Sunday, 3 July 2022
BENKI YA CRDB YAKABIDHI PIKIPIKI 8 KWA WARAJISI WA USHIRIKA
Saturday, 2 July 2022
YANGA YAENDELEA KUCHEKA, YANYAKUA KOMBE LA ASFC
Friday, 1 July 2022
COSTECH KUENDELEA KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI KWA WABUNIFU NCHINI.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania -COSTECH Dkt Amos Nungu akizungumza na waandishi wa habari wakati alipotembelea na kuzungumza kwenye Banda la Tume hiyo katika Maonyesho ya 46 ya kimataifa ya Biashara Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania -COSTECH Dkt Amos Nungu akitembelea na kujionea kazi za wabunifu mbalimbali katika Banda la Tume hiyo katika Maonyesho ya 46 ya kimataifa ya Biashara Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es salaam. Watumishi wa Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania – COSTECH kwenye Banda la Tume hiyo katika Maonyesho ya 46 ya kimataifa ya Biashara Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es salaam.Baadhi ya wananchi wakiwemo wanafunzi waliojitokeza kujionea na kujifunza kwenye Banda la Tume hiyo katika Maonyesho ya 46 ya kimataifa ya Biashara Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es salaam.
Picha ya pamoja
..............................
NA MUSSA KHALID
Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia -COSTECH imesema itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wabunifu mbalimbali nchini ili kusaidia bunifu zao ziweze kwenda sokoni.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, Dkt Amos Nungu wakati alipotembelea na kuzungumza kwenye Banda la Tume hiyo katika Maonyesho ya 46 ya kimataifa ya Biashara Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es salaam.
"Wabunifu Rai yangu kwanza waendee kubuni suluhisho kwenye changamoto ambazo zipo lakini pia wafikirie jambo la kibiashara ili wasikose fursa mbalimbali zinazojitokeza"amesema Dkt Nungu
Dkt Nungu amefafanua kuwa Serikali itaendelea kuunga mkono juhudi za vijana wabunifu nchini ili kusaidia kurahisisha matumizi ya teknolojia za ndani na kuachana na utamaduni wa kuagiza bidhaa kutoka Nje.
Aidha, ameongeza kuwa kwa Mwaka huu 2022 wameweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha bunifu mbalimbali kutoka sekta isiyo rasmi wanapata nafasi ya kuzitangaza bunifu hizo kupitia maonesho ya sabasaba zinawanufaisha wabunifu pamoja na kutoa suluhisho kwa wanachi katika maisha yao.
Kwa upande wake Elia Kinshaga kutoka kampuni inayohusika na Ubunifu DTBi iliyopo chini ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) amewahimiza vijana kujikita katika ubunifu wa teknolojia ili kuweza kurahisisha kazi na mawasilino.
Hata hivyo vijana wametakiwa kuonesha bunifu zenye tija kwenye mfumo ili kuweza kupata nafasi kwa wakati pindi fursa zinapojitokeza ili kuweza kutatua matatizo yanayoikabli jamii.