023 katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kujadili namna bora ya utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini mkoani humo.


Sehemu ya washiriki wakifuatilia mjadala katika kikao cha Wadau wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mkoa wa Lindi, kilichoketi Januri 27, 2023 katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kujadili namna bora ya utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini mkoani humo.

******************

Veronica Simba – Lindi

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Wadau wake mbalimbali mkoani Lindi, wamekubaliana kuunganisha nguvu katika kusimamia utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini ili kuhakikisha inakamilika kwa wakati na viwango vinavyotakiwa.

Azimio hilo limefikiwa leo Januari 27, 2023 katika kikao kazi kilichojumuisha Ujumbe kutoka REA ukiongozwa na mmoja wa Wajumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini, Oswald Urassa, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Lindi ambaye ni Katibu Tawala wa Mkoa huo Ngusa Samike, Ujumbe kutoka TANESCO, Wabunge wa Lindi pamoja na Wakandarasi wanaotekeleza miradi ya umeme vijijini mkoani humo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Urassa amesema kikao kimekubaliana kuwa kila Mkandarasi atatakiwa kuandaa na kuwasilisha Mpango Mkakati unaodadavua namna atakavyotekeleza kazi zake kwa mlengo wa kukamilisha Mradi kwa wakati.

Akifafanua, amesema Mpango Mkakati huo utaainisha taarifa ya kila wiki na kila mwezi kuanzia sasa hadi Aprili 30 mwaka huu ambayo ndiyo siku ya hitimisho kwa kila mmoja kuwa amekamilisha na kukabidhi Mradi.

Amesema Bodi ya REA itahakikisha inafuatilia kwa ukaribu na hatua kwa hatua, utekelezaji wa Mradi kwa kila Mkandarasi ili malengo ya Serikali kuwekeza fedha nyingi kwa ajili ya kuwapelekea huduma ya umeme wananchi waishio vijijini itimie.

“Fedha hizi ni za wananchi hivyo ni lazima zitumike kama inavyopaswa. Hivyo, ni jukumu lenu ninyi Wakandarasi kuhakikisha mnatimiza makubaliano yetu tuliyoazimia leo ya kukamilisha miradi kwa wakati," amesisitiza Mjumbe huyo wa Bodi.

Akizungumza katika kikao hicho, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Thomas Mbaga amewaasa Wakandarasi kuheshimu Mikataba yao ya kazi na kutenda kadri inavyoelekeza ili kuepuka changamoto mbalimbali.

Aidha, amesema kuwa katika kuhakikisha Miradi inatekelezwa na kukamilishwa kwa wakati, REA imemwongezea nguvu kazi Mshauri Mwelekezi kwa kuongeza idadi ya wasimamizi wa miradi kutoka 10 hadi 20.

Vilevile amesema REA imejipanga kuhakikisha kwamba kila Mkoa unakuwa na usimamizi thabiti wa miradi na kwamba itaendelea kushirikiana na TANESCO katika kutekeleza kazi hiyo.

Mhandisi Mbaga amesema Mpango Kazi utakaowasilishwa na Wakadarasi sasa utatumika kama ‘Msahafu’ kwa wote ikiwemo REA, TANESCO na wadau wengine hivyo ndiyo utakaotumika kwa wakandarasi wenyewe kujihukumu kutokana na kazi itakayofanyika.

“Tutawapima kulingana na huo Mpango Kazi ili kuhakikisha juhudi za Serikali katika kuwapelekea umeme wananchi wa vijijini zinazaa matunda,” amesisitiza.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa kikao hicho, Kaimu Mkuu wa Mkoa, Ngusa Samike amesema Serikali ina nia njema kuwatumia wakandarasi wazawa kwani miradi hiyo wangepewa wageni, asilimia kubwa ya fedha ingeenda nje ya nchi.

Ni kwa sababu hiyo, Kaimu Mkuu wa Mkoa amewataka wakandarasi walioaminiwa na Serikali kutoipoteza imani hiyo kwa kutekeleza kwa viwango na wakati miradi husika.

“Mliomba kazi, mkapewa kazi, fanyeni kazi kwa uaminifu. Ni wakati sasa wa kuidhihirishia Serikali kuwa imani iliyowapatia haipotei bure ili muendelee kuaminiwa,” amesisitiza.

Aidha, amesema Ofisi ya Mkuu wa Mkoa itafuatilia kikamilifu makubaliano ya kikao hicho ambacho kimepitisha azimio la kwamba baada ya mwezi mmoja kutoka siku ya kikao, utafanyika ufuatiliaji kuona kila mkandarasi anavyotekeleza maagizo ya kuongeza kasi ya kazi ambapo hatua itakayokuwa imefikiwa itatoa dira endapo Mradi utakamilika kwa wakati au la na kuchukua hatua stahiki.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, Meneja Mradi wa Kampuni ya White City International Contractors LTD, Mhandisi Jacqueline Mushi na Meneja Mradi wa Kampuni ya Nakuroi Investment Company Limited, Mhandisi William Madibu wameahidi kufanyia kazi makubaliano ya kikao hicho na kwamba watakamilisha miradi kwa wakati.

Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Mbunge wa Kilwa Kusini, Ally Kasinge pamoja na Makatibu wa Wabunge wa Mkoa wa Lindi ambao wote wamepongeza hatua ya REA kukutana na Wadau ili kuweka mikakati ya pamoja katika kusimamia utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini katika Mkoa wa Lindi.

Taarifa ya Msimamizi wa Miradi ya REA Mkoa wa Lindi, Mhandisi Daniel Mwandupe inaeleza kuwa mkoa huo una jumla ya vijiji 524 ambapo kati yake, vyenye umeme ni 326 na vilivyobaki 198 vitapatiwa umeme kupitia Mradi wa REA Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili kwa gharama ya shilingi bilioni 71.9

Kampuni mbili za Ukandarasi zinatekeleza Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu mkoani Lindi ambapo kampuni ya Nakuroi Investment inatekeleza katika Wilaya za Kilwa, Lindi Vijijini na Ruangwa huku kampuni ya White City ikitekeleza katika Wilaya za Liwale na Nachingwea.

Share:

KAMANDA WA POLISI ILALA ATUNUKIWA TUZO YA HESHIMA.....SASA NI DR. ACP DEBORA MAGILIGIMBA


The Academy Universal Global Peace yenye Chuo Kikuu Cha The American University Global Peace chenye matawi nchi 120 duniani ikiwemo Tanzania (www.augpusa.education) kinachoongozwa na Profesa Madhu Krishan kimetunuku Tuzo ya Heshima Kamanda wa Polisi Ilala ACP Debora Magiligimba.

Kufuatia Tuzo hiyo ya Heshima Kamanda wa Polisi Ilala ACP Debora Magiligimba, sasa ni Dr. ACP Debora Magiligimba.

Chuo hicho katika mwendelezo wa kuwachunguza watu waliogusa kazi za kijamii duniani kimemgundua Mfanyakazi wa Jeshi la Polisi Tanzania ACP Debora Magiligimba kuwa ni mwanamke Shujaa aliyefanya kazi nyingi za jamii.


Chuo hicho kimemfuatilia ACP Debora Magiligimba kupitia mitandao ya kijamii ikiwemo Youtube na njia zingine na kugundua kuwa amejikita sana kwenye shughuli za jamii hususani masuala ya kupinga ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto ambapo amekuwa akijitoa katika kuelimisha jamii kujiepusha na kukemea vitendo vya kikatili kupitia makongamano, mikutano ya wananchi, kutoa elimu kwenye nyumba za ibada,kutoa elimu kwa wake za askari na askari wenyewe, kutatua migogoro ya ndoa, kutoa elimu kwa njia ya Tv na Redio.

"Katika kumfuatilia tumebaini kuwa mikoa yote aliyowahi kufanya kazi vituo tofauti pamoja na majukumu mbalimbali. Kwa kazi nyingi alizofanya tumeona ni Mwanamke kiongozi wa tofauti anayestahili kutunukiwa Tuzo ya Heshima",amesema Profesa Madhu Krishan.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger