Thursday, 26 January 2023

WIZARA YA UWEKEZAJI VIWANDA NA BIASHARA, YATOA MAFUNZO YA KAIZEN KWA WAMILIKI WA VIWANDA NA WATUMISHI WA SERIKALI


Mafunzo ya uhamasishaji falsafa ya KAIZEN yakitolewa kwa Wamiliki wa Viwanda Wafanyakazi na Watumishi wa Serikali

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

WIZARA ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara imetoa mafunzo ya uhamasishaji wa falsafa ya kupunguza gharama za uzalishaji kwenye viwanda, na kuongeza ufanisi wa utendaji kazi kwenye Ofisi za Serikali (KAIZEN).

Mafunzo hayo ambayo ni ya siku moja yametolewa leo Januari 26, 2023 katika ukumbi wa Mikutano wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

Mkuu wa Kitendo cha KAIZEN kutoka Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Richard Pweleza, akisoma hotuba kwa niaba ya Mkurugenzi wa Idara ya Viwanda kwenye mafunzo hayo, amesema Falsafa ya KAIZEN imechangia kukuza uchumi katika nchi ya Japan, na Tanzania ni miongoni mwa nchi 16 Barani Afrika ambazo zinatekeleza falsafa hiyo.

Amesema faida ya KAIZEN ni kuwezesha uongezaji endelevu wa ubora na tija wa bidhaa za viwandani, kupunguza muda wa utendaji kazi, gharama za uzalishaji, kuboresha usimamizi wa Rasilimali watu, fedha, na vitendea kazi.

“Neno KAIZEN linatokana na maeneno mawili ya KIJAPAN, KAI maana yake ni badiliko zuri na neon ZEN likiwa na maana ya maboresho endelevu, hivyo KAIZEN ni mabadiliko endelevu mazuri kuelekea kwenye ukuaji wa uchumi,”amesema Pweleza.

“Falsafa ya KAIZEN inahimiza ushirikishwaji, uwajibikaji kwenye taasisi, kampuni au kiwanda katika mlolongi mzima wa uzalishaji ili kuhimili ushindani, pia kuwepo na ubunifu katika kupunguza gharama zisizo za lazima viwandani ili kuongeza tija na ubora kwenye mnyororo wa thamani wa bidhaa na huduma,”ameongeza.

Naye Mgeni Rasmi Kaimu Katibu Tawala msaidizi sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji mkoani Shinyanga Dotto Maligisa, akisoma hotuba ya ufunguzi wa mafunzo hayo kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, ameipongeza Serikali ya awamu ya sita kwa kuithamini sekta ya viwanda na kutambua mchango wake mkubwa na kuleta mafunzo hayo ya KAIZEN ili kuifikisha Tanzania kwenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

“Nchi ya Japan haikujaliwa kuwa na rasilimali madini, misitu, mifugo, mafuta ya petrol, gesi asilia wala mazao ya kilimo, na Japani ni miongoni mwa nchi Nane zinazoitwa “G8” moja ya siri ya mafaniko ya Japan ni kuwekeza kwenye rasilimali watu na ubora wa bidhaa za viwandani,”amesema Maligisa.

Aidha, amewataka washiriki wa mafunzo hayo wakaitekeleze Falsafa hiyo ya KAIZEN kwa vitendo pamoja na kwenda kuwa mabalozi kwa wenzao na kujituma katika kazi, kuwa wabunifu na kuzingatia ubora wa bidhaa.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wameipongeza Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara kwa kuwapatia mafunzo hayo ya falsafa ya KAIZEN ambayo yamewajenga kiutendaji kazi.
Kaimu Katibu Tawala msaidizi sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji mkoani Shinyanga Dotto Maligisa, akisoma hotuba ya ufunguzi wa mafunzo hayo kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga.

Mkuu wa Kitendo cha KAIZEN kutoka Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Richard Pweleza, akizungumza kwenye mafunzo hayo.

Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabishara wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA), Mkoa wa Shinyanga Dk. Kulwa Meshack.

Meneja wa Shrika la kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) Mkoa wa Shinyanga Hopeness Elia akizungumza kwenye mafunzo hayo.

Mkufunzi Emmanuel Zacharia akitoa mafunzo ya KAIZEN kwa washiriki.

Mkufunzi Juma Mantakara akitoa mafunzo ya KAIZEN kwa washiriki.

Washiriki wakifautilia mafunzo ya uhamasishaji wa Falsafa ya KAIZEN.

Washiriki wakiendelea na mafunzo.

Washiriki wakiendelea na mafunzo.

Washiriki wakiendelea na mafunzo.

Washiriki wakiendelea na mafunzo.

Washiriki wakiendelea na mafunzo.

Washiriki wakiendelea na mafunzo.

Washiriki wakiendelea na mafunzo.

Washiriki wakiendelea na mafunzo.

Washiriki wakiendelea na mafunzo.

Washiriki wakiendelea na mafunzo.

Washiriki wakiendelea na mafunzo.

Washiriki wakiendelea na mafunzo.

Washiriki wakiendelea na mafunzo.

Washiriki wakiendelea na mafunzo.

Washiriki wakiendelea na mafunzo.

Washiriki wakiendelea na mafunzo.

Washiriki wakiendelea na mafunzo.

Washiriki wakiendelea na mafunzo.

Washiriki wakiendelea na mafunzo.

Washiriki wakiendelea na mafunzo.
Share:

KIKWETE ATAKA MIPANGO MIJI KUPITIWA UPYA



Na Dotto Kwilasa, Malunde I Blog-DODOMA.


NAIBU Waziri wa Ardhi ,Nyumba na maendeleo ya makazi Ridhiwan Kikwete 
amezielekeza Mamlaka za upangaji, wataalamu wa ardhi na mipango Miji kuona haja ya kupitia upya suala la mpangilio wa ujenzi wa makazi ya Jiji la Dodoma ili kuondoa ongezeko la migogoro ya ardhi na makazi holela. 

Kikwete ameeleza hayo leo Jijini hapa kwenye uzinduzi wa bodi mpya ya wakurugenzi ya usajili wa wataalamu wa mipango Miji na kueleza kuwa kutokana na ujenzi holela kumekuwa na malalamiko mengi ya uvamizi wa ardhi Jijini Dodoma Kutokana ma ujenzi holela usiofuata taratibu na kanuni za mipango Miji.

Amesema ili Jiji liwe la kisasa mipango Miji inapaswa izingatie makazi ya watu na kueleza kuwa hakutakiwi kuwe na sehemu za starehe katika maeneo ya makazi huku akiwaonya wataalamu wa ardhi kutowaruhusu wanasiasa kuwaongoza. 

Amesema ili kuondokana na ujenzi holela ni lazima wananchi  waelimishwe, wajue kwa undani, na wakiri kukerwa na ujenzi au uendelezaji ardhi kiholela na kwamba elimu hiyo itawahamasisha wananchi walioendeleza ardhi kiholela kuchangia gharama za uandaaji wa mipango ya matumizi ya ardhi hasa kupitia upangaji shirikishi (urasimishaji).

"Tunayo kazi ya kusimamaia zaidi,Bado masta plani ya Jiji hili haiko sawa kuna baadhi ya viwanja vimepimwa kiwanja  juu ya viwanja natoa rai kwa Wakurugenzi wa Halmashauri kutoa kipaumbele kuhusu utoaji elimu ya upangaji wa matumizi ya ardhi na kuhimiza uandaaji na utekelezaji wa mipango ya matumizi 
ya ardhi katika miji, miji midogo na vijiji,"amesema.  
 
Amesema ushirikishaji wa wadau wote katika upangaji wa Ardhi ni suala la msingi ili kuepusha migogoro pamoja na hasara za kiuchumi na kimazingira, ambazo zinaweza kujitokeza wakati wa utekelezaji wa mipango hiyo. 

"Ushiriki wa wadau wengine wenye maslahi katika ardhi kwa sasa siyo wa kuridhisha sana, jambo linalosababisha maslahi yao kutozingatiwa kikamilifu kwenye mipango ya matumizi inayoandaliwa hili linajidhihirisha kwa kuwepo na migogoro mingi ya mwingiliano wa matumizi ya ardhi mijini na vijijini,"amesema na kuongeza;

Mfano eneo la nzuguni kuna watu walitolewa kwenye maeneo yao huo ni uonevu mkubwa,matokeo yake kuna watu waliotoka Dar ndio wanao milikishwa maeneo hayo kwa kuonekana wao ndio Wenye hadhi ya kuishi nzuguni,"amesema

Naibu Waziri huyo amefafanua kuwa Migogoro ya aina hiyo hukwamisha shughuli nyingi za maendeleo hivyo, ni muhimu  kuwashirikisha wadau kutoka sekta nyingine za maendeleo wakati wa kuandaa mipango miji ili isikinzane na mipango ya sekta zao.  

Kuhusu kukabiliana na uhaba wa watumishi amesema Bodi kwa kushirikiana na Wizara hiyo, itaendelea kuomba vibali vya uhamisho wa watumishi kuhamia Bodi, kupitia Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora pamoja na kuwajengea uwezo watumishi waliopo.  

Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi hiyo Prof.John Lupala amesema bodi hiyo itafanya kazi ya kusimamia utekelezaji wa bodi kwa kuzingatia sheria na  kanuni zinazoongoza mipango Miji. 

Amesema kwa kuzingatia uzoefu na weledi walionao katika fani mbalimbali watashirikiana kikamilifu na Wizara kuendeleza taaluma ya Mipangomiji kwa pamoja na kufikia lengo la kusimamia Wataalam wa Mipangomiji na kampuni za upangaji miji. 

Prof.Lupala amesema bodi hiyo itasimamia Wataalam na Kampuni za Mipangomiji kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia Sheria, Kanuni na taratibu za upangaji miji, kutoa huduma bora, kuweka mazingira ya kuvutia Wataalam wa Mipangomji waliokidhi vigezo vya kusajiliwa ili wasajiliwe, pia kuzalisha fursa zaidi za ajira na kuongeza mchango katika pato la taifa.

Amesema kwa mujibu wa Sheria, Bodi imepewa dhamana ya kuisimamia taaluma ya Mipangomiji pamoja na Wataalam wa Mipangomiji, hivyo watahakikisha wanaweka mipango kuifanya taaluma ijulikane kwa wananchi na pale ambapo mtaalam au kampuni imefanya kazi kinyume na maadili zichukuliwe hatua stahiki kwa mujibu wa Sheria.  
 
"Tunaahidi kufanya kazi kwa uadilifu na weledi wa hali ya juu, kwa maslahi mapana ya nchi yetu na kwa kuzingatia Sheria na Kanuni zilizopo ili kuhakikisha kwamba, Bodi inakidhi matarajio ya wadau na kuleta tija katika utekelezaji wa majukumu lakini jambo kubwa zaidi tutabuni mbinu za namna bora ya kuimarisha utendaji kazi wa Wataalam na Kampuni za Upangaji Miji pamoja na kuibua mikakati ya kutatua changamoto zinazoikabili taaluma hii na Sekta ya Ardhi kwa ujumla,"amesisitiza  
 
Naye Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri ameeleza kuwa ili ardhi ithaminiwe lazima kuwe na uhifadhi ardhi ili miji ipangwe na kuwa na hadhi nzuri.

Aidha ameishauri bodi hiyo kutengeneza na kuandaa mpango kazi wa ardhi ili kuboresha miundombinu ya majiji 
ikiwa ni pamoja na kusajili wataalamu wa ardhi kwa kuhusisha makampuni ya upimaji ardhi kuondoa migogoro ya ardhi.

Mkuu huyo wa Wilaya pia ameishauri elimu kwa Umma ifanyike ili wananchi wajue namna ya kuimiliki ardhi kihalali  na kuondokana na migogoro iliyopo ambayo kwa kiasi fulani inakwamisha shughuli za maendeleo.

"Tuwaelimishe wananchi kuhusu ardhi,nguvu tunayotumia zaidi kubomoa makazi tuielekeze zaidi kwenye elimu kwa Umma hii itasaidia uwepo wa udhibiti wa mpango Miji,"amesema





Share:

MUME WANGU ANASUSA KULA CHAKULA CHA SIKU

Jina langu ni Mama Jamal kutokea Kakamega nchini Kenya, niliolewa mwaka 2018, mimi na mume wangu tunapenda sana ila kuna jambo fulani kipindi cha katikati karibia livunje ndoa yetu.

Nalo ni kwamba mume wangu ilikuwa anasusa kula chakula cha usiku, yaani kila nikitaka kumpa haki yake ya ndoa alikuwa anasema amechoka, mara hajisikiii, basi ni limradi tu asishiriki tendo hilo.

Nilikuwa na wasiwasi mkubwa sana na mashaka mengi, nilisema huyo atakuwa na mpango wa kando huko nje ambao unampatia mapenzi ya kutosha, hivyo akija kwangu anakuwa hana hamu tena.

Usiku mmoja niliamua kumuuliza kuhusu hilo, alikataa kabisa kuwa mpango wa kando, lakini nikamwambia anipatie haki yangu hakuwa tayari kufanya hivyo.

Ndipo kakachoka hali hiyo na kuamua kuchukua vitu vyangu na kurudi kwa wazazi wangu maana sikuona sababu ya kuendelea kuishi na mwanaume ambaye hanitumiziii mahitaji yangu ya kindoa.

Nilikaa kwa wazazi wangu miezi mitatu, ndipo mume wangu alikuja nyumbani kwetu kunibembeleza nirudi nyumbani, nilimkatalia kabisa na kusema siwezi hadi pale ambapo atakuwa ananitimizia haki yangu.

Katika mazungumzo yetu, ndipo akaniambia amekumbwa na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume ila alikuwa anaona aibu kuniambia.

Nikamwambia kama ni hilo tu mbona ni jambo dogo sana, tunaweza kutafuta dawa na kufanikiwa bila ya tabu yoyote ile, ndipo tukawapata AfricanDoctors ambao naweza kusema ndio wamekuja kuikoa ndoa yetu.

Rafiki yangu mmoja ndiye alinipatia namba za AfricanDoctors ambazo ni +254719153099 na kuniambia kuwa hata mume wake aliwahi kukumbana na changamoto hiyo lakini AfricanDoctors wakaweza kuwasaidia na sasa wanafurahia ndoa yao.

Baada ya kuwasiliana nao, waliweza kumtumia mume wangu dawa namna ambavyo anapaswa kutumia, basi alifuata maelekezo yale na baada ya muda alianza kurejea katika hali yake ya kawaida na sasa anakula chakula cha usiku vizuri tu.

Wasiliana na AfricanDoctors kwa namba +254719153099.

Mwisho.
Share:

MIGODI YA BARRICK YAWEKA REKODI YA UZALISHAJI NA KUPATA THAMANI YA MUDA MREFU


Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow akizungumza na Waandishi wa habari katika Mgodi wa Bulyanhulu. Kushoto ni Meneja wa Barrick Tanzania, Melkiory Ngido, kulia ni Naibu Waziri wa Madin Dkt. Steven Kiruswa.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

 Kampuni ya Dhahabu ya Barrick  inayomiliki Migodi miwili ya North Mara na Bulyanhulu imeongeza pato lake kwa pamoja hadi kufikia wakia 547,000 kwa mwaka 2022, na kufanikisha hatua nyingine ya kuelekea hadhi ya Daraja la Kwanza.

Mgodi wa Dhahabu wa Daraja la Kwanza ni ule wenye hifadhi ya dhahabu yenye uwezo wa kuzalisha kwa angalau kipindi cha miaka 10, angalau wakia 500,000 za dhahabu kwa mwaka na jumla ya gharama za fedha taslimu kwa kila wakia kwa kipindi cha uhai wa mgodi ambazo ziko katika nusu ya chini ya grafu ya gharama za tasnia husika.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari na wadau wengine katika Mgodi wa Bulyanhulu Januari 25,2023 , Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow, amesema tangu kampuni ichukue jukumu la udhibiti wa migodi hiyo mwaka 2019 imefanikiwa kufanya mageuzi makubwa katika shughuli zilizokuwa zimekufa au zikielekea kufa na kuwa mali zenye thamani ya hali ya juu kwa utendaji wake kwa sasa, matarajio yake ya baadaye, na kukubalika kwake katika jamii.


Aidha amesema utafutaji wa madini unaendelea kutoa fursa za kuongeza ukubwa wa akiba ya miamba yenye madini katika migodi yote miwili huku akieleza kuwa kipindi cha mpito cha mgodi wa North Mara kuelekea uchimbaji wa mmiliki unafanikiwa kwa kuongeza kwa kasi upanuzi wake unaoendelea wa chimbo la wazi kukiwa na uboreshaji wa ufanisi na gharama, wakati maendeleo ya kiteknolojia katika shughuli za uchimbaji wa chini kwa chini yanaongeza tija. 

Ameongeza kuwa Mipango ya kuanzisha upya uchimbaji katika chimbo la Gena inaendelea vizuri.


Katika mgodi wa Bulyanhulu, amesema shabaha kuu ni kuharakisha maendeleo ili kuukabili upungufu wake kwa kuifikia akiba mpya ya madini katika upande wa magharibi na upatikanaji wa wake.


"Leo hii, migodi hiyo inatambuliwa na serikali na jamii kama biashara zinazowajibika kwa jamii kwa kutengeneza fursa zenye manufaa makubwa na kuzishirikisha jamii na wadau wote katika fursa hizo na katika manufaa yenyewe, na kama mbia mkuu katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini Tanzania," alisema.


"Mwaka jana, North Mara ilitambuliwa rasmi kama mlipakodi mkubwa zaidi wa Tanzania na Bulyanhulu ilitunukiwa tuzo ya Mwajiri Bora Anazingatia Masharti na Matakwa ya Sheria, iliyotolewa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii. North Mara na Bulyanhulu pia zilipokea tuzo za mshindi wa kwanza na wa pili mtawalia za kutambua mchango wao kwa Uuzaji wa Madini nje ya nchi na kwa uzalishaji wa fedha za kigeni.

Migodi yote miwili imetoka safari ya mbali sana na tunatarajia kuendelea na safari hiyo kupitia ubia wetu wa Twiga na serikali”, alisema Bristow

Alisema tangu ichukue jukumu la udhibiti mnamo mwaka 2019, Barrick imeingiza dola za kimarekani bilioni 2.4 katika uchumi wa Tanzania. Mwaka jana, ililipa dola za kimarekani milioni 303 za kodi, mrabaha, ushuru, gawio na ulipaji wa mikopo ya wanahisa na dola za kimarekani milioni 476 kwa wasambazaji na watoaji wa huduma wa ndani .


"Kadiri migodi ilivyoendelea kukua, imeendelea kuweka kipaumbele cha utoaji wa ajira kwa watu wa ndani. Nguvu kazi yake hivi sasa tayari ina Watanzania wapatao 96%, huku 45% ya waajiriwa wapya wakitoka katika jamii zinazoizunguka migodi. Kupitia kamati zake za maendeleo ya jamii, migodi hiyo imewekeza zaidi ya dola za kimarekani milioni 10 katika miradi ya kuboresha huduma za afya, elimu, upatikanaji wa maji ya bomba na miundombinu ya barabara",alieleza.


Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Madin Dkt. Steven Kiruswa ameishukuru Barrick na Kampuni tanzu ya Twiga kwa mafanikio makubwa yanayozidi kuonekana kupitia uwekezaji hapa nchini.

“Tuendelee kupiga vita utoroshaji madini, tuendelee kuwapa ushirikiano kampuni ya Barrick ili uwekezaji uwe na tija kwa wananchi. Tunataka kampuni ziwape kipaumbele wazawa ambapo tunashukuru Barrick imeajiri watanzania asilimia 96%”,alisema Dkt. Kiruswa.


Naye Mbunge wa Jimbo la Msalala Mhe. Idd Kassim amesema uhusiano uliopo kati ya Mgodi wa Bulyanhulu na jamii ni mzuri ambapo fedha zinazotolewa na mgodi zinaleta tija kwa jamii.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yahaya Nawanda wamesema wataendelea kushirikiana na Kampuni ya Barrick na kuhakikisha fedha zinazotolewa zinainufaisha jamii.
Naibu Waziri wa Madin Dkt. Steven Kiruswa akizungumza na waandishi wa habari
Naibu Waziri wa Madin Dkt. Steven Kiruswa akizungumza na waandishi wa habari
Naibu Waziri wa Madin Dkt. Steven Kiruswa akizungumza na waandishi wa habari
Naibu Waziri wa Madin Dkt. Steven Kiruswa akizungumza na waandishi wa habari
Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow akiteta na Naibu Waziri wa Madin Dkt. Steven Kiruswa (kulia).
Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow akizungumza na Waandishi wa habari katika Mgodi wa Bulyanhulu. Kushoto ni Meneja wa Barrick Tanzania, Melkiory Ngido, kulia ni Naibu Waziri wa Madin Dkt. Steven Kiruswa.
Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow akizungumza na Waandishi wa habari katika Mgodi wa Bulyanhulu. Kushoto ni Meneja wa Barrick Tanzania, Melkiory Ngido, kulia ni Naibu Waziri wa Madin Dkt. Steven Kiruswa.
Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow akizungumza na Waandishi wa habari katika Mgodi wa Bulyanhulu.
Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow akizungumza na Waandishi wa habari katika Mgodi wa Bulyanhulu.
Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow akizungumza na Waandishi wa habari katika Mgodi wa Bulyanhulu. 
Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow akizungumza na Waandishi wa habari katika Mgodi wa Bulyanhulu. 

Meneja wa Barrick Tanzania, Melkiory Ngido akizungumza na waandishi wa habari

Meneja wa Barrick Tanzania, Melkiory Ngido akizungumza na waandishi wa habari
 Mbunge wa Jimbo la Msalala Mhe. Idd Kassim akizungumza
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yahaya Nawanda akizungumza 
Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela akizungumza
Wadau wakiwa ukumbini
Wafanyakazi wa Barrick wakiwa ukumbini
Wafanyakazi wa Barrick wakiwa ukumbini
Viongozi  wa mikoa ya Geita na Shinyanga wakiwa ukumbini
Wafanyakazi wa Barrick na wadau wakiwa ukumbini
Wafanyakazi wa Barrick na wadau wakiwa ukumbini
Wafanyakazi wa Barrick wakiwa ukumbini.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger