Friday, 17 September 2021

Regional Community Program Coordinator at THPS

ADVERTISEMENT FOR JOB VACANCIES   Tanzania Health Promotion Support (THPS) is an indigenous NGO established under nongovernmental organization act No 24 of 2002 in 2011. THPS works in partnership with the Ministries of Health Community Development Gender Elderly and Children (MoHCDGEC) Regional Administration and Local Governments (PORALG), Ministry of Home Affairs (MoHA) and Ministry of […]

This post Regional Community Program Coordinator at THPS has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Regional VMMC Program Coordinator at THPS

ADVERTISEMENT FOR JOB VACANCIES   Tanzania Health Promotion Support (THPS) is an indigenous NGO established under nongovernmental organization act No 24 of 2002 in 2011. THPS works in partnership with the Ministries of Health Community Development Gender Elderly and Children (MoHCDGEC) Regional Administration and Local Governments (PORALG), Ministry of Home Affairs (MoHA) and Ministry of […]

This post Regional VMMC Program Coordinator at THPS has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Regional Program Manager – Shinyanga at THPS

ADVERTISEMENT FOR JOB VACANCIES   Tanzania Health Promotion Support (THPS) is an indigenous NGO established under nongovernmental organization act No 24 of 2002 in 2011. THPS works in partnership with the Ministries of Health Community Development Gender Elderly and Children (MoHCDGEC) Regional Administration and Local Governments (PORALG), Ministry of Home Affairs (MoHA) and Ministry of […]

This post Regional Program Manager – Shinyanga at THPS has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

MREMBO ATEMBEA MTAANI DAR NA BANGO LA 'NATAFUTA MUME'


Picha ya Baby Nai akiwa na bango lake la kutafuta mume mtaani

Mrembo Baby Nai kutoka Buza Temeke amesema anatufuta mume wa maisha wa kumuoa mwenye miaka 20 hadi 70 na kigezo chake anataka awe mstaarabu na mcha Mungu.

Baby Nai ameongeza kusema hii ni siku ya tano kutembea na bango la kutafuta mume mtaani pia haoni shida ya kutembea na bango hilo kwa sababu havunji sheria za nchi.

Mwisho amemaliza kusema akikosa mume anayemtaka Dar es Salaam ataenda Arusha, Mwanza na Mbeya na akikosa hapo ataenda nchini Kenya na Uganda.

Chanzo - EATV
Share:

WADAU WA UKAGUZI WAKUTANA SINGIDA KUJADILI NAMNA BORA KUEPUKA HATI CHAFU,ZENYE MASHAKA

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI Profesa Riziki Shemdoe (katikati waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na wataalamu na wadau mbalimbali wa Fedha na Ukaguzi muda mfupi baada ya kufungua kikao kazi cha kujadili matokeo ya Ukaguzi wa Hesabu za Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa Mwaka wa Fedha 2019/20.

Naibu Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Divisheni ya Serikali za Mitaa Benjamin Mashauri akizungumza kwenye kikao hicho. 

Kikao kikiendelea.

 Kikao kikiendelea.


Na Godwin Myovela, Singida.


WATAALAMU mbalimbali wa Fedha wamekutana mkoani hapa kutafuta mwarobaini wa namna ya kurekebisha na ikiwezekana kuondoa kabisa dosari zilizopelekea baadhi ya Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini kupata hati chafu na zile za mashaka- kulingana na Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka wa Fedha 2019/20.

Imeelezwa pamoja na mambo mengine, lengo la kikao hicho ni kukubaliana na kuweka mikakati ya pamoja itakayosaidia wakaguzi na wakaguliwa kutekeleza wajibu wa kisheria kwa namna ambayo itaongeza tija na kuboresha utendaji.

Akizungumza wakati akifungua kikao kazi hicho, Katibu Mkuu TAMISEMI Profesa Riziki Shemdoe alisema matokeo ya ukaguzi huo hayakuwa ya kuridhisha kutokana na mwenendo usioridhisha wa Hati za Ukaguzi zilizopatikana ikilinganishwa na mwaka wa fedha uliotangulia wa 2018/19.

"Kumekuwa na poromoko la halmashauri kupata hati safi na hii haikubaliki. Haiwezekani  kuwe na poromoko la hati safi kutoka halmashauri 176 mwaka 2018/19 hadi halmashauri 124 mwaka 2019/20...nahitaji kikao hiki kije na mkakati madhubuti na maazimio yatakayosaidia kuleta maboresho stahiki," alisema.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, halmashauri zilizopata Hati Zenye Shaka ziliongezeka kutoka 9 mwaka 2018/19 hadi halmashauri 53 mwaka 2019/20,  huku 8 zikijikuta zinapata Hati Chafu.

Alisisitiza kwa kuzitaka Mamlaka za Serikali za Mitaa kupitia Waweka Hazina na Maafisa Masuuli kuwa makini katika kipindi hiki wanapokwenda kufunga vitabu, kwa kuhakikisha zinajiepusha na aina yoyote ya ubadhirifu na matumizi yasiyofaa ya fedha za umma ili kuepuka hati chafu na zile zenye mashaka.

"Ni matumaini yangu baada ya kikao hiki ambacho namuona mwakilishi wa Ofisi ya CAG, Mhasibu Mkuu wa Serikali, Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Maafisa Masuuli na wadau wengine mliopo tuhakikishe tunajadili kwa kina changamoto zote zilizojitokeza na kuhakikisha hazijirudii," alisema.

Aidha, Prof. Shemdoe alisisitiza baada ya kikao hicho kilichofadhiliwa na USAID kupitia Mradi wa PS3+, Ofisi ya Rais-TAMISEMI itakuwa tayari kutekeleza makubaliano yatakayofikiwa na kuratibu utekelezaji wa yale yote yatakayopaswa kutekelezwa na Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa katika muktadha wa maboresho ya huduma bora kwa wananchi.

Kwa upande wake, Naibu Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Divisheni ya Serikali za Mitaa, Benjamin Mashauri, alibainisha sababu kubwa ya ongezeko la hati chafu na zile zenye mashaka kuwa kubwa ni changamoto kwenye eneo la uandaaji wa Hesabu.

Pia Mashauri alisema eneo lingine linalopelekea hali hiyo ni kwenye mapato ambayo pamoja na mambo mengine, mapato mengine hukusanywa lakini hayapelekwi benki wala kwenye mifumo stahiki.

Aliongeza kuwa changamoto nyingine ni kwamba taarifa za kwenye vitabu haziendani na taarifa halisi za mapato yanayokusanywa. Hali inayopelekea kiasi kikubwa cha matumizi ya  Fedha za Umma kujikuta zikifanyiwa matumizi bila ya kuwa na viambatanisho stahiki.

"Vilevile kuna masuala ya changamoto za matumizi ya mifumo ya kisasa katika uandaaji wa hesabu kulingana na Kanuni za Mfumo wa Kimataifa za uandaaji wa Hesabu za Taasisi za Umma.., huko nyuma tulikuwa na mfumo wa Epicor sasa ni Muce, hivi vyote visipozingatiwa hupelekea pmatokeo ya uzalishaji huu wa hati chafu na zenye mashaka," alisema Mashauri.

Share:

WANAMUZIKI DAR WAFANYA MATENDO YA HURUMA SHULE YA SEKONDARI JANGWANI

Baadhi ya Wanamuziki kupitia Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO) wakiwa na Wanafunzi wa Sekondari ya Wasichana ya Jangwani jijini Dar es Salaam jana  ikiwa ni Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Muziki Duniani ambayo kitaifa kwa mara ya kwanza yataadhimishwa  Jijini Arusha Uwanja wa Sheikh Amri Abeid kuanzia  Septemba 24 hadi OKtoba 1 ambapo ndio itakuwa kilele chake.
Wanafunzi wa Sekondari ya Wasichana ya Jangwani wakiwa shuleni hapo walipotembelewa na wanamziki hao jana.
Wanafunzi wa Sekondari ya Wasichana ya Jangwani wakiwa katika picha ya pamoja na wanamziki hao
Baadhi ya Wanamuziki kupitia Umoja wa Wanamuzi Tanzania (TAMUFO) wakipata maelezo walipotembelea Makumbusho ya Taifa ya Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya picha zilizomo Makumbusho ya Taifa ya Jijini Dar es Salaam.


Na Dotto Mwaibale 


WANAMUZIKI mbalimbali kupitia Umoja wa Wanamuzi Tanzania (TAMUFO) jana Wamefanya ziara ya matendo ya huruma na Kuhamasisha shughuli za maendeleo  ya jamii ikiwa ni Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Muziki Duniani ambayo kitaifa kwa mara ya kwanza yataadhimishwa  Jijini Arusha Uwanja wa Sheikh Amri Abeid kuanzia  Septemba 24 hadi OKtoba 1 ambapo ndio itakuwa kilele chake.

Akizungumzia ziara hiyo Katibu Mkuu wa TAMUFO Stella Joel alisema katika ziara hiyo wanamuziki hao  walitembelea Shule ya Sekondari ya Jangwani ya  jijini Dar es Slaam ambapo waliweza kujumuika na kutoa zawadi kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum na baada ya hapo waliendelea na ziara hiyo ya uhamasishaji wa maendeleo kwenda maeneo mengine yakiwemo Makumbusho ya Taifa ya Jijini Dar es Salaam.

Joel alitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi na wanamuziki wote kushiriki maadhimisho hayo kwa kujitokeza kwa wingi siku hizo za maadhimisho hayo kuelekea Oktoba 1, 2021 ambayo itakuwa ni kilele chake ambapo kutakuwa na mambo mengi na burudani kubwa ya muziki kutoka  kada tofauti ya wanamuziki wakiwepo wa Bongo Fleva, Dansi, Zuku, Injili, ngoma za asili na mingine mingi.

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA SEPTEMBA 17,2021




























Share:

MKUTANO WA 18 WA BARAZA LA MAWAZIRI WA MAZINGIRA NCHI ZA AFRIKA 'AMCEN' WAFANYIKA

Share:

BENKI YA EQUITY YAZINDUA HUDUMA YA MIAMALA YA FEDHA ZA KIGENI KUPITIA EazzyFX


  Benki ya Equity leo hii imezindua huduma yake mpya ya EazzyFX itakayomuwezesha mteja kununua na kuuza fedha za kigeni kwa njia ya mtandao pasipo kufika benki au vituo vya kubadilisha fedha.

 Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi rasmi wa huduma hiyo, jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa benki ya Equity Robert Kiboti amesema kuwa huduma hiyo itarahisha huduma ya 'Forex' na itaondoa ulazima wa wateja kufika benki kila watakapo badilisha fedha za kigeni.

Aidha, mkuu wa kitengo cha hazina Raymond Njuu amesema kuwa huduma hiyo ni rahisi, salama na itapunguza muda ambao wateja walikuwa wanatumia kuwasiliana na benki, au kwa kutumia barua pepe au kwa njia ya ana kwa ana.

Pia, Njuu amesema kuwa sasa huduma za kibenki zime hararishwa kutoka benki kuwa sehemu ambayo mteja anakwenda kwenye huduma ambayo mtu anaweza kuipata popote pale alipo na kuongeza kuwa mteja atatakiwa kuingia ndani ya tovuti ya EazzyFX mtandaoni na ataweza kufurahia huduma hio katika siku 5 za kazi kila wiki kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 11 jioni. 

Aidha, watumiaji wa huduma hiyo wataweza kufanya miamala ya fedha hizo za kigeni kwa kuangalia viwango vya kubadilisha fedha duniani na hii itarahisisha mambo mbalimbali kama vile manunuzi ya bidhaa kutoka nchi za kigeni, ulipaji wa bili na huduma zingine.

 Benki ya Equity inakuwa benki ya kwanza kutoka nchini Tanzania kuleta huduma hii ya miamala ya fedha za kigeni kwa njia ya mtandao na kuwaasa wateja kuchangamkia fursa hio kwani ni rahisi na ni ya haraka zaidi.
 
Share:

Thursday, 16 September 2021

WANAFUNZI WAMTEMBEZEA KICHAPO MWALIMU WAO



Wanafunzi watatu wa kidato cha nne katika shule ya upili/sekondari ya St John Sikinwa kaunti ya Trans Nzoia nchini Kenya wamemvamia na kumpiga mwalimu wao wa Hisabati nyumbani kwake. 

Nicholas Bett ambaye ni mwalimu wa taasisi hiyo iliyoko eneo la Saboti alishambuliwa nyumbani kwake na wanafunzi hao majira ya saa moja unusu alasiri.

Walivamia makazi yake ambayo yapo mkabala na bweni la shule hiyo kulingana na ripoti ya TV 47. 

Waliripotiwa kumpiga Bett kwa kifaa butu shingoni na baada ya hapo, wakaanza kumyeshea ngumi na mateke wakati walipomzidi nguvu.

 Waliripotiwa kumpiga Bett kwa kifaa butu shingoni na baada ya hapo, wakaanza kumnyeshea ngumi na mateke wakati walipomzidi nguvu. 
Inaarifiwa kwamba mzozo uliibuka wakati wanafunzi hao walikuwa wakilipiza kisasi kwa kumshambulia mwalimu huyo ambaye aliwasisitizia ni sharti wapendezwe na masomo yake. 

Walimu wengine wawili ambao wanaishi katika kiwanja kimoja na mwathiriwa walifanikiwa kutoroka jaribu hilo bila kujeruhiwa. 

John Naibei na Michael Odhiambo walitoroka baada ya majirani kupiga kamsa na kuwalazimu wanafunzi hao kuhepa. 

Naibei na Odhiambo walipiga ripoti katika Kituo cha Polisi cha Gituamba wakishinikiza kukamatwa kwa wanafunzi hao watoro. Wanataka pia wanafunzi hao washtakiwe kortini.

Katibu Mkuu wa Muungano wa Walimu wa Shule za Msingi (KUPPET) tawi la Trans-Nzoia Furaha Lusweti alitoa wito kwa Tume ya Kuajiri Walimu kuwahamisha walimu hao watatu.

 Wanafunzi hao watatu wangali mafichoni na tangu Jumatatu hawajaonekana shuleni. 

Tangu mwaka wa 2021 kuanza, kumekuwa na ongezeko la mizozo ya walimu na wanafunzi huku kisa hiki kikiongezea tu katika takwimu hizo.
Share:

RAIS SAMIA AMTEUA DKT. YAMUNGU KUWA MWENYEKITI BODI YA NDC, KATUNZI MWENYEKITI TEWW



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi wafuatao:-

(1) Amemteua Dkt. Yamungu Kayandabila kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC). Dkt. Kayandabila ni Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

(2) Mhe. Rais Samia amemteua Dkt. Naomi Bakunzi Katunzi kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) kwa kipindi kingine cha miaka mitatu (3).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu,Jaffar Haniu uteuzi huu umeanza tarehe 14 Septemba, 2021.
Share:

PROF. JAMES MDOE AKUMBUSHA WANAFUNZI KUSOMA KWA MALENGO


Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof. James Mdoe, akivishwa Skafu na vijana wa Shule ya Sekondari Kihesa baada ya kuwasili shuleni hapo kwa ajili ya kukagua mradi wa kukuza ujuzi wa matumizi ya Kompyuta kwa wanafunzi wa shule za Sekondari mkoani Iringa unaoendeshwa na Shirika la Global - Outreach Tanzania la mjini Iringa kupitia ufadhili wa Mfuko wa Kukuza Ujuzi (SDF) unaosimamiwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA).


Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof. James Mdoe katika picha ya pamoja na maafisa wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) na wale wa Global - Outreach Tanzania alipotembelea ofisi za Shirika hilo la mjini Iringa. Shirika hilo linaendesha mradi wa kukuza ujuzi wa matumizi ya Kompyuta kwa wanafunzi wa shule za Sekondari mkoani Iringa kwa ufadhili wa Mfuko wa Kukuza Ujuzi (SDF) unaosimamiwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA).


Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof. James Mdoe akiwa katika chumba cha Kompyuta katika Shule ya Sekondari Ihesa mkoani Iringa ambayo ni miongoni mwa shule sita zilizonufaika na mradi wa kukuza ujuzi wa matumizi ya Kompyuta kwa wanafunzi wa shule za Sekodari mkoani Iringa kupitia ufadhili wa Mfuko wa Kukuza Ujuzi (SDF) unaosimamiwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania(TEA).

Wanafunzi wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari Kihesa mkoani Iringa wakimskiliza Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof. James Mdoe alipotembelea shule hiyo kwa ajili ya kukagua mradi wa kukuza ujuzi wa matumizi ya Kompyuta kwa wanafunzi wa shule za Sekondari mkoani Iringa kwa ufadhili wa Mfuko wa Kukuza Ujuzi (SDF) unaosimamiwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA).


Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari Kihesa mkoani Iringa wakiwa katika chumba cha Kompyuta ambacho ni sehemu ya mradi wa kukuza ujuzi wa matumizi ya Kompyuta kwa wanafunzi wa Sekondari mkoani Iringa unaoendeshwa na Shirika la Global- Outreach Tanzania kupitia ufadhili wa Mfuko wa Kukuza Ujuzi (SDF) unaosimamiwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania(TEA).



*********************************

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof. James Mdoe amekumbusha wanafunzi walioko mashuleni kusoma kwa malengo na kuyafanyia kazi kwa bidii na nidhamu ili kufanikisha ndoto zao za kitaaluma badala ya kusoma kwa mazoea.

Akizungumza na wanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya Sekondari Kihesa, mkoani Iringa, Prof. Mdoe amesisitiza kuwa mafanikio ya wanafunzi yatatokana na wao kujua wanataka nini katika maisha pamoja na kuweka bidii ya kufanikisha malengo hayo. Ametoa mfano kwa wale wanaotaka kuwa Madaktari au Wahandisi lazima wafanye vizuri katika masomo ya Sayansi.

Ametumia fursa hiyo kuwahimiza wanafunzi hao kuwa na mawazo ya kijasiriamali yatawawezesha kujiajiri badala ya kutegemea kuajiriwa pindi wanapohitimu masomo “hata kama unataka uingie mtaani lazima ujue unaenda kufanya nini” amesema Prof. Mdoe.

Naibu Katibu Mkuu huyo, amezungumza na wanafunzi hao ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kutembelea taasisi tano kati ya 81 zinazonufaika na ufadhili wa Mfuko wa Kukuza Ujuzi (SDF) unaoratibiwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA).

Shule ya Sekondari Kihesa ni miongoni mwa shule sita za Sekondari mkoani Iringa zinazonufaika na mradi wa kukuza ujuzi wa matumizi ya Kompyuta kwa wanafunzi wa shule za Sekondari mkoani Iringa unaoendeshwa na Shirika la Global Tanzania kwa ufadhili wa Mfuko wa Kukuza Ujuzi (SDF) unaosimamiwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA).

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Global Outreach Tanzania, Maryline Mamuya ameishukuru Serikali kwa kutoa ufadhili kupitia Mfuko wa SDF ambao unaowezesha shule sita za sekondari mkoani Iringa kupata elimu ya matumizi ya Kompyuta ambayo ni muhimu katika zama hizi za kidijitali.

Aidha Naibu Katibu Mkuu ametembelea na kuzungumza na wanufaika wa mradi wa kukuza ujuzi katika usindikaji wa mazao na stadi za ujasiriamali, unaoendeshwa na Shirika la Kuendeleza Viwanda Vidogo Nchini (SIDO) mkoani Singida ambao pia umefadhiliwa na Mfuko wa Kukuza Ujuzi.

Akiwa SIDO amekutana na kuzungumza na wanufaika wa mafunzo hayo pamoja na kujionea bidhaa zinazotengenezwa na wanufaika hao ambao baadhi yao wamefanikiwa kupata usajiri wa nembo ya ubora wa TBS baada ya kupata mafunzo hayo yaliyofadhiliwa na SDF

Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (SDF) ni Mfuko unaolenga kuwezesha Taasisi zinazotoa mafunzo kuongeza ubora na ufanisi katika kutoa mafunzo ya ujuzi na stadi za kazi katika sekta sita za kipaumbele nchini ambazo ni Kilimo - Uchumi, Utalii na Huduma za Ukarimu, Uchukuzi, Ujenzi, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) na Nishati.

Taasisi 81 zimenufaika na awamu ya pili ya Mfuko wa SDF ambapo kiasi cha Shilingi Bilioni 9.7 zinatumika katika ufadhili huo. Mamlaka ya Elimu Tanzania imepewa jukumu na kuratibu utekelezaji wa Mfuko huo.
Share:

RUGEMALIRA AFUTIWA MASHTAKA...AACHIWA HURU


Mfanyabiashara James Rugemalira akiwa na familia yake nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo Septemba 16,2021.
***
Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) amefuta mashtaka yanayomkabili Mfanyabiashara James Rugemalira na mahakama kumwachia huru.

Juni 2017, Taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa nchini Tanzania TAKUKURU iliwafikisha Mahakamani Mkurugenzi wa Kampuni ya Kufua Umeme (IPTL), Herbinder Seth na Rugemalira kwa makosa sita ya uhujumu uchumi ikiwemo kosa la kuisababishia serikali hasara.

Aidha katika shtaka jingine, Washtakiwa wote, wanadaiwa kuwa kati ya Novemba 28/29, 2011 na Januari23,2014 makao makuu ya benki ya Stanbic Kinondoni na Benki ya Mkombozi tawi St Joseph zote za Dar es salaam, kwa ulaghai, walijipatia kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BOT), USD 22,198,544.60 na shilingi 309, 461,300,158.27.

Iliendelea kudaiwa kuwa katika shtaka la kusababisha hasara, washtakiwa hao wanadaiwa kwamba mnamo Novemba 29, 2013 katika Benki ya Stanbic tawi la kati Kinondoni kwa vitendo vyao waliisababishia Serikali hasara ya USD 22, 198, 544.60 na Tsh 309,461,300,158.27.
Share:

Data Entry Administration Assistan at AUMS

Data Entry Administration Assistan   African Underground Mining Services (AUMS) is an international leader in mechanised hard rock underground mining. AUMS is part of Perenti (Formerly the Ausdrill Group), an ASX 200 company and Australia’s second largest integrated mining services provider. We are a global leader in hard rock underground mining; together with Barminco we […]

This post Data Entry Administration Assistan at AUMS has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

RC MALIMA AITAKA TOC KUSHIRIKI MASHINDANO OLIMPIKI MWAKA 2024

 

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima akisistiza jambo wakati akifungua mafunzo ya walimu wa Mchezo wa Mpira wa Magongo yaliyoanza septemba 15 Jijini Tanga kwa kushirikisha washiriki kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Visiwani yakiratibiwa na Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC)na Chama cha Mpira wa Magongo Tanzania (THA) wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) Filbert Bayi
Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) Filbert Bayi akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo
Makamu wa Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Henry Tandau akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo
Mwenyekiti wa Mchezo wa Mpira wa Magongo Tanzania Abdulrahman Syskes akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo 
Mkufunzi wa Kimataifa Maggid Muhamid Elati akieleza jambo
Mkufunzi wa Kimataifa Maggid Muhamid Elati akieleza jambo
Meza Kuu wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa mafunzo hayo
Picha ya Pamoja
Washiriki wakifuatilia mafunzo hayo

NA OSCAR ASSENGA, TANGA.

MKUU wa Mkoa wa Tanga Adam Malima ameitaka Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) kuhakikisha wanajiwekea malengo makubwa ya kuhakikisha timu ya Mpira wa Magongo inashiriki mashindano ya Olimpiki mwaka 2024 ili kutengeneza alama ya mchezo huo kama ilivyokuwa mengine.

Malima aliyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya walimuwa Mchezo wa Mpira wa Magongo  yaliyoanza septemba 15 Jijini Tanga kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Nyumbani kwa kushirikisha washiriki kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Visiwani yakiratibiwa na Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC)na Chama cha Mpira wa Magongo Tanzania (THA)

Alisema lazima watengeneze malengo ya lazima wajiwekee malengo makubwa yatakayokuwa na tija siku za usoni kwa kuhakikisha wanashiriki mashindano makubwa na wanafanya vizuri ili kuweza kuweka alama kubwa kupitia mchezo huo hapa nchini

“Ndugu zangu tuwe na malengo..Tujiwekee malengo makubwa ya kushiriki mashindano ya Olimpiki mwaka 2024 nafikria malengo ya muda mrefu na kati ni kushiriki huko na muda kufikiria ni sasa lazima mzingatie hilo na kuwa na maono ya mbali”Alisema

Alisema kwa sababu bila malengo itakuwa ni ndoto kuweza kufika huko hivyo ni lazima waweze kutengeneza alama kwenye mpira wa magogo kwani bila kufanya hivyo watakuwa wanapoteza muda lakini wakiutumia vizuri wanaweza kufika huko.

 “Lazima muanze kuota leo mpo Parisi bila malengo bila njozi tutapoteza muda mtafute kila mbinu ya kuwa walimu bora na hilo ndilo ambalo litatupa dira na mwanga mzuri wa kufikia kufikia malengo yetu ambao tunajiwekea ya kufika mbali”Alisema

Awali akizungumza wakati wa mafunzo hayo ambayo yatafanyika kwa siku 10 Jijini Tanga,Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) Filbert Bayi alisema mafunzo hayo yalikuwa yafanyike mwaka jana lakini walilamika kuhairisha.

Alisema yalihairishwa kutokana na na taratibu za baadhi ya nchi waliona bado mapema kutoka nchi zao mfano Misri kumleta Mkufunzo wa Kimataifa Maggid Muhamid Elati kutokana na Covid 19 lakini walikubali baada ya chama kuwasailina nao nao wakakubali na mafunzo yaendelee.

Alisema mchezo wa Mpira wa Magongo ni mkongwe kwa sababu hakuna chama cha mchezo ambacho kimekwisha kushiriki mashindano olimpiki na timu pekee yenye wachezaji wengi kushiki olimipiki huku akieleza tokea mwaka 1980 mchezo huo umekuwa na mafanikio makubwa.

Katibu Mkuu huyo alisema kubwa ambalo hajalijua ni mashindano ya mikoa,vilabu ni muhimu sana lakini kwanini hakuna mashindano ya mkoa au vilabu kwa sababu zamani kulikuwa na vilabu vikubwa sana na nani atayayaleta mahindano ya Taifa na vilabu.

Alisema wameendesha kozi hiyo mwaka 2012 na  wameanza kufundisha kwenye uongozi wao tokea mwaka 2005 Zanzibar na 2021 wapo Jijini Tanga  ambayo ni mafunzo ya tatu hivyo kwa idadi kubwa ya walimu waliofundishwa TOC hivyo  wanategmea vyama husika Zanzibar na Bara vinawafuatilila na kuwatumia ipasavyo ili  kuinua kueneneza mchezo huo nchi nzima

“Badala ya mikoa michache tungependa mtakaporudi nyumbani vyama viendeleze na mkahakikisha mnashirikiana kwa lengo la kuhakikisha mchezo huo unaenea na kupendwa kutokana na ujuzi ambao mtakuwa mmeupata kwenye mafunzo hayo “Alisema Katibu huyo.

Aidha alisema idadi ya washiriki ni 30 walioiweka kutokana na gharama  na bajeti yao huku akieleza kwa muda mrefu TOC ,IOC imekuwa ikifadhili mafunzo ya michezo mbalimbali ya walimu wa vyama wanachama TOC ikwemo  Chama cha Mpira wa Magogo ambapo ni kati ya vyama vya michezo ambavyo vimefaidika na ufadhili huo .

Mwisho.

Share:

Finance Officer at KNCV

KNCV Tuberculosis Foundation is looking for a fulltime Finance Officer  Duty station: Dar es Salaam, Tanzania KNCV Tuberculosis Foundation KNCV Tuberculosis Foundation (KNCV) is one of the leading international non-profit organizations dedicated to fighting tuberculosis (TB) worldwide. We are an international center of expertise for TB control that stimulates effective, efficient and sustainable tuberculosis control […]

This post Finance Officer at KNCV has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Temporary Drivers at IMA World Health

TEMPORARY DRIVERS JOB DESCRIPTION Organization profile: IMA World Health (IMA) is a member of Corus International, a consortium of organizations working together to deliver holistic, durable solutions to the interconnected challenges of poverty, poor health outcomes, and climate change. Established in 1960, IMA has a long history of successfully collaborating with governments, faith-based organizations, national […]

This post Temporary Drivers at IMA World Health has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger