Sunday, 1 August 2021
MABINTI WA RAFIKI SDO WASHIRIKI MAONESHO YA BIASHARA NA TEKNOLOJIA YA MADINI SHINYANGA..WAONESHA BIDHAA ZAO
Afisa Mabinti wa Shirika la Rafiki SDO, Maria Kamage (kushoto) na Mabinti wakionesha bidhaa wanazozalisha kwenye Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Shinyanga katika uwanja wa Zainab Telack Butulwa kata ya Old Shinyanga.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Shirika la Rafiki SDO limeshiriki Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga yaliyofungwa leo Jumapili Agosti 1,2021 na Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko kwa kuonesha na kuuza bidhaa zinazotengenezwa na Mabinti wanaofadhiliwa na shirika hilo kwa lengo kuwainua kiuchumi.
Afisa Mabinti wa Shirika la Rafiki SDO, Maria Kamage amesema wanawasaidia mabinti kujikwamua kiuchumi kwa kuwapa elimu za ujasiriamali, akiba na uchumi ambayo inawawezesha kupitia hizo akiba kupata mikopo katika vikundi vyao kuanzisha biashara zao binafsi na kuwafanya wasiwe wategemezi na kuwaepusha na vishawishi na kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.
Mabinti kutoka Rafiki SDO wakionesha bidhaa wanazozalisha kwenye Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Shinyanga katika uwanja wa Zainab Telack Butulwa kata ya Old Shinyanga.
Afisa Mabinti wa Shirika la Rafiki SDO, Maria Kamage (kushoto) akiwa banda la Rafiki SDO kwenye Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Shinyanga katika uwanja wa Zainab Telack Butulwa kata ya Old Shinyanga.
Wananchi wakiangalia bidhaa zinazozalishwa na mabinti katika banda la Rafiki SDO kwenye Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Shinyanga katika uwanja wa Zainab Telack Butulwa kata ya Old Shinyanga.
Soma pia :
Picha : BITEKO AFUNGA MAONESHO YA BIASHARA NA TEKNOLOJIA YA MADINI SHINYANGA....ATANGAZA KUZINGUA WALIOSHIKILIA LESENI ZA UCHIMBAJI
BENKI YA TCB YASHIKA NAFASI YA PILI TAASISI ZA FEDHA MAONESHO YA BIASHARA NA TEKNOLOJIA YA MADINI SHINYANGA
Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko akimkabidhi Meneja wa Benki ya Biashara ya Tanzania (Tanzania Commercial Bank- TCB PLC) Tawi la Shinyanga Julius Mataso (kulia) Cheti cha Ushindi ambapo Benki ya TCB (zamani ikiitwa Benki ya TPB) imeshika nafasi ya Pili katika kundi la Taasisi za Fedha katika Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga yalifungwa leo Jumapili Agosti 1,2021 katika uwanja wa Zainab Telack Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
WAZIRI BITEKO ATEMBELEA BANDA LA BENKI YA NBC AKIFUNGA MAONESHO SHINYANGA
Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko (kushoto) akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa Benki ya NBC tawi la Shinyanga, Joyce Chagonja kuhusu huduma zinazotolewa katika Benki ya NBC ikiwemo Mikopo kwa wafanyabiashara leo Jumapili Agosti 1,2021 wakati akifunga Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga katika uwanja wa Zainab Telack Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko (kushoto) akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa Benki ya NBC tawi la Shinyanga, Joyce Chagonja kuhusu huduma zinazotolewa katika Benki ya NBC ikiwemo Mikopo kwa wafanyabiashara leo Jumapili Agosti 1,2021 wakati akifunga Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga katika uwanja wa Zainab Telack Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga
Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko (kushoto) akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa Benki ya NBC tawi la Shinyanga, Joyce Chagonja kuhusu huduma zinazotolewa katika Benki ya NBC ikiwemo Mikopo kwa wafanyabiashara leo Jumapili Agosti 1,2021 wakati akifunga Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga katika uwanja wa Zainab Telack Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.
Soma pia:
WAZIRI WA MADINI DOTO BITEKO ATEMBELEA BANDA LA BENKI YA NMB MAONESHO YA BIASHARA NA TEKNOLOJIA YA MADINI SHINYANGA
Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko (kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa Benki ya NMB tawi la Manonga, Sebastian Kayaga huduma zinazotolewa katika Benki ya NMB ikiwemo Mikopo kwa wachimbaji wa madini leo Jumapili Agosti 1,2021 wakati akifunga Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga katika uwanja wa Zainab Telack Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kulia ni Meneja wa Benki ya NMB tawi la Manonga, Sebastian Kayaga akimwelezea Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko huduma zinazotolewa na Benki ya NMB alipotembelea banda la NMB kwenye Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga.
Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko (kulia) akizungumza kwenye banda la benki ya NMB leo Jumapili Agosti 1,2021 wakati akifunga Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga katika uwanja wa Zainab Telack Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.
Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
WAZIRI BITEKO ATEMBELEA BANDA LA SHINYANGA BEST IRON MAONESHO SHINYANGA
Mkurugenzi wa Kampuni ya Uundaji wa Vifaa vya Uchimbaji na Uchenjuaji Madini ya Shinyanga Best Iron, Kashi Salula (kulia) akimwelezea Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko kuhusu changamoto ya umeme inayowakabili wachimbaji wadogo ambapo aliishukuru serikali kwa kupeleka umeme maeneo ya machimbo lakini umeme huo hauna nguvu ya kuwasha mitambo hivyo akaomba changamoto hiyo itatuliwe.
Waziri Biteko ametembelea Banda la Shinyanga Best Iron wakati akifunga Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga katika uwanja wa Zainab Telack Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.
Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko (katikati) akiangalia shughuli za uchimbaji na uchenjuaji madini ya dhahabu katika banda la Kampuni ya Uundaji wa Vifaa vya Uchimbaji na Uchenjuaji Madini ya Shinyanga Best Iron
Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko (kulia) akiangalia shughuli za uchimbaji na uchenjuaji madini ya dhahabu katika banda la Kampuni ya Uundaji wa Vifaa vya Uchimbaji na Uchenjuaji Madini ya Shinyanga Best Iron
Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko akiwa katika banda la Kampuni ya Uundaji wa Vifaa vya Uchimbaji na Uchenjuaji Madini ya Shinyanga Best Iron
WAZIRI BITEKO ATEMBELEA BANDA LA BARRICK AKIFUNGA MAONESHO YA BIASHARA NA TEKNOLOJIA YA MADINI SHINYANGA
Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko (kulia) akisikiliza maelezo kuhusu shughuli zinazofanywa na Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Dhahabu ya Barrick kupitia migodi yake ya Buzwagi na Bulyanhulu leo Jumapili Agosti 1,2021 wakati akifunga Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga katika uwanja wa Zainab Telack Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga . Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko (kulia) akiwa katika banda la Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Dhahabu ya Barrick kupitia migodi yake ya Buzwagi na Bulyanhulu leo Jumapili Agosti 1,2021 wakati akifunga Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga katika uwanja wa Zainab Telack Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga
Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko (kulia) akiwa katika banda la Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Dhahabu ya Barrick kupitia migodi yake ya Buzwagi na Bulyanhulu leo Jumapili Agosti 1,2021 wakati akifunga Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga katika uwanja wa Zainab Telack Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga
Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko akizungumza katika banda la Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Dhahabu ya Barrick kupitia migodi yake ya Buzwagi na Bulyanhulu leo Jumapili Agosti 1,2021 wakati akifunga Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga katika uwanja wa Zainab Telack Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga
WAZIRI WA MADINI DOTO BITEKO ATEMBELEA BANDA LA BENKI YA CRDB AKIFUNGA MAONESHO SHINYANGA
Kushoto ni Meneja Biashara wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Mwanahamisi Iddi akimuelezea Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko (katikati) kuhusu huduma zinazotolewa na Benki ya CRDB zikiwemo huduma za Bima, Mikopo na Akaunti ya Hodari ambayo ni akaunti maalumu kwa ajili ya wajasiriamali wadogo na wa kati wakiwemo Machinga, Bodaboda, Mama lishe, Wafanyabiashara kwenye masoko, Mafundi vyerehani, Seremala, Wachimbaji Wadogo wa Madini na makundi mengine. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Meneja Biashara wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Mwanahamisi Iddi akielezea huduma mbalimbali zinazotolewa na Benki ya CRDB wakati Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko (kushoto) alipotembelea Banda la Benki ya CRDB wakati wa kufunga Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga leo Jumapili Agosti 1,2021
Meneja Biashara wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Mwanahamisi Iddi akielezea huduma mbalimbali zinazotolewa na Benki ya CRDB wakati Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko (kushoto) alipotembelea Banda la Benki ya CRDB wakati wa kufunga Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga leo Jumapili Agosti 1,2021
Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko (kulia) akishuhudia shughuli za kibenki ikiwemo kufungua akaunti na kutoa fedha zikiendelea kwenye Banda la Benki ya CRDB wakati wa kufunga Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga leo Jumapili Agosti 1,2021
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Saidi Pamui akizungumza wakati Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko akifunga Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini mkoa wa Shinyanga ambapo alisema Benki ya CRDB inatoa huduma za mikopo hivyo wachimbaji wa madini na wajasiriamali wachangamkie fursa hiyo.
Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko akimkabidhi Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Saidi Pamui (kulia) cheti cha utoaji huduma bora wakati wa Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini mkoa wa Shinyanga.
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Said Pamui ambao ni miongoni mwa Wadhamini wakuu wa Maonesho hayo akionesha zawadi aliyopewa na Kamati ya Maonesho wakati wa ufungaji wa Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga.
Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Soma pia:
BOSI WA CHUO CHA SAYANSI ZA AFYA KOLANDOTO AELEZA KUFAIDI MAONESHO YA BIASHARA NA TEKNOLOJIA YA MADINI SHINYANGA
Mkuu wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto kinachomilikiwa na Kanisa la Africa Inland Church Tanzania (AICT) kilichopo katika Manispaa ya Shinyanga, Dkt. Paschal Shiluka amesema Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga yamekuwa na manufaa makubwa kwani zaidi ya watu 450 wametembelea banda lao na kujionea kuonesha shughuli wanazofanya kwenye chuo chao, kupata elimu ya afya ,kupima afya ikiwemo upimaji wa Sukari, Shinikizo la damu na malaria.
Dkt. Shiluka amesema Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga yaliyoanza Julai 23,2021 na kufungwa leo Agosti 1, 2021 na Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko katika uwanja wa Zainab Telack kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga yamewasaidia pia kutangaza chuo chao.
"Banda letu limekuwa Busy muda wote, wananchi wamejitokeza kupima afya zao,mpaka tunafunga walikuwa bado wanahitaji kupata huduma ya kupima shinikizo la damu, malaria, urefu na uzito na wote waliojitokeza kupima afya zao tumewapa ushauri na kuwashauri hatua za kuchukua ikiwa ni pamoja na kuwapa Rufaa kwenda kutibiwa wale waliobainika kuwa na magonjwa tuliyokuwa tunapima",amesema Dkt. Shiluka
"Kupitia maonesho haya tumejitangaza na kutangaza huduma tunazozitoa. Zaidi ya watu 450 wametembelea banda letu na kusaini kitabu chetu. Pia zaidi ya watu 150 wamechukua fomu za kujiunga na mafunzo ya Sayansi za Afya katika kada za Nursing, Maabara, Utabibu, Famasia na Mafunzo ya Maabara Viwandani yanayotarajia kuanza Mwezi Septemba 2021. Milango ya maombi bado iko wazi naomba wananchi watumie Mwezi huu Agosti kutuma maombi yao kwa kufika chuoni au kupitia website yetu ya https://kchs.ac.tz",amesema Dkt. Shiluka.
Soma pia
WANANCHI WAMIMINIKA BANDA LA CHUO CHA SAYANSI ZA AFYA KOLANDOTO KUPIMA AFYA MAONESHO SHINYANGA
Mkuu wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto , Dkt. Paschal Shiluka akizungumza baada ya Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga kufungwa leo Jumapili Agosti 1,2021 na Waziri wa Madini Doto Biteko
Wanafunzi na Wafanyakazi wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto , Dkt. Paschal Shiluka wakipiga picha ya kumbukumbu nje ya banda lao baada ya Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga kufungwa leo Jumapili Agosti 1,2021 na Waziri wa Madini Doto Biteko
Wanafunzi na Wafanyakazi wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto , Dkt. Paschal Shiluka wakipiga picha ya kumbukumbu nje ya banda lao baada ya Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga kufungwa leo Jumapili Agosti 1,2021 na Waziri wa Madini Doto Biteko.
Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog