Thursday, 4 August 2022

UPANGAJI SAFU KASULU UCHAGUZI MKUU 2025 KWAMCHEFUA NAIBU KATIBU MKUU CCM


Naibu Katibu Mkuu huyo wa CCM Bara Christina Mndeme (aliyesimama katikati akizungumza na wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Kasulu akiwa kwenye ziara ya kichama mkoani Kigoma.
Naibu Katibu Mkuu huyo wa CCM Bara Christina Mndeme (aliyesimama katikati akizungumza na wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Kasulu akiwa kwenye ziara ya kichama mkoani Kigoma.
Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Kasulu, viongozi wa serikali wa wilaya hiyo na viongozi wa taasisi za serikali wilayani humo wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Christina Mndeme alipokuwa kwenye ziara ya kichama ya siku moja wilayani humo.
Katibu wa CCM mkoa Kigoma Mobutu Malima (aliyesimama kushoto) akizungumza mbele ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM bara Christina Mndeme wakati wa kikao cha wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Kasulu ambacho kilikuwa maalum kwa ziara ya Naibu Katibu Mkuu huyo wa CCM bara ambaye yuko kwenye ziara ya kichama mkoani Kigoma.
Naibu Katibu Mkuu huyo wa CCM Bara Christina Mndeme (wa pili kushoto mstari wa mbele) akiwasili katika eneo la shule ya Sekondari Nkundutsi wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma ambapo alitembelea shule hiyo na baadaye kuzungumza na wanafunzi, walimu na jumuia ya shule hiyo akiwa kwenye ziara ya kichama mkoani Kigoma.(Picha na Fadhili Abdallah)
**

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

UPANGAJI safu za ugombea ubunge na udiwani kwa uchaguzi wa mwaka 2025 umemchefua Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Christina Mndeme ambapo amekemea mpango huo na kuwataka viongozi na wanachama wa CCM wilaya ya Kasulu wanaopanga mpango huo kuacha mara moja.

Naibu Katibu Mkuu huyo wa CCM Bara akizungumza na wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM ya wilaya Kasulu alisema kuwa hali hiyo inachafua taswira nzuri nay a kuigwa ya CCM na kwamba watakaokaidi agizo la kuachana na mpango huo wataadhibiwa.

“Kuna shetani amewaingia hapa ambaye ameanza kuwavuruga ni lazime tukemee shetani huyo kwani pamoja na kuvuruga huku lakini pia anakivuruga chama na kuvuruga mipango ya Mwenyekiti wetu na Raisi wetu, hatutakubali,”Alisema Naibu Katibu Mkuu wa CCM.

Alisema kuwa amekuwa akipokea sifa mbaya ya viongozi na wanachama wa CCM kuhusu kupanga makundi ya nani wa kuchaguliwa na nani asichaguliwe kwenye uchaguzi mkuu mwaka 2025 hasa nafasi za wabunge na madiwani na vitendo vya rushwa na kudhalilishana vimekuwa vikitawala michakato hiyo.

Mpango huo unadaiwa kuyakumba majimbo ya Kasulu Mjini ambalo kwa sasa Mbunge wake ni waziri wa nchi ofisi ya waziri Mkuu kazi,ajira,vijana na watu wenye ulemavu, profesa Joyce Ndalichako na jimbo la Kasulu Vijijini ambalo mbunge wake ni Augustino Hole Vuma.

“Kasulu kuna watu wanapanga safu kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka 2025 na hali hiyo imeanza kuleta shida na kuchafuana hatutakubali naomba mliache vinginevyo tutachukua hatua,mnapanga safu,mnatoa rushwa,mnachafuana mnafanya vibaya sana,”Alisema Mndeme.

Sambamba na hilo Naibu Katibu Mkuu huyo wa CCM alisema kuwa walioshindwa kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 wakubali matokeo na pia waungane na wenzao katika kujenga chama wakiendelea kuvuruga chama na viongozi wake tutachukua hatua.

Aidha aliwataka viongozi na wanachama kufanya chaguzi za chama zinazoendelea kwa kuzingatia kanuni za uchaguzi zinazotokana na katiba ya CCM ikiwemo kanuni za uongozi na maadili na kwamba ni lazima slogan ya chama inayosema kwamba chama kwanza mtu baadaye izingatiwe.

Naibu Katibu Mkuu bara alisema kuwa Wagombea ni lazima wazingatie miiko na maadili ya uongozi ambayo miongoni mwa vitendo vinavypigwa vita ni pamoja na utoaji na upokeaji wa rushwa, utoaji wa siri za vikao.

Kutoa siri za vikao kunatengeneza uadui baina yetu lakini siri hizo zinadhoofisha wagombea wetu katika chaguzi za nje ya chama au kuwapa nafasi wagombea ambao wana mapungufu.

Awali Katibu wa CCM mkoa Kigoma, Mobutu Malima alisema kuwa asilimia 90 ya viongozi wa chama wanaomaliza muda wao wamerudishwa na kupitishwa kugombea tena nafasi mbalimbali ndani ya chama hicho na kwamba vikao vimezingatia taarifa mbalimbali za matendo yao, nidhamu na yale waliyofanya kwenye chama.

Malima alisema kuwa Wapo wagombea ambao hawakupitishwa na vikao vya uchujaji wagombea vya chama hasa baada ya kujiridhisha kwamba makosa waliyokuwa wanatuhumiwa nayo yamethibitika ikiwemo usaliti ndani ya chama katika uchaguzi mkuu uliopita.
Share:

WAZIRI NDALICHAKO ATOA MWELEKEO WA WIZARA YAKE


Waziri wa nchi ofisi ya waziri Mkuu kazi,ajira,vijana na watu wenye ulemavu Profesa Joyce Ndalichako akizungumza na waandishi wa habari akitoa taarifa ya mwelekeo wa utekelezaji wa mipango ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2022/2023.(Picha na Fadhili Abdallah)
waandishi wa habari wa mkoa Kigoma wakisikiliza taarifa iliyokuwa ikitolewa na Waziri wa nchi ofisi ya waziri Mkuu kazi,ajira,vijana na watu wenye ulemavu Profesa Joyce Ndalichako kuhusu mwelekeo wa utekelezaji wa mipango ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2022/2023


****

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu kazi,vijana, ajira na watu wenye ulemavu Profesa Joyce Ndalichako amesema kuwa serikali imeanza kutekeleza mpango kabambe wa uwezeshaji kiuchumi kwa vijana kwa kuwapatia mafunzo na mitaji ili waweze kujiajiri na kutoa ajira kwa vijana wenzao.

Waziri Ndalichako alisema hayo mjini katika mkutano na waandishi wa habari na kueleza kuwa vijana ndiyo nguvu kazi ya Taifa na hivyo ni lazima kundi hili liweze kuwekewa mazingira mazuri ambayo yatawafanya kutoa mchango wao kwa taifa.

Moja ya mipango hiyo ameitaja inafanywa na wizara hiyo ni kutenga kiasi cha shilingi bilioni moja ambazo zitatolewa mikopo kwa vijana na kwa sasa kiwango kimeongezwa kutoka shilingi milioni 10 kwa kiwango cha juu na kufikia shilingi milioni 50 ambazo zitawezesha kuanzisha au kuendeleza miradi yenye tija kubwa.

“Sambamba na mikopo inayotolewa kupitia wizara ya kazi inayosimamia na ofisi ya Waziri Mkuu pia tutasimamia mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri ambapo vijana wanapata asilimia nne hivyo vijana wanapaswa wajipange vizuri kuhakikisha wanatumia fursa hiyo,”Alisema waziri Ndalichako.

Sambamba na hilo alisema kuwa wizara imeanza kutoa mafunzo ya ujuzi na uana genzi kwa vijana 22,200 katika fani mbalimbali ili waweze kuwa na ujuzi ambao watatutumia kuanzisha miradi ikiwa ni mpango wa serikali kuwafanya vijana kujajiri na kuajiri vijana wenzao kwa wingi.

Alisema vijana 1500 waliopata ujuzi nje ya mfumo rasmi watatathminiwa na kuthibitishwa ujuzi wao, vijana 3000 watapata mafunzo ya ujuzi wa uana genzi, vijana 2400 watapatiwa mafunzo ya kitalu nyumba na vijana 500 watapatiwa mafunzo ya uchumi wa bluu ambapo wataweza kuanzisha miradi ya uvuvi na ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba.

Akizungumzia suala la watu wenye ulemavu Waziri Ndalichako alisema kuwa kwa mwaka huu wa fedha Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu kazi,ajira na watu wenye ulemavu Profesa Joyce Ndalichako amesema kuwa serikali imeanza kutekeleza mpango kabambe wa kusaidia watu wenye ulemavu kwa kujenga vyuo vipya vitatu vya ufundi stadi na marekebisho ili kuwewezesha kujikwamua na kuwa na uwezo wa kujitegemea kiuchumi.

Vyuo hivyo alisema kuwa vitajengwa katika mikoa ya Mwanza, Kigoma na Songwe ambavyo vitaenda sambamba na ukarabati wa vyuo vinne katika mikoa ya Dar es Salaam,Tabora,Singida na Mtwara ambavyo vitasaidia watu hao.

Katika taarifa yake Waziri Ndalichako alisema kuwa serikali inachukua hatua mahsusi ya kuhakikisha mafao ya wastaa yanalipwa kwa wakati sambamba na kuboresha mifuko ya jamii na kuhakikisha pensheni za wastaafu hao zinalipwa kwa wakati.

Amesema kuwa serikali ya raisi Samia Suluhu imelipa kiasi cha shilingi bilioni 500 la deni la serikali kwa mifuko ya pensheni jambo ambalo linatoa taswira sahihi ya kuhakikisha mifuko hiyo inalipa pensheni za wastaafu kwa wakati.

Alisema kuwa hali hiyo pia inachangiwa na serikali kutoa hati fungani ya shilingi trilioni 2.1 ili kupunguza deni la shilingi trilioni 4.6 ambapo wanachama walikuwa hawachangii tangu mwaka 1999 na kwamba malipo hayo yanaimarisha utendaji wa mifuko hiyo kulipa wastaafu.

Waziri Ndalichako aliwataka watumishi kutumia mfumo wa simu kiganjani katika kuhakiki taarifa za uchangiaji zinazotolewa na waajiri ili kujua kama wamechangia jambo litakalowafanya kupunguza usumbufu wa kwenda ofisini kufuatilia taarifa hizo


Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI AGOSTI 4,2022


















Share:

Wednesday, 3 August 2022

WAKULIMA WA SOYA WASHAURIWA KUTUMIA MBOLEA YA ASILI


****************

Na Mwandishi Wetu-Arusha



Wakulima wa zao la Soya (soyalishe) nchini wameshauriwa kutumia mbolea asilia ili kuongeza uzalishaji wa zao hilo.

Rai hiyo imetolewa na Mwanafunzi wa Shahada ya Uzamivu (PhD) ya Kilimo Endelevu ya Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Bi. Monica Nakei katika maonesho ya 28 ya Nanenane Kanda ya Kaskazini yanayoendelea viwanja vya Themi Arusha Agosti 2, 2022.

Bi. Monica amesema kwa sasa anafanya utafiti mbolea asilia itokanayo na vimelea vya bakteria jamii ya rhizobia ambayo inasaidia kuongeza virutubisho vya nitrogeni na fosforasi kwa mimea ya Soya.

" nimefanya utafiti wa mbolea hii kupitia zao la Soya na matokeo ni mazuri ,utafiti utakapokamilika mbolea hii itakuwa tayari kwa matumizi" amesema Bi .Monica

Aidha, ameeleza kuwa, mbolea hiyo ina faida nyingi ikiwemo kuimarisha afya ya udongo na kuweka usawa katika mfumo wa ikilojia ya udongo pamoja na kutunza mazingira kama maji, hewa na udongo.

Bi. Monica ameeleza kuwa, faida nyingine ni pamoja na mazao yatokanayo na mbolea hiyo kutokuwa na kemikali zenye kuleta madhara kwa walaji na gharama yake ni nafuu kwa wakulima.

Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela imekuwa mstari wa mbele katika kutoa elimu iliyolenga kusaidia jamii na kukuza viwanda kupitia tafiti na bunifu zinazofanywa na wanafunzi wa Taasisi hiyo, ambao wanashiriki katika maonesho ya 28 ya nanenane Kanda ya Kaskazini kwa nia ya kutoa elimu na kuonesha bunifu mbalimbali zinazozalishwa na taasisi hiyo.

Mbali na bunifu ya mbolea asilia , Taasisi hiyo imetoa elimu ya migomba iliyoboreshwa, kiatilifu biologia cha kudhibiti wadudu katika zao la Kabeji, upimaji wa udongo , chakula cha samaki chenye lishe, buheri wa Afya,Nutrano,NUSA,Omega -3DHA,Ngwara,Kweme na vyakula visivyo vya kemikali.

Share:

WATUMISHI WA WILAYA YA TEMEKE WAMPONGEZA RAIS SAMIA KWENYE NYONGEZA YA MSHAHARA

Mtumishi wa Wilaya ya Temeke Bi.Makungu Shomari akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 3,2022 wakati wakitoa pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya. Mtumishi wa Wilaya ya Temeke Bi.Makungu Shomari akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 3,2022 wakati wakitoa pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya. Mtumishi wa Wilaya ya Temeke Bi.Makungu Shomari akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 3,2022 wakati wakitoa pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya. Baadhi ya watumishi wa Wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam wakiwa katika mkutano na waandishi wa habari leo Agosti 3,2022 wakati wakitoa pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya. Baadhi ya watumishi wa Wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam wakiwa katika mkutano na waandishi wa habari leo Agosti 3,2022 wakati wakitoa pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

*********************

Na Mwandishi wetu.

WATUMISHI wa kada mbalimbali katika Wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam wamempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa juhudi ambazo anazifanya hasa kuwajali watumishi na kuzingatia maslahi yao.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 3,2022 Jijini Dar es Salaam,Mtumishi wa Wilaya ya Temeke Bi.Makungu Shomari amesema kuwa Rais Samia ndani ya kipindi chake cha muda mfupi ameweza kuleta nafuu na faraja kwa watumishi wa Umma.

"Kuhusu suala la nyongeza ya asilimia 23 sisi watumishi tumelielewa sana mana lengo kuu Rais Samia amezingatia kuboresha Hali za kiuchumi za watumishi wa kiwango cha chini ambao ni wengi zaidi katika kada mbalimbali za utumishi wa umma, hapa amezingatia wenye viwango vidogo vya mishahara". Amesema Bi.Makungu

Aidha amesema kuwa Rais Samia amejipambanua kuwa anawajali watumishi sana na kwa kuzingatia maslahi yao na alianza kwa kuwaondolea kadhia ya watumishi wenye deni la mkopo wa elimu ya juu,

"Rais Samia alipoingia madarakani alifuta penati hii na imeleta ahueeni kubwa na Sasa Deni linalipika, baada ya mabadiliko hayo aliyekuwa analipa milioni 8 Sasa analipa milioni 4 pekee."Amesema

Pamoja na hayo amesema kuwa suala la posho na nauli amesema Rais Samia ameongeza kiwango kwa asilimia 100 na hii imeleta ahueni kwa watumishi wanapopewa kazi maalumu.
Share:

AMUUA MKEWE KWA KUMPIGA NA KUMNG'ATA KIDEVU UKWENI KWENYE MSIBA


Sehemu ya mauaji yalipofanyika
**

Mariam Masanja 22, mkazi wa Kijiji cha Nyabugela, Kata ya Mganza wilayani Chato mkoani Geita, ameuawa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani na kung'atwa kidevu na mme wake Edward Franscis 20, ambao walikutana kwenye familia ya mwanamke kuhani msiba baada ya ugomvi wao wa muda mrefu.

Wawili hao walikutana kwenye msiba wa kaka wa marehemu ambapo marehemu alikuwa mkoani Mwanza kwa dada yake baada ya kugombana na mme wake ndipo aliporudi kwao baada ya kusikia kaka yake amefariki.

Wazazi wa marehemu wameeleza walivyopata taarifa za mtoto wao kuuawa na mme wake huku baba mzazi wa marehemu anasema wawili hao walikuwa na ugomvi wa mara kwa mara wa wivu wa kimapenzi.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyabugela Metusela Mgema, amesema wawili hao walifika mara kadhaa kwenye ofisi yake kwa ajili ya migogoro ndani ya familia yao ambayo ilikuwa inasuruhishwa mara kwa mara lakini mpaka kufikia kifo cha mwanamke wawili hao walikuwa wameachana.

Share:

NILIPATA NG’OMBE WANGU WAWILI BAADA YA KUIBIWA

Share:

KARSAN ANG'ATUKA RASMI, MKURUGENZI MPYA WA UTPC KENNETH SIMBAYA AKABIDHIWA MIKOBA


Mkurugenzi mpya wa muungano wa Klabu za Waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Bw. Kenneth Simbaya (kulia), kushoto ni Rais wa Utpc Bw. Deogratius Nsokolo na katikati ni Bw. Abubakar Karsan Mkurugenzi ambaye amemaliza muda wake
Rais wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania(UTPC)  Deogratius Nsokolo amemkabidhi rasmi ofisi Bw. Kenneth Simbaya ambaye ni Mkurugenzi mpya wa UTPC. 

Bw. Simbaya anachukua nafasi ya Bw. Abubakar Karsan ambaye amemaliza muda wake.

Makabidhiano hayo yamefanyika tarehe 1/8/2022 katika ofisi za UTPC zilizopo Isamilo Jijini Mwanza ambapo Rais Nsokolo amesema UTPC ina matarajio makubwa kutoka kwa Bw. Simbaya na kwamba uzoefu wake kwenye kazi utasaidia kuendeleza kazi nzuri iliyoachwa na mtangulizi wake na kuipeleka taasisi mbali zaidi.

Pamoja na mambo mengine Rais Nsokolo ametoa nasaha zake kwa mkurugenzi mpya, huku akigusia zaidi kuendeleza ushirikiano kati ya UTPC na wadau mbalimbali lakini pia kutumia fursa ya uwepo wa mkurugenzi aliyemaliza muda wake katika kubadilishana maarifa ya kiuongozi.

Pia amemtaka Bw. Simbaya kushirikiana na wafanyakazi wa UTPC, Bodi ya Wakurugenzi pamoja na viongozi wa Klabu za waandishi wa habari katika utendaji wa kazi kwani anaamini ushirikishwaji huleta tija zaidi kwa maendeleo ya taasisi na kwamba taasisi haiwezi kuendeshwa na mawazo ya mtu mmoja.

Aidha amesisitiza kuhusu uadilifu na ubunifu katika utendaji wake wa kazi na kuimarisha ushirikiano na wafadhili ikiwemo kutafuta fursa mpya za kupata fedha. 

Hata hivyo alimdokeza kuhusu uwepo wa changamoto ndogondogo zilizopo katika klabu za waandishi wa habari licha ya jitihada zilizofanyika kutatua changamoto hizo.

"Uhai wa UTPC unategemea uwepo wa klabu za waandishi wa habari hivyo ni lazima tuhakikishe tunashirikiana kuzisimamia na kuzijengea uwezo klabu zetu'' ,amesema Rais Nsokolo.

Naye Mkurugenzi anayemaliza muda wake ndugu Abubakar Karsan ameeleza changamoto iliyokuwepo wakati anakabidhiwa nafasi ya ukurugenzi na kwamba hapakuwa na nyaraka zozote za makabidhiano hali iliyompa wakati mgumu katika kuifufua na kuiendeleza taasisi hiyo mpaka kuifikisha hapa ilipo leo.

"Nilikabidhiwa ukurugenzi hapa bila kuwa na nyaraka zozote, niliambiwa chukua kijiti nenda ukafufue taasisi" Karsan.

Hata hivyo Bw. Karsan ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa mkurugenzi mpya kwa kipindi cha muda wa miezi mitatu ili kubadilishana uzoefu wa kiutendaji na ndugu Kenneth Simbaya.

Kwa upande wake Bw. Kenneth Simbaya amesema nafasi ya ukurugenzi ni nafasi ambayo anaweza kupewa mtu yeyote hivyo ameahidi kuhakikisha anataguliza mbele maslahi ya waandishi wa habari na klabu zake na yale yote mazuri yatabaki kuwa mazuri kwa maslahi ya waandishi wa habari Tanzania.


Pia ameahidi kushirikiana na wafanyakazi pamoja na wadau wa UTPC katika kuhakikisha taasisi inasonga mbele "Maamuzi binafsi huyumbisha mwelekeo wa taasisi, hivyo niwahakikishe Bodi ya Wakurugenzi kwamba kila kitu kitaenda sawa kulingana taratibu zilizowekwa na kwa mujibu wa miongozo ya UTPC ", amesema Simbaya.

Aidha ameongeza kuwa kesho ya UTPC inategemea maamuzi mazuri yatakayofanywa leo, hivyo ili kuacha alama ni lazima kufanya kazi kwa ufanisi na weledi wa hali ya juu na kwa maslahi ya waandishi wa habari nchini.

Share:

Tuesday, 2 August 2022

TANGA JIJI YAONGOZA UKUSANYAJI MAPATO, MANISPAA YA SHINYANGA YANG'ARA, MBULU MJI BALAA, KIBAHA DC YATISHA


NA GODFREY NNKO


KATIKA kipindi cha Julai hadi Juni 2022 Halmashauri ya Jiji la Tanga imeongoza kwa kukusanya mapato kwa asilimia 113 ya makisio yake ya mwaka ikifuatiwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam asilimia 108.

Huku Halmashauri ya Jiji la Arusha ikiwa asilimia 104, Halmashauri ya jiji la Dodoma asilimia 103, Halmashauri ya Jiji la Mwanza asilimia 100 na Halmashauri ya Jiji la Mbeya imekua ya mwisho kwa kukusanya asilimia 92.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhesshimiwa Innocent Bashungwa ameyasema hayo leo Agosti 2, 2022 jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa kuhusu mapato na matumizi ya ndani ya halmashauri kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

Wakati huo huo, kwa upande wa halmashauri za manispaa, Mheshimiwa Bashungwa amesema kuwa, Manispaa ya Shinyanga imeongoza kwa kukusanya mapato kwa asilimia 125 ya makisio yake ya mwaka ikifuatiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni na Ubungo asilimia 118 na Halmashauri ya Manispaa ya Moshi asilimia 117.

“Katika kundi hili Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara imekuwa ya mwisho kwa kukusanya asilimia 78 ya makisio ya mwaka ikifuatiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Lindi asilimia 90 na Manispaa ya Morogoro asilimia 91,”amefafanua Mheshimiwa Waziri Bashungwa.

Akizungumzia kwa upande wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu amesema kuwa, imeongoza kwa kukusanya asilimia 140 ya makisio ya mwaka ikifuatiwa na Halmashauri ya Mji wa Mafinga asilimia 129 na Halmashauri ya Mji wa Ifakara asilimia 125.

Aidha, Halmashauri ya Mji wa Nanyamba imekuwa ya mwisho kwa kukusanya asilimia 71 ya makisio ya mwaka ikifuatiwa na Halmashauri za Mji wa Korogwe asilimia 84 na Halmashauri ya Mji wa Geita asilimia 88.

Halmashauri ya Mji wa Mbulu imeongeza ufanisi kwani kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo imekuwa ikishika nafasi ya mwisho kwenye Halmashauri za Miji kwa kukusanya chini ya Shilingi Bilioni moja kwa mwaka.

Kwa upande wa halmashauri za wilaya, amesema kuwa, Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha imeongoza kwa kukusanya asilimia 247 ya makisio ya mwaka ikifuatiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Mlele asilimia 185 na Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro asilimia 158.

Aidha, Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli imekuwa ya mwisho kwa kukusanya asilimia 58 ya makisio ya mwaka ikifuatiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe asilimia 67 ya makisio ya mwaka na Halmashauri ya Wilaya ya Bunda asilimia 70.

Chanzo - Dira Makini blog

Share:

RAIS WA MAREKANI JOE BIDEN ATOA KAULI NZITO JUU YA KIFO CHA KIONGOZI WA KUNDI LA KIGAIDI LA AL QAEDA


Ayman al- Zawahiri akiwa na aliyekuwa Kiongozi wa kundi la Al-Qaeda Osama Bin Laden
Ayman al-Zawahiri aliyekuwa kiongozi wa kundi la lkigaidi la Al- Qaeda

***
RAIS wa Marekani Joe Biden amelihutubia Taifa hilo na kutoa kauli nzito juu ya kifo cha kiongozi wa kundi la kigaidi la Al Qaeda Ayman al-Zawahiri, aliyeuawa na ndege ya Marekani isiyokuwa na Rubani.

Rais Biden amesema kuwa kifo cha al- Zawahiri ni malipo ya unyama alioufanya kwa wananchi wa Taifa hilo kufuatia kuhusika katika utekelezaji wa shambuliola kigaidi la Septemba 11 mwaka 2001 ambalo liliua zaidi ya raia 3000 nchini humo.

Rais wa Marekani Joe Biden

“Kiongozi wa ugaidi hayupo tena.” Alinukuliwa akisema Rais Biden ambaye aliendelea kwa kusisitiza kuwa kifo cha gaidi huyo kinarudisha tena faraja kwa familia za wahanga wa shambulio la Septemba 11.

Rais huyo wa Marekani amesisitiza kuwa Afghanistan haitakuwa tena makazi ya ugaidi baada ya shambulio hilo kutekelezwa ikiwa ni mwaka mmoja tangu vikosi vya Marekani vindoke nchini humo.

Aidha kiongozi huyo wa kundi la kigaidi ambaye ana asili ya Misri aliuawa majira ya asubuhi wakati akiwa katika nyumba yake kwenye mji wa Kabul ambapo kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Rais Biden ni kwamba hakuna mtu mwingine yeyote yule kutoka katika familia ya al- Zawahiri aliyeathirika au kujeruhiwa katika shambulio hilo.


Al-Zawahiri aliuawa vipi?

Maafisa wa Marekani wamesema Zawahiri alikuwa amesimama kwenye veranda ya nyumba yake ya mafichoni. Ghafla, ndege isiyokuwa na rubani- inayofahamika kama drone- ikadondosha makombora mawili.


Taarifa inasema kuwa kombora lilimpiga Zawahiri ambaye alikuwa amesimama nyumbani kwake.


Ndugu wengine wa familia ya Ayman Al-Zawahiri walikuwepo pamoja naye katika eneo hilo, lakini hakuna mtu mwingine aliyeuawa wala kujeruhiwa katika shambulio hilo, na kiongozi wa Al-Qaeda akafa mara moja pale peke yake, maafisa walisema.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger