Friday, 22 April 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA APRILI 22,2022

Magazetini leo Ijumaa April 22 2022

Share:

UONGOZI WA CHAMA CHA USHIRIKA MACHINJIO YA VINGUNGUTI WALALAMIKIWA KUTOTOA TAARIFA YA FEDHA KWA ZAIDI YA MIAKA 5



Wafanyabiashara wa nyama katika machinjio ya Vingunguti wakiwa katika shuguli zao za uuzaji wa nyama katika machinjio ya Vingunguti Jijini Dar es Salaam
Wafanyabiashara wa nyama katika machinjio ya Vingunguti wakifuatilia mahojiano ya wenzao (hawamo pichani) waliokuwa wakihojiwa na wana habari machinjioni hapo.

January Jonas Mfanyabiashara katika machinjio ya Vingunguti Dar es Salaam akitoa malalamiko yake mbele ya waandishiwa habari juu ya uongozi wao wa ushirika kushindwa kuitisha mkutano mkuu na kusoma taarifa ya mapato na matumizi kwa kipindi cha miaka saba mfululizo toka viongozi hao wachaguliwe kuongoza ushirika huo.
Fredrick Daudi mfanyabiashara Vingunguti
Fredrick Ndahani mfanyabiashara machinjio ya Vingunguti.
Mfanyabiashara ndani ya machinjio ya Vingunguti Shadrack Mabumo akizungumza kuulalamikia uongozi wao kushindwa kuwasomea taarifa ya fedha ya mapato na matumizi wakiwa madarakani.
Mwenyekiti wa umoja wa ushirika wa wafanyabiashara Joel Meshack akizungumza katika Ofisi za Ushirika huo akijibu Malalamiko ya wafanyabiashara hao alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kutolea ufafanuzi tuhuma za wafanyabiashara hao

PICHA ZOTE NA: HUGHES DUGILO

DAR ES SALAAM.

WANYABIASHARA wa Nyama Machinjio ya Vingunguti wameulalamikia uongozi wao kushindwa kuitisha mkutano na kusoma mapato na matumizi tangu walivyoshika nafasi za uongozi kwa zaidi ya miaka mitano sasa.

Wamesema kuwa katiba yao inawataka kila baada ya miaka mitatu lazima wafanye uchaguzi wa viongozi ikiwa sambamba na kuitisha mkutano wa kawaida wa kusoma mapato na matumizi kwa wanachama.

Akizungumzia malalamiko hayo leo kwenye mkutano uliowakutanisha wanahabari kwaniaba wenzake January Jonas amesema wamechoshwa na hali hiyo huku wakiziomba mamlaka zinazohusika kuchukua hatua stahiki dhidi ya viongozi hao ambao wamekaa madaraka kwa zaidi ya miaka saba sasa pasipokuitisha mkutano wowote.


"Ndugu waandishi wa habari sisi kama wanachama kuna kiingilio pindi tuapoingia kwenye ushirika wetu ambapo kila mwanachama anatoa shilingi 60000 .lakini viongozi hawajawahi kusoma mapato na matumizi jambo ambalo linakidhana na katiba yetu",amesema January.


Amesema licha ya changamoto hiyo ya uchaguzi na taarifa za mapato na matumizi lakini pia kuna changamoto zingine mbalimbali zikiwemo za ngozi na damu ambapo wao kama wafanyabiashara wanaona hawatendewi haki sokoni.


Akijibu Malalamiko hayo Mwenyekiti wa umoja wa ushirika wa wafanyabiashara Joel Meshack amekiri kuwepo kwa ucheleweshaji wa kufanyika kwa mkutano nakudai kwamba hiyo imetokana na kachelewa kuijenga ofisi yenyewe.


Pia amesema kuwa kutokana na hapo awali kuwepo kwa changamoto lukuki lakini hivi sasa wamejipanga vyema nakuwahamikishia wanachama wao kuwa mnamo April 27 mwaka huu watafanya mkutano na baadaye watatangaza tarehe ya mkutano mkuu.


Amewataka wafanya biashara kuwa watulivu wakati viongozi wao wanapopanga kukamilisha kwa michakato mbalimbali ambayo wanayo kwa manufaa ya wanachama wao hao ikiwa pamoja na kuitisha mkutano. na kuelekea kwenye uchaguzi Mkuu.


"Niwahakikishie wafanyabiashara kwamba kila kitu kipo sawa na sisi Kama viongozi tupo hatua za mwisho kufanya mkutano na mambo mengine. Na kuhusu wao kama viongozi ni binadamu kama kuna mapungufu mengine ni ya kibadamu lakini kwa ujumla tuna mambo mazuri kwa ajili ya watu wetu."amesisitiza January


Share:

Thursday, 21 April 2022

WASANII WASHINDI WA TUZO ZA MUZIKI TANZANIA WAPATA ELIMU NA KUJIUNGA NA NSSF



Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma wa NSSF, Lulu Mengele, akitoa mada kuhusu umuhimu wa kujiwekea akiba kwa baadhi ya wasanii walioshinda Tuzo za Tanzania Music Award. Ambapo Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ilitoa zawadi mbalimbali kwa wasanii walioshinda ikiwepo zawadi ya kuwachangia NSSF na NHIF katika kipindi cha mwaka mmoja na baada ya hapo wasanii wenyewe wataendelea kuchangia.
Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), Matiko Mniko, akitoa neno la utangulizi wakati wa Semina ya kuwajengea uelewa baadhi ya wasanii washindi wa Tuzo za Muziki Tanzania kuhusu elimu ya Hifadhi ya Jamii kwa upande wa NSSF na Bima ya Afya (NHIF).
Afisa Matekelezo Mkuu wa Sekta Isiyo Rasmi, Abdulaziz Abeid akitoa mada kwa baadhi ya wasanii washindi wa Tuzo za Muziki Tanzania kuhusu umuhimu wa kujiunga, kuchangia ili wajiwekea akiba kwa maisha yao ya sasa na baadaye.
Msanii wa Muziki, Snura Mushi ambaye ni mmoja wa mshindi kwenye Tuzo za Muziki Tanzania akiuliza maswali mbalimbali kuhusu NSSF mara baada ya mada zilizotolewa na NSSF kwenye Semina ya kuwaongezea uelewa wa Hifadhi ya Jamii iliyoandaliwa na BASATA.
Baadhi ya maofisa wa NSSF wakijibu maswali mbalimbali kutoka kwa baadhi ya wasani walioshinda Tuzo za Muziki Tanzania mara baada ya kupata elimu ya Hifadhi ya Jamii ili waweze kujiunga na kujiwekea akiba kwa maisha yao ya sasa na baadaye.
Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma wa NSSF, Lulu Mengele akifuatilia jinsi wasani Snura Mushi na Sholo Mwaba wakijaza fomu za kujiunga na NSSF, ambapo mwaka huu katika Tuzo za Wanamuziki Bora wasanii hao walikuwa miongoni mwa wasanii bora
Baadhi ya Wafanyakazi wa NSSF wakiwasaidia wasanii kujaza fomu za kujiunga na NSSF ambapo Wizara itawalipia michango ya mwaka mmoja na baada ya hapo wasanii hao wataendelea kuchangia wenyewe


****


NA MWANDISHI WETU


Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umetoa elimu ya Hifadhi ya Jamii kwa baadhi ya wasanii ambao ni washindi wa Tuzo za Muziki Tanzania kuhusu umuhimu wa kujiunga na kujiwekea akiba kwa maisha yao ya sasa na baadaye.


Baada ya elimu hiyo wasanii hao walipata fursa ya kujiunga na NSSF ikiwa ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kupitia kwa Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Mohamed Mchengerwa ambaye aliahidi kuwa Wizara pamoja na kutoa zawadi kwa wasanii walioshinda vilevile Wizara iliona ni vema kuwalipia NSSF wasanii hao ambao wameshinda kwa kipindi cha mwaka mmoja na baadaye wataendelea wenyewe.


Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma wa NSSF, Lulu Mengele alieleza umuhimu wa wasanii kujiunga, kuchangia ili wajiweke akiba kwa maisha yao ya sasa baadaye ambapo pindi watakapokosa kipato waweze kunufaika na mafao mbalimbali ikiwemo pensheni ya uzee.


Naye, Abdulaziz Abeid ambaye ni Afisa Matekekezo Mkuu wa Sekta Isiyo Rasmi alisema Mfuko umeweka mifumo rahisi na rafiki kwa kila Mtanzania aliyejiajiri mwenyewe kujiwekea akiba. Hivyo alitoa wito kwa wasanii kuchangamkia fursa hiyo.


Kwa upande wake, Mratibu wa Tuzo za Muziki kutoka BASATA, Mrisho Mrisho, aliwataka wasanii kujiunga na NSSF kwa ajili ya kujiwekea akiba ya maisha ya baadaye kwani kuna faida nyingi ambazo watanufaika nazo.


Msanii wa muziki wa singeli, ambaye alichukua Tuzo ya Mwanamuziki bora wa Singeli kwa wasanii wanawake, Snura Mushi, aliishukuru NSSF kwa kuwafikia wasanii ili waweze kujiunga na kujiwekea akiba kwa maisha yao ya sasa na baadaye.


Naye, mkali wa singeli, Sholo Mwamba aliipongeza NSSF kwa kuwafikia wasanii na kuwaomba wasanii wengine ambao hawajashinda kuchangamkia fursa hiyo ya kujiunga na NSSF kwani ni Mfuko wenye faida kubwa sana.
Share:

Wednesday, 20 April 2022

WANANCHI WAISHUKURU RUWASA KISHAPU KUWAFUNGIA MOTA MPYA MRADI WA MAJI NG'WANG'HOLO - NYENZE


Mhandisi kutoka Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wilaya ya Kishapu, Nicholaus Mathias (wa pili) kushoto na Mhandisi kutoka Kampuni ya Ukandarasi Hydrotech,  Innocent Msacky ( wa kwanza kushoto) wakiwa wameshikilia Mota mpya ya kuendesha Pampu ya kusukuma maji katika mradi wa maji safi wa Nyenze – Ng’wang’holo. Katikati ni Meneja wa RUWASA wilaya ya Kishapu, Mhandisi Dickson Protas Kamazima, wa kwanza kulia ni Katibu wa Kamati ya Watumiaji Maji katika mradi wa maji safi wa Nyenze – Ng’wang’holo, Anna Moshi.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Wananchi wa vijiji vya Ng’wang’holo na Nyenze kata ya Mwadui – Lohumbo wilayani Kishapu wameishukuru Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wilaya ya Kishapu Mkoa wa Shinyanga kwa kuwafungia Mota mpya ya kuendesha Pampu ya kusukuma maji katika mradi wa maji safi wa Nyenze – Ng’wang’holo na Kiimarishaji 'Stablizer' kutokana na iliyokuwepo kuharibika kutokana na hitilafu ya umeme.

RUWASA Kishapu imetumia shilingi Milioni 5 kwa ajili ya kununua na kufunga Mota ya kuendesha Pampu ya kusukuma maji na Kiimarishaji 'Stablizer' katika mradi huo wa maji safi wa Nyenze – Ng’wang’holo.

Wakizungumza leo Jumatano Aprili 20,2021 wakati wakishiriki zoezi la kufunga mota hiyo pamoja na Stablizer vilivyonunuliwa na RUWASA Kishapu, wananchi wamesema sasa wataanza kupata huduma ya maji safi na salama baada ya mota kuharibika mwezi Desemba 2021.

Mmoja wa wakazi wa Ng’wang’oholo Bi. Sayi Kulwa amesema baada ya mota hiyo kuharibika wamekuwa wakitumia muda mrefu kutafuta huduma ya maji kwenye mabwawa na mito.

“Maji yamekuwa ya shida sana hali iliyokuwa inatulazimu kuamka usiku kufuata maji kwenye visima vilivyochimbwa pembezoni mwa mito. Maji hayo siyo salama lakini pia tunahatarisha maisha yetu kwa kushambuliwa na wanyama wakali lakini watoto wa kike wanaweza kubakwa sambamba na ndoa kuvunjika. Tunawashukuru RUWASA kwa kusikia kilio chetu na sasa tumefungiwa mtambo huu tuanze kupata huduma ya maji safi na salama”,amesema Kulwa.


“Tunashukuru RUWASA kwa kutupatia mtambo huu, baada ya mota kuharibika tulianza tena kufuata maji kwenye mabwawa na mito,maji ambayo kimsingi hayakuwa salama, lakini sasa tutapata maji safi na salama”,ameongeza Tungu Kwangulija.


Naye Bw. Sumai Salum Sabhi amesema licha kwamba mradi huo unanufaisha vitongoji viwili vya Ng’wang’holo na Nyenze, kufungwa kwa mtambo huo kutaondoa changamoto ya wananchi hasa akina mama kutumia muda mrefu kutafuta maji hivyo kushiriki katika shughuli za maendeleo huku akiomba serikali kuwapatia huduma ya maji ya Ziwa Victoria kutokana na kwamba bomba la maji hayo linapita kwenye eneo lao kuelekea wilayani Maswa mkoani Simiyu.

Mwenyekiti wa kijiji cha Ng’wang’holo Bw. William Bulugu Kabisi mradi wa maji Nyenze – Ng’wang’holo uliojengwa na RUWASA Kishapu, umesaidia kupunguza shida ya maji katika vitongoji viwili vya kijiji cha Ng’wang’holo na Nyenze.

“Tunawashukuru RUWASA kwa kusikiliza na kufanyia kazi ombi letu tulilolitoa kupitia Kamati ya watumiaji maji kwenye mradi huu kuwa tunahitaji kupatiwa Mota mpya baada ya ile iliyokuwepo kupata hitilafu. Leo wametufungia mtambo/kifaa hiki ili kutatua changamoto ya maji kwa wananchi ambao wamekuwa wakilazimika kutumia maji yasiyo salama kutoka kwenye Chemchemi, mito na mabwawa”,amesema Kabisi.

Mwenyekiti huyo wa kijiji ametumia fursa hiyo kuiomba serikali kuwapatia huduma ya maji kwenye vitongoji vilivyosalia ili wananchi wote katika vijiji vya Nyenze na Ng’wang’holo wapate huduma ya maji safi na salama.

Katibu wa Kamati ya Watumiaji Maji katika mradi wa maji safi wa Nyenze – Ng’wang’holo, Anna Moshi amesema sasa huduma ya maji safi na salama itapatikana baada ya mota mpya kufungwa tangu iharibike mnamo Desemba 27,2021 huku akibainisha kuwa bei ya maji kwa ujazo wa lita 20 ni shilingi 50 na Unit moja ni shilingi 2500.

Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wilaya ya Kishapu, Mhandisi Dickson Protas Kamazima amesema mradi wa maji ya kisima kirefu cha Ng’wang’holo - Nyenze ulikamilika mwaka 2020 baada ya RUWASA kufanya maboresho ya mradi kutoka Kisima cha mkono ‘Pampu ya mkono’ na sasa una vituo sita vya kuchotea maji ukihudumia wananchi zaidi ya 3000.

“Tulifanya maboresho ya mradi huu kupitia fedha za Programu ya Lipa kwa Matokeo (PBR) shilingi Milioni 72. Baada ya kumaliza kuboresha mradi huu wananchi walianza kupata huduma ya maji safi na salama lakini tarehe 27,2021 Desemba 2021 mota iliungua kutokana na hitilafu ya umeme”,amesema Mhandisi Kamazima.

“Baada Mota ya kuendesha Pampu ya kusukuma maji kuharibika, Kamati ya watumiaji maji iliandika barua ikaomba RUWASA inunue kifaa kilichoharibika. RUWASA huwa tuna fungu la uendelevu wa miradi ya maji hivyo tulipokea ombi hilo lakini tulikwama kutokana na taratibu za manunuzi lakini leo tunafunga mota mpya na Stablizer kupitia Mkandarasi Hydrotech ili wananchi waanze kupata huduma ya maji mara moja kama hapo awali”,amesema Mhandisi Kamazima.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mhandisi kutoka Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wilaya ya Kishapu, Nicholaus Mathias (wa pili) kushoto na Mhandisi kutoka Kampuni ya Ukandarasi Hydrotech,  Innocent Msacky ( wa kwanza kushoto) wakiwa wameshikilia Mota mpya ya kuendesha Pampu ya kusukuma maji katika mradi wa maji safi wa Nyenze – Ng’wang’holo. Katikati ni Meneja wa RUWASA wilaya ya Kishapu, Mhandisi Dickson Protas Kamazima, wa kwanza kulia ni Katibu wa Kamati ya Watumiaji Maji katika mradi wa maji safi wa Nyenze – Ng’wang’holo, Anna Moshi. Kifaa kingine chini ni Kiimarishaji 'Stablizer' . Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog 
Meneja wa RUWASA wilaya ya Kishapu, Mhandisi Dickson Protas Kamazima (kushoto) akiangalia Kiimarishaji 'Stablizer' katika mradi wa maji safi wa Nyenze – Ng’wang’holo kata ya Mwadui - Lohumbo wilayani Kishapu.
Wananchi wakiwa kwenye eneo la mradi wa maji safi wa Nyenze – Ng’wang’holo kata ya Mwadui - Lohumbo wilayani Kishapu.
Meneja wa RUWASA wilaya ya Kishapu, Mhandisi Dickson Protas Kamazima  akionesha Tanki la maji kwenye mradi wa maji safi wa Nyenze – Ng’wang’holo kata ya Mwadui - Lohumbo wilayani Kishapu.
Mhandisi kutoka Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wilaya ya Kishapu, Nicholaus Mathias (kulia) na Mhandisi kutoka Kampuni ya Ukandarasi Hydrotech,  Innocent Msacky wakirekebisha mfumo wa umeme katika mradi wa maji safi wa Nyenze – Ng’wang’holo kata ya Mwadui - Lohumbo wilayani Kishapu.
Meneja wa RUWASA wilaya ya Kishapu, Mhandisi Dickson Protas Kamazima akizungumza wakati wa zoezi la kufunga Mota mpya ya kuendesha Pampu ya kusukuma maji katika mradi wa maji safi wa Nyenze – Ng’wang’holo. Kushoto ni Mwenyekiti wa kijiji cha Ng’wang’holo Bw. William Bulugu Kabisi.
Mhandisi kutoka Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wilaya ya Kishapu, Nicholaus Mathias (kushoto) na Mhandisi kutoka Kampuni ya Ukandarasi Hydrotech,  Innocent Msacky wakifunga Mota mpya ya kuendesha Pampu ya kusukuma maji katika mradi wa maji safi wa Nyenze – Ng’wang’holo.
Meneja wa RUWASA wilaya ya Kishapu, Mhandisi Dickson Protas Kamazima (kulia) akizungumza wakati wa zoezi la kufunga Mota mpya ya kuendesha Pampu ya kusukuma maji katika mradi wa maji safi wa Nyenze – Ng’wang’holo.
Meneja wa RUWASA wilaya ya Kishapu, Mhandisi Dickson Protas Kamazima (kulia) akishirikiana na wananchi kufunga Mota mpya ya kuendesha Pampu ya kusukuma maji katika mradi wa maji safi wa Nyenze – Ng’wang’holo
Meneja wa RUWASA wilaya ya Kishapu, Mhandisi Dickson Protas Kamazima (kulia) akishirikiana na wananchi kufunga Mota mpya ya kuendesha Pampu ya kusukuma maji katika mradi wa maji safi wa Nyenze – Ng’wang’holo.
Wananchi wakishiriki zoezi la kufunga Mota mpya ya kuendesha Pampu ya kusukuma maji katika mradi wa maji safi wa Nyenze – Ng’wang’holo.
Wananchi wakishiriki zoezi la kufunga Mota mpya ya kuendesha Pampu ya kusukuma maji katika mradi wa maji safi wa Nyenze – Ng’wang’holo.
Wananchi wakishiriki zoezi la kufunga Mota mpya ya kuendesha Pampu ya kusukuma maji katika mradi wa maji safi wa Nyenze – Ng’wang’holo.
Wananchi wakishiriki zoezi la kufunga Mota mpya ya kuendesha Pampu ya kusukuma maji katika mradi wa maji safi wa Nyenze – Ng’wang’holo.
Zoezi la kufunga Mota mpya ya kuendesha Pampu ya kusukuma maji katika mradi wa maji safi wa Nyenze – Ng’wang’holo likiendelea.
Zoezi la kufunga Mota mpya ya kuendesha Pampu ya kusukuma maji katika mradi wa maji safi wa Nyenze – Ng’wang’holo likiendelea.
Zoezi la kufunga Mota mpya ya kuendesha Pampu ya kusukuma maji katika mradi wa maji safi wa Nyenze – Ng’wang’holo likiendelea.
Mwenyekiti wa kijiji cha Ng’wang’holo Bw. William Bulugu Kabisi akiishukuru RUWASA Kishapu Mota mpya ya kuendesha Pampu ya kusukuma maji katika mradi wa maji safi wa Nyenze – Ng’wang’holo wilayani Kishapu.
Katibu wa Kamati ya Watumiaji Maji katika mradi wa maji safi wa Nyenze – Ng’wang’holo, Anna Moshi akielezea namna wananchi watavyonufaika na mradi wa maji katika mradi wa maji safi wa Nyenze – Ng’wang’holo wilayani Kishapu.
Akina mama wakizungumza wakati wa zoezi la kufunga Mota mpya ya kuendesha Pampu ya kusukuma maji katika mradi wa maji safi wa Nyenze – Ng’wang’holo wilayani Kishapu.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger