Thursday, 12 January 2023

KISHAPU WAADHIMISHA MIAKA 59 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR KWA KUPANDA MITI

Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog Kishapu
Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga leo January 12,2023 imeadhimisha miaka 59 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar kwa kupanda miti pembezoni mwa eneo la Bwawa la maji kijiji cha Kishapu, ambapo zaidi ya miche 1000 ya miti imepandwa.




Katika zoezi hilo liliongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude ameambatana na Viongozi mbalimbali wa Serikali akiwepo katibu Tawala wa Wilaya, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkurugenzi Mtendaji, Wakuu wa Idara na Taasisi mbalimbali Wilayani Kishapu.


Akizungumza baada ya zoezi la upandaji miti amewashukuru wote kwa waliojitokeza katika zoezi hilo.


"Ninawashukuru sana Ndugu zangu wote mliojitokeza katika zoezi hili la upandaji wa miti lakini nitoe wito Wananchi wote kuzitumia vizuri mvua zinazoendelea kunyesha kupanda miti hasusani miti ya matunda lakini pia miti hii inayotunza maji tuendelee kupanda katika Vyanzo vyote vya maji", amesema Mkude.



Amesisitiza kuwa jitihada kubwa za Serikali ambazo zinafanywa kulinda mazingira ziungwe mkono na wananchi kwani ni jukumu la kila mmoja.

Aidha Mkuu wa Wilaya amewataka Wananchi wote wanaozamia katika eneo hilo kwaajili ya kufanya kilimo na makazi kupisha mara moja kuepusha uchafuzi wa mazingira.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Emmanuel Johnson, amesema kuwa kwa ujumla maeneo ya Wilaya ya Kishapu yana mvua kidogo, katika kilimo wanategemea sana kilimo cha umwagiliaji.

"Kwa ujumla kama tunavyofahamu Wilaya ya Kishapu ni kame ina mvua kidogo kwa hiyo tunategemea sana kilimo cha umwagiliaji kwa kutumia mabwawa na mkakati uliopo ni kuhakikisha kuna mabwawa ya kutosha kila sehemu na jitihada ambazo zinafanyika kwa sasa ni kufufua mabwawa yaliyoharibika, tumefufua Bwawa la Kiloleli, Mihama na Beledi", amesema.

"Kwa Mwaka huu Halmashauri imetenga Fedha kwa ajili ya kufufua mabwawa zaidi kauli mbiu yetu ni kuhakikisha Wilaya yetu inakuwa na mabwawa zaidi kwaajili ya kilimo na ufugaji", ameongeza.




Naye Diwani wa kata ya Kishapu Mheshimiwa Joel Charles Ndettoson ameeleza kuwa Bwawa hilo linahudumia zaidi ya kata Nane mpaka na Wilaya jirani ya Maswa wote wanatumia Bwawa hilo

"Bwawa hili linasaidia zaidi ya kata nane, Bwawa hili mbali na wanakijiji wanaotumia Kuna Shughuli za kimaendeleo zinazotumika eneo hili tumeona leo tupande miti zaidi ya 1000 pia tumeweka mikakati ya kusimamia Bwana hili ili liendelee kutusaidia", amesema.




Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kishapu Bw Elikana Masanja amefurahishwa na ujio wa Mkuu wa Wilaya pamoja na msafara wake kwa uamzi wa kupanda miti katika eneo hilo.

"Nafurahia sana kwa ujio wa Mkuu wa Wilaya katika Bwawa hili na kuamua kupanda miti katika eneo hilo kwa Sababu itasaidia sana katika utunzaji wa Vyanzo vya maji na Bwawa hili litarejea katika thamani yake", amesema.
Share:

Wimbo Mpyaaa : SISHA - AMSHA POPO.......NGOMA TAMU KINOMA


Msanii Sisha
Msanii Sisha kutoka ShyTown 'Shinyanga! ameachia wimbo Mpya unaitwa Amsha Popo.. Ni Ngoma nzuri sana.. Isikilize hapa mtu wangu utaipendaa!!

Share:

VIONGOZI WA KAMATI YA UTEKEKEZAJI JUMUIYA YA WAZAZI CCM DAR ES SALAAM WAPEWA SEMINA


Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Abbas Mtemvu akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya Viongozi wa Kamati ya utekekezaji Chama Cha Mapinduzi yaliyoanza leo katika hotel ya Star Breeze Kigamboni, jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Abbas Mtemvu akifungua mafunzo ya siku tatu ya Viongozi wa Kamati ya utekekezaji Chama Cha Mapinduzi yaliyoanza leo katika hotel ya Star Breeze Kigamboni, jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Abbas Mtemvu akisisitiza jambo wakati akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya Viongozi wa Kamati ya utekekezaji Chama Cha Mapinduzi yaliyoanza leo katika hotel ya Star Breeze Kigamboni, jijini Dar es Salaam.Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Abbas Mtemvu akiwasili na kupokelea na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salam, Bi.Khadija Ally katika ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya Viongozi wa Kamati ya utekekezaji Chama Cha Mapinduzi yaliyoanza leo katika hotel ya Star Breeze Kigamboni, jijini Dar es Salaam. Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Bw.Adam Ngallawa akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya Viongozi wa Kamati ya utekekezaji Chama Cha Mapinduzi yaliyoanza leo katika hotel ya Star Breeze Kigamboni, jijini Dar es Salaam.Katibu wa Organization ya Wazazi CCM Taifa Bw.Saidi King'eng'ena akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya Viongozi wa Kamati ya utekekezaji Chama Cha Mapinduzi yaliyoanza leo katika hotel ya Star Breeze Kigamboni, jijini Dar es Salaam.Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salam, Bi.Khadija Ally akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya Viongozi wa Kamati ya utekekezaji Chama Cha Mapinduzi yaliyoanza leo katika hotel ya Star Breeze Kigamboni, jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Abbas Mtemvu akipata picha ya pamoja na Viongozi wa kamati ya Utekelezaji Chama cha Mapinduzi (CCM) katika ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya Viongozi hao yaliyoanza leo katika hotel ya Star Breeze Kigamboni, jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Abbas Mtemvu akipata picha ya pamoja na watoa Mafunzo katika ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya Viongozi wa Kamati ya utekekezaji Chama Cha Mapinduzi yaliyoanza leo katika hotel ya Star Breeze Kigamboni, jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

***********************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Uongozi wa Kamati ya Utekelezaji Chama cha Mapinduzi (CCM) wametakiwa kuendeleza mshikamano na ushirikiano ili kuhakikisha kazi zinatendeka kupitia Ilani ya CCM ili wanachama na wananchi kwa ujumla waendelee kuwa na imani na Chama hicho.

Ameyasema hayo leo Januari 12,2023 Jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Abbas Mtemvu wakati akifungua Semina ya Siku tatu ya Uongozi wa Kamati ya Utekelezaji Chama cha Mapinduzi (CCM) iliyoandaliwa na Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dar es Salaam.

Amesema kuna umuhimu wa viongozi wa chama hicho kuhakikisha kamati ya Siasa kutoa hamasa kwa wanachama na wananchi kwa ujumla ili kuhakikisha Chama hicho kinafanya vizuri katika chaguzi zijazo.

Aidha amewataka viongozi hao kushuka kwenye kata, wilaya na matawi kutoa elimu kuhusu masuala ya chama hasa Ilani ya Chama na utekelezaji wake katika maeneo mbalimbali kwenye mkoa wa Dar es Salaam.

Amesema kuna changamoto ya upatikanaji wa kadi za uanachama ingawa wanachama wengi wanaingia kwenye chama hicho hivyo ameshalifikisha kwenye uongozi wa juu na linashughulikiwa ikiwezekana uwepo wa mfumo wa kielektroniki.

"Wanachama wengi sasa wanahitaji kuja CCM lakini upatikanaji wa kadi zetu ni tatizo kwahiyo nitaliwasilisha kwa kinamna yake kwa mwenyekiti suala hili la kadi walipe kipaumbele ikiwezekana ziweze kupatikana kwa wakati". Amesema

Kwa upande wake Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Bw.Adam Ngallawa amewasihi kamati ya utekelezaji wa chama cha Mapinduzi kuhakikisha wanatumia michango kutekeleza miradi mbalimbali ili Juhudi za Jumuiya ya Wazazi zionekane na wanachama kuwa na imani na Chama hicho.

Amewataka viongozi wa kamati ya Utekelezaji kuwa kiungo kwa wazazi wote wa Mkoa wa Dar es Salaam na kwa wananchi wa mkoa huo kwani ndani yenu wamo vijana, wanawake,hivyo wametakiwa kuhakikisha Chama kinakuwa imara.

Nae Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salam, Bi.Khadija Ally amesema watahakikisha wanahamasiisha ili ushindi wa kishindo unapatikana katika mkoa wa Dar es Salaam kwani wamejipanga kikamilifu kufanya vizuri kwenye kuelekea chaguzi zijazo.

Amesema kwa kuwa amechaguliwa kwa kuaminiwa hatahikikisha anatoa ushirikiano wa kutosha katika utekelezaji wa chama hicho na ndo maana wakaona kuna umuhimu wa kupata mafunzo ya uongozi ili kila mmoja ajue mipaka yake.

Share:

MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU MoCU AJIUA KISA KUKATALIWA NA MREMBO ALIYEMLIPIA KODI NA KUMNUNULIA IPHONE

 Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU), Gunze Luhangija aliyekuwa akisomea Shahada ya Menejimenti ya Ushirika na Uhasibu (BCMA), amekutwa amejinyonga chanzo kikisemekana ni kutokana na msongo wa mawazo uliosababishwa na kukataliwa na mpenzi wake.

Inadaiwa alishawahi kujaribu kujiua kwa kunywa sumu Januari 4 mwaka huu lakini aliokolewa baada ya kukataliwa ilihali ikieleza kuwa alimgharamikia mpenzi wake huyo ikiwemo kumpangishia nyumba.

Baadhi ya wanafunzi kutoka chuoni hapo wamedai marehemu alikuwa na ugomvi na mpenzi wake siku chache baada ya kumnunulia simu janja aina ya iPhone 14 iliyopelekea kuwa katika hali ya msongo wa mawazo.

“Siku ya Boxing Day alimnunulia mpenzi wake iPhone 14 na baada ya siku chache demu (mpenzi) alimkataa kwamba kapata mtu mwingine [..] dogo kajitundika,” mmoja wa wanafunzi chuoni hapo.

Aidha, Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Yahya Mdogo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa jeshi linaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo cha kifo chake.


Via: Swahili Times


Share:

ATUPWA JELA MIAKA 30 KWA KUMBAKA BINTI WA KIDATO CHA PILI


Jacob Okafyulilo, mwenye umri wa miaka 38, Mbena na Mkazi wa Kijiji cha Itambo wilayani Wanging'ombe Mkoani Njombe, amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela na kuamriwa kulipa fidia ya shilingi milioni moja baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka binti wa kidato cha pili.

Kupitia taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi imeeleza kuwa hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mhomi J. E Januari 10, 2023 baada ya mahakama hiyo kujiridhisha pasi na shaka na ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri uliothibitisha kuwa, mtuhumiwa alitenda kosa la kumbaka binti wa miaka 16 wa kidato cha pili tarehe 10 Oktoba 2022.

Mwendesha mashtaka wa Serikali Kamwela, aliiomba mahakama itoe adhabu kali ili iwe fundisho kwa mtuhumiwa ambaye ni mjomba wa mhanga na wengine wenye mawazo ya kutenda uhalifu wa kikatili kama huo.
Share:

Wednesday, 11 January 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI JANUARI 12,2023














Share:

FANYA JAMBO HILI KUKABILIANA NA MIGOGORO YA ARDHI!

Hadi kufikia umri wangu wa miaka 47, nimekuja kuamini hakuna kitu kibaya kama migogoro ya ardhi, watu wengi wamepoteza mali zao kama mazao na mifugo kisa migogoro ya ardhi.

Jina langu ni Hussein kutokea Meru nchini Kenya, miaka kama minne iliyopita kuliibuka mgogoro mkubwa wa ardhi katika familia yetu, kuna ndugu walikuwa wanasema eneo letu ni la kwao kutokana waliachiwa kama urithi kutoka kwa Babu zao.

Walikuja na hati za kimila ambazo zilionyesha kweli eneo hilo walikabidhiwa mingi sana, lakini sisi tumeishi katika ardhi hiyo kwa miaka mingi, tumejengaa na kuanzisha familia zetu hapo na tumelima kwa miaka nenda rudi.

Hivyo walichokuwa anataka ni sisi kuhama na kuwapisha katika eneo hilo ambalo wanadai ni lao, tulipouliza kuhusu nyumba na mazao yetu walisema tuwaachie maana vipo juu ya ardhi ambayo ni ya kwao!.

Sisi tukuweza kukubali jambo hilo hata kidogo, ndipo mgogoro mkubwa ulipozuka, tuliwaambia kama ni kweli wanaona wana haki na ardhi hiyo, basi waende kufungua kesi mahakamni, sheria ndio itakayosema ukweli.

Basi waliamua kufanya hivyo, waliweka wanasheria wao na kulipa fedha nyingi za kesi, ama kwa hakika walikuwa na dhamira kubwa ya kupora ardhi yetu, binafsi hadi leo hatujui sababu ni nini hasa lakini huku duniani kuna watu wanachuki zao na wengine bila sababu.

Wakati kesi imeanza kusikilizwa, ndugu yetu mmoja wa mbali alifika nyumbani baada ya kupata habari kuhusu sakata hilo, alituaminia kama kesi tayari imefika mahakamani, tunaweza kufanya jambo moja tu la ushindi!.

Nalo ni kuwasiliana na AfricanDoctors ili waweza kutufanyia dawa ya kuweza kushinda shauri hilo ambalo kwa hakika ulikuwa ni mtihani mkubwa kwetu maana hatukuwa na fedha zozote zile mikono mwetu.

Basi baada ya kuwaliana na AfricanDoctors waliweza kutupatia huduma hiyo ya kushinda kesi mahakamani na kutuhakikishia jambo hilo litamalizika vizuri tu upande wetu, hivyo tuendelee kuwa wavumilivu kuhusu sakata hilo.

Nashukuru baada ya miezi miwili mbele, hatimaye mahakama ilitoa uamuzi wake na kusema madai yao ni batili maana hakuna ushahidi wa kisheria unaothibisha ni kweli walipewa ardhi hiyo na Babu zao wa kale kama wanavyosema. Hivyo sisi tuendelee kukalia ardhi yetu bila wasiwasi wowote ule.

Wasiliana na AfricanDoctors kwa namba +254719153099

Mwisho.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger