Saturday, 22 October 2022

UTEUZI:RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI MBALIMBALI

Share:

ATUPWA JELA MIAKA 7 NA FAINI YA MIL. 15 KWA KUMKASHFU RAIS SAMIA KWENYE 'GROUP LA WHATSAPP'


Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Simiyu imemhukumu kifungo cha miaka saba na faini ya Sh15 milioni, Levinus Kidanabi maarufu kama 'Chief Son's kwa makosa matatu ikiwamo kumkashifu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Hukumu hiyo imetolewa leo Ijumaa Oktoba 21, 2022 na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Matha Mahumbuga ambapo alieleza kuwa mtuhumiwa alitoa taarifa za uongo kinyume cha Sheria ya Makosa ya Kimtandao ya Mwaka 2015.

Katika taarifa iliyotolewa Wakili wa Serikali Daniel Masambu imeeleza kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa anashtakiwa kwa kosa la kuchapisha taarifa za uongo katika Jukwaa la Mtandao wa Whatsapp la "Simiyu

Ameeleza kuwa shtaka la kwanza na la pili alitenda Desemba 03 na 04, 2021 mtuhumiwa huyo aliandika kwenye jukwaa hilo maneno ya kumkashifu Rais Samia Suluhu Hassan.

Shtaka la tatu ni kutumia namba ya simu 0764996612 isivyo kihalali iliyokuwa imesajiliwa kwa jina la Hollo Yonas bila kuwa na kibali kutoka mamlaka husika.

"Katika makosa hayo yote mshtakiwa amehukumiwa kutumia kifungu cha miaka mitatu jela na faini ya Sh5 milioni kwa kosa la kwanza, miaka miwili jela na faini ya Sh5 milioni kwa kosa la pili na miaka miwili jela pamoja na faini ya Sh5 milioni kwa kosa la tatu," amesema Masambu.

CHANZO: Mwananchi
Share:

Friday, 21 October 2022

MBINU SAHIHI YA KUWAKABILI WEZI


Jina langu ni Ibra kutokea Nairobi nchini Kenya, ni kijana ambaye nimejikita katika biashara ndogo ndogo hapa jijini kwa miaka zaidi ya 10 sasa.

Katika biashara zangu hizi nimewahi kupitia changamoto nyingi sana kiasi kwamba nilitaka hadi kuachana na kazi yenyewe licha ndio ilikuwa inaniingizia kipato.

Changamoto yangu kubwa ilikuwa ni wizi ambao ulikuwa unafanywa na vijana wasio na kazi ambao pia hawataki kujishughulisha kivyovyote vile.

Kila mara nilikuwa nikija asubuhi katika kibanda changu cha biashara muda wa asubuhi nilikuwa nakuta kimevunjwa na kuibiwa kila kitu. Hilo lilikuwa linanichanganya sana maana ilikuwa inanibidi nianze kutafuta fedha nyingine kwa ajili ya kuanza upya.

Mwisho wa siku nilichoka hali hiyo na kuanza kutafuta suluhisho ya kudumu, ndipo nilikutana na mtu anayeitwa Dr. Kiwanga kupitia mitandao ya kijamii.

Huyu ni mtu ambaye anaweza kuwadhibiti wezi kwenye biashara yako, ukipata tiba yake hakuna mwizi atajaribu kugusa biashara yako hata kidogo.

Nilipopata dawa ya Dr. Kiwanga, asubuhi moja ninafika katika ofisi yangu na kukuta vijana watatu wameganda karibuni na kibanda changu huku wameshika mbali ambazo walikuwa wameziiba.

Hapo hapo nilichukua simu na kuwasiliana na Dr. Kiwanga ambaye alinipa maelezo ya kufanya kuhusu jambo hilo. Tangu wakati huo hakuna tena mwizi ambaye amegusa mali yangu kutokana tukio hilo lilifahamika na watu wengi. Asante sana Dr. Kiwanga kwa tiba yako.

Kumbuka Dr. Kiwanga ana uwezo kumfanya mtu kuwa na bahati maishani mwake, kushinda katika michezo ya bahati nasibu, kukukinga na maadui zako, kukufanya ushinde migogoro kama ya ardhi, kuwa na mvuto wa kimapenzi, kuongeza mauzo katika biashara.

Pia anatibu magonjwa kama Kaswende, Kisonono, Kifua Kikuu, Presha na mengine mengi, kwa mawasiliano zaidi  piga simu +254 769404965


Share:

CHAMA CHA WALIMU MANISPAA YA SHINYANGA KIMEFANYA MKUTANO MKUU, SATURA AAHIDI KUSHUGHULIKIA MATATIZO YAO

Mwenyekiti wa chama cha walimu Manispaa ya Shinyanga Meshack Mashigala akizungumza kwenye mkutano huo.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

CHAMA cha Walimu Manispaa ya Shinyanga (CWT) kimefanya mkutano mkuu wa nusu mhula, huku wakimpongeza Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Jomaary Satura kwa kujali watumishi na kutatua matatizo yao.

Mkutano huo umefanyika leo Oktoba 21, 2022 katika ukumbi wa mikutano Shule ya Msingi Buhangija Manispaa ya Shinyanga.

Mwenyekiti wa chama cha walimu Mkoa wa Shinyanga Mathias Balele, akizungumza kwenye mkutano huo, amesema Manispaa ya Shinyanga kwa sasa ina Mkurugenzi ambaye anajali maslahi ya watumishi wake, ambapo walimu wanapanda madaraja na kulipwa mapunjo ya mshahara, na katika halmashauri zote za mkoa huo Shinyanga ndiyo inaongoza kwa malipo hayo.

“Mkurugenzi tunakubali utendaji wako kazi, lakini tunakuomba tufikishie kilio chetu cha Teaching Allowance kirudi, ambacho kilikuwepo hapo awali lakini Serikali ilikiondoa, ili walimu wapate kipato cha ziada nje ya mshahara,”amesema Balele.

Naye Mwenyekiti wa chama cha walimu Manispaa ya Shinyanga Meshack Mashigala, amewasilisha baadhi ya changamoto ambazo zinawakabili walimu ikiwamo kupunguziwa nauli zao, pamoja na wengine kulipwa hadi watoke rikizo, na kuomba walimu wanapaswa walipwe pesa zao kabla ya kwenda rikizo.

Aidha, Katibu wa chama cha walimu Manispaa ya Shinyanga Allen Shuli, akisoma taarifa kwenye mkutano huo, amesema wamejikita kujadili mambo muhimu mawili ambayo ni kupokea taarifa ya utendaji kazi wa chama kwa kipindi cha miaka miwili na nusu tangu uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka 2020.

Pia kupokea na kujadili taarifa ya fedha mapato na matumzi kwa kipindi cha kuanzia Mei 2020 hadi Septemba mwaka huo.

Amesema sanjali na hayo pia wanamuomba Mkurugenzi kushughulikia tatizo la walimu waliopunjwa madaraja yao toka mwaka 2013 hadi 2022, jambo ambalo limesababisha walimu walioanza kazi pamoja kutofautiana mishahara, na hata walimu waliotangulia kazini kuzidiwa mishahara na wanafunzi.

Tatizo jingine ni mapunjo ya nauli na Posho ya kujikimu kwa walimu wapya ambao walilipwa kwa utaratibu wa zamani badala ya maelekezo mapya ya Serikali, mapunjo ya mishahara wanayodai walimu tangu mwaka (2013-2022) na fedha za uhamisho, nauli na matibabu.

Katika hatua nyingine, amesema wanasisitiza nidhamu, uwajibikaji na utii kwa walimu wote, pamoja na kukemea vitendo viovu vya kudhalilisha wanafunzi, ulevi, wizi wa mitihani pamoja na kukopa mikopo ya kupindukia.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura ambaye alikuwa mgeni Rasmi kwenye mkutano huo, amewasisitiza walimu suala la uwajibikaji na kuchapa kazi kwa bidii, wakati Serikali ikiendelea kushughulikia matatizo yao moja baada ya jingine.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura akizungumza kwenye mkutano mkuu wa chama cha walimu Manispaa ya Shinyanga.

Mwenyekiti wa chama cha walimu Mkoa wa Shinyanga Mathias Balele, akizungumza kwenye mkutano huo.

Mwenyekiti wa chama cha walimu Manispaa ya Shinyanga Meshack Mashigala akizungumza kwenye mkutano huo.

Katibu wa chama cha walimu Manispaa ya Shinyanga Allen Shuli, akisoma taarifa kwenye mkutano huo.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura akikata keki kwenye mkutano huo.

Mkutano Mkuu wa chama cha walimu Manispaa ya Shinyanga ukiendelea.

Mkutano Mkuu wa chama cha walimu Manispaa ya Shinyanga ukiendelea.

Mkutano Mkuu wa chama cha walimu Manispaa ya Shinyanga ukiendelea.

Mkutano Mkuu wa chama cha walimu Manispaa ya Shinyanga ukiendelea.

Mkutano Mkuu wa chama cha walimu Manispaa ya Shinyanga ukiendelea.

Mkutano Mkuu wa chama cha walimu Manispaa ya Shinyanga ukiendelea.

Mkutano Mkuu wa chama cha walimu Manispaa ya Shinyanga ukiendelea.
Mkutano Mkuu wa chama cha walimu Manispaa ya Shinyanga ukiendelea.

Mkutano Mkuu wa chama cha walimu Manispaa ya Shinyanga ukiendelea.

Mkutano Mkuu wa chama cha walimu Manispaa ya Shinyanga ukiendelea.

Mkutano Mkuu wa chama cha walimu Manispaa ya Shinyanga ukiendelea.
Mkutano Mkuu wa chama cha walimu Manispaa ya Shinyanga ukiendelea.

Mkutano Mkuu wa chama cha walimu Manispaa ya Shinyanga ukiendelea.

Mkutano Mkuu wa chama cha walimu Manispaa ya Shinyanga ukiendelea.

Mkutano Mkuu wa chama cha walimu Manispaa ya Shinyanga ukiendelea.

Mkutano Mkuu wa chama cha walimu Manispaa ya Shinyanga ukiendelea.
Share:

WAKURUGENZI WA HALMASHAURI WATAKIWA KUTENGA BAJETI KUWEZESHA WANAOSIMAMIA ELIMU YA WATU WAZIMA

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omari Kipanga akipokea maelezo kutoka kwa mmoja washiriki katika maadhimisho ya Juma la Elimu ya Watu Wazima yaliyofanyika katika Viwanja vya DUCE Jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omari Kipanga akipokea maelezo kutoka kwa mmoja washiriki katika maadhimisho ya Juma la Elimu ya Watu Wazima yaliyofanyika katika Viwanja vya DUCE Jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omari Kipanga akipokea maelezo kutoka kwa mmoja washiriki katika maadhimisho ya Juma la Elimu ya Watu Wazima yaliyofanyika katika Viwanja vya DUCE Jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omari Kipanga akizungumza wakati wa kufunga Maadhimisho ya Juma la Elimu ya Watu Wazima yaliyofanyika katika Viwanja vya DUCE Jijini Dar es Salaam Kamishna wa Elimu, Dkt. Lyabwene Mtahabwa akizungumza wakati wa kufunga Maadhimisho ya Juma la Elimu ya Watu Wazima yaliyofanyika katika Viwanja vya DUCE Jijini Dar es Salaam Amidi, Shule Kuu ya Elimu Dkt.Eugenia Kafanabo akizungumza wakati wa kufunga Maadhimisho ya Juma la Elimu ya Watu Wazima yaliyofanyika katika Viwanja vya DUCE Jijini Dar es Salaam

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

**********************

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omari Kipanga ametoa wito kwa Wakurugenzi wa Halmashauri kutenga bajeti kwa ajili ya kuwawezesha Maafisa wanaosimamia Elimu ya Watu Wazima kuwafikia walengwa kwa urahisi.

Mhe. Kipanga ametoa wito huo wakati akifunga maadhimisho ya Juma la Elimu ya Watu Wazima yaliyofanyika katika Viwanja vya DUCE Jijini Dar es Salaam ambapo amesema kwa kufanya hivyo itawezesha utekelezaji wa shughuli za elimu ya watu wazima katika eneo husika kwa ufanisi.

Amesema katika kuipa uhai elimu ya watu wazima pamoja na kutengewa bajeti maafisa elimu wanaoshughulika na eneo hilo ndani ya Mikoa na Halmashauri wanapaswa kuhakikisha wanahamasisha, kuanzisha, kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa Programu mbalimbali za Elimu ya Watu Wazima.

“Niwasihi Maafisa Elimu Elimu ya Watu Wazima pamoja na kusimamia kazi katika maeneo yenu shirikianeni na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima kuendeleza jitihada za kuhakikisha kuwa madarasa ya MEMKWA yanasimamiwa na kuwa na vitendea kazi vinavyokidhi mahitaji ya ufundishaji na ujifunzaji,” amesema Mhe Kipanga.

Akizungumzia mapitio ya Sera na mitaala yanayoendelea Mhe. Kipanga amesema Wizara bado inapokea maoni ya wadau kuhusu maboresho hayo huku ikiendelea na uchambuzi wa maoni ambayo yamepokelewa ili kukamilisha kazi hiyo.

Amesema kumekuwa na taarifa ambazo si za kweli zinazosambaa kwenye mitandao zikisema kuwa “Sera ya Elimu inayotarajiwa kuzinduliwa hapo baadae elimu ya msingi itakomea darasa la sita.”

“Nilikuwa kwenye Kongamano la Wanataaluma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, wakati nazungumza nilisema kuwa tunaendelea na mapitio ya Sera ya Elimu na kwamba kuna maoni mbalimbali yameshatolewa na katika uchambuzi yapo maoni yaliyosema elimu ya msingi ikomee darasa la sita na baada kumaliza kuwe na mifumo na njia mbili kuu ambazo zinawapeleka vijana kwenye taaluma na ujuzi. Sasa zipo nukuu kwenye mitandao zikisema nimesema elimu ya msingi mwisho darasa la sita, si kweli,” amefafanua Mhe. Kipanga.

Aidha amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha kila mtoto wa Kitanzania anapata fursa ya kupata elimu iliyo bora na ndio maana imeweka Sera ya Elimu bure kuanzia elimu ya awali hadi kidato cha sita huku ikiwarudisha shule wanafunzi waliokatisha masomo kwa sababu mbalimbali waweze kuendela na masomo ili watimize ndoto zao.

Akimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara katika kilele hicho Kamishna wa Elimu, Dkt. Lyabwene Mtahabwa amesema katika kukabiliana na changamoto ya idadi ya watu wasiojua Kusoma, Kuandika na Kuhesabu, Wizara inatekeleza Mkakati wa Kitaifa wa Kisomo cha Elimu kwa Umma ambao unalenga kuboresha programu za kisomo na elimu kwa njia mbadala. Pia imeandaa “National Qualification Framework” mfumo ambao kwa mara ya kwanza umetambua programu za Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi.

Maonesho ya Maadhimisho ya Juma la Elimu ya Watu Wazima yaliyofanyika Jijini Dar es Salam kuanzia Oktoba 17-21, 2022 yalikuwa na kaulimbiu isemayo “Kuboresha mazingira ya kujifunza kusoma na kuandika yatakayozingatia ubora, usawa na ujumuishi wa makundi yote” na yameshirikisha Vyuo Vikuu, Taasisi zilizo chini ya Wizara, Maafisa Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi Wilaya na Mikoa yote Tanzania Bara, Mashirika ya Kimataifa pamoja na wadau mbalimbali wanaojishughulisha na utoaji wa Elimu ya Watu wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi hapa nchini.
Share:

NCHI 47 KUSHIRIKI MASHINDANO YA DUNIA YA UTANASHATI NA UREMBO KWA VIZIWI TANZANIA


MATUNDA ya filamu ya The Royal Tour yanaendelea kushamiri baada ya Tanzania kuwa mwenyeji wa shindano la Dunia la utanashati, urembo na mitindo wanaume na wanawake kwa watu wenye changamoto ya usikivu.

Shindano hilo linalotarajia kufanyika Oktoba 29 mwaka huu katika Ukumbi wa Kimataifa ws Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.


Akizungumza na wanahabari kambini hoteli ya Peackock Mkurugenzi idara ya Maendeleo ya sanaa Dkt.Emmanuel Ishengoma amesema Tanzania kama nchi mwenyeji wa Mashindano makubwa ya utanashati, urembo na mitindo bora ya dunia wamejipanga kwa maandalizi ya awali kuanzia washiriki pamoja kwani maandalizi ya awali yalianza mapema tangu mwezi agosti mwaka huu katika chuo cha sanaa cha Bagamoyo (Tasuba).

Hata hivyo Ishengoma amefafanua kuwa tayari idara ya uhamiaji imeanza kupokea wageni kutoka nchi mbalimbali kwa ajili ya kuanza kuwasili kambini kusubiri fainali rasmi ambayo inatarajiwa kufanyika octoba 29 mwaka huu katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam.


Aidha amesema washiriki wanaowakilishi nchi ya Tanzania wapo washiriki 6 ambapo walifanya vizuri kwenye ngazi ya Mashindano ya Afrika , wanawake wakiwa 4 na wanaume wawili ambapo Serikali imewapa ushirikiano mkubwa kuanzia gharama zote wawapo kambini hadi kuisha kwa shindano hilo.

Aidha, Shindano hilo limeshirikisha nchi 47 huku Tanzania ikiwa Mwenyeji wa Shindano hilo.

Kwa upande wake Mshiriki wa Shindano hilo ambae pia ni Mshindi wa pili wa ngazi ya Afrika Carolyne Mwakasasa ametoa ushauri kwa vijana ambao wana ulemavu wa kusikia wajitokeze kwa wingi kushiriki mashindano mbalimbali wasione aibu.

"Wajitokeze kushiriki mashindano mbalimbali ili kuweza kuonyesha uwezo wao katika jamii."

Hata hivyo Mwakasasa amesema amejipanga vizuri na anaamini ataipeperusha vizuri bendera ya Tanzania katika Mashindano hayo ya dunia.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger