Spika wa Bunge, Job Ndugai leo Jumanne Juni Mosi, 2021 amemtoa katika ukumbi wa Bunge mbunge wa Momba (CCM), Condester Sichwale kutokana na kuvaa suruali iliyombana.
Kwa mujibu wa kanuni za Bunge, wabunge wanawake hawaruhusiwi kuvaa suruali za kubana.
Mara baada ya kipindi cha maswali na majibu, alisimama mbunge wa Nyang'wale (CCM), Hussein Amar na kuomba mwongozo wa Spika.
"Spika nasimama kwa kanuni ya 70 inayohusu mavazi ya staha kwa wabunge, kanuni imeeleza wazi kuhusu mavazi hayo na kwa akina dada lakini humu ndani kuna wabunge wamevaa nguo ambazo hazina staha," amesema Amar.
Spika Ndugai alimpa nafasi mbunge huyo kumtaja mwenzake aliyevaa mavazi ambayo hayakuwa na staha ili iwe mfano.
"Mbunge huyo yuko hapo katika mkono wangu wa kulia, amevalia tisheti lakini naomba umuite mbele uone suruali aliyovaa namna ilivyobana, amevaa miwani," amesema Ameir bila kumtaja jina.
Spika alisimama na kumtaka mbunge aliyevaa mavazi hayo asimame na aondoke ndani ya ukumbi ili akavae mavazi yenye staha ndipo atarejea tena bungeni.
Sichwale alisimama akabeba mkoba wake na kutoka nje ya ukumbi wa Bunge.
Spika Ndugai ameagiza askari wote katika milango ya kuingia bungeni wawe makini wasiruhusu wabunge kuingia wakiwa wamevaa mavazi yaliyokatazwa.
Tuesday, 1 June 2021
PICHA: Ndugai amtimua mbunge aliyevaa suruali ya kubana bungeni
Rais Samia awasimamisha kazi viongozi soko la Kariakoo
Rais Samia Suluhu Hassan ameusimamisha kwa muda uongozi wa soko la Kariakoo lililopo jijini Dar es salaam, na kuagiza uchunguzi ufanyike kuhusu tuhuma mbalimbali zinazoukabili uongozi huo.
Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza hatua hiyo wakati wa ziara yake ya kushtukiza katika soko hilo, ambapo pia amesikiliza kero za Wafanyabiashara mbalimbali wa soko hilo.
Amesema hali ya soko hilo la Kariakoo hairidhishi, na kwamba Serikali kwa sasa inaenda kufanya tahmini ya kina kuona namna ya kuliendesha soko hilo.
Rais Samia Suluhu Hassan amesema lengo la kuanzishwa kwa soko hilo ni kuwasadia Wafanyabiashara wadogo, lakini kwa sasa jambo hilo halipo na kinachofanyika ni kuwanufaisha viongozi wa soko hilo pekee.
Ameongeza kuwa mpangilio wa bidhaa ndani ya soko hilo ni mbaya, jambo ambalo linahitaji kufanyiwa marekebisho ya haraka.
International Individual Consultant – COVAX communication at UNICEF June 2021
This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content
Job no: 540837 Contract type: Consultancy Level: Consultancy Location: Tanzania,Uni.Re Categories: Communication for Development (C4D), Consultancy UNICEF works in some of the world’s toughest places, to reach the world’s most disadvantaged children. To save their lives,To defend their rights and to help them fulfill their potential. Across 190 countries and territories, we work for every child, everywhere, every day, to […]
This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details
Relationship Manager; Mass Affluent (2 year contract) at NMB Bank
This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content
Job Purpose To create new and manage existing relationships effectively in order to facilitate the growth of Affluent and Mass Affluent Liability and Asset portfolio as well as income within Private Banking. To make effective sales activation – Account opening and enrolment to digital channels to all clients new and existing from Private schemes. Main […]
This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details
Head of Retail Credit at NBC Bank
This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content
NBC is the oldest serving bank in Tanzania with over five decades of experience. We offer a range of retail, business, corporate and investment banking, wealth management products and services. Job Summary To develop tactical strategy and delivery plans, formulate associated practice/s and to ensure operational implementation and adoption i.t.o. credit risk management methodology, practice, […]
This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details
Head, Corporate Affairs, Brand & Marketing at Standard Chartered Bank
This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content
About Standard Chartered We are a leading international bank focused on helping people and companies prosper across Asia, Africa and the Middle East. To us, good performance is about much more than turning a profit. It’s about showing how you embody our valued behaviours – do the right thing, better together and never settle – […]
This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details
MRADI WA ADGG WAWANUFAISHA WAFUGAJI WA MIKOA 7
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), Prof. Erick Komba akisikiliza mada iliyokuwa ikiwasilishwa kuhusu mradi wa Uboreshaji na Uendelezaji wa Mbari za Ng'ombe wa Maziwa katika kikao kilichofanyika katika Makao Makuu ya Taasisi hiyo Jijini Dodoma.
Msimamizi Mkuu wa Mradi Uboreshaji na Uendelezaji wa Mbari za Ng'ombe wa Maziwa (ADGG), Dkt. Daniel Komwihangilo akifafanua jambo kuhusu mradi huo katika kikao cha tathmini kilichofanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) Jijini Dodoma. Kulia ni Mshauri wa Mradi huo, Dkt. Maria Mashingo ambaye pia alishawahi kuwa Katibu Mkuu Mifugo.
Mratibu wa mradi wa ADGG, Dkt. Eliamoni Lyatuu akiwasilisha mada kuhusu mradi wa Uboreshaji na Uendelezaji wa Mbari za Ng'ombe wa Maziwa katika kikao kilichofanyika katika Makao Makuu ya Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania Jijini Dodoma.
Picha ya pamoja ya Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), Prof. Erick Komba (aliyevaa suti nyeusi) na wajumbe wa kikao kilichofanya tathmini ya maendeleo ya mradi wa Uboreshaji na Uendelezaji wa Mbari za Ng'ombe wa Maziwa mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho kilichofanyika katika Makao Makuu ya Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania Jijini Dodoma.
***
Mradi wa uboreshaji na uendelezaji mbari za ng’ombe wa maziwa (ADGG) ambao umefanyika katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Iringa, Mbeya Njombe, na Songwe wawanufaisha wafugaji katika maeneo hayo.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), Prof. Erick Komba (31.05.2021) baada ya kumalizika kwa kikao cha tathmini ya maendeleo ya mradi huo ambao kwa hapa Tanzania unafanyika katika mikoa saba (7) na Halmashauri ishirini nan ne (24).
Prof. Komba amesema mradi huo ulikuwa ni wa miaka sita na unatarajiwa kumalizika mwaka 2022 mwezi wa nne. Lengo la kikao hicho cha tathmini ilikuwa ni kuangalia mazuri yaliyofanyika kupitia mradi na namna gani yanaweza kuendelezwa ili wafugaji waendelee kupata tija na kukuza kipato ufugaji.
“Wafugaji wamenufaika sana kutokana na uwepo wa mradi huu kutokana na ushauri mbalimbali waliokuwa wakiupata kutoka kwa wataalamu juu ya nini cha kufanya pale mifugo yao inapopata matatizo na aina gani ya mbegu bora za ng’ombe wa maziwa wanatakiwa kufuga,” alisema Prof. Kombe.
Katika kikao hicho pia wamejadili namna ya kuwashirikisha wadau mbalimbali ambao watasaidia kuendeleza kazi zilizofanywa na mradi ili ziwe kuwa endelevu ikiwepo serikali, wadau wa maziwa na wadau wa mawasiliano.
Lengo ni kuhakikisha uzalishaji wa maziwa unaongezeka hapa nchini na hivyo kupunguza uagizaji wa maziwa kutoka nje ya nchi na hivyo kumnufaisha mfugaji wa hapa nchini kwa kukuza kipato chake.
Naye Mshauri wa Mradi wa kuendeleza mbari za ng’ombe wa maziwa, Dkt. Maria Mashingo ambaye pia alishawahi kuwa Katibu Mkuu Mifugo amesema mradi huu ni muhimu sana katika kuleta mageuzi kwenye sekta ya maziwa kwa kuhakikisha kuna kuwa na mbegu au vizazi bora vya ng’ombe ambao wanauwezo mkubwa wa kutoa maziwa mengi.
Dkt. Mashingo amesema mradi huu umetekelezwa kwa kutumia mbinu kubwa ambayo katika Sekta ya Mifugo haijawahi kufanyika kwani kinachofanyika ni pamoja na utambuzi wa ng’ombe kwa kujua uzazi na ubora wake.
Hivyo ameshauri itafutwe njia ya kuhakikisha matokeo ya mradi huu yanaendelezwa kwani watafiti wamefanya kazi kubwa ambayo imeleta tija kwa wafugaji kwa kuongeza uzalishaji wa maziwa na kuongeza kipato chao.
Msimamizi Mkuu wa Mradi wa ADGG, Dkt. Daniel Mwakihangilo amesema wamekuwa wakiwashauri wafugaji juu ya matumizi ya mbegu bora za ng’ombe wa maziwa ikiwa ni pamoja na matumizi ya madume bora ambayo yanapatikana katika maeneo wanayoishi na kwa kutumia njia ya uhimilishaji ili wapate ng’ombe wenye uwezo wa kutoa maziwa mengi.
Mratibu wa mradi wa ADGG na Mtafiti wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Duniani, Dkt. Eliamoni Lyatuu amesema kwanza walikuwa na lengo la kuwa na mfumo wa ukusanyaji wa taarifa za mifugo, pili kuweza kurejesha mrejesho kwa wafugaji pale wanapokuwa na maswali au maoni na tatu ni kuipanga mifugo kulingana na ubora wake ili kuwasaidia wafugaji kupata mifugo sahihi yenye uwezo wa kutoa maziwa mengi.
Akizungumzia kuhusu mradi huu, Bi. Yusta Elisha ambaye ni mfugaji wa ng’ombe wa maziwa amesema kupitia mradi wa ADGG wameweza kupata maelekezo juu ya ufugaji bora, wamekuwa wakipata ujembe kupitia simu juu ya namna ya kuendeleza shughuli zao za ufugaji ambazo zimewasaidi kuongeza uzalishaji wa maziwa tofauti na kiwango cha maziwa walichokuwa wakikipata kipindi cha nyuma ambapo kwa sasa wanapata lita 20 kwa siku tofauti na lita kumi walizokuwa wakipata kabla ya mradi.
ASKARI POLISI AMUUA KWA KUMPIGA RISASI JAMAA WAKIGOMBANIA MWANAMKE
Afisa huyo Titus Kipchirchiri Kirui anasemekana kumpiga risasi Charles Karugu Kikuyu mwenye umri wa miaka 32 kwa madai kwamba alikuwa akimnyemelea mpenzi wake.
Kulingana na ripoti ya polisi, Maafisa wenzake wa polisi kutoka Embakasi waliofika katika eneo la tukio waliupata mwili wa Kikuyu ukielea kwenye damu sakafuni katika buchari moja mtaani Embakasi.
Kikuyu alikimbizwa katika hospitali ya Mama Lucy lakini alifariki dunia kabla ya kuhudumiwa, upasuaji wa maiti unatarajiwa kufanywa wakati wowote. Kirui alikamatwa baadaye na yuko kizuizini huku uchunguzi zaidi ukiendelea.
Maafisa wa polisi walipata risasi moja ambayo itatumika kama ushahidi katika kesi dhidi ya Kirui.
Chanzo - Tuko news
MKURUGENZI MKUU TBS DKT NGENYA ATOA WITO KWA WATANZANIA WASINUNUE BIDHAA BILA KUHAKIKISHA INA ALAMA YA UBORA
MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Dkt Yusuph Ngenya akizungumza na waandishi wa habari |
NA OSCAR ASSENGA, TANGA
MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Dkt Yusuph Ngenya ametoa wito kwa watanzania wasinunue bidhaa yoyote bila kuhakikisha kwamba ina alama ya ubora kwa bidhaa zinazozalishwa nchini.
Ngenya aliyasema hayo eneo la Mwahako Jijini Tanga kunakoendelea maonyesho ya nane ya Biashara ambapo alisema hatua hiyo itasaidia kuwaondolea hasara ambazo wamekuwa wakikumbana nazo kutokana na bidhaa wanazonunua kutokuwa na ubora unaotakiwa.
Alisema kwani bidhaa zimekuwa na athari nyingi katika matumizi ya binadamu hiyo ni muhimu watanzania kutambua kwamba wanaponunua bidhaa wanapaswa kuzikagua na kuona kama zina ubora unaotakiwa ili kuweza kuepukana na majanga ambayo yanaweza kuwakuta kutokana na bidhaa feki.
“Lakini hata katika operesheni zetu ambazo tumekuwa tukizifanya tunagundua bidhaa gani ambazo zinaingizwa kwenye masoko na hazina ubora ikiwemo bidhaa za ujenzi ,vifaa vya umeme vingi vinakuja feki hivyo tujitahidi kuvitambua na kuviondoa kwenye soko kwani mfano vifaa vya umeme madhara yake vinaweza kushika moto na kuweza kuharibu mali”Alisema Mkurugenzi huyo wa TBS
Akizungumzia lengo la uwepo wao kwenye maonyesho hayo ya nane ya biashara alisema wapo kwa ajili ya kuwaelimisha wananchi kuhusu shughuli za TBS na namna ya kupata huduma zao
“TBS pamoja na mambo megine kwenye maonyesho kama haya tunawakaribisha wananchi kuweza kuwaelimisha kwa mfano wale wanaotaka kupata huduma za TBS ikiwemo bidhaa zao ziweze kupata alama ya ubora lakini pia tunashughulikia uuzaji wa bidhaa za chakula na vipodozi kuweza kupata usajili wa shughuli zao”Alisema Mkurugenzi huyo mkuu wa TBS.
Hata hivyo aliwataka wajasiriamali watengenezaji wa bidhaa ndogo ndogo ni rahisi kwanza kwenda sido kupata mafunzo ambayo yatawasaidia kupata cheti kitachowawezesha kupata barua kutoka sido na baadae waende TBS kuweza kutambulika na wao watafanya kazi iliyobakia mpaka kuhakikisha bidhaa yao inapata ubora.
Mwisho.
SERIKALI KUENDELEA KUWAWEZESHA WAJASIRIAMALI NA WAFANYABIASHARA WADOGO WADOGO NCHINI
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil T. Abdallah, akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa Mafundi Cherehani Dodoma (UMACHEDO) uliofanyika jijini Dodoma alipokuwaa akimuwakilisha Waziri wa Viwanda na Biashara Prof.Kitila Mkumbo
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil T. Abdallah,akisisitiza jambo kwa washiri wa Mkutano Mkuu wa Mafundi Cherehani Dodoma (UMACHEDO) uliofanyika jijini Dodoma alipokuwaa akimuwakilisha Waziri wa Viwanda na Biashara Prof.Kitila Mkumbo
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka ,akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Mafundi Cherehani Dodoma (UMACHEDO) uliofanyika jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil T. Abdallah,akifurahia jambo na Mlezi wa umoja wa Mafundi Cherehani Dodoma ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mhe.Anthony Mavunde (katikati) ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka wakati wa Mkutano Mkuu wa Mafundi Cherehani Dodoma (UMACHEDO) uliofanyika jijini Dodoma alipokuwaa akimuwakilisha Waziri wa Viwanda na Biashara Prof.Kitila Mkumbo
Baadhi ya washiriki wakifatilia hotuba ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil T. Abdallah,(hayupo pichani) wakati akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Mafundi Cherehani Dodoma (UMACHEDO) uliofanyika jijini Dodoma alipokuwaa akimuwakilisha Waziri wa Viwanda na Biashara Prof.Kitila Mkumbo.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil T. Abdallah,akifatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa katika Mkutano Mkuu wa Mafundi Cherehani Dodoma (UMACHEDO) uliofanyika jijini Dodoma alipokuwaa akimuwakilisha Waziri wa Viwanda na Biashara Prof.Kitila Mkumbo.
Mlezi wa umoja wa Mafundi Cherehani Dodoma ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mhe.Anthony Mavunde akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa Mafundi Cherehani Dodoma (UMACHEDO) uliofanyika jijini Dodoma
Mwenyekiti wa umoja wa Mafundi Cherehani Dodoma (UMACHEDO) Bw.Sadoki Kasuka,akielezea umuhimu wa umoja huo wakati wa Mkutano Mkuu wa Mafundi Cherehani Dodoma (UMACHEDO) uliofanyika jijini Dodoma
Mlezi wa umoja wa Mafundi Cherehani Dodoma ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mhe.Anthony Mavunde akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka wakati wa Mkutano Mkuu wa Mafundi Cherehani Dodoma (UMACHEDO) uliofanyika jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna,Dodoma
NAIBU Katibu Mkuu wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah,amesema kuwa Serikali itaendelea kuwezesha wajasiriamali na wafanyabiashara wadogo kupata mafunzo ya kuendesha shughuli zao pamoja na kuwapatia mitaji ili kutimiza azma ya serikali ya viwanda.
Dkt.Abdallah ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mafundi Cherehani Dodoma (UMACHEDO) uliofanyika jijini Dodoma.
Dk. Abdallah amesema kuwa serikali ipo tayari kuwezesha wajasiriamali kufanya shughuli zao bila ya kuwepo na kikwazo chochote kwa mujibu wa sheria ili waweze kufikia malengo yao.
“Wajasiriamali wamekuwa wakilalamika kuwa moja kati ya changamoto wanazokabiliana nazo ni pamoja na elimu ya biashara pamoja na mitaji, hili sisi kama serikali tutahakikisha tunalifanyia kazi kupitia taasisi yetu ya Sido kwa kuendesha mafunzo na kutoa mitaji kwa kuzingitia vigezo”amesema Dk. Abdallah
Pia amesema kuwa pamoja na kutoa mitaji na elimu pia kupitia Sido wataendelea kuwezesha wajasiriamali nyenzo zenye ubora ili kuzalisha bidhaa zenye ubora.
“Mfuko wetu wa kuwezesha wajasiriamali unaouwezo kwa kila mtu ambaye atakidhi vigezo kukopeshwa kiasi cha Sh. milioni tano lakini pia serikali kupitia shirika la NSSF na Sido wameingia makubalinaoa na benki ya Azania ili kukopesha mtaji wajasiriamali kiasi cha Sh. miliini 50 hadi 100”amesisitiza
Hata hivyo amesema kuwa serikali inaendelea kuwasilina na mamlaka husika katika maeneo mbalimbali nchini ili kupata maeneo rasmi ambayo yatatengwa kwa ajili ya wajasiriamali kufanya kushughuli zao.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Antony Mtaka amewataka wajasiriamali wa mkoa wa Dodoma, kuwa wabunifu katika shughuli zao za kila siku ili kulikamata soko la bidhaa zao.
“Msipokuwa makini ujio wa makao makuu ya serikali nyinyi manaweza kuwa waangaliaji tu na fursa zote wakachukua wageni hivyo basi mnapaswa kuvaa sura za kazi ili mfikie malengo yenu kwa kubani zaidi bidhaa”amesema Mtaka
Awali Mlezi wa umoja wa mafundi cherehani ambaye ni mbunge wa Dodoma mjini, Antony Mavunde amesema kuwa tayari jiji la Dodoma limetenga ekari 8 kwa ajili ya wajasiriamali ili waweze kukidhi mahitaji yao.
“Tumetenga kiasi hicho cha eneo lakini pia na fedha ya kuanzia kiasi cha Sh. milioni 600 kwa ajili ya kuandaa eneo hili kwa ajili ya wajasirimali katika maeneo ya Nzunguni jijini Dodoma”amesema Mavunde