Wednesday, 8 June 2022

Tazama Picha : TAMASHA LA UTAMADUNI LAHITIMISHWA KWA KISHINDO SHINYANGA...RC MJEMA ASEMA KILA WIKI KUNA JAMBO KIJIJI CHA UTAMADUNI BUTULWA



Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akizungumza wakati wa kufunga Tamasha la Utamaduni Mkoa wa Shinyanga katika Kijiji cha Utamaduni wa Kabila la Wasukuma Butulwa – Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga Jumanne Juni 7,2022 . Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Tamasha la Kwanza la Utamaduni Mkoa wa Shinyanga lililokwenda sanjari na uzinduzi wa Kijiji cha utamaduni wa kabila la Wasukuma na Filamu ya The Royal Tour kwa Mkoa wa Shinyanga limehitimishwa kwa shangwe kubwa huku Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Sophia Mjema akiahidi shughuli mbalimbali za Kiutamaduni kuendelea kufanyika katika kijiji hicho kila wiki.

Tamasha hilo lilizinduliwa Juni 7,2022 na Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt. Pindi Chana kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa na kufungwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema Juni 8,2022 katika kijiji cha Utamaduni wa Kabila la Wasukuma cha Butulwa kata ya Old – Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.

Akizungumza wakati wa kufunga Tamasha hilo, Mhe. Mjema amewapongeza na kuwashukuru wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki tamasha la utamaduni ili kutii na kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan la kuhakikisha kila Mkoa unaenzi na kudumisha tamaduni zao hivyo kuwakumbusha wananchi kuenzi tamaduni zao kama Rais Samia anavyosisitiza mara kwa mara juu ya umuhimu wa kuenzi utamaduni zikiwemo mila na desturi.

Mhe. Mjema amesema kufuatia uzinduzi wa kijiji cha Utamaduni shughuli mbalimbali za utamaduni zitaendelea kufanyika kila wiki katika kijiji hicho cha Butulwa – Old Shinyanga hivyo kuwasihi wananchi kuendelea kutembelea kijiji cha utamaduni ili kujifunza masuala ya utamaduni wa Kabila la Wasukuma.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akizungumza wakati wa kufunga Tamasha la Utamaduni Mkoa wa Shinyanga katika Kijiji cha Utamaduni wa Kabila la Wasukuma Butulwa – Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga Jumanne Juni 7,2022 . Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akizungumza wakati wa kufunga Tamasha la Utamaduni Mkoa wa Shinyanga katika Kijiji cha Utamaduni wa Kabila la Wasukuma Butulwa – Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga Jumanne Juni 7,2022 
Wananchi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akizungumza wakati wa kufunga Tamasha la Utamaduni Mkoa wa Shinyanga katika Kijiji cha Utamaduni wa Kabila la Wasukuma Butulwa – Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga Jumanne Juni 7,2022 
Mwenyekiti wa Machifu Mkoa wa Shinyanga Chifu Jidola akizungumza kwenye Tamasha la Utamaduni Mkoa wa Shinyanga katika Kijiji cha Utamaduni wa Kabila la Wasukuma Butulwa – Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zuwena Omary akizungumza kwenye Tamasha la Utamaduni Mkoa wa Shinyanga katika Kijiji cha Utamaduni wa Kabila la Wasukuma Butulwa – Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga Jumanne Juni 7,2022 .

Burudani ya ngoma ya Waswezi ikiendelea kwenye Tamasha la Utamaduni Mkoa wa Shinyanga katika Kijiji cha Utamaduni wa Kabila la Wasukuma Butulwa – Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga
Akina mama wakitwanga nafaka kwenye Tamasha la Utamaduni Mkoa wa Shinyanga katika Kijiji cha Utamaduni wa Kabila la Wasukuma Butulwa – Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga
Akina mama wakisaga nafaka kwenye Tamasha la Utamaduni Mkoa wa Shinyanga katika Kijiji cha Utamaduni wa Kabila la Wasukuma Butulwa – Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga na Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude (kulia) wakitwanga kwenye Tamasha la Utamaduni Mkoa wa Shinyanga katika Kijiji cha Utamaduni wa Kabila la Wasukuma Butulwa – Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga
Mwananchi akirekodi matukio kwa kutumia simu yake ya Kitochi 'Kiswaswadu kwenye tamasha la utamaduni
Wafugaji kutoka Kishapu wakicheza mchezo wa Kuchapana Fimbo kwenye Tamasha la Utamaduni Mkoa wa Shinyanga katika Kijiji cha Utamaduni wa Kabila la Wasukuma Butulwa – Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga
Wafugaji kutoka Kishapu wakicheza mchezo wa Kuchapana Fimbo kwenye Tamasha la Utamaduni Mkoa wa Shinyanga katika Kijiji cha Utamaduni wa Kabila la Wasukuma Butulwa – Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga
Askari wa Jeshi la Jadi Sungusungu Usanda akiwa amebeba kinu kwa meno kwenye Tamasha la Utamaduni Mkoa wa Shinyanga katika Kijiji cha Utamaduni wa Kabila la Wasukuma Butulwa – Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga
Askari wa Jeshi la Jadi Sungusungu Usanda akionesha mbwembwe kwenye Tamasha la Utamaduni Mkoa wa Shinyanga katika Kijiji cha Utamaduni wa Kabila la Wasukuma Butulwa – Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP George Kyando (kushoto) akicheza ngoma ya askari wa Jeshi la Jadi Sungusungu Usanda kwenye Tamasha la Utamaduni Mkoa wa Shinyanga katika Kijiji cha Utamaduni wa Kabila la Wasukuma Butulwa – Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP George Kyando (kushoto) akicheza ngoma ya askari wa Jeshi la Jadi Sungusungu Usanda kwenye Tamasha la Utamaduni Mkoa wa Shinyanga katika Kijiji cha Utamaduni wa Kabila la Wasukuma Butulwa – Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga
Wanafunzi wa shule ya Little Treasures wakicheza ngoma ya asili kwenye Tamasha la Utamaduni Mkoa wa Shinyanga katika Kijiji cha Utamaduni wa Kabila la Wasukuma Butulwa – Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga
Wananchi wakifuatilia burudani kwenye Tamasha la Utamaduni Mkoa wa Shinyanga katika Kijiji cha Utamaduni wa Kabila la Wasukuma Butulwa – Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga
Burudani ikiendelea kwenye Tamasha la Utamaduni Mkoa wa Shinyanga katika Kijiji cha Utamaduni wa Kabila la Wasukuma Butulwa – Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga
Msanii wa Nyimbo za asili Shoka kutoka Chamaguha Manispaa ya Shinyanga akitoa burudani kwenye Tamasha la Utamaduni Mkoa wa Shinyanga katika Kijiji cha Utamaduni wa Kabila la Wasukuma Butulwa – Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga
Banda la Kampuni ya Jambo kwenye Tamasha la Utamaduni Mkoa wa Shinyanga katika Kijiji cha Utamaduni wa Kabila la Wasukuma Butulwa – Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga
Gari la Matangazo la Kampuni ya Jambo likiwa kwenye Tamasha la Utamaduni Mkoa wa Shinyanga katika Kijiji cha Utamaduni wa Kabila la Wasukuma Butulwa – Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga
Wadau wakiwa kwenye Tamasha la Utamaduni Mkoa wa Shinyanga katika Kijiji cha Utamaduni wa Kabila la Wasukuma Butulwa – Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga
Wadau wakiwa kwenye Tamasha la Utamaduni Mkoa wa Shinyanga katika Kijiji cha Utamaduni wa Kabila la Wasukuma Butulwa – Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga
Katibu Tawala Wilaya ya Shinyanga, Boniphace Chambi akizungumza kwenye Tamasha la Utamaduni Mkoa wa Shinyanga katika Kijiji cha Utamaduni wa Kabila la Wasukuma Butulwa – Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga

Wadau wakiwa kwenye Tamasha la Utamaduni Mkoa wa Shinyanga katika Kijiji cha Utamaduni wa Kabila la Wasukuma Butulwa – Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga. Katikati ni Mbunge wa Jimbo la Ushetu Mhe. Emmanuel Cherehani
Mbunge wa Jimbo la Ushetu Mhe. Emmanuel Cherehani akisalimiana na wananchi kwenye Tamasha la Utamaduni
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akizungumza wakati akijiandaa kukabidhi vyeti vya Shukrani kutambua ushiriki na mchango wa wadau mbalimbali kwenye Tamasha la Utamaduni Mkoa wa Shinyanga katika Kijiji cha Utamaduni wa Kabila la Wasukuma Butulwa – Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga Jumanne Juni 7,2022.


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akizungumza (katikati) akipiga picha ya kumbukumbu na wadau waliotembelea  Kijiji cha Utamaduni wa Kabila la Wasukuma Butulwa – Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga kwenye Tamasha la Utamaduni Mkoa wa Shinyanga  Jumanne Juni 7,2022 . 

Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog



Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO JUNI 8,2022


Magazetini leo Jumatano June 8 2022


Sabaya aumwa, ahitaji upasuaji wa kichwa...
Share:

TANESCO NI-KONEKT YAIBUA SHANGWE CHATO

Meneja wa Tanesco wilaya ya Chato ukitoka maelezo ya namna ya kutumia njia Bora ya kidijitali ya Ni-konekt
Wafanyakazi na mafundi wa Tanesco chato wakiwa kazini

Na Daniel Limbe, Chato

WAKAZI wa kata ya Bwina wilayani Chato mkoani Geita, wamepata fura kubwa baada ya shirika la umeme nchini (Tanesco) kuwaunganisha na huduma ya nishati hiyo majumbani mwao.


Shangwe,nderemo na vifijo vimeibuka leo Juni 7,2022 muda mfupi baada ya meneja wa Tanesco wilaya ya Chato,Emily Ntazimila, kuwasha umeme kwenye nyumba ya Getruda Mremwa,mkazi wa kijiji cha Zanzibar kata ya Bwina, ikiwa ni ishara ya wananchi hao kuanza kunufaika na nishati hiyo kwa mfumo wa kidijitali.



Akizungumza na wakazi hao, Meneja huyo amesema shirika la umeme nchini(Tanesco) limekuja na mpango mpya wa Ni-konekt ili kurahisisha huduma kwa wateja wake kwa kufanya maombi ya kuunganishiwa umeme pasipo kufika ofisi za Tanesco.



"Mpango huu unarahisisha sana maombi ya wateja wetu kupata umeme pasipo kuja ofisini...mteja wetu atalazimika kutumia simu yake ya mkononi, kompyuta mpakato au intanet badala ya kutumia gharama kubwa za kutufikia ofsini kwetu"amesema



Ofisa huduma kwa wateja Tanesco wilaya ya Chato, Salma Mbwana, amedai kuwa huduma ya Ni-Konekt ina faida rukuki kwa wateja ikilinganishwa na awali ambapo wateja walipaswa kufika kwenye ofisi za Tanesco.



"Ni-Konekt inamrahisishia mteja kupata kwa urahisi zaidi, inaokoa muda, inaondoa kero za vishoka, inaongeza ufanisi wa kazi katika upatikanaji wa huduma na kwamba huduma hizi sasa zinapatikana kwa kutumia simu ya mkononi kwa kupiga alama ya *152*00# kisha unaendelea kupata maelekezo zaidi",amesema.



Hata hivyo amewataka wakazi wa wilaya ya chato kuchangamkia fursa hiyo ambayo imelenga kuondoa malalamiko ya awali ambapo wananchi walikuwa wakitapeliwa fedha zao na vishoka.



Kwa upande wake, Bi Mremwa, amelishukuru shirika la umeme nchini, kwa kumpatia haraka huduma ya umeme baada ya kufanya maombi jana juni 6 mwaka huu kabla ya leo kuwashiwa.



Akatumia fursa hiyo kuwasihi wananchi kutumia njia mpya ya kidijitali ya Ni-Konekt kufanya maombi ya kuunganishiwa umeme kwa kuwa ni bora na haraka zaidi.
Share:

Tuesday, 7 June 2022

TBS YAWAELIMISHA WAZALISHAJI WA MAZAO NAMNA YA UDHIBITI WA SUMUKUVU





**********************


SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limeendelea kutoa mafunzo kuhusu Udhibiti wa Sumukuvu kwa Mazao ya Mahindi,Karanga pamoja na bidhaa zake kwa wafanyabiashara, Wazalishaji na Wasindikaji kutoka Buchosa wilayani Sengerema.

Akizungumza wakati akifungua Mafunzo hayo wilayani hapo, Katibu Tawala wa Wilaya ya Sengerema Allan Augustin o Mrema amesema Sumukuvu imekuwa ikiathiri zaidi mazao ambayo ni sehemu ya chakula chetu hapa nchini hivyo basi tunapaswa kuzingatia mikakati ya kukabiliana na changamoto ya sumukuvu ili vyakula viendelee kuwa salama kwa muda wote.

Amesema kupitia mafunzo hayo ambayo TBS wameyakusudia kuyatoa kwa wahusika yatasaidia kwa kiasi kikubwa kukabiliana na sumukuvu na hivyo kuzalisha na kuuza bidhaa ambazo ni salama.

"Niwapongeze TBS kupitia Mradi wa Kudhibiti Sumukuvu Tanzania -TANIPAC kwa kutoa kipaumbele katika suala la kuelimisha jamii ya Wilaya ya Sengerema juu ya usalama wa chakula hususan katika kudhibiti Sumukuvu ili kuweza kukabiliana na tatizo hili". Amesema Mrema.
Share:

MAADHIMISHO YA SIKU YA CHAKULA SALAMA DUNIANI: TBS YAHIMIZA UZINGATIAJI WA USALAMA WA CHAKULA

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Mhandisi Johaness Maganga (katikati) akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Chakula Salama Duniani (World Food Safety Day) yaliyofanyika leo Juni 7,2022 katika ofisi za TBS Jijini Dar es Salaam. Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Mhandisi Johaness Maganga akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Chakula Salama Duniani (World Food Safety Day) yaliyofanyika leo Juni 7,2022 katika ofisi za TBS Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora Shirika la Viwango Tanzania, Bw.Lazaro Msasalaga akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Chakula Salama Duniani (World Food Safety Day) yaliyofanyika leo Juni 7,2022 katika ofisi za TBS Jijini Dar es Salaam. Mwakilishi kutoka Shirika la Afya la Umoja wa Kimataifa (WHO) Bi.Rose Shija akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Chakula Salama Duniani (World Food Safety Day) yaliyofanyika leo Juni 7,2022 katika ofisi za TBS Jijini Dar es Salaam. Afisa Afya na Mazingira kutoka Wizara ya Afya (Wizara ya Afya) Bi.Josephine Kapinga akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Chakula Salama Duniani (World Food Safety Day) yaliyofanyika leo Juni 7,2022 katika ofisi za TBS Jijini Dar es Salaam. Afisa Biashara kutoka Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Bw.Denis Mzamily akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Chakula Salama Duniani (World Food Safety Day) yaliyofanyika leo Juni 7,2022 katika ofisi za TBS Jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wadau mbalimbali wakiwa katika maadhimisho ya Siku ya Chakula Salama Duniani (World Food Safety Day) yaliyofanyika leo Juni 7,2022 katika ofisi za TBS Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

**************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Makadirio yaliyofanywa na Shirika la Afya Duniani (WHO) mwaka 2015 yanaonesha kuwa kila mwaka, zaidi ya watu milioni 600 duniani huugua, na watu 420,000 kati yao hufa kutokana na kula chakula kisicho salama. Magonjwa haya hutokea zaidi kwa watu wenye kipato cha chini na zaidi kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.

TBS imeweka mifumo ya kiudhibiti ili kuhakikisha kuwa chakula kilichopo katika soko hapa nchini ni salama ili kuilinda jamii dhidi ya madhara yatokanayo na kula chakula kisicho salama.

Ameyasema hayo leo Juni 7,2022 katika Ofisi za TBs Jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Mhandisi Johaness Maganga wakati akizungumza na wadau mbalimbali katika kuadhimisha Siku ya Chakula Salama Duniani (World Food Safety Day).

Amesema mara kadhaa TBS imekuwa ikishirikiana na wadau wa chakula ili kufikia lengo la kuwa na chakula salama katika soko, hivyo basi maadhimisho haya yamewashirikisha pia wadau wa usalama wa chakula kutoka wizara na taasisi mbalimbali za serikali na za kimataifa, ikiwemo Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Wizara ya Afya, Wizara ya Kilimo, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Taasisi ya Chakula na Lishe pamoja na Mamlaka ya Mkemia Mkuu wa Serikali. Vilevile, ofizi za mashirika ya kimataifa, Shirika la Afya la Umoja wa Kimataifa (WHO) pamoja na Shirika la Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) wamejumuika nao katika maadhimisho haya.

"Tunatambua mchango mkubwa kutoka kwa wadau hawa katika kuhakikisha usalama wa chakula nchini, ikiwa ni pamoja na kushiriki katika masuala mbalimbali kama vile kuandaa sera, kanuni na miongazo mbalimbali katika uzalishaji, usafirishaji, uuzaji na uandaaji wa chakula". Amesema Mhandisi Maganga.

Aidha Mhandisi Maganga amesema kutokana na suala la usalama wa chakula kuwa mtambuka, mfumo thabiti wa udhibiti wake unapaswa kuwa shirikishi, ukihusisha afya ya binadamu, wanyama, mimea na mazingira.

"Wanyama na mimea ndio chanzo kikubwa cha chakula cha binadamu. Afya ya wanyama ni muhimu ili kuepuka magonjwa yanayoambukizwa kwa binadamu kwa kula nyama kutoka kwa wanyama hao". Amesema

Pamoja na hayo ameeleza kuwa kuadhimisha Siku ya Chakula Salama Duniani kwa mwaka 2022, TBS imejikita katika kutoa elimu kwa jamii kupitia vyombo mbalimbali vya habari. Mada na matangazo kuhusu usalama na ubora wa chakula zimekuwa zikitolewa katika redio, televisheni, magazeti na mitandao ya kujamii kwa wiki moja, kuanzia tarehe 30 Mei,

Kwa upande wake Mwakilishi kutoka Shirika la Afya la Umoja wa Kimataifa (WHO) Bi.Rose Shija amesema WHO imeongoza juhudi za kutathmini ukubwa wa tatizo la magonjwa yatokanayo na chakula kisicho salama duniani na imesaidia nchi kujenga au kuimarisha mifumo ya kitaifa ya ufuatiliaji wa magonjwa yatokanayo na chakula kisicho salama.

Amesema WHO imehakikisha kuwa viwango vya kimataifa vya usalama wa chakula Codex Alimentarius vinazingatia afya ya Umma na kwamba nchi zilizo na uwezo mdogo zinajengewa uwezo ka kushiriki kwenye mafunzo ya Codex.

"Tunatoa wito kwa wadau wote kukuza na kuendeleza utamaduni wa usalama wa chakula na pia kuzingatia viwango vya chakula vya kimataifa na vya ndani, kukuza utunzaji salama wa chakula pamoja na kutoa elimu ya usalama wa chakula.
Share:

Video : TAMASHA LA UTAMADUNI WA KISUKUMA 2022...RAIS SAMIA APEWA FRIJI ISIYOTUMIA UMEME

Share:

TBS YAWATAKA WAJASIRIAMALI WA BIDHAA ZA USINDIKAJI WA VYAKULA KUTUMIA MAFUNZO WANAYOPEWA KUKUZA BIASHARA ZAO


Maafisa wa TBS wakimweleza mjasiriamali taratibu za kupata leseni ya kutumia alama ya ubora ya TBS sambamba na taratibu za kuzalisha bidhaa zenye ubora kama uzingatiaji wa usafi na mpangilio sahihi wa eneo.

Meneja wa Huduma za Maktaba na Taarifa, Bi. Bahati Samilani akiwaelekeza wateja jinsi kuangalia viwango kupitia tovuti ya TBS.

*************

Taasisi za Serikali, asasi na sekta binafsi na wajasiriamali wadogo wa bidhaa za usindakaji vyakula mbalimbali zikiwemo za mkonge, viungo na zinginezo wameshauriwa kuyapa kipaumbele mafunzo yanayotolewa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwani yana faida kubwa katika suala zima la kukuza biashara nchini.

Ushauri huo umetolewa na Afisa Usalama wa Chakula wa TBS,William Mhina, wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na washiriki pamoja na wananchi kwenye Monesho ya Biashara Tanga yaliyoandaliwa na TCCIA yaliyofanyika Viwanja vya Mwahako mkoani Tanga kuanzia Mei 28 hadi Juni Juni 6, mwaka huu.

Mhina aliwaambia washiriki na wananchi waliohudhuria maonesho hayo kwamba TBS ipo kwa ajili ya kusaidia uzalishaji wa bidhaa zenye viwango ili kuziwezesha kushindana kwenye masoko ya ndani na nje ya nchi bila vikwazo vya kibiashara. "TBS ni wadau wakubwa ukizingatia lengo mojawapo la kuanzishwa kwa shirika hili ni kuwezesha biashara.

Tumekuja kwenye maonesho haya ili kuwasogezea huduma wajasiriamali tuweze kujua changamoto zao sambamba na kuwapa elimu ya kuthibitisha ubora wa bidhaa zao hasa ukizingatia kwamba huduma hii inatolewa bure kwao," alisema Mhina na kuongeza;

"Serikali inatenga kati ya sh. milioni 150 hadi 200 kila mwaka kwa ajili ya kuwahudumia wajasiriamali, hivyo ni fursa nzuri kwao kujitokeza kuthibitisha ubora wa bidhaa zao bure ili waweze kuondokana na vikwazo vya kibiashara." Kwa mujibu wa Mhina hadi sasa sasa zaidi ya wajasiriamali wadogo 500 kutoka mikoa mbalimbali wamepata leseni chini ya mpango huo wa bure

Akizungumza kwenye maonesho hayo mjasiriamali, Ashura Omari anayezalisha mafuta ya alizeti wilayani Kilindi mkoani Tanga, alisema;

"Nilishaanza uzalishaji wa mafuta ya alizeti na kuna wakati sikufuata utatatibu nikafungiwa kwa sababu nilikuwa nazalisha bila kufuata taratibu sahihi za uzalishaji kwa kuogopa kufuatilia TBS, lakini sasa nimeelimika nimejua TBS hawakuwa na nia mbaya nimejipanga upya na kwa sasa nimefahamu utaratibu wa kufuata baada ya kuhudhuria semina za TBS," alisema Omari.

Aliwashauri wajasiriamali wenzake na wazalishaji wa bidhaa za aina mbalimbali kwa ujumla wasiikimbie TBS na badala yake wakisikia mafunzo yanayotolewa na Shirika hili wahudhurie kwa wingi kwa kuwa yana faida nyingi kwenye uzalishaji wao.

Alisema TBS wapo kwa nia ya kusaidia kutoa elimu na kuwezesha uzalishaji unaozingatia viwango.

TBS hutoa mafunzo kwa wazalishaji katika ngazi za mikoa na wilaya bila malipo yoyote kwa lengo la kukuza ulewa wa viwango na kuhakikisha uzalishali wa bidhaa zenye ubora unaongezeka.

Maonesho hayo yalifungwa juzi na Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar,Mhe. Simai Mohamned Said, ambapo kauli mbiu ilikuwa na ujumbe usemao; "Ushirikiano na sekta ya umma na binafsi ndio injini ya maendeleo ya uchumi.

Share:

CCU KUTUMIA BILIONI 9.6 KUNUNUA PAMBA CHATO




Na Daniel Limbe, Chato

MSIMU wa ununuzi wa pamba ukiwa umezinduliwa hivi karibuni nchini, Chama kikuu cha ushirika cha Chato (CCU) kinatarajia kutumia takribani shilingi 9.6 bilioni, kununua pamba safi kwa msimu wa 2022/23.

Mwenyekiti wa Chama hicho, Greon Chandika, amesema hayo leo wakati akizungumza na mwandishi wetu aliyetaka kujua mpango mkakati ya Chama hicho kikuu cha ushirika kuhimili ushindani wa soko huria dhidi ya makampuni binafsi.

"Tayari tumeshafanikiwa kupata pesa kiasi cha shilingi 9.6 bilioni  kwaajili ya kununua pamba mbegu kutoka kwa wakulima...nimatarajio yetu kuwa tutakabiliana vizuri na ushindani wa wanunuzi binafsi".

"Kesho tunataraji kuanza kununua pamba safi iwapo taratibu za serikali zitakuwa zimekamilika ikiwemo ukaguzi wa mizani ya kupimia"amesema Chandika.

Hata hivyo,amedai kuwa Chama hicho kikuu kinao wakulima wa pamba ambao ni wanachama toka Amcos 53 zinazounda ushirika huo kwenye wilaya ya Chato na Biharamulo mkoani Kagera.

Mmoja wa wakulima wa pamba wilayani hapa mkoani Geita, Malima Mgonya, amekiomba chama hicho kikuu cha ushirika,kununua pamba kwa bei ya shilingi 2,000 kwa kila kg 1 ili kuwahamasisha wakulima wengine kuzalisha zaidi.

"Pamoja na ushindani wa makampuni ya watu binafsi tunawaomba CCU wapandishe bei ya kununulia pamba ifike angalau 2,000 kwa kila kilo moja...bei hiyo itawahamasisha wakulima wengi kurudi kwenye kilimo cha pamba ambacho wengi walikuwa wameshakitelekeza na kuhamia mazao mengine kutokana na bei kuwa chini"amedai Mgonya.

Hivi karibuni serikali ilizindua msimu mpya wa ununuzi wa pamba mbegu kwa mwaka 2022/23 huku ikitangaza bei elekezi ya shilingi 1,560 kuwa ndiyo bei ya kuanzia ikilinganishwa na msimu wa 2021/22 ambapo bei dira ilikuwa 1,050.

                 


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger