Friday, 24 September 2021

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA SEPTEMBA 24,2021






Share:

Thursday, 23 September 2021

WAZAZI NA WALEZI SERENGETI WAASWA KUSOMESHA MTOTO WA KIKE

Na Frankius Cleophace Serengeti.
Kituo cha watoto wenye Ulemavu cha St: Justin kilichopo Manispaa ya MusomaMkoani Mara kwa kushirikiana na Shirika la Right to Play kupitia mradi wa elimu Jumuishi kimewapatia elimu wanafunzi shule ya msingi Regicha na wazazi kuhusu umuhimu wa elimu kwa mtoto wa kike,usawa wa kijinsia na ulinzi kwa mtoto.

Emmanuel Omenda ambaye ni Meneja Mradi wa Elimu Jumuishi kutoka kituo cha watoto wenye ulemavu cha St:Justin kilichopo Musoma alisema kuwa wanatumia michezo mbalimbali kufikisha elimu hiyo nakueleza kuwa wanafunzi wa shule ya msingi Regicha 498 na wazazi 60 wamefikiwa na elimu hiyo.

"Tunatumia Ngonjera, Maigizo, Mpira wa Miguu hata kwa watoto wa kike lengo nikufikisha ujumbe uliokusudiwa kupitia Mradi wa Elimu Jumuishi na Elimu hii ni endelevu tutaemdela kutoa Elimu katika kata nyingine wilaya ya Serengeti Mkoani Mara ili jamii iwezekuondokana na suala la Ukatili",alisema Emmanuel.

Kwa upande wake Afisa elimu kata ya Regicha Jumamosi Regata alisema kuwa akipongeza kituo hicho kuendelea kutoa elimu kwa wazazi na walezi pamoja na wanafunzo ili jamii iondokane na ukatili.

Aidha wanafunzi kutoka shule ya msingi Regicha iliyopo wilayani Serengeti Mkoani Mara walilisisitiza elimu hiyo kuendelea kutolewa jamii iweze kuthamini na kutambua haki za motto wa kike.

Share:

MATUKIO KATIKA PICHA TULIA TRADITIONAL DANCES FESTIVAL JIJINI MBEYA


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akizungumza na wananchi katika Tamasha la Utamaduni la Ngoma za Asili lijulikanalo Tulia ambapo amesema utamaduni wa ngoma za asili utasaidia kukuza utalii hivyo ni vema wananchi wajitokeze kufanya matamasha kama hayo ambayo pia yanaongeza kipato kwa washiriki. Tamasha hilo limefanyika katika Viwanja vya Airport ya zamani jijini Mbeya


Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb) akimtambulisha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) wakati wa Tamasha la Utamaduni la Ngoma za Asili lijulikanalo kama Tulia Traditional Dance Festival lililofanyika leo katika Viwanja vya Airport ya zamani jijini Mbeya.


Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb) akimkaribisha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) (kulia) katika Tamasha la Utamaduni la Ngoma za Asili lijulikanalo kama Tulia Traditional Dance Festival lililofanyika leo katika Viwanja vya Airport ya zamani jijini Mbeya. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mjini, Dkt. Rashid Chuachua.


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akipokea zawadi ya T-shirt kutoka kwa Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) alipotembelea banda la Maryprisca Foundation katika Tamasha la Utamaduni la Ngoma za Asili lijulikanalo kama Tulia Traditional Dance Festival lililofanyika leo katika Viwanja vya Airport ya zamani jijini Mbeya. Anayeshuhudia ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb).


Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb)(katikati), Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) (kulia) na Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) (wa pili kutoka kulia) katika picha ya pamoja na wadhamini waTamasha la Utamaduni la Ngoma za Asili lijulikanalo kama Tulia Traditional Dance Festival lililofanyika leo katika Viwanja vya Airport ya zamani jijini Mbeya.


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) na Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) wakifuatilia Tamasha la Utamaduni la Ngoma za Asili lijulikanalo kama Tulia Traditional Dance Festival lililofanyika leo katika Viwanja vya Airport ya zamani jijini Mbeya.
Share:

MILIONI 700 ZA UJENZI WA BARABARA VIJIJINI , KARAGWE WAMSHUKURU RAIS SAMIA

Mbunge wa jimbo la Karagwe Mhe. Innocent Bashungwa katikati aliyevalia kofia ya kijani akionesha moja ya eneo linalohitaji kufanyiwa marekebisho wakati alipofanya ziara ya kukagua mwenendo wa ukarabati wa barabara yenye urefu wa kilometa 96 inayofanyiwa ukarabati katika jimbo lake. Wa kwanza kushoto ni meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini TARURA wilaya ya Karagwe Kalimbula Malimi, wa pili ni diwani wa kata ya Nyakakika Mhe. Exsavery Buguzi na wa kwanza kulia ni Ivo Ndisanye Katibu wa mbunge na Samson Mushi mkaguzi wa barabara mkoa wa Kagera TANROADS.

***

Na Mwandishi Wetu, Karagwe

Serikali imetoa Shilingi milioni 700 kusaidia ukarabati wa barabara za vijijini katika jimbo la Karagwe mkoani Kagera ili kuboresha miundombinu ya jimbo hilo hatua inayosaidia kurahisisha mawasiliano na kuboresha huduma za kijamii jimboni humo.

Akiwa ziarani jimboni humo kukagua miundombinu ya barabara zinazokarabatiwa, Mhe. Innocent Bashungwa amesema fedha zilizotolewa kwa ajili ya ukarabati wa barabara jimboni humo zitumike kulingana na malengo yaliyokusudiwa kwa kuzingatia matumizi sahihi ya fedha zilizotolewa. 

Mhe. Bashungwa amewahimiza wabunge wenzake mkoani Kagera kuwa mstari wa mbele kufanya ukaguzi wa mara kwa mara ili fedha iliyotolewa na Serikali kwa ajili ya kuboresha barabara za vijijini zifanye kazi iliyokusudiwa kufikia malengo ya kuwahudumia wananchi kwa kuboresha uchumi wao na taifa kwa ujumla. 

“Sisi tunamshukuru Mhe. Rais Mama Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia kutupa kiasi hiki kikubwa cha fedha ili tuboreshe barabara kwenye majimbo yetu lakini wito wangu ni kwamba hawa wataalumu wasisubiri mbunge aende site ili kuwaambia eneo fulani mlitakiwa muweke mataleo au mitaro ya maji ili yasiaharibu barabara, wataalamu wenyewe wanatakiwa wajue tangu wanaposanifu ujenzi husika” alisema Mhe. Bashungwa.

Akizungumzia hatua hiyo meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini TARURA wilaya ya Karagwe Bw. Kalimbula Malimi amesema baada ya ziara hiyo sehemu zote zilizoainishwa ambazozinahitaji marekebisho zitafanyia kazi haraka iwezekanavyo.

Katika ziara hiyo Mhe. Bashungwa aliambatana na Madiwani wa kata mbalimbali, watendaji wa TARURA na TANROAD ambapo ameleza kushutushwa kwake na namna mkandarasi anayetekeleza ukarabati wa barabara yenye urefu wa kilometa 96 inaanzia kata ya Nyakahanga kwenda kata za Nyabiyonza, Bweranyange, Nyakakika, Nyakabanga, Kibondo mpaka Lukanja ambayo imejengwa bila kuweka matoleo ya maji na mitaro ya barabara.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakazi wa wilaya ya Karagwe akiwemo diwani wa kata ya Nyakakika Mhe. Exsavery Buguzi wameeleza matarajio yao kuwa kukamilika kwa barabara hiyo kutaongeza urahisi wa shughuli za biashara kwa maana ya usafiri na kusafirisha mizigo kati ya wakazi wa mkoa wa Kagera na nchi jirani ya Rwanda kupitia kivuko cha  Bweranyange ambacho kinaziunganisha nchi hizo mbili kwa usafiri wa majini.

Vile vile, wakazi wa Karagwe wanaamini kukamilika kwa barabara hiyo kutaongeza urahisi kwa watalii kufanya shughuli za utalii wilayani humo katika mbuga mpya mbalimbali ikiwemo, Karagwe, Lumanyika, Ibanda na Burigi Chato.
Mkaguzi wa barabara mkoa wa Kagera TANROADS Samson Mushi akimuelezea jambo 
 Mbunge wa jimbo la Karagwe Mhe. Innocent Bashungwa katikati aliyevalia kofia ya kijani wakati alipofanya ziara ya kukagua mwenendo wa ukarabati wa barabara yenye urefu wa kilometa 96 inayofanyiwa ukarabati katika jimbo la Karagwe mkoani Kagera.
Mbunge wa jimbo la Karagwe Mhe. Innocent Bashungwa aliyevalia kofia ya kijani akihoji jambo kwa wataalam wa TANROAD na TARURA wakati wa ziara yake ya kukagua mwenendo wa ukarabati wa barabara yenye urefu wa kilometa 96 inayofanyiwa ukarabati katika jimbo la Karagwe
Mbunge wa jimbo la Karagwe Mhe. Innocent Bashungwa katikati aliyevalia kofia ya kijani akiwasikiliza wakazi wa Kata ya Nyabiyonza wakati wa ziara yake ya kukagua mwenendo wa ukarabati wa barabara yenye urefu wa kilometa 96 inayofanyiwa ukarabati katika jimbo lake.
Sehemu ya barabara inayofanyiwa ukarabati kwa kiwango cha Moramu kuanzia kata ya Nyakahanga kwenda kata za Nyabiyonza, Bweranyange,  Nyakakika, Nyakabanga, Kibondo mpaka Lukanja 
Sehemu ya barabara inayofanyiwa ukarabati kwa kiwango cha Moramu kuanzia kata ya Nyakahanga kwenda kata za Nyabiyonza, Bweranyange,  Nyakakika, Nyakabanga, Kibondo mpaka Lukanja 

Share:

TAKUKURU, CHAMA CHA SKAUTI TANZANIA WAZINDUA MWONGOZO KUPAMBANA NA RUSHWA

Naibu Waziri wa nchi,Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma  na utawala bora Deogratius Ndejembi  akiongea Kwenye uzinduzi wa  mwongozo wa mapambano dhidi ya rushwa

Na Dotto Kwilasa - Dodoma
SERIKALI kupitia Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini (TAKUKURU)imezindua Muongozo wa Mkakati wa makubaliano baina yake na Chama cha Skauti Tanzania wenye lengo la kusisitiza ushirikishwaji wa wadau katika mapambano dhidi ya rushwa  rushwa kuanzia ngazi ya chini.

Akiongea kwenye uzinduzi huo,Naibu Waziri wa nchi,Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma  na utawala bora Deogratius Ndejembi  amesema mwongozo huo utasaidia kujenga uchumi imara na kuchochea maendeleo ya huduma za kijamii.

Amesema Muongozo huo pia unajenga kuelimisha jamii kuacha vitendo vya rushwa huku akitoa   maelekezo  kwa maafisa elimu mikoa ,wilaya   na maafisa TAKUKURU, kuhakikisha wanatenga muda wa kuelimisha vijana na jamii kwa ujumla  kuhusu madhara ya rushwa.

Naibu Waziri Ndejembi amesema kutokana na kwamba vijana wengi wa Skauti wapo masomoni itakuwa rahisi kwao kufanya uelimishaji kupitia makundi mbalimbali huku akitoa agizo kwa wanufaika mafunzo hayo kupeleka kwa jamii elimu wanayoipata Kuhusu suala la rushwa.

Mbali na hayo ameeleza kuwa Serikali kwa upande wake itaendelea kuunga mkono juhudi hizo na kuleta mafanikio ambayo yatafikisha ujumbe kimataifa kwamba Skauti ni kundi muhimu linaloshiriki kurudisha haki kwa kuzingatia uzalendo na uwajibikaji.

Kutokana na hayo,Skauti Mkuu Mwantumu Mahiza ametumia nafasi hiyo kuwataka Viongozi na Wakuu wa idara  kuwapa ruhusa watumishi wa Umma kushiriki masuala ya Skauti pindi wanapohitajika na kuwapatia ruzuku Kwa ajili ya kujikimu Kwa kuwa kada hiyo haina fungu la ruzuku kwa wananchama wake.

Amefafanua kuwa,linapokuja Suala la Skauti kukutana ,baadhi ya Viongozi wa Taasisi za Serikali wamekuwa wagumu kutoa ruhusa kwa wafanyakazi wao ambao ni wananchama wa Chama cha Skauti Tanzania kwa kisingizia cha kutokiwa na ruzuku jambo ambalo amesema linabomoa miiko na maadili ya utumishi wa Umma.

"Ziko baadhi ya Taasisi ambazo hadi sasa hazielewi wala kutilia  maanani masuala ya skauti,kupitia hili naomba Serikali itoe mwongozo ili vijana wetu wa Skauti wasidharirike,Skauti sio uhuni,vijana hawa wana thamani ,wasomi na waadilifu lazima tuwaheshimu,"amesisitiza.

Mbali na hayo Skauti  huyo Mkuu nchini,ameiomba serikali kuwaona vijana hao wa Skauti pindi linapokuja Suala la uteuzi wa Viongozi na kuihakikishia Serikali kuwa vijana hao ni waadilifu na wawajibikaji wasiopenda rushwa.

Skauti Mkuu Tanzania,Bi.Mwantumu Mahiza amesema mwongozo huo wa kufundishia masuala ya rushwa utakuwa na tija kubwa kwani vijana walio wengi  hususan shuleni  ndio waathirika wa rushwa  kwa sababu rushwa huchelewesha maendeleo.

Aidha,amesema haiwezekani Tanzania tangu ipate uhuru mwaka 1961 bado inahangaika na miundombinu ya zahanati ,barabara kwani nchi zilizoendelea kuna masuala walishaacha na kujikita mambo mengine ya maendeleo.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu TAKUKURU Neema Mwakalyelye amesema mwaka 2019 walisaini mkataba wa makubaliano na chama cha Skauti Tanzania katika mapambano dhini ya rushwa   na malengo ya mashirikiano hayo ni kuelimisha jamii madhara ya rushwa katika jamii .

Kupitia mkakati wa utekelezaji wa mwongozo huo,wanatarajia kuongeza upana wa makundi ya mapambano dhidi  ya rushwa  nchini ambapo kuna takriban vijana 105 wamenufaika na mafunzo hayo.

Mkurugenzi Elimu kwa Umma TAKUKURU  Dkt. Emmanuel Kiyabo amesema mafunzo hayo yamehusisha wadau mbalimbali ikiwemo chama  cha Maskauti Tanzania na watumishi kutoka TAKUKURU.

Share:

WATUMISHI WATATU WA AFYA WAKAMATWA KWA WIZI WA MASHINE YA OKSIJENI SIMIYU

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Kamshina Msaidizi wa Polisi Richard Abwao akiongea na waandishi wa Habari (hawapo pichani), ofisini kwake.

Mfano wa Mashine ya kuangalia Mapigo ya Moyo, Upumuaji, Wingi wa hewa ya Oksijeni katika damu kwa mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji (Cadiac Monitoring Accessories), kwa hisani ya Mtandao.

Na Costantine Mathias - Simiyu.
JESHI la Polisi Mkoani Simiyu linawashikilia watumishi watatu wa Idara ya Afya kwa wizi wa Mashine ya kuangalia Mapigo ya Moyo, Upumuaji, Wingi wa hewa ya Oksijeni katika damu kwa mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji ambapo mashine hiyo iliibiwa ikiwa ndani ya chumba cha upasuaji mkubwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu (Nyaumata).

Katika taarifa iliyolewa leo kwa waandishi wa Habari na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Kamishna Msaidizi wa Polisi Richard Abwao imeeleza kuwa uchunguzi katika eneo la tukio (Hospitali) ulibaini kuwa chumba hicho cha upasuaji hakikuvunjwa.

"Mnamo tarehe 20/09/2021 majira ya saa 07:30 asubuhi huko Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Simiyu (Nyaumata), iliyopo mtaa wa Nyaumata, Wilaya ya Bariadi, Mkoa wa Simiyu, Getrude Emmanuel (45), msukuma, mkristo na katibu wa hospitali ya mkoa Simiyu, aligundua kuibiwa kwa mashine 01 inayojulikana kwa jina la Cadiac Monitor Accessories yenye namba za usajili ex-7c051585 yenye thamani ya tsh .7,820,000/= iliyokuwa kwenye chumba cha kufanyia upasuaji wa macho’’ amesema Kamanda Abwao.

Amefafanua kuwa "Kiini cha tukio hili ni kujipatia kipato kisicho halali, wafanyakazi katika chumba hicho cha upasuaji wamekamatwa na wanahojiwa kuhusiana na tukio hili ni Paul Igosha (37), msukuma, mkazi wa Somanda, Neema Msekile (24), mnyakyusa, mkazi wa Kidinda na Edward Yirika (27), muha, mkazi wa somanda ambao wote ni wauguzi katika chumba cha upasuaji wa macho hospitali ya nyaumata’’.

Kamanda Abwao ameeleza kuwa baada ya tukio hilo kuripotiwa kituoni hapo upelelezi mkali ulianza mara moja kwa kukagua eneo la tukio na kuhoji baadhi ya mashahidi na baada ya mahojiano hayo timu hiyo ya makachero waliwakamata watumishi wa chumba cha upasuaji wa hospatali hiyo ambao ni Paul Igosha, Neema Msekile na Edward Yirika ambao walihojiwa lakini walikana kuhusika na tukio hilo.

Ameendelea kuwaambia Waandishi wa Habari kuwa (jana) tarehe 22/09/2021 majira ya saa 09:0hrs alikamatwa Allen Cosmas (30), Daktari wa usingizi, chumba cha upasuaji ambaye pia alihojiwa na makachero na hatimaye kukiri kuhusika na tukio hilo, ambapo alieleza kuwa mashine hiyo ameuza mkoani Mwanza .

Ameongeza kuwa timu hiyo ya makachero ilielekea Mkoani Mwanza eneo la kona ya Bwiru wilaya ya Ilemela, Mkoani Mwanza na kufanikiwa kumkamata rafiki wa Daktari huyo aitwaye Enord Iginatio Kalekezi (29), Daktari kituo cha afya Kisorya wilayani Bunda Mkaoni Mara, ambaye alihojiwa na kueleza kuwa ameuza kwa Daktari aitwaye David Omollo (32),  Daktari wa hospitali binafsi iitwayo Royal Hosptal iliyopo kona ya Bwiru wilaya ya mkoa wa Mwanza.

Amesema timu ya makachero ilifika hospitalini hapo na kufanikiwa kuikamata mashine hiyo iliyokuwa kwenye chumba cha upasuaji hospitalini hapo (Royal Hospital) na tayari imeshaletwa na imeifadhiwa kituo cha polisi Bariadi kama kielelezo.

Akaongeza kuwa mpaka sasa watuhumiwa watatu ambao ni Allen Cosmas, David Omollo na Edward Ignatio wapo mahabusu kituo cha polisi bariadi kwa mahojiano na baada ya mahojiano kukamilika watafikisha mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.

Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk. Mike Mabimbi amedhibitisha kutokea kwa tukio hilo, huku akidai kuwa wizi huo umetokea usiku wa kuamkia Jumapili (Sept 19, 2021) wiki iliyopita, na kwamba jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.

DK. Mabimbi ameongeza kuwa licha ya mashine hiyo kuibiwa huduma kwa wagonjwa hazijasimama kwa kuwa hospitali hiyo ilikuwa na mashine tatu za kwa ajili ya utaoji wa huduma kwa wagonjwa, pia ameongeza kuwa washatoa taarifa Wizara ya Afya, Jeshi la Polisi pamoja na Ofisi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu.
Share:

WAZIRI MKUU AIPONGEZA GGML KUAJIRI WATANZANIA 5,000


Mshauri wa matibabu wa GGML Michael Mgonea (kulia) akionyesha jinsi ya kufanya ufufuaji wa moyo na mishipa katika maonyesho ya nne ya teknolojia ya madini yanayoendelea kwenye uwanja wa EPZA katika mji wa Geita.
**
Na Mwandishi wetu 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameipongeza Kampuni ya Uchimbaji Dhahabu Geita (GGML) kwa kutoa ajira zaidi ya 5000 kwa Watanzania huku asilimia zaidi ya 83 ya uongozi wa kampuni hiyo wakiwa ni Watanzania.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana tarehe 22 Septemba 2021 mkoani Geita wakati akizindua maonesho maonesho ya nne ya teknolojia za uchimbaji madini mkoani Geita.

Amesema licha ya GGML kushirikiana na Serikali na kutoa ajira za kutosha kwa Watanzania wengi, bado kumekuwapo na baadhi ya Watanzania ambao sio waamini jambo ambalo linatakiwa kushughulikiwa.

Kutokana na hali hiyo, amewaagiza maofisa madini mkoani humo, kushughulikia wafanyakazi wote ambao si waadilifu.

Aidha, ametoa wito kwa Watanzania kuchangamkia fursa katika maeneo ambayo madini mbalimbali yanagundulika ili kujikwamua kiuchumi.

Alisema Tanzania ni nchi yenye madini mengi mbali na dhahabu ambayo inachimbwa maeneo mengi.

“Huko Ulanga- Morogoro tumegundua graphite zaidi ya tani milioni 152 inatarajiwa kwa miaka 35, Kyerwa- Kagera tuna madini ya bati (Tin) ya kutosha zaidi ya tani bilioni nne zitachimbwa zaidi ya miaka 70 . Madini hayo ya bati yamepanda thamani kubwa baada ya wizara kusimamia, kg 1 ilikuwa inauzwa 6000, sasa ni 34,000 kwa kilo.

“Nimewaambia wanakerwa, Bukoba wajipange… pesa ipo Tanzania bado ni tajiri. Nitoe rai kwa vijana kuchangamkia fursa zilizopo katika maeneo yenye miradi ya madini,” alisema.

Aidha, akizungumza katika maonesho hayo, Makamu wa Rais wa GGML, Simon Shayo alisema mbali na ulipaji wa mapato ya Serikali na uwekezaji kwenye jamii, Kampuni hiyo imetoa ajira kwa Watanzania zaidi ya 5,000 ikiwa ni pamoja na wale wanaofanya kazi chini ya wakandarasi wetu.

Alisema hadi kufikia sasa takriban asilimia 98 ya wafanyakazi wa GGML na asilimia 83 ya menejimenti ni Watanzania.

"Tunafurahi pia kuona kuwa uwepo wetu mkoani Geita na Tanzania kwa ujumla umekuwa na tija kubwa kwa maendeleo.

“Lengo letu ni kuendelea kuwa mdau mwaminifu wa maendeleo kwa Tanzania na watu wake kwa miaka yote ambayo tutakuwa hapa, ikiwa ni pamoja na kuwa sehemu ya mustakabali wa kujenga uchumi wa viwanda na kufikia dira ya 2025 ambapo sekta ya madini imelengwa kuchangia walao 10% ya pato ghafi la taifa,” alisema

Hata hivyo, alisema kampuni hiyo imedhamini maonesho hayo mfululizo kwa muda wa miaka minne tangu yaanzishwe kwa kuwa yamekuwa na tija kubwa kwa Watanzania.

“Tunafurahi pia kuona eneo hili tulipo, tumeshirikiana na Halmashauri ya Geita Mji kuwekeza kiasi cha Shilingi Milioni 800 katika kuendeleza eneo hili la viwanja vya Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji na Mauzo Nje ya Nchi (EPZA) lenye ekari zaidi ya 200 ambalo litakuwa kitovu cha uwekezaji na biashara Mkoani Geita,” alisema.

Shayo alisema GGML inafarijika kutokana na ushirikiano wa kutosha wanaoupata kutoka Serikalini katika kutekeleza kwa vitendo sheria mpya ya madini ambayo imewapa mwongozo mzuri wa ulipaji kodi, mrabaha na matumizi mazuri ya fedha za wajibu wa kampuni kwa jamii sanjari.

“Pia naipongeza sana Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluh Hassan kwa namna ambavyo inaendelea kukuza mazingira ya uwekezaji nchini.

“Ndani ya muda mfupi tumeshuhudia dhamira yake ya dhati ya kukutana na sekta binafsi pamoja na wadau wa sekta ya madini ili kuangalia changamoto zinazokabili sekta zao na kwa kweli tunafurahi kuona mwanga mzuri zaidi katika sekta ya madini nchini Tanzania,” alisema.

Alisema kwa kipindi cha miaka minne mfululizo GGML imekuwa mdau mkubwa wa maendeleo kwani kwa kushirikiana na Serikali mkoani Geita imetekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kupitia fedha za wajibu wa Kampuni kwa Jamii (CSR) zenye gharama zaidi ya Shilingi bilioni 40.
Share:

WAANDISHI WA HABARI WAPATA AJALI GEITA


Waandishi wa habari mkoani Geita, Consolata Evarist wa Global TV, Esther Sumira wa Azam TV na Muta Robert wa Majira, wamenusurika kifo katika ajali baada ya gari aina ya Pajero Mitsubish waliyokuwa wanatumia kuacha njia na kuanguka.

Consolata na wenzake walikuwa wanaelekea Wilaya ya Nyang’hwale mkoani Geita kutafuta habari ambapo walipata ajali hiyo wakiwa hawajafika safari yao.

Hata hivyo waandishi hao wa habari wamesema wanamshukuru Mungu kwani licha ya gari walioyokuwa wakitumia kuanguka lakini wao wametoka salama zaidi wamepata maumivu madogo madogo na baada ya kutoka salama, taratibu za kipolisi zimefanyika na wao kuweza kuendelea na majukumu yao ya kazi.
Share:

WANANCHI MAENEO LINAPOPITA BOMBA LA MAFUTA TANZANIA KULIPWA FIDIA YA SH. BILIONI 25

Afisa Mazingira Mwandamizi kutoka shirika la maendeleo ya Petrol Nchini Anamaria Simoni 

Na Mwamvita Issa na Neema Sawaka - Kahama

MRADI mkubwa wa Bomba la Mafuta ghafi (EACOP) kutoka Nchini Uganda kwenda Tanga unatazamiwa kuwalipa wananchi walio karibu na mradi unapopita kiasi cha shilingi bilioni 25 kama fidia ya maeneo yao kupisha ujenzi wake.

Mradi huo ambao utapita katika mikoa nane iliyopo Tanzania , Wilaya 24, Kata 134 ambapo utandazaji wa mabomba yake unatazamiwa kuwa wa kilometa 1443 kutoka nchini Uganda hadi Mkoani Tanga Nchini Tanzania.

Hayo yalisemwa jana na Afisa Mazingira Mwandamizi kutoka shirika la maendeleo ya Petrol Nchini Anamaria Simoni wakati akiongea na Wafanyabiashara wa Wilaya ya Kahama juu ya fursa ambazo zitakuwa rafiki kwao wakati ujenzi wa mradi huo uifanyika.

Simoni alisema kuwa katika Wilaya ya Kahama ambapo Bomba hilo litapita kwa umbali wa kilometa 54, Wafanyabiashara wanaweza kupata fursa ya kuangalia mazingira mazuri ya kufanya shughuli za kiujasilimali katika eneo husika.

Alisema kuwa bomba hilo lina uwezo wa kusafirisha jumla ya mapipa 216,000 kwa siku huku ujenzi wake ukigharimu kiasi cha dola za kimarekani bilioni 3.5 sawa na trilioni nane fedha za kitanzania.

Akizungumzika kuhusu EACOP, Simon ambaye ndiye mkandarasi Mkuu,alisema kuwa Kampuni hiyo inaundwa na makampuni manne ambayo yenye hisa ambayo ni Shirika la Maendeleo ya Petrol Nchini (TPDC) yenye asilimia 15, Kampuni ya Total kutoka Nchini ufaransa asilimia 65, UNOC asilimia 15 pamoja na Kampuni ya CNOOC yenye asilimia 8.

Aidha alisema kuwa katika kuelekea ujenzi wa mradi huo hatua iliyopo kwa sasa ni ile ya uchukuaji wa ardhi kutoka kwa wananchi huku akiongeza kuwa Bomba hilo litafanya kazi kwa muda wa miaka 25na jumla ya wananchi 607 watalipwa fidia katika kata nane zilizopo katika Wilaya ya Kahama.

Kwa upande wake Mhandisi kutoka katika mamlaka ya udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) kutoka makao makuu Dodoma Nyaso Makwaya alisema kuwa kwa sasa ni bora kwa wamiliki wa makampuni ya wazawa kusajili kampuni zao ili waweze kupata fursa ya kufanya biashara na mradi huo.

Alisema kuwa hadi kufikia mwezi agust 31 mwaka 2021 jumla ya makampuni 852 yaliweza kusajiliwa na mamlaka hiyo na kuongeza kuwa katika makampuni ya mafuta wameayaambia kutumia bidhaa zinazotoka hapa hapa nchini.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kaham a Festo Kiswaga alisema kuwa wafanyabiashara walipo katika Wilaya ya Kahama wanapoitwa katika vikao vinavyohusu fursa ni bora wakajitokeza kwa lengo la kupata maarifa na kuongeza kuwa mradi huo ni mkubwa na utawanufaisha.

Aliwataka wafanyabiashara kuungana ili waweze kuupokea mradi huo na kufanya kazi naoi li kuongeza mitaji yao na kuongeza kuwa muda umefika sasa kukaa chini na kuona jinsi gani ya wao wataweza kukidhi vigezo na kupata fursa hiyo.
Share:

Office Assistant at Americares

POSITION DESCRIPTION TITLE:  Office Assistant   DEPARTMENT:            Operations REPORTS TO:               HR & Logistics Office ASSIGNMENT TYPE: Full -time LOCATION:                  Mwanza, Tanzania LENGTH: 24-months with possibility to extend based on performance and budget ABOUT AMERICARES: Americares is a health-focused relief […]

This post Office Assistant at Americares has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

MGANGA MAARUFU WA JADI NG'WANA NDALO ALIYEOA WAKE 21 AZIKWA NYUMBANI KWAKE MWAKATA KAHAMA


Machimu Mshono Ndalo maarufu Ng'wana Ndalo enzi za uhai wake

Na Suzy Luhende, Shinyanga
Mazishi ya Mwili wa Mganga Maarufu wa kutoa tiba asili Machimu Mshono Ndalo almaarufu Ng'wanandalo  aliyefariki dunia Septemba 20,2021 yamefanyika  nyumbani kwake katika kata ya Mwakata wilayani Kahama mkoani Shinyanga  Septemba 22,2021.

Marehemu Ng'wanandalo alianza kuugua tangu mwaka 2017 ambapo alikuwa akisumbuliwa na kansa ya kibofu cha mkojo kwa muda mrefu, hivyo akitibiwa na kupata nafuu lakini ilipofika tarehe 20/9/2021 majira ya saa sita usiku alifariki dunia.

Ng'wanandalo alizaliwa mwaka 1955 na alisoma shule ya msingi Imalilo mwaka 1967, alikuwa mkulima, mfugaji, mfanyabiashara na alikuwa ni Mganga wa kutoa huduma ya tiba asili na katika uhai wake alifanikiwa kuoa wake 21 ameacha wake 4 na ameacha watoto 56 wajukuu 73 na vitukuu saba.

Katibu wa Wazazi CCM mkoa wa Shinyanga Masanja Salu amesema Mwanandalo alijiunga katika Chama Cha Mapinduzi mwaka 1977/5/2, amekuwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu katika Jumuia ya Wazazi CCM Taifa na alikuwa Kiongozi mzuri wa kujitolea hivyo wameondokewa na Kiongozi Mahiri Mungu ampumzishe kwa amani.

Kwa upande wake Shemeji wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Mama Tumaini alisema kwa sababu shemeji yake alikuwa na roho nzuri na akioa katika familia anamhudumia mke pamoja na familia ya mke wake aliwaomba wanawake walioachwa wasiolewe wamuenzi Ng'wanandalo.

Baadhi ya wananchi waliohudhuria mazishi hayo Monika George na Kwangu Maige walisema marehemu alikuwa ni mtu wa kusaidia kwa yeyote atakayekuwa na shida alikuwa akimsaidia hivyo wameachiwa pengo kubwa sana.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Msalala Idd Kasim alisema wameondokewa na mtu muhimu sana katika chama kwani alikuwa ni mshauri mzuri Mungu ampokee huko aliko, kwani Mungu amempenda zaidi
Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi wakitoka kumzika Mwanandalo 
Share:

Program Development Advisor, Great Lakes at International Rescue Committee

Requisition ID: req20268   Job Title: Program Development Advisor, Great Lakes Employment Category: Permanent Employment Type: Full-Time with up to 20% International Travel Location: Nairobi, Kenya Background Over the past 80 years, the International Rescue Committee (IRC) has developed unparalleled expertise in responding to emergencies and helping uprooted communities to rebuild. Founded in 1933 at the request of Albert […]

This post Program Development Advisor, Great Lakes at International Rescue Committee has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Accountant Assistant at Tetra Tech International

The Tanzania Maji na Usafi wa Mazingira (MUM) Activity funded by USAID/Tanzania and implemented by Tetra Tech International Development (https://ift.tt/1JGwAiR) is currently accepting expressions of interest for qualified candidates to fill various positions. The purpose of Maji na Usafi wa Mazingira (MUM) Activity is to expand and sustain the provision and governance of WASH services […]

This post Accountant Assistant at Tetra Tech International has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

8 Job Opportunities at Tetra Tech International

The Tanzania Maji na Usafi wa Mazingira (MUM) Activity funded by USAID/Tanzania and implemented by Tetra Tech International Development (https://ift.tt/1JGwAiR) is currently accepting expressions of interest for qualified candidates to fill various positions. The purpose of Maji na Usafi wa Mazingira (MUM) Activity is to expand and sustain the provision and governance of WASH services by […]

This post 8 Job Opportunities at Tetra Tech International has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Senior Manager of Integrated Design Team (Location: Remote/Global) at Compassion International

PLEASE NOTE: The hiring range applies to US-based employment and may be higher in certain US geographic locations.   This  senior manager leads the Integrated Design Team who will utilize design thinking to ensure that Compassion’s cross-cutting commitments to age-appropriate child and youth development, environmental sustainability, gender and disability inclusion are embedded throughout all the Program […]

This post Senior Manager of Integrated Design Team (Location: Remote/Global) at Compassion International has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Senior Manager of Disaster Resilience Advisory Team (Location: Remote/Global) at Compassion International

PLEASE NOTE: The hiring range applies to US-based employment and may be higher in certain US geographic locations.   This senior manager leads the Disaster Resilience Advisory Team supporting National Offices to build Frontline Church Partners’ resilience capacity through increasing their ability to anticipate, plan and reduce their risk, as well as support effective disaster response […]

This post Senior Manager of Disaster Resilience Advisory Team (Location: Remote/Global) at Compassion International has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Health Information Systems Analyst at University of California San Francisco

JOB OPPORTUNITY – HEALTH INFORMATION SYSTEMS ANALYST   Location                                 Dar es Salaam Application deadline             September 27, 2021 Start date                              November 1,2021 […]

This post Health Information Systems Analyst at University of California San Francisco has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger