Friday, 5 August 2022

RAIS SAMIA ARIDHISHWA NA UJENZI JENGO LA OFISI YA MKUU WA MKOA WA MBEYA


OR-TAMISEMI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amesema kuwa ameridhishwa matumizi ya fedha za ujenzi wa jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya lililogharimu kiasi cha shilingi bilioni 6.7

Ametoa kauli hiyo leo Agosti 05, 2022 wakati akiweka jiwe la msingi katika jengo hilo kwenye ziara yake ya siku Nne ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa jijini Mbeya.

Amesema kuwa katika suala la utawala bora Serikali ya awamu ya sita inaboresha maeneo ya wananchi  wanapoenda kupata huduma kuwe na mazingira mazuri ya kuhudumiwa na wale wanaotoa huduma kuweza kutoa huduma bora kwa jamii wakiwa kwenye mazingira mazuri.

Amesema kuwa Serikali itaendelea kuboresha  na kujenga majengo ya Ofisi za Wakuu wa Mikoa, Majengo ya Halmashauri, nyumba za wakuu wa Wilaya, lengo likiwa ni kuboresha mazingira ili kuweza kutoa huduma bora kwa jamii.

“Utafiti unaonyesha kuwa tunapofanya kazi  kwenye mazingira mazuri, utoaji wa huduma hutolewa vizuri hivyo Serikali imeamua kutumia fedha nyingi kujenga Ofisi za Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Aidha, Mheshimiwa Samia amesema Serikali itaendelea kujenga majengo kama hayo katika Mikoa yote hasa katika maeneo ya Kikanda  

Mheshimiwa Samia amesema kuwa Serikali inatoa fedha nyingi kwa Halmashauri kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo hivyo niwatake Madiwani kuhakikisha wanasimamia fedha hizo ili ziweze kutekeleza miradi iliyokusudiwa na Serikali.

Jengo la Ofisi ya Mkuu w Mkoa lina urefu wa mita 84.2 na upana wa mita 33.5 ambapo vyumba vya ofisi vipo 72, stoo moja kubwa, Maktaba mbili,  kumbi mbili ndogo na ukumbi mmoja mkubwa wenye uwezo wa kuchukua watu 250.
Share:

JINSI NILIVYOPUNGUZA UZITO, HALI YA KUNENEPA ILIKUWA IMENIPA AIBU KWA MUDA MREFU

Share:

RAIS SAMIA AANZA ZIARA MKOANI MBEYA KWA KUZUNGUMZA NA WANANCHI PAMOJA NA KUZINDUA MIRADI MBALIMBALI YA MAENDELEO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na viongozi mbalimbali wakati akizindua Mradi wa Maji safi wa Mbalizi, Shongo-Igale katika eneo la Mbalizi Mkoani Mbeya leo tarehe 05 Agosti, 2022. Wengine katika picha ni Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifungulia maji kuashiria uzinduzi wa mradi wa maji safi wa Shongo-Mbalizi katika eneo la Mbalizi Mkoani Mbeya leo tarehe 05 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa Mbalizi mkoani Mbeya mara baada ya kuzindua mradi wa maji safi wa Shongo-Mbalizi tarehe 05 Agosti, 2022.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi pamoja na Wafanyakazi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya Kitengo cha Wazazi na Watoto Wachanga Meta mara baada ya kuzindua ujenzi wa jengo la afya ya huduma ya mama na mtoto Meta Mkoani Mbeya tarehe 05 Agosti, 2022.
Jengo la afya ya Huduma ya Mama na Mtoto lililopo Meta Mkoani Mbeya ambalo limewekewa jiwe la Msingi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan tarehe 05 Agosti, 2022.



Share:

TUMEFUNGUA MZIGO MPYAA!! KARIBU NNIENET TUNAZO NGUO ZA NDANI NZURI SANA....HEBU TAZAMA HAPA




Karibu katika duka la NNIENET Under Wear !

Tunauza nguo za ndani kutoka Uturuki; rika zote wanaume, wanawake na watoto

Tunazo Chupi, Boxer, Vest, Night dress, Brazia, Mikoba, perfume aina zote oil/alcohol, socks,tight ndefu na fupi, stockings aina zote, mikanda ya suruali kiume pure leather. Wallet za wanaume na wanawake, Belly wrap na corsets zote zinapatikana.


Simu: 0766062899/ 0757290980
Tupo Uhuru Road - Shinyanga Mjini kwenye Zebra jirani na Uwanja wa SHYCOM/ Kanisa Katoliki Mjini Shinyanga


Share:

VETA WABUNI KIFAA CHA KUKAUSHA NGUO ZA NDANI



Mfano wa nguo za ndani
MWALIMU Mbunifu kutoka Chuo cha Ufundi Stadi (VETA ) Chang'ombe, Dar es Salaam Emmanuel Bukuku akizungumza na baadhi ya wananchi waliotembelea banda la VETA kuhusu teknolojia ya kifaa cha kukaushia nguo za ndani kitakavyopunguza mangonjwa ya fangasi ya Ngozi na Ugonjwa wa Mfumo wa Mkojo (U.T.I ) katika kundi la wanawake na watoto, kwenye maonesho ya Kilimo na Ufugaji Kitaifa Nane Nane yanayoendelea katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.


*Kuwa suluhu ya kupunguza magonjwa ya ngozi na U.T.I

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV Mbeya
MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kupitia chuo cha Ufundi Stadi cha VETA Chang'ombe Dar es Salaam kimebuni kifaa cha kukaushia nguo za ndani kinachoitwa Dhydrator mashine lengo kupunguza, kutokomeza magonjwa yatokanayo na Fangasi ya ngozi pamoja na Ugonjwa wa Mfumo wa mkojo (U.T.I)


Pia Watanzania wametakiwa kukubali teknolojia ambazo zinabuniwa na wazawa ili kuwapa hamasa wabunifu katika kuendelea kuongeza juhudi za ubunifu ikiwa ni kuzinunua bidhaa.


Akizungimza kwenye Maonesho ya Kilimo na Ufugaji Kitaifa Nane Nane 2022 yanayoendelea kwenye viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya Mbunifu wa Chuo hocho Mwalimu Emmanuel Bukuku amesema kuwa watanzania wanaamini bidhaa zinazotoka chini kuliko kuuamini zinazobuniwa na wazawa hivyo kunafanya ubunifu wa ndani usiendelee.


Mwalimu Bukuku amesema kuwa baada ya kuona changamoto ya uanikaji wa nguo za ndani aligundua kufanya ubunifu mashine ambayo itaondoa changamoto hiyo ya kukausha nguo hizo kwa muda mfupi na mashine hiyo inatumia umeme kidogo.


Bukuku amesema nguo za ndani mara nyingi zikifuliwa huwa zinaanikwa ndani hali inayowasababishia watumiaji kupata magonjwa kutokana na kukuza wadudu ambao wanasababisha magonjwa kama Fangasi.


Kilichomsababishia kubuni mashine hiyo Mwalimu huyo amesema kuwa aliona jamii ina changamoto ya kupata magonjwa kama vile Fangasi, ya ngozi na U.T.I kwa watu wazima na watoto hivyo kifaa hicho kitasaidia kupunguza magonjwa hayo au kuyatokomeza kabisha.


"Kwa upande wa afya hii ni teknolojia nzuri na jamii bado haijajua hii mashine kwa ubunifu huu tunaweza kuwakomboa watoto wengi wanaokumbana na magonjwa ya U.T.I na Fangasi, pamoja na wanawake hii inaweza kuwa mkombozi kwao."ameongeza.


"Katika maonesho ya mwaka huu ya Nane nane tumeweza kuja na teknolojia mpya ya kifaa, mashine ya kukaushia nguo za ndani," amesema Mwalimu Bukuku.


Bukuku amefafanua kuwa mashine hiyo ametengeneza kwa muda wa wiki tatu na kuifanyia majaribio ambapo ilionesha ipo vizuri na inauzwa kwa shilingi 350,000.


Amesema mashine ipo kama dressing table ambapo mtumiaji atanufanika na vitu viwili atatumia kukuangalia kupitia kioo na chini kukaushia nguo za ndani.
Share:

HER DIGNITY, AGAPE KUPAMBANA NA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO MAENEO YA MGODI WA MWADUI


Mkurugenzi wa Taasisi ya HER DIGNITY Annagrace Rwehumbiza akizungumza kwenye kuhitimisha mafunzo ya MTAKUWWA ngazi ya vijiji kwenye maeneo ambayo yanazungukwa na Mgodi wa Mwadui. 
 
Na Michael Abel, KISHAPU 
 
TAASISI YA  HER DIGNITY, na Shirika la AGAPE wamekutana na Kamati ya Mpango Mkakati wa Taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA) ngazi ya vijiji, kutoka kwenye vijiji 11 ambavyo vinazunguka Mgodi wa Almasi Mwadui wilayani Kishapu, kutoa mafunzo na kujadili namna ya kupunguza matukio ya ukatili.

Mafunzo hayo yamefanyika kwa muda wa mwezi mmoja, na yamehitimishwa leo Agost 4, 2022 katika ukumbi wa Mikutano ndani ya Mgodi wa Mwadui.

Mkurugenzi wa taasisi ya HER DIGNITY Annagrace Rwehumbiza, akizungumza wakati wa kuhitimisha mafunzo hayo, amesema kwenye maeneo ya Migodi kumekuwa na matukio mengi ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto, na ndiyo maana wamekutana na kamati hizo za MTAKUWWA Ngazi vya vijiji ili kutoa elimu na kujadiliana namna ya kupunguza matuko hayo au kuyamaliza kabisa.

“Maeneo ya Migodi hua kuna matukio mengi ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto sababu ya muingiliano wa watu wengi, ndiyo maana Shirika letu la HER DIGNITY na AGAPE, tumeamua kutoa elimu kwenye Kamati hizi za MTAKUWWA ngazi ya vijiji kwenye maeneo ambayo yanazungukwa na Mgodi wa Mwadui ili kupunguza ukatili huo,”amesema Rwehumbiza.

“Kamati hizi za MTAKUWWA zinajumuisha viongozi mbalimbali wakiwamo wa kidini, Serikali, na Jeshi la Jadi Sungusungu hivyo tunaimani kabisa kupitia mafunzo hayo ambayo mmeyapata ndani ya mwezi mzima tunaimani mtakwenda kuyafanyia kazi kwa vitendo na kupunguza vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto,”ameongeza.

Naye Mkufunzi wa Mafunzo hayo Rose Shao, amesema changamoto kubwa ambayo amekuwa akiiona kwenye maeneo ambayo yanazungukwa na Migodi, hasa kwenye Masuala ya ukatili dhidi ya watoto, ni wazazi kushindwa kutekeleza majukumu yao katika familia na kusababisha watoto kujiingiza kwenye ajira za migodini katika umri mdogo.

Baadhi ya wanufaika wa mafunzo hayo akiwamo Magreth Ngeleja, amesema mafunzo yamewajengea uwezo mkubwa namna ya kupambana na matukio ya ukatili wa jinsia dhidi ya wanawake na watoto

"Mafunzo haya yametuelimisha juu ya masuala ya ukatili kwetu sisi wanawake na watoto, ukizingatia hali ya matukio haya kwetu sisi ambao tunaoishi kwenye maeneo ya Migodi familia nyingi zimetekezwa na wazazi kusahau majukumu na kusababisha familia nyingi watoto wao kujiendesha wenyewe, hivyo kupitia elimu hii nitakwenda kutoa elimu pia kwa familia na jamii inayonizunguka".amesema Ngeleja.
Mkurugenzi wa taasisi ya HER DIGNITY Annagrace Rwehumbiza akizungumza kwenye kuhitimisha mafunzo ya MTAKUWWA ngazi ya vijiji kwenye maeneo ambayo yanazungumwa na Mgodi wa Mwadui.

Mwezeshaji Lukia Masawanyika akitoa elimu kwenye mafunzo ya kamati ya MTAKUWWA.

Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.

Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.

Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.

Washiriki wakiwa kwenye kazi ya makundi.

Washiriki wakiwa kwenye kazi ya makundi.

Washiriki wakiwa kwenye kazi ya makundi.


Share:

Thursday, 4 August 2022

TEA KUTUMIA BILIONI 8.9 KUBORESHA MIUNDOMBINU YA ELIMU NCHINI

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bi. Bahati I. Geuzye akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 4,2022 kuhusu Utekezaji wa Majukumu ya Mamlaka hiyo ambayo ni Taasisi ya umma iliyopewa jukumu la kisheria la kuratibu Mfuko wa Elimu wa Taifa.

*******************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Katika mwaka wa fedha wa 2022/2023 Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) imepanga kutumia kiasi cha Sh. Bilioni 8.9 kwa ajili ya kufadhili miradi ya kuboresha miundombinu ya elimu nchini.

Kiasi hicho cha fedha kitatumika kufadhili wa miradi 96 katika shule 96 za msingi na sekondari katika maeneo mbali mbali ya Tanzania Bara pamoja na Taasisi mbili za elimu ya juu kwa upande wa Tanzania Zanzibar.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 4,2022 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bi. Bahati I. Geuzye amesema Miradi itakayofadhiliwa ni pamoja na Ujenzi wa madarasa 99, matundu ya vyoo 792, maabara kumi za masomo ya sayansi kwa ajili ya shule 05 za sekondari, nyumba za walimu 52 na Mabweni 10.

Amesema miradi mingine itakayotekelezwa ni ujenzi wa miundombinu ya wanafunzi wenye mahitaji maalum inayojumuisha madarasa 10, matundu ya vyoo 40 pamoja na mabweni mawili katika shule 6 za msingi na moja ya sekondari.

Bi.Geuzye amesema katika mwaka huu wa fedha 2022/23 Mfuko wa Elimu wa Taifa utaboresha miundombinu na kuwezesha ununuzi wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia kwa taasisi mbili za elimu ya juu zilizopo Tanzania - Zanzibar. Miradi hiyo imepangwa kutumia Shilingi Milioni 500 katika utekelezaji wake.

Amesema Mamlaka imewezesha utekelezaji wa miradi 3,314 yenye thamani ya shilingi bilioni 212.6 ambapo taasisi za elimu zikiwemo shule za awali, shule za msingi, shule za sekondari, vyuo vya ualimu, vyuo vya ufundi na vyuo vikuu vimenufaika.

Aidha amesema katika mwaka wa fedha wa 2021/2022, TEA ilipokea michango na kutekeleza miradi ya pamoja na mashirika ya Umma na yasiyo ya kiserikali yenye thamani ya Shilingi Milioni 556.3.

"Mashirika hayo yaliyoshirikiana na TEA ni pamoja na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Taasisi ya Flaviana Matata, BRAC- Maendeleo Tanzania, Taasisi ya Asilia Giving, Taasisi ya SAMAKIBA na Kampuni ya Dash Industries". Amesema Bi.Geuzye.

Pamoja na hayo amesema kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa unaoratibiwa na TEA, katika mwaka wa fedha 2021/2022, Shilingi bilioni 8.6 ziligharimia ufadhili wa miradi 160 ya kuboresha miundombinu ya elimu katika shule 151 nchini.

"Miradi hiyo ilijumuisha ujenzi wa madarasa 210 katika shule 65 (za msingi 53 na sekondari 22), Maabara 4 za sayansi katika Shule 2 za Sekondari, Matundu ya vyoo 1920 katika shule 80 (za msingi 58 na sekondari 22), vifaa vya kujifunzia na kufundishia katika shule 09 za wanafunzi wenye mahitaji maalum(shule 08 za msingi na moja ya sekondari) na ujenzi wa ofisi mbili za walimu katika shule mbili za sekondari". Amesema

Hata hivyo amesema kuwa katika awamu ya kwanza ya utekelezaji wa miradi yakuratibu Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (Skills Development Fund-SDF), mafunzo yalijikita katika sekta ya Kilimo na Kilimo - Biashara, shilingi bilioni 3.1 zilitumika kufadhili taasisi 15 za kutoa mafunzo ya ujuzi.

Ameeleza kuwa kupitia mfuko huo kiasi cha Shilingi Milioni 385.8 kimetolewa kunufaisha vijana 1,018 katika programu ya Utarajari (Internship Program) katika sekta za TEHAMA, Utalii na huduma za ukarimu; Nishati; Ujenzi na Uchukuzi.

Amesema Mfuko wa SDF pia unafadhili mafunzo ya Ujuzi kwa wanufaika 4,000 kutoka Kaya Maskini na Makundi Maalum (Bursary Scheme) hadi ifikapo Desemba 2022 lengo ni kuwezesha vijana wanaotoka katika kaya maskini kupata ujuzi na kujikwamua kiuchumi.



Share:

RAIS SAMIA ALETA MAFURIKO YA WATALII

* Zitto atabiri utalii kuingiza dola bilioni 3 kwa mwaka, sawa na Shilingi trilioni 7

* Royal Tour yaleta kishindo

* Watalii wafurika kila kona, ikiwemo Arusha, Zanzibar, Serengeti


IDADI ya watalii wanaokuja nchini baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuongoza ziara ya uzinduzi wa filamu ya Royal Tour nchini Marekani imezidi kuongezeka, huku viwanja vya ndege, mahoteli na mbuga za wanyama zikiona mafuriko ya watalii ambayo hawajawahi kutokea nchini.


Mkoa wa Arusha sasa hivi umetapakaa watalii kutoka nje, kiasi kwamba hata kampuni za watalii zimekumbwa na uhaba wa magari ya kuwapeleka watalii mbugani.


Visiwa vya Zanzibar kwa sasa navyo vinapokea idadi kubwa ya watalii.

"Arusha imejaa watalii" Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, alisema kupitia ukurasa wake wa Twitter Julai 24.

Akimjibu Zitto, Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Bima la Zanzibar (ZIC), Arafat Haji, alisema kuwa Zanzibar nayo inapata mafuriko ya watalii.

Zitto na Haji wote wamezishauri serikali za Tanzania na Zanzibar kuwekeza kwenye upanuzi wa miundombinu, ikiwemo viwanja vya ndege na bandari, ili kukabiliana na ongezeko hilo la watalii.


Zitto amebashiri kuwa huenda Tanzania sasa ikaweka rekodi kwa kupata dola za Marekani bilioni 3 kwa mwaka 2022 kutoka kwenye utalii, sawa na Shilingi trilioni 7.


Mwaka jana, Tanzania ilipata dola za Marekani bilioni 1.4 kutoka kwenye sekta utalii 


Naye Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, amesema kuwa ndege ya Shirika la Ndege la KLM la Uholanzi usiku wa tarege 1 Agosti mwaka huu imeshusha abiria zaidi ya 250 katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).


"Kwa kweli kishindo ambacho Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Samia amekisababisha katika sekta ya utalii ni kikubwa sana," amesema Msigwa kupitia ukurasa wake wa Twitter.


Uwanja wa Ndege wa Arusha kwa siku sasa unapokea idadi kubwa ya ndege ambayo haijawahi kutokea.


Mbuga za wanyama na vivutio vikubwa vya watalii nchini, ikiwemo Ngorongoro, Serengeti, Kilimanjaro, Arusha, Zanzibar na kwingineko sasa kumefurika watalii hadi idadi ya hoteli na vyumba havitoshi.


"Kwa kweli hii haijawahi kutokea. sijawahi kuona idadi kubwa ya watalii namna hii Arusha tangu nizaliwe. Rais Samia anastahili pongezi kwa kutuletea neema hii kupitia Royal Tour," alisema Paul Mollel, dereva wa watalii jijini Arusha.

Share:

POLISI, WAANDISHI WA HABARI SHINYANGA WAFANYA MDAHALO KUJADILI MASUALA YA ULINZI NA USALAMA KWA WANAHABARI

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger