SERIKALI imewaonya wakuu wote wa Taasisi za Serikali ambao wamekuwa wakianzisha mifumo ya kimtandao bila kuzingatia kanuni,Sheria na taratibu zinazoongozwa kwa misingi ya sheria ya Serikali Mtandao namba 10 ya mwaka 2019 na kanuni zake za mwaka 2020'
Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Mohamed Mchengerwa jijini Dar es Salaama wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea ofisi hiyo na kuzungumza na watumishi wa Mamlaka hiyo ya Serikali Mtandao ambapo pia amewaonya wakuu wa Taasisi za umma nchini wenye lengo la kujitoa katika matumizi ya mifumo iliyotengenezwa na Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) na kusema kuwa kufanya hivyo ni kosa kwa mujibu wa Sheria
''Ninafahamu kuna baadhi ya Taasisi za Serikali kushirikiana na wadau wao wanaotaka kujitoa katika matumizi ya mifumo inayotengenezwa na eGA,kujitoa katika mifumo ambayo tayari tumeirasimisha kwa misingi ya sheria ya Serikali Mtandao namba 10 ya mwaka 2019 na kanuni zake za mwaka 2020 ni kinyume cha Sheria''Alisema Waziri wa Mchengerwa
''Nitoe rai na onyo kwa wakuu wote wa Taasisi za Serikali kuwa hakuna Taasisi wala Ofisi yoyote ya Serikali ambayo inaruhusiwa kujitoa kwenye mifumoinayosimamiwa na eGA''Aliongeza Waziri Mchengerwa
Aidha pia ameiagiza eGA kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuhakikisha wanadhibiti uvujaji wa siri lakini pia utolewaji wa taarifa ambazo hazistahili kwenda moja kwa moja kwa watumiaji wa kawaida
Vile vile ameipongeza eGA kwa jitihada kubwa wanazofanya za kuendelea kubuni mifumo ambayo ina rahisisha utendaji kazi Serikalini ambapo pia amewasihi kuendelea kutekeleza jukumu hilo kwa kuzingatia kasi ya Serikali ya Awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) Mhandisi Benedict Ndomba yeye ametaja baadhi ya athari zinazoweza kujitokeza endapo Taasisi za umma hazitopeleka taarifa za mifumo inayoanzisha kuwa ni pamoja na kutokufata viwango na miongozo jambo linalopelekea mifumo kutowasiliana
Thursday, 20 May 2021
Serikali Yawaonya Wakuu Wa Taasisi Wanaoanzisha Mifumo Bila Kuzingatia Sheria
Prof. Mkumbo Aongoza Kikao Cha 32 Cha Bodi Ya Wakurugenzi Wa EPZA
Waziri wa Viwanda na Biashara na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa EPZA, Prof. Kitila Mkumbo ameongoza kikao cha kawaida cha 32 cha bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uzalishaji kwa Mauzo ya nje (Export Processing Zones Authorty -EPZA).
Kikao kimefanyika Mei 19, 2021 Jijini Dodoma katika ukumbi wa Mkutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Jengo la Mkapa na kimeudhuliwa na viongozi mbalimbali; Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe, Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Dotto James, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil Abdallah, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EPZA, Mathew Mnali na wajumbe wengine wa bodi ya wakurugenzi wa EPZA.
Kikao hicho kimekuwa na lengo la kujadili mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ripoti ya Mkurugenzi wa EPZA kwa kipindi cha Januari – Machi 2021, Makadirio ya mapato na matumizi ya Mamlaka ya (EPZA) kwa mwaka 2021/2022, utaratibu wa kuendeleza Mradi wa kurasini SEZ, mradi wa kubangua korosho kwa kushirikiana na wajasiriamali (SMEs) na mengineyo
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni kufanya ziara ya kikazi ya siku moja Hapa Nchini
Akiwa nchini Mhe. Rais Museveni na Mhe. Rais Samia watashuhudia utiaji saini wa mikataba ya bomba la mafuta la Hoima - Tanga kati ya Tanzania na kampuni za uwekezaji katika mradi huo.
Rais wa Uganda, Mhe. Museveni leo Mei 20, 2021 atafanya ziara ya kikazi ya siku 1 hapa nchini.
— Gerson Msigwa (@MsigwaGerson) May 20, 2021
Akiwa nchini Mhe. Rais Museveni na Mhe. Rais Samia watashuhudia utiaji saini wa mikataba ya bomba la mafuta la Hoima - Tanga kati ya Tanzania na kampuni za uwekezaji katika mradi huo. pic.twitter.com/z5blE4olJl
Rais Samia amteua Brigedia Generali Nduku Mabele kuwa Mkuu wa JKT, na Kanali Lyanga Shausi kuwa Mkurugenzi wa SUMA - JKT
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Brigedia Jenerali Rajabu Mabele
**
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan tarehe 19 Mei 2021 amemteua Brigedia Jenerali Rajabu Nduku Mabele kuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa. Hatua hiyo inafuatia kuteuliwa kwa aliyekuwa Mkuu wa Jeshi hilo, Meja Jenerali Charles Mbugekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera hivi karibuni.
Brigedia Jenerali Mabele alijiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania tarehe 25 Novemba 1993 na kutunukiwa Kamisheni kuwa Afisa tarehe 25 Machi 1995. Pamoja na taaluma nyingine za Kijeshi, Jenerali Mabele ana Shahada ya Uzamili katika Usimamizi wa Biashara (Master of Business Administration), alijikita katika Usimamizi wa Mashirika (Corporate Management).
Katika utumishi wake Brigedia Jenerali Mabele amewahi kushika nyadhifa mbalimbali zikiwemo Afisa Usalama na Utambuzi katika Vikosi kadhaa; Afisa Mnadhimu Malipo na Afisa Malipo wa Kikosi Makao Makuu ya Jeshi; Mkurugenzi wa Fedha za Umma na Uhasibu (Director for Public Finance and Accounting) na baadae alihamishiwa Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA-JKT), nafasi aliyohudumu hadi kuteuliwa kwake kuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa.
Sambamba na uteuzi huo, Mhe. Rais amemteua pia Kanali Absolomon Lyanga Shausi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa SUMA-JKT. Kabla ya uteuzi huo Kanali Shausi alikuwa Naibu Mkurugenzi wa Shirika hilo.
Kwa niaba ya Maafisa, Askari na Watumishi wa Umma, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Salvatory Mabeyo anawapongeza Brigedia Jenerali Mabele na Kanali Shausi kwa kuaminiwa katika nyaadhifa hizo na kuwatakia heri na fanaka katika utendaji wao.
Pakistan, Iran Zaahidi Kuimarisha Diplomasia Ya Uchumi
Na Mwandishi wetu
Pakistan na Iran zimeahidi kuendelea kuimarisha diplomasia ya uchumi na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa maslahi mapana ya pande zote.
Ahadi hizo zimetolewa kwa nyakati tofauti wakati Mabalozi wa Pakistan na Iran walipokutana kwa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.
Mabalozi waliokutana na Waziri Mulamula ni Balozi wa Pakistani hapa nchini Mhe. Mohammad Saleem pamoja na Kaimu Balozi wa Irani hapa nchini Mhe. Hossein Alvandi Behineh ambapo viongozi hao wamejadili masuala ya kuimarisha uhusiano baina ya Tanzania na Nchi zao lakini pia kuimarisha na kuboresha diplomasia ya uchumi kwa maslahi mapana ya nchi zote.
Pamoja na mambo mengine, Balozi wa Pakistan Mhe. Saleem ameelezea kufurahishwa na uhusiano mzuri uliopo baina ya Iran na Tanzania na amepongeza hatua mbalimbali ambazo Serikali ya Tanzania imeendelea kuzichukua katika kuimarisha diplomasia ya uchumi.
Nae Kaimu Balozi wa Iran amesisitiza juu ya uwekezaji na biashara ambapo amesema kuwa Serikali yake ipo tayari kufanya biashara na Tanzania na kuinua uchumi wa wananchi wan chi zote mbili.
Kwa upande wake Balozi Liberata Mulamula (Mb) amewahakikishia mazingira salama ya biashara na uwekezaji na kuwaahidi ushirikiano wa kutosha kutoka Tanzania.
Kadhalika, Waziri Mulamula amesema ushirikiano wa diplomasia ya uchumi kati ya Tanzania na Pakistan unatoa fursa nyingi ikiwemo kukuza biashara hasa katika sekta ya kilimo ikiwemo chai, pamba, korosho, mbegu za mafuta, Madini ya Tanzanite, pamoja na uwekezaji.
Program Support Specialist at Compassion International
This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content
The role of Program Health Support Specialist will provide subject matter expertise regarding the health of all program beneficiaries (pregnancy through youth). This role will collaborate with other Support Specialists, Program Trainers and Partnership Facilitators to ensure staff and Frontline Church Partners (FCP) are adequately informed and equipped to ensure preventative and curative care for all beneficiaries. […]
This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details
Fieldworker (2 posts) at Ifakara Health Institute 2021
This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content
Job Summary Position: Fieldworker (2 posts) Reports To: Project Leader/Supervisor Work Station: Mtwara Institute Overview Ifakara Health Institute (IHI) is a leading research organization in Africa with a strong track record in developing, testing and validating innovations for health. Driven by a core strategic mandate for research, training and services, the […]
This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details
Research Scientist at Ifakara Health Institute
This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content
Job Summary Position: Research Scientist (1 post) Reports To: Principal Investigator Work Station: Rufiji/Kibiti Institute Overview Ifakara Health Institute (IHI) is a leading research organization in Africa with a strong track record in developing, testing and validating innovations for health. Driven by a core strategic mandate for research, training and services, the Institute’s […]
This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details
Field Supervisor at Ifakara Health Institute
This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content
Job Summary Position: Field Supervisor (1 post) Reports To: Project Leader Work Station: Mtwara Institute Overview Ifakara Health Institute (IHI) is a leading research organization in Africa with a strong track record in developing, testing and validating innovations for health. Driven by a core strategic mandate for research, training and services, […]
This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details
Wednesday, 19 May 2021
MHANDISI MALONGO AWATAKA WAHANDISI KUTEMBELEA MIRADI MIKUBWA....AFUNGUA MAFUNZO YA SIKU TATU
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi) Mhandisi Joseph Malongo,akifungua mafunzo ya Wahandisi yanayofanyika kwa siku tatu kuanzia leo Mei 19 hadi 21,2021 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi) Mhandisi Joseph Malongo,akisisitiza jambo kwa washiriki wa mafunzo ya Wahandisi yanayofanyika kwa siku tatu kuanzia leo Mei 19 hadi 21,2021 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi) Mhandisi Joseph Malongo,akizungumza na washiriki (hawapo pichani) wakati wa mafunzo ya Wahandisi yanayofanyika kwa siku tatu kuanzia leo Mei 19 hadi 21,2021 jijini Dodoma.
Baadhi ya Wahandisi wakifatilia hotuba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi) Mhandisi Joseph Malongo,(hayupo pichani) wakati akifungua mafunzo ya Wahandisi yanayofanyika kwa siku tatu kuanzia leo Mei 19 hadi 21,2021 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wahandisi,Mhandisi Ninatubu Lema,akizungumza wakati wa mafunzo ya Wahandisi yanayofanyika kwa siku tatu jijini Dodoma kuanzia leo Mei 19 hadi 21,2021.
Msajili wa Bodi ya Wahandisi,Mhandisi Patrick Barozi,akielezea lengo la mafunzo hayo ya Wahandisi yanayofanyika kwa siku tatu jijini Dodoma kuanzia leo Mei 19 hadi 21,2021.
Msajili wa Bodi ya Wahandisi,Mhandisi Patrick Barozi,akionyesha kitabu chenye mwongozo wakati wa mafunzo ya Wahandisi yanayofanyika kwa siku tatu jijini Dodoma kuanzia leo Mei 19 hadi 21,2021.
Na.Alex Sonna,Dodoma
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Malongo,amefungua mafunzo ya siku tatu ya Wahandishi wenye lengo la kujadili miradi ya kimkakati ili iweze kusaidia Taifa katika utekelezaji na usimamizi wa miradi hiyo huku akiwataka kutembelea miradi mikubwa nchini ili kujionea changamoto zilizopo.
Akizungumza leo Mei 19,2021 wakati akifungua mafunzo hayo kuhusu uendeshaji wa maswala ya miradi ya kimkakati kwa wahandisi itakayosaidia kukidhi mahitaji ya watanzania yalioandaliwa na Bodi ya Usajili wa Wahandisi nchini (ERB) yanayofanyika kwa siku tatu jijini Dodoma.
Mhandisi Malongo amesema kuwa Serikali imewekeza kwa kiasi kikubwa kwenye sekta ya ujenzi hivyo wahandisi wanatakiwa kupata elimu ili kukabiliana na malalamiko kwa Wahandisi kwenye utekelezaji wa miardi yao.
Amewataka kuanzisha mafunzo yajayo yasihusishe wahandisi pekee bali ihusishe wote wanaofanya miradi kutimia.
“Ni vizuri tukianzisha mafunzo mengine tuhakikishe kuwa wahandisi, watunza fedha na wanasiasa watakuwepo ili kuwe na mchanganuo mzuri wa mawazo” amesema Mhandisi Malongo
Hata hivyo ameipoongeza bodi ya usajili wa wahandisi (ERB) kwa kuanzisha mafunzo hayo badala ya kuitegemea serikali kujiendeleza kitaaluma kwani ilikuwa inawarudisha nyuma wahandisi.
Aidha amewaomba wahandisi kuanza kutembelea miradi mikubwa inayoendelea nchini ili kujifunza changamoto zilizopo na kuzipatia ufumbuzi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wahandisi Ninatubu Lema amesema kuwa mafunzo hayo yatawajengea uwezo wahandisi kuhusu nini kifanyike katika kuendana na kasi ya teknolojia huku kuwaongezea elimu kuibua, kusimamia miradi ya kimkakati itakayoleta tija kwa Taifa.
Awali Msajili wa Wahandisi, Mhandisi Patrick Barozi, amesema kuwa mafunzo ya usimamizi wa miradi yataendelea kutolewa ili kuimarisha uwezo wa wahandisi nchini na kuwataka wahandisi wenye sifa kujisajili na Bodi hiyo.
Picha : MAMIA WAMIMINIKA KUSAKA UMEME 'LUKU' TANESCO SHINYANGA
Tyre Fitter at dangote
This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content
Description Key Duties and Responsibilities · Inspect tire casing for defects such as holes and tears. · Rotate tires to different positions on vehicles, using hand tools · Prepare rims and wheel drums for reassembly. · Reassemble tires onto wheels. · Tire scrap analysis · Tire retreading · Tire care and tire management · Seal […]
This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details
Public Health Administrative Management Assistant (Finance) at U.S. Embassy Dar es Salaam
This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content
The U.S. Mission in Dar es Salaam is seeking eligible and qualified applicants for the position below. Position Title: Public Health Administrative Management Assistant (Finance) Vacancy Number: DaresSalaam-2021 -021 Duties Extramural Budget Execution/Analysis/Management 35% Provides expert technical advice to implementing partners in the development of long and short term financial strategies and plans to achieve […]
This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

































