Saturday, 21 January 2023

WASABATO SHINYANGA MJINI WAFUNGA SIKU 10 MAOMBI...WALIOMBEA TAIFA, WATAKA MAUAJI YAKOMESHWE


Maombi maalum yakiendelea Kanisa la Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini
Mchungaji wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Mtaa wa Sengerema Mjini, Brian Abdallah (kulia) na Mchungaji Lazaro Mbogo wa Kanisa la Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini wakiongoza maombi wakati wa Ibada ya kufunga Siku 10 za Maombi Maalumu.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kanisa la Waadventista Wasabato Shinyanga mjini limefunga Siku 10 za Maombi Maalumu pamoja na kuombea Taifa Amani  huku likihamasisha binadamu kuthaminiana, kupendana na kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Maombi hayo yaliongozwa na Mchungaji Brian Abdallah wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Mtaa wa  Sengerema Mjini Mkoani Mwanza ambayo yalianza Januari 11,2023 na kuhitimishwa leo Jumamosi Januari 21,2023 katika Kanisa la Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini yakiongozwa na Somo lisemalo ‘Kurejea Madhabahuni’.

Akiongoza Maombi ya kufunga Siku 10 za Maombi wakati wa Ibada leo Jumamosi Januari 21,2023, Mchungaji wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Mtaa wa Sengerema Mjini, Brian Abdallah amesema maombi hayo yamekuwa na baraka nyingi.

"Maombi haya ya siku 10 za mfungo yamekuwa na muitiko mkubwa awali tulikuwa ndani ya Kanisa lakini watu walikuwa wengi ikabidi tuhamie nje ya Kanisa, na watu wote wamebarikiwa,"amesema Mchungaji Brian.

Amesema katika siku hizo 10 za mfungo wa maombi, pia wameliombea Taifa kuendelea kuwa na amani, ikiwemo kukoma kwa matukio ya ukatili wa kijinsia na mauaji.

“Tumemuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais Mhe. Dkt Philip Mpango, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Mawaziri, Wabunge, Madiwani na viongozi wote. Tunataka nchi hii iendelee kuwa na amani, watu waishi kwa amani na upendo, wathaminiane na kuachana na vitendo vya ukatili wa kijinsia”,amesema Mchungaji Brian.

“Kumekuwa na matukio ya ukatili yanatokea katika jamii mfano mme anaua mke wake,tunalaani matukio haya na hatupendi kuyasikia, naomba binadamu tuwe na upendo. Ni lazima tuwe na upendo ili jamii iishi kwa amani. Eee Mwenyezi Mungu ingilia kati vitendo vya mauaji yanayoendelea katika jamii, komesha ukatili wa kijinsia ukalete amani na utulivu”,amesema Mchungaji Brian.

Kwa upande wake Mchungaji Lazaro Mbogo wa Kanisa la Waadventista Wasabato Mtaa wa  Shinyanga Mjini amewaomba viongozi wa dini kote nchini kuongeza kufundisha waumini wao kuishi kwa kuthaminiana na kupendana pamoja na jamii kumrudia Mungu ili kutokomeza matukio ya ukatili wa kijinsia nchini.

Na baadhi ya Waumini wa Kanisa hilo akiwemo Elizabeth Kasuka na Tumaini Nduta, wamesema katika siku hizo 10 za maombi wamebarikiwa na bwana, na kutoa wito kwa Watanzania wamrudie Mungu na kuacha kufanya vitendo viovu.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Muonekano wa mbele sehemu ya Kanisa  la  Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini
Mchungaji wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Mtaa wa Sengerema Mjini Mkoani Mwanza Brian Abdallah akitoa Mahubiri wakati wa Ibada ya kufunga Siku 10 za Maombi katika Kanisa  la  Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini leo Jumamosi Januari 21,2023. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mchungaji wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Mtaa wa Sengerema Mjini Mkoani Mwanza Brian Abdallah akitoa Mahubiri wakati wa Ibada ya kufunga Siku 10 za Maombi katika Kanisa  la  Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini leo Jumamosi Januari 21,2023.
Mchungaji wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Mtaa wa Sengerema Mjini Mkoani Mwanza Brian Abdallah akitoa Mahubiri wakati wa kufunga Siku 10 za Maombi katika Kanisa  la  Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini leo Jumamosi Januari 21,2023.
Wanakwaya wakihubiri kwa Nyimbo wakati wa Ibada ya kufunga Siku 10 za Maombi katika Kanisa  la  Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini leo Jumamosi Januari 21,2023.
Wanakwaya wakihubiri kwa Nyimbo wakati wa Ibada ya kufunga Siku 10 za Maombi katika Kanisa  la  Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini
 Mchungaji Lazaro Mbogo wa Kanisa la Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini akizungumza wakati wa Ibada ya kufunga Siku 10 za Maombi katika Kanisa  la  Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini
Mchungaji Lazaro Mbogo wa Kanisa la Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini akizungumza wakati wa Ibada ya kufunga Siku 10 za Maombi katika Kanisa  la  Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini
Mchungaji wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Mtaa wa Sengerema Mjini Mkoani Mwanza Brian Abdallah (kulia) na Mchungaji Lazaro Mbogo wa Kanisa la Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini wakiongoza maombi wakati wa Ibada ya kufunga Siku 10 za Maombi.
Mchungaji wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Mtaa wa Sengerema Mjini Mkoani Mwanza Brian Abdallah (kulia) na Mchungaji Lazaro Mbogo wa Kanisa la Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini wakiongoza maombi wakati wa Ibada ya kufunga Siku 10 za Maombi.
Mchungaji wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Mtaa wa Sengerema Mjini Mkoani Mwanza Brian Abdallah(kulia) na Mchungaji Lazaro Mbogo wa Kanisa la Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini wakiongoza maombi wakati wa Ibada ya kufunga Siku 10 za Maombi.
Maombi maalum yakiendelea Kanisa la Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini
Maombi maalum yakiendelea Kanisa la Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini
Maombi maalum yakiendelea Kanisa la Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini
Maombi maalum yakiendelea Kanisa la Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini

Maombi maalum yakiendelea Kanisa la Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini
Maombi maalum yakiendelea Kanisa la Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini
Maombi maalum yakiendelea Kanisa la Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini
Maombi maalum yakiendelea Kanisa la Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini
Maombi maalum yakiendelea Kanisa la Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini
Maombi Maalum kuliombea Taifa yakiendelea Kanisa la Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini
Maombi maalum yakiendelea Kanisa la Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini
Maombi maalum yakiendelea Kanisa la Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini
Maombi maalum yakiendelea Kanisa la Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini
Wanakwaya wakihubiri kwa Nyimbo wakati wa Ibada ya kufunga Siku 10 za Maombi katika Kanisa  la  Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini
Wanakwaya wakihubiri kwa Nyimbo wakati wa Ibada ya kufunga Siku 10 za Maombi katika Kanisa  la  Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini
Wanakwaya wakihubiri kwa Nyimbo wakati wa Ibada ya kufunga Siku 10 za Maombi katika Kanisa  la  Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini
Waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini wakiendelea na Ibada
Waumini wa Kanisa la  Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini wakiendelea na Ibada
Wanakwaya wakihubiri kwa Nyimbo wakati wa Ibada ya kufunga Siku 10 za Maombi katika Kanisa  la  Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini

Waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini wakiendelea na Ibada
Waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini wakiendelea na Ibada
Waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini wakiendelea na Ibada
Waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini wakiendelea na Ibada
Waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini wakiendelea na Ibada
Waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini wakiendelea na Ibada
Waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini wakiendelea na Ibada
Waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini wakiendelea na Ibada
Waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini wakiendelea na Ibada
Waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini wakiendelea na Ibada
Waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini wakiendelea na Ibada
Waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini wakiendelea na Ibada
Waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini wakiendelea na Ibada
Waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini wakiendelea na Ibada
Waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini wakiendelea na Ibada
Waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini wakiendelea na Ibada

Mchungaji Lazaro Mbogo wa Kanisa la Waadventista Wasabato Mtaa wa  Shinyanga Mjini akibatiza baada ya kufunga siku 10 za maombi
Mchungaji Lazaro Mbogo wa Kanisa la Waadventista Wasabato Mtaa wa  Shinyanga Mjini akibatiza baada ya kufunga siku 10 za maombi
Mchungaji Lazaro Mbogo wa Kanisa la Waadventista Wasabato Mtaa wa  Shinyanga Mjini akibatiza baada ya kufunga siku 10 za maombi
Mchungaji Lazaro Mbogo wa Kanisa la Waadventista Wasabato Mtaa wa  Shinyanga Mjini akibatiza baada ya kufunga siku 10 za maombi
Mchungaji Lazaro Mbogo wa Kanisa la Waadventista Wasabato Mtaa wa  Shinyanga Mjini akibatiza baada ya kufunga siku 10 za maombi
Mchungaji Lazaro Mbogo wa Kanisa la Waadventista Wasabato Mtaa wa  Shinyanga Mjini akibatiza baada ya kufunga siku 10 za maombi
Mchungaji Lazaro Mbogo wa Kanisa la Waadventista Wasabato Mtaa wa  Shinyanga Mjini akibatiza baada ya kufunga siku 10 za maombi
Mchungaji Lazaro Mbogo wa Kanisa la Waadventista Wasabato Mtaa wa  Shinyanga Mjini akibatiza baada ya kufunga siku 10 za maombi

Wanakwaya wakihubiri kwa Nyimbo wakati wa Ibada ya kufunga Siku 10 za Maombi Maalum katika Kanisa  la  Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Share:

MHANDISI KAMANDO:’UCHUMI WA RUVUMA WAENDELEA KUPAA KUPITIA MAKAA YA MAWE’


RUVUMA

Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Ruvuma, Mhandisi Hamis Kamando amesema kuwa kutokana na uwepo wa wingi wa madini ya makaa ya mawe katika mkoa wa Ruvuma ikiwa ni tani milioni 328, kampuni nyingi za kitanzania zimepata mwamko na kuwekeza hali iliyopelekea ofisi yake kuendelea kufanya vizuri kwenye ukusanyaji wa maduhuli kwa kuvuka malengo ya kila mwaka yanayowekwa na Serikali katika ofisi yake.

Mhandisi Kamando aliyasema hayo mapema jana tarehe 20 Januari, 2023 mkoani Ruvuma kwenye mahojiano maalum ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kipindi maalum chenye lengo la kuangalia mchango wa Sekta ya Madini katika kuwawezesha watanzania kiuchumi pamoja na uboreshaji wa huduma za jamii katika mikoa ya Njombe, Ruvuma na Mtwara.

Akieleza mafanikio ya Sekta ya Madini katika mkoa wa Ruvuma yaliyochangiwa na uwekezaji katika uchimbaji wa makaa ya mawe, Mhandisi Kamando alisema kuwa katika kipindi cha mwaka wa fedha 2021-2022 ofisi yake ilipangiwa kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 12 na kufanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 21 ikiwa ni asilimia 175 ya lengo lililowekwa katika mwaka husika.

Aliendelea kusema kuwa katika mwaka wa fedha 2022-2023 ofisi yake iliwekewa lengo la kukusanya shilingi bilioni 26.3 na kuongeza kuwa kuanzia kipindi cha mwezi Julai mwaka 2022 hadi tarehe 19 Januari, 2023 ofisi imefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 23.1 ikiwa ni asilimia 87 ya lengo la mwaka husika na kuendelea kusema kuwa ofisi imejipanga kukusanya hadi shilingi bilioni 35 ifikapo mwezi Juni mwaka huu.

Katika hatua nyingine, Mhandisi Kamando alieleza kuwa ofisi yake imeendelea kubuni mikakati mbalimbali ya usimamizi wa ukusanyaji wa maduhuli kwa ubunifu wa hali ya juu ambapo inatarajia kuwa miongoni mwa mikoa minne inayoongoza kwenye ukusanyaji wa maduhuli katika Sekta ya Madini.

Alieleza kuwa mafanikio mengine kuwa ni pamoja na kampuni za uchimbaji wa madini ya makaa ya mawe katika mkoa wa Ruvuma kuendelea kushirikisha wananchi kwenye utoaji wa huduma kwenye migodi kupitia kanuni za ushirikishwaji wa watanzania katika Sekta ya Madini na uboreshaji wa huduma za jamii.

“Kutokana na elimu ambayo imekuwa inatolewa na Ofisi ya Madini Mkoa wa Ruvuma kwa kampuni za uchimbaji wa makaa ya mawe kuhusu ushirikishwaji wa watanzania katika Sekta ya Madini, kampuni zimeanza kutoa zabuni mbalimbali ikiwa ni pamoja na usambazaji wa bidhaa za vyakula na vifaa kwenye migodi hivyo kupelekea wananchi kujipatia kipato huku Serikali ikikusanya kodi mbalimbali,” alisisitiza Mhandisi Kamando.

Katika hatua nyingine, sambamba na kupongeza kazi kubwa inayofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais, Philip Mpango, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko pamoja na uongozi wa Wizara ya Madini kwa kushirikiana na uongozi wa Tume ya Madini kwenye usimamizi wa Sekta ya Madini, aliwataka wananchi wengi kuchangamkia fursa za uwekezaji katika mkoa wa Ruvuma.

“Sambamba na uwepo wa madini ya makaa ya mawe, yapo madini mengine ya vito mbalimbali vya thamani ikiwa ni pamoja na almasi yanayopatikana katika maeneo tofauti ya mkoa wa Ruvuma, wawekezaji wote wanakaribishwa na milango ya ofisi ipo wazi muda wote kutoa msaada ili wananchi wengi zaidi waweze kunufaika,” alisema Mhandisi Kamando.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wawekezaji waliowekeza katika mkoa huo waliipongeza Serikali kupitia Wizara ya Madini na Tume ya Madini kwa kuweka mazingira ambayo ni rafiki na kuendelea kutatua changamoto mbalimbali kwenye Sekta ya Madini.

Akielezea manufaa ya uchimbaji wa madini ya makaa ya mawe, Mjumbe wa Bodi na Msimamizi wa Mradi wa Kampuni ya Jitegemee Holdings Company Limited inayojihusisha na uchimbaji wa makaa ya mawe katika Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma Boscow Mabena, alisema kuwa tangu kuanza kwa shughuli za uzalishaji mwaka 2021 kampuni imefanikiwa kulipa kiasi cha shilingi bilioni 7.01 ikiwa ni kodi, tozo na michango mbalimbali Serikalini.

Aliendelea kutaja mafanikio mengine kuwa ni pamoja na ajira kwa watumishi wa kada mbalimbali 147, utoaji wa michango mbalimbali kwenye vijiji vinavyozunguka mgodi na kuongeza kuwa kampuni imeshakaa na vijiji kwa ajili mapendekezo ya miradi mbalimbali ikiwa ni pamoja na ujenzi wa zahanati, mabweni katika shule za msingi na sekondari na maji kabla ya utekelezaji wake pamoja na utoaji wa fursa za huduma za vyakula kwenye mgodi.

Alitaja mafanikio mengine kuwa ni pamoja na kutwaa tuzo mbili kutoka katika mamlaka za Serikali ikiwemo tuzo ya mshindi wa pili ya mchangiaji mkubwa wa tozo za Serikali katika pato la nchi kutoka Wizara ya Madini na tuzo ya pili ikiwa ni ya mshindi wa pili wa mchangiaji mkubwa wa kodi za Serikali katika mkoa wa Ruvuma kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Wakati huohuo, Meneja wa Mgodi wa Ruvuma Coal Limited, Benedict Mushingwe akielezea hali ya uzalishaji wa makaa ya mawe katika mgodi huo tangu kuanzishwa kwake mwaka 2020 alisema kuwa mgodi umeendelea kufanya vizuri ambapo katika kipindi cha Januari hadi Desemba mwaka 2020 mgodi ulizalisha tani 600,000 na katika kipindi cha Januari hadi Desemba, 2022 mgodi ulizalisha tani milioni 1.9 na kuuza ndani ya nchi na katika nchi za nje kama vile Kenya, Uganda, Rwanda, Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Senegal, Ghana, Poland, India, Ufaransa, Uholanzi na nchi nyingine za Ulaya.

Alisema kuwa kupitia uzalishaji wa makaa ya mawe kampuni ilifanikiwa kulipa kiasi cha shilingi bilioni 66.8 Serikalini tangu kuanzishwa kwake sambamba na kutoa ajira 785 huku waajiriwa 379 wakiwa wanatoka maeneo ya karibu na mgodi.

Aliendelea kueleza mafanikio mengine kuwa ni pamoja na utoaji wa fursa mbalimbali za utoaji wa huduma kwenye mgodi ambapo wananchi wameunda vikundi na kuanza kutoa huduma za vyakula, ujenzi wa ofisi ya kijiji cha Paradiso, zahanati na kusisitiza kuwa mgodi unajipanga zaidi kuendelea kuboresha maisha ya wananachi wanaoishi katika mgodi pamoja na utunzaji wa mazingira.
Share:

Friday, 20 January 2023

NABII MKUU DKT GEORDAVIE AGAWA MILIONI 100 KWA WAFANYABIASHARA WA SOKO LA SAMUNGE

Nabii mkuu wa kanisa la Ngurumo ya Upako ambaye pia ni balozi wa amani Dkt. Geordavie Kasambale akiongea na wafanyabiashara kabla ya kukabidhi hundi ya shilingi milioni 100

Na Woinde Shizza , ARUSHA


Nabii mkuu wa kanisa la Ngurumo ya upako ambaye pia ni balozi wa amani Dkt Geordavie Kasambale amekabidhi hundi ya shilingi milioni 100 kwa ajili ya ukarabati na kuwasaidia wajasiriamali wenye mitaji midogo katika soko la Samunge lililopo kata ya mjini kati mkoani Arusha.


Akikabidhi hundi hiyo leo jijini Arusha katika soko la Samunge ,Nabii Mkuu amesema kuwa amewiwa kufanya hivyo baada ya kupata barua aliyoandikiwa ya kuhitaji msaada kwa ajili ya kukarabati na kusaidia wajasiriamali wenye mitaji midogo katika soko hilo ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Nabii Mkuu akimkabidhi hundi hiyo mbunge wa Jimbo la Arusha mjini pamoja na muwakilishi wa Mkuu wa wilaya ya Arusha mjini


Amesema kuwa kiasi cha shilingi milioni 80 watagawiwa mtaji wajasiriamali wenye mitaji midogo na huku kiasi kilichobaki cha milioni 20 kikitumika kwa ajili ya kukaratabati soko hilo.

“Mimi huu msaada ninatoa sitafuti waumini sipo hapa kumbadilisha mtu dini nipo hapa kuwasaidia wananchi katika kuondokana na matatizo mbalimbali na asanteni sana kwa mabango na picha haya ni mahaba makubwa sana na asanteni kwa heshima yenu ya kunipa kuwa mlezi wa soko ila mniwie radhi tutakuwa tunashirikiana popote mnapohitaji msaada ila swala la kuwa mlezi sitaweza maana nina majukumu mengi sana”, amesema Nabii.
Mbunge wa Arusha mjini Mrisho Gambo akiongea na wafanyabiashara wa soko la Samunge

Amesema kinachomsukuma kusaidia jamii ni Mungu kwani awali alipoitwa kutumikia Mungu alipewa maono ya kueneza injili ya kinabii na aliifanya lakini Kwa Sasa Mungu alimwambia afanye injili kwa matendo na ndio maana ameanza kueneza matendo kama Moja ya kauli mbiu yake inavyosema maneno machache kazi kubwa zaidi.


Aidha amewataka Viongozi wa dini kutochukua sadaka tu wakati umefika wa kuanza kurudisha kile wanachokipata kwa wananchi ,ni wakati sasa kurejesha fadhila kwa jamii wawasaidie maana watu wanateseka ,hivyo ni vyema wakajitoa na kujitahidi kuwasaidia wenye uhitaji.


“Msaada huu nilioutoa ni baada ya kupokea barua yenu ya kuomba msaada na nimekuja kuwaunga mkono na kila mmoja anapaswa kutambua kuwa tunaposaidia jamii tutakuwa tumemsaidia pia Rais Samia Suluhu Hassan katika suala la maendeleo ,unajua serikali inasaidia wananchi wake lakini haiwezi kuwafikia wote hivyo ni vyema watu kama sisi tujifunze kujitoa na kuwasaidia wenye uhitaji. “amesema.


Naye Mbunge wa Arusha mjini,Mrisho Gambo amesema kuwa,kazi ya viongozi wa serikali ni kuwaheshimu viongozi wote wa dini na kuwapa heshima yao pamoja na kuheshimu kipawa walichopatiwa ,aliongeza kuwa Mungu tunaemuabudu ni mmoja sema majina tu ndio yanatofautiana hivyo ni vyema kila mmoja akaheshimu imani ya mwenzake.
Share:

MLOGANZILA YAANZA KUPOKEA WAGONJWA WANAOHITAJI HUDUMA TIBA YA PUTO (INTRAGASTRICK BALLON) KUTOKA NJE


Naibu Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila Dkt. Julieth Magandi wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu kambi maalumu ya huduma tiba ya kuweka puto maalum (intragastic ballon) kwenye tumbo la chakula inayoendelea hospitalini hapo ambayo inaendeshwa na wataalamu wazalendo wa MNH-Mloganzila. Mjumbe wa kamati ya kitaifa ya kuratibu utalii tiba (medical tourism), Bw. Abdulmarik Mollel akielezea mipango ya kamati juu ya kutangaza huduma ya puto ndani na nje ya Nchi. 

Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Dkt. Faraja Chinga akieleze namna jopo la wataalamu linavyo shirikiana wakati wa kumuhudumia mtu anayehitaji kuwekewa puto. 

Daktari Bingwa wa Upasuaji na Mtaalamu wa Endoskopia MNH-Mloganzila Dkt. Eric Muhumba akielezea namna mwitikio wa watu wanaokuja kupata huduma kutoka ndani na nje ya nchi ulivyokuwa mkubwa. 

Kaimu Mkuu wa Huduma za Uuguzi na Ukunga Sis. Zuhura Mawona akielezea namna wauguzi walivyojipanga kuwahudumia wagonjwa kwanzia wanapofika hadi wanapomaliza kupatiwa huduma. 

Daktari Bingwa wa Upasuaji na Mtaalamu wa Endoskopia MNH-Mloganzila Dkt. Edwin Muhondezi akizungumza na waandishi wa habari namna zoezi la uwekaji wa puto linavyoendelea. 

Daktari Bingwa wa Upasuaji Mfumo wa Chakula MNH-Mloganzila Dkt. Richard Mliwa akizunguma na waandhishi wa habari kuhusu kambi hiyo. 

Daktari Bingwa wa Usingizi na Ganzi MNH-Mloganzila Dkt. Fillip Muhochi akizungumza na waandishi wa hapari wakati wa uzinduzi wa kambi hiyo. 

*************** 

Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila imeanza kupokea wagonjwa mbalimbali kutoka nje ya nchi, wanaofuata huduma za kibingwa ikiwemo huduma tiba ya kuweka puto kwenye tumbo la chakula ili kusaidia watu wenye uzito mkubwa kupungua. 

Hayo yameelezwa na Naibu Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila Dkt. Julieth Magandi wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu kambi maalumu ya huduma tiba ya kuweka puto maalum (intragastic ballon) kwenye tumbo la chakula inayoendelea katika hospitali hiyo ambayo inaendeshwa na wataalamu wazalendo wa MNH-Mloganzila. 

Dkt. Magandi ameeleza kuwa uwekezaji mkubwa uliofanywa na serikali pamoja na maboresho makubwa yaliyofanywa na uongozi wa hospitali ikiwemo uanzishwaji wa huduma za kibingwa umevutia raia wa kigeni kufika Mloganzila kufuata huduma. 

“Tumeanzisha huduma za kibingwa, lakini pia tumeboresha huduma kwa wateja. Kuna dawati la huduma kwa wateja ambalo linafanya kazi saa 24 ili kuhakikisha wateja wetu wanahudumiwa vizuri, jambo hili limevutia raia wa nchi mbalimbali ikiwemo Kenya, Afrika Kusini na Malawi kufuata huduma Mloganzila” ameeleza Dkt. Magandi 

Ameeleza kuwa mteja anapofika Mloganzila anaonwa na jopo la wataalamu kwa pamoja (Multdisplinary approch) ambalo linaundwa na madaktari bingwa wa magonjwa ya ndani, wa usingizi na ganzi, pamoja na wa pasuaji, wataalamu wa maabara na wauguzi ili kupunguza mzunguko na kufanya utaratibu wa matibabu ukamilike ndani ya muda mfupi. 

Dkt. Magandi ametaja huduma za kibingwa ambazo zinapatikana Mloganzila hadi sasa kuwa ni pamoja na kuvunja mawe kwenye figo kwa kutumia mawimbi mshtuko, upasuaji wa kubadilisha nyonga, pamoja na huduma tiba ya kuweka puto kwenye tumbo la chakula ili kusaidia kudhibiti uzito. 

Mjumbe wa kamati ya kitaifa ya kuratibu utalii tiba (medical tourism), Bw. Abdulmarik Mollel ameeleza kuwa kamati imejiridhisha na ubora wa huduma zinazotolewa Mloganzila na kwamba tayari imeanza kutengeneza utaratibu wa kutangaza fursa hiyo ya matibabu nje ya nchi. 

Naye Daktari Bingwa wa Upasuaji na Mtaalamu wa Endoskopia MNH-Mloganzila Dkt. Eric Muhumba amesema kuwa toka huduma hiyo ianzishwe mwezi uliopita tayari wagonjwa 20 wamenufaika na kwamba hadi mwisho wa kambi wanategemea idadi itafikia watu 30. 

Ameeleza kuwa huduma tiba ya kuweka puto maalumu kwenye tumbo la chakula kwa watu wenye uzito uliopitiliza (intragastic ballon) inasaidia kupunguza nafasi kwenye tumbo la chakula hivyo kusababisha mtu kula kidogo jambo ambalo litapelekea kupungua uzito.
Share:

SERIKALI YAVITAKA VYUO VYA MAFUNZO KWA WALEZI WA WATOTO KUWA NA MPANGO WA PAMOJA

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Wakili Amon Mpanju,akizungumza wakati akifungua kikao kazi cha Wakuu wa Vyuo vinavyotoa mafunzo ya Malezi wa Watoto nchini kilichofanyika leo Januari 19,2023 jijini Dodoma. 


Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Wakili Amon Mpanju,wakati akifungua kikao kazi cha Wakuu wa Vyuo vinavyotoa mafunzo ya Malezi wa Watoto nchini kilichofanyika leo Januari 19,2023 jijini Dodoma. 


Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum,Dkt. Nandera Mhando,akizungumza wakati wa kikao kazi cha Wakuu wa Vyuo vinavyotoa mafunzo ya Malezi wa Watoto nchini kilichofanyika leo Januari 19,2023 jijini Dodoma. 


Mkurugenzi Msaidizi anayesimamia huduma za Jamii Ofisi ya Raisi-TAMISEMI Bi Amina Mfaki,akizungumza wakati wa kikao kazi cha Wakuu wa Vyuo vinavyotoa mafunzo ya Malezi wa Watoto nchini kilichofanyika leo Januari 19,2023 jijini Dodoma. 


Kaimu Mkurugenzi Idara ya watoto kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Bi Asha Shami,akizungumza wakati wa kikao kazi cha Wakuu wa Vyuo vinavyotoa mafunzo ya Malezi wa Watoto nchini kilichofanyika leo Januari 19,2023 jijini Dodoma. 

Mkurungenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la Karibu Tanzania Organization (KTO) Bw.Majid Mjengwa,akielezea taasisi hiyo ilivyoanza mpango huo wakati wa kikao kazi cha Wakuu wa Vyuo vinavyotoa mafunzo ya Malezi wa Watoto nchini kilichofanyika leo Januari 19,2023 jijini Dodoma. 


Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Wananachi Karumo Bi.Osmunda Kilasi,akizungumzia umuhimu wa mpango huo wakati wa kikao kazi cha Wakuu wa Vyuo vinavyotoa mafunzo ya Malezi wa Watoto nchini kilichofanyika leo Januari 19,2023 jijini Dodoma 

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Wakili Amon Mpanju,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua kikao kazi cha Wakuu wa Vyuo vinavyotoa mafunzo ya Malezi wa Watoto nchini kilichofanyika leo Januari 19,2023 jijini Dodoma. 

....................................... 

Na Alex Sonna-DODOMA 

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Wakili Amon Mpanju amewataka watoa Mafunzo ya Walezi wa Watoto nchini kuwa na Mpango kazi wa pamoja utakaotumika kuwafundishia walezi wa Watoto. 

Hayo ameyasema leo Januari 19,2023 jijini Dodoma wakati akifungua kikao kazi cha Wakuu wa Vyuo vinavyotoa mafunzo hayo ya Malezi. 


“Kuna haja ya kuja na Mtaala wa pamoja ili kutatua changamoto ya Malezi na Makuzi ya Awali kwa watoto. Iwepo pia bodi ya usimamazi na Mwongozo utakaosaidia kuratibu eneo hili ili wahitimu wawe na Ujuzi utakaosaidia Watoto wetu”Alisema Wakili Mpanju. 

Wakili Mpanju amewasisitiza Wadau hao juu ya umuhimu wa kuwekeza kwenye malezi na makuzi ya awali ya Watoto Nchini Ili kujenga watu wenye maadili na nidhamu kwa Taifa. 

Mpango wa ufundishaji wa mtaala mmoja uliasisiwa na Shirika lisilo la kiserikali la Karibu Tanzania Organization (KTO) ambao walianza mafunzo kwa chuo kimoja Kisha wakapeleka kwa vyuo 10 kati ya 54 vya Maendeleo ya Jamii. 

“Tusipowekeza vya kutosha tutapata majanga ,Mnyonyoko wa Maadili utaendelea na hatimaye Taifa litapotea.”Ameongeza Mpanju. 

Kwa upande wake Kamishna wa Ustawi wa Jamii,Dkt. Nandera Mhando amesema lengo ni kuweza kufikia yale yaliyokusudiwa kupatikana kwenye Vyuo hivyo vinavyotoa Mafunzo kwa walezi Wa Watoto. 

“Kwa pamoja tuweke igezo vya pamoja ikiwemo Mitaala na mitihani ili tuweze kupata Wahitimu wanaokidhi na hatimaye kufanikisha nia ya Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii”amesema Dk.Mhando 

Aidha Dk.Mhando amesema kuwa msingi uliopandwa na KTO unapaswa kuendelezwa ili kuzaa matunda yatakayosambaa nchi nzima badala ya kuwa walalamikaji kuhusu kuharibiwa kwa maadili ya watoto. 

Naye Mkurungenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la Karibu Tanzania Organization (KTO) Bw.Majid Mjengwa amesema kuwa taasisi hiyo ilianza mpango huo mapema kwa kushirikiana na baadhi ya vyuo ndipo wakabaini kwamba kuna ulazima wa kupeleka elimu hiyo Kwa vyuo vyote. 


Mjengwa amesema mwelekeo wa sasa ni kuona mtoto wa Kitanzania analelewa na kufundishwa misingi impasayo mwanadamu kuliko ilivyo sasa ambapo vituo ni vingi lakini kila mmoja anatoa mafunzo ya mwelekeo wake. 

Hata hivyo Bw. Mjengwa amesema kuwa mitaala inayotazamwa ni ya vituo vya watoto wadogo (Day care) ambako ndiko uliko msingi wa Mkuu wa ujifunzaji kwa mwanafunzi. 

"Tunashukuru Serikali imekubali mpango huu na kuahidi kupeleka vyuo vyote 54, hili ni jambo jema sana kwamba tunakwenda kuzalisha wataalamu wazuri wa malezi ya watoto Wetu," amesema Bw. Mjengwa. 


Mkurugenzi Msaidizi anayesimamia huduma za Jamii Ofisi ya Raisi-TAMISEMI Bi Amina Mfaki amesema Serikali inatoa kipaumbele kwa malezi na Makuzi ya Awali kwa watoto Nchini ili kujenga Taifa la Wananchi Wazalendo. 

“Mnaowandaa Walezi wa Watoto mna jukumu kubwa la kuhakikisha Mafunzo yanayotolewa Vyuoni yanaweza kuwakuza watoto na Vipaji vyao na Mwisho wa siku tutapata vijana wabunifu watakaoleta Maendeleo katika Taifa letu”amesema Bi.Mfaki 

Awali Kaimu Mkurugenzi Idara ya watoto kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Bi Asha Shami amesisitiza juu ya Maudhui ya kuzingatia katika utoaji wa Elimu ya Awali kwa Watoto. 

“Tunategemea mtawalinda watoto kwa kuzingatia maudhui sahihi katika ufundishaji maana kumekua na changamoto nyingi za kimaadili zitokanazo na vitu ambavyo watoto wanajifunza mashuleni na Majumbani,Hivyo Maudhui yenye kuzingatia Mila na Tamaduni zetu ni muhimu.”Alisema Bi Asha . 


Nao Wakuu wa Vyuo na Wadau wanaotoa Mafunzo Kwa Walezi wa Watoto Nchini wameiomba Serikali kuhakikisha Mchakato wa kupata Mtaala wa Pamoja Nchini unakamilika Haraka ili waweze kuuanza kuutumia Katika Mafunzo yao .
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger