Monday, 16 August 2021

MAAFISA BIASHARA WANAOGHUSHI LESENI WAONYWA


Na Dotto Kwilasa, Dodoma

AFISA Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) Godfrey Nyaisa amewaonya Maafisa biashara nchini  wanaoghushi leseni na kutengeneza vitabu feki kuacha tabia hiyo huku akisisitiza kuwa kitendo hicho kosa kisheria kwani  kinahujumu uchumi.

 Nyaisa  ametoa onyo hilo leo Jijini Dodoma wakati  akifungua mafunzo ya siku tano kwa Maafisa biashara kutoka mikoa ya Morogoro,Singida na Dodoma kuhusu sheria ya leseni za biashara.

Amesema kuna Halmashauri flani (hakuitaja)Afisa biashara wake  alifoji vitabu vya risiti  na mwisho wa siku alikamatwa jambo linaloleta aibu kwa jamii .

"Maendeleo hayataki uongo uongo ,kutokana na kuepukana na mambo kama haya tunataka kuweka mfumo mzuri wa kuchukua vitabu na leseni kwa njia ya mtandao,njia hii itakomesha wizi,"amesema.

Licha ya hayo amewataka kuzingatia majukumu yao na kuepuka kuwa kikwazo kwa wafanya biashara hali itakayoleta mawasiliano mazuri baina yao na kutengeneza mtandao wa maendeleo.

Amesema kuwa Maafisa biashara wanatakiwa kuwa mstari wa mbele kuwatembelea wafanyabiashara katika maeneo yao na kuwapa elimu  ya ulipaji wa kodi.

"Najua kunasheria za biashara lakini wakati mwingine lazima muongozwe na busara ili kuweza kupata matokeo yaliyo chanya,kwani kufunga biashara siyo suluhisho na pia ilishapitwa na wakati"amesema Nyaisa.

Amesema,Serikali haifanyi biashara ila inatoa huduma hivyo kupitia mafunzo hayo anaamini Maafisa biashara watabadilika na watapata fikra mpya ambapo wataenda kutumika katika kuongoza biashara.

"Kuna maafisa biashara wanapiga sana hela,wawekezaji wanakuja lakini mnawapiga urasimu sana wakati nyie ndio mlitakiwa kuwapa ushirikiano mkubwa",alisema.

Alisema mojawapo ya kazi ya Afisa biashara ni kuhakikisha eneo lake lina wafanyabiashara na wanafahamiana ,lakini utakuta wengine hawatafuti wawekezaji na hata wakija bado tena wanawakandamiza.

Pamoja na hayo Mtendaji Mkuu huyo amewataka kuwatembelea na kutoa elimu kwa wafanyabiashara kwasababu wapo ambao wanafanya biashara bila kuwa na leseni kutokana na kuogopa.

"Mfanya biashara asipokuwa na leseni hawezi kuendelea kwani hatoweza kupata mkopo kutoka bank,lakini pia hakuna biashara inayokuwa yenyewe bila mkopo hata kama una mshahara bado haitoshi kuikuza biashara yako bila mkopo",alisema.

Share:

SERIKALI YAAGIZA WIZARA KUFANYA MAPITIO YA SERA ZAKE


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama.

Na Dotto Kwilasa, Dodoma

SERIKALI  imeziagiza  Wizara zote nchini zenye sera za muda mrefu kuzifanyia mapitio na kuandaa taarifa ya Utekelezaji wake kwa kuziwekea mkataba na muda  ili kuendana na mazingira ya sasa.

 Hayo yamesemwa leo Jijini Dodoma na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri mkuu (Sera ,Bunge, Kazi, Ajira,Vijana na Watu wenye Ulemavu) Jenister Mhagama wakati akizindua  mfumo wa kielektroniki wa uratibu na ufuatiliaji  wa shughuli za serikali(Dashboard).

Akizungumza katika uzinduzi huo, Waziri huyo  amesema Utekelezaji huo wa mapitio ya sera utaongeza ari ya uwajibikaji ikiwa ni Pamoja na kuisaidia serikali katika uratibu wa shughuli zote kwa njia ya utendaji na upokeaji wa taarifa sahihi ,kwa wakati sahihi katika sekta zote nchini.

Pamoja na hayo amesema kupitia Mfumo huo wa kielekroniki shughuli za Serikali zitafanyika na kuratibiwa kwa weledi hali itakayochochea Maendeleo kwa kiasi kikubwa.

"Niwaombe watendaji wote  wa serikali  nchini kuwajibika ipasavyo katika majukumu yenu  kwa kuwa mfumo huo utakwenda kubaini utekelezaji wa shughuli zote za serikali katika kila sekta, ni lazima kila mmoja ahakikishe anasimamia majukumu yake ipasavyo,"amesisitiza.

Naye Waziri wa mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Faustine Ndugulile ambae alihudhuria uzinduzi huo amesema kuwa mfumo huo ni muhimu kwa  Wizara yake kwa kuwa unakwenda kutimiza sera ya TEHAMA nchini na  kuongeza uwajibikaji,ufanisi na uwazi kwa watumishi.

"Tunatarajia mfumo huu utarahisisha shughuli zote za kiserikali na uongeza ufanishi kwa watendaji wote katika sekta mbalimbali nchini,"amesema.

Share:

MWILI WA MWANAMUZIKI ALIYEUAWA WAGOMA KUINGIA KWENYE JENEZA LA BEI RAHISI


Mwanamuziki Peter Oteng almaarufu Storm Dwarchild
***
Kumetokea na hali ya kushangaza katika makafani ya Hospitali ya Rufaa ya Bungoma nchini Kenya baada ya mwili wa Mwanamuziki Peter Oteng almaarufu Storm Dwarchild ulikataa kuingia katika jeneza duni hadi la bei ghali liliponunuliwa.

Oteng ambaye pia alikuwa afisa wa mawasiliano wa mbunge wa Kanduyi, Wafula Wamunyinyi, mwili wake ulikataa kutoshea kwenye jeneza hadi lingine la bei ghali liliponunuliwa.

 Mmoja wa marafiki zake marehemu aliambia gazeti la Taifa Leo kuwa huenda alikataa kuwekwa katika sanduku kwa sababu pesa nyingi zilichangwa ili afanyiwe mazishi ya hadhi.

Swahiba huyo pia alidai kuwa huenda waliomuua Oteng walikuwepo katika mochwari hiyo na hivyo alikasirika kuwaona.

 "Kunaweza kuwa na sababu nyingi za kufanya agome kuingia katika jeneza. Pengine familia yake na jamaa kutoka Uganda walikasirika na kufanya tambiko kuhakikisha kuwa wauaji wake hawatakuwa na amani maishani," rafiki huyo alisema.

Peter Oteng almaarufu Storm Dwarchild alipatikana ameuawa na mwili wake kutupwa kando ya viungani vya mji wa Bungoma. 

Akizungumza na waandishi wa habari, Jumamosi, Agosti 7, Kamanda Mkuu wa polisi kata ndogo ya Bungoma Benjamin Kiwele alidhibitisha kifo cha Storm akisema mwili wa mwendazake ulipatikana na majeraha ya panga. 

Kulingana na Kiwele ilibainika kwamba aliabiri bodaboda kuelekea nyumbani kwake baada ya kukutana na bosi wake mbunge Wamunyinyi. 

Kiwele aliongeza kwamba polisi wameanzisha uchunguzi wakiwa tayari wamepata ujumbe muhimu kwenye simu unayoonyesha aliyemlipia nauli ya boda boda kumfikisha nyumbani. 

Mbunge Wamunyinyi alikashifu mauaji hayo na akisema atahakikisha haki inatendeka kwa mwenda zake.

Chanzo - Tuko News 
Share:

WABUNGE SASA KUANZA KUFANYIWA 'MASSAGE' BUNGENI KUONDOA UCHOVU WANAPOTUNGA SHERIA



Wabunge nchini Kenya wanatazamiwa kuanza kupata huduma za ukandaji 'Massage' katika majengo ya bunge iwapo ripoti iliyowasilishwa na kamati ya Huduma za Vifaa Hitajika Bungeni itapitishwa.

Kamati hiyo ilisema pendekezo hilo ni kwa minajili ya kuimarisha afya ya wabunge kutokana na kukabiliwa na wakati mgumu wanapotunga sheria. 

Kando na hayo, pia inataka kituo cha afya bungeni kikarabatiwe kulingana na sheria za Wizara ya Afya za kuzuia msambao wa corona.

Kamati hiyo inayoongozwa na Mbunge wa Nyaribari Masaba, Ezekiel Machogu ilisema kituo hicho pia kinatakiwa kipanuliwe ili kuongeza vyumba vya ukandaji, kinyozi na ususi. 

"Kitengo cha wanaume kipanuliwe ili kiwe na vyumba vya kutoa ulimwende na mazoezi ya viungo," ilisoma ripoti hiyo.

Kamati hiyo pia inataka kitengo cha wanawake kiwe na huduma za kurembesha kucha na kutengeneza nywele.

 Wafanyakazi wa kituo hicho cha afya watapewa kandarasi ya miaka mitano yenye uwezekano wa kurefusha kulingana na utendakazi iwapo ripot hiyo itapitishwa.

 Chanzo - Tuko News
Share:

RAIS SAMIA AWASILI NCHINI MALAWI KUSHIRIKI MKUTANO WA SADC

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kamuzu Lilongwe nchini Malawi kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 41wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaotarajiwa kuanza hapo kesho tarehe 17 hadi 18 nchini Malawi. PICHA NA IKULU





Share:

JAMII ZAASWA KUWEKEZA KWENYE MISITU



Na Mwandishi Wetu

Katika kukabiliana na Mabadiliko ya tabia ya nchi jamii imeshauriwa kuchangamkia fursa za Uwekezaji katika sekta ya Misitu nchini ili kuhakikisha wanalinda uoto wa Asili wa misitu pamoja na kukabiliana na mabadiliko ya nchi.

Wito huo umetolewa Jijini Dar es salaam na Kaimu Mkurugenzi wa African Forest Kikolo Mwakasungura wakati wa Mkutano na Wadau wa uwekezaji wa sekta ya Misitu wanaoishi mijini .

Mwakasungura amesema kuwa Mkutano huo umelenga kuwakutanisha wadau wa Misitu hasa wanao ishi Mijini ili waweze kuchangamkiwa fursa ya kuwekeza katika sekta hiyo Muhimu nchini hasa maeneo ya Vijijini.

Aidha amesema kuwa kila mtu ana uwezo wa kuwekeza kwenye misitu hata kwa kuanza na hekalu moja.

"Suala la kuwekeza kwenye misitu ni la kila mtanzania na kwa hapa Nchini mikoa ya Nyanda za juu kusaini ndiyo sehemu zinazostawi zaidi ikiwemo Mbeya,Iringa,Songea,Njombe na Makete ni maeneo yanayostawi zaidi", alisema Mwakasungura.

Kwa upande wao baadhi ya Wawekezaji katika sekta ya Misitu waliohudhuria mkutano huo wameiomba Serikali kuhakikisha wanakabiliana na changamoto ya Uchomaji moto wa Misitu ambayo kwa sasa imekisili katika Maeneo ya Vijijini.





Share:

MWENGE WA UHURU KUTUA HALMASHAURI YA JIJI LA ILALA AGOSTI 18


Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ng'wilabuzu Ludigija 
***
Na Magrethy Katengu - Dar es salaam

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ng'wilabuzu Ludigija amewaomba wananchi wa Halmashauri ya Jiji hilo kujitokeza kwa wingi kuupokea Mwenge wa Uhuru unaokuja kuzindua miradi mbalimbali uliobeba dhima ya Uhuru na Umoja 

Akitoa taarifa hiyo katika kikao cha baraza la Madiwani amesema Mwege huo wa Uhuru utakimbizwa Tarehe 18 Agosti, 2021 na unatarajiwa kuzindua, kukagua na kuweka mawe ya msingi katika miradi mbalimbali ya kimaendeleo iliyotekelezwa, na moja kati ya miradi itakayotembelewa ni 'Kituo cha Mapato cha Buguruni' na kuonesha Wilaya ya Ilala inavyotumia kwa usahihi TEHAMA kuwahudumia Wananchi ipasavyo chini ya kaulimbiu ya Mwenge isemayo "TEHAMA ni msingi wa Taifa endelevu. Itumie kwa usahihi na Uwajibikaji”.

Sanjari na hayo amesema Mwenge huo utakimbizwa katika miradi hiyo baada ya hapo utaenda kukesha katika shule ya Msingi Kiwalani wananchi watapata viburudisho mbalimbali ikiwemo muziki na ulinzi mkaliutaimarishwa siku hiyo

"Karibu Mwenge Maalum wa Uhuru Wilaya ya Ilala, Wilaya iliyobeba sehemu kubwa ya Historia ya Mkoa wa Dar es Salaam, kwa maana ya vivutio na uzuri unaolifanya Jiji la Dar es Salaam kuwa miongoni mwa Majiji 10 yenye mvuto zaidi Barani Afrika, vivutio vilivyopo Ilala ni kama vile; Sanamu ya Askari, Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere, Ikulu ya DSM, Ukumbi wa Karimjee, Bandari ya DSM, Soko la Kariakoo, Viwanja vya Mashujaa Mnazi Mmoja, Kituo cha Reli ya DSM, Hospitali ya Muhimbili, Mnara wa Saa, Hoteli zenye hadhi ya Kimataifa, Soko la Samaki Feri, Benki Kuu ya Tanzania, Boma la Kale, Sekondari ya Pugu, Ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere",alisema Ludigija

Pamoja na vivutio vyote hivyo kuwepo Wilaya ya Ilala, lakini pia shughuli mbalimbali za kibiashara hufanyika kwenye Wilaya hii inayoongozwa na Mhe. Ludigija, hivyo Ilala imeitambulisha Dar es salaam kuwa Jiji mashuhuri kwa biashara.
Share:

RAIS SAMIA AONDOKA NCHINI KUELEKEA MALAWI KUSHIRIKI MKUTANO WA 41 WA SADC



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan hii leo Agosti 16, 2021 ameondoka Nchini kuelekea Nchini Malawi kwaajili ya kushiriki Mkutano wa 41 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) utakaofanyika kuanzia tarehe 17-18 Agosti, 2021.



Katika uwanja wa ndege wa Jijini Dodoma , Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan amesindikizwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango, Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Dodoma wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Anthony Mtaka.
Share:

FHI 360 YATOA BAISKELI 242 KWA WAWEZESHAJI UCHUMI KUPAMBANA NA VVU SHINYANGA


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati (wa pili kushoto) akikabidhi baiskeli kwa Mwezeshaji Uchumi, Yasinta Moses (kulia). Kushoto ni  Meneja wa Mradi wa EPIC Mkoa wa Shinyanga Dkt. Shinje Msuka, Wa pili kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zuwena Omary.

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Shirika la Family Health International (FHI 360) limetoa msaada wa Baiskeli 242 kwa Wawezeshaji uchumi (Empowerment Workers) ngazi ya kata ili kuwafikia wasichana balehe na wamama vijana katika mapambano dhidi ya maambukizi ya VVU/UKIMWI mkoani Shinyanga.

Hafla fupi ya makabidhiano ya Baiskeli hizo imefanyika leo Jumatatu Agosti 16,2021 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati.

Akipokea baiskeli hizo, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati amelipongeza Shirika la Family Health International (FHI 360) kupitia mradi wa EPIC, wafadhili wa mradi USAID na PEPFAR pamoja na asasi za kiraia kwa kazi nzuri wanayoifanya katika kuchangia na kusaidiana na serikali katika mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI kwa makundi yaliyoko kwenye athari za kupata maambukizi ya VVU hasa mabinti.

“Wawezeshaji kiuchumi nendeni mkafanye kazi kwa niaba ya serikali. Kafanyeni kazi ya kuwafikia mabinti ili tupunguze maambukizi ya VVU katika jamii yetu,toeni elimu ya miundo na uchumi ili wasichana wafanye kazi na kupata mitaji na kupunguza tabia hatarishi za kupata maambukizi ya VVU”,amesema Dkt. Sengati.

Amesema kwa mujibu wa Tanzania HIV Impact Survey ,2016-17, takwimu zinaonesha hali ya maambukizi ya VVU kwa wasichana balehe na wamama vijana ni asilimia 15.3% ukilinganisha na umri wao huo ambao ni asilimia 6.6%.

“Pia kwa mujibu wa Utafiti wa Idadi ya Watu na Afya Tanzania na Utafiti wa Kiashiria cha Malaria, 2015 - 16 takwimu zinaonesha asilimia 27 ya wasichana balehe wenye umri wa miaka kati ya 15-19 wamepata mtoto au ujauzito”,ameeleza.

“Kutokana na takwimu hizo inaonesha ni jinsi gani wasichana balehe na wamama vijana wako katika athari kubwa na wanapaswa kulindwa na kuhakikisha tunapunguza maambukizi ya VVU/UKIMWI miongoni mwao”,ameongeza Dkt. Sengati.

Mkuu huyo wa mkoa ameyataka mashirika yasiyo ya kiserikali kuhakikisha yanaifikia jamii na kutoa eleimu ya kutosha ili kupunguza changamoto zinazowakumba wasichana zikiwemo mimba za utotoni,ukatili wa kijinsia na maambukizi ya VVU na kwamba serikali itaendelea kushirikiana nao ili kuwa na jamii inayomthamini mtoto wa kike na kumpa ulinzi wa kutosha.

“Serikai tunatambua na kuthamini mchango wa wadau na hatuwezi kufanya kila kitu ndiyo maana nyinyi kama wadau mko mstari wa mbele kuisaidia serikali kutekeleza agenda ya maendeleo ya 2030 na kuhakikisha kwamba 95-95-95 (95 % ya watu wanaoishi na VVU wanajua hali yao ya maambukizi, 95% ya waliopima wameanza kutumia dawa na 95% ya walioanza dawa wamepunguza makali ya VVU”, amesema Dkt. Sengati.

Akikabidhi baiskeli 24 kati ya 242 Meneja wa Mradi wa EPIC Mkoa wa Shinyanga Dkt. Shinje Msuka amesema Shirika la Family Health International (FHI 360) limetoa baiskeli hizo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa Kimataifa wa EPIC kwa Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa kukabiliana na UKIMWI (PEPFAR) na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID).

“Kupitia mradi huu tumetoa jumla ya baiskeli 242 kwa mkoa wa Shinyanga ambazo zinagawiwa kwa walengwa katika halmashauri 5 za wilaya ambazo ni Shinyanga, Manispaa ya Shinyanga na Kahama, Ushetu na Msalala. Leo tumekusanyika hapa kwa dhumuni la kugawa baiskeli kwa wawezeshaji uchumi 24 wa Manispaa ya Shinyanga”,amesema Dkt. Msuka.

Ameeleza kuwa baiskeli hizo zitasaidia Wawezeshaji Kiuchumi kuwafikia wa wasichana balehe na wamama vijana na kuchangia jitihada za serikali katika kuhakikisha maambukizi ya VVU/UKIMWI yanapunguzwa na kufikia malengo ya 95-95-95.

“Baiskeli hizi ni sehemu ya vitendea kazi kwa wawezeshaji uchumi,tunaamini zitapunguza changamoto ya usafiri na kuwawezesha kuwafikia wasichana wengi zaidi katika kata, vijiji,vitongoji na hata ngazi ya kaya”,amesema Dkt. Msuka.

“Baiskeli hizi zinapaswa kutumika kwa matumizi ya mradi tu na si vinginevyo ili kuboresha hali ya mabinti na kutokomeza janga la UKIMWI. Tanzania bila UKIMWI inawezekana, tuendelee kutoa elimu kwa kila mtu asimame katika nafasi yake kufikia na kuendeleza udhibiti wa janga la VVU/UKIMWI nchini Tanzani”,ameongeza Dkt. Msuka.

Dkt. Msuka amesema Mradi wa EPIC unatekeleza afua za utoaji wa huduma zinazohusiana na VVU zikiwalenga makundi maalumu na yanayohitaji kupewa kipaumbele ikiwemo wasichana wa rika balehe na wamama vijana, wanaume na wanawake walio katika hatari ya kupata maambukizi ya VVU.

Amefafanua kuwa Mpango wa DREAMS ni kati ya afua zinazotekelezwa na mradi wa EPIC wenye lengo la kupunguza maambukizi ya VVU kwa wasichana balehe na wanawake vijana wenye umri wa miaka 9 hadi 24, wanaoishi katika mazingira hatarishi na wanafanya ngono katika umri mdogo ili waweze kumudu gharama za maisha.

Mradi wa EPIC unatekeleza mpango wa DREAMS katika halmashauri 6 za mkoa wa Shinyanga tangu mwezi Februari 2020 kupitia mashirika manne ya kijamii ambayo ni Rafiki SDO, TADEPA, HUHESO Foundation na SHIDEPHA. Tayari jumla ya wasichana 100,000 wamefikiwa.

“Wasichana 20,000 wamefikiwa na huduma za kitabibu kama upimaji wa VVU kwa hiari,uchunguzi wa ukatili wa kijinsia,huduma za uzazi wa mpango,uchunguzi wa magonjwa ya zinaa na huduma za dawa kinga (PREP), 38,000 wamefikiwa na huduma za miundo ambako wanaweka akiba na kukopa, 13,000 wameweza kuanzisha biashara zao wenyewe na 100,000 wamefikiwa na huduma za mabadiliko ya tabia”,ameongeza.

Akizungumza kwa niaba ya Wawezeshaji Uchumi,Sophia Chamba amelishukuru Shirika la FHI 360 na Mradi wa EPIC kwa kuwapatia baiskeli hizo ambazo watazitumia kuifikia jamii kutekeleza majukumu yao ambayo ni pamoja na kuwafundisha mabinti balehe na wanawake vijana masomo ya uchumi na yanayosaidia kujikinga na maambukizi mapya ya VVU.

Ameyataja majukumu mengine kuwa ni kutoa elimua ya mabadiliko ya tabia na upimaji wa VVU kwa kushirikiana na waelimisha rika,kufundisha masuala ya ujasiriamali na kuandikisha mabinti balehe na wanawake vijana katika vikundi kulinga na umri wao.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akizungumza leo Jumatatu Agosti 16,2021 wakati akipokea baiskeli 242 zilizotolewa na Shirika la Family Health International (FHI 360) kupitia Mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR kwa Wawezeshaji uchumi (Empowerment Workers) ngazi ya kata ili kuwafikia wasichana balehe na wamama vijana katika mapambano dhidi ya maambukizi ya VVU/UKIMWI mkoani Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akizungumza wakati akipokea baiskeli 242 zilizotolewa na Shirika la Family Health International (FHI 360) kupitia mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR kwa Wawezeshaji uchumi (Empowerment Workers) ngazi ya kata ili kuwafikia wasichana balehe na wamama vijana katika mapambano dhidi ya maambukizi ya VVU/UKIMWI mkoani Shinyanga.
 Meneja wa Mradi wa EPIC Mkoa wa Shinyanga Dkt. Shinje Msuka akizungumza leo Jumatatu Agosti 16,2021 wakati akikabidhi baiskeli 242 zilizotolewa na Shirika la Family Health International (FHI 360) kupitia Mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR kwa Wawezeshaji uchumi ngazi ya kata ili kuwafikia wasichana balehe na wamama vijana katika mapambano dhidi ya maambukizi ya VVU/UKIMWI mkoani Shinyanga.
 Meneja wa Mradi wa EPIC Mkoa wa Shinyanga Dkt. Shinje Msuka akizungumza leo Jumatatu Agosti 16,2021 wakati akikabidhi baiskeli 242 zilizotolewa na Shirika la Family Health International (FHI 360) kupitia Mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR kwa Wawezeshaji uchumi ngazi ya kata ili kuwafikia wasichana balehe na wamama vijana katika mapambano dhidi ya maambukizi ya VVU/UKIMWI mkoani Shinyanga.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zuwena Omary akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya baiskeli 242 zilizotolewa na Shirika la Family Health International (FHI 360) kupitia Mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR kwa Wawezeshaji uchumi ngazi ya kata ili kuwafikia wasichana balehe na wamama vijana katika mapambano dhidi ya maambukizi ya VVU/UKIMWI mkoani Shinyanga.
Mwezeshaji Uchumi,Sophia Chamba akilishukuru Shirika la FHI 360 na Mradi wa EPIC kwa kuwapatia baiskeli hizo ambazo watazitumia kuifikia jamii kutekeleza majukumu yao.
Mratibu wa TACAIDS mkoa wa Shinyanga Geofrey Mambo akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya baiskeli 242 zilizotolewa na Shirika la Family Health International (FHI 360) kupitia Mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR kwa Wawezeshaji uchumi ngazi ya kata mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akikagua baiskeli moja kati ya baiskeli 242 zilizotolewa na Shirika la Family Health International (FHI 360) kupitia mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR kwa Wawezeshaji uchumi  ngazi ya kata ili kuwafikia wasichana balehe na wamama vijana katika mapambano dhidi ya maambukizi ya VVU/UKIMWI mkoani Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akiendesha baiskeli ambayo kati ya baiskeli 242 zilizotolewa na Shirika la Family Health International (FHI 360) kupitia Mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR kwa Wawezeshaji uchumi  ngazi ya kata ili kuwafikia wasichana balehe na wamama vijana katika mapambano dhidi ya maambukizi ya VVU/UKIMWI mkoani Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akiendesha baiskeli ambayo kati ya baiskeli 242 zilizotolewa na Shirika la Family Health International (FHI 360) kupitia Mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR kwa Wawezeshaji uchumi  ngazi ya kata ili kuwafikia wasichana balehe na wamama vijana katika mapambano dhidi ya maambukizi ya VVU/UKIMWI mkoani Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati (wa pili kushoto) akikabidhi baiskeli kwa Mwezeshaji Uchumi, Rachel Manga (kulia). Kushoto ni  Meneja wa Mradi wa EPIC Mkoa wa Shinyanga Dkt. Shinje Msuka, Wa pili kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zuwena Omary. Hizi ni sehemu ya baiskeli 242 zilizotolewa na Shirika la Family Health International (FHI 360) kupitia Mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR kwa Wawezeshaji uchumi  ngazi ya kata mkoani Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati (wa pili kushoto) akikabidhi baiskeli kwa Mwezeshaji Uchumi, Amina Bundala (kulia). Kushoto ni  Meneja wa Mradi wa EPIC Mkoa wa Shinyanga Dkt. Shinje Msuka, Wa pili kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zuwena Omary. Hizi ni sehemu ya baiskeli 242 zilizotolewa na Shirika la Family Health International (FHI 360) kupitia Mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR kwa Wawezeshaji uchumi  ngazi ya kata mkoani Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati (wa pili kushoto) akikabidhi baiskeli kwa Mwezeshaji Uchumi, Elizabeth Sollo (kulia). Kushoto ni  Meneja wa Mradi wa EPIC Mkoa wa Shinyanga Dkt. Shinje Msuka, Wa pili kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zuwena Omary. Hizi ni sehemu ya baiskeli 242 zilizotolewa na Shirika la Family Health International (FHI 360) kupitia Mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR kwa Wawezeshaji uchumi  ngazi ya kata mkoani Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati (wa pili kushoto) akikabidhi baiskeli kwa Mwezeshaji Uchumi, Mary Ford (kulia). Kushoto ni  Meneja wa Mradi wa EPIC Mkoa wa Shinyanga Dkt. Shinje Msuka, Wa pili kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zuwena Omary. Hizi ni sehemu ya baiskeli 242 zilizotolewa na Shirika la Family Health International (FHI 360) kupitia Mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR kwa Wawezeshaji uchumi  ngazi ya kata mkoani Shinyanga.
Wawezeshaji Uchumi wakiendesha baiskeli zilizotolewa na Shirika la Family Health International (FHI 360) kupitia Mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR kwa Wawezeshaji uchumi  ngazi ya kata mkoani Shinyanga.
Wawezeshaji Uchumi wakiendesha baiskeli zilizotolewa na Shirika la Family Health International (FHI 360) kupitia Mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR kwa Wawezeshaji uchumi  ngazi ya kata mkoani Shinyanga.
Muonekano wa sehemu ya baiskeli zilizotolewa na Shirika la Family Health International (FHI 360) kupitia Mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR kwa Wawezeshaji uchumi  ngazi ya kata mkoani Shinyanga.
Muonekano wa sehemu ya baiskeli zilizotolewa na Shirika la Family Health International (FHI 360) kupitia mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR kwa Wawezeshaji uchumi  ngazi ya kata mkoani Shinyanga.
Wawezeshaji Uchumi wakipiga picha ya kumbukumbu baada ya kukabidhiwa baiskeli zilizotolewa na Shirika la Family Health International (FHI 360) kupitia mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR kwa Wawezeshaji uchumi  ngazi ya kata mkoani Shinyanga.
Meneja wa Mradi wa EPIC Mkoa wa Shinyanga Dkt. Shinje Msuka (kulia) akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati wakati wa hafla ya makabidhiano ya baiskeli 242 zilizotolewa na Shirika la Family Health International (FHI 360) kupitia Mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR kwa Wawezeshaji uchumi  ngazi ya kata mkoani Shinyanga.
Wadau wa VVU/UKIMWI na Wawezeshaji Uchumi wakiwa ukumbini wakati wa hafla ya makabidhiano ya baiskeli 242 zilizotolewa na Shirika la Family Health International (FHI 360) kupitia Mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR kwa Wawezeshaji uchumi  ngazi ya kata mkoani Shinyanga.
Wadau wa VVU/UKIMWI na Wawezeshaji Uchumi wakiwa ukumbini wakati wa hafla ya makabidhiano ya baiskeli 242 zilizotolewa na Shirika la Family Health International (FHI 360) kupitia Mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR kwa Wawezeshaji uchumi  ngazi ya kata mkoani Shinyanga.
Wadau wa VVU/UKIMWI na Wawezeshaji Uchumi wakiwa ukumbini wakati wa hafla ya makabidhiano ya baiskeli 242 zilizotolewa na Shirika la Family Health International (FHI 360) kupitia Mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR kwa Wawezeshaji uchumi  ngazi ya kata mkoani Shinyanga.
Wadau wa VVU/UKIMWI na Wawezeshaji Uchumi wakiwa ukumbini wakati wa hafla ya makabidhiano ya baiskeli 242 zilizotolewa na Shirika la Family Health International (FHI 360) kupitia Mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR kwa Wawezeshaji uchumi  ngazi ya kata mkoani Shinyanga.
Wadau wa VVU/UKIMWI na Wawezeshaji Uchumi wakiwa ukumbini wakati wa hafla ya makabidhiano ya baiskeli 242 zilizotolewa na Shirika la Family Health International (FHI 360) kupitia Mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR kwa Wawezeshaji uchumi  ngazi ya kata mkoani Shinyanga.
Wadau wa VVU/UKIMWI na Wawezeshaji Uchumi wakiwa ukumbini wakati wa hafla ya makabidhiano ya baiskeli 242 zilizotolewa na Shirika la Family Health International (FHI 360) kupitia Mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR kwa Wawezeshaji uchumi  ngazi ya kata mkoani Shinyanga.
Wadau wa VVU/UKIMWI na Wawezeshaji Uchumi wakiwa ukumbini wakati wa hafla ya makabidhiano ya baiskeli 242 zilizotolewa na Shirika la Family Health International (FHI 360) kupitia Mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR kwa Wawezeshaji uchumi  ngazi ya kata mkoani Shinyanga.
Wadau wa VVU/UKIMWI na Wawezeshaji Uchumi wakiwa ukumbini wakati wa hafla ya makabidhiano ya baiskeli 242 zilizotolewa na Shirika la Family Health International (FHI 360) kupitia Mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR kwa Wawezeshaji uchumi  ngazi ya kata mkoani Shinyanga.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger