Saturday, 30 July 2022

SERIKALI INAPAMBANA KUTATUA CHANGAMOTO YA WANYAMAPORI WAKALI NA WAHARIBIFU


********************

Naibu Waziri Mary Masanja (Mb) amesema kuwa Serikali itahakikisha inapata ufumbuzi wa changamoto ya wanyamapori wakali na waharibifu wanaovamia Makazi ya watu hususan tembo.

Ameyasema hayo leo katika ziara ya kikazi alipotembelea Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) mjini Morogoro. Amesema kuwa Serikali haifurahishwi na matukio ya wananchi kuuawa na tembo au kuliwa mazao yao.

"Serikali inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan haifurahii matukio ya tembo kuuwa watu kwa sababu uhai wa mtu hauwezi kurudishwa" Mhe. Masanja amesisitiza

Amesema moja ya mikakati ya kutatua changamoto hiyo ni kutoa elimu kwa wananchi kuhusu mbinu za kukabiliana na tembo.

Ameongeza kuwa njia nyingine ya kutatua tatizo hilo ni kuwavisha tembo viongozi kola maalum ili kuwawezesha Askari Uhifadhi kujua mwelekeo wa kundi la tembo.

Pia, amesema Serikali inaendelea kutafuta mbinu za muda mrefu za kutatua changamoto hiyo.

Ziara hiyo ni mwendelezo wa ziara za kusikiliza changamoto za Taasisi na kuangalia utekelezaji wa majukumu yake iili kutafuta ufumbuzi.
Share:

DON BOSCO DIDIA YATANGAZA NAFASI ZA KUJIUNGA NA FORM ONE 2023

 

Share:

MWANAMKE AISHI NA MAITI YA KAKA YAKE...MWENYEWE ADAI NI MUNGU

Polisi mjini Kakamega nchini Kenya wamemzuilia mwanamke wa makamo kwa madai ya kuishi na maiti kinyume na sheria.

Shamim Kabere, mkazi wa Iyala, eneo bunge la Lurambi, anasemekana kuuhifadhi mwili wa Ainea Tavava, 48, ndani ya nyumba yake kwa zaidi ya siku 10.

Juhudi za wakazi kutafuta chanzo cha uvundo huo usiokuwa wa kawaida ziliwafikisha hadi kwenye nyumba ya mtuhumiwa huyo ambapo walilazimika kuvunja mlango wake na kukuta mwili wa mtu ukioza kitandani.

"Nzi na ndege wengi walikuwa wakizunguka nyumba ya mshukiwa iliyokuwa inanuka, jaribio letu la mara moja kubaini chanzo cha harufu hiyo lilikuwa hadi wakati nzi walianza kujaa nyumbani kwake.

"Mwili uliooza ukitoka funza ulikuwa umelala kitandani, ishara kwamba aliaga dunia muda mrefu uliopita," alisema Josephine Nawire, jirani wa mshukiwa. 

Kulingana na wakazi wa eneo hilo, aliyejiita mungu huyo na mtumishi wake walihamia kijijini humo miezi michache iliyopita.

 Waliishi maisha ya siri, hawakuwahi kutangamana na wengine.


Shamim alikiri kuishi na maiti hiyo akisema ni mungu wake na aliamriwa kufungiwa ndani ya chumba hicho kwa siku nyingi ili kuombea Uchaguzi Mkuu wa Agosti 9. 

"Kati ya siku 14 zilizohitajika, 9 zilikiwa tayari zimekamilika. Hapo awali alikuwa amenionya dhidi ya kufungua mlango kabla ya siku zilizotajwa kuisha," alisema.

 Chifu wa eneo hilo Simon Aketch alithibitisha kisa hicho akiwaomba wakaazi kuwa watulivu huku uchunguzi kuhusu suala hilo ukianzishwa.

“Mshukiwa alitumia chumba kimoja huku mwili wa mwathiriwa ukiwa katika chumba kingine, alidai kuwa hakufahamu ulikotoka uvundo huo. 
Polisi kutoka kituo cha Kakamega wameanza uchunguzi,” alisema.

 Kwa mujibu wa sheria za Kenya, mara baada ya mtu kufariki dunia akiwa nyumbani, wale walio karibu na mwili huo wanapaswa kupiga ripoti kwa chifu, ambao huwasiliana na idara ya afya na kuanza taratibu za kisheria za kushughulikia mwili huo.

Chanzo - Tuko News
Share:

AKUTWA AMEFARIKI GESTI BAADA YA KURUSHANA ROHO NA MREMBO


Polisi huko Migori wanachunguza kisa ambacho kinaripotiwa kuwa mwanaume mwenye umri wa miaka 52 anadaiwa kuzimia na kufariki katika nyumba ya kulala wageni (Guest House) asubuhi ya jana ijumaa nchini Kenya.

Kwa mujibu wa Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), marehemu; Naftali Nyandera, na mpenzi wake wa miaka 24 walikuwa kwenye nyakati nzuri kwenye nyumba ya kulala wageni kabla ya kifo chake.

"Katika kisa hicho ambacho kiliwashangaza wakazi wa Kanyarwanda, mwili wa Naftali Nyandera uligunduliwa ukiwa umetulia bila ya kutikisika kwenye kitanda katika nyumba ya kulala wageni ya Lavanda, baada ya shughuli nyingi zilizofanyika jioni na msichana huyo," ilisema taarifa ya DCI.

Uchunguzi wa awali wa DCI ulibaini kuwa mwanaume huyo alianguka saa chache baada ya kuingia chumbani na mwanamke huyo.

"Maafisa wa polisi wa kituo cha polisi cha Macalder waliitwa katika eneo la tukio na kubaini kuwa mzee huyo mwenye umri wa miaka 52 aliingia ndani ya chumba hicho akiwa ameongozana na msichana mwenye nusu ya umri wake, na kuzimia saa kadhaa baadaye kufuatia tukio la jioni," DCI alisema.

Mwili wa marehemu ulihamishwa kupelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Migori level IV ukisubiri uchunguzi wa maiti kufanyika.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI JULAI 30,2022





Magazetini leo Jumamosi July 30 2022














Share:

Friday, 29 July 2022

RAIS DKT. MWINYI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA MTANGAZAJI WA ZBC



RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi ametoa salamu za pole kwa familia, ndugu jamaa wa marafiki kufuatia kifo cha mtangazaji mkongwe wa ZBC televisheni, Bi.Sharifa Maulid.


Katika salamu hizo za pole, Rais Dkt. Mwinyi ameeleza kusikitishwa na kifo cha mtangazaji huyo mkongwe na kuisihi familia ya marehemu kuwa na subira katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo.


“Natoa mkono wa pole kufuatia kifo cha mtangazaji mkongwe wa ZBC televisheni, marehemu bibi Sharifa Maulid, naukumbuka umahiri wake katika utangazaji kwani alikuwa hodari katika kazi yake hiyo na kazi zake nyingine alizozifanya mbali ya utangazaji,”ilieleza sehemu ya salamu za pole alizozitoa Rais Dkt.Mwinyi.


Aidha, Rais Dkt. Mwinyi amewasihi watangazaji na wafanyakazi wote wa sekta ya habari nchini kufuata nyayo na uzalendo wa marehemu bibi Sharifa Maulid ambaye hadi anafariki dunia alikuwa Afisa Habari katika Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto.


Rais Dkt. Mwinyi amemuomba Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi, Amin.
Share:

JITIBU TATIZO LA NGUVU ZA KIUME KWA KUTUMIA FULL POWER

Upungufu wa nguvu za kiume ni hali ya kushindwa kufanya tendo la ndoa kikamilifu ,shughuli ya tendo la ndoa huhusisha akili, homoni, neva, misuli, hisia na mirija ya damu. Upungufu wa nguvu za kiume huashiria kutokuwa sawa kiafya hivyo ni tatizo linalohitaji tiba.

CHANZO CHA TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

Tatizo la nguvu za kiume lina vyanzo vingi ambavyo mara nyingi wengi huvipuuza, hivyo vyanzo huathiri taratibu na vingine huathiri haraka, tunashauri watu kuwa makini sana ili kujiimarisha vizuri. Kuna mitindo ya maisha inayoweza kukuweka hatarini kupata tatizo la nguvu za kiume nayo ni pamoja na;


1. Kuwa na halemu (Cholesterol) na Shinikizo la damu (B.P) au ugonjwa wa moyo

2. Kuvuta sigala na unywaji wa pombe

3. Uzito kupita kiasi na unene uliozidi

4. Ulaji holela wa vyakula vyenye mafuta mengi na sukari nyingi

5. Kisukari

6. Kuwa na mawazo na wasiwasi

7. Matumizi ya madawa mbalimbali

8. Umri hasa wazee

9. Utumiaji wa vinywaji vinavyobadili hali ya mwili

10. Kuwa na tatizo la kibofu

11. Tabia za kujichua kwa muda mrefu

12. Kutopata usingizi kamili

13. Matumizi makubwa ya dawa zenye kemikali za kutibia magonjwa kama kansa, vidonda vya tumbo, moyo, kisukari, B.P, na magonjwa mengine


DALILI ZA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

Dalili za kuonesha kuwa una tatizo la upungufu wa nguvu za kiume karibia zote zinahusiana na hali itakayo onekana katika tendo la ndoa au mda wa kujamiiana, hizo dalili zake ni kama;


1. Kuwahi kufika kileleni

2. Kukosa hamu ya mapenzi

3. Kushindwa kurudia tendo la ndoa

4. Uume kusimama kwa ulegevu au kushindwa kusimamisha

5. Kuchoka sana baada ya tendo la ndoa na hata kukinai kabisa au hata kusikia kichefuchefu; Miguu, uso na tumbo kuvimba na kujaa maji

6. Kuhisi maumivu wakati wa tendo la ndoa au baada ya tendo hilo

7. Kuchelewa sana kufika kileleni (au kushindwa kufika kileleni kabisa)

8. Kukosa pumzi na uchangamfu wa mwili katika utendaji


TIBA SAHIHI YA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME

FULL POWER

⇨Ni dawa ya vidonge ya miti shamba inaongeza nguvu za kiume na kutibu kabisa tatizo hilo.

⇨Inaongeza hamu ya tendo la ndoa

⇨Inakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya Dakika 30 na kurudia tendo zaidi ya mara nne na zaidi.


ZAT 50
⇨ Inarutubisha maumbile ya uume na kunenepesha urefu nchi 6,unene sentimita 4

⇨Dawa hii ni ya kutibu kabisa tatizo hilo.


Pia tunatibu Magonjwa mengine kama


Matatizo ya pumu,Bawasiri, vidonda vya tumbo, Kisukari, Magonjwa sugu ya zinaa,Kaswende,U.T.I , kiuno,miguu kuwaka moto, Fangasi sehemu za Siri, kupunguza unene wa mwili,tumbo kuunguruma,kujaa gesi, matatizo ya uzazi kwa wanawake, kurutubisha mbegu za uzazi kwa akina baba, matatizo ya meno tunatibu bila kung’oa


Ndugu mteja Epuka midawa inayouzwa mitaani ambayo sio sahihi kwa matumizi ya binadamu JALI AFYA YAKO OKOA NDOA NA MAISHA YAKO

Kliniki yetu inapatikana Zanzibar, Dar es salaam na Shinyanga

Wasiliana nasi kwa simu namba 071770 22 27 au 0754568767  utatumiwa sehemu yoyote ulipo
Share:

MUME WANGU ALIPANGA KUNIFURUSHA BAADA TU YA KUPATA KIDOSHO MJINI


Kwa jina ni Elizabeth kutoka katika kaunti ya Bungoma. Tulikuwa kwenye ndoa na mume wangu Benson kwa muda wa miaka minne sasa. Tulikuwa na maisha mazuri kwani hakuna lolote lililokuwa na kuvunja uhusiano wetu kuja miogoni mwetu.

 Benson alikuwa ni mwanaume ambaye alijali maslahi yangu nami nilikuwa wa kuzingatia yote aliyonishauri kwenye ndoa kwani sikutaka kukosana naye. Baadaye alipata kazi mjini Nairobi na hapo tukawa na makubaliano baina yetu kwamba angeenda mjini kuifanya kazi ile name ningebaki kijijini. Aliupokelea uamuzi ule kwa mikono yote na hapo akawa mwenye furaha ajabu.

Kila mwezi alikuwa akinitumia hela za kufanya shuguli mbalimbali pale nyumbani kwetu. Nilimwamini kwani hakuna hata wakati mmoja mume wangu alionekana kuwavizia vidosho wengine. Jambo hili lilinipelekea mimi kumwonyesha mapenzi ya dhati. 

Kila baada ya mwezi mmoja alikuwa akitembea nyumbani kunijulia hali na hapo sikuwa na shaka ya uwepo wake mjini Nairobi ilhali hatukuwa naye. Baada ya siku kupita tabia yake ilianza kubadilika. Hakuwa akipiga simu tena kama ilivyokuwa kawaida yake kila siku.

 Nilianza kushuku mienendo hii yake kwani nilishuku alikuwa amepata kidosho mjini. Pesa alizokuwa akituma kila mwisho wa mwezi zilipungua kwani hata wakati mwingine hakuwa akituma hata senti moja.

Wakati mwingine nilipompigia simu sauti ya mwanamke ilisikika kwenye simu yake ishara tu alikuwa keshapata mpenzi mwingine. Nilifunga safari na kwenda Nairobi kujua alipokuwa akiishi. Hakuwa akishika simu yangu nilipofika.


 Nyumbani pake nilipigwa na butwaa baada ya kupata mwanamke mwingine kwenye nyumba ile aliyeniambia kwamba alikuwa mke wake na hakuna lolote ningefanya. Nilienda kulala kwa dada yangu usiku ule kwani sikutaka mapigano baina yangu na mwanamke yule.

Dadangu alinihurumia kwa mambo yaliyonikumba na hata akanipa ushauri kwamba palikuwepo na dakatari tajika wa miti shamba kwa jina Kiwanga ambaye angenisaidia. Alinipa nambari za Daktari Kiwanga na hapo nikampigia simu na kutenga siku ambayo tungekutana kwa ajili ya usaidizi wake.

Baada ya wiki moja nilikuwa kwenye ofisi ya dakatri Kiwanga. Nilimwelezea yote yaliyonikumba. Alifanya shughuli zake za mitishamba na kunipa hakikisho kwamba yote yangekuwa sawa na kwamba mume wangu angerejea nyumbani kwa msamaha. Nilirejea nyumbani na baada ya siku tatu sikuyaamini macho yangu. Mume wangu alikuja nyumbani akiwa mnyonge ajabu. Aliniomba msamaha kwa yote yalikyoukuwa kesha tokea.

 Nilimsamehea kwa kuwa nilikuwa mwenye mapenzi ya dhati kwake. Baadaye tulienda naye mjini. Tangu siku ile mume wangu amekuwa ni mtu mwaminifu ajabu kwenye ndoa. Pongezi sana kwa daktari Kiwanga kwa huduma yako. Mtu yeyote ambaye ana shida kama hii anaweza kumtembelea daktari Kiwanga kwani ndiye daktari tajika wa miti shamba katika eno zima la Afrika ya Mashariki.

Daktari Kiwanga hutibu maradhi kama kifua kikuu, kisukari, msukomo wa damu, kifafa na magonjwa mengineyo. Husuluhisha shida za kifamilia kama kutokouwa na uwezo wa kupata mtoto, kutopata mchumba wako wa maisha, shida za ndoa, kuwa na bahati katika maisha haswa katika michezo ya kamari na mengineyo. 


Ama kwa hakika daktri Kiwanga ni mtu wa kutegemewa katika jamii kwa ajili ya kusuluhisha mambo yanayowakosesha watu mbalimbali usingizi ama maisha bora yenye matamanio. Kwa mahojiano na daktari Kiwanga kwa ajili ya kusuluhisha shida zako, piga simu kwa nambari +254769404965/barua pepe kiwangadoctors@gmail.com ama tembelea wavuti wwww.kiwangadoctors.com kwa mengi zaidi.

Share:

HATUPELEKI UMEME VIJIJINI KUWASHA TAA PEKEE – MAKAMBA


Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba (wa pili kutoka) akizungumza na Meneja wa Kiwanda cha KUZA Afrika, Rob Clowes ambacho kinachakata maparachichi ili kutengeneza mafuta na bidhaa nyingine wilayani Rungwe mkoani Mbeya. Kiwanda hicho kinafanya uzalishaji kwa kutumia umeme uliunganishwa na TANESCO.
Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba akifungua valvu ili kuruhusu majimoto yanayotoka ardhini kupita katika kisima kifupi cha utafiti wa Jotoardhi kilichochorongwa katika eneo la Kiejo-Mbaka wilayani Rungwe mkoani Mbeya

………………………

Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba amesema kuwa, Serikali haisambazi umeme vijijini kwa ajili ya kuwasha taa peke yake bali kuchagiza pia shughuli za kiuchumi ikiwemo uanzishaji wa viwanda.

Amesema hayo tarehe 28 Julai, 2022 baada ya kutembelea kiwanda kinachochakata parachichi ili kutengeneza mafuta cha KUZA AFRIKA kilichopo wilayani Rungwe Mkoa wa Mbeya mbacho kimeunganishiwa umeme na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Makamba alisema kuwa, uwepo wa kiwanda hicho ni matokeo ya uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali katika sekta ya Nishati ambao umezaa matunda kwani kiwanda hicho pamoja na kuongezea thamani mazao ya Wakulima, kimezalisha ajira zaidi ya 200 ndani ya kiwanda na katika mashamba ya parachichi.

Aliongeza kuwa, msingi mzima wa kupeleka umeme vijijini ni kusawazisha maendeleo kati ya watu wa vijijini na mijini kwani shughuli za kiuchumi kama za viwanda zinaboresha pia uchumi wa wananchi wa vijijini.

Meneja wa TANESCO, Wilaya ya Rungwe, Mhandisi Mukhsin Kijemkuu alimweleza Waziri wa Nishati kuwa, kiwanda hicho kabla ya kufungiwa transforma yake kilikuwa kikizalisha lita 2000 kwa siku lakini baada ya kupata Transfoma wiki moja iliyopita kinazalisha lita 4000 kwa siku.

Aliongeza kuwa kwa lita 4000 zinazotarajiwa kuzalishwa kwenye kiwanda hicho mwekezaji angetumia shilingi milioni 50 kununua dizeli ya kuendesha mitambo ila kwa kuwa sasa anatumia takriban shilingi milioni 30 kwa gharama za umeme ambayo ni pungufu ya gharama alizokuwa akiingia awali.

Pamoja na kuishukuru Wizara ya Nishati kwa kutenga fedha za kupeleka umeme kwenye maeneo kama hayo, Mhandisi Kijemkuu amekaribisha wawekezaji wengine kuwekeza kwenye miradi kama hiyo kwani hali ya upatikanaji umeme sasa imeimarika na pia TANESCO itaongeza mapato yake.

Katika hatua nyingine, Waziri wa Nishati alifika kwenye Kijiji cha Iramba Kata ya Ntaba wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya ili kukagua kazi zinazoendelea katika chanzo cha Jotoardhi cha Kiejo-Mbaka ambacho kinatarajiwa kuzalisha umeme utakaoingizwa kwenye gridi ya Taifa.

Waziri Makamba mara baada ya kukagua chanzo hicho, alisema kuwa “Serikali imeamua kuweka nguvu katika kuzalisha umeme kwa njia mbalimbali, tuna umeme wa Maji, Umeme wa Gesi na safari hii tumewekeza kwenye umeme wa Joto ardhi, hapa Kiejo-Mbaka ni moja ya vyanzo vya Jotoardhi ambavyo vina uwezekano wa kuzalisha umeme wa Joto ardhi.”

Alisema kuwa katika bajeti ya Wizara ya Nishati ya mwaka 2022/2023, Serikali imetenga shilingi Bilioni 5 kwa ajili ya kuendeleza miradi hiyo na kwamba Serikali imenunua mtambo maalum wa kuchoronga mpaka Kilometa 3 chini ili kuweza kulifikia joto ambalo litatoa mvuke utakaozungusha mtambo wa kuzalisha umeme.

Aliongeza kuwa, matarajio ni kuzalisha umeme wa kiasi cha megawati 200 ifikapo mwaka 2025 huku akitaja kuwa Tanzania kuna maeneo mengi yanayoweza kutoa nishati ya Jotoardhi ya kiasi cha megawati 5000.

Licha ya kuzalisha umeme, alitaja faida nyingine za Jotoardhi kuwa ni pamoja na ukaushaji wa mazao na kupasha moto nyumba kitalu ili kuongeza thamani ya mazao na ufugaji wa samaki kwani maji yanayotokana na jotoardhi hutumika kuongeza joto katika bwawa la samaki katika mazingira ya baridi na hivyo kupelekea samaki kukua kwa haraka.

Nishati ya Jotoardhi inatokana na joto linalotoka kwenye mwamba wenye joto unaochemsha maji yaliyoingia ardhini
Share:

KANISA KATOLIKI JIMBO LA SHINYANGA LAPATA MAPADRE WAPYA


MASHEMASI Watano ambao wanatarajiwa kupewa daraja la Upadre hapo kesho, na askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu, leo wamekiri imani Katoliki mbele ya askofu na Kanisa,ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya utolewaji wa daraja la Upadre.

Mashemasi hao ambao ni Emmanuel Kimambo wa Parokia teule ya Shishiyu, Emmanuel Gembuya wa Parokia ya Buhangija, Paul Mahona wa Parokia ya Wila, Simon Lutamula wa Parokia ya Mwamapalala na Eliasi Vumba wa Shirika la Ndugu wadogo wa Mtakatifu Francisco (Wakapuchini) wamekiri imani na kutia saini viapo vyao kupitia ibada ya masifu ya jioni, ambayo imefanyika katika Kanisa kuu la Mama Mwenye Huruma,Ngokolo mjini Shinyanga.
SAUTI ZA MASHEMASI WAKIKIRI IMANI


Akitoa mafundisho yake katika ibada hiyo, Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu,anewaomba waamini kuendelea kuwaombea Mashemasi hao ili watakapopewa daraja la Upadre ,waweze kutekeleza kwa uaminifu utume watakaokabidhiwa na kanisa.

Askofu Sangu amefafanua kuwa, daraja la Upadre ambalo watapewa hapo kesho, ni njia itakayowashirikisha katika huduma ya kikuhani ya kuokoa roho za watu na kuwatafuta wale waliopotea.
SAUTI YA ASKOFU SANGUMashemasi wakitia saini viapo vyao mbele ya AskofuMashemasi wakirudi katika nafasi zao baada ya kusaini viapo vyaoVicar wa Shirika la Wakapuchini kanda ya Tanzania Pd.Paschal Vincent Dohho (mwenye kanzu ya Ugoro) akiwa katika ibada ya masifu ya jioni Kanisa kuu NgokoloAskofu Sangu akiwa katika picha ya pamoja na Mashemasi mara baada ya Ibada ya Masifu ya jioni(Kushoto ni Katibu wa askofu Pd. Deusdedith Kisumo na Kulia ni Paroko wa Parokia ya Mwadui Pd.Michael Msabila)

Chanzo - http://radiofaraja.com/
Share:

Thursday, 28 July 2022

NAIBU WAZIRI MASANJA AKAGUA UJENZI WA NYUMBA MPYA 400 MSOMERA WILAYANI HANDENI


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe, Mary Masanja (Mb) akiwa ameongozana na Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Mhe. Siriel Mchembe (kushoto) na Askari wa SUMA JKT kukagua ujenzi wa nyumba 400 kijiji cha Msomera Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga leo.


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe, Mary Masanja (Mb) (katikati) akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Mhe. Siriel Mchembe (kushoto) wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa nyumba 400 kijiji cha Msomera Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga leo.


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe, Mary Masanja (Mb) akiwaelekeza Askari wa SUMA JKT kuhakikisha ifikapo tarehe 30 Agosti 2022 kaya zaidi ya 50 ziwe zimeletwa Msomera ,wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa nyumba 400 kijiji cha Msomera Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga leo.


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe, Mary Masanja (Mb) akiwasisitiza na vijana wanaojenga nyumba 400 katika kijiji cha Msomera kufanya kazi kwa uzalendo,wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa nyumba 400 kijiji cha Msomera Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga leo.


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe, Mary Masanja (Mb) akichota zege wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa nyumba 400 kijiji cha Msomera Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga leo.

**************************

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amekagua ujenzi wa nyumba mpya 400 katika kijiji cha Msomera Wilayani Handeni, Mkoani Tanga watakazohamia kwa hiari wananchi kutoka Ngorongoro.

Akizungumza katika ziara hiyo leo, Mhe. Masanja amewapongeza SUMA JKT kwa kufanya kazi vizuri kuhakikisha nyumba hizo zinakamilika kwa wakati.

“Maelekezo yetu ni kwamba hadi kufikia tarehe 30 Agosti 2022 kaya zaidi ya 50 ziwe zimeletwa katika nyumba hizi na hatuna mashaka na kazi mnayoifanya” Mhe. Masanja amesisitiza.

Aidha, Mhe. Masanja ameagiza watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni kukamilisha ujenzi wa kituo cha afya kwa wakati.

“Kwa kuwa Halmashauri mmepewa jukumu la kujenga kituo cha afya, kinatakiwa kikamilike ndani ya miezi minne, fanyeni kazi usiku na mchana kuhakikisha mnakamilisha. Tusingependa nyumba ziwe zimekamilika, huduma za afya ziwe bado”Mhe. Masanja amefafanua.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Mhe. Siriel Mchembe amesema kuwa agenda muhimu ni kuhakikisha wanafanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha ujenzi wa kituo cha afya.

Kwa upande wake Operation Commander ,Luteni Kanali Edward Anthony Mwanga amesema kuwa ndani ya miezi miwili watahakikisha wanakamilisha nyumba zote na kumuahidi Naibu Waziri kuwa hadi kufikia terehe 20 Agosti 2022 familia zaidi ya 50 zitakuwa zimehamia Msomera.

Ziara hiyo ina lengo la kuangalia utekelezaji wa majukumu ya Wizara na kuangalia changamoto ili kuzipatia ufumbuzi.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger