Wednesday, 19 October 2022

UFUNGUZI WA KONGAMANO LA MIAKA 60 UDSM NA MIAKA 17 DUCE

Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mh. Dkt. Francis Michael akieleza jambo mbele ya Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi ya Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam, Prof. William Anangisye wakati akitembelea mabanda ya watafiti na wabunifu katika Ufunguzi wa Kongamano la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na miaka 17 ya Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam lililofanyika leo Oktoba 19,2022 Jijini Dar es SalaamKatibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mh. Dkt. Francis Michael akizungumza jambo mara baada ya kutembelea moja ya banda la wabunifu DUCE katika hafla ya ufunguzi wa Kongamano la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na miaka 17 ya Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam lililofanyika leo Oktoba 19,2022 Jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mh. Dkt. Francis Michael akitembelea baadhi ya mabanda ya wabunifu DUCE katika hafla ya ufunguzi wa Kongamano la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na miaka 17 ya Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam lililofanyika leo Oktoba 19,2022 Jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mh. Dkt. Francis Michael akizungumza katika ufunguzi wa Kongamano la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na miaka 17 ya Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam lililofanyika leo Oktoba 19,2022 Jijini Dar es Salaam Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi ya Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam, Prof. William Anangisye akizungumza katika ufunguzi wa Kongamano la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na miaka 17 ya Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam lililofanyika leo Oktoba 19,2022 Jijini Dar es Salaam Rasi wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE),Prof.Stephen Maluka akizungumza katika ufunguzi wa Kongamano la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na miaka 17 ya Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam lililofanyika leo Oktoba 19,2022 Jijini Dar es Salaam Baadhi ya wadau wa elimu wakiwa katika ufunguzi wa Kongamano la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na miaka 17 ya Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam lililofanyika leo Oktoba 19,2022 Jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mh. Dkt. Francis Michael akiwa na baadhi ya viongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam wakipata picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa elimu katika Ufunguzi wa Kongamano la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na miaka 17 ya Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam lililofanyika leo Oktoba 19,2022 Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

***********************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

CHUO Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) kimetakiwa kutengeneza mkakati maalumu wa kuwawezesha wahitaji wa Chuo hicho kuwa na uwezo wa kujiajiri kwa kutegemea elimu na maalifa ambayo wameyapata Chuoni.

Wito huo umetolewa leo Oktoba 19,2022 na Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mh. Dkt. Francis Michael wakati akifungua Kongamano la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na miaka 17 ya Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam, hafla ambayo imefanyika Chuoni DUCE.

Amesema wahitimu wengi wapo mtaani wakisubiri kuajiriwa na hata wengine wamekuwa hawana uelewa wa kujiajiri lakini kama chuo kikitengeneza mikakati ambayo itaweza kumsaidia muhitimu kujiajiri basi vijana wengi watapata ajira.

Aidha Dkt.Francis amewapongeza wanataaluma wa DUCE na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kuhakikisha wanafikia malengo wanayojiwekea kama taifa, hususani kwenye sekta ya elimu.

"Natambua kabisa ugumu wa kazi hii kwa kuwa nimeifanya mwenyewe kwa miaka mingi. Pamoja na ugumu huo, bado mmeendelea kuwa imara katika kutekeleza majukumu yetu". Amesema Dkt.Francis.

Pamoja na hayo amesema Serikali inatambua mchango mkubwa wa elimu ya juu kwenye maendeleo ya taifa letu na ngezeko la bajeti ya mikopo ya elimu ya juu ni moja tu ya mifano michache ya nia njema ya serikali ya kupanua wigo wa upatikanaji wa elimu ya juu.

Amesema ni wajibu wa vyuo vikuu nchini kufanya tafiti mbalimbali, zikiwemo tafiti kuhusu namna ambayo elimu ya juu itakidhi matakwa ya sasa ya jamii ya kitanzania.

"Mna wajibu wa kufanya uchunguzi wa kina kuhusu mwelekeo wa sasa wa kitaifa na kimataifa na kisha kutafakari ni namna gani vyuo vyetu vitawawezesha wahitimu kuendana na mwelekeo huo". Amesema

Nae Rasi wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE),Prof.Stephen Maluka amesema katika kipindi cha miaka 17, Chuo kimepata mafanikio mbalimbali na kutoa mchango mkubwa kwa taifa ikiwemo kushuhudia idadi ya wanafunzi wahitimu kuongezeka kutoka 522 Mwaka 2008 yalipofanyika mahafali ya kwanza, hadi kufikia wahitimu 16,330 Mwaka 2021.

Aidha, amesema katika mahafali ya 14, Mwaka 2021, idadi ya wahitimu ilikuwa 1,565, ikiwa ni idadi mara tatu zaidi ikilinganishwa na idadi ya wahitimu wa kwanza Mwaka 2008. Wahitimu hawa wamesaidia sana kupunguza uhaba wa walimu na wataalamu wa elimu nchini.

Amesema Chuo kimekuwa ni mahali pa kuchochea ubunifu unaowezesha wahitimu wetu kutatua tatizo la ajira kwa kuajiri na kuajiri watu wengine. Aidha, kutokana na kuwa na wanataaluma wabobezi katika fani mbalimbali, Chuo kimeweza kufanya tafiti mbalimbali zinazotatua matatizo ya jamii ya na pia kutoa huduma za ushauri wa kitaalamu katika maeneo ya elimu, insia, sayansi na sayansi jamii.

Prof.Maluka ameeleza kuwa Chuo kimekuwa kikikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo gharama kubwa ya usomeshaji wa wanataaluma ili wafikie kiwango cha Ph.D., ambacho hasa ndicho kinatakiwa kwao.

"Ili kukabiliana na changamoto hii, Chuo kimeendelea na utaratibu wake wa kusomesha wafanyakazi kwa awamu kwa kutumia vyanzo vyake vya ndani, kutumia fursa za ufadhili kupitia vyuo rafiki nje ya nchi na kuomba uwezeshaji kutoka Serikalini". Amesema Prof.Maluka

Amesema Chuo kimekuwa na uhaba wa vyumba vya kufundishia na kujifunzia, maktaba za TEHAMA zenye vifaa vyote muhimu na ofisi za watumishi wa Chuo na katika changamoto hizi, wanaishukuru Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kuwasaidia katika usomeshaji wa baadhi ya watumishi wa Chuo na ujenzi na upanuzi wa miundombinu ya Chuo kupitia miradi yake mbalimbali.
Share:

NGELELA ASHINDA NAFASI YA MWENYEKITI CCM WILAYA YA SHINYANGA VIJIJINI UCHAGUZI WA MARUDIO, MGEJA AGOMEA MATOKEO


Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Vijijiji Edward Ngelela, ambaye ametetea kiti chake kwa kupata ushindi wa kishindo.
Edward Ngelela (kushoto) akiwa katika uchaguzi wa awali akitetea kiti chake cha Uenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Vijijini, (wapili kutoka kulia) ni Mwenzetu Mgeja naye akiwania nafasi hiyo, ambapo katika uchaguzi wa marudio ameshindwa tena na kugoma kusaini matokeo.

Wajumbe wakipiga kura.

Na Halma Khoya ,SHINYANGA

CHAMA cha Mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga Vijijini kimefanya uchaguzi wa marudio kwa nafasi ya Mwenyekiti, pamoja Katibu wa Itikadi na Uenezi, mara baada ya uchaguzi wa awali kuingiwa na dosari.

Uchaguzi huo umefanyika Jana katika Uwanja wa CCM Kambarage Manispaa ya Shinyanga, ambapo uchaguzi wa awali ulifanyika Oktoba Mosi mwaka huu, na Edward Ngelela alitangazwa kushinda nafasi ya Uenyekiti, pamoja na Emmanuel Lukanda kushinda nafasi ya Uenezi.

Katika uchaguzi huo wa marudio, Edward Ngelela ametangazwa kushinda tena nafasi ya Uenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Vijijini kwa kupata kura 741, akifuatiwa na Mwezetu Mgeja kura 157, Peter Kawiza kura 48, na Anna Ng’wagi kura 11.

Aidha, kwa upande wanafasi ya Katibu wa Itikadi na Uenezi Emmanuel Lukanda, ameshinda tena nafasi hiyo kwa mara ya pili kwa kupata kura 120, akifuatiwa na Mohamed Hussein kura 10 na Rojas Samsoni kura Tatu.

Hata hivyo katika uchaguzi huo wa marudio Mmoja wa Wagombea wa nafasi ya Uenyekiti Mwezetu Mgeja, aligoma kusaini matokeo hayo kwa madai kuwa uchaguzi huo umegubikwa na figisu figisu.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Solwa Ahmad Salum, amesema uchaguzi huo umekuwa wa demokrasia na haki, na amewaomba viongozi wawe na ushirikiano ili kuleta maendeleo ya ndani na nje ya chama.

"Uchaguzi umekuwa wa haki kwa kila mtu na hakuna ubishi wowote uliotokea na washindi wamepatikana, kinachofuata sasa ni kuchapa kazi kwa ushirikiano,”amesema Salum.
Share:

Tuesday, 18 October 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO OKTOBA 19,2022
















Share:

TBS YASHIRIKI WIKI YA MAADHIMISHO YA SIKU YA CHAKULA DUNIANI MKOANI SIMIYU


*******************

SHIRIKA la Viwango Tanzania limeshiriki katika wiki ya maadhimisho ya siku ya chakula Duniani yaliyofanyika kitaifa Mkoani Simiyu ambapo shirika limeendela kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa uzalishaji na uuzaji wa bidhaa za chakula zenye ubora na znazokidhi matakwa ya Viwango.

Akizungumza katika maadhimisho hayo Afisa Usalama wa Chakula (TBS) Bw. Makaya Nsonda amesema ili kuwa na afya bora wazalishaji wanatakiwa kuzalisha bidhaa za chalula zilizokidhi matakwa ya viwango kwani kwa kufanya hivyo taifa litapata nguvu kazi kubwa kwani walaji wa bodhaa hizi hawataathirika na bidhaa hafifu.

Aidha ameongeza kuwa ni fursa kwa wajasilimali wa mkoani Simiyu na mikoa jirani kuweza kutembelea banda la TBS na kuweza kupewa elimu ya udhibiti ubora ili kuzalisha na kununua biidhaa zilizokidhi viwango .

"Ni fursa kwa wajasiriamali kuzalisha bidhaa na kuthibitishwa na TBS, kwaajili ya biashara ndani na nje ya nchi, kwani huthibitishwa na TBS bure”

Pia ameotoa wito kwa wajasirimali kutumia vyema fursa hii ya uthibitishaji ubora bure ili kuongeza thamani katika bidhaa zao chakula.
Share:

WAZIRI JAFO APOKEA MALALAMIKO YA WANANCHI WAISHIO KANDO YA MTO MSIMBAZI KATA YA MOGO KIPAWA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mheshimiwa Dkt. Selemani Jafo akimsikiliza Mwenyekiti wa Kikosi kazi cha kuratibu usafishaji wa Mito na mabonde Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Elizabeth Mshote mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea Mto Msimbazi kata ya Mogo mtaa wa Kipawa leo Oktoba 18,2022 Jijini Dar es Salaam Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mheshimiwa Dkt. Selemani Jafo akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea Mto Msimbazi kata ya Mogo mtaa wa Kipawa leo Oktoba 18,2022 Jijini Dar es Salaam Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mheshimiwa Dkt. Selemani Jafo akipata picha ya pamoja na wakazi wa Mto Msimbazi kata ya Mogo mtaa wa Kipawa Jijini Dar es Salaam mara baada ya kutembelea eneo hilo leo Oktoba 18,2022. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mheshimiwa Dkt. Selemani Jafo akimsikiliza mmoja wa mkazi wa eneo la Mogo mtaa wa Kipawa mara baada ya kutembelea Mto Msimbazi uliopita eneo hilo leo Oktoba 18,2022 Jijini Dar es Salaam Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mheshimiwa Dkt. Selemani Jafo akielekeza jambo akiwa katika Mto Msimbazi kata ya Mogo mtaa wa Kipawa Jijini Dar es Salaam mara baada ya kutembelea eneo hilo leo Oktoba 18,2022.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mheshimiwa Dkt. Selemani Jafo akiwa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe.Ng`wilabuzu Ludigija wakiwa katika Mto Msimbazi kata ya Mogo mtaa wa Kipawa Jijini Dar es Salaam mara baada ya kutembelea eneo hilo leo Oktoba 18,2022.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mheshimiwa Dkt. Selemani Jafo akiwa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe.Ng`wilabuzu Ludigija wakiwa katika Mto Msimbazi kata ya Mogo mtaa wa Kipawa Jijini Dar es Salaam mara baada ya kutembelea eneo hilo leo Oktoba 18,2022. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mheshimiwa Dkt. Selemani Jafo akiwa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe.Ng`wilabuzu Ludigija wakiwa katika Mto Msimbazi kata ya Mogo mtaa wa Kipawa Jijini Dar es Salaam mara baada ya kutembelea eneo hilo leo Oktoba 18,2022. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mheshimiwa Dkt. Selemani Jafo akiwa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe.Ng`wilabuzu Ludigija wakimsikiliza mmoja wa wasimamizi wa shughuli katika Mto Msimbazi kata ya Mogo mtaa wa Kipawa Jijini Dar es Salaam mara baada ya kutembelea eneo hilo leo Oktoba 18,2022.

***************************

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mheshimiwa Dkt. Selemani Jafo ametoa muda wa siku nne kwa Kikosi kazi cha kusimamia Muongozo wa usafishaji mchanga kwa Mkoa wa Dar es Salaam kumpelekea taarifa ya nini kifanyike kuhusiana na kutafuta suluhisho na kupata ufumbuzi juu ya athari zinazotokana na uchimbaji wa mchanga katika Mto Msimbazi.

Ameyasema hayo leo Oktoba 17,2022 Jijini Dar es Salaam alipokua katika ziara ya kutembelea Mto Msimbazi katika Kata ya Mogo Mtaa wa Kipawa katika jiji la Ilala Mkoani Dar es Salaam.

“Nimekuja hapa sababu Ofisi yangu imepokea malalamiko kuhusiana na athari za kimazingira zinazotokana na suala zima la usafishaji wa mto huu wa Msimbazi. Na kwa sababu kuna mawazo kinzani kutoka kwa pande mbili. Ninawapa siku tano mjadiliane kwa kina nini kifanyike na mniletee taarifa hiyo Ofisini kwangu”.

Aidha ameongeza kuwa baada ya kufika katika eneo hilo la Mto huo amesikiliza maoni ya Wananchi na amepata maoni yanayokinzana kwani wengine wanasema baada ya shughuli za usafishaji mto huo kuanza zimeleta athari kwa mazingira na wengine wamesema baada ya shughuli hizo kuanza usafishaji umeleta manufaa makubwa kwa jamii inayozunguka eneo hilo.

Akiongea baada ya maelekezo hayo Mkuu wa Wilaya wa Manispaa ya Ilala Mheshimiwa Ng’wilabuzu Ludigija amemuhakikishia Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mheshimiwa Dkt. Selemani Jafo kuwa amepokea maelekezo hayo na watayafanyia kazi na kuyasimamia kwa karibu sana.

Naye Meneja wa NEMC Kanda ya Mashariki- Kaskazini Bw. Arnold Mapinduzi amesema kuwa Muongozo wa usafishaji mchanga umeelekeza suala hilo lifanyike kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa ikiwa ni pamoja wote wanaotaka kujishughulisha na suala hilo waombe vibali kutoka Mamlaka yay a Usimamizi wa Bonde la Wami Ruvu.
Share:

SNV WAADHIMISHA SIKU YA UNAWAJI MIKONO DUNIANI SHULE YA SEKONDARI NGOKOLO MANISPAA YA SHINYANGA


Mwenyekiti wa Klabu ya Mazingira Shule ya Sekondari Ngokolo Manispaa ya Shinyanga Mariamu Enock (wakwanza kushoto) akitoa elimu ya unawaji mikono kwa wanafunzi wenzake shuleni hapo.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

SHIRIKA la Maendeleo la Uholanzi (SNV), wameadhimisha siku ya unawaji mikono duniani katika Shule ya Sekondari Ngokolo Manispaa ya Shinyanga, kwa kutoa elimu ya unawaji mikono sahihi kwa wanafunzi ili kuwaepusha na maradhi mbalimbali.

Afisa Msaidizi wa Mradi wa usafi wa mazingira mijini (WASH SDG) kutoka SNV Izack Msumba, akizungumza shuleni hapo, amesema siku ya unawaji mikono duniani huadhimishwa kila mwaka Oktoba 15, lakini wao wameadhimisha leo Oktoba 18, 2022, kutokana na siku hiyo kuangukia jumamosi ambayo wanafunzi wapo majumbani mwao.

Amesema wamefanya maadhimisho hayo katika shule hiyo ambayo ni miongoni mwa shule walizozipatia mafunzo ya usafi wa mazingira pamoja na kuunda klabu ya Mazingira, ambapo wanafunzi kupitia klabu yao hufundishana wao kwa wao namna ya kuzingatia usafi kwa kunawa mikono.

“Wanafunzi wakielewa zaidi namna ya unawaji mikono kwa usahihi, wataisambaza elimu hii majumbani mwao na kuwa mabalozi wazuri,” amesema Msumba.

Naye Afisa elimu masuala ya Afya katika Shule za Sekondari na Msingi Manispaa ya Shinyanga Beatrice Mbonea, akizungumza katika maadhimisho hayo, amewataka wanafunzi wazingatie usafi muda wote kwa kunawa mikono kwa sabuni na maji tiririka ili kuepuka kula uchafu na hatimaye kupata maradhi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Klabu ya Mazingira shuleni hapo Mariamu Enock, amesema elimu hiyo ya usafi wa mazingira imewasaidia wanafunzi kuzingatia usafi muda wote, kwa kunawa mikono mara kwa mara, na kuwaepusha na maradhi mbalimbali yatokanayo na uchafu.

Afisa Msaidizi wa Mradi wa usafi wa mazingira mijini (WASH SDG) kutoka Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV) Izack Msumba akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya unawaji mikono duniani katika Shule ya Sekondari Ngokolo Manispaa ya Shinyanga.

Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari Ngokolo Manispaa ya Shinyanga Martine Mponda akizungumza kwenye maadhimisho hayo ya siku ya unawaji mikono.

Naye Afisa elimu masuala ya Afya katika Shule za Sekondari na Msingi Manispaa ya Shinyanga Beatrice Mbonea akizungumza katika maadhimisho hayo ya siku ya unawaji mikono katika shule ya Sekondari Ngokolo Manispaa ya Shinyanga.

Mwalimu wa Mazingira Shule ya Sekondari Ngokolo Manispaa ya Shinyanga Ernest Ngarama akizungumza kwenye maadhimisho hayo ya siku ya unawaji mikono shuleni hapo.

Mwenyekiti wa Klabu ya Mazingira Shule ya Sekondari Ngokolo Manispaa ya Shinyanga Mariamu Enock, akizungumza kwenye maadhimisho ya unawaji mikono duniani shuleni hapo.

Mwenyekiti wa Klabu ya Mazingira Shule ya Sekondari Ngokolo Manispaa ya Shinyanga Mariamu Enock, akitoa elimu ya unawaji mikono kwa usahihi kwa wanafunzi wenzake, mafunzo ambayo awali walishapewa na SNV kupitia klabu yao.

Mfunzo ya unawaji mikono kwa usahihi yakiendelea kutolewa kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ngokolo Manispaa ya Shinyanga ili kujikinga na maradhi mbalimbali hasa wanapotoka chooni kujisaidia.
Mfunzo ya unawaji mikono kwa usahihi yakiendelea kutolewa kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ngokolo Manispaa ya Shinyanga ili kujikinga na maradhi mbalimbali hasa wanapotoka chooni kujisaidia.

Mfunzo ya unawaji mikono kwa usahihi yakiendelea kutolewa kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ngokolo Manispaa ya Shinyanga ili kujikinga na maradhi mbalimbali hasa wanapotoka chooni kujisaidia.

Walimu wa shule ya Sekondari Ngokolo Manispaa ya Shinyanga wakinawa mikono kwenye maadhimisho hayo ya siku ya unawaji mikono duniani.

Wanafunzi wa shule ya Sekondari Ngokolo Manispaa ya Shinyanga wakiwa wameshika bango lenye ujumbe wa kunawa mikono ili kuepuka maradhi.

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ngokolo Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya unawaji mikono duniani shuleni hapo.

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ngokolo Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya unawaji mikono duniani shuleni hapo.

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ngokolo Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya unawaji mikono duniani shuleni hapo.

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ngokolo Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya unawaji mikono duniani shuleni hapo.
Share:

UNAWEZA KUJIKINGA NA MADUI KATIKA MAISHA KWA KUFANYA HAYA!

Share:

BENKI YA DUNIA YASHANGAZWA NA MIUJIZA YA UCHUMI WA TANZANIA CHINI YA RAIS SAMIA


* Yasema Tanzania ni mfano wa kuigwa duniani kudhibiti mfumuko wa bei, nakisi ya bajeti

* Yapongeza sera za fedha na za uchumi za Tanzania


Washington, DC

MAKAMU Rais wa Benki ya Dunia wa Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Victoria Kwaka, ameipongeza serikali ya Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuleta "miujiza" kwenye uchumi.


Kwaka ameipongeza Tanzania kwa utulivu wa uchumi wake wakati nchi mbalimbali duniani zikiwa kwenye msukosuko wa uchumi unaotokana na vita ya Ukraine na sababu nyingine.


Amesema wakati nchi mbalimbali zikihangaika na janga la mfumuko wa bei wa tarakimu mbili, huku akiitaja Ghana kuwa na mfumuko wa bei wa asilimia 30, Tanzania imeweza kuwa na mfumuko wa bei wa tarakimu moja tu.


Taarifa kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) zinaonesha kuwa Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba 2022 ni asilimia 4.8.


"Tumeona karibu nchi zote duniani zikiwa na akiba ya fedha za kigeni dhaifu, lakini Tanzania imeweza kuwa na akiba ya fedha za kigeni inayotosha kuagiza bidhaa na huduma kutoka nje za kipindi cha takribani miezi mitano," Kwaka alisema katika mazungumzo jijini Washington DC na msafara wa viongozi wa Tanzania ulioongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mwigulu Nchemba.


"Tunaona mataifa mengi yakihangaika na nakisi kubwa ya bajeti, wakati Tanzania nakisi yake ya bajeti ni sawa na asilimia 3.5 tu ya Pato la Taifa. Nimemuuliza Waziri wa Fedha wa Tanzania kuwa wamewezaje kufanya miujiza hii? Hili ni jambo la kupongezwa sana na niwape moyo muendelee na usimamizi huu makini wa uchumi."


Kwaka pia aliipongeza Tanzania kwa kuwa na sera nzuri za fedha na uchumi zinazoleta utulivu kwenye uchumi.


"Mfumuko wa bei ni kama kodi mbaya ambayo inaumiza zaidi wananchi masikini. Naipongeza Tanzania kwa jitihada zake zote za kudhibiti mfumuko wa bei," alisema.


"Ni matarajio yetu kuwa tutaitumia Tanzania kama mfano bora wa kuigwa na nchi nyingine duniani."
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger