Wednesday, 6 July 2022
IMANI POTOFU MAFUTA YA KENGE KUCHANGANYWA KWENYE PAMBA KUONGEZA UZITO
ANAYEDAIWA KUUA WATU SABA WA FAMILIA MOJA KIGOMA AKAMATWA..MAPENZI YAHUSISHWA
Kamishna wa operesheni na mafunzo jeshi la polisi Liberatus Sabas (kushoto) akitoa taarifa kwa waandishi wa habari (kulia) kuhusu kukamatwa kwa mtu mmoja akituhumiwa kuhusika na mauaji ya watu saba kwenye kijiji cha Kiganza Halmashauri ya wilaya Kigoma. (Picha na Fadhili Abdallah)WIVU wa mapenzi inaelezwa kuwa ndiyo chanzo cha mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Peter Moris Mwandelema (33) kutekeleza tukio la kuua watu saba wa familia moja mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye kijiji cha Kiganza Kigoma Vijijini mkoani Kigoma ambapo Jeshi la polisi limemtia mbaroni mtu huyo.
Kamishna wa Operesheni na mafunzo wa jeshi la polisi, Liberatus Sabas akitoa taarifa kwa waandishi wa habari mjini Kigoma jana alisema kuwa mtuhumiwa ambaye fundi ujenzi na mkazi wa eneo la Mlole mjini Kigoma alikamatwa jana mjini Kigoma.
Kamishna Sabas alisema kuwa kulingana na mahojiano na upelelezi uliofanyika polisi wamejiridhisha pasi na shaka kwamba mtuhumiwa huyo ndiye aliyehusika na tukio hilo la mauaji ya watu saba akiwa peke yake bila kushirikiana na mtu yeyote ambapo wananchi wametoa ushirikiano mkubwa wa kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo.
Akieleza chanzo cha tukio hilo Kamishna Sabas alisema kuwa mtuhumiwa Mwandelema alikuwa akimtuhumu Januari Mussa mmoja wa watu waliouawa katika tukio hilo kwamba alikuwa akitembea na mke wa mtuhumiwa ambaye kwa sasa jina lake limehifadhiwa.
Aidha Kamishna huyo wa operesheni na mafunzo alisema kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la vitendo vya mauaji vinavyotokana na visa vya mapenzi jambo ambalo linatishia ustawi bora wa familia.
Akizungumzia hali hiyo Askofu wa Kanisa la EAGT kanda ya Magharibi, Omary Mlenda alisema kuwa watu kutokuwa na hofu ya Mungu ndiyo chanzo cha mauaji yanayotokea kwa binadamu kuuana.
Askofu Mlenda alisema kuwa haitoshi kuingia msikitini au kanisani kuonyesha kuwa mtu huyo ni muumini na ana hofu ya Mungu lakini matendo yake yanapaswa kuonyesha kwa vitendo ikiwemo kuwa na uvumilivu anapopatwa na jambo.
TCRA YAKUTANA NA WATOA HUDUMA ZA MAUDHUI KWA NJIA YA MTANDAO 'Blogs na Online Tv' KANDA YA ZIWA
KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA BAJETI YAIPONGEZA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII KWA MATUMIZI MAZURI YA FEDHA ZA UMMA

Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof. Eliamani Sedoyeka akiishukuru Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti baada ya ziara ya kukagua miradi ya ujenzi wa lango la kuingilia wageni, barabara ya kilomita 47.2 na ujenzi wa Picnic Site. kwenye Pori la Akiba Mkungunero lililopo Wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma.
Afisa Uhifadhi Miundombinu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Noti Mgaya akitoa maelezo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuhusu ujenzi wa Picnic Site katika Pori la Akiba Mkungunero lililopo Wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akitoa ufafanuzi kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuhusu mradi wa ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilomita 47.2 katika Pori la Akiba Mkungunero lililopo Wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti ikikagua mradi wa ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilomita 47.2 katika Pori la Akiba Mkungunero lililopo Wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma.



