Monday, 18 July 2022

SIMBACHAWENE: KAMPENI GGM KILI CHALLENGE IMESAIDIA MAPAMBANO YA KUDHIBITI UKIMWI


WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Bunge na Uratibu, George Simbachawene (wa pili kushoto) akimkabidhi mmoja wa washiriki wanaopanda mlima Kilimanjaro kwa lengo la kuchangisha fedha za mapambano dhidi ya VVU kupitia kampeni ya GGM Kili Challenge 2022. Kushoto ni Mkurugenzi wa TACAIDS Dk. Leonard Maboko.


Na Mwandishi wetu

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Bunge na Uratibu, George Simbachawene amesema jitihada za Kampeni ya GGM Kili Chalenge pamoja na wadau mbalimbali kwa kushirikiana na Serikali, zimesaidia kupunguza vifo vitokanavyo na VVU/Ukimwi kwa asilimia 50 kutoka vifo 64,000 mwaka 2010 hadi 32,000 mwaka 2020.

 

Pia amesema maambukizi mapya ya VVU kwa watu wazima (miaka 15 na zaidi) yameshuka kutoka 110,000 mwaka 2010 hadi 68,000 mwaka 2020 wakati maambukizi mapya kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto yameshuka kutoka asilimia 18 mwaka 2010 hadi asilimia 7 mwaka 2020.

 

Simbachawene ametoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki wakati akiwaaga wapanda mlima Kilimanjaro 52 ambao kati yao 28 wanauzunguka mlima kwa baiskeli na 24 kwa kutembea kwa miguu.

 

Zoezi hilo lililoanza Julai 15, 2022, linaratibiwa na Kampuni ya Geita Gold Mine Limited (GGML) kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) kwa lengo la kuchangia fedha kwa ajili ya shughuli za udhibiti wa ukimwi. Wapanda mlima hao, watashuka Julai 21 mwaka huu.

 

Pamoja na mambo mengine Simbachawene alisema serikali itaendelea kuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa afua zinazotekelezwa za mwitikio wa VVU na UKIMWI zinaleta tija kwa makundi mbalimbali katika jamii.

 

Alisema ili kufikia malengo haya pamoja na mengine katika kuishinda vita hii dhidi ya VVU na UKIMWI, kunahitaji nguvu ya pamoja kati ya serikali na wadau wengine, hususan sekta binafsi ili kupata rasilimali fedha ya kutosha.

 

 “Kili challenge inalenga kupunguza athari za kupungua kwa misaada ya wahisani na kuiwezesha Nchi kuimarisha uwezo wa ndani kwa ajili ya kudhibiti UKIMWI”

 

Aidha, Makamu wa Rais wa AngloGold Ashanti - GGML anayesimami miradi endelevu kwa upande wa Ghana na Tanzania, Simon Shayo alisema kampeni hiyo ya GGM Kili Challenge imepiga hatua kubwa tangu kuanzishwa kwake mwaka 2002 hadi kufikia kuwa mfuko wa kimataifa, wenye kushirikisha wapanda mlima na waendesha baiskeli zaidi ya 700 kutoka mabara 6 na zaidi ya nchi 20.

 

Alisema kupitia kampeni ya hiyo, taasisi mbalimbali zimenufaika kwa kupata fedha za kutekeleza shughuli za mwitikio wa VVU na Ukimwi nchini.

 

“Kwa mfano, mwaka 2020 Mfuko wa Kilimanjaro Challenge ulitoa fedha taslim milioni 800 kwa taasisi 20 zisizo za kiserikali.

 

“Tunawakaribisha sana wadau na makampuni mbalimbali kuchangia na kushiriki katika kampeni hii,” alisema Shayo.

 

Aidha, aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa msaada wake na ushirikiano wa TACAIDS katika kampeni ya Kili Challenge tangu kuanzishwa kwake mwaka 2002.

 

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Dk. Leonard Maboko, alisema kwa muda wa miaka 20 tangu kampeni hiyo ianzishwe zaidi ya Sh bilioni 11 zimekusanywa na kusaidia katika kuendeleza mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI.

 

Alisema licha ya maendeleo mazuri yatokanayo na jitihada hizo, bado kuna maeneo ambayo yanahitajika nguvu zaidi ili kudhibiti VVU na UKIMWI na hatimaye kutokomeza VVU/UKIMWI ifikapo mwaka 2030 kama inavyoelekezwa katika malengo ya kidunia.

 

“Mojawapo ya malengo hayo ni kuzuia maambukizi mapya ya VVU hasa kwa vijana kwani zaidi ya theluthi moja ya maambukizi mapya hutokea kwa vijana wenye umri wa miaka 15-24, hususan vijana wa kike,” alisema.



Share:

JUVENTUS YAKUBALI KUMUUZA BEKI WAKE WA KIMATAIFA MATTHIS De LIGT KWENDA BAYERN MUNICH





Beki wa kimataifa wa Uholanzi, Matthijs de Ligt ambaye amekubali kujiunga Bayern Munich akitokea Juventus

KLABU ya Juventus ya Italia imekubali kumuuza Beki wake wa kati, Matthijs de Ligt (22) kwenda kwa mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich kwa ada ya Paundi Milioni 68 (Tsh. 186,320,000,000)

Taarifa kutoka Ujerumani zinaeleza kuwa beki huyo wa kimataifa wa Uholanzi atasaini mkataba wa miaka mitano na Bayern mara baada ya kukamilisha vipimo vya afya anavyotarajia kufanya leo katika jiji la Munich.

De Ligt anaondoka Juventus akiwa amekaa kwa misimu mitatu, akicheza mechi 177 na kufunga magoli nane. pia, alishinda taji la Serie A katika msimu wa 2019/20.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU JULAI 18,2022

Magazetini leo Jumatatu July 18,2022






































Share:

Sunday, 17 July 2022

VITUO VYA AFYA TANGA VYAPATIWA VIFAA TIBA NA MSD


Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Makorora mkoani Tanga, Dkt.Angelina Meshack akizungumza na baadhi ya watumishi wa MSD (hawapo picha) mara baada ya kutembelea kituo cha afya cha Makorora kilichopo mkoani Tanga

Vifaa tiba kwaajili ya upasuaji vilivyopo katika kituo cha afya Makorora mkoani Tanga vikiwa tayari kwaajili ya kutoa huduma ya upasuaji. Vifaa hivyo vimekabidhiwa hivi karibuni na Bohari ya Dawa (MSD). Vifaa tiba kwaajili ya upasuaji vilivyopo katika kituo cha afya Makorora mkoani Tanga vikiwa tayari kwaajili ya kutoa huduma ya upasuaji. Vifaa hivyo vimekabidhiwa hivi karibuni na Bohari ya Dawa (MSD).   Mfamasia Kituo cha Afya Makorora Tanga Bi.Gloria Urio akionesha baadhi ya vifaa tiba kwaajili ya upasuaji walivyokabidhiwa na Bohari ya Dawa hivi karibuni baada ya kuwa na changamoto ya vifaa tiba hivyo na kutokutoa huduma ya upasuaji kwenye kituo hicho cha Afya Mkoani Tanga.Mfamasia Kituo cha Afya Ngamiani mkoani Tanga, Bw.Michael Mrosso akiangalia vifaa tiba ambavyo wamekabidhiwa na MSD hivi karibuni Jenerata ambalo litatumika kuzalisha umeme pindi umeme wa kawaida unapotokea kukatia katika Kituo cha Afya Ngamiani mkoani Tanga. Jenereta hilo limekabidhiwa na Bohari ya Dawa (MSD) hivi karibuni.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

***********************

NA EMMANUEL MBATILO, TANGA

SERIKALI kupitia Bohari ya Dawa imepongezwa kwa kuwezesha kukabidhi vifaa tiba katika vituo vya afya mkoani Tanga, vifaa ambavyo vilikuwa changamoto katika utoaji huduma kwa baadhi ya vituo vya afya kwenye mkoa huo.

Akizungumza leo Julai 17,2022 mara baada ya kutembelewa na watumishi wa MSD mkoani humo, Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Makorora mkoani Tanga, Dkt.Angelina Meshack amesema walipokea vifaa vya kufanyia upasuaji ikiwemo kitanda cha upasuaji, mashine ya dawa ya usingizi na taa zinazotumika wakati wa upasuaji ambavyo vimekuwa msaada mkubwa katika hospitali kwani mwanzo kulikuwa na changamoto kwnye hutoaji huduma.

"Awali tulikuwa hatufanyi upasuaji kabisa kwahiyo tulivyopokea fedha kwaajili ya ukarabati majengo kwaajili ya kufanyia upasuaji na tulifanya hivyo na baadae vifaa vililetwa na MSD na kuanza kutoa huduma za upasuaji". Amesema Dkt.Angelina

Amesema baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo walianza kutoa huduma ya upasuaji na kwasasa wanafanya upasuaji mbalimbali wa mama wajawazito pamoja na upasuaji mdogo kwani hapo awali walikuwa wanawapeleka wagonjwa Bombo kwasababu huduma hiyo haikuwepo hapo kituoni.

Aidha Dkt.Angelina amesema kwa siku wanapokea wamama takribani 60 lakini mwanzo walikuwa wanashindwa kutoa huduma na hata pale mama anakuwa na uzazi pingamizi usiku inakuwa ni changamoto kumkimbiza mama na kuchelewa kupata huduma kwa mama mjamzito.

"Kwa ujio wa vifaa hivi imerahisisha mama mjamzito anaposhindwa kujifungua moja kwa moja tunaweza kumpa huduma ya upasuaji na tunaokoa maisha ya mama pamoja na kachanga". Amesema.

Pamoja na hayo Dkt.Angelina amesema walikabidhiwa pia na jenereta kwaajili kuzalisha umeme kwenye hospitali hiyo lakini wakaamua kuwasiliana na ofisi ya mganga mkuu ili waweze kuichukua ili waikabidhi kwenye vituo vingine ambavyo haina jenerata kwasababu kituo hicho kilikuwa na jenerata ambalo walikuwa wameshanunua awali.

Ameeleza kuwa hali ya upatikanaji wa dawa katika kituo hicho ni nzuri kwasababu kunadawa ambazo zinahitajika kwa muda wote na ngazi ya kituo, dawa hizo wanazo kwa asilimia 90 na wanaendelea kutoa huduma bora kwa wananchi .

Nae Mfamasia Kituo cha Afya Ngamiani mkoani humo, Bw.Michael Mrosso amesema walipokea vifaa tiba kwaaajili upasuaji pamoja na jenerata, vifaa ambavyo vilikuwa ni kilio kwao kwa muda mrefu.

Amesema wataendelea kujitahidi kutoa huduma bora kwakuwa kuna vifaa bora ambavyo wamekabidhiwa na serikali kwaajili ya kuwahudumia wananchi
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JULAI 17,2022


Magazetini leo Jumapili July 17,2022















Share:

Utafiti : HAKUNA FAIDA YA KUNYWA POMBE KWA WATU CHINI YA MIAKA 40


Kiasi kidogo cha pombe kinaweza kupunguza hatari ya ugonjwa wa moyo na mishipa, kiharusi na kisukari.

****
Hakuna kiasi cha pombe kinachofaa kwa watu chini ya umri wa miaka 40, hasa kutokana na vifo vinavyotokana na pombe kwa watu chini ya umri huo kwa mujibu wa utafiti mpya wa Chuo Cha Dawa cha Washington.


Utafiti huo uliofanywa kwa watu kuanzia umri wa miaka 15 hadi 95 katika mataifa 204 duniani, uligundua kwamba unywaji pombe hauna faida yoyote kiafya kwa watu walio chini ya umri wa miaka 40 lakini una athari kubwa kama vile ajali za magari na vifo.


Athari ni ndogo kwa watu wenye umri kuanzia miaka 65 ambao wengi huzingatia hunywaji wa pombe kwa kiwango kutokana na matatizo ya kiafya.

Via EATV
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger