Friday, 4 November 2022

MASHINDANO YA TAIFA YA MPIRA WA KIKAPU 'CRDB BANK TAIFA CUP 2022' YAFUNGULIWA RASMI JIJINI TANGA


Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Omary Mgumba (katikati) akifurahi jambo na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa (wanne kulia) wakati wa ufunguzi rasmi wa Mashindano ya taifa ya mpira wa kikapu 2022 (CRDB Bank Taifa Cup), yaliyoanza leo kwenye uwanja wa Bandari jijini Tanga na kilele chake kitakuwa Novemba 12, 2022.

Mashindano haya yanaendelea kwa msimu wa tatu mfululizo ikiwa ni sehemu ya jitihada za Benki ya CRDB kuwawezesha vijana wa Kitanzania kupitia michezo, ambapo mshindi wa kwanza kwa timu za wanawake na wanaume katika mashindano haya ataondoka na kitita cha Shilingi Milioni 10 kila mmoja na washindi wa pili wataondoka na kitita cha Shilingi Milioni 5.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Omary Mgumba akizngumza wakati wa ufunguzi rasmi wa Mashindano ya taifa ya mpira wa kikapu 2022 (CRDB Bank Taifa Cup), yaliyoanza leo kwenye uwanja wa Bandari jijini Tanga na kilele chake kitakuwa Novemba 12, 2022.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa akizngumza wakati wa ufunguzi rasmi wa Mashindano ya taifa ya mpira wa kikapu 2022 (CRDB Bank Taifa Cup), yaliyoanza leo kwenye uwanja wa Bandari jijini Tanga na kilele chake kitakuwa Novemba 12, 2022.
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Kaskazini, Chiku Issa akizngumza wakati wa ufunguzi rasmi wa Mashindano ya taifa ya mpira wa kikapu 2022 (CRDB Bank Taifa Cup), yaliyoanza leo kwenye uwanja wa Bandari jijini Tanga na kilele chake kitakuwa Novemba 12, 2022.
Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu nchini (TBF), Rwehabura Barongo akizngumza wakati wa ufunguzi rasmi wa Mashindano ya taifa ya mpira wa kikapu 2022 (CRDB Bank Taifa Cup), yaliyoanza leo kwenye uwanja wa Bandari jijini Tanga na kilele chake kitakuwa Novemba 12, 2022.
































Share:

RUAHA YAHARIBIWA KWA WANANCHI KWA KUVAMIA VYANZO VYA MAJI

Mragibishi na Mdau wa Mazingira Seleman Msindi akizungumza mara baada kufika katika Mto Ruaha Mkuu eneo Ngiliama- Madibira mkoani Mbeya

Sehemu ya mawe hii kwa kipindi hiki cha kiangazi kinakuwa maji lakini hakuna hata tone la maji Bwawa ambalo sehemu ya weusi ni wanyama aina viboko. Bwawa lenye wanyama aina tembo wakiwa wanakunywa maji baada kutoka safari ya mbali kufuata maji.

*************************

*Shughuli za Kilimo na Ufugaji ndio matokeo ya mto Ruaha kukauka

Na Chalila Kibuda,Michuzi Tv

Kituo cha Wanahabari ,Watetezi wa Rasilimali na Taarifa (MECIRA) kimesema kuwa athari za Hifadhi ya Ruaha ni matokeo ya shughuli za kibinadamu kuingia katika hifadhi hiyo.

Adhari hiyo imesababishwa na bonde la usangu -Ihefu wananchi kuvamia hifadhi kuendesha kilimo na ufugaji na kuathiri mto Ruaha kushindwa kutirisha maji na madhara yake yanaonekana kwa wanyama kutegemea mabwawa katika mto huo.

Kituo cha Wanahabari ,Watetezi wa Rasilimali na Taarifa (MECIRA)kilitembea sehemu moja ya mto Ruaha Ngeliama iliyopo Kata Madibira ya Madibira wilayani Mbarali mkoani Mbeya (Bonde la Usangu) na kuona namna mto Ruaha ukiwa umekauka kutokana na eneo kubwa ya uhifadhi kuingiliwa na shughuli za kilimo ,Ufugaji pamoja na uvuvi na kusababisha maji kushindwa kufika katika mto huo. Akizungumza katika hifadhi ya Ruaha Mragibishi na Mdau wa Mazingira Msanii Selaman Msinde 'Afande Sele' amesema Mto Ruaha na hifadhi ya Ruaha sasa inakabiliwa na ukame kutokana vyanzo vya maji kukauka katika mto huo ambapo kumesabishwa na mikono ya wanadamu.

Msindi amesema kuwa katika maoneo waliyopita kumekuwa na mashamba makubwa yaliyoko katika hifadhi huku wakulima wakiona ni haki yao kuendesha kilimo ,ufugaji pamoja na ukataji miti.

Amesema kuwa baada ya kupeleleza katika vijiji vilivyopo ndani ya hifadhi ambapo kuna vijiji havijihusishi na kilimo wa ufugaji hapo ni kujiuza wanafanya nini wakati kuna ujangili ambapo ni nani anafanya hivyo hayo maswali yote changamoto kwenye jamii.

Msindi amesema kuna ripoti mbalimbali katika vijiji vilivyopo ndani ya hifadhi watu wanakamatwa na silaha za kivita lakini vizingizio vilivyopo wanasema wanafanya kilimo.

Amesema kuwa Mto Ruaha na Mbuga ya Uhifadhi inatakiwa jamii na watunga sera kuangaliwa kwa ukaribu sana na kupata utashi wa kisiasa katika kukabilina.

Aidha amesema wanyama wanatembea umbali mrefu kutafuta maji ambapo kwa sasa yamebaki mabwawa hivyo mabwawa yakikauka wanyama wataenda wapi.

Amesema kwa sasa kuna changamoto ya nishati ya umeme ambayo imesababishwa na maji kupungua kwa kiwango kikubwa kwenye mto Ruaha.

Afande Sele anasema Mto Ruaha unapeleka maji katika vituo vya kuzalisha Umeme ambavyo ni Kidatu ,Mtera pamoja na Kihansi lakini kwa sasa uzalishaji wake unapungua kila siku.

Amesema kuwa uchumi wa unatagemea nishati ya umeme kwa kwa watu zaidi milioni 61 kwa mujibu wa sensa ya mwaka huu hivyo kunahitaji kulinda mto huo pamoja na Ikolojia ya Uhifadhi ya Mbuga ya Ruaha na Selous.

Msindi amesema mto Ruaha kwa sasa hatarini kukauka kwa kipindi kifupi baada ya Masika kutokana sehemu vyanzo vidogo vidogo kushindwa kuingiza maji katika mto mkuu Ruaha.

Amesma Kwa mujibu wa Ripoti mbalimbali zinaeleza mto Ruaha ndio sehemu kubwa ya uzalishaji wa Nishati Umeme huku kuwa chanzo kikubwa katika cha maji kwenye Bwawa la Nyerere na kufuatia utunzaji wa Ikolojia katika hifadhi Selous na Ruaha.

Hifadhi ya Ruaha na Selous na ndio hifadhi kubwa zenye makundi ya wanyama wanaotembea kwa pamoja hivyo kukosekana na kwa maji ni hatari wanyama hao wakafa au kuondoka kutokana na kukosekana kwa maji.
Share:

MAHAFALI YA 16 CHUO CHA UANDISHI WA HABARI NA UTANGAZAJI FANIKIWA YAFANYIKA ARUSHA...WAHITIMU WAONESHWA FURSA MTANDAONI

Mkurugenzi wa shirika la MAIPAC Bw Musa Juma akitoa hotuba. 
Mkuu wa Chuo cha waandishi wa habari na Utangazaji Fanikiwa Bw Andrea Ngobole akitoa hotuba kwa wahitimu.
katika picha ni wahitimu wa Chuo Cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Fanikiwa arusha.
Wahitimu Wa Chuo Cha Uandishi wa Habari na Utangazazji Fanikiwa Ausha. Picha na Marystela Bryson.

NA ONESMO ELIA MBISE-ARUSHA.

Waandishi wa habari nchini wametakiwa kujiajiri wao wenyewe katika sekta ya habari na utangazaji kwa kuanzisha vyombo mbalimbali vya mtandaoni kwa kuzingatia ukuaji wa teknolojia ili kuharakisha zoezi la kuipasha jamii habari kwa wepesi na haraka zaidi.


Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Media Aid for Indigenous Pastoralist Community (MAIPAC) na mjumbe wa bodi ya MISA-Tanzania Bw. Mussa Juma akizungumza katika mahafali ya 16 ya Chuo cha Uandishi wa Habari na Uangazaji Fanikiwa yaliyofanyika katika ukumbi wa PPS jijini Arusha.

Bw.  Musa ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo amesema kuwa ulimwengu wa sasa umekua, hasa katika eneo la sayansi na teknolojia hivyo wana habari wanapaswa kukimbia na ukuaji huo kwa kuanzisha vyombo vya habari vya mitandaoni ambavyo vitawasaidia wao kujiajiri kitaaluma.

Hata hvyo ameeleza kuwa waandishi wengi wanaweza kufungua "Blog, radio mtandao na Tv za Mitandaoni ambazo wanaweza kupeleka maudhui mbali mbali ya kihabari na kupitia vyombo hvyo watapatikana wawekezaji mbalimbali ambao wataweka matangazo ya biashara zao ili zionekane na watazamaji au pengine wasomaji.

Mbali na hayo amewataka wahitimu hao wa ngazi ya Stashahada kuzingatia maadili wawapo kazini lakini pia kuwa wabunifu katika kuandika habari za mazingira,kilimo,uchumi, na hata mabadiliko ya hali ya hewa ili kusaidia kuwaweka katika mazingira mazuri zaidi ya kihabari.

Naye mkuu wa chuo hicho Bwana Andrea Ngobole, amewataka wazazi wa wahitimu hao kuwaendeleza zaidi vijana hao katika chuo kikuu ili waendelee kupata elimu zaidi juu ya tasnia ya habari na sekta nyinginezo.


Aidha katika Mahafali Hayo wahitimu wapatao 40 wamehitimu mafunzo yao ya umahiri katika Tasnia ya habari na utangazaji ambapo pia wamedhamiria kwenda kuleta mabadiliko makubwa katika sekta ya habari na utangazaji.



Share:

UTEUZI:RAIS AFANYA UTEUZI WA MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI WA MICHEZO YA KUBAHATISHA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua Balozi Modest Jonathan Mero (Mstaafu) kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Michezo ya Kubahatisha (GBT).

Balozi Mero ni Mkurugenzi wa Bodi ya Kampuni ya African Discovery Group, New York nchini Marekani.

Uteuzi huu unaanza mara moja.

Zuhura Yunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu
Share:

SPIKA WA BUNGE LA AFRIKA KUSINI : NCHI ZA AFRIKA TUNAPIGA HATUA NZURI KATIKA KUWAPA NAFASI ZA UONGOZI WANAWAKE


Spika wa Bunge la Serikali ya Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Mapisa Nqakula kwenye Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge la Afrika juu ya Haki za Wanawake.

 Na Kadama Malunde - Midrand Afrika Kusini
Spika wa Bunge la Serikali ya Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Mapisa Nqakula amesema Bara la Afrika limepiga hatua linafanya vizuri katika kuwapa nafasi wanawake kwenye nafasi za uongozi.


Mhe. Nqakula amesema hayo leo Ijumaa Novemba 4,2022 kwenye Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge la Afrika juu ya Haki za Wanawake unaoendelea katika ukumbi wa Bunge la Afrika Midrand Afrika Kusini ukiongozwa na mada ‘Uwezeshaji na ushirikishwaji wa wanawake katika utawala’,

“Tunashukuru Barani tunaendelea kufanya vizuri katika kuwapa nafasi wanawake kwenye nafasi za uongozi. Sisi wanawake tunafanya kazi vizuri, Tumeona katika siasa idadi ya wanawake inaongezeka mfano idadi kubwa ya maspika wa bunge kwenye nchi zetu ni wanawake”,amesema Mhe. Nqakula.


“Wanawake washirikishwe katika masuala ya amani kwani panapotokea vurugu wanaoathirika zaidi ni wanawake, wanaoumia zaidi ni wanawake. Bado wanawake hawajajumuishwa katika masuala ya uchumi.

Usawa wa kijinsia unahitaji utashi wa kisiasa. Ni jukumu la wabunge kuhakikisha wanasimamia masuala ya usawa kijinsia yanapewa kipaumbele ili kuhakikisha kuwa wanawake hawatengwi hivyo wanawake wawe kwenye tabaka la watu wengi”,amesema.

Hata hivyo amesema hali za maisha za wanawake bado hazijaboreshwa, wanawake wanaajiriwa katika nafasi za chini na hata mishahara wanayolipwa wanawake na wanaume tofauti ni kubwa.

"Tunataka pia kuona idadi ya wanawake inaongezeka katika bodi za Mashirika na Makampuni. Ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha kuna usawa wa kijinsia katika kila eneo",amesema Mhe. Nqakula.
Spika wa Bunge la Serikali ya Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Mapisa Nqakula kwenye Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge la Afrika juu ya Haki za Wanawake. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Spika wa Bunge la Serikali ya Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Mapisa Nqakula kwenye Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge la Afrika juu ya Haki za Wanawake.
Spika wa Bunge la Serikali ya Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Mapisa Nqakula kwenye Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge la Afrika juu ya Haki za Wanawake.
Makamu wa Rais wa Tatu wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament - PAP), Mhe. Lucia Doss Passos  akizungumza wakati wa Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge la Afrika juu ya Haki za Wanawake
Makamu wa Rais wa Tatu wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament - PAP), Mhe. Lucia Doss Passos  (kulia) akizungumza wakati wa Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge la Afrika juu ya Haki za Wanawake
Share:

MWENYEKITI WA KIJIJI AJIUA KWENYE MPARACHICHI

Geofrey Massawe (45), Mwenyekiti wa kitongoji Somanga mkoani Kilimanjaro amejiua kwa kujinyonga kwa kutumia kamba ya kufungia ng'ombe aliyoifunga juu ya mti wa mparachichi jirani na nyumbani kwake.


Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Simoni Maigwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo leo Alhamisi Novemba 3 ambapo amesema mwili wa Mwenyekiti huyo ulikutwa juu ya mti na kwamba wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili kubaini chanzo chake.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII <<HAPA>>

Via Mwananchi

Share:

Thursday, 3 November 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA NOVEMBA 4,2022


















Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger