Thursday, 26 January 2023

SERIKALI: TaSUBa ITAENDELEA KUWA KITUO BORA CHA MAFUNZO YA SANAA NA UTAMADUNI


Na Mwandishi Wetu. 

KATIBU Mkuu Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi amesema Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) ili kuifanya kuwa na mazingira bora zaidi ya utoaji wa taaluma ya sanaa na utamaduni. 

Hayo ameyasema Januari 25, 2023 alipotembelea Taasisi Wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani katika ziara ya kukagua ukarabati wa miundombini na vifaa mbalimbali vya kufundishia na kijifunzia vilivyopatikana kwa fedha za maendeleo zinazotolewa na Serikali kila mwaka. 

Dkt. Abbasi amesema Serikali itandelea kuongeza upatikanaji wa fedha za maendeleo ili kuhakikisha mazingira ya chuo yanaimarika kwa kukarabati miundombinu pamoja na kuongeza vifaa vya kisasa vya kujifunzia na kufundishia. 

"Serikali itaendelea kutimiza ahadi yake ili kuifanya TaSUBa iendelee kua Chuo bora zaidi cha mafunzo ya sanaa na utamaduni Afrika na Duniani," amesema Dkt. Abbasi. 

Amesema changamoto haziwezi kwisha kwa mara moja lakini TaSUBa imekua ikienda juu kila mwaka na kuongeza tija kwa sababu Serikali ina matashi mema kwa Taasisi na wananchi wake wote kwa ujumla. 

Ameitaka TaSUBa kuendelea kubuni miradi mipya yenye tija kwa lengo la kukuza Chuo na Serikali itaendelea kutoa fedha. 

"Sekta hii ndio Sekta shawishi inayochangia katika kuitangaza nchi kimataifa, mfano Brazil inafahamika kimataifa kupitia soka," amesema Dkt. Abbasi. 

Katibu Mkuu Dkt. Abbasi amewataka watumishi wa TaSUBa kutumia elimu waliyonayo kubadili mazingira ya Chuo wakijua kwamba hakuna mwingine atakayekuja kubadilisha hali zao isipokua wao wenyewe kwa kuwa kama una elimu na huitumii ni kazi bure "Education without Application is Useless." 

Aidha Dkt. Abbasi amewataka watumishi wa TaSUBa kuwa tayari kupokea mageuzi na kukubali kuacha kufanya kazi kwa mazoea jambo ambalo kwa kasi ya dunia ya sasa ni la msingi. 

Sambamba na hayo Katibu Mkuu Dkt. Abbasi amemsimamisha kazi Naibu Mkuu wa Chuo TaSUBa Mipango Fedha na Utawala Bw. Emmanuel Bwire kwa tuhuma za ukiukwaji wa maadili ya utumishi kazini na misingi ya utawala bora kwa nyakati tofauti alipokua akitumikia wadhifa wake huo. Bw. Bwire amesimamishwa kazi kuanzia January 25, 2023 ili kupisha uchunguzi wa tuhuma hizo. Nao Mwenyekiti ya Bodi ya Ushauri ya Taasisi hio, Bw. George Yambesi pamoja na Mkuu wa Chuo Dkt. Herbert Makoye wamemshukuru Katibu Mkuu kwa ziara aliyoifanya TaSUBa na kuahidi kuyafanyia kazi yale yote aliyoelekeza na kuendelea kutimiza wajibu wao kadiri ya maelekezo ya viongozi na kuendelea kushirikiana katika utekelezaji wa mipango mbalimbali.
Share:

Wednesday, 25 January 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI JANUARI 26,2023










Share:

SERIKALI YAAHIDI KUZIHAKIKI UPYA HOTELI ZA KITALII


***************************

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja ameiambia Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii kuwa Wizara ya Maliasili na Utalii itayafanyia kazi maelekezo yaliyotolewa na kamati hiyo kuhusu kuzifanyia upya uhakiki hoteli na loji za kitalii ambazo hazifanyi kazi vizuri ili kukabiliana na changamoto ya huduma za malazi kwa watalii hapa nchini.

Mhe. Mary Masanja ameyasema hayo kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii leo jijini Dodoma mara baada ya kupokea maoni, ushauri na maelekezo yaliyotolewa na Kamati ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii kuhusu taarifa ya Wizara ya Utendaji kazi wa Hoteli na Loji za kitalii za Serikali zilizobinafsishwa.

Amesema Tanzania imekua ikipokea watalii wengi hali iliyosababisha kuongezeka kwa mahitaji ya huduma za malazi kwa watalii kufuatia kazi kubwa iliyofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kutangaza vivutio vya utalii kupitia Filamu ya Royal Tour.

“Namshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuzindua filamu ya Royal Tour ambayo kwa sasa matunda yake yanaonekana kwa kuongezeka kwa mahitaji ya huduma za malazi kwa watalii hapa nchini” amebainisha Mhe. Masanja.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mhe. Ally Juma Makoa ameeleza kuwa Wizara ya Maliasili na Utalii inapaswa kufanya maamuzi kwa kufuata sheria zilizopo ili hoteli na loji ambazo hazifanyi kazi ziweze kutoa huduma ili kwenda na kasi ya idadi ya watalii pia kuongeza mapato yatokanayo na biashara za utalii, kuongeza tija na ufanisi katika uendeshaji wa hoteli za kitalii.

“Inabidi tufanye maamuzi ya haraka sana ya kuona namna gani tunaweza kuboresha huduma za hoteli na loji ambazo hazifanyi kazi ili kuendana na kasi ya idadi ya watalii wanaokuja nchini baada ya kuzinduliwa kwa Royal Tour” amesisitiza Mhe. Makoa.

Awali akiwasilisha taarifa ya hali ya loji na hoteli za kitalii Afisa Usimamizi wa Fedha Mkuu kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina Thabiti Dokodoko amesema uwekezaji katika hoteli na loji umeisaidia Serikali kuingiza kiasi cha shilingi bilioni 60.38 kwa kipindi cha miaka mitano (2018/19-Desemba,2022).

Ameongeza kuwa uwekezaji katika hoteli na loji za kitalii unalenga katika kutatua changamoto ya huduma za malazi hususan idadi ya vyumba na vitanda.
Share:

UVCCM SHINYANGA WAADHIMISHA MIAKA 46 YA CCM

Madhimisho ya miaka 46 ya Chama Cha Mapinduzi CCM

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Shinyanga, umeadhimisha miaka 46 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), huku vijana wa chama hicho wakitakiwa kuanzisha miradi ya maendeleo ili wajikwamue kiuchumi.

Madhimisho hayo yamefanyika leo Januari 25 katika ukumbi wa Mikutano wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Shinyanga Mjini, na katika maadhimisho hayo kulikuwa na matukio ya kupanda miti katika Shule mpya ya Sekondari Lubaga, na kutoa misaada mbalimbali katika kituo cha kulea watoto wenye ulemavu Buhangija.

Akizungumza katika maadhimisho hayo mgeni rasmi Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa (NEC) kupitia kundi la vijana Ramadhani Mlao, amewataka vijana wa chama hicho (UVCCM) waanzishe miradi ambayo itawainua kiuchumi.

“Vijana lazima tujishughulishe vinginevyo tutaendelea kuwa vibara wa watu, hakuna kitu kibaya kama kuwa omba omba kutakufanya uwe mnyonge, tumieni fursa zilizopo ikiwamo kuanzisha miradi ya kilimo,”amesema Mlao.

Katika hatua nyingine amewataka vijana wa Chama hicho, wawe mstari wa mbele kukipigania chama kupitia mikutano ya hadhara kwakushindana kwa hoja na kuwaeleza wananchi miradi ya maendeleo ambayo imetekelezwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

“Mikutano ya hadhara imefunguliwa vijana ndiyo Askari wa Chama tumlinde Rais wetu kwa hoja na siyo matusi, wenzetu wakitoa matusi, sisi tushindane kwa hoja,”amesema Mlao.

Naye Mwenyekiti wa (UVCCM) Mkoa wa Shinyanga Clement Madinda, amesema maagizo yote yaliyotolewa na MNEC huyo, watayafanyia kazi ikiwamo kuendelea kutumia fursa ya kupata mikopo ya Halmashauri asilimia 10 na kuanzisha miradi ya kiuchumi.

Amesema wanaishukuru pia Serikali kwa kuendelea kuwa amini vijana na hata kuwapatia mikopo, ambapo katika Manispaa ya Shinyanga vijana wamepewa Coaster Mbili, Pikipiki 30, na Trekta mbili kwa upande wa Kahama, huku akiiomba Serikali kuwapatia pia vijana elimu ujasiriamali na usimamizi wa miradi.

Kwa upande wake Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, amewataka vijana kuendelea kuchangamkia fursa za mikopo asilimia 10 ambayo hutolewa asilimia 4 kwa vijana, na kubainisha Manispaa hiyo katika mwaka wa fedha (2021-2022) imeshatoa kiasi cha fedha Sh.milioni 126 fedha za mikopo kwa vijana.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa (NEC) kupitia kundi la vijana (UVCCM) Ramadhani Mlao, akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 46 ya CCM mkoani Shinyanga.

Mwenyekiti wa UVCCM Mkoani Shinyanga Clement Madinda akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 46 ya CCM.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Anorld Makombe akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 46 ya CCM.

Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko akizungumza kwenye Maadhimisho ya miaka 46 ya CCM.

Katibu wa (UVCCM) Mkoa wa Shinyanga Raphael Nyandi akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 46 ya CCM.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa (NEC) kupitia kundi la vijana (UVCCM) Ramadhani Mlao, (katikati) akiwa na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga Clement Madinda na Mjumbe wa Baraza Kuu la CCM Taifa kupitia umoja wa vijana (UVCCM) kutoka mkoa wa Shinyanga Mwanalisa Faustine kwenye maadhimisho ya miaka 46 ya CCM.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Anorld Makombe, (kushoto) akiwa na Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko kwenye maadhimisho ya miaka 46 ya CCM.

Maadhimisho ya miaka 46 ya CCM yakiendelea.

Maadhimisho ya miaka 46 ya CCM yakiendelea.

Maadhimisho ya miaka 46 ya CCM yakiendelea.

Maadhimisho ya miaka 46 ya CCM yakiendelea.

Maadhimisho ya miaka 46 ya CCM yakiendelea.

Maadhimisho ya miaka 46 ya CCM yakiendelea.

Maadhimisho ya miaka 46 ya CCM yakiendelea.
Maadhimisho ya miaka 46 ya CCM yakiendelea.

Maadhimisho ya miaka 46 ya CCM yakiendelea.

Maadhimisho ya miaka 46 ya CCM yakiendelea.

Maadhimisho ya miaka 46 ya CCM yakiendelea.

Maadhimisho ya miaka 46 ya CCM yakiendelea.
 
 Watoto wenye ulemavu ambao wanalelewa kituo cha Buhangija Manispaa ya Shinyanga wakipokea msaada wa vitu mbalimbali.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa (NEC) kupitia kundi la vijana (UVCCM) Ramadhani Mlao, (wapili kutoka kulia) akiendesha baiskeli kuelekea kwa balozi wa tawi la CCM Shina namba 2 Mwajuma Ramadhani na kupandisha Bendera ya Chama.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa (NEC) kupitia kundi la vijana (UVCCM) Ramadhani Mlao, akipandisha Bendera ya Chama.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa (NEC) kupitia kundi la vijana (UVCCM) Ramadhani Mlao, akipanda Mti katika Shule mpya ya Sekondari Lubaga.

Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Shinyanga Clement Madinda akipanda mti katika Shule mpya ya Sekondari Lubaga.

Mjumbe wa Baraza Kuu la CCM Taifa kupitia umoja wa vijana (UVCCM) kutoka Mkoa wa Shinyanga Mwanalisa akipanda mti katika Shule mpya ya Sekondari Lubaga.

Katibu wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga Raphael Nyandi akipanda mti katika shule mpya ya Sekondari Lubaga.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa (NEC) kupitia kundi la vijana (UVCCM) Ramadhani Mlao, akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Anorld Makombe alipowasili mkoani Shinyanga kwenye maadhimisho ya miaka 46 ya CCM.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa (NEC) kupitia kundi la vijana (UVCCM) Ramadhani Mlao, akisalimiana Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, alipowasili mkoani Shinyanga kwenye maadhimisho ya miaka 46 ya CCM.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa (NEC) kupitia kundi la vijana (UVCCM) Ramadhani Mlao, akisalimiana na Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Ester Makune, alipowasili mkoani Shinyanga kwenye maadhimisho ya miaka 46 ya CCM.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa (NEC) kupitia kundi la vijana (UVCCM) Ramadhani Mlao, akisalimiana na Katibu wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga Raphael Nyandi, alipowasili mkoani Shinyanga kwenye maadhimisho ya miaka 46 ya CCM.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa (NEC) kupitia kundi la vijana (UVCCM) Ramadhani Mlao, akisalimiana na Katibu wa Hamasa Mkoa wa Shinyanga Severine Luhende,alipowasili mkoani Shinyanga kwenye maadhimisho ya miaka 46 ya CCM.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa (NEC) kupitia kundi la vijana (UVCCM) Ramadhani Mlao, akiwa mkoani Shinyanga kwenye maadhimisho ya miaka 46 ya CCM.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger