Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga wakifurahia zawadi ya Mbuzi baada ya kuibuka washindi kwa kuichapa Timu ya Watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga bao 3-2
Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Sherehe za kumaliza mwaka 2022 na kukaribisha mwaka 2023 katika mkoa wa Shinyanga zimependezeshwa na bonanza la mpira wa miguu lililoshirikisha timu nne ndani ya Manispaa ya Shinyanga ambapo Timu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga imewachapa Watumishi wa Manispaa ya Shinyanga bao 3-2.
Bonanza hilo la michezo lililoongozwa na Kauli Mbiu 'Kataa Uhalifu toa taarifa, Shinyanga bila uhalifu inawezekana' limefanyika leo Jumamosi Desemba 31,2022 viwanja ya shule ya msingi Balina kata ya Ndembezi limendaliwa na Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na MC Mzungu Mweusi ambapo Mgeni rasmi alikuwa Kamanda wa jeshi la pollisi mkoa wa Shinyanga, ACP Janeth Magomi.
Bonanza hilo lililoambatana na michezo ya sarakasi limeshirikisha Timu nne za mpira wa miguu ambazo ni Waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga, Watumishi wa manispaa ya Shinyanga, Bodaboda wa kata ya Ndembezi na Wauzaji wa miti ya ujenzi (Milunda FC).
Akizungumza wakati wa Bonanza hilo, Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga ,ACP Janeth Magomi amesema ,michezo ni afya na michezo inajenga mahusiano katika jamii.
Kamanda Magomi ametumia fursa hiyo kuwataka wananchi Mkoa wa Shinyanga kusherehekea sikukuu ya Mwaka Mpya 2023 kwa amani na utulivu huku akibainisha kuwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limejipanga kikamilifu kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo yote.
Katika mchezo wake Timu ya waandishi wa habari iliweza kushinda na kuwanyakua mbuzi mnyama kwa kupata penati 3 dhidi ya 2 za wapinzani wao ,Timu ya watumishi Manispaa ya Shinyanga huku waendesha bodaboda kata ya Ndembezi wakiichapa Milunda FC bao 7-6 kwa mikwaju ya penalti.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi
MC Mzungu Mweusi (Amos John) akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akikabidhi zawadi ya Mbuzi kwa Timu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga
Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga wakifurahia zawadi ya Mbuzi baada ya kuibuka washindi kwa kuichapa Timu ya Watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga bao 3-2
Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga wakifurahia zawadi ya Mbuzi baada ya kuibuka washindi kwa kuichapa Timu ya Watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga bao 3-2
Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga wakifurahia zawadi ya Mbuzi baada ya kuibuka washindi kwa kuichapa Timu ya Watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga bao 3-2
Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga wakifurahia zawadi ya Mbuzi baada ya kuibuka washindi kwa kuichapa Timu ya Watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga bao 3-2
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akikabidhi zawadi ya Mbuzi kwa Timu ya Waendesha Bodaboda
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akikabidhi zawadi ya Mbuzi kwa Timu ya Waendesha Bodaboda
Timu ya Waendesha Bodaboda wakifurahia zawadi ya Mbuzi
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akikabidhi zawadi ya Juisi kwa Timu ya Milunda FC
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akikabidhi zawadi ya Juisi na Soda kwa timu ya Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga