Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga ACP George Kyando
Na Marco Mipawa - Kahama
Mwanamke aliyejulikana kwa jina la Zuena au Ashura Salum (25-30) mkazi wa Dar es Salaam, amekutwa chumbani akiwa ameuawa kwa kuchomwa kisu na mtu anayedhaniwa kuwa ni mwenza wake katika nyumba ya kulala wageni ya Kalunde iliyoko mjini Kahama, usiku wa kuamkia Mei 22, 2022.
Kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga George Kyando amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba, Zuena na mwanaume huyo waliingia chumbani hapo majira ya saa 11:00 alfajiri na kwamba mwanaume alitoka na kutokomea kusikojulikana kabla ya wahudumu wa nyumba hiyo kugundua mauaji hayo.
Kyando amesema, mapema asubuhi siku hiyo wahudumu wa nyumba hiyo waliukuta Mwili wa marehemu chumbani pamoja na simu mbili zenye laini zinaonesha majina hayo.
Amesema jeshi la polisi linaendelea kufuatilia tukio hilo, huku akitoa Rai kwa jamii kujihadhari na watu wasiotambulika vizuri.







Akitoa maoni yake kuhusu kampeni hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa LG Afrika Mashariki, Sa Nyoung Kim alisema, “Kupitia ubunifu na bidhaa zetu za hivi punde, lengo letu ni kuwasaidia wateja wetu kuishi maisha bora na rahisi zaidi. Huu ukiwa ni mwezi wa Eid al-Fitr, tunatoa nafasi kubwa kwa kila mtu kuchagua maisha haya bora sio tu ya leo bali ya kesho pia”.
































