Friday, 15 April 2022

KIJANA ATUPWA JELA KWA KUIBA MAFUTA YA KUPIKIA, MAJANI YA CHAI


Kijana mwenye umri wa miaka 21 amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja gerezani au kulipa faini ya KSh 100,000 sawa na shilingi 2,100,000/- za Tanzania kwa tuhuma za kushiriki wizi dukani.

Alvin Linus Chivondo alishtakiwa kwa kuiba kilo 5 za mchele, lita 5 za mafuta ya kupikia, kilo 2 za sukari, asali na majani ya chai bidhaa zote zenye thamani ya KSh 3,165 sawa na shilingi 66,000 za Tanzania kutoka kwa duka la jumla la Naivas karibu na Moi Avenue nchini Kenya.

Akiwa mbele ya hakimu mkuu wa Mahakama ya Milimani Wendy Micheni mnamo Jumatano, Aprili 13,2022 Chivondo alikiri mashtaka mawili ya kuiba na kumiliki bidhaa za wizi.

 Mshukiwa huyo ambaye husukuma mkokoteni jijini aliiarifu mahakama kwamba yeye na familia yake walikuwa wamelala njaa kwa siku tatu.

"Nina mtoto wa miezi minne na nilikuwa nimeshindwa kuilisha familia yangu. Unaona niliiba tu chakula. Tangu nilipopoteza ajira yangu sijakuwa na uwezo wa kuilisha familia yangu,” alijitetea.

 Mahakama iliambiwa kuwa Chivondo alijifanya mteja, akaokota bidhaa kisha kuvipakia kwenye begi alilokuwa nalo.

 Hata hivyo, alinaswa na wafanyakazi wa duka wanaosimamia kamera za CCTV, alipojaribu kutoka katika duka hilo bila kulipa.

 Korti iliarifiwa kwamba mshukiwa alikuwa ameshikwa hapo awali akiiba dukani humo na kusamehewa.
Share:

AKAMATWA NA MENO YA TEMBO, NYAMA YA TEMBO NDANI YA HIFADHI YA KATAVI


Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Ali Makame Hamad akionesha meno mawili ya tembo mbele ya waandishi wa Habari ambayo amekamatwa nayo mtuhumiwa Mashaka Mavunje mkazi wa Kijiji cha Mtakuja Tarafa ya Nsimbo Wilaya ya Mpanda amekamatwa nayo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Katavi. Picha na Walter Mguluchuma
Kamanda Polisi Mkoa wa Katavi Ally Makame Hamad akionesha bunduki aina ya gobore aliyokamatwa nayo mtuhumiwa Mashaka Mavunje Mkazi wa Kijiji cha Mtakuja aliyokutwa nayo akiwa na meno mawili ya tembo na nyama kilo tisini akiwa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Katavi akifanya ujangili wa kuua wanyama

Na Walter Mguluchuma -Katavi

Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi kwa kushirikiana na askari wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi wamefanikiwa kumkamata Mashaka Mavunje (42) Mkazi Kijiji cha Mtakuja Tarafa ya Nsimbo Wilaya ya Mpanda akiwa na meno ya tembo mawili na nyama ya tembo kilo 90 akiwa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Katavi .

Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Katavi Ali Makame Hamad mtuhumiwa huyo amekamatwa Aprili 13,2022 majira ya saa saa nane mchana katika maeneo ya Kashoka ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Katavi .

Amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa kufuatia taarifa walizokuwa wamezipata jeshi la polisi na TANAPA za kuwa mtu huyo anajihusisha na ujangili wa kuua wanyama ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Katavi na ndipo walipoanza kufanya msako mkali wa kumsaka mtuhumiwa huyo .

Kamanda Hamad ameeleza kuwa mtuhumiwa Mashaka Mavunje siku hiyo ya tukio alikamatwa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Katavi akiwa na meno mawili ya mnyama tembo yenye uzito wa kilogramu 3.1 na nyama ya tembo kili tisini .

Pia alikamatwa akiwa na silaha moja aina ya gobore ambayo ilitumika kwa ajiri ya kumuuwa tembo huyo pamoja na panga moja na kisu kikubwa aina ya sime .

Amebainisha kuwa mtuhumiwa huyo aliingia ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Katavi akiwa na silaha bunduki aina ya gobore ambapo alimpiga na kumuua mnyama tembo na kisha alimtoa meno yake na kisha aliweza kubeba kilo hizo tisini za mnyama huyo alizokutwa nazo.

Mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa ili kuweza kupata washiriki wenzake na mara baada ya upelelezi kukamilika jalada litafikishwa katika ofisi ya Taifa ya mashitaka Mkoa wa Katavi kwa taratibu za kisheria .
Share:

MTANZANIA AKAMATWA AKISAFIRISHA WAHAMIAJI HARAMU DODOMA


Na Doreen Aloyce, Dodoma
Jeshi la Uhamiaji Mkoa wa Dodoma linawashikilia raia watano wa Ethiopia akiwemo Mtanzania mmoja kutokana na kuingia nchini kinyume cha sheria na utaratibu wa nchi pamoja na raia mmoja wa Tanzania Tito Mbwilo mwenye umri wa miaka 43 mkazi wa Iringa na Tunduma ambaye alikuwa akisafirisha wahamiaji hao.

Akiongea na waandishi wa Habari Afisa uhamiaji Mkoa wa Dodoma Bahati Mwaifuge amesema  wahamiaji hao haramu walikamatwa April 3 mwaka huu katika kijiji cha Mtera wakielekea Tunduma Mkoa wa Songwe.

"Jeshi letu la uhamiaji tumefanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu watano akiwemo mtanzania mmoja wakisafirishwa kwenye gari yenye namba za usajiri T991 DXB Toyota Rumioni ambalo lilikuwa linaendeshwa na Tito Mbwilo akijua ni kosa",amesema Bahati.

Aidha amesema baada ya kuwatia mbaroni wahamiaji haramu hao, Dereva wao Tito Mbwilo alijaribu kutoroka bila mafanikio kutokana na umahili wa Askari ambapo waliweza kimdhibiti na kumuweka chini ya ulinzi.

Hata hivyo alitoa onyo kwa wasafirishaji wote wanaojihusisha na wahamiaji haramu katika Mkoa wa Dodoma kuacha mara moja na kwamba jeshi tayari limebaini wamebadili mbinu kutoka magari makubwa na kutumia magari madogo.

"Niwaombe wananchi wote wakiwemo wa Mtera kuendelea na ushirikiano kutoa taarifa za kusafirisha wahamiaji haramu jambo ambalo litasaidia katika utendaji kazi wetu",alisema Bahati.
Share:

Brand New Hit: AGGY BABY Ft Mr. LG - ON THE BED

Msanii Aggy Baby
Msanii wa Bongo Fleva Agness Suleiman maarufu 'Aggy Baby' ameachia wimbo Mpya unaitwa 'On The Bed' wenye mtindo wa Amapiano aliomshirikisha msanii Mr LG.


Tayari wimbo huu unapatikana kwenye platform zote za muziki za mitandaoni ikiwemo Boomplay, Youtube.

 Mbali ya kuimba pia Aggy Baby ni rapa , msanii wa filamu , mtunzi, Mwandishi wa nyimbo na Mwanaharakati wa Vijana katika mambo ya kusaidia jamii.

Sikiliza Muziki huu mzuri Brand New hit #OntheBed Aggy Baby ft Mr LG

Share na Marafiki na wapendanao na usisahau ku subscribe youtube account ya Aggybaby

Share:

Thursday, 14 April 2022

RAIS SAMIA MGENI RASMI KILELE CHA MEI MOSI




Na Dotto Kwilasa,Malunde 1Blog-DODOMA .

RAIS wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hasani anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye kilele cha siku ya wafanyakazi-Mei Mosi itakayofanyika Kitaifa jijini Dodoma. 

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka ameeleza hayo leo wakati akiongea na vyombo vya habari kuhusu Mkoa wa Dodoma kuwa mwenyeji wa maadhimisho ya sherehe za Mei Mosi kitaifa,2022 huku akiwataka wakaazi wa mkoa huu kutumia tukio hilo kama fursa kibiashara .

"Mkoa wetu umepewa heshima ya kuwa mwenyeji wa sherehe za Mei Mosi kitaifa ,sherehe hii itaambatana na matukio na shughuli mbalimbali katika juma la maadhimisho kabla ya kilele hivyo niwaombe wafanyabiashara kujiandaa kuwahudumia zaidi ya watu 3000 ambao watahitaji huduma za kijamii kama vile malazi ,chakula ,mavazi na nyinginezo."Amesema Mtaka

Ameeleza kuwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma inashirikiana kwa ukaribu na shirikishio la wafanyakazi (TUCTA),Chama kinachoratibu maadhimisho ya 2022 TALGWU,Ofisi ya Waziri Mkuu_KAZI na wadau wengine wa maendeleo nchini. Akielezea fursa zitakazopatikana kupitia maadhimisho hayo,

Mtaka amesema katika kufikia azma ya Serikali ya kuhakikisha kila fursa inayojitokeza inachangia ujenzi wa uchumi imara,Ofisi yake kwa kushirikiana na wadau imeazimia kutumia fursa hiyo kuziunganisha sekta zote za kiuchumi kwa manufaa ya taifa.

"Tumepanga kuandaa maadhimisho ya kipekee ,kwani maadhimisho haya ni ya pili kwa Rais Samia tangu awepo madarakani."amesema Mkuu huyo wa mkoa wa Dodoma.

Pamoja na hayo Mtaka amezitaja shughuli mbalimbali kuelekea kilele cha maadhimisho ya Mei Mosi kuwa ni pamoja na kikao cha wahariri na uzinduzi wa hashtag,michezo mbalimbali ikihusisha Drafti,riadha,mpira wa miguu,mpira wa Pete,kuvuta kamba,kufukuza kuku na bao. 

"Michezo hii itafanyika kwenye viwanja vya Jamhuri,Kilimani Veteran,St John University,sheli wajenzi,Chinangali park,Vijana na mtekelezo -Dodoma Central"amefafanua Mtaka 

Mkuu huyo wa mkoa wa Dodoma amesema maonyesho mbalimbali ya Mei Mosi yakiambatana na maonyesho ya OSHA yatafanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Center kuanzia tarehe 22 Aprili hadi 30 Aprili 2022 ambayo yatashirikisha makundi mbalimbali yakiwemo Viwanda,Wizara ,Vyama vya wafanyakazi na taasisi za fedha.

Mengine ni wafanya biashara wa kati na wakubwa,Taasisi za Umma na za huduma, wajasiriamali wadogo na wa kati pamoja na wadau wengine wa maendeleo Kwa kuhusisha upimaji wa VVU,uchangiaji damu pamoja na utoaji wa chanjo ya UVICO-19.

"Kutakuwa pia na kongamano la midahalo kupitia vyombo vya habari na Katika na Katika kumbi za mikutano ambapo mada mbalimbali zitajadiliwa na Vyama vya wafanyakazi,waajiri na Serikali,kutunuku wafanyakazi hodari ngazi ya Mkoa ,kufanya ziara za utalii wa miradi ,burudani,maandamano ya wafanyakazi na zana za kazi,"amefafanua na kuongeza;

 ''Katika kuwakumbusha watanzania uzalendo tumeandaa kauli mbalimbali za Viongozi na nukuu zao ambazo watazisikiliza Katika maadhimisho ya Mei Mosi na zitakuwa zikitoka Kila Siku kupitia vyombo vya habari,niwaombe mpate fursa kusikiliza Ili mjifunze mengi kupitia hashtag yetu ya #MEIMOSI2022dodomakivingine,"amesema 

Kwa upande wake rais wa TUCTA Tumaini Nyamhokya ametumia nafasi hiyo kuwataka wafanyakazi kuhudhuria kwa wakati maadhimisho hayo ili kutimiza malengo na kutaka sherehe hizo ziambatane na shughuli za maendeleo na watu. 



 "Nitumie nafasi hii kuwakumbusha wafanyakazi kushiriki kikamilifu akatika zoezi la sensa ya watu na makazi linalotarajiwa kuanza hivi karibuni, wafanyakazi pia mnapaswa kutumia fursa hii kuwashawishi watu wengine kuwa na utayari wa kuhesabiwa,"amesisitiza 


Share:

Video Mpya ya Injili : RISANDI LAIZER - WEWE NI BWANA


Mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka Jijini Arusha Risandi Laizer anakukaribisha kutazama Video ya Wimbo wake Mpya wa Injili unaoitwa 'Wewe ni Bwana' Unaweza kuwasiliana na Risandi Laizer kwa simu namba 0766200459 au barua Pepe rlaizer.tz108@gmail.coma

Tazama video hapa chini
Share:

RAIS SAMIA ATUA WASHINGTON MAREKANI



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Viongozi, Watumishi wa Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania pamoja na Baadhi ya Wawakilishi kutoka nchi za SADC waliofika kumpokea alipowasili Jijini Washington Nchini Marekani kwa ajili ya kuanza ziara ya Kikazi leo tarehe 13 April 2022.
Share:

Wednesday, 13 April 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI APRILI 14,2022

Magazetini leo Alhamis April 14 2022


Share:

KIVULINI, POLISI MWANZA WATAKA BODABODA KUEPUKA NGONO NA WANAFUNZI, WAKE ZA WATU, KUZAA NA KUTELEKEZA


Mkurugenzi wa Shirika la Kivulini Yassin Ally akizungumza na waendesha pikipiki kata ya Mirongo jijini Mwanza.

Na Mwandishi wetu - Mwanza
Waendesha pikipiki mkoani Mwanza wametakiwa kuwa mstari wa mbele kupinga vitendo vya uhalifu ikiwemo tabia ya kushawishi wanafunzi na kujihusisha nao kimapenzi.

Wito huo umetolewa Aprili 13,2022 na Mkurugenzi wa Shirika la kutetea haki za wanawake na watoto la KIVULINI Yassin Ally wakati wa kampeni ya kuzuia na kutokomeza watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu.

“Ukilinganisha sababu za watoto kuwepo ama kutowepo mtaani unakuta hasara za kuwepo kwao mtaani ni nyingi mno kuliko faida, hivyo ni hatuna budi kama jamii mkiwemo waendesha bodaboda na makundi yote yakiwemo ya wanawake wajasiriamali,viongozi wa dini na kila mmoja wetu kushiriki kikamilifu ili kufanikisha kampeni hiyo itakayodumu kwa muda wa wiki nane”, alisema Yassin.

Aidha Yassin aliwataka waendesha pikipiki kufanya kazi hiyo kwa malengo ili kujikomboa kiuchumi badala ya kuendekeza mambo yasiyo na tija ikiwemo ngono pamoja na ulevi wa kupindukia.

“Mfanye kazi hii kwa faida ya familia zenu,mkumbuke kuwa ngono na ulevi haziwahi kubadilisha maisha ya mtu ,hivyo acheni kuweka heshima baa bali wekeni heshima majumbani mwenu”,aliongeza mkurugenzi huyo wa shirika la Kivulini.

Kampeni hiyo imewafikia waendesha pikipiki kufuatia baadhi yao kunyoshewa vidole kwa kuwa chanzo cha ongezeko la watoto wa mitaani katika mkoa wa Mwanza.

“Watoto wengi wa mtaani wanatokana na sisi waendesha bodaboda kutokana na wengi wengi kuwa na tabia ya kuzaa na kisha kutelekeza,ni lazima tuambiane ukweli kama tukitaka kutibu tatizo hili”, alisema Francis John mmoja wa waendesha pikipiki katika kata ya Mirongo.

Baadhi ya waendesha pikipiki wakizungumza katika mkutano huo walikiri wengi wao kuwa na tabia ya kuwarubuni wanafunzi pamoja na kutembea na wake za watu huku wakidai baadhi yao wamekuwa wakifanya hivyo kwa kushawishiwa.

Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Waendesha pikipiki Kanda ya Mjini Kati Ramadhan Jacobo aliwaasa waendesha pikipiki kujiepusha na tabia ya kutongoza pamoja na kujihusisha na mapenzi na wateja wao.

“Asilimia tisini ya abiria tunaowabeba na wanaotulipa fedha ni wadada, na nyie ni mashahidi ukimpata na kumtongoza tu huyo umempoteza na akikubali umeanza kula hasara”, alisema Jacob.

Kwa upande wake, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi kata ya Mirongo Fatuma Mpinga aliwaasa waendesha pikipiki kuzingatia sheria za usalama barabara ili kuepusha ajali zinazoepukika.

“Fuateni sheria za usalama barabarani kwa manufaa yenu wenyewe sio yangu,hakikisheni mnakuwa na helmet mimi nikikukamata huna helmet zinakutoza elfu kumi ya faini nitakuambia paki pikipiki yako hapa kituoni kanunue helmet”, alisema Fatuma.

Aidha Fatuma aliwassa waendesha pikipiki kufichua wahalifu pamoja na kutunza familia zao.

“Natambua mnafahamiana na watu wengi sana wema na wahalifu,niombe muwafichue wahalifu maanake sisi sote tunahitaji usalama. Pia tunzeni familia zenu acheni kudanganya wanafunzi kwa chipsi huku nyumbani mnaacha elfu mbili halafu unarudi nyumbani unakuta kuku na unakula bila aibu”, aliongeza Fatuma.

Mkurugenzi mtendaji wa shirika la kutetea haki za wanawake na watoto la KIVULINI Yassin Ally (kulia) na Mkaguzi Msaidizi wa polisi kata ya Mirongo Fatuma Mpinga wakipiga makofi wakati wa mkutano wa waendesha pikipiki kata ya Mirongo uliolenga kuhimiza ushiriki wao katika kampeni ya kuzuia na kutokomeza tatizo la watoto wa mitaani mkoani Mwanza.
Mkurugenzi wa Kivulini Yassin Ally akizungumza na waendesha pikipiki kata ya Mirongo jijini Mwanza
Mkurugenzi wa Kivulini Yassin Ally akizungumza na waendesha pikipiki kata ya Mirongo jijini Mwanza
Mkurugenzi wa Kivulini Yassin Ally akizungumza na waendesha pikipiki kata ya Mirongo
Mkurugenzi wa Kivulini Yassin Ally akizungumza na waendesha pikipiki kata ya Mirongo
Mkaguzi Msaidizi wa polisi kata ya Mirongo Fatuma Mpinga akizungumza na kusisitiza jambo wakati wa mkutano wa waendesha pikipiki kata ya Mirongo.
Mkaguzi Msaidizi wa polisi kata ya Mirongo Fatuma Mpinga akizungumza na kusisitiza jambo wakati wa mkutano wa waendesha pikipiki kata ya Mirongo.
Mkaguzi Msaidizi wa polisi kata ya Mirongo Fatuma Mpinga akizungumza na kusisitiza jambo wakati wa mkutano wa waendesha pikipiki kata ya Mirongo.
Wa tatu kulia ni Mkurugenzi mtendaji wa shirika la kutetea haki za wanawake na watoto la KIVULINI Yassin Ally akifuatilia mjadala wakati wa mkutano wa waendesha pikipiki kata ya Mirongo uliolenga kuhimiza ushiriki wao katika kampeni ya kuzuia na kutokomeza tatizo la watoto wa mitaani mkoani Mwanza.
Mkaguzi Msaidizi wa Polisi kata ya Isamilo akizungumza katika mkutano wa waendesha bodaboda kata ya Mirongo kuhusu umuhimu wa kuzingatia sheria za usalama barabarani,kufichua wahalifu n.k
Mkaguzi Msaidizi wa Polisi kata ya Isamilo akizungumza katika mkutano wa waendesha bodaboda kata ya Mirongo kuhusu umuhimu wa kuzingatia sheria za usalama barabarani,kufichua wahalifu n.k
Waendesha pikipiki wakifuatilia mada mbalimbali
Waendesha pikipiki wakifuatilia mada mbalimbali
Waendesha pikipiki wakifuatilia mada mbalimbali
Waendesha pikipiki wakifuatilia mada mbalimbali
Mmoja wa waendesha pikipiki kata ya Mirongo akizungumza kwenye mkutano huo
Mmoja wa waendesha pikipiki kata ya Mirongo akizungumza kwenye mkutano huo

Share:

Tuesday, 12 April 2022

JINSI MATAJIRI WANAPATA PESA ZAO


Watafiti Watoa Habari Wengi huwa wanajiuliza ni mbona hawapati pesa? Jibu ni rahisi lakini wengi pia bado hawafahamu sababu au kiini cha umaskini wao. 

Kuna watu ambao wamesoma wako na makaratasi ya Degree na Diploma lakini hawajawahi kufanikiwa kupata kibarua cha kufanya kama wenzao ambao hata hawakufuzu kama wao. Maisha ndivyo yalivyo.

 Sasa wacha niseme ukweli kuwa pesa zinapenda wale wanaozipenda. Kama hupendi pesa na kushukuru kila mara unapozipata basi wewe utabaki kuangamia na kulia huku marafiki wako wakinunua magari na kuyabadilisha kama surauri.

 Penda pesa na wakati wowote unapozishika hakikisha unashukuru na kuziombea baraka la sivyo zitaponyoka na kuendea mwenye anajua kushukuru. Kando na hilo, pia pesa lazima zifanyiwe baraka fulani. Kwa mfano mimi napenda kujifanyia Money Spells. 

Kila mara ninapojifanyia Money Spells ama Wealth Spells ninaanza kushika pesa nyingi mno. Mikono zangu huwa zinashika hela kiwango kikubwa yaani mamilioni. Mimi tangu niaze kufanya Money Spells nimefanikiwa na hata biashara zangu zimeendelea mno. 

 Kwa maelezo kamili kuhusu Spell Casting hakikisha unatembelea wavuti www.kiwangadoctors.com na pia unaweza piga simu kupitia nambari ya Kiwanga Doctors ya +254 769404965 au andika barua pepe kwa: kiwangadoctors@gmail.com. Daktari Kiwanga vilevile anatibu magonjwa kama Kisonono, Kisukari na mengine mengi. 


Pia huwa wanatatua migogoro ya mapenzi, kurudisha mali iliyo ibiwa, mpenzi aliyetoroka na mengineyo. Dr. Kiwanga pia anaweza kushika wezi, kuzuia mikosi, kumaliza na kushinda kesi kotini, kuimarisha nyota yako ya maisha na kikazi na kurudish mke au bwana nyumbani.

Share:

SERIKALI YAANZA MCHAKATO KITAMBULISHO CHA NIDA KITUMIKE KUPIGIA KURA

Serikali ya Tanzania imesema imeanza mchakato wa kuunganisha kitambulisho cha Taifa na kitambulisho cha mpiga kura ili kumfanya mtanzania kutumia kitambulisho cha taifa katika zoezi la kupiga kura.

Akiuliza swali bungeni leo Mbunge wa Kawe Askofu Josephat Gwajima alitaka kujua kama Serikali haioni umuhimu wa kuunganisha mifumo ya Kitambulisho cha Mpiga Kura na Kitambulisho cha Taifa ili kuepusha usumbufu kwa Wananchi,

Akijibu swali hilo kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Hamis Hamis amesema serikali imeanza mchakato wa kuunganisha vitambulisho hivyo viwili na kufanya sasa mtanzania kutumia kitambulisho cha taifa katika mchakato wa Uchaguzi wa kawaida na ule wa kieletroniki ‘e-voting’.

Naibu Waziri Hamis amesema kuwa matumizi hayo yatapunguza gharama kwa Serikali katika kuandikisha na kutengeneza daftari pamoja na kurahisisha usimamizi wa wapiga kura.

Ameeleza kuwa Mawasiliano kati ya Taasisi hizo mbili yenye dhumuni la kuiwezesha Kanzidata ya NIDA kutumika katika zoezi la uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura yameanza mwezi Machi, 2022.

Chanzo - EATV
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger