Sunday, 16 October 2022

RC MJEMA APONGEZA UTOLEWAJI MATIBABU YA MACHO, WANANCHI 116 WAFANYIWA UPASUAJI MTOTO WA JICHO



Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema akipima Macho akiwa na Mbunge wa Vitimaalum wa Mkoa huo Lucy Mayenga, alipofanya ziara ya kukagua zoezi la utolewaji matibabu ya macho bure kwa wananchi wa Shinyanga kutoka kwa Madaktari Bingwa wa Macho zoezi lililoratibiwa na Mbunge Lucy Mayenga.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema akipima Macho alipofanya ziara ya kukagua zoezi la utolewaji matibabu ya macho bure kwa wananchi wa Shinyanga ,kutoka kwa Madaktari Bingwa wa Macho zoezi lililoratibiwa na Mbunge wa Vitimaalum Mkoa wa Shinyanga Lucy Mayenga.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, ametembelea kuona zoezi la wananchi wa Mkoa huo wakipatiwa huduma ya matibabu ya macho bure, ambalo limeratibiwa na Mbunge wa Vitimaalum mkoani humo Lucy Mayenga.  
Mjema amefanya ziara hiyo leo Oktoba 16, 2022, ambapo zoezi hilo la utoaji matibabu bure ya macho lilianza rasmi Oktoba 14 mwaka huu na linahitimishwa leo, na lilikuwa likifanyika katika chuo cha Ualimu Shinyanga (SHYCOM) pamoja na Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya wagonjwa waliohitajika kufanyiwa upasuaji.

Akizungumza katika ziara hiyo amempongeza Mbunge Lucy Mayenga, kwa kuguswa na kuratibu matibabu hayo, ambayo wananchi wamepatiwa tiba bure ya macho, na ambao walikuwa hawaoni kabisa sasa wanaona na watakwenda kufanya shughuli za maendeleo.

“Mbunge Lucy Mayenga ni Mbunge Machachari sana, anafanya kazi na ana Roho ya kupenda wananchi wake, ndiyo maana ameratibu matibabu haya ya macho ili wananchi watibiwe na huduma hii imetolewa bure kabisa,” amesema Mjema.

“Tumpongeze pia Rais wetu Samia Suluhu Hassan kwa kuifungua Tanzania, sababu bila yeye madaktari hawa bingwa wa macho wasinge weza kuja kutoa huduma hii ya matibabu ya macho kwa wananchi wetu hapa Shinyanga,”ameongeza

Aidha, amewaomba Madaktari hao bingwa wa macho wasichoke kuja mkoani Shinyanga kuendelea kutoa tiba hiyo ya macho, sababu bado kuna uhitaji mkubwa wa wananchi kapata huduma hiyo, na ikiwezekana waje tena januari mwakani.

Naye Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa mkoani Shinyanga Dk, John Luzila, amepongeza huduma hiyo ya matibabu ya macho kwa wananchi wa Mkoa huo, na kubainisha kuwa pia Serikali imeshapeleka daktari wake masomoni, ambaye anasomea ubingwa wa matatizo ya macho na atakuwa wakifanya kazi katika hospitali hiyo.

Aidha, Mbunge Lucy Mayenga, amesema baada ya kuona katika Mkoa huo kuna upungufu wa madaktari bingwa wa macho, ndipo akaona ni vyema aratibu matibabu hayo ili wananchi wapate huduma bure, sababu baadhi yao hawezi kumudu gharama za matibabu kwenda katika hospitali kubwa.

Amesema pia katika nafasi yake ya ubunge atalipigia kelele suala hilo la upatikanaji wa madaktari bingwa macho katika Hospitali mbalimbali hapa nchini ukiwamo na Mkoa huo wa Shinyanga, ili wananchi wapate huduma kwa urahisi.

Nao baadhi ya wananchi waliopewa huduma hiyo akiwamo Happines Wiliamu, amesema tangu mwaka 2013 aligunduliwa kuwa na tatizo la mtoto wa jicho, lakini kutokana na ukosefu wa fedha za matibabu ili bidi akae bila tiba hadi jana ndipo akafanyiwa upasuaji bure, na sasa macho yake yote ni mazima na aona vizuri.

Kwa upande wake Mratibu wa Taasisi ya Bilal Muslim Mission Of Tanzania Free eye Camp, ambaye pia ni kiongozi wa jopo la madaktari hao bingwa wa macho Ain Sharif, kwa kushirikiana na Beta Charitable Trust ya Uingereza, amesema katika Mkoa huo wa Shinyanga wamevunja Rekodi ya utoaji wa matibabu bure ya macho, kuwa ndani ya miaka yao 25 hawajawahi kuwafanyiwa watu 116 upasuaji wa macho kwa siku moja.

Amesema kutokana na bado kuna uhitaji wa watu wengi bado hawajapata matibabu hayo ya macho na muda umeshakwisha, itabidi baadhi ya madaktari wao wabaki kuendelea na huduma hiyo kwa siku kadhaa.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema akizungumza kwenye zoezi la utoaji matibabu ya macho bure, lililoratibiwa na Mbunge wa Vitimaalum Mkoa wa Shinyanga Lucy Mayenga.

Mbunge wa Vitimaalum Mkoa wa Shinyanga Lucy Mayenga akielezea namna alivyoguswa na kuratibu matibabu hayo ya Macho na kuleta madaktari bingwa wa macho mkoani Shinyanga na kutoa huduma bure kwa wananchi.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga Dk. John Luzila akizungumza kwenye uhitimishaji wa zoezi hilo la utoaji matibabu ya macho bure mkoani Shinyanga kutoka kwa madaktari bingwa wa macho.

Mratibu wa Taasisi ya Bilal Muslim Missioni Of Tanzania Free Eye Camp Ain Sharif akielezea namna walivyotoa matibabu hayo ya macho kwa wananchi wa Mkoa wa Shinyanga.

Mwananchi Happines Wiliam akielezea namna alivyopata huduma ya matibabu ya macho na sasa anaona vizuri tofauti na hapo awali.

Mwanachi George Mwandu akielezea namna alivyopata matibabu ya macho.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akiangalia namna wananchi wanavyopata huduma ya matibabu ya macho bure kutoka kwa madaktari bingwa wa macho.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema akipokea maelezo kutoka kwa Madaktari bingwa wa macho namna wanavyotoa huduma.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema akipokea maelezo kutoka kwa Madaktari bingwa wa macho namna wanavyotoa huduma.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema (kushoto) akipokea maelezo kutoka kwa Mratibu wa Taasisi ya Bilal Muslim Mission of Tanzania Free Eye Camp Ain Sharif namna wanavyotoa huduma ya matibabu ya macho.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema (kulia) akipokea maelezo kutoka kwa Mratibu wa Taasisi ya Bilal Muslim Mission of Tanzania Free Eye Camp Ain Sharif namna wanavyotoa huduma ya matibabu ya macho, katikati ni Mbunge wa Vitimaalum Mkoa wa Shinyanga Lucy Mayenga.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema akipima Macho akiwa na Mbunge wa Vitimaalum wa Mkoa huo Lucy Mayenga, alipofanya ziara ya kukagua zoezi la utolewaji matibabu ya macho bure kwa wananchi wa Shinyanga kutoka kwa Madaktari Bingwa wa Macho zoezi lililoratibiwa na Mbunge Lucy Mayenga.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema akipima Macho akiwa na Mbunge wa Vitimaalum wa Mkoa huo Lucy Mayenga, alipofanya ziara ya kukagua zoezi la utolewaji matibabu ya macho bure kwa wananchi wa Shinyanga kutoka kwa Madaktari Bingwa wa Macho zoezi lililoratibiwa na Mbunge Lucy Mayenga.

Afisa wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Jackson Mwakagonda akipima macho.

Zoezi la upimaji macho likiendelea.

Zoezi la upimaji macho likiendelea.

Zoezi la upimaji macho likiendelea.

Zoezi la upimaji macho likiendelea.

Zoezi la upimaji macho likiendelea.

Zoezi la upimaji macho likiendelea.

Zoezi la upimaji macho likiendelea.

Daktari Bingwa wa Macho Nazneen Shariff akimwekea dawa ya macho Mwananchi Chambi Ndinganya.

Matibabu ya macho yakiendelea na uwekaji wa dawa za macho.

Matibabu ya macho yakiendelea na uwekaji wa dawa za macho.
Daktari Bingwa wa Macho Dk, Secodri Njau akitoa elimu ya matumizi ya dawa na namna ya kulinda macho yao kwa wananchi ambao wamefanyiwa upasuaji wa macho.

Wananchi wakiendelea kusikiliza elimu ya matumizi ya dawa na namna ya kulinda macho yao.

Wananchi wakiendelea kusikiliza elimu ya matumizi ya dawa na namna ya kulinda macho yao.

Wananchi wakiendelea kusikiliza elimu ya matumizi ya dawa na namna ya kulinda macho yao.

Baadhi ya Madaktari bingwa wa macho kutoka Taasisi ya Bilali Muslim Mission of Tanzania Free Eye Camp akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema akizungumza na wananchi waliopata matibabu ya macho.

Mbunge wa Vitimaalum Mkoa wa Shinyanga Lucy Mayenga, (kushoto) akimkabidhi msaada wa magongo ya kutembelea Bibi Marry Dotto, ambaye pia alifika kupata huduma ya matibabu ya macho kutoka kwa madaktari bingwa wa macho.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akiwa katika ziara ya kujionea namna wananchi wa Mkoa huo wanavyopata huduma ya matibabu ya macho bure kutoka kwa madaktari bingwa wa macho kutoka Taasisi ya Bilal Muslim Mission Of Tanzania Free Eye Camp, zoezi ambalo limehitishwa leo.
Share:

MLIPUKO MGODINI WAUA WATU 41


Takriban watu 41 wamethibitishwa kufariki baada ya mlipuko kutokea kwenye mgodi wa makaa katika mji wa Amasra kaskazini mwa Uturuki, katika jimbo la pwani la Bartin kwenye Black Sea, maafisa wamesema Jumamosi jioni.


Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uturuki, Suleyman Soylu alilitembea eneo hilo na kutoa habari za ziada kuhusu tukio hilo.


“Tuliondoa mabaki ya watu 40 kwenye migodi yetu, majeruhi wetu tuliwapeleka hospitali. Watu 11 waliojeruhiwa walipatiwa matibabu katika hospitali kadhaa. Kati ya wachimbaji 110, wachimbaji 58 ama waliokolewa wakati juhudi kubwa za kuwatafuta na kuwaokoa waathirika kazi iliyofanywa na timu maalum, au wengine walitoka wenyewe kwenye migodi.”


Uchunguzi kuhusiana na sababu za ajali hiyo tayari zilikuwa zinaendelea, mamlaka zimesema, lakini tathminiya awali iliashiria kwamba mlipuko huo ulisababishwa na gesi maalum ambayo inatumika kwenye mgodi na inaweza kulipuka.


Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan aliitembelea Amasra siku ya Jumamosi na kuthibitisha idadi ya waliofariki wakati akiwa katika ziara kwenye eneo la tukio.

Kiasi cha wachimbaji mkaa 300 waliuawa katika mlipuko mwaka 2014 katika mji wa magharibi wa Soma, kiasi cha kilometa 350 kutoka Istanbul. Ilikuwa ni ajali mbaya sana kuwahi kutokea katika mgodi nchini Uturuki.
Share:

BARAZA LA WAFANYAKAZI PURA LARIDHISHWA UTENDAJI KAZI WA TAASISI


Sehemu ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi PURA wakiwa katika kikao kilicholenga kujadili taarifa za utekelezaji wa Taasisi hiyo kwa mwaka 2021/22 na robo ya mwaka 2022/23. Kikao hicho kilifanyika Jijini Arusha hivi karibuni na kuongozwa na Mwenyekiti wa Baraza hilo, Mha. Charles Sangweni.Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi PURA katika picha ya pamoja mara baada ya kikao. Walioketi kutoka kulia ni Katibu wa TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam (Bi. Sara Rwezaula), Katibu wa TUGHE Tawi la PURA (Mha. Fabian Mwose), Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi PURA (Mha. Charles Sangweni), Katibu Msaidizi wa Baraza la Wafanyakazi PURA (Bw. Ebeneza Mollel) na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Taasisi PURA (Bw. Rogasian Ngumbi)

Sehemu ya Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi PURA wakifuatilia taarifa zilizokuwa zikiwasilishwa katika kikao hicho

Mjumbe wa Baraza kutoka Idara ya Ufundi, Bw. Paul Matumbi akiwasilisha taarifa za idara hiyo wakati wa kikao cha Baraza.

************************

Baraza la Wafanyakazi la Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) limesema limeridhishwa na utendaji kazi wa Taasisi hiyo na kuwapongeza watumishi kwa kuifanya Taasisi iendelee kutekeleza majukumu yake kwa ufasaha na ufanisi.

Hayo yamesemwa wakati wa kikao cha Baraza la Wafanyakazi PURA kilichofanyika hivi karibuni Jijini Arusha kwa lengo la kupokea na kujadili taarifa za utekelezaji kutoka idara na vitengo vya Taasisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2021/22 na robo ya mwaka wa fedha 2022/23.

Akizungumza katika kikao hicho, Katibu wa TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam (Ms. Sara Rwezaula) ambaye ni mjumbe wa Baraza amesema kuwa utendaji wa Mamlaka hiyo umeendelea kuimarika mwaka hadi mwaka, jambo ambalo linastahili pongezi.

"Nipende kutumia fursa hii kuwapongeza wafanyakazi wote wa PURA kwa kufanya kazi kwa bidii kufikia malengo ya Taasisi. Kupitia Taarifa tulizozipokea na kujadili tumeona dhahiri kuwa Taasisi imekuwa na utendaji unaoridhisha. Pongezi nyingi pia kwa menejimenti ya PURA kwa kuendelea kuboresha mazingira ya kazi, jambo muhimu katika kufanikisha utendaji"

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi PURA ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo, Mha. Charles Sangweni amesema pongezi zilizotolewa ni chachu kwa wafanyakazi wa PURA kuendelea kufanya kazi kwa bidii zaidi ili kufikia malengo kama yalivyo katika Mpango Mkakati wa Taasisi.

"Nipende kutumia fursa hii kuwahimiza wafanyakazi wote wa PURA kuendelea kufanya kazi kwa bidii, weledi na kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma. Tusibweteke kwa pongezi hizi bali ziwe kichocheo kwa sisi kufanya vizuri zaidi na zaidi" alieleza Mha. Sangweni.

Baraza la Wafanyakazi PURA linaundwa na wajumbe 34 na lilizinduliwa rasmi mwezi Novemba, 2022. Miongoni mwa wajumbe wa Baraza hilo ni Katibu TUGHE Taifa, Katibu TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam, menejimenti ya PURA na wawakilishi kutoka idara na vitengo vya Taasisi.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI OKTOBA 16,2022


Magazetini leo Jumapili October 16 2022





Share:

Saturday, 15 October 2022

NEWALA MJI YAANZA KUTEKELEZA MAAGIZO YA WAZIRI WA ARDHI

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Newala mkoani Mtwara Shamim Daudi Mwariko (kulia) alikabidhiwa hatimiliki za ardhi saba na Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Mtwara Rehema Mwinuka mkoani Mtwara jana.
Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Mtwara Rehema Mwinuka (kulia) akimsikiliza mmoja wa wateja wakati Ofisi ya Ardhi Mkoa ilipotoa huduma jumuishi za sekta ya ardhi. Watumishi wa sekta ya ardhi wakitoa huduma za ardhi katika kituo jumuishi Mtwara.

Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Mtwara Rehema Mwinuka akiwa katika picha ya pamoja na wananchi aliowakabidhi hati (PICHA NA WIZARA YA ARDHI)

**************************

WANMM, MTWARA

Halmashauri ya Mji wa Newala mkoa wa Mtwara imeanza kutekeleza maagizo ya Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula ya kuzitaka halmashauri zote nchini kuhakikisha zinapima na kumilikishwa maeneo yake yakiwemo ya shule, zahanani na vituo vya mabasi ili kuepuka migogoro ya ardhi.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Newala Shamim Daudi Mwariko alikabidhiwa jumla ya hati saba na Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Mtwara Rehema Mwinuka ambapo hati tano kati ya alizokabidhiwà ni za shule za msingi na hati mbili ni za zahanati.

Shule za msingi zilizopata hatimiliki za ardhi ni Mtangalanga, Kiduni, Butiama, Mcholi II na Mkoma I huku upande wa zahanati zikiwa ni Mkoma I na ile ya Makondeko.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi hati hizo mkoani Mtwara jana Kamishna wa Ardhi mkoa wa Mtwara Rehema Mwinuka aliipongeza halmashauri ya Mji wa Newala kwa uamuzi wa kupimiwa maeneo yake na kuzitaka halmashauri nyingine katika mkoa huo kuiga mfano wa halmashauri hiyo kwa kupima na kumilikishwa maeneo yake ili kuepuka uvamizi katika maeneo hayo.

"Nichukue fursa hii kuwapongeza halmashauri ya Mji wa Newala kwa uamuzi wenu wa kupima maeneo yenu, hii itasaidia sana kupunguza migogoro ya ardhi inayotokana na uvamizi na niombe hakmashauri nyingine ziige mfano wenu" alisema Rehema.

Mbali na kukabidhi hati kwa halmahauri ya Mji wa Newala kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Mtwara aliwaongoza watumishi wa mkoa wake kutoa hati kwa wamiliki wa ardhi waliokamikisha taratibu za kupatiwa hati sambamba na kusikiliza na kutatua changamoto za sekta ya ardhi katila kituo jumuishi.

Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeanzisha utaratibu wa ofisi zake za ardhi katika mikoa kuwa na vituo jumuishi vya kusikiliza na kutatua changamoto za ardhi pamoja na kutoa hatimiliki za ardhi ikiwa ni juhudi za kusogeza huduma karibu na wananchi.
Share:

WAFANYAKAZI TASAF WAKUSANYA MIL.3.2/- KUSAIDIA WAGONJWA OCEAN ROAD

Ofisa Ustawi wa Jamii wa Taasisi ya Saratani Ocean Road, Justine Chambo akiwashukuru na kujibu baadhi ya maswali ya wafanyakazi wa TASAF waliotoa msaada wa vifaa na dawa kwa wagonjwa waliolazwa kwenye taasisi hiyo.

Baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kukabidhi msaada huo kwa wagonjwa waliolazwa kwenye Taasisi ya Saratani Ocean Road jijini Dar es Salaam leo Oktoba 15,2022.

**********************

Na Irene Mark

WAFANYAKAZI wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), wametoa msaada wa dawa na vifaa mbalimbali vyenye thamani ya sh. 3,247,800 kwa ajili ya wagonjwa waliolazwa katika Taasisi ya Saratani Ocean Road jijini Dar es Salaam.

Msaada huo umetolewa leo Oktoba 15,2022 na baadhi ya wafanyakazi ambao walipata fursa ya kuwaona, kuzungumza na kuwapa msaada wagonjwa waliolazwa kwenye taasisi hiyo.

Akizungumza baada ya kukabidhi msaada kwa wagonjwa, mwakilishi wa wafanyakazi wa TASAF, Marylinda Meero amesema wafanyakazi wanaguswa na matatizo ya wananchi hivyo wamejichangisha fedha hizo ili kuwasaidia wenye uhitaji zaidi.

Meero amesema jumla ya fedha iliyopatikana iligawanywa kwenye manunuzi ya vifaa na dawa za wagonjwa kama walivyoelekezwa na uongozi wa Taasisi ya Saratani Ocean Road.

“Ni wafanyakazi tumeguswa tukaona ni vema kuja hapa kwa kuwa wapo wahitaji ambao hawana uwezo ndio maana tumejichangisha tukapata sh. 3,247,800.

“...Tumefuata ushauri wa hospitali tumenunua vifaa ambavyo ni sabuni za unga, miche, dawa za miswaki, miswaki yenyewe, maji ya kunywa, malapa na ‘dypers’ za wakubwa.

“Jumla ya sh. 627,000 tumenunua vifaa na iliyobaki sh. 2,600,800 tumenunua dawa mbalimbali kwa ajili ya wagonjwa wetu na sisi wachache tumewawakilisha wenzetu wengi kuja hapa leo.

“Tunaushukuru uongozi wa Taasisi ya Ocean Road na wafanyakazi wenzangu kwa msaada huu na muda wao kwa kweli tumefarijika kuwashika mkono wagonjwa tunawaombea kwa Mungu awaponye,” amesema Meero.

Ofisa Ustawi wa Jamii wa Taasisi ya Ocean Road, Justine Chambo amewashukuru wafanyakazi wa TASAF kwa ukarimu na kuwakumbuka wagonjwa huku akiwaombe heri na afya njema wote walioshiriki kwa michango na muda wao.

Chambo amesema msaada huo umewafariji wagonjwa na kuwapa tabasamu licha ya maumivu makali wanayopitia.

Kwa mujibu wa Chambo, asilimia 70 ya matibabu yote mpaka chakula katika taasisi hiyo hutolewa bure hivyo wanapopata msaada kutoka kwa jamii wanashukuru na wanapata moyo zaidi wa kuwahudumia wagonjwa hao.

“Tunapotembelewa kama hivi na sisi watoa huduma tunafurahi na kufarijika pia kuona kwamba jamii inatambua mchango wetu. Mungu awabariki na msichoke kutusaidia,” amesema Chambo.
Share:

UHURU FM, TANCDA WAZINDUA KAMPENI YA KUKABILIANA NA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA.

Meya wa Jiji la Dar es salaam, Mh.Omary Kumbilamoto akiwaongoza watumishi wa Uhuru Fm pamoja na Shirikisho la vyama vya magonjwa yasioambukiza Tanzania-TANCDA kwenye Jogging katika uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha wananchi kufanya mazoezi mara kwa mara ikiwa ni njia moja wapo ya kujikinga na magonjwa yasioambukiza iliyofanyika leo Oktoba 15,2022 Jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Ilala, Said Sultan Sidde akifanya usafi kwenye Zahanati ya Vingunguti katika uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha wananchi kufanya mazoezi mara kwa mara ikiwa ni njia moja wapo ya kujikinga na magonjwa yasioambukiza iliyofanyika leo Oktoba 15,2022 Jijini Dar es Salaam. Meya wa Jiji la Dar es salaam, Mh.Omary Kumbilamoto akifanya usafi kwenye Zahanati ya Vingunguti katika uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha wananchi kufanya mazoezi mara kwa mara ikiwa ni njia moja wapo ya kujikinga na magonjwa yasioambukiza iliyofanyika leo Oktoba 15,2022 Jijini Dar es Salaam. Meya wa Jiji la Dar es salaam, Mh.Omary Kumbilamoto na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Ilala, Said Sultan Sidde wakipata picha ya pamoja na watumishi wa Uhuru Fm pamoja na Shirikisho la vyama vya magonjwa yasioambukiza Tanzania-TANCDA katika uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha wananchi kufanya mazoezi mara kwa mara ikiwa ni njia moja wapo ya kujikinga na magonjwa yasioambukiza iliyofanyika leo Oktoba 15,2022 Jijini Dar es Salaam. Meya wa Jiji la Dar es salaam, Mh.Omary Kumbilamoto na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Ilala, Said Sultan Sidde wakipata picha ya pamoja na watumishi wa Uhuru Fm pamoja na Shirikisho la vyama vya magonjwa yasioambukiza Tanzania-TANCDA katika uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha wananchi kufanya mazoezi mara kwa mara ikiwa ni njia moja wapo ya kujikinga na magonjwa yasioambukiza iliyofanyika leo Oktoba 15,2022 Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

*******************

Na Mwandishi wetu, 15.10.2022

Katika kukabiliana na magonjwa yasiambukiza, Uhuru fm kwa kushirikiana na Shirikisho la vyama vya magonjwa yasioambukiza Tanzania-TANCDA, wamezindua kampeni ya kuhamasisha wananchi kufanya mazoezi mara kwa mara ikiwa ni njia moja wapo ya kujikinga na magonjwa yasioambukiza.

Kampeni hiyo imezinduliwa na Meya wa Jiji la Dar es salaam, Mh.Omary Kumbilamoto kwa kufanya maazoezi ya Jogging kuanzia Buguruni Sheli hadi Vingunguti iliyoshirikisha vikundi mbalimbali vya Jogging na kisha baadaye kufanya usafi katika Hospitali ya Vingunguti.

Katika uzinduzi wa kampeni hiyo ya magonjwa yasiyoambukizwa alikuwepo pia Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Ilala, Said Sultan Sidde.

Chini ya mpango huo wa kuhamasisha wananchi kufanya mazoezi zaidi ili kujikinga na magonjwa yasioambukiza, Meya wa Jiji la Dar es salaam, Kumbilamoto, ameiomba jamii kufanya mazoezi ili kujikinga ma magonjwa hayo ambayo yamekuwa ni tishio hapa nchini na Duniani kwa ujumla.

Magonjwa yasioambukiza ni pamoja na Kisukari, Saratani, Kiharusi, maradhi ya Moyo, pamoja na Figo.

Aidha, kwa mujibu wa kitabu cha TANCDA, dalili za magonjwa yasioambukiza ni pamoja na kuchoka bila sababu, kichwa kuuma, kuona kizunguzungu, kutoona vizuri, ganzi ya meno, kupumua kwa shida, moyo kwenda kwa haraka, kutokwa na damu sehemu yoyote, kukosa pumzi wakati wa kulala pamoja na vidonda visivyopona.

Kutokana hali hiyo jamii imetakiwa kufanya mazoezi mara kwa mara angalau mara tatu kwa wiki.

Naye Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala, Sidde, ameishukuru Uhuru Fm kwa kuwa na kampeni hiyo ambayo amesema itasaidia jamii kujenga tabia ya kufanya mazoezi ili kuweka miili yao sawa kiafya. Naye Mhariri Mkuu wa Uhuru FM, Pius Ntiga, akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Uhuru Fm, Amina Azizi, amesema kampeni hiyo itakayokuwa ikifanyika kila mwisho wa wiki itakuwa ni mwendelezo lengo pia likiwa ni kuisaidia pia jamii kubadili mtindo wa maisha hasa katika ulaji wa vyakula na kuwasisitiza kufanya mazoezi ili kjjikinga na magonjwa yasioambukiza.

"Hii ni awamu ya pili ya Jogging ya Uhuru fm, ambapo awamu ya kwanza tulijikita zaidi katika masuala ya sensa ya watu na makazi 2022, ambayo kwa kiasi kikubwa tulifanukiwa, tukaona tusiishie hapo na sasa yaani leo tumezindua tena Jogging itakayojikita katika magonjwa yasiyoambukiza, tuhamasishe jamii ifanye mazoezi" alisema Ntiga.

Aidha, Ntiga amevishukuru vikundi mbalimbali vilivyojitokeza katika uzinduzi huo ikiwemo Jogging ya Vingunguti, Miembeni, Ukonga, pamoja na Tabata veteran.
Share:

AMFUATA MKEWE KAZINI KISHA KUMUUA KISA HATAKI WARUDIANE

 Mwanaume mmoja amemfuata mke wake kazini eneo la Mai Mahiu na kumuua baada ya mwanamke huyo kukataa ombi lake la kurudiana naye.


Kwa mujibu wa Idara ya Upelelezi wa Jinai nchini Kenya (DCI), mshukiwa alimuua Veronicah Wanjiru baada ya kugundua kuwa hakuwa tayari kwa maridhiano.

Ripoti ya DCI inasema kuwa mshukiwa alijaribu kujiangamiza kwa kujidunga lakini hakufanikiwa, kwa sasa akiwa amelazwa hospitalini.

Idara hiyo inasubiri mshukiwa apone kabla ya kumfikisha mahakamani kwa mashtaka ya kumuua mke wake.

Wanjiru alishambuliwa katika eneo la burudani la Club 8 alikofanya kazi ya usafi.

“Wanjiru alikuwa akisafisha eneo hilo, mumewe alipofika na kumwomba kusuluhisha mzozo wao na warudiane lakini akakataa,” taarifa ya DCI inasema.

Baada ya ombi lake la kurudiana kukataliwa, mwanamume huyo alichomoa kisu cha kukata mboga alichokuwa nacho mfukoni.

Alimdungadunga mwendazake mara kadhaa shingoni na kumuua papo hapo.

“Kisha akaamua akaamua kujidunga kwa kisu hicho. Alijidunga kwenye mbavu zake kwa lengo la kujiua. Hata hivyo, hakufanikiwa kujiangamiza,” DCI inasema.

Kwa sasa mshukiwa amelazwa katika hospitali ya Mai Mahiu akiwa katika hali mahututi.
Share:

NIMEMFUMANIA MKE WANGU GESTI NA RAFIKI YANGU WA KARIBU SANA

Share:

Friday, 14 October 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI OKTOBA 15,2022











Share:

KAMATI YA BUNGE YA BAJETI YAKAGUA SHUGHULI ZA UPAKUAJI NA UPIMAJI MAFUTA DAR ES SALAAM

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti wakiwa katika eneo la gati ya kushushia mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam mara baada ya kufika bandarini hapo kuona jinsi shughuli za ushushaji na upimaji mafuta zinavyofanyikaMwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Mhe. Daniel Sillo akizungumza jambo wakati Kamati hiyo ikiwa katika sehemu ambayo inaruhusu mafuta kutoka kwenye meli kwenda kwenye sehemu za kuhifadhia mafuta zinazomilikiwa na kampuni mbalimbali zinazofanya biashara ya mafutaWajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti wakiwa katika eneo la kupima mafuta katika eneo la Kigamboni mkoani Dar es Salaam.

Baadhi ya miundombinu iliyopo katika eneo lililofungwa mita za kupimia mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam.

.........................

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti imefanya ziara katika maeneo yanayotumika kupakua mafuta kutoka kwenye Meli na kupima katika Bandari ya Dar es Salaam na Kigamboni mkoani Dar es Salaam.

Ziara hiyo ilifanyika tarehe 13 Oktoba, 2022 ikiwa na lengo la kujihakikishia kuwa kazi za ushushaji wa mafuta na upimaji mafuta katika sehemu hizo zinafanyika kwa ufanisi na Serikali inapata mapato stahiki.

Baada ya kufanya ukaguzi huo, Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti, Mhe.Daniel Sillo, aliipongeza Serikali kwa jinsi ilivyowekeza katika miundombinu ya ushushaji wa mafuta pamoja na mita za kupimia mafuta hayo ambazo kwa miaka ya nyuma zilikuwa hazipo na hivyo Serikali ilikuwa haipati mapato stahiki.

Alisema kuwa, mita hizo za kupimia mafuta licha ya kuiwezesha Serikali kupata mapato inayostahili, kampuni zinazoagiza mafuta hayo kutoka nje ya nchi pia zinapata uhakika wa kiasi cha mafuta ambacho wamekiagiza.

Vilevile alisema kuwa, Kamati hiyo ilifanya ziara katika Bandari ya Mtwara ambapo pia Wajumbe walishuhudia juhudi zinazofanywa na Serikali katika kuiendesha sekta ya mafuta kwa ufanisi kwani mita za kupimia mafuta katika bandari hiyo zinafanya kazi vizuri na pia upanuzi wa bandari pamoja na sehemu za kuhifadhia mafuta unaendelea vizuri hali itakayofanya bandari hiyo kupokea mafuta kwa wingi zaidi.
Share:

MTAYARISHAJI NGULI WA MUZIKI KUTOKA NIGERIA MASTERKRAFTS KUJA NA EP


Sunday Ginikachukwu Nweke maarufu kwa jina la Masterkraft mtayarishaji wa muziki kutoka nchini Bigeria ambaye amefanikiwa kufanya kazi na wasanii mbalimbali kutoka nchini Nigeria akiwemo Mr Flavour,Davido ,Tekno,Phyno na wengine wengi yuko mbioni kuachia kazi yake mpya rasmi

Mbali na kuwa mtayarishaji wa Muziki Masterkraft ni mwandishi wa nyimbo ,muongozaji wa bendi pamoja na mwimbaji.

Masterkraft 

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger