Wednesday, 18 August 2021

RAIS SAMIA AWASILI ZANZIBAR AKITOKEA NCHINI MALAWI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na Rais Mstaafu wa Malawi Bi. Joyce Banda Lilongwe nchini Malawi. Rais Mstaafu Joyce Banda alifika Lilongwe kuzungumza na kumpongeza Rais Mhe. Samia kwa kuwa Rais wa kwanza Mwanamke nchini Tanzania.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiagana na Rais Mstaafu wa Malawi Bi. Joyce Banda mara baada ya mazungumzo yao yaliofanyika Lilongwe nchini Malawi leo tarehe 18 Agosti, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiondoka katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kamuzu mara baada ya kushiriki Mkutano wa 41 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliomalizika leo tarehe 18 Agosti katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Bingu uliopo Jijini Lilongwe nchini Malawi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwasili Zanzibar wakati akitokea nchini Malawi ambapo alishiriki Mkutano wa 41 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliomalizika leo tarehe 18 Agosti nchini Malawi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Phillip Mpango mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume wakati akitokea nchini Malawi leo tarehe 18 Agosti, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisalimiana na viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume wakati akitokea nchini Malawi leo tarehe 18 Agosti, 2021.

PICHA NA IKULU
Share:

WATATU WAKAMATWA WAKIJIFANYA MAOFISA WA TANESCO ARUSHA


Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha ACP Justine Masejo

Na  Abel Paul Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha
Jeshi la Polisi mkoani Arusha linawashikilia vijana watatu wenye umri kati ya miaka 20 hadi 26 wakazi wa mkoani humo kwa kosa la kuwadanganya wananchi wanaohitaji kuunganishiwa umeme kwamba wanaweza kuwapatia huduma hiyo kwa njia ya mkato kwa kuwa wao ni maofisa wa TANESCO.

Taarifa hiyo imetolewa leo Agosti 18, 2021, na Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha ACP Justine Masejo  na kusema kwamba watuhumiwa hao walikamatwa Agosti 17, 2021, katika ofisi za TANESCO zilizopo Mtaa wa Old Line, Kata ya Themi, Halmashauri ya Jiji la Arusha.

"Jeshi la Polisi Mkoani hapa lilifanikiwa kuwakamata watu watatu ambao ni Gidioni William (26) mkazi wa Sombetini, Richard Frank  (20) Mkazi wa Daraja la II, Godson Erick  (20) Mkazi wa Moshono wakijifanya watumishi wa Shirika la Umeme (Tanesco) Mkoa wa Arusha.

"Watuhumiwa hao walikamatwa mara baada ya Jeshi la Polisi kupokea taarifa toka kwa raia wema kwamba, wamekuwa wakijihusisha na wakuwadanganya wananchi ambao wanahitaji huduma za kuunganishiwa umeme kuwa wao ni Maofisa wa Shirika hilo na wana uwezo wa kuwapatia huduma wanazozihitaji kwa njia ya mkato, ndipo timu ya makachero wa Polisi wakishrikiana na maofisa wa shirika la Umeme waliweka mtego na kufanikisha kuwakamata watuhumiwa hao",amesema Kamanda.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha amesema kutokana na tuhuma hizo Jeshi la Polisi Mkoani Arusha linaendelea kuwahoji watuhumiwa ili kupata mtandao mzima unaohusika na vitendo hivyo vya kitapeli katika ofisi za shirika la umeme (Tanesco) Mkoa wa Arusha.

Ameeleza kuwa pindi upelelezi utakapokamilika jalada litapelekwa ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa hatua zaidi za kisheria.

Kamanda Masejo ametoa wito kwa wananchi kuzitumia ofisi na taasisi za umma ambazo zipo kwa ajili yao pindi wanapohitaji huduma yoyote hali hii itasadia kuwakwepa walaghai ambapo wanaweza kuwaingiza katika matatizo au hasara.

Aidha amewaomba wananchi wa mkoa wa Arusha kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha.
Share:

WADAU DODOMA WAKUTANA KUJADILI UHAMASISHAJI NA UTOAJI ELIMU YA SENSA YA WATU NA MAKAZI





Na Dotto Kwilasa, Dodoma

OFISI ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Takwimu imewakutanisha  viongozi wawakilishi wa Serikali ngazi mbalimbali,makundi ya kijamii ,Taasisi za dini,Umma ,binafsi na vyama vya siasa katika kikao cha pamoja kwa lengo la uhamasishaji na utoaji wa elimu ya sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika mwaka 2022 .

Akieleza umuhimu wa kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka amesema wameandaa kikao hicho na kuyashirikisha makundi hayo ili kurahisisha utoaji wa elimu ya sensa kwa jamii huku akisisitiza kwamba kwa kufanya hivyo zoezi hilo litafanikiwa kama inavyotarajiwa.

Kwa kutambua umuhimu wa zoezi hilo, Waziri  wa Mambo ya Ndani ya Nchi,George Simbachawene  amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi katika zoezi  la  sensa ya watu na makazi linalotarajiwa kufanyika mwakani  ili kuiwezesha Serikali kupanga maendeleo na kukuza uchumi.

Akiongea katika  kikao hicho amesema “Serikali inategemea sana zoezi hili,hatuwezi kuwa na maendeleo bila kujua idadi ya watanzania,kila mmoja kwa nafasi yake anatapaswa kuwa balozi wa uhamasishaji  ni muhimu hivyo watanzania wanatakiwa kujitokeza kwa wingi ili kuisaidia Serikali kupanga mipango ya maendeleo”.

Mbali na hayo ametumia nafasi hiyo kumshukuru Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Antony Mtaka  kwa kuona haja ya kuandaa mkutano huo huku akisisitiza kwamba sensa ni muhimu kwani inaleta ushahidi wa kisayansi na maendeleo.

Naye Spika wa Bunge na Mbunge wa Jimbo la Kongwa, Job  Ndugai amesema zoezi hilo ni muhimu kwa Taifa kwani litasaidia Nchi kupanga maendeleo hivyo watanzania wanatakiwa kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo.

“Tarehe 31 vikao vyetu vya Bunge vitaanza na vikao vilivyopita tumepitisha mambo mengi ikiwemo na tozo,safari hii itakuwa salama,hili ni jambo muhimu sana hivyo niwaombe watanzania wajitokeze kwa wingi,sisi wagogo hata zoezi la kuhesabu mifugo linakuwa na shida ni utamaduni wetu,”amesema.

Naye Kamisaa wa Sensa nchini ambaye pia ni Spika wa Bunge Mstaafu,Anne Makinda ametoa wito kwa watanzania kujitokeza katika zoezi la kuhesabiwa kwani hilo sio suala la kisiasa na kwamba  zoezi hilo watatumia tehama katika maeneo ya kuhesabiwa lengo likiwa ni kuwafikia watanzania wengi ambapo amedai watawafikia watu wengi mpaka katika maeneo ya vijijini.

Makinda amesema wamejipanga kuhakikisha zoezi hilo linafanyika kwa ufanisi  kwani kwa sasa wataaalamu wameongezeka tofauti na miaka ya nyuma.

Kutokana na hayo Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt. Albina Chuwa amesema Serikali imejipanga kikamilifu  kusimamia  zoezi la Sensa ya Watu na Makazi inayotarajiwa  kufanyika mwakani huku akitoa wito kwa watanzania kujitokeza kwa wingi wakati wa zoezi hilo.

“Sensa hii itakuwa ni ya sita itasimamiwa na Serikali ya awamu ya sita kwa weledi  mkubwa tunatarajia watahesabiwa zaidi ya watu milioni 64 kwani kila mwaka watu wanaongezeka milioni 3.1 na sensa mwisho ya mwaka 2012 tulikuwa milioni 49,”amesema.

Amesema kwa sasa wanauzoefu wa kutosha na wamejipanga kuhesabu watu mbalimbali ikiwemo watu wenye ulemavu ambapo ambapo amedai zoezi hilo lipo kwa mujibu wa sheria hivyo ni lazima watu wahesabiwe.

Kwa upande wake,Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bill Chidabwa ameiomba Ofisi  ya Taifa ya Takwimu (NBS)  kutoa elimu kwa wananchi kuhusiana na umuhimu wa kuhesabiwa katika zoezi la  sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika mwakani  ili kuiwezesha Serikali kupanga maendeleo na kukuza uchumi.

Amesema wao vijana wanaunga mkono zoezi hilo ambapo ameitaka pia NBS mara baada ya zoezi hilo kuja na majibu vijana wapo wangapi na wanatakiwa kupewa kipaumbele kwa kaisi gani.
Share:

WAZIRI MKUU MAJALIWA AKUTANA NA WAJUMBE WA KAMATI KUU WA CCM, WILAYA YA RUANGWA, MKOANI LINDI


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Akizungumza na wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ruangwa, kwenye ukumbi wa Narungombe, Mkoani Lindi, Agosti 18, 2021
Share:

MKURUGENZI MTENDAJI WA TACAIDS ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MWITIKIO WA UKIMWI MKOANI MTWARA


Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS Dkt Leonard Maboko aliyekaa katikati akitoa ufafanuzi juu ya hali ya VVU nchini kwa kaimu katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara Bw.Renatus Mongongwela aliyekaa kulia kwake na kushoto, kwake Bw.Yasin Abasi Mkurugenzi wa fedha na Utawala wa TACAIDS wakati wa ziara ya kikazi katika Mkoa wa Mtwara.

****************************

 Tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania imeridhishwa na utekelezaji wa shughuli za mwitikio wa UKIMWI zilizotekelezwa Mkoani Mtwara katika kipindi cha mwaka wa fedha 2020/2021.

Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa afua za VVU na UKIMWI mratibu wa UKIMWI mkoa wa Mtwara Bi Tabitha Kilangi amesema kwamba, kiwango cha maambukizi kimeendelea kushuka kutoka silimia 4.1 kwa utafiti wa viashiria vya UKIMWI vya mwaka 2011/12 hadi asilimia 2.0 kwa utafiti wa mwaka 2016/2017.

Ameongeza kuwa, watu wanaoishi na VVU wanafahamu hali zao za maambukizi kwa asilimia 82 na watu waliopo kwenye utaratibu wa kutumia dawa za kufubaza VVU (ARV) hadi kufikia Januari, 2021 ilikua ni asilimia 92. Watumiaji wa dawa hizo wameweza kupunguza kiwango cha VVU kwenye miili yao kwa asilimia 94.

Aidha ameainisha njia zinazotumika katika mkoa huo ni pamoja na kusisitiza upimaji wa hiari, kuendesha kampeni na ushawishi, kutoa elimu kupitia redio za kijamii, mikutano ya hadhara, vikundi vya Sanaa, vipeperushi, majarida na mabango, kutoa huduma za VVU na UKIMWI majumbani, kutoa huduma kwa watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi kama vile sare za shule ,vifaa vya shule ada ana matibabu. utoaji wa elimu kuhusu matumizi sahihi na endelevu ya kondomu na kutambua makundi maalum kama wafanyabishara ya ngono na kupanga mikakati ya kuzuia maambukizi mapya.

Aidha amesema pia serikali inashirikiana kwa karibu na wadau wa nje na wa ndani katika kupambana na maambukizi ya VVU ambapo katika mwaka 2020/2021 mkoa kwa kushirikiana na halimashuri na wadau mbalimbali uliweza kuchangia sh. 254,086,963 kwa ajili ya utekelezaji wa afua za VVU na UKIMWI.

Naye kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara Bwana Renatus Mongogwela amesema kwamba, kwa kushirikana na wadau bado kuna umuhimu wa kusisitizia matumizi sahihi na endelevu ya kondomu, ili wananchi wasione aibu kwenda dukani kununua kondomu kutokana na umuhimu wake.

“kwa sasa suala la matumizi ya kondomu bado lina unyanyapaa sana kwa kuwa mtu akikuona una nunua kondomu lazima akushangae, kumbe kwa sasa kondomu ni bidhaa kama bidhaa nyingine, kwa kuwa ni kwa faida yetu binafsi. Nawasihi watanzania tusinyanyapaane kwa kuwa kondomu inasaidia mambo mengi sana mbali na kukinga maambukizi ya VVU lakini pia inakinga mimba zisizotarajiwa na magonjwa ya ngono” amesema Mongogwela.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS Dkt Leonard Maboko ameupongeza uongozi wa mkoa huo jinsi walivyojipanga katika kupambana na maambukizi mapya ya VVU.

Amesema kama kila Mkoa utajipanga na kufanya kazi hivi basi ifikapo 2030 tutaweza kufikia malengo yatu ya Tanzania bila UKIMWI inawezekana, suala la kushirikiana na wadau ni la muhimu sana kwakuwa sasa hivi ni muhimu tujipange kutumia raslimali zetu za ndani katika mapambano ya VVU.

Dkt Maboko alitembelea Mkoa wa Mtwara kwa lengo la kufanya ufuatiliaji na Tathimini ya afua za VVU na UKIMWI zinazotekelezwa katika mkoa huo.
Share:

CHANJO YA UKIMWI YAANZA KUFANYIWA MAJARIBIO LEO



Chanjo ya Virusi vya Ukimwi (VVU) iliyokuwa inafanyiwa utafiti muda mrefu na Kampuni ya Moderna ya Marekani inatarajiwa kuanza majaribio kwa binadamu leo Jumatano, Agosti 18, 2021.

Hatua hii imekuja baada ya kampuni hiyo ambayo inatengeneza chanjo za aina mbili za Ukimwi, kufuzu hatua za awali za kimajaribio na hivyo kuanza kutumika kwa binadamu katika awamu ya tatu.

Chanjo hizo ni pamoja na mRNA-1644 na mRNA-1644v2-Core, ambazo zimeshachunguzwa na kufanyiwa majaribio ya awali na kuonekana salama kabla ya kujaribiwa kwa binadamu kwa mara ya kwanza.


Soma kwa kina habari kuhusu CHANJO YA UKIMWI katika gazeti la Mwananchi toleo la Leo Jumatano
Share:

RC SENGATI AWASILISHA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM HALMASHAURI KUU CCM MKOA WA SHINYANGA

Share:

CEO WA MALUNDE 1 BLOG ,LULEKIA WASHIRIKI KUSAMBAZA TABASAMU CRDB BANK INTERNATIONAL MARATHON 2021

Share:

CCM SINGIDA YAKAGUA MIRADI YA MAENDELEO WILAYANI MKALAMA

Share:

🔺 TAZAMA HAPA MAJINA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA AWAMU YA PILI KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO MWAKA 2021


Students selected to join form five and Technical Colleges 2021/22 academic year -Waliochaguliwa Kidato Cha Tano 2021( Second Selection)

First Selection, 2021
Second Selection, 2021

List of students selected to join Form Five (TAMISEMI) Form five Selection 2021):( Second Selection)


Wanafunzi 4,105 wamechaguliwa kujiunga kidato cha tano kwa mwaka huu katika uchaguzi wa awamu ya pili kutokana na waliochaguliwa awamu ya kwanza kutoripoti kwenye shule walizopangiwa.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Prof.Riziki Shemdoe, wakati akitangaza matokeo ya uchaguzi wa awamu ya pili mbele ya waandishi wa habari jijini Dodoma.

Prof. Shemdoe amesema kuwa kati ya wanafunzi waliochaguliwa, wanafunzi 499 (wavulana 424 na wasichana 75) wamepangiwa tahasusi za Sayansi na Hisabati na wanafunzi 3,604 wakiwemo wavulana 3,461 na wasichana 143 wamepangiwa tahasusi za masomo ya Sanaa na Biashara.

Amebainisha kuwa upangaji wa awamu ya pili umefanyika baada ya Wizara kujiridhisha na nafasi zilizo wazi katika shule ambazo wanafunzi hawakuripoti.


“ Kwa kuangalia idadi ya wasichana waliopangiwa kujiunga na kidato cha tano awamu ya pili imekuwa ndogo, hii ni kwa sababu katika uchaguzi wa awamu ya kwanza wanafunzi wote wasichana waliokuwa na vigezo walichaguliwa hivyo hapakuwa na wanafunzi wasichana waliokuwa wamebakia,”amesema Prof. Shemdoe

Amefafanua kuwa wanafunzi wasichana waliochaguliwa katika awamu ya pili ni wale ambao waliomba kubadilishiwa machaguo yao kutoka vyuo mbalimbali walivyokuwa wamechaguliwa awali na kupelekwa kidato cha tano.

“Wanafunzi waliopangwa awamu ya pili wanatakiwa kuripoti katika Shule walizopangiwa kuanzia tarehe 16 hadi 30 Agosti, 2021, hivyo mwanafunzi ambaye atashindwa kuripoti hadi tarehe 30 Agosti, 2021 atakuwa amepoteza nafasi yake,”amesisitiza Prof . Shemdoe.

Aidha, amewaomba wazazi na walezi waelewe kwamba hakutakuwa na nafasi yoyote ya wanafunzi hawa kubadilishiwa shule kwa kuwa shule walizopangwa ni zile zilizobainika kuwa na nafasi kwa tahasusi husika.
Share:

HII HAPA RATIBA YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2021 - CSEE 2021 EXAM TIMETABLE

Share:

Tuesday, 17 August 2021

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO AGOSTI 18,2021





Magazetini leo Jumatano Habari kubwa :CHANJO YA UKIMWI KUANZA NA WATU 56, ASKOFU GWAJIMA KUKAMATWA












Share:

MWANAFUNZI SEKONDARI AWAOKOA WAKULIMA ABUNI KIFAA CHA KUSAMBAZIA DAWA SHAMBANI


MWANAFUNZI wa kidato cha kwanza shule ya Sekondari ya Ufundi Ifunda ya Mkoani Iringa, Isaya William (14),akizungumza na wandishi wa habari leo Agosti 17 2021 akielezea jinsi alivyobuni Roboti ambayo itawasaidia wakulima kunyunyuzia dawa shambani.


MWANAFUNZI wa kidato cha kwanza shule ya Sekondari ya Ufundi Ifunda ya Mkoani Iringa, Isaya William (14),akiwaonyesha vifaa vilivyotumika kubuni Roboti ambayo itawasaidia wakulima kunyunyuzia dawa shambani waandishi wa habari , waliofika shuleni hapo kujionea jinsi ambavyo Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia inavyoendelea kuwasaidia wabunifu mbalimbali,


Mwanafunzi wa Kidato cha sita, katika shule hiyo anaesomea masomo ya PCM, Oscar Mletwa,akizungumzia jinsi alivyobuni kifaa ambacho kitakuwa kikitoa taarifa kwa uongozi wa shule na Matroni mara baada ya kutokea kwa janga la moto.


Mwalimu Mkuu wa Shule ya Ufundi Ifunda, Yusuph Mwagala,akielezea mafaniko na wanavyowaendeleza wabunifu hao kwa kuwakutanisha na Taasisi mbalimbali za ubunifu pamoja na Chama cha ubunifu na Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) waandishi wa habari waliofika shuleni hapo kujionea jinsi ambavyo Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia inavyoendelea kuwasaidia wabunifu mbalimbali,


Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Ufundi Ifunda ya Mkoani Iringa wakielekea darasani


Muonekano wa majengo ya shule ya Sekondari ya Ufundi Ifunda iliyopo Mkoani Iringa iliyokarabatiwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia.

..........................................................................................

Na,Alex Sonna,Iringa

MWANAFUNZI wa kidato cha kwanza shule ya Sekondari ya Ufundi ya Ifunda ya Mkoani Iringa, Isaya William (14) amebuni Roboti ambalo litakuwa likiwasaidia wakulima kunyunyuzia dawa shambani lengo likiwa ni kumwepusha kupata magonjwa mbalimbali ikiwemo ugonjwa wa Pumu.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Agosti 17,2021, waliofika shuleni hapo kujionea jinsi ambavyo Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia inavyoendelea kuwasaidia wabunifu mbalimbali, mwanafunzi huyo amesema Roboti hilo litasaidia kusambaza dawa mashambani ili kuepuka mkulima kupata magonjwa mbalimbali.

“Nashiriki kutengeneza Project kwa kushirikiana na wenzangu ambalo litasaidia kupuliza dawa mashambani, nitatumia Roboti ambaye atasaidia kusambaza dawa katika mashamba ili kuepukana na kupata matatizo mbalimbali wakati wa kupulizia dawa,” amesema.

Amesema roboti hilo litatumia ramani ya shamba kwa kutumia Application maalum ambayo itakuwa katika simu ya mkulima.

“Application hiyo itakuwa katika simu ya mkulima ambayo atatumia ramani ya shamba na roboti atakuwa anazunguka katika shamba, itasaidia kuokoa muda ataenda shambani na kumuepusha na maradhi mbalimbali na magonjwa kama pumu.

William amesema roboti atakuwa kama kigari fulani na kutakuwa na tenki juu na kutakuwa na bomba na kwenye matairi kutakuwa na miyororo kama ya pikipiki kwa ajili ya kupita chini,”amesema.

Amesema itachukua muda wa wiki moja kukamilisha ubunifu huo ambapo amesema lengo ni kusaidia sekta ya kilimo na kuhakikisha wakulima wanafanya kilimo cha kisasa.

“Serikali ina mapenzi ya dhati kuisaidia Serikali sisi kama wabunifu tutaiendeleza sekta ya kilimo na itasaidia sana katika sekta ya kilimo na mtu asiwe anapoteza muda,”anasema.

JANGA LA MOTO LAPATIWA UFUMBUZI

Katika hatua nyingine, Mwanafunzi wa Kidato cha sita, katika shule hiyo anaesomea masomo ya PCM, Oscar Mletwa amesema amebuni kifaa mbacho kitakuwa kikitoa taarifa kwa uongozi wa shule na Matroni mara baada ya kutokea kwa janga la moto.

Amesema kwa miaka mitatu 2019, 2020 na 2021 shule nyingi zimeungua moto ambapo amedai chanzo chake ni wanafunzi kujititengenezea shoti juu ya madari.

Alipoulizwa muda aliotumia kukitengeneza kifaa hicho, mwanafunzi huyo amesema ametumia miezi sita ambapo amedai malengo yake ni kuwa Mhandisi mkubwa nchini ili kuisaidia nchi katika mambo mbalimbali.

UBUNIFU WAO WAENDELEZWA

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Ufundi Ifunda, Yusuphu Mwagala amesema shule hiyo ilianzishwa mwaka 1950 na ina mchepuo wa ufundi kwa O level na A level kwa masomo ya Sayansi ambapo amesema katika masomo ya ufundi kuna ufundi wa ujenzi, umeme na mitambo.

Amesema kwa sasa wanaendelea kuwaendeleza wabunifu hao kwa kuwakutanisha na Taasisi mbalimbali za ubunifu pamoja na Chama cha ubunifu na Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST)

Amesema mara baada ya kupata changamoto ya mabweni kuungua walipata wazo na kuwaomba wanafunzi kuwa wabunifu ili kubuni jinsi ya kukabiliana na majanga hayo.

“Ndivyo ambavyo wanafundishwa hivyo wamekuwa wabunifu tumepata changamoto ya mabweni kuungua tukapata wazo la kuwaomba wanafunzi mojawapo ni hii ya wanafunzi walifikiria namna ya kurahisisha kazi za mikono na mfumo wa kuzima taa kwa giza likiingia tu zinawaka na likiingia giza zinazima,”amesema.
Share:

TAA ZA SHINYANGA MJINI ZAZUA GUMZO. ..KITINYA AHOJI KWANINI HAZIWAKI TENA

 


Diwani wa Kizumbi Manispaa ya Shinyanga Ruben Kitinya, akihoji hatma ya matengenezo ya Taa za Barabarani Mjini Shinyanga kwenye kikao cha Baraza la Madiwani


Na Marco Maduhu,Shinyanga

DIWANI wa Kata ya Kizumbi Manispaa ya Shinyanga Reuben Kitinya, amesikitishwa na ubovu wa Taa za Barabarani Mjini Shinyanga, ambapo sasa haziwaki na kusababisha giza.

Kitinya amebainisha hayo leo Jumanne Agosti 17,2021 kwenye kikao cha kawaida cha baraza la madiwani wa Manispaa ya Shinyanga, wakati wa ajenda ya kuuliza maswali ya papo kwa papo.

Amesema Taa hizo zimewekwa hivi karibuni na zilikuwa zikiupendezesha mji wa Shinyanga lakini sasa haziwaki tena na kusababisha mji kuwa na giza.

"Nauliza ni lini Halmashauri mtazifanyia matengenezo Taa za Barabarani ili ziwake kama zamani na kuupendezesha mji wetu," aliuliza Kitinya.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga John Tesha, ambaye ni Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii, akijibu swali hilo, alisema matengenezo ya Taa hizo siyo la Halmashauri bali lipo chini ya Mkandarasi husika na.

Aidha, alisema Serikali ilishazungumza na Mkandarasi aliyeziweka Taa hizo awali, na zitafanyiwa matengenezo hivi karibuni, ambapo tayari zipo Bandarini.


Diwani wa Kizumbi Manispaa ya Shinyanga Ruben Kitinya, akihoji hatma ya matengenezo ya Taa za Barabarani Mjini humo kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.

Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga John Tesha, akijibu maswali ya Papo kwa Papo kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.

Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Ester Makune, akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.

Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao cha Baraza la madiwani.

Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao cha Baraza la madiwani.

Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao cha Baraza la madiwani.

Na Marco Maduhu- Shinyanga




Share:

WIZARA YA ELIMU,SAYANSI NA TEKNOLOJIA YAFANYA MABORESHO MAKUBWA KATIKA MAKTABA SABA NCHINI


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe,akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kuzindua Maktaba ya Mkoa wa Iringa iliyofanyiwa ukarabati na Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.


Mkurugenzi wa Maktaba Tanzania Dkt.Mboni Ruzegela,akitoa taarifa fupi ya utekelezaji wa ukarabati wa Maktaba hiyo uliofanywa na Serikali Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe,akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Maktaba ya Mkoa wa Iringa iliyofanyiwa ukarabati na Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe,akikagua Maktaba ya Mkoa wa Iringa mara baada ya kuizindua baada ya kufanyiwa ukarabati pamoja na maboresho na Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.


Muonekano wa Vitabu mbalimbali vilivyomo katika Maktaba ya Mkoa wa Iringa iliyozinduliwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe baada ya kufanyiwa ukarabati pamoja na maboresho na Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.


Muonekano wa Jengo la Maktaba ya Mkoa wa Iringa lililozinduliwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe baada ya kufanyiwa ukarabati pamoja na maboresho na Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

........................................................

Na Alex Sonna,Iringa

SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia imetumia zaidi ya Shilingi bilioni 1.5 kufanya maboresho makubwa katika maktaba saba za mikoa nchini.

Akizungumza na Waandishi wa Habari wakati akizindua Maktaba ya Mkoa wa Iringa ambayo imefanyiwa ukarabati, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia, Prof. James Mdoe amesema ukarabati huo ulilenga kuinua ubora wa elimu nchini.

“Bodi ya Huduma ya Maktaba nchini ilikuwa na changamoto nyingi ambapo mwaka wa fedha wa 2020/2021 tumetenga zaidi ya bilioni 1.5, tukaamua kuanzia maktaba za Mikoa saba na Iringa ni mojawapo" amesema Profesa Mdoe.

Katibu Mkuu huyo amesema ukarabati wa maktaba ya Iringa umehjarimu milioni 150 kwa ajili ya kukarabati huo na kwamba kabla ya ukarabati hali haikuwa nzuri.

Prof Mdoe amesema lengo ni kuinua ubora wa elimu ambapo amesema serikali itaemdelea kukarabati maktaba zilizobaki ili kuhakikisha zote zinakuwa na mazingira mazuri.

Kuhusiana na Changamoto ya upungufu wa fedha, Naibu Katibu Mkuu huyo amesema kadri hali itakavyokuwa nzuri zaidi watazidi kuboresha na kuleta fedha zaidi.

Kuhusu changamoto ya rasiliamli watu amesema : “Yote tunayachukua kubwa ni hili la mkongo wa Taifa haya ni masuala ambayo tunayachukua, tutaona jinsi ya kuyaboresha,

AWATAKA WATUMISHI KUONGEZA UBUNIFU

Katika hatua nyingine, Naibu Katibu Mkuu huyo amewataka watumishi wa maktaba nchini kuongeza ubunifu katika utendaji kazi wao ili kurejesha utamaduni wa zamani wa watanzania kujisomea.

“Nawaomba muongeze ubunifu maktaba hizi zimejengwa siku nyingi wenzetu wa zamani waliona mbali lakini sisi wa kizazi hichi tumeanza kupoteza utamadini wa zamani,ningependa tuurudishe umuhimu wa kusoma fanyeni kazi kwa bidii tupo kwa pamoja,” amesema Prof Mdoe.

Amesema Wizara hiyo ina taasisi 35 ambapo Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi vipo 54 na zililetwa mwaka 2015-2016 kutoka Wizara ya Afya.Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto

Pia, amesema wanazo Ofisi za Uthibiti ubora wa shule ambazo zipo za Kanda na Wilaya,Vyuo 35 vya ualimu vya Serikali ambavyo vinatoa cheti na Diploma.

Amesema katika kipindi cha Serikali ya awamu ya tano na sita wameboresha miundombinu katika Vyuo vikuu na vyuo mbalimbali akitolea mfano Vyuo vya Maendeleo ambavyo vilikuwa na hali mbaya na udahili ulikuwa chini.

Amesema wameweza kuvikarabati vyuo vyote 54 vya Maendeleo ya Wananchi kiasi kwamba udahili umeongezeka kwa kiasi kikubwa.

“Pia tumekarabati na kujenga katika vyuo vyote 35 vya ualimu na vingine ukarabati unaendelea kwenye udhibiti ubora tunazo kanda 14 kufikia mwaka mwaka 2020 tulikuwa tumejenga ofisi mpya uthibiti ubora wa shule katika Halmashauri za 100.

Naibu Katibu Mkuu huyo amesema mwaka 2020-2021 wamejenga ofisi 55 na kukarabati ofisi 31 yote hiyo ni katika kuongeza ubora wa elimu ambapo amesema ubora wa elimu unaendana na miundombinu bora.

SERIKALI YATOA BILIONI 1.1 KWA AJILI YA UKARABATI MAKTABA SABA

Kwa upande wake,Mkurugenzi Mkuu wa Maktaba Taifa, Mboni Ruzegea ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia kwa kuweza kutoa zaidi ya shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya ukarabati wa maktaba saba nchini.

Amezitaja Maktaba zilizofanyiwa ukarabati ni za Mikoa ya Iringa, Bukoba, Rukwa l, Kilimanjaro, Tabora, Kigoma na Morogoro.

Mkurugenzi Mkuu huyo amesema mpango wa Mkakati wa Bodi ya Maktaba nchini ni pamoja na kushughulikia ramani za majengo katika sehemu ambazo hakuna huduma za maktaba.

Amesema wamepangiwa shilingi bilioni 2 kwa ajili ya Maktaba mtandao kwa Maktaba zote ambazo zipo 43 na 22 za Mikoa na 19 ni za Wilaya.

Amesema changamoto wanazokutana nazo ni pamoja na kupokea fedha pungufu, kutokuunganishwa katika mkongo wa Taifa.

Kwa upande wake mwanachama wa Maktaba ya mkoa wa Iringa ambaye pia ni Mtumishi wa Halmashauri ya Kilolo Juma Kimenya amesema baada ya ukarabati huo wamenufaika kwani kwa sasa hali ya hewa ni nzuri kutokana na madirisha kuwa mengi.

WAELIMISHWE UMUHIMU WA KUJISOMEA

Kuhusina na utaratibu wa watanzania kujisomea, Kimenya amesema sio kila mtu anapenda kusoma hivyo kuna haja ya kuelimishana ili watu wajue umuhimu wa kusoma.

“Kujisomea hili suala kidogo unajua ni ‘altitude’ ya mtu pia na ‘traditional’ kwa sababu sio kila mtu anapenda kusoma inategemea na mtu anataka kusoma agundue nini labda tungekuwa na uwanja wa kuelimishana kuhusiana na namna ya kusoma watu wagekuja kusoma kwa sababu sio lazima usome kile ambacho umefundishwa inategemea unahitaji nini tungekuwa na uwanja wa kuelimishana,” amesema

Kwa upande wake mwanachama wa Maktaba hiyo ambaye ni mwalimu, Shida Mgaya amesema kutokana na ukatabati na maboresho hayo idadi ya wanachama imeongezeka ambapo ameomba vitabu vya kisasa viongezwe.

“Kwa sasa wanachama wameongezeka kutokana na maboresho ambayo yamefanyika madirisha meza viti na wameongeza Internet tunaomba waendelee kuongeza vitabu vya kisasa.Mwitikio sio mkubwa kwa wanaojiunga na tuendelee kutangaza kuhusu huduma za maktaba watu walikuwa hawaji lakini kwa sasa wanakuja,” amesema.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger