Thursday, 13 May 2021

Watatu washikiliwa kwa tuhuma za mauaji Moshi


 Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro linawashikilia watuhumiwa watatu kwa madai ya kuhusika na tukio la mauaji ya kijana wa bodaboda, Rogers Kesy, mkazi wa Mnazi- Kiboroloni, Manispaa ya Moshi.


Akisimulia tukio hilo mbele ya waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Amon Kakwale amesema mmoja wa watuhumiwa, Sifael Sarun alimkodisha marehemu ampeleke nyumbani kwake lakini baada ya kufikishwa nyumbani alimuua kijana huyo kwa kumpiga na nyundo kichwani na kisha kumnyonga na waya shingoni.

Kamanda Kakwale amesema mara baada ya mtuhumiwa huyo kutekeleza mauaji hayo waliuweka mwili wa kijana huyo kwenye mfuko wa sandarusi na kuutupa pembeni mwa barabara kuu ya Moshi - Himo.

Amesema Sifael Sarun alishirikiana na wenzake wawili Emanuel Sarun na Elia Laizer ambao wote wako chini ya ulinzi wa Jeshi la Polisi na kuwa uchunguzi utakapokamilika watafikishwa Mahakamani.

Aidha, amesema Jeshi la Polisi limefanikiwa kukamata pikipiki yenye namba MC 880 AYR ambayo ilitumika kubeba mwili wa marehemu na kwenda kuutupa barabarani.




Share:

Mwalimu atuhumiwa kufanya mapenz kitanda kimoja na wanafunzi wawili

Mkuu wa  Wilaya  ya Magu mkoani Mwanza, Salim Kali, ameagiza kuhamishwa  wilayani kwake mwalimu anayetuhumiwa  kufanya mapenzi na wanafunzi watatu wa kike wa shule ya msingi ya Ilungu  katika kitanda kimoja.

Mwalimu huyo aliyetajwa na Mkuu wa wilaya kwa jina la Martin  Mambosasa anadaiwa kufanya vitendo hivyo kwa nyakati tofauti kwa miaka saba.

Mkuu huyo wa wilaya, alisema mwalimu huyo aliwahi kukamatwa na vyombo vya  dola na kufikshwa mahakamani, lakini akahonga wazazi wa watoto hao wakaharibu ushahidi.

Alitoa agizo hilo juzi kwenye kongamano la kuweka mikakati ya kukabiliana na ongezeko la vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto, mimba katika umri  mdogo na utoro kwa wanafunzi.

Alisema  mikakati hiyo itasaidia  kuongeza ufaulu na kwamba  mwaka 2020, takwimu zinaonyesha matukio ya ukatili wa kijinsia yalikuwa 304.

Alimuagiza mratibu Elimu wa  kata na ofisa elimu wa wilaya kumhamishia mwalimu huyo  sehemu nyingine Ili asionekane wilayani kwake.

"Huyu mwalimu amekuwa akidhalilisha watoto wadogo kwa kipindi kirefu na naagiza ahamishwe sitaki kumsikia wala kumuona hapa wilayani kwangu," alisema

Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii wa  Wilaya ya  Magu,  Amandus Mboya alisema  mambo yanayochangia ongezeko la vitendo vya ukatili wa kijinsia ni pamoja na wazazi kushindwa kuwapatia huduma muhimu.

Alitaja huduma zingine wanazokosa kuwa ni pamoja na kukosa taulo za kike, mafuta ya kupaka pamoja  na kukosa fedha za kunyoa nywele 

 

Credit:Nipashe




Share:

Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) Kusogeza Huduma Kwenye Kanda

 


Na Asteria Muhozya, Ruvuma
Imeelezwa kuwa, Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) inatarajia kuongeza wigo wa huduma kwa kuanzisha Vituo vya Huduma za Maabara na Ushauri Elekezi katika Kanda zenye uzalishaji wa Madini kwa wingi.

Hayo yamebainishwa Mei 12, 2021 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila wakati akifungua mafunzo kwa wachimbaji wadogo wa madini ya mwongozo wa namna bora ya uchukuaji wa sampuli za uchunguzi na uchenjuaji madini  Mkoani Ruvuma.

Prof. Msanjila ameongeza kuwa, hivi karibuni GST itaanza kutoa huduma hizo katika Mkoa wa Geita na baadaye Chunya, na hivyo kuwataka wachimbaji wadogo nchini kuitumia vyema taasisi hiyo kutokana na manufaa watakayoyapata kutoka kwa wataalam wenye ujuzi na waliobobea katika fani mbalimbali katika Sekta ya Madini.

‘’Ni muda muafaka sasa kushirikiana na GST kwa karibu zaidi kwa kuanza kuchukua sampuli zitakazozingatia mafunzo haya na kuziwasilisha maabara ya GST kwa huduma bora na majibu ya uhakika ikizingatiwa kwamba, maabara ya GST inatambuliwa kimataifa kwa kuwa na ITHIBATI ya ubora katika uchunguzi wa dhahabu,’’ amesisistiza Prof. Msanjila.

Ameongeza kwamba, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu inatambua umuhimu wa wachimbaji wadogo, hivyo, kutokana na wajibu wa GST katika kuhakikisha sekta inafanya vizuri imepelekea kufanyika kwa mafunzo hayo ambayo yanalenga kuwasaidia wachimbaji wadogo kuondokana na uchimbaji wa kubahatisha kwa kufanya uchimbaji endelevu na wenye tija ili kuwasaidia wachimbaji kuongeza uzalishaji na hatimaye kuongeza mchango wao kwenye pato la taifa ambao  hivi sasa bado ni mdogo .

Aidha, Prof. Msanjila ameipongeza GST kwa jitihada inazozifanya katika kuwasaidia wachimbaji wadogo nchini ikiwemo kuwa karibu nao kwa kuwapatia elimu mbalimbali zinazohusiana na masuala ya madini kupitia machapisho, vitabu, huduma za maabara, ushauri elekezi na mafunzo mbalimbali yakiwemo hayo ambayo  yanatolewa katika maeneo mbalimbali nchini.

Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu Prof. Msanjila ameipongeza Ofisi ya Madini Mkoa wa Ruvuma kwa kuvuka lengo la makusanyo katika Mwaka wa Fedha 2020/2021 ambapo hadi kufikia mwezi Aprili, 2021 imekusanya shilingi bilioni 8.9 sawa na asilimia 141 na hivyo kuvuka lengo la kukusanya shilingi  bilioni 7.5 iliyopangiwa kukusanya.

‘’ Nipende kuwaambia mnafanya kazi nzuri sana. Kama wizara, tunajua Ruvuma mnafanya vizuri ndiyo sababu hata migogoro hakuna. Nawaomba pamoja na kuendelea na majukumu yenu lakini mzidi kujiendeleza kielimu,’’ amesisitiza Prof. Msanjila.

Kwa upande wake, Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma Steven Ndaki ameipongeza wizara

na GST kwa kuwezesha mafunzo hayo kufanyika mkoani humo na kueleza kwamba, yatawawezesha wachimbaji kufanya shughuli zao kwa uhakika. Aidha, ameipongeza wizara kwa kuanzisha masoko ya madini mkoani humo hivyo kurahisisha biashara ya madini.

Naye, Mwenyekiti  wa Chama Cha Wachimbaji Wadogo Mkoa wa Ruvuma , Issack Ngaladela ameishukuru GST kuwezesha mafunzo hayo na kusema kuwa, awali wachimbaji walikuwa wanachimba kwa hisia na kwa miaka mingi imewapelekea kupoteza muda mwingi na mitaji. ‘’ Mafunzo haya yatatubadilisha, sasa tutachimba kisayansi,’’ amesema.

Mbali na wachimbaji, katika siku ya kwanza mafunzo hayo pia  yamewashirikisha  Wakuu wa Wilaya za Mkoa huo, Makatibu Tawala na viongozi wa wachimbaji wa mkoa husika.

Vilevile, katika ziara hiyo pia, Prof, Msanjila ametembelea Mgodi wa wachimbaji wadogo wa Makaa ya Mawe wa GodMwanga uliopo katika kijiji cha Malinyi wilaya ya Nyasa kwa lengo la kusikiliza changamoto na kushauri namna bora ya kufanya shughuli zao.


Share:

VIDEO : Wini Ft. Darassa – I Do

 VIDEO : Wini Ft. Darassa – I Do



Share:

Ntobo Mik 1....Ni Dawa Ya Asili ya Vidonda Vya Tumbo Iliyofanyiwa Utafiti Kwa Miaka Mingi


 NTOBO MIK 1
Ni Dawa ya vidonda vya tumbo iliyofanyiwa utafiti kwa miaka mingi  mwanga wa matumaini kwa wanao teseka na Vidonda vya Tumbo.

Huwezi kuzungumzia magonjwa yanayotesa Jamii ya watu wengi Duniani bila kuzungumzia Vidonda vya Tumbo.

Ugonjwa huu husababishwa na aina ya bakteria anayeitwa kwa jina la HP (Helicobacter Palory) mtu hujikuta anateseka na maumivu makali ya Tumbo bila kujuwa kuwa ni vidonda vya tumbo

DALILI ZAKE:
1.     Tumbo kuwaka moto
2.     Tumbo kujaa gesi au haja kubwa kuwa ngumu
3.     Kutokupata choo vizuri
4.     Kiungulia cha mara kwa mara
5.     Kichwa kuuma
6.     Maumivu makali ya tumbo lajuu wengi huuita chembe ya moyo
7.     Kukosa hamu ya kula
8.     Kizunguzungu
9.     Kichefu chefu

Ugonjwa huu ukishamili sana mgonjwa hujikuta anatapika damu au kujisaidia choo chenye mchanganyiko na damu.

Nini suluhisho;
BABU MADUHU MTAALAMU MWENYE UWEZO MKUBWA WA KUTIBU VIDONDA VYA TUMBO
BABU MADUHU ANAPATIKANA MAGOMENI MOROCCO HOTEL KITUO CHA KANISANI
PIGA SIMU NO. 0755 684 297/ +255 652 102 152 (WHATSAPP)

 




Share:

RC SHIGELLA AKABIDHI ZAWADI ZA EID EL FITR KWA MAKUNDI MATATU MAALUMU MKOANI TANGA

MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella katikati aliyevaa suti akimkabidhi Msaada wa Chakula kwa ajili ya sikuu ya Eid El Fitr Afisa Mfawidhi wa Makazi ya Wazee Wasiojiwezea Msufini Muheza Anna Mgelwa kushoto ambapo msaada huo ulitolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga (RAS) Judica Omari
MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella katikati aliyevaa suti akiendelea kukabidhi Msaada wa Chakula kwa ajili ya sikuu ya Eid El Fitr ambapo msaada huo ulitolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga (RAS) Judica Omari
MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella katikati aliyevaa suti akiendelea kukabidhi Msaada wa Chakula kwa ajili ya sikuu ya Eid El Fitr ambapo msaada huo ulitolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga (RAS) Judica Omari
MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga (RAS) Judica Omari
MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella katikati akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kukabidhi msaada huo wa pili kutoka kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga (RAS) Judica Omari




MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella ametoa msaada wa chakula na vifaa mbalimbali kwa makundi ya watu wenye mahitaji maalumu mkoani humo vyenye thamani ya Sh .Milioni 3.6 kwa ajili ya sikukuu ya Eid El Fitri.

Msaada huo umekabidhiwa kwenye makundi hayo maalumu ya watu wenye mahitaji maalumu kupitia kituo cha Wazee cha Mwanzange,Misufini na kituo cha Kulea Watoto wenye mahitaji maalumu kilichopo eneo la Pongwe Jijini Tanga katika halfa iliyofanyika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga.

Msaada uliotolewa ni pamoja na Mbuzi wa tano,mchele,mafuta ya kula,sabuni,mashuka,mavazi na vyengine kwa ajili ya huduma za afya ikiwemo Taulo za kike na pampasi.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo,RC Shigella alisema kwamba wameamua kutoa msaada huo ili kuwawezesha makundi hayo maalumu waweze kusheherekea sikuuu ya Eid El Fitri  vema kwa kuwawezesha mahitaji hayo muhimu

Alisema wameona waweke utaratibu huo mzuri zaidi badala ya kuwaalika na kula nao pamoja wakaona waandae kutengeneza chakula kwa ajili ya sikukuu wakiwa kwenye maeneo hayo kwa kusheherekea.

“Nimpongeze Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Judica Omari na Menejimenti ya Ofisi kwa utaratibu  huu ambao unaenda kugusa furaha ya ndugu zetu waliopo kwenye mazingira magumu na mazingira ya uhitaji na msaada huu ni mahususi kwa ajili ya Sherehe kwani kipindi cha siku 30 waislamu kote dunia na mkoa wa Tanga wameshiriki kikamilifu kwenye kufunga  na kwenye funga ndio mahala pekee walikuwa wakiwasiliana na mwenyezi mungu kwa ajili ya toba na kuiombea nchi yetu”Alisema

 Mkuu huyo wa Mkoa alisema wanapohitimisha funga wanakuwa na sherehe watu wanasherekea na kuomba baraka wakaona watengeneza utaratibu wa kugusa nafsi na nyoyo za makundi hayo maalumu mkoani Tanga ili angaliu watakaposherehe wasihangaike wapata wapi chakula kwani angalau vitu hivyo vikiwepo wanaweza kusheherekea vizuri.

 “Nitumie nafasi hii kuwapongeza viongozi wa dini kwa namna walivyoshiriki kwenye kipindi cha mwenzi wa ramadhani watu wameendelea kushirikiana hivyo tuendelee kuiweka nchi yetu kwenye maombo ili Rais wetu Samia Suluhu aweze kuyatumiza malengo aliyokusudia kwenye kipindi chake cha awamu ya sita”Alisema RC Shigella.

Hata hivyo aliwatakia waislamu kote nchini na mkoani Tanga maadhimisho mema ya sikukuu ya Eid El Fitri huku akieleza kwamba wataimarisha ulinzi na usalama ili wananchi mahala watakaposhiriki washeherekee kwa usalama,amani na furaha.

Awali akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Judica Omari alisema mkuu wa mkoa ametoa mchango wake kwenye mwezi huu wa ramadhani kwani ameona kama mkoa wasiweze kuishia kimyakimya wao waweze kushiriki kutoa sadaka kwa dugu zao wazee wanaoishi kwenye vituo vya serikali na watoto wanaoisni kwenye mazingira magumu.

Hata hivyo aliwatakia heri ya sikuuu ya Eid El Fitri waislamu wote mkoani Tanga na kuwataka washeherekee kwa utulivu na amani

Naye kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Tanga Imani Clemence alisema vituo ambavyo vimeainishwa kupatiwa mahitaji hayo ni kituo cha Wazee Mwanzange,Kituo cha Wazee Misufini na Kituo cha watoto wenye mahitaji Maalumu cha Pongwe .

Imani alisema mafanikio walioyapata ni Serikali kutenga fedha kwa ajili ya kutatua changamoto nyingi zilizokuwa zinakabili makazi ya wazee mfano huduma ya afya ambapo kwa sasa imetenga fedha kwa ajili ya kununua dawa ambazo hazipatikani hospitalini.

“Lakini mafanikio mengine ni Serikali kutenga fedha kwa ajili ya matumizi madogo ya vituo kama dharura ndogo ndogo zinazojitokeza”Alisema

Share:

RPC MAGILIGIMBA AONYA WAVUNJIFU WA AMANI SIKUKUU YA EID EL-FITR SHINYANGA….ASHUKURU WADAU KWA USHIRIKIANO

Share:

Project Officer – SAUTI Youth Project at World Vision

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

The SAUTI YOUTH Project Officer, will be responsible of  Formation and mobilizing CVA (Citizen Voice Action) Youth groups, To empowers the youth to have the capacity to engage with the communities and monitor relevant government services and policy influence to climate change trough CVA Preparation of Monthly and quarterly project report Monitoring of the groups, […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

NIMEMLIPIA ADA YA CHUO KIKUUU MCHUMBA WANGU NA BAADA YA MASOMO ETI ANATAKA KUOLEWA NA MWANAUME MWINGINE

  Sisi wanaume tunatumia nguvu nyingi katika kutafuta pesa na mtu yoyote akichezea jasho lako haki inauma sana.

Nimi naitwa Mbaraka mkazi wa Gongo la Mboto najishughulisha na Biashara ndogo ndogo hapa mjini. Katika pitapita zangu nilikutana na msichana anaitwa Rehema.Nilimfahamu Rehema kupitia kwa dada yake Zainabu ambaye alikuwa rafiki yangu sana na mteja wangu wa uhakika.

Nilivutiwa sana muonekano na tabia aliyekuwa nayo Rehema hadi ikafika hatua ya kuwa wapenzi.Kipindi nafahamiana nae alikuwa amemaliza kidato cha sita hivyo alikuwa kwa dada yake Zainabu akiwa anasubiri matokeo ya mtihani kutoka.

Kulingana na jinsi tulivyopendana dada yake alikuwa anamruhusu anakuja kazini kwangu na kunisaidia kazi mara kwa mara. Miezi 3 kupita matokeo yalitoka na yeye alikuwa miongoni mwa wenye sifa za kujiunga masomo ya Chuo Kikuu. Kwa Upande wangu nilifurahi sana kuona mke wangu mtajariwa anaenda kujiunga na masomo ya Chuo Kikuu na muda si muda alijiunga na chuo cha Makumira Arusha kwa kozi ya Sheria.

Siku ilipowadia ya kuripot chuoni niliweza kwenda nae hadi chuo na kumpangishia sehemu ambayo atakuwa anaishi. Semister ya kwanza ilipoisha mchumba wangu alirudi Dar na kufikia kwangu maana dada yake na mama yake walikuwa wanafahamu mahusiano yetu na ada ya kujiunga chuo mimi ndiyo nilimlipia mchumba wangu maana mama yake alikuwa amekosa pesa ya kumlipia hata mkopo kutoka kwa serikari hakupewa.

Baada ya likizo alirudi chuo kwa ajili ya semister ya pili ila muda wa kufunga ulipowadia Rehema hakuja Dar au kwenda kwao Mtwara bali alibaki Arusha. Mimi nilifunga safari hadi Arusha nikakaa nae kwa siku mbili tu na kurejea Dar na katika mazungumzo nilimuuliza mbona hukuja Dar akaniambia kuwa semester ya pili ilikuwa ngumu kwake.

Tangu hapo Rehema kuna muda alikuwa anakuja Dar na muda mwingine haji kabisa . Hiyo tabia iliniumiza sana ikabidi nitafute usaidizi ndipo nilikutana na rafiki yangu Amimu na kuniambia kuwa Dr.Kiwanga anaweza nisaidia kwa sababu huyo Dr ndiye alimsaidia yeye na mke wake kupata mtoto baada ya kuhangaika kwa miaka 6 wakitafuta mtoto na bila mafanikio.

Alinipatia namba ya simu ya Dr. Kiwanga ambayo ni +254 769404965. Nilipanga safari kutoka Dar Hadi Kenya kwa Dr. Kiwanga niliweza fika kwenye ofisi ya Kiwangadoctors kisha kueleza shida iliyonileta, .Ndipo niliambiwa kuwa mchumba wangu Rehema kuna Mwalimu ambaye anataka kumuoa baada ya masomo.

Kulingana na maelezo ya Dr Kiwanga asilimi 100 nilikubali maana kuna kipindi mchumba wangu alikuwa anawasiliana na mwalimu moja mara kwa mara nilikuwa nauliza anasema kuwa ni mtu anawasaidia tu wala hakuna kitu kingine.Mwalimu yule mwaka wa kwanza hadi wa nne ila kwa kuwa sikufika chuo kikuu hivyo sikuweza fahamu zaidi.

 Nikiwa ofisini kwake Dr.Kiwanga akaniambia kuwa atanisaidia na relationship spells hadi nimpate Rehema kwa muda wa masaa 48.Baada ya kutoka ofisini kwake haukupita muda Rehema alijileta hadi kwangu na kuomba tufunge ndoa haraka maana kachoka na kusumbuliwa na wanaume,bila kupoteza muda nikijulisha baadhi ya ndugu na Jamaa kisha ndoa ikawepo na kwa sasa tuna watoto wawili na Rehema kanisaidia Biashara yangu kupanda kwa asilimia 75.

Natoa uwito kwa mwenye shida ya mapenzi,kumpata mpenzi wa ndoto zako,Nguvu za kiume,mwenye nuksi na mikosi wasiliana Dr. Kiwanga kwa Namba: +254 769404965 Website: www.kiwangadoctors.com Emails: kiwangadoctors@gmail.com

Share:

Project Manager at North Mara Gold Mine Limited

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

POSITION DESCRIPTION: North Mara Gold Mine Limited is seeking to recruit one (01) Project Manager to join North Mara Gold Mine team. The successful candidate for this role will report to Engineering Manager and the role holder will be involved in initiation, planning, execution, monitoring/control and closure of capital and maintenance-based projects, to meet company business targets in accordance with Barrick […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Data Manager at ASUTA

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Job Title:  Data Manager Job Location: Dar es salaam. Temeke District Organisation: Asasi ya Uwezeshaji Tanzania – ASUTA Asasi ya Uwezeshaji Tanzania – ASUTA working in partnership with FHI 360 on  Epidemic Control (EpiC) which is a global project funded by the U.S. President’s Emergency Plan for AIDS Relief (PEPFAR) and the U.S. Agency for International Development (USAID) […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Wizara Ya Madini Kufanyia Kazi Mapendekezo Sita Ya Wachimbaji Wakubwa

 


Na Grace Semfuko, MAELEZO.
Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko amesema Wizara yake itayafanyia kazi mapendekezo sita, yaliyotolewa na Wachimbaji wakubwa na wa kati wa madini kwenye kikao cha wadau wa sekta hiyo waliokutana Mei 12, Jijini Dar es Salaam.

Mapendekezo hayo ni pamoja na kuweka vivutio na sera nzuri za biashara ya Madini ili kuwavuta wawekezaji wengi zaidi wa ndani na nje ya nchi, kufanya tafiti za madini, kuweka mazingira wezeshi ya biashara hiyo, kuwa na ulinzi na usalama wa uhakika wa biashara hiyo, uibuaji wa vipaji na mafundi wa madini wa kitanzania na uboreshwaji wa mindombinu kwenye maeneo ya migodi.

Akifungua mkutano wa siku moja wa majadiliano baina ya Serikali na Wachimbaji wa Madini wakubwa na wa kati, wenye lengo la kukuza sekta hiyo nchini, Biteko amesema Wizara yake inayafanyia kazi mapendekezo ya wachimbaji hao ili yaweze kuleta tija ya kiuchumi.

“Naomba niwahakikishie tutayafanyia kazi mapendekezo yenu yote mliyoyatoa hapa, lengo letu ni kuhakikisha biashara hii inazidi kukua na kuleta tija ya kiuchumi” amesema Waziri Biteko.

Amesema Serikali inaendelea kusimamia sekta ya madini ili iendelee kuwa na tija, kutokana na sekta hiyo kuongoza kwa ukuaji wa uchumi wa asilimia saba kutoka asilimia 3.8 ya mwaka 2015, na kutajwa kuongoza kwa kuliingizia Taifa pato la kigeni.

Biteko pia amesema asilimia 52.4 ya bidhaa za Tanzania zinazouzwa nje ya nchi, zinatokana na mazao ya madini na hivyo kuifanya sekta hiyo izidi kuimarika kwenye mapato na kuchangia sekta nyingine katika ukuaji wa uchumi.

“Sekta ya Madini imetoka mbali, imepita katika historia ndefu sana, historia mbaya na nzuri, imetoka kwenye kundi ambalo biashara ilikuwa ikifanywa kwa kificho, leo imekuwa ni sekta ambayo biashara inafanywa kwa uwazi, mchango wake unaweza kupimwa katika maeneo mbalimbali ikiwepo kukuza uchumi wa nchi kutoka asilimia 3.8 hadi asilimia 7” amesema Biteko.

Naye, Mwenyekiti wa Chemba ya Madini Mhandisi Philbert Rweyemamu ameishauri Wizara hiyo, kujadiliana na wadau ili kuangalia namna bora ya kuongeza migodi mipya ya uchimbaji wa madini, na kuongeza mitaji kutoka katika masoko ya hisa ya nchi za nje.

“Tunahitaji pesa za wawekezaji kutoka nje ya nchi kwa sababu soko la hisa la Dar es Salaam halijakidhi mahitaji ya sasa, na mara nyingi pesa za kuanzisha hii miradi zinatoka kwenye masoko makubwa ya hisa ya nchi za nje, kwa hiyo tunashauri Wizara tujadiliane kwa yale ambayo tunafikiri kama yakiwekewa mkazo au yakabadilishwa, yataongeza tija na tutaona migodi mipya ikianzishwa” amesema Mhandisi Rweyemamu.


Share:

Waziri Mkuu Azitaka TPA, TRA, TASAC NA EGA Zifanye Kazi Kwa Ushirikiano

 


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania, Mamlaka ya Bandari Tanzania na Mamlaka ya Serikali Mtandao kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuboresha utendaji wa Bandari ya Dar es Salaam

Ameyasema hayo jana(Jumatano, Mei 12, 2021) alipotembelea bandari ya Dar es Salaam ili kuona utendaji wa bandari hiyo.

“TPA endeleeni kuiimarisha bandari yetu, hii ni sura ya uchumi wa nchi yetu, zungumzeni lugha moja ya uwajibikaji, TRA muwepo maeneo yote yanayohitaji uwepo wenu na muda wote wateja wetu wahudumiwe ili bandari yetu iendelee kuwa bora. Nchi nyingi zinatutegemea”

Amesema kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania ihakikishe mfumo wa pamoja wa forodha Tanzania (TANCIS) unafanya kazi kwa ufanisi ili kupuinguza malalamiko ya wateja kuhusu mfumo huo.

“Dosari zote za mfumo wa TANCIS zifanyiwe kazi, mfumo usituharibie, mnapoona kuna madhaifu fanyeni marekebisho ya haraka, tunataka wateja waingie na kutoka kwa muda mfupi” Amesema.

Aidha, Waziri Mkuu amemuagiza Kamishna Mkuu wa TRA apeleke watumishi katika mizani ya TANROADS iliyopo Kurasini Dar es Salam ili kurahisisha ukaguzi wa ‘seal’ pale ambapo magari yamezidisha uzito na yanahitaji kukaguliwa

“TRA kuna foleni kwenye mizani, hakuna watu, kuanzia leo peleka watumishi pale tunataka ukaguzi uwe muda wote”.

Akitolea ufafanuzi kuhusu video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii ya uwepo wa foleni bandarini hapo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania Eric Hamissi amesema suala hilo halina ukweli na hakuna dereva anayekaa bandarini kwa siku tatu.

“Hata sisi tulishangaa sana kuona ile clip, haina ukweli wowote, dereva Omari Mambo Mei 10, 2021 aliingia saa nane mchana, na ilipofika saa 10.38 alishusha mzigo na kuondoka saa 11.00 jioni”

Aliongeza kuwa kwa sasa asilimia arobaini ya eneo la bandari lipo kwenye ujenzi ikihusisha ujenzi wa njia nne za barabara na ujenzi wa gati namba moja mpaka saba lengo ni kuifanya bandari iweze kuhudumia wateja kwa ufanisi mkubwa “mpaka sasa gati namba moja mpaka tano zimekamilika na gati namba sita na saba zitakamilika mwezi Agosti,2021”

Wakizungumza kwa nyakati tofauti madereva wa malori wanaoingia na kutoka kwenye Bandari ya Dar es Salaam wamesema wanaridhishwa na utendaji kazi wa bandari kwani hawatumii muda mrefu kuingia na kutoka bandarini hapo.

(Mwisho)
IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU,


Share:

Waziri Ummy : Uuguzi ni Taaluma Sio Siasa


Nteghenjwa Hosseah, Manyara
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Ummy Mwalimu amesema Wauguzi ni miongoni mwa wataalamu wa Afya wanaopaswa kuheshimiwa na kupewa thamani inayostahili na wasichukuliwe kisiasa.

Waziri Ummy ameyasema hayo wakati alipokuwa akihutubia kwenye maadhimisho ya siku ya Wauguzi Duniani yakiyofanyika Mkoani Manyara tarehe 12 Mei,2021.

Amesema uuguzi ni fani adhimu na kuwataka viongozi wa Mikoa na Wilaya kuacha kuwadhalilisha kwa kuwaweka ndani kwa tuhuma zisizo na ushahidi.

“Viongozi wa Mikoa na Wilaya niwatake kuelewa kuwa uuguzi ni taalamu adhimu na muache kuamuru wawekwe ndani au kuwachukulia hatua kali ambazo haziendani na taalum yao kwa tuhuma ambazo hazina ushahidi, hili tuliache mara moja,”amesema

Ameongeza “Kama Muuguzi amekosea akashitakiwe kwenye Baraza la Wauguzi na Wakunga ambapo atachukuliwa hatua kwa matakwa ya taaluma yake na sio kwa utashi wa kisiasa.”

Hata hivyo, amesema kiongozi yeyote atakayemuweka ndani muuguzi awe amethibitisha ameiba lakini kwa tuhuma nyingine akashitakiwe kwenye Baraza lao la Kitaaluma.

Pia Mhe.Ummy amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri kuacha kuwakatalia wauguzi kwenda kusoma mara wanapopata fursa za kwenda kujiendeleza kielimu.

“Wauguzi lazima wathaminiwe kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuhudumia wagonjwa sababu mara zote ukienda hospitali Daktari atakuona kwa muda mchache sana na wakati mwingi utakuwa na nesi katika kukuhudumia hivyo wapewe moyo,”amesema.

Amewapongeza na kuwashukuru Wauguzi kwa kazi kubwa walioifanya wakati wa wimbi la ugonjwa wa Corona na amewataka kuendelea kutimiza wajibu wao na kuokoa maisha ya watu.

Akijibu hoja zilizowasilishwa na Wauguzi katika risala yao, Waziri Ummy amesema suala la muundo linafanyiwa kazi na lilishawasilishwa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma kwa hatua zaidi.

Mhe. Ummy amesema kwa sasa Madaktari na wauguzi wafanye kazi kama timu moja ili kuleta matokeo chanya kwa jamii inayowategemea na hayo ya kiutawala yataendelea kuangaliwa na kufanyiwa kazi.

Kuhusu posho ya majukumu, amesema Ofisi ya Rais TAMISEMI itaangalia ni namna gani inaweka mazingira bora kwa wauguzi walioko TAMISEMI kwa kadri rasilimali zitakavyopatikana.

“Ofisi yangu itahakikisha inatoa kipaumbele katika kutatua changamoto ya uhaba wa nyumba za watumishi wa Afya kwa kujenga nyumba za kutosha ili watumishi hao waweze kukaa kwenye vituo vyao na kufanya kazi kwa amani,”amesema.

Katika hatua nyingine, Mhe. Ummy ametoa zawadi ya sh.500,000 kwa Muuguzi Aldolefina Shayo wa Zahanati ya Kilangare iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Same ambaye amevunja rekodi ya kuhudumia wagonjwa hamsini kwa siku bila kunung’unika na leo ameshindwa kushiriki maadhimisho hayo kwa kuwa yuko peke yake kwenye zahanati hiyo na hakuna mtu wa kumsaidia.

Waziri Ummy amesema katika ajira mpya zilizotangazwa watapelekwa wauguzi wawili na Mganga mmoja ili kuboresha zaidi huduma za Zahanati hiyo.


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo May 13



Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI MEI 12,2021


Share:

SIKUKUU YA EID -EL- FITR NI IJUMAA MEI 14


Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zuberi ametangaza kuwa Sikukuu ya Eid El-Fitr ni Ijumaa Mei 14, 2021.

Amesema leo Mei 12, 2021 mwezi haujaonekana hivyo waumini wa dini ya Kiislamu wataendelea kufunga kwa siku ya 30.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger