Friday, 2 September 2022

RC MJEMA AONGOZA KIKAO CHA TATHMINI UTEKELEZAJI MKATABA WA LISHE, CHANJO YA UVIKO -19 NA POLIO SHINYANGA...AGEUKA MBOGO UPATIKANAJI TAKWIMU

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akizungumza wakati akifungua kikao cha Tathmini ya  Utekelezaji wa Mktaba wa Lishe kwa kipindi cha 2021/2022 na Kampeni ya Polio kwa awamu ya tatu kwa watoto chini ya miaka mitano. 

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema ameziagiza Halmashauri za wilaya katika mkoa huo zitoe shilingi 1000 kwa kila mtoto aliye chini ya miaka mitano kila mwezi na kufanya vikao vya tathmini ya lishe ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mkataba wa Lishe.

Mjema ametoa agizo hilo leo Ijumaa Septemba 2,2022 wakati wa Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji wa Mktaba wa Lishe kwa kipindi cha 2021/2022 na Kampeni ya Polio kwa awamu ya tatu kwa watoto chini ya miaka mitano iliyoanza Septemba 1,2022.

Mjema amesema kikao hicho cha tathmini ni fursa ya kujipima na kuchukua hatua kwa kila halmashauri kubaini changamoto zinazokwamisha ili wazifanyie kazi na kuondokana na hali isiyoridhisha ya utekelezaji wa afua za lishe.

“Tukumbuke kuwa Lishe bora na Chanjo ya Polio ni msingi wa maendeleo ya taifa letu, nawatakia Utekelezaji mwema wa Kampeni ya Polio na shughuli za lishe ili kufikia lengo la uchanjaji na utekelezaji wa mkataba wa lishe”,amesema Mjema.

“Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan inaendelea na utekelezaji wa mkataba wa Lishe kupitia Mikoa, Halmashauri, kata na Vijiji/mitaa tangu mwaka 2018, utekelezaji huu wa mkataba wa Lishe umewezesha kuboresha utoaji wa huduma za lishe kwa wananchi”, ameongeza.

Amesema lengo la Mkataba wa Lishe ni kusimamia utekelezaji wa maelekezo ya serikali ya kutenga na kutumia shilingi 1000 kwa kila mtoto mwenye umri chini ya miaka mitano kwa ajili ya kutekeleza afua za lishe ngazi ya halmashauri.

“Katika utekelezaji wa Mkataba wa Lishe ngazi ya halmashauri kwa kipindi cha Julai 2021 hadi Juni 2022, mkoa wa Shinyanga umetoa fedha kwa asilimia 76.56 ambapo Manispaa ya Shinyanga imeongoza kwa utoaji wa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa afua za lishe kwa kutoa fedha kwa asilimia 100”,amefafanua.

Mkuu huyo wa Mkoa amewapongeza Wakuu wa Wilaya na viongozi wengine kwa kusimamia mkataba wa lishe na kufanya vikao vya tathmini kila baada ya miezi mitatu kama mwongozo unavyoelekeza.

Akizungumzia kuhusu Kampeni ya Chanjo ya Polio kwa awamu ya tatu iliyoanza Septemba 1,2022 , Mjema amesema Kampeni hiyo itafanyika hadi Septemba nyumba kwa nyumba ambapo walengwa kimkoa ni 445,681 walio chini ya miaka mitano.

Amesema Chanjo zinazotolewa na Serikali ni salama na zimedhibitishwa na Wizara ya Afya pamoja na Shirika la Afya Duniani (WHO) hivyo kuwaomba wadau wa afya kukanusha upotoshaji wowote unaoweza kujitokeza katika jamii kuhusu kampeni za chanjo pamoja na kuhamasisha wananchi kupata chanjo na kusimamia shughuli zote za utekelezaji wa kampeni za chanjo.

“Kwenye eneo la utoaji wa Chanjo za UVIKO 19, Mkoa unaendelea na utoaji wa chanjo hizo. Walengwa wa chanjo za UVIKO -19 ni watu walio chini ya umri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea ambao kimkoa ni 1,011,085 na hadi kufikia Agosti 31,2022 wateja wapatao 735,844 wamepata kinga kamili dhidi ya ugonjwa wa UVIKO – 19 ambao ni sawa na asilimia 73 na kufanya mkoa wetu kushika nafasi ya tano kitaifa”, ameeleza Mjema.

“Kwa upande wa dirisha la dawa kwa wazee, tuhakikishe wazee wanapata dawa, malalamiko yapungue, wazee wapate dawa”,amesema.

Mjema pia ameziagiza halmashauri za wilaya kuhakikisha zinatoa takwimu kwa wakati

“Nimeona kuna tatizo kubwa la Takwimu kwenye Halmashauri zetu, hili donda ndugu nataka liondoke, kwenye kutoa taarifa naona kuna tatizo,unakuta kazi imefanywa vizuri sana lakini changamoto inakuja kwenye takwimu”,amesema

“Mimi sitaki kuona tena tatizo la takwimu, takwimu zikihitajika nataka tuzipate haraka, hili tatizo la taarifa sitaki kulisikia, zikitakiwa mkoani lazima tuzipate, hii iwe mwisho. Haiwezekani Mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya , kamati ya usalama inahangaika kutafuta takwimu…. Wafichueni wanaokwamisha, ukijiona wewe ni Slow Learner tuambie tukusaidie.

“Nataka takwimu ziwe zinakuja kwa wakati na zinaenda kwa wakati, hatuhitaji kugombana kuhusu takwimu, Mhe, RAS Ondoa mtu anayekwamisha, hatutaki kurudishwa nyuma” ,amesema Mjema.

“Siyo kazi ya Mkuu wa Mkoa, Kamati ya Usalama, Mkuu wa Wilaya kwenda kuhangaika kutafuta takwimu.. Unapochelewesha takwimu unakwamisha mambo, RAS niondolee watu wanaokwamisha upatikanaji wa takwimu. Tunataka kila mmoja afanye kazi, hatutawavumilia wanaoturudisha nyuma, ni lazima tumsaidie Mhe. Rais Samia Suluhu ambaye anafanya jitihada kubwa za kuleta fedha kwa ajili ya maendeleo”,ameongeza Mjema

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akizungumza leo Ijumaa Septemba 2,2022 wakati akifungua kikao cha Tathmini ya Utekelezaji wa Mktaba wa Lishe kwa kipindi cha 2021/2022, Chanjo ya UVIKO - 19 na Kampeni ya Polio kwa awamu ya tatu kwa watoto chini ya miaka mitano. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akizungumza leo Ijumaa Septemba 2,2022 wakati akifungua kikao cha Tathmini ya Utekelezaji wa Mktaba wa Lishe kwa kipindi cha 2021/2022, Chanjo ya UVIKO - 19 na Kampeni ya Polio kwa awamu ya tatu kwa watoto chini ya miaka mitano.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza kwenye kikao cha Tathmini ya Utekelezaji wa Mktaba wa Lishe kwa kipindi cha 2021/2022, Chanjo ya UVIKO - 19 na Kampeni ya Polio kwa awamu ya tatu kwa watoto chini ya miaka mitano.

Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga akizungumza kwenye kikao cha Tathmini ya Utekelezaji wa Mktaba wa Lishe kwa kipindi cha 2021/2022, Chanjo ya UVIKO - 19 na Kampeni ya Polio kwa awamu ya tatu kwa watoto chini ya miaka mitano.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akiongoza kikao cha Tathmini ya Utekelezaji wa Mktaba wa Lishe kwa kipindi cha 2021/2022, Chanjo ya UVIKO - 19 na Kampeni ya Polio kwa awamu ya tatu kwa watoto chini ya miaka mitano.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile akizungumza kwenye kikao cha Tathmini ya Utekelezaji wa Mktaba wa Lishe kwa kipindi cha 2021/2022, Chanjo ya UVIKO - 19 na Kampeni ya Polio kwa awamu ya tatu kwa watoto chini ya miaka mitano.

Wadau wa afya wakiwa kwenye kikao cha Tathmini ya Utekelezaji wa Mktaba wa Lishe kwa kipindi cha 2021/2022, Chanjo ya UVIKO - 19 na Kampeni ya Polio kwa awamu ya tatu kwa watoto chini ya miaka mitano.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Share:

RAIS SAMIA AZINDUA MAABARA YA SAYANSI SKULI YA KIZIMKAZI ILIYOJENGWA NA BENKI YA CRDB

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suhuhu Hassan (watatu kushoto) kwa pamoja na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Lela Mohammed Musa (wapili kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela wakikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Maabara ya Sayansi katika Skuli ya Sekondari ya Kizimkazi yenye thamani ya Sh. Milioni 50 iliyojengwa kwa msaada wa Benki ya CRDB  leo Agosti 02, 2022. Wengine pichani kutoka kulia ni Waziri wa Utumishi na Utawala bora Zanzibar, Haroun Ali Suleiman, Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Abdalla Juma Sadala pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Rashid Hadid Rashid.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suhuhu Hassan kwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela wakifungua kitambaa kwenye jiwe la msingi  kuashiria uzinduzi rasmi wa Maabara ya Sayansi katika Skuli ya Sekondari ya Kizimkazi yenye thamani ya Sh. Milioni 50 iliyojengwa kwa msaada wa Benki ya CRDB  leo Agosti 02, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suhuhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Lela Mohammed Musa (kulia), wakati wa uzinduzi rasmi wa Maabara ya Sayansi katika Skuli ya Sekondari ya Kizimkazi yenye thamani ya Sh. Milioni 50 iliyojengwa kwa msaada wa Benki ya CRDB  leo Agosti 02, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suhuhu Hassan akifurahia burudani kutoka kwa wanafunzi wa Skuli ya maandalizi Kizimkazi wakati wa uzinduzi rasmi wa Maabara ya Sayansi katika Skuli ya Sekondari ya Kizimkazi yenye thamani ya Sh. Milioni 50 iliyojengwa kwa msaada wa Benki ya CRDB  leo Agosti 02, 2022. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suhuhu Hassan akipata maelezo ya mradi wa maabara kutoka kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa, wakati wa uzinduzi rasmi wa Maabara ya Sayansi katika Skuli ya Sekondari ya Kizimkazi yenye thamani ya Sh. Milioni 50 iliyojengwa kwa msaada wa Benki ya CRDB  leo Agosti 02, 2022. 

Share:

DARAJA LA ESURI LALETA UKOMBOZI KWA WANANCHI OLORESHO

Wananchi wa Oloesho katika kata ya Olasiti na Olmoti, Halmashauri ya Jiji la Arusha wamepata faraja na kufurahia ujenzi wa daraja la Esuri lenye urefu wa meta 17 na upana wa meta nane (8) lililojengwa na Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) kwa takribani shilingi 335,092,557.00.

Akisoma taarifa ya ujenzi wa daraja hilo kwa Bodi ya Ushauri ya TARURA wakati wa ziara ya ukaguzi, meneja wa TARURA Mkoa wa Arusha Mhandisi Laynas Sanya alisema kuwa daraja hilo lenye uwezo wa kuhimili uzito wa tani 30, litarahisisha huduma ya usafiri kwa wananchi kutoka kata ya Olasiti na Olmoti na maeneo mengine ya jirani na kuondoa adha ya kutopitika kwa barabara kipindi cha mvua.

Inoti Shedrack, mkazi wa Oloresho alisema kuwa walikuwa wanateseka sana kabla ya daraja halijajegwa, hasa wakina mama na watoto lakini kwa sasa wanamshukuru Mugu daraja limekua ni mkombozi kwao.

“Tumejengewa daraja ambalo sasa hivi hatusumbuki kabisa na watoto wanaenda shule bila shida yoyote. Sisi wananchi wa Oloresho tunaishukuru sana Serikali na TARURA kwa kutengeneza daraja na barabara hii,” alisema Inoti.

Naye Mhe. Alex Martin diwani wa kata ya Olasiti alisema wanaishukuru sana TARURA kwa kutengeneza daraja hilo kwasababu walikuwa wakipata shida sana wakati wa mvua, na wakinamama wengi walikuwa wakijifungua watoto wao eneo hilo kwa wakunga wa kienyeji kutokana na kushindwa kuvuka kwenda hospitali.

“Kwa kweli tunaishukuru Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa sababu tumejengewa daraja hili ambalo limekuwa ni ukombozi kwetu kwa kutupunguzia adha tulizokuwa tunazipata,” alisema Alex.

Naye Mhe. Mrisho Gambo mbunge wa Arusha mjini alisema kuwa kwao imekuwa kama ndoto kwasababu walizoea kuona TANROAD ndiyo wanaweza kujenga madaraja yenye viwango bora kama hilo. 
“Tumeona kuwa kumbe TARURA ikiwezeshwa inaweza kufanya mambo makubwa zaidi na kuwafikia wananchi wengi zaidi. Tunaishukuru sana bodi yako mwenyekiti; mtendaji mkuu pamoja na watumishi wa TARURA ambao wametoa ushirikiano mkubwa sana kukamilika kwa daraja hili. Niwasihi madiwani wangu tuendelee kuiamini TARURA na wataendelea kufanya mambo makubwa tukiwaunga mkono,” alisema Mhe. Gambo.

Kwa upande wake Mhandisi Florian Kabaka, Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya TARURA aliwashukuru wananchi pamoja na mbunge kwa kutambua na kuona kazi ambayo TARURA inafanya ya kuwahudumia wananchi na kurahisisha utoaji huduma kupitia barabara.

“Nimefarijika sana kuona daraja hili limewanufaisha sana sasa watu hawachukui muda mrefu sana kama zamani, wanaweza kukatisha hapa na kufika wanapotaka kwenda kwa urahisi na kupata huduma zao, na hili ndilo lengo la TARURA,”alisema Mhandisi Kabaka.

Aidha aliwashukuru wananchi kwa kutambua kuwa Rais Samia Suluhu Hassan anawapenda na kuwajali kwa kuwawezesha TARURA kuwafikia na akaahidi kuwa TARURA itaendelea kuboresha zaidi kadiri inavyowezeshwa.

Mhandisi Victor Seff, Mtendaji Mkuu wa TARURA aliwaasa viongozi na wananchi wa eneo hilo kuilinda miundo mbinu hiyo na hasa alama za usalama zilizowekwa ili ziwanufaishe wao pamoja na vizazi vijavyo.

Share:

BODABODA AKATWA SHINGO, APORWA PIKIPIKI BUNDA

Na Adelinus Banenwa - Bunda
Mtu mmoja ambaye ni dereva bodaboda aliyetambulika kwa jina la ISSA SAGUDA (22) mkazi wa Rubana kata ya Balili, Halmashauri ya Mji wa Bunda mkoani Mara amekutwa amepoteza Maisha kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali shingoni na tumboni maeneo ya shule ya msingi Rubana.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia tarehe 29/8/2022.

Mashuhuda wa tukio hilo wakizungumza na radio Mazingira Fm katika eneo la tukio wamesema wanafunzi waliokuwa wanaenda shule ndo waliogundua kuwepo kwa mwili huo.

“Ilikuwa asubuhi kwenye muda wa saa Moja wanafunzi walikuja kutuita kwamba kuna mtu amekatwa shingo amelala karibu na choo tukaamka haraka na tulipofika tukamuangalia alivyovaa mbele kidogo tukaona alama za break ya pikipiki na pembeni kuna damu na funguo za pikipiki ndipo tulipogundua kwamba huyu ni dereva bodaboda”, amesema shuhuda.

Kwa upande wake mwenyekiti wa waendesha pikipiki maalufu (bodaboda) Wilaya ya Bunda Dickson Joseph amesema tayari wamemtambua.

“Ni bodaboda mwenzetu alikuwa anapaki kwenye kituo Cha NM Bunda Mjini nimepigiwa simu asubuhi kwamba mwenzetu amekutwa amepoteza Maisha na pikipiki imeibiwa ndo nimefika hapa”

Dickson ameongeza kuwa suala ulinzi kwa bodaboda juu ya wateja hasa nyakati za usiku wameshaambizana kutokubali kubeba abiria bila wenzao kuwa na taarifa za mteja unayembeba anatoka wapi na anakwenda wapi.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Balili Mhe Thomas Tamka amesema mauaji yaliyotokea katika kata yake yanaumiza sana na hayakubariki amesema yeye kama mwenyekiti wa kamati ya maendeleo ya kata ataitisha kikao ili suala la ulinzi shirikishi uanze mara Moja

Baada ya mauji ya kijana Issa Saguda na kuporwa pikipiki katika mtaa wa Rubana Kata ya Balili Halmashauri ya mji wa Bunda, jeshi la Polisi limesema pikipiki hiyo imepatika eneo la Nyamikoma Wilayani Busega Mkoani Simiyu

Akizungumza na Radio Mazingira Fm Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Kamishina Msaidizi wa Polisi Dismas Kisusi amesema pikipiki hiyo yenye namba za usajili MC 499 CDH aina King lion ilikamatwa na walinzi shirikishi usiku wa tarehe 29 Agosti 2022 masaa machache baada ya kutendeka tukio hilo huku mtuhumiwa akifanikiwa kutoroka.

Amesema Jeshi la Polisi linaendelea kuwasaka waliohusika na mauaji hayo huku likitoa wito kwa wananchi kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama ili kukomesha vitendo hivyo.

CHANZO - RADIO MAZINGIRA FM
Share:

WAWEKEZAJI ARUSHA WAMWAGIA SIFA RAIS SAMIA UJENZI WA BARABARA ZA TARURA

Wawekezaji na wananchi wa kata ya Themi, Halmashauri ya Jiji la Arusha wamemsifu na wamempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali na kuwajengea kwa kiwango cha lami barabara za Themi -Viwandani zenye urefu wa kilometa 1.4 kwagharama ya shiligi 1,175,141,850.00.

Pongezi hizo zimetolewa wakati wa ziara ya kukagua miradi ya ujenzi wa barabara na madaraja jijini Arusha iliyofaywa na bodi ya ushauri ya Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA).

Akitoa pongezi hizo mkurugenzi wa “Spanish Tiles” Bobby Chadha alisema kuwa anamshukuru sana Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali na kuwapatia barabara nzuri na bora za lami maeneo ya viwandani. 

“Ninamshukuru sana rais kwa sababu kwa mara ya kwanza tumepata barabara hizi za lami kwa zaidi ya miaka 40 niliyokuwa hapa. Barabara hizi zitasaidia sana kupungza gharama za usafiri, kukuza biashara 
na pia kupendezesha mji,” alisema Bobby.

Naye ndugu Satbir Hanspaul mkurugezi mtendaji wa “Hanspaul Group” alisema kuwa anamshukuru na kumpongeza sana Rais Samia Suluhu Hassan kwa sababu walikuwa wanapata changamoto kubwa sana kwa magari kufika viwandani na magari mengi yalikuwa yanaharibika lakini sasa barabara imewaondolea kero hizo.

“Wageni walikuwa wakija eneo la Kiwanda na kuona miundombinu mibovu walikuwa wanapata wasiwasi na kiwanda pia, lakini tumeona Serikali yetu imeona changamoto na kuifanyia kazi haraka, sasa tunaaminika kwa sababu mazigira yameboreshwa,” alisema Hanspaul.

Mama Veronica Saimon mfanyabiashara wa eneo la viwandani alisema kuwa kabala ya barabara haijajengwa walikuwa wakipata shida sana kutokana na vumbi jingi pamoja na matope wakati wa mvua hali iliyokuwa inaathiri biashara yao.

Alieleza kuwa kwa sasa anamshukuru sana Rais Samia kwa kuwajali, sababu kwa sasa wanafanyabishara bila shida na wateja wengi wanawapata baada ya barabara kujengwa.

Kwa upande wake Mhe. Mrisho Gambo, Mbunge wa Arusha Mjini aliwashukuru watendaji na wataalamu wa TARURA kwa kazi kubwa wanayofanya na ameona tofauti kubwa sana baada ya TARURA kuanzishwa.

“Huko nyuma kaba ya kuanzishwa TARURA ilikuwa ngumu kupeleka mradi sehemu inayoeleweka na ukaleta tija kwa sababu kila diwani alikuwa akivutia upandewa wake. Leo mmewasikia hapa wawekezaji wamesubiri barabara kwa takribani miaka 40 lakini baada ya TARURA kuanzishwa barabara imejengwa,’alisema Mhe. Gambo.

Aidha alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa Kuendelea kuenzi falsafa ya Serikali ya “Tanzania ya Viwanda” kwa kuboresha miundombinu katika maeneo hayo ya viwandani yenye viwanda zaidi ya 20, ambapo ajira zinaogezeka na uchumi wa wanachi wa maeneo ya viwandani wanaofikia takribani 11,000 unaboreka.

Mtendaji mkuu wa TARURA Mhandisi Victor Seff kwa upande wake alisema kuwa wamejipanga kuwafikia wannachi katika sehemu ambazo hazifikiki na pia katika maeneo ya kimkakati.

“TARURA tunakufikisha kusikofika lakini nasema pia Penye nia pana njia na pasipo na njia TARURA tupo, “alisema Mhandisi Seff.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive

Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger