Sunday, 10 July 2022

KAGAME KUWANIA TENA URAIS RWANDA

Rais wa Rwanda, Paul Kagame,amesema atagombea tena urais katika uchaguzi wa mwaka 2024.

Katika mahojiano na televisheni ya Ufaransa, Bwana Kagame mwenye umri wa miaka 64 amesema kuwa "anaangalia uwezekano wa kugombea kwa miaka mingine 20".

"Uchaguzi ni kuhusu watu kuchagua," aliongeza.

Katika mwaka 2015 Bw Kagame alibadilisha katiba na hivyo kumruhusu kubakia mamlakani hadi mwaka 2034.

Katika uchaguzi wa mwishii miaka mitano iliyopita, takwimu rasmi zilionyesha kuwa alishinda kwa 99%ya kura – jambo ambalo wengi nje ya nchi hiyo walilipinga kuwa lisilowezekana.

Rais Kagame alitetea vikali rekodi ya haki za binadamuya Rwanda katika Mkutano wa Jumuiya ya Madola uliofanyika mwezi Juni mjini Kigali.
Share:

CHUMA YA UVCCM 'CHIEF MAKWAIYA' AJITOSA KUGOMBEA UENYEKITI SHINYANGA MJINI


CHIEF Fravian Patrick Makwaiya (kushoto) akikabidhi Fomu ya kugombea nafasi ya Uenyekiti wa UVCCM wilaya ya Shinyanga, (kulia) ni Katibu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Naibu Katalambula akipokea Fomu hiyo.
 CHIEF Fravian Patrick Makwaiya (kushoto) akikabidhi Fomu ya kugombea nafasi ya Uenyekiti wa UVCCM wilaya ya Shinyanga, (kulia) ni Katibu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Naibu Katalambula akipokea Fomu hiyo.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

CHIEF Fravian Patrick Makwaiya aliyekuwa Afisa Masoko wa Kampuni ya Jambo Food Products ya mkoani Shinyanga, amechukua na kuirejesha kwa wakati fomu ya kugombea nafasi ya Uenyekiti ya Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Shinyanga Mjini.

Amechukua Fomu hiyo leo Julai 10 ,2022 katika Ofisi za (UVCCM) wilaya ya Shinyanga Mjini na kuirejesha.

Akizungumza wakati wa uchukuaji na urejeshaji wa fomu hiyo, amesema Umoja huo wa Vijana wa CCM (UVCCM) wilaya ya Shinyanga Mjini, unahitaji kijana makini, mwenye ushawishi ndani ya Chama na Serikali, na mwenye kuziishi changamoto za vijana na kuzitatua kwa wakati, sifa ambazo yeye anazo.

Makwaiya almaarufu kwa jina la Chuma cha UVCCM, ameongeza sifa zingine ni kusimamia ajenda za vijana kwenye vikao na nje ya vikao, ili aweze kuleta maendeleo ndani ya umoja wa vijana.

"Umoja wa Vijana (UVCCM) wilaya ya Shinyanga mjini, unahitaji kuwa na Mwenyekiti Mchapakazi na Mwaminifu kama mimi Makwaiya na siyo kijana asiyeweza kutatua shida za vijana," amesema Chief Makwaiya.

Aidha, amesema kutokana uzoefu wake wa uongozi alionao ndani ya Chama na Serikali, na amewahi kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi ndiyo sababu iliyomsukuma kugombea nafasi hiyo ya Uenyekiti UVCCM wilaya ya Shinyanga, ili kuleta maendeleo ndani ya umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM).

Kwa upande wake Katibu wa Umoja wa Vijana (UVCCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini Naibu Katalambula, amesema mpaka sasa waliochukua Fomu kugombea nafasi ya Uenyekiti (UVCCM) wilayani humo wamefika 10.

 CHIEF; Fravian Patrick Makwaiya (kushoto) akikabidhi Fomu ya kugombea nafasi ya Uenyekiti wa UVCCM wilaya ya Shinyanga, (kulia) ni Katibu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Naibu Katalambula akipokea Fomu hiyo.
Share:

WAZIRI MAKAMBA KUFANYA ZIARA YA SIKU 21 KUKAGUA MIRADI KATIKA MIKOA 14 NCHINI

Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 10,2022 katika Ofisi za Wizara hiyo Jijini Dar es Salaam.

**********************

Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba anatarajia kufanya ziara ya siku 21 kuanzia kesho Julai 11, 2022, katika mikoa 14 na Wilaya 38 kwa lengo la kukagua na kusimamia miradi inayotekelezwa na Wizara hiyo kwa lengo la kuinua uchumi wa Watanzania.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam, Waziri Makamba amesema kuwa katika ziara yake hiyo atapokea kero na maoni kutoka kwa wananchi kuhusu utekelezaji na changamoto za upatikanaji wa umeme ili Serikali iweze kuzitatua na kuweka sekta hiyo imara Zaidi kwa maendeleo ya Taifa.

“Nitapita katika maeneo niliyoyataja katika mikoa ya Mara, Mwanza, Geita, Simiyu, Kagera, Shinyanga, Tabora, Katavi, Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe, Ruvuma, na mwisho ni mkoa wa Mtwara lakini mikoa mingine itahusika katika awamu ijayo, na katika maeneo haya nitazungumza na wananchi na kupokea kero na maoni ili kuimarisha utendaji wa sekta ya nishati nchini”, Alisema Waziri Makamba.

Waziri Makamba alisema Kipaumbele katika ziara hiyo itakuwa ni kuelimisha wananchi kuhusu upatikanaji wa matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia, usambaaji wa umeme vijijini na Vitongoji pamoja na upatikanaji wa umeme wa uhakika katika maeneo tajwa.

Maeneo mengine ya kipaumbele katika ziara hiyo ni uboreshaji wa huduma zinazotolewa na Wizara na Taasisi zake na usambazaji wa mafuta salama na ya bei nafuu kwa wananchi ili kuzuia matumizi ya mafuta machafu ambayo yanasababisha uharibifu wa vyombo vyao vya moyo .

Aidha, Waziri Makamba alisema lengo la jumla la ziara hiyo ni kusogeza huduma za Wizara kwa wananchi hasa wale wa maeneo ya vijijini na pia kuongeza uelewa kwa Watanzania kuhusu sekta ya nishati na mageuzi makubwa yanayofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita Chini ya Uongozi wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan yenye lengo la kuhakikisha kwamba sekta ya nishati inachangia katika ukuaji wa uchumi na kuboresha Maisha ya Watanzania
Share:

SIMBA GAS YAJIWEKA TAYARI KWA UCHIMBAJI WA GESI YA UKAA BAADA YA KUPOKEA RIPOTI YA UTAFITI KUTOKA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM


Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa William Anangisye (wa pili kushoto) akimkabidhi Ripoti ya Utafiti wa Gesi Ukaa, Mkurugenzi Mtendaji wa Simbagas, David Ndelwa (wa pili kulia) kwa ajili ya kampuni hiyo kuanza uchimbaji wa gesi hiyo mkoani Mbeya, hafla ya makabidhiano ilifanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ,wa pili kutoka kulia ni Mkuu wa kitivo cha Jiolojia na Madini wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt Elisante Mshiu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera.
**


Kampuni ya Kitanzania ya Simba Gas, inajiandaa na uchimbaji wa gesi ya ukaa (Carbon dioxide) huku ikilenga kukidhi mahitaji yanayoongezeka ya bidhaa hiyo katika soko la ndani na nje.

Uchimbaji utaanza baada ya kupata vibali vyote vya udhibiti kutoka katika taasisi zote zinazohusika.

Haya yanajiri wakati kampuni hiyo ikipata uhakika wa upatikanaji wa gesi ya ukaa katika eneo la Kata ya Suma lililopo Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya baada ya zoezi la utafiti wa miezi miwili lililofanywa na wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Simba Gas - ambayo ilisajiliwa mwaka 2021 kama sehemu ya kundi la makampuni ya Simba ikijikita katika kuchimba na kuuza gesi ya ukaa imepokea matokeo ya utafiti kutoka kitivo cha jiologia na Madini cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakati wa hafla iliyohudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya Nishati na Madini ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mh. Juma Zuberi Homera.

Gesi ya Ukaa hutumika katika utengenezaji wa vinywaji vyenye gesi, Pia hutumiwa kama kipoozo katika vizima moto kwa kuingizwa katika vifaa vya uokoaji, uchomelea vyuma katika miradi mikubwa, utengenezaji wa barafu kavu (dry ice) zinazotumika kupozea vinjwaji , ulipuaji wa makaa ya mawe, utengenezaji wa vifaa vya mpira na plastiki, ukuzaji wa mimea katika vitalu nyumba na pia kupunguza nguvu za wanyama kabla ya kuchinjwa.

Akiongea wakati wa hafla ya kupokea ripoti ya utafiti, Mkurugenzi wa kampuni Simba Gas ndugu David Ndelwa, alisema soko la gesi ya ukaa linakua kwa kasi kubwa ndani na nje ya nchi. "Kwa sasa, mahitaji ya gesi ukaa katika soko la ndani yanafikia tani 1,060 kwa wiki na tunao upungufu wa tani 360 kwa wiki,” alisema.

Vile vile, mahitaji ya soko la mauzo ya nje la gesi ya ukaa kwa sasa ni takribani tani 2,000 ambapo upungufu ni tani 1,460.

"Inakadiriwa kuwa hadi sasa, soko la kimataifa la gesi ukaa linafikia thamani ya dola bilioni 10.36. Kampuni yetu imejiandaa vya kutosha na itawekeza kwa kiasi kikubwa ili kuhakikisha kuwa tunatumia rasilimali tulizo nazo ili kukidhi mahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi,” alisema David Ndelwa

David Ndelwa alisema Simba Gas, imefanya utafiti na kuona soko kubwa la gesi ukaa katika nchi za Zambia, Zimbabwe, Congo, Malawi, Msumbiji, Afrika Kusini, Botswana, Angola, Sudan Kusini, Rwanda na Namibia pamoja na nchi nyinginezo.

“tunatambua kwa kusafirisha gesi yetu nje ya nchi, tutaleta fedha za kigeni nchini. Pia tutazalisha nafasi za ajira za moja kwa moja 150 na zingine 300 za muda maalum” alisema.

Hata hivyo alibainisha kuwa tafiti zaidi zitalazimika kufanyika ili kukidhi matakwa ya kimataifa ya uvunaji wa bidhaa hiyo na ameiomba Serikali kuendelea kuweka mazingira mazuri yatakayovutia ufadhili zaidi wa shughuli hizo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mh. Juma Zuberi Homera, alisema Serikali, inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan, inajitahidi kuboresha mazingira ya biashara na kuvutia uwekezaji katika sekta ya nishati na viwanda miongoni mwa mambo mengine.

Aliipongeza Simba Gas kwa kuwekeza Mbeya, na kubainisha kuwa kwa kufanya hivyo, kampuni hiyo itakuwa na mchango mkubwa katika kufanikisha azma ya serikali ya kukuza sekta ya uwekezaji na kuisaidia nchi kukuza uchumi wake.

"Mradi huu utakapoanza rasmi, utazalisha ajira, kuongeza mapato ya serikali za mitaa na kusaidia jamii kupitia mipango ya uwajibikaji kwa jamii," alisema, akibainisha kuwa Serikali itaendelea kuunga mkono uwekezaji huo.

Naye Mkuu wa kitivo cha Jiolojia na Madini wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt Elisante Mshiu alisema anawashukuru kampuni ya Simba Gas kwa kuwaamini wataalamu wa ndani ambao wamejikita kuleta ukombozi na mageuzi makubwa ya kufanya tafiti za kimkakati na kuhakikisha taifa linanufaika na rasilimali zake.

Simba gesi wamedhubutu kufanya tafiti katika uchimbaji wa gesi ukaa, tunaamini watafungua fursa nyingi pia kwa vijana wetu ambao tunawazalisha wakiwa wamebobea katika kuendesha mitambo ya gesi na itafungua milango ya ajira kwa vijana wetu.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa William Anangisye (wa pili kushoto) akimkabidhi Ripoti ya Utafiti wa Gesi Ukaa, Mkurugenzi Mtendaji wa Simbagas, David Ndelwa (wa pili kulia) kwa ajili ya kampuni hiyo kuanza uchimbaji wa gesi hiyo mkoani Mbeya, hafla ya makabidhiano ilifanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam . Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera na kulia ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Simba, Farid Nahdi(kushoto) ni (Kushoto) ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Angelina Ngalula .
Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia matukio wakati wa hafla hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Simbagas, David Ndelwa, akizungumza wakati wa hafla
Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia matukio wakati wa hafla hiyo.
Baadhi ya viongozi wa Serikali kutoka mkoani Mbeya wakifuatilia matukio wakati wa hafla hiyo.
Share:

Tanzia : BI HINDU AFARIKI DUNIA


Picha ya Bi Hindu enzi za uhai wake

Mmoja wa waasisi wa Kaole Sanaa Bi Chuma Suleiman maarufu kama 'Bi Hindu' amefariki dunia leo nyumbani kwake Magomeni, Dar es Salaam baada ya kusumbuliwa na maradhi ya muda mrefu.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JULAI 10,2022





Share:

Saturday, 9 July 2022

RAIS SAMIA AMTEUA HABIBU JUMA SULUO KUWA MKURUGENZI MKUU LATRA

Share:

KABATI AONGOZA MAMIA YA WATU WENYE ULEMAVU KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA IRINGA



Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Iringa Mhe. Rita Kabati akiwasalimu wageni waalikwa wakiwemo watu wenye ulemavu waliohudhuria Kongamano la watu wenye ulemavu wa Mkoa huo mara baada ya kupokea maandamano maalum ya watu wenye ulemavu yaliyoanzia katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa na kupokelewa katika viwanja vya Garden vilivypo Posta katikati ya Mji wa Iringa leo Julai 9,2022 ambapo pamoja na mambo mengine lililenga kutoa Elimu ya Sensa kwa watu wenye ulemavu.


Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Iringa Mhe. Rita Kabati akizungumza na watu wenyeulemavu na wageni wengine waalikwa alipokuwa akitoa hotuba yake juu ya Kongamano hilo na kumkaribisha Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Iinga Queen Sendiga kuzungumza,


Mkuu wa Mkoa wa Iinga Queen Sendiga akizungumza na hadhara iliyohudhuria katika Kongamano hilo alipokuwa akitoa hotuba yake kuzindua rasmi kongamano hilo lililofanyika leo Julai 9,2022 kwenye viwanja vya Posta katikati ya Mji wa Iringa. Mhe. Sendika ametumia jukwaa hilo kukemea vitendo vya ukatili wa kijinsia viivyokithiri katika mkoa huo na kuwataka wazazi wenye watoto wenye ulemavu kutowaficha katika zoezi la Sensa linalotarajia kufanyika mwezi Ogasti, Mwaka huu.


Sehemu ya Umati wa watu wenye ulemavu wakisikiliza Hotuba zilizokuwa zikitolewa na viongozi waliokuwa wakizungumza kwenye Kongamano hilo.


Mwalimu wa Shule ya Msingi visiwi Mkoa wa Iringa ambaye ni mtaalamu wa Lugha ya alama Mwl. Alikasuswe Mwandosya (kulia) akiwaongoza wanafunzi wake wenye ulemavu wa kusikia kutafasili hotuba mbalimbali zilizokuwa zinatolewa na wageni waliopo meza kuu akiwemo Mgeni rasmi Mhe. Queen sendiga (hayumo pichani) kwenye Kongamano hilo lililofanyika Mkoani Irnga leo Julai 9,2022. PICHA ZOTE NA: HUGHES DUGILO


Na: Hughes Dugilo, IRINGA.


Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Iringa Mhe. Rita Kabati amewaongoza mamia ya watu wenye ulemavu wa Mkoa huo katika Kongamano maalum lililolenga kupinga ukatili wa kijinsia pamoja na kutoa elimu ya Sensa ili kuwajengea uelewa na kujitokeza kuhesabiwa katika zoezi la Sensa linalotarajiwa kufanyika Mwezi Ogasti Mwaka huu.


Kongamano hilo lililohudhuriwa na mamia ya watu wenye ulemavu kutoka katika wilaya zote za mkoa wa Iringa lilianza kwa maandamano maalum yaliyoanzia katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo na kupokelewa na Mgeni rasmi wa shughuli hiyo Mkuu wa Mkoa huo Queen Sendiga katika Viwanja vya Garden vilivyopo Posta katikati ya Mji wa Iringa.


Akizungumza alipokuwa akitoa hotuba yake ya utangulizi alipokuwa akimkaribisha mgeni rasmi, Mhe. Kabati amesema kuwa imekuwa ni ndoto na kiu yake ya muda mrefu pia imetokana na kushuhudia changamoto nyingi wanazokumbana nazo watu wa makundi maalum hususani wenye ulemavu, wazee, watoto, yatima na wanawake ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri a Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan za kupinga ukatili wa Kijinsia.

"Mhe Mgeni Rasmi kutokana na changamoto hizo nilianza kuchukua hatua mbalimbali kuhakikisha napunguza au kuondoa changamoto hizo kabisa"

"Baadhi ya hatua hizo ni pamoja na kupeleka maswali na hoja zinazohusu watu wenye Ulemavu Bungeni ili kutafuta ufumbuzi ikiwemo mabadiliko ya kisheria na sera mbalimbali kuendana na mazingira yao"

"Hatua nyingine niliamua kuanzisha kampeni maalum ya kusaidia vifaa saidizi ikiwemo fimbo, basikeli, mafuta na hata kuboresha miundombinu katika baadhi ya maeneo ili wasikutane na changamoto hiyo" amesema Mhe. Kabati.



Aidha, ameongeza kuwa baada ya kuona hali ya uhitaji katika jamii ni kubwa, aliamua kuanzisha Taasisi maalum ya kushughulikia changamoto zinazowakabili watu waliopo kwenye makundi maalum inayoitwa RITTA KABATI TRUST FUND, ambayo itajihusisha moja kwa moja kutafuta ufumbuzi wa changamoto za watu wenye mahitaji maalum kwa kuwafuata kwenye maeneo yao na kuwatambua ili kufanya uratibu wa kuwasaidia.

"Taasisi hii inalenga Kukuza utu na heshima kwa watu wenye ulemavu na kutoa ushauri wa matibabu bila malipo kwa walemavu pamoaja na kusaidia miradi na shughuli nyingine za kiuchumi zinazoendeshwa na watu wenye ulemavu" ameongeza Mhe. Kabati.

Aidha amebainisha kuwa kazi nyingine ni kuanzisha na kudumisha vituo vya walemavu ili kusaidia jamii na kujihusisha katika michezo hususani ya watu wenye ulemavu kwa kuanzisha mashindano mbalimbali ya michezo na burudani katika Mkoa wa Iringa.

Kazi nyingine ni pamoja na kusaidia programu na mipango inayolenga kuwaelimisha na kwafahamisha wazazi na walezi wa watoto wenye ulemavu kuhusu changamoto mahususi zinazowakabili watoto wenye ulemavu na jinsi ya kuwatunza.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Iringa Queen Sendiga amempongeza Mbunge Kabati kwa hatua yake ya kusaidia watu wenye mahitaji maalum na kwamba kwa kufanya hivyo anaunga mkono jitihada za Serkali ya awamu ya sita ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kupiga vita unyanyasaji wa kijinsia na vitendo vya ukatili hasa kwa watoto na walemavu.

Sendiga amsema kuwa takwimu zinaonesha kuwa Mkoa huo unaongoza kwa ukatili wa kijinsia na kwamba jamii yote hususani wakazi wa Mkoa huo wanapaswa kuunga mkono juhudi zinazofanywa na wadau mbalimbali katika kutokomeza vitendo hivyo kama anavyofanya Mbunge Kabati.

"Ni aibu sana na fedheha kwa mkoa wetu kuongoza katika vitendo vya ukatili wa kijinsia, tunapaswa kupiga vita kwa nguvu zetu zote na mtu akikutwa na hatia ya kuhusishwa na vitendo hivi anapaswa kuchukuliwa hatua kali hata kufungwa maisha" amsema Mkuu wa Mkoa huyo huku akionesha kukasirishwa na vitendo hivyo.

katika hatua nyingine amezungumzia umuhimu wa watu wenye ulemavu kushiriki katika Sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika mwezi Ogasti mwaka huu na kuhimiza kuhesabiwa kwa watu wenye ulemavu na kwamba zoezi hilo litaifanya Serikali kutambua idadi ya watu hao na hivyo kupata huduma kwa urahisi kutokana na mahitaji yao na maeneo walipo.

"Ndugu zangu naomba sana kuhamasisha wazazi na walezi kuhakikisha watu wote wenye ulemavu tulinao majumbani wanahesabiwa, usimfiche mtu mwenye ulemavu kwani kwa kufanya hivyo utaifanya Serikali kukosa idadi yao na hivyo kushindwa kuwafikia kuwapatia huduma zao wanazostahili" amesisitiza RC Sendinga. MATUKIO KATIKA PICHA MBALIMBALI ZA MAANDAMANO

















Share:

WANAJESHI WAWILI WAFARIKI AJALI YA GARI KUPINDUKA KIGOMA



Mabaki ya gari ya jeshi iliyosababisha vifo vya wanajeshi wawili na wengine wanne kujeruhiwa baada ya kupinduka katika eneo la Kidahwe halmashauri ya wilaya Kigoma.
(Picha na Fadhili Abdallah)

Na Fadhili Abdallah,Kigoma


Askari wawili wa jeshi la wananchi wa Tanzania wamefariki dunia na wengine wanne kujeruhiwa vibaya kufuatia gari walilokuwa wakisafiria kuachia njia na kupinduka.


Kaimu Kamanda wa polisi mkoawa Kigoma,Menrad Sindani akitoa taarifa kwa waandishi wa habari mapema leo  amesema kuwa ajali hiyo imetokea eneo la kijiji cha Kidahwe wilaya ya Kigoma mkoani Kigoma jana mchana.


Ameitaja gari  iliyopata ajali kuwa ni aina ya Toyota Land Cruiser Hard top lenye namba za usajili 3186 JW 9768 la kikosi cha 825 JKT Mtabila wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma.


Kamanda Sindani amewataja waliofariki kwenye ajali hiyo kuwa ni Havent Michael (31) na Nicholaus Mbinda (31) ambao walifariki wakikimbizwa hospitali ya wilaya mkoa Kigoma Maweni.


Aidha Kamanda huyo wa polisi mkoa Kigoma amewataja waliojeruhiwa kwenye ajali hiyo kuwa Andrea Mathayo (32), Manyama Karilo (32), Ngongolina Julius (19) na Ramadhani Kapile  Dereva wa gari lililopata ajali.


"Kwa sasa miili ya marehemu ipo chumba cha kuhifadhia maiti hospitali ya mkoa Kigoma Maweni na majeruhi wamelazwa hospitalini hapo huku taratibu zikifanywa kuwapeleka majeruhi hospitali ya jeshi Lugalo Jijini Dar es Salaam,"Alisema Kamanda Sindani.
Share:

MSEMAJI WA SERIKALI AWATAKA WADAU KUSHIRIKIANA NA OSHA


Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa akipata ufafanuzi kutoka kwa wakaguzi wa OSHA, Simon Lwaho na Maria Ndaskoy kuhusu huduma mbalimbali zinazopatikana katika banda la OSHA katika Maonesho ya 46 ya Sabasaba


Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, akipata elimu kutoka kwa Mkaguzi wa Afya ya Mazingira wa OSHA, Simon Lwaho juu ya namna sahihi ya ukaaji katika dawati la kazi


Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa akipimwa macho na Mkaguzi wa Afya wa OSHA, Dkt. Zakayo Mmbaga kwa kutumia mashine ya kisasa alipotembelea banda la Maonesho la OSHA


Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa akipata maelezo kutoka kwa mtaalam wa afya wa OSHA, Dkt, Zakayo Mmbaga juu ya vipimo mbalimbali vya magonjwa yatokanayo na kazi vinavyofanywa na OSHA


Wadau mbali mbali wakipatiwa elimu ya usalama na afya katika banda la OSHA kwenye maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (DITF)- Saba Saba.

************************

Na Mwandishi Wetu

Mkurugenzi wa Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Bw. Gerson Msigwa, ametoa wito kwa waajiri na wafanyakazi kutoa ushirikiano kwa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) ili waweze kunufaika na ushauri na miongozo ya kitaalam juu ya uboreshaji wa mazingira ya kazi ambayo hutolewa na Taasisi hiyo.

Ametoa wito huo alipotembelea banda la OSHA katika maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea katika viwanja vya Saba Saba jijini Dar es Salaam.

“Kwanza niwapongeze OSHA kwa kazi nzuri ya kuhakikisha wanasimamia usalama mahali pa kazi wanayoifanya hivyo napenda kutoa wito katika eneo hili, watu wengi wakisikia OSHA wanakuwa na hofu lakini naomba tuwaone kama marafiki wa sehemu zetu za kazi kwakuwa wao ndio wanaokuja kutushauri ni vitu gani tuvizingatie tukiwa kazini ili tufanye kazi zetu na kurejea majumbani kwetu tukiwa salama,” amesema Msigwa nakuongeza:

“Hivyo niendelee kuwapongeza OSHA najua mnafika katika maeneo mengi nasasa mnajulikana kila mahali kwasababu kazi yenu inaonekana na watu wanaanza kutambua. Niwaombe watanzania tuendelee kutoa ushirikiano ili majukumu haya yafanyike kikamilifu jambo ambalo ni muhimu sana kwani tukiwapa ushirikiano ndivyo wanavyoweza kutushauri na kutuongoza vizuri zaidi na hivyo tutapunguza sana athari zinazoweza kuwapata wafanyakazi katika maeneo yetu ya kazi.”

Aidha, Msemaji Mkuu wa Serikali amewataka waajiri wote kushirikiana kikamilifu na OSHA katika kujenga mifumo madhubuti ya usalama na afya katika maeneo yao ya kazi ili kuwa na uzalishaji endelevu na wenye tija unaokwenda sambamba na kujali afya za wafanyakazi.

“Wakati mwingine tunaangalia sana gharama zinazotumika katika kushughulikia masuala ya usalama na afya lakini hatuangalii thamani ya kazi kubwa inayofanywa na OSHA kwenye maeneo yetu ya kazi hivyo ni lazima tutambue kwamba tukiwa na wafanyakazi wenye afya njema watazalisha zaidi na tutaokoa fedha nyingi zinazopotea katika matibabu ya wafanyakazi wanaoumia au kuugua kila mara pamoja na zile zinazotumika kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wapya,” amesema Msigwa.

Kwa upande wao baadhi ya waajiri na wafanyakazi waliotembelea banda la OSHA katika maonesho hayo wametoa maoni yao kuhusu huduma za OSHA.

“Kiukweli kupitia maonesho haya OSHA wametusaidia sana kwa kutupatia elimu na huduma mbali mbali ikiwemo usajili wa maeneo ya kazi na vyeti vya kukidhi matakwa ya awali ya usalama na afya mahali pa kazi (compliance license) huduma ambazo pengine tungeweza kuzipata kwa gharama kubwa,” amesema Bright Dickson Fue ambaye ni mmiliki wa eneo la kazi.

Nae Mhandisi Mary Estomihi ambaye ni mfanyakazi amesema: “Nimepita hapa katika banda la OSHA na nimejifunza mambo mengi ikiwemo masuala ya usalama wa umeme mahali pa kazi pamoja na namna ya kufanya tathmini ya vihatarishi vya usalama na afya mahali pa kazi.”



OSHA ni Taasisi chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu yenye jukumu la kulinda afya na usalama wa wafanyakazi katika sekta zote hapa nchini. Taasisi hii husajili maeneo ya kazi, kufanya kaguzi mbali mbali za usalama na afya pamoja na kuto katika maeneo ya kazi husika.

Mwisho………………..
Share:

BWANKU M BWANKU AVUTA FOMU UENYEKITI WA VIJANA MKOA WA MTWARA

 

Kada wa CCM Bwanku M Bwanku amechukua fomu kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa Vijana CCM mkoa wa Mtwara.

Kabla ya kuchukua Uamuzi wa Kugombea Uenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Bwanku M Bwanku amefanya kazi Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jijini Dodoma akiwa kama Afisa kwenye Kitengo cha TEHAMA na MAWASILIANO- Makao Makuu alikohudumu na kuwa Moja ya nguzo imara kwa kushirikiana na wengine kusemea CCM na Sera zake, kueleza umma mambo makubwa yanayofanywa na Serikali ya CCM na Viongozi wake Wakuu na wote Nchi nzima.


Pia, Kijana Bwanku M Bwanku, alikuwepo kwenye Kituo Kikuu cha Uchaguzi Cha Makao Makuu ya CCM Jijini Dodoma kilichoratibu na kusimamia Uchaguzi Mkuu wa CCM wa Rais, Wabunge na Madiwani 2020 na kwa kushirikiana na Wana- CCM wenzake Nchi nzima kufanikisha ushindi mkubwa na wa Kihistoria wa CCM wa asilimia 84 ambao haukuwahi kupatikana toka mfumo wa Vyama vingi urejee 1992 na kufanyika kwa Uchaguzi wa kwanza wa Vyama vingi baada ya kurejea Mwaka 1995.


Bwanku M Bwanku ni Mwandishi wa Habari na Mchambuzi mkubwa sana wa Masuala mbalimbali ya Kisiasa, Kiuchumi, Maendeleo, Kijamii na kadhalika anayefanya kazi na kuchangia Mijadala na Uandishi wa Makala na Habari kwenye Magazeti mengi sana Tanzania na Vyombo vya Habari vikubwa vya Kitaifa.


Bwanku, amekuwa Mtanzania pekee anayeandikia na kuchangia Habari na Makala kwenye Magazeti mengi sana Nchini Tanzania kuliko Mtanzania yeyote yule. Mpaka sasa Bwanku amekuwa akiandikia na kuchangia Makala na Habari kwenye Magazeti ya TANZANIA LEO, MAJIRA, MZALENDO, HOJA, LAJIJI, UHURU, HABARI LEO na Magazeti mengine mengi sana. 


Bwanku M Bwanku amekuwa Mwanamapinduzi ya Maendeleo hasa kwenye Mikoa ya Kusini (Mtwara na Lindi) ambapo mara nyingi sana amekuwa akishiriki kwenye masuala mbalimbali ya kusukuma Maendeleo yake. Mwaka 2019 alikuwa na Kampeni yake kubwa sana ya Kuhamasisha Elimu kwa mikoa ya Mtwara na Lindi ili kuinua hali ya Elimu kwa Mikoa hiyo na kuongeza ufaulu ambapo aliandika mpaka Kitabu chake Maalum cha kuhamasishia Elimu- Kusini kwa lengo la kuhamasisha umma wa Kusini kuanzia kwa Wazazi, Wanafunzi, Wananchi na Wadau wengine wote kuwekeza na kuweka nguvu kubwa zaidi kwenye Elimu.


Kijana Bwanku M Bwanku amehitimu Masomo yake ya Elimu ya Juu Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) alikopata Shahada (Degree) yake ya Sayansi ya Siasa na Utumishi wa Umma kwa maana Political Science and Public Administration (BA- PSPA)


Akiwa Chuo Kikuu Ndugu Bwanku M Bwanku alikuwa Kijana mahiri sana aliyesaidia sana kwa kushirikiana na Wanachama wengine wa CCM kujenga Chama ndani na Nje ya Chuo kabla ya kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Utawala Bora.


Pia, alikuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Mikoa ya Mtwara na Lindi (MTWALISO) wanaosoma Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM-CHSS & CBSL) na nyadhifa nyingine nyingi kwenye masuala ya Hamasa ndani ya Chama na kujitolea kwa ajili ya Ujenzi wa CCM.

Share:

LEMBELI ACHUKUA FOMU KUGOMBEA UENYEKITI CCM MKOA WA SHINYANGA

 


James Lembeli akiwa ameshika fomu ya kugombea nafasi ya Uenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga.
 

Na Marco Maduhu, SHINYANGA


Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) James Lembeli amejitosa kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga.

 Lembeli ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Kahama Mjini kuanzia mwaka (2005-2015) kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, baadae akajiunga CHADEMA na kurudi tena CCM, amechukua fomu ya kugombea nafasi ya Uenyekiti CCM Mkoa wa Shinyanga leo Julai 9, 2022 katika Ofisi za Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga, na kukabidhiwa na Katibu wa Chama hicho Donald Magesa.

Akizungumza wakati wa kuchukua fomu hiyo,Lembeli amesema ameamua kugombea nafasi hiyo ya Uenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, mara baada ya kujipima na kujitathmini na kujiona kuwa nafasi hiyo anaiweza kwa  sababu ana uzoefu ndani ya Chama, na pia ni kiongozi mzoefu ndani na nje ya nchi na anaweza kuongoza vizuri Chama.

Lembeli ambaye pia amewahi kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Ardhi, Maliasili na Mazingira (2010-2015),amesema Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga, kinahitaji viongozi thabiti, makini na hawana makando kando, sifa ambazo anazo na kuamua kugombea nafasi hiyo ya Uenyekiti CCM Mkoa.

“Nimejipima na kujitathmini nikaona nije nichukue fomu ili nigombee nafasi ya Uenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga kwa sababu sifa zote ninazo, hasa katika zama hizi ambapo kuna changamoto nyingi,” amesema Lembeli.

Makada wa CCM wameendelea kuchukua fomu za kuwania uongozi ambapo Julai 6 mwaka huu aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Hamis Mgeja (2007-2015) kisha akahamia CHADEMA na kurudi tena CCM, naye amechukua fomu ya kugombea tena nafasi hiyo ya Uenyekiti wa CCM Mkoa huo, uchaguzi ambao utafanyika mwaka huu.


Kwa upande wake Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga Donald Magesa, amesema idadi kamili ya wagombea wote ambao wamechukua fomu ataitaja kesho siku ya hitimisho la uchukuaji fomu.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger