Thursday, 18 August 2022
SIDO , NELICO & PACT WATOA MAFUNZO YA VITENDO KWA WAJASIRIAMALI MANISPAA YA SHINYANGA
JAPAN YAWATAKA VIJANA WAKE KUONGEZA KASI YA KUNYWA POMBE
SHAKA:RAIS SAMIA ANAIFUNGUA NCHI KUPITIA UJENZI WA BARABARA NCHINI

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, akizungumza na Wananchi wa Ushokola katika Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM mkoani Tabora.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, akisoma baadhi ya Nyaraka zilizowasilishwa kwake na mmoja wa Wananchi kwenye mkutano wa Ushokola katika Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM mkoani Tabora.

DEREVA WA DALADALA MBARONI TUHUMA ZA KUUA KONDAKTA 'MPENZI WAKE'
RADI YAUA WATU WATATU WA FAMILIA MOJA
Wednesday, 17 August 2022
TAWI LA CHUO KIKUU CHA MISRI KUANZISHWA TANZANIA
Picha ya pamoja kati ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda na Balozi wa Misri nchini Tanzania Mohamed Gaber Abulwafa.
Na Dotto Kwilasa, DODOMA
CHUO Kikuu cha Misri kimeeleza kusudio la kuanzisha tawi lake nchini Tanzania kwa ajili ya kuanza kutoa elimu katika fani mbalimbali.
Kutokana na hayo Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amemuelekeza Mkurugenzi anayeshughulikia Vyuo Vikuu katika Wizara hiyo Dkt.Kenedy Hosea kuhakikisha anaanza mazungumzo na vyuo vikuu nchini ili kuona ni chuo gani kipo tayari kuanza ushirikiano huo ili utekelezaji uanze mara moja .
Waziri Mkenda ameeleza hayo leo 16, Agosti 2022 wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Misri nchini Tanzania Mohamed Gaber Abulwafa katika ukumbi wa mikutano wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jijini Dodoma.
Amemweleza Balozi huyo kuwa serikali ya Tanzania imetoa fursa ya wawekezaji kuja nchini kwa kufuata taratibu za kisheria na kuwekeza haraka iwezekanavyo.
Amesema wakati taratibu zingine zinaendelea za uwekezaji huo, Chuo kikuu hicho kinaweza kuunda ushirika na Chuo Kikuu chochote kilichopo nchini ili kuanza kutoa elimu kusudiwa kwa haraka.
Kwa upande wake Balozi wa Misri nchini Tanzania Mohamed Gaber Abulwafa amemuhakikishia Waziri Mkenda kuwa nchi yake itaendeleza ushirikiano na Tanzania katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya elimu.
Katika mazungumzo hayo wamejadiliana pia namna ya kuanza utekelezaji wa haraka wa (MOU) zilizosainiwa wakati wa ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyoifanya nchini Misri.
Pia Balozi Abulwafa amewasilisha mualiko wa Waziri wa Nishati wa Misri kumualika katika mkutano utakaokuwa unajadili masuala ya Atomiki pamoja na mwaliko wa Waziri wa elimu wa Misri ili kujadili kwa kina umuhimu wa kuimarisha ushirikiano katika sekta ya elimu.
WAZIRI MBARAWA ATEMBELEA MRADI WA BRT II, AFURAHISHWA NA KASI YA UJENZI

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (mwenye kofia nyeusi) akimuelekeza jambo Msimamizi wa Mradi wa BRT II, Mhandisi Bw.Frank Mbilinyi mara baada ya kutembelea mradi wa BRT II leo Agosti 17,2022 Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (mwenye kofia nyeusi) akiwa pamoja na wahandisi wa ujenzi akitembelea mradi wa BRT II leo Agosti 17,2022 Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea mradi wa BRT II leo Agosti 17,2022 Jijini Dar es Salaam.
Msimamizi wa Mradi wa BRT II, Mhandisi Bw.Frank Mbilinyi akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa kutembelea mradi wa BRT II leo Agosti 17,2022 Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (mwenye kofia nyeusi) akizungumza na wanaohusika na ujenzi wa mradi wa BRT II Mbagara mara baada ya kutembelea mradi wa huo leo Agosti 17,2022 Jijini Dar es Salaam.
Ujenzi wa daraja bandari kwaajili ya kutumika mradi wa BRT II
















