Sunday, 9 May 2021

AZIKWA KISHA KUFUKULIWA NA KURUDISHWA MOCHWARI KIMYA KIMYA

Linaweza kuwa tukio la ajabu, lakini ndio limetokea huku usiri mkubwa ukitawala. Ndugu wa familia ya marehemu Danielson Lema (72), aliyekuwa mkazi wa Kijiji cha Nkwansira wilayani Hai, Kilimanjaro, wamepewa maiti ya mtu mwingine, Shanshandumi Kimaro (82) na kwenda kuzika bila kubaini kuwa sio ndugu yao.

Mwili wa Kimaro, aliyekuwa mkazi wa Kijiji cha Isuki ulizikwa na familia ya Lema Mei Mosi, mwaka huu baada ya kukabidhiwa kimakosa na wahudumu wa chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Wilaya ya Hai.

Hata hivyo, Mei 2 mwili huo ulifukuliwa kisha kurudishwa kwenye chumba cha maiti kimya kimya bila uongozi wa hospitali hiyo kubaini.

Tukio hilo ambalo lilifanyika kwa usiri mkubwa, limeibua maswali mengi tata kuhusu usalama na umakini wa wahudumu wa chumba cha maiti pamoja na ndugu husika kushindwa kutofautisha miili ya wapendwa wao licha ya kuwepo kwa taratibu za ndugu kutambua mwili kabla ya kukabidhiwa.

Via Mwananchi
Share:

Tablets packing assis­tants 13 Positions at Vista Pharma LTD

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

VISTA PHARMA LTD, has constructed a new pharmaceutical manufacturing factory, at Zegereni, Kibaha, in the Coast Region. The pharmaceutical factory will manufacture and supply various hu­man tablet and syrup medicines. The factory plans to start the production operations in July 2021. In this regard, the company invites the qualified and experienced Tanzanian applicants in the field […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Technician at Vista Pharma LTD

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

VISTA PHARMA LTD, has constructed a new pharmaceutical manufacturing factory, at Zegereni, Kibaha, in the Coast Region. The pharmaceutical factory will manufacture and supply various hu­man tablet and syrup medicines. The factory plans to start the production operations in July 2021. In this regard, the company invites the qualified and experienced Tanzanian applicants in the field […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

TFF Yaomba Radhi Mechi Ya Yanga na Simba Kuarishwa



Share:

Syrup preparation 4 Positions at Vista Pharma LTD

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

VISTA PHARMA LTD, has constructed a new pharmaceutical manufacturing factory, at Zegereni, Kibaha, in the Coast Region. The pharmaceutical factory will manufacture and supply various hu­man tablet and syrup medicines. The factory plans to start the production operations in July 2021. In this regard, the company invites the qualified and experienced Tanzanian applicants in the field […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Weighing & dispensing 4 Positions at Vista Pharma LTD

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

VISTA PHARMA LTD, has constructed a new pharmaceutical manufacturing factory, at Zegereni, Kibaha, in the Coast Region. The pharmaceutical factory will manufacture and supply various hu­man tablet and syrup medicines. The factory plans to start the production operations in July 2021. In this regard, the company invites the qualified and experienced Tanzanian applicants in the field […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Human Resource (HR) officer at Vista Pharma LTD

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

VISTA PHARMA LTD, has constructed a new pharmaceutical manufacturing factory, at Zegereni, Kibaha, in the Coast Region. The pharmaceutical factory will manufacture and supply various hu­man tablet and syrup medicines. The factory plans to start the production operations in July 2021. In this regard, the company invites the qualified and experienced Tanzanian applicants in the field […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

MHANDISI MIGODI STAMICO AIBUKA MFANYAKAZI BORA 2021

 

Mhandisi Migodi kutoka Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Peter Maha ameibuka mfanyakazi bora na kujinyakulia kitita cha shilingi milioni moja kwenye maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani Mei Mosi 2021 yaliyofanyika kitaifa katika uwanja wa CCM Kirumba Wilaya Ilemela mkoani Mwanza.
Tazama BMG TV hapa chini
Share:

WANAVIJIJI 30 SIMIYU WAPEWA MAFUNZO YA KUKABILIANA NA TEMBO


Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Wizara ya Maliasili na Utalii, Pellage Kauzeni akizungumza na madiwani wa Wilaya ya Meatu kuhusu mikakati ya Wizara ya Maliasili na Utalii ya kukabiliana na tembo wanaovamia makazi ya watu katika kikao kilichofanyika Wilayani Meatu mwishoni mwa wiki.
Wananchi waliopewa mafunzo ya kukabiliana na tembo wakionyesha kwa vitendo namna ya kutumia honi ili kumfukuza tembo aliyevamia makazi ya watu katika onesho lililofanyika baada kikao cha Wizara ya Maliasili na Utalii na Madiwani wa Wilaya Meatu kilichofanyika mwishoni mwa wiki.
Wananchi waliopewa mafunzo ya kukabiliana na tembo wakionyesha kwa vitendo namna ya kutumia wigo wa pilipili na oili chafu ili kumfukuza tembo aliyevamia makazi ya watu katika onesho lililofanyika baada kikao cha Wizara ya Maliasili na Utalii na Madiwani wa Wilaya Meatu kilichofanyika mwishoni mwa wiki.

*******************************

Na Happiness Shayo- MEATU

Wanavijiji 30 kutoka wilaya zote za mkoa wa Simiyu wamefundishwa namna ya kukabiliana na wanyama waharibifu hasa tembo ikiwa ni mwendelezo wa mikakati ya Wizara ya Maliasili na Utalii ya kuhakikisha usalama wa wananchi wanaoishi kwenye maeneo yenye changamoto ya kuvamiwa na tembo.

Hayo yamesemwa na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw. Pellage Kauzeni alipofanya kikao na madiwani wa Wilaya ya Meatu mwishoni mwa wiki.

Bw. Kauzeni amefafanua kuwa mafunzo hayo yamefanyika chini ya Mradi wa utafiti wa tembo kwa ukanda wa Serengeti, Maswa na Ngorongoro.

Ametaja mafunzo yaliyotolewa kwa wananchi hao kuwa ni kutumia honi, kutumia mabomu ya pilipili na kutumia mabomu ya kisasa ya kufukuza tembo.

Njia nyingine zilizofundishwa za kupambana na tembo ni kutumia wigo wa pilipili na oili chafu pamoja na kutengeneza tofali au mkate wa pilipili na kinyesi cha wanyama kama ngombe,mbuzi n.k.

Bw. Kauzeni ameweka bayana kuwa njia hizo za kupambana na wanyama waharibifu zimeshawahi kutumika katika maeneo mbalimbali na zimeleta matokeo chanya.

“Njia hizi zimeshawahi kutumika na Jumuiya za Hifadhi kwa Jamii (WMA) za Kaskazini mwa Tanzania kupitia mradi wa Fredkin na pia Kusini mwa Tanzania upande wa Selous Game Reserve na zimeonyesha mafanikio makubwa” amefafanua Bw. Kauzeni.

Akizungumzia mikakati ya Serikali ya kuendelea kupambana na wanyama waharibifu Bw. Kauzeni amesema Serikali kupitia taasisi ya Tanzania Wildlife Research Institute (TAWIRI) inaendelea na tafiti ili kugundua mbinu za gharama nafuu zaidi zitakazotumiwa na wananchi kupambana na tembo na pia Wizara ya Maliasili na Utalii inaendelea kuelimisha wananchi ili kupunguza changamoto ya uvamizi wa wanyama waharibifu katika makazi ya watu.

Naye, Mkazi wa Kijiji cha Mwanzalamba Wilaya ya Meatu, Sololo Malando amesema kuwa amefundishwa mbinu mbalimbali za kujilinda na wanyama waharibifu kama kutumia vilipuzi vya kurusha kwa mkono.

“Mbinu hii ya kutumia vilipuzi ikitumika vizuri itasaidia sana wananchi kuondokana na hili tatizo la tembo kwa kuwa inasaidia kuwakimbiza tembo endapo wamevamia mashamba” amesema Malando.

Mkazi mwingine wa wilaya ya Meatu, Magembe Sita ametaja mafunzo aliyoyapata akitolea mfano wa mafunzo ya kutumia tochi, honi na baruti ya kutumia mchanga na pilipili kufukuza tembo.

Kikao hicho kiliambatana na maonyesho ya mbinu za kukabiliana na tembo yaliyofanywa na wanavijiji kutoka wilaya za Mkoa wa Simiyu na kushuhudiwa na wakuu wa wilaya za Busega, Itilima na Meatu

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI MEI 9,2021




Share:

Saturday, 8 May 2021

Picha : RAIS SAMIA AZINDUA KITABU CHA HISTORIA YA MAISHA YA RAIS MSTAAFU MZEE ALI HASSAN MWINYI...AMKABIDHI GARI JIPYA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akinyanyua juu Kitabu cha Historia ya Maisha ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi mara baada ya kukizindua katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Convention Centre Jijini Dar es Salaam leo tarehe 08 Mei, 2021.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akikata utepe ili kuzindua Kitabu cha Historia ya Maisha ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Convention Centre Jijini Dar es Salaam leo tarehe 08 Mei, 2021.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi akinyanyua juu Kitabu cha Historia ya Maisha yake mara baada ya kuzinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Gari Jipya Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi pamoja na Mkewe Mama Sitti Mwinyi mara baada ya kuzindua Kitabu chake cha Historia ya Maisha yake ili liweze kumsaidia katika shughuli mbalimbali za usafiri.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi akizungumza na viongozi mbalimbali waliofika katika uzinduzi wa Kitabu chake cha Historia ya Maisha yake katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Convention Centre.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa Kitabu cha Historia ya Maisha ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi iliyofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Convention Centre.

PICHA NA IKULU
Share:

DC SELELA: UNAWEZA KWENDA SEHEMU USIONE CHANGAMOTO LAKINI JICHO LA MWANAHABARI LINAMULIKA KILA MAHALI NA KUONESHA NJIA



Mkuu Wilaya ya Kongwa Dkt. Suleiman Serera (katikati) kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma akimkabidhi tuzo Afisa Uhusiano wa TANESCO mkoa wa Dodoma Innocent Lupenza ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika ukumbi wa Jiji (Madiwani) jijini Dodoma. Tuzo hiyo imetolewa leo na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Dodoma (CPC) kutambua mchango wa Bw Lupenza katika tasnia ya habari.CPC imeanzisha tuzo hizo ili kutambua mchango wa wadau mbalimbali wanaotoa ushirikiano,na kufanikisha waandishi kutimiza majukumu yao.
Wadau wa Habari wakiwa katika maadhimisho ya Uhuru wa Habari duniani kwa Mkoa wa Dodoma yakiadhimishwa Mei 8,2021
***
Na Faustine Gimu Galafoni,Dodoma

Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma Seleman Selela  amesema  tasnia ya Habari ina mchango mkubwa katika kuibua changamoto za jamii ili kuweza kutatuliwa na serikali.

Mkuu huyo wa wilaya amebainisha hayo leo Mei 8,2021  katika maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya Habari mkoa wa Dodoma yaliyoandaliwa na Klabu ya  Waandishi wa Habari mkoa wa Dodoma[CPC] kwa kushirikiana na Klabu ya Waandishi wa Habari Tanzania [UTPC],Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa[TANAPA]pamoja na mamlaka ya maji safi na Usafi wa Mazingira jijini Dodoma[DUWASA].

Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge ,mkuu huyo wa wilaya amesema vyombo vya habari vimekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya kiuchumi  huku pia akiwataka wanahabari kuendelea kuwa na ubunifu katika uchakataji wa habari.

Katika hatua nyingine Selela amewataka wanahabari kwendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia na kuhakikisha wanaandika habari zenye mizania[balance]ili kuweza kuepusha migogoro inayoweza kujitokeza.

Mwenyekiti wa klabu ya Waandishi wa habari mkoa wa  Dodoma [CPC]Musa Yusuph ameainisha changamoto zilizopo katika tasnia ya   habari ni pamoja na ubaguzi wa baadhi ya taasisi za serikali kuita vyombo vya habari kuelezea mambo nyeti ya kitaifa huku Katibu wa klabu hiyo Ben Bago akiwaasa baadhi ya maafisa habari serikalini kuacha tabia ya  kutoa lugha isiyokuwa na staha kwa wanahabari pindi wanapotekeleza majukumu yao.

Afisa Mhifadhi mkuu Mamlaka ya Hifadhi Tanzania[TANAPA]Jully Lyimo pamoja afisa utalii mkoa wa Manyara Cecilia Mkwabi wamelezea mchango wa Habari katika sekta ya utalii nchini.

Maadhimisho ya Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani yalifanyika Mei 3,2021  ambapo mkoa wa Dodoma yakifanyika Mei,8,2021 yakienda sambamba na kaulimbiu isemayo Habari kwa maufaa ya umma  ambapo tuzo zimetolewa kwa taasisi zilizo na ushirikiano mkubwa kwa tasnia ya Habari kuwa ni TANAPA  na Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira Dodoma [DUWASA  na Mwanachama bora wa mwaka akiwa ni Sebastian Warioba huku tuzo iliyokwenda kwa afisa habari mwenye ushirikiano mzuri ni Innocent Lupenza kutoka TANESCO.


Share:

MWANAMKE AZUA GUMZO AKIWEKA NYOKA KWENYE JENEZA LA MME WAKE


Mwanamke mmoja kutoka Ghana amezua hisia mseto kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuonekana kwenye video akiweka nyoka ndani ya jeneza la mumewe.

Iliripotiwa kuwa mwanamke huwa alikuwa ameghadhabishwa na waliohusika na kifo cha mumewe na alitaka wapate adhabu kali.

Kwenye video hiyo ambayo imesambaa mitandaoni, mwanamke huyo alidai kwamba mumewe aliuawa kwa kuumwa na nyoka kwenye ulimi na anaamini kuna watu walipanga njama hiyo.

 Ilisemekana kwamba jamaa huyo aliuawa kwa kuumwa na nyoka kwenye ulimi kwa hivyo mkewe akamua kumzika nayo ambapo kulingana na mila, mwanamke huyo alifanya hivyo ili nyoka huyo akabiliane na wale waliohusika na kifo cha mumewe 

Video hiyo iliibua hisia tofauti miongoni mwa wanamitandao  baadhi ya maoni;

 @funghana_ Alisema inaaminika kwamba jamaa huyo aliuawa, kwa hivyo nia yake kuwekewa nyoka ilikuwa ni kukabiliana na waliohusika na kifo chake.

 @bby__naa." Naye alisema .“Hii ni kama kukiuka haki za nyoka , wao pia wana haki zao”

 @cabi_diana: “Haya ni maajabu.

” @wurdzfreeman “Ati aliumwa na nyoka kwa ulimi? kivipi na inawezakanaje?”

 @ericaabyna: “Eish, hii inamaanisha nini?”

 @jerryjustice: “Aaah, Hii ni nini sasa?” 

@1plus1builders: “Hii ni muvi ama nini?”

TAZAMA HAPA
Share:

BAADA YA KUHANGAIKA MIAKA 6 HATIMAYE NIKAPATA MTOTO



Natanguliza shukrani zangu za dhati kwa Kiwangadoctors kuniwezesha na mimi kuitwa mama baada ya kuhangaika kwa kipindi cha miaka 6 nikiwa kwenye ndoa na bila mtoto.Kwa sasa nina umri wa miaka 36 na niliolewa nikiwa na miaka 30.

Mwanzo kabisa nilipendwa na ndugu na Jamaa wa Bwana yangu,lakini kadri miaka ilivyozidi kwenda bila kupata mimba,baadhi ya ndugu na Jamaa kwa upande wa Bwana wangu walianza kuwa na visa mbalimbali hasa walikuwa wanakuja kututembelea hapa mkoa wa Mwanza wakitoka Bukoba.

Tabia yao sikupendi ila nilivumilia kwa sababu tulipendana sana na Mume wangu lakini mimi mwenyewe nilikuwa naumia sana haswa Bwana yangu akienda kazini na mimi nikibaki pekee yangu nilikuwa najiuliza kwa nini sijapata mimba muda wote huo.

Miaka 2 kupita tulishauriana mimi na bwana yangu twende hospitali ya Bugando hapa Mwanza tuweze tambua shida ni nini.

Tulimuona doctor na kupata vipimo vya aina mbalimbali,kulingana na maneno ya Doctor wa Hospitali ya Bugando alisema siwezi kupata mimba kulingana na matokeo ya vipimo vyake na upande wa Mme wangu aligundurika kuwa ana uwezo wa kutwisha mimba.

Siku hiyo ilikuwa ni siku mbaya sana maishani mwangu nilivyokuwa namtazama mme wangu,nakumbuka jinsi tulivyokuwa tunaongea na kupanga watoto wetu tutakaopata na maisha gani tungependa waishi.

Hakika mwili wangu uliregea na kukosa nguvu kabisa. Mme wangu alinifikisha nyumbani kisha akachukua gari yake na kwenda kazini kwake.

Baada ya matokeo hayo yalinifanya nikose amani na furaha kwa ndoa yangu haswa.

Mme wangu alianza tabia ya kurudi nyumbani amechelewa na muda mwingine akilala nje bila kurudi nyumbani.

 Maumivu yalizidi kila kukicha kwa tabia yake hiyo. Baada ya miezi 6 akiwa na hiyo tabia nilimuuliza mme wangu kipi umekosa kwangu hadi kunifanyia hivi na madharau haya, Mme wangu alijibu,

“Mwanamke gani sasa kazi yako kula na kwenda chooni,wenzio wanazidisha ukoo wao kila mwaka wewe chooni na kuvimbisha Makalio tu"

Sikuwai kufikiria kuwa mme wangu anaweza nijibu hivyo,nilijikuta natokwa na machozi na kukimbilia kwa chumbani. Nikiwa chumbani nalia mme wangu alinifuata na kuniomba msamaha mimi mwenyewe niligundua kuwa ni mawazo ambayo mme wangu anayo kuhusu kupata mtoto nilimsamehe mme wangu na kumkumbatia kifuani mwake.

Kesho yake asubuhi nilimpigia simu rafiki yangu Jane na kumuomba aje nyumbani. Jane hakuwawia maana alikuwa anaishi mtaa jirani nikamueleza shida yangu na maneno aliyoyatoa jana mme wangu kwangu kisa sipati mtoto.

Ndipo Jane aliponiambia kuwa muda mrefu kuna doctor yupo Kenya anamjua anaweza kunisaidia.

Baada ya mwezi mmoja niliomba ruhusa mme wangu kwenda Dar kumuona Shangazi yangu ila nilitumia nafasi hiyo kwenda na Jane hadi Kenya-Nakuru kwa ofisi ya Dr Kiwanga.

Niliweza kumuona Dr na kumueleza maisha yangu ya ndoa jinsi yalivyo na kuomba msaaada niweze kupata mtoto maana ndiyo chanzo cha mme wangu kubadilika.

Katika mazungumzo Dr alisema kuwa ana uwezo wa kutibu mtu popote alipo hata bila kufika ofisini kwake Nakuru.

Dr aliniuliza maswali kadhaa na kuniahidi kuwa atanisaidia na Pregnancy spells na nitapata matokeo ndani ya mwezi mmoja.

Baada ya mwezi mmoja nilianza kujihisikuwa na dalili za mimba na kumwambia mme wangu anipeleke hospitali.Tulifika hospitali ile ile ya Bugando na kupimwa nikaambiwa kuwa nina mimba. AsanteDr. Kiwanga leo hii mimi ni mama wa watoto 2 na maisha yangu na mme wangu ni mazuri.

Natoa wito kwa mwenye shida kama Love spells,Pressure,Diabetes,Badluck,Magicring,Magic wallet na kukosampenzimpigieDr.kwanga kwa +254 769404965 au tembelea website yao www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.


Share:

ATUPWA JELA MIAKA 200 KESI YA UHUJUMU UCHUMI TANZANIA


Mahakama ya Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe, imemhukumu Semeni Gwewa Mswima ambaye alikuwa Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Mlowo, kifungo cha miaka 200 Jela au kulipa faini ya Sh.52,000,000 pamoja na kurejesha kiasi cha Sh.30,850,000 alichoiibia Halmashauri Wilaya ya Mbozi.

Kesi hiyo ambayo ni kesi ya Uhujumu Uchumi Na.01/2021 ilifunguliwa na TAKUKURU Mkoa wa Songwe mbele ya Hakimu Mkazi wa wilaya hiyo, Vitalis Changwe ambapo mshtakiwa alikuwa akikabiliwa na makosa 60 ambapo ndani yake kuna makosa ya kutumia nyaraka za uongo kinyume na kifungu cha 342 na 337 vya Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 ya mwaka 2019 na makosa ya wizi kwa mtumishi wa umma kinyume na vifungu vya 258(1) na 270 vya Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 ya Mwaka 2019.

Akisomewa Mashtaka hayo, Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU, Mkoa wa Songwe, Emanuel Ndembeka akisaidiana na Simona Mapunda, alieleza mahakamani hapo kwamba mshtakiwa kwa tarehe tofauti tofauti kati ya tarehe 04/07/2019 hadi tarehe 08/05/2020 kwa kutumia hati za malipo na hundi zilizoghushiwa aliweza kutoa na kuiba fedha jumla ya Sh.30,850,000 toka katika akaunti Na.61210014674 ambazo ni mali ya Halmshauri ya Wilaya ya Mbozi.

Mshtakiwa alikiri makosa yote 60 yaliyokuwa yakimkabili.

Akitoa hukumu hiyo,Hakimu Changwe alimwamuru mshtakiwa kulipa faini ya Sh.800,000 au kwenda jela miaka mitatu kwa kila kosa la kuwasilisha nyaraka za uwongo,ambapo kulikuwa na jumla ya makosa 40.

Hakimu huyo pia alimwamuru mshtakiwa alipe faini ya Sh.1,000,000 au kwenda jela miaka minne kwa kila kosa la wizi kwa mtumishi wa umma ,ambapo kulikuwa na jumla ya makosa 20. Pamoja na kulipa faini hizo,Mahakama ilimwamuru mshtakiwa ajereshe katika halmashauri husika fedha alizoiba kiasi cha Sh. 30,850,000, mshtakiwa alishindwa kulipa fedha.

Share:

OSHA YAWANOA WAFANYAKAZI WA KIWANDA CHA NONDO MIKOCHENI

Mwezeshaji wa mafunzo ya usalama na afya kutoka OSHA, Respicious Kundawa , akitoa mafunzo kwa wafanyakazi wa kiwanda cha PNP Industries Limited.
Mwezeshaji wa mafunzo ya usalama na afya kutoka OSHA, Respicious Kundawa , akizungumza na mmoja ya washiriki wa mafunzo wa kiwanda cha PNP Industries Limited. OSHA imetoa mafunzo hayo kuwawezesha wafanyakazi kujilinda dhidi ya vihatarishi wanapokuwa kazini.
Mwezeshaji wa mafunzo ya usalama na afya kutoka OSHA, Respicious Kundawa , akitoa maelekezo kuhusu kuboresha mazingira ya kazi kwa wasimamizi wa wafanyakazi wa kiwanda cha PNP Industries Limited mara baada ya kutoa mafunzo ya usalama na afya kiwandani hapo.
Wafanyakazi wa kiwanda cha PNP Industries Limited wakifuatilia mafunzo ya usalama na afya yaliyotolewa na OSHA kiwandani hapo. Mafunzo hayo yalilenga kuwawezesha wafanyakazi kujilinda dhidi ya vihatarishi wanapokuwa kazini.

******************************

Na Mwandishi Wetu

Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) umetoa mafunzo maalum ya usalama na afya kwa wafanyakazi wa kiwanda cha kuzalisha nondo cha PNP Industries Limited yenye lengo la kuwajengea uwezo wa kujilinda dhidi ya ajali na magojwa yanayotokana na mazingira yao ya kazi.

Mwezeshaji wa Mafunzo hayo kutoka OSHA, Respicious Kundawa, amesema mafunzo hayo ni muhimu hususan kwa wafanyakazi wanaohusika moja kwa moja katika mchakato mzima wa uzalishaji wa bidhaa hiyo muhimu.

“Katika mafunzo ya leo tumewalenga wafanyakazi katika viwanda vya kuzalisha nondo ambao tunafahamu wanakabiliwa na vihatarishi mbali mbali katika mlolongo mzima wa uzalishaji wa bidhaa husika kuanzia wanapopokea vyuma chakavu, kuvichambua, kuviyeyusha, kutengeneza nondo zenyewe na hata kuzipakia katika magari tayari kwa kuzisafirisha kwenda kutumika,” alieleza Kundawa.

Aliongeza: “Katika hatua zote hizo mfanyakazi anaweza kuumia hivyo ni muhimu kuwapa wafanyakazi nyenzo za kujilinda.”

Kwa upande wa uongozi wa kiwanda hicho umeeleza kuridhishwa na mafunzo yaliyotolewa na OSHA na kuahidi kuyafanyia kazi maelekezo yaliyotolewa kupitia mafunzo hayo.

“Tunashukuru OSHA kwa mafunzo waliyotupatia kwa siku ya leo ambayo yatatusaidia sana katika kuboresha mazingira yetu ya kazi pamoja na namna ambavyo tunafanya kazi,” alisema Iddy Hamis, Afisa Rasilimali Watu wa Kiwanda cha PNP Industries Limited.

Aidha, wafanyakazi walioshiriki katika mafunzo hayo wamesema akiwemo Juma Kajembe na Solomon Lukas wamesema mafunzo waliyoyapata yatasaidia katika kuboresha namna ambavyo wamekuwa wakitekeleza majukumu yao na hivyo kujiepusha na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi.

“Tunashukuru kwa mafunzo tuliyoyapata kwa siku ya leo, tunaimani yatatutoa kutoka hatua moja kwenda nyingine kahusiana na usalama wetu tuwapo kazini. Kwasasa tunaweza kutambua vitu gana ni hatarishi katika maeneo yetu kazini pamoja na matumizi sahihi ya vitendea kazi na vifaa kinga,” alisema Juma Kajembe ambaye ni mfanyakazi wa kiwanda cha PNP.

Mafunzo hayo ambayo yamefanyika katika eneo la kiwanda, Mikocheni jijini Dar es Salaam, yamejumuisha wafanyakazi zaidi ya 90 ambao wanahusika na shughuli mbali mbali katika mlolongo mzima wa uzalishaji nondo pamoja na wasimamizi wao.

Wakati huo huo, OSHA imehitimisha darasa la mafunzo ya usalama na afya katika sekta ya mafuta na gesi yaliyofanyika katika ofisi za OSHA ambayo yalijikita katika kuwaandaa wataalam ambao watatumika kusimamia usalama wa wafanyakazi katika miradi ya mafuta na gesi inayotarajiwa kuanza kutekelezwa hapa nchini.

Share:

MECHI YA SIMBA SC Vs YANGA YAAHIRISHWA....YANGA SC WATAJA SABABU KUPINGA MCHEZO KUHAMISHIWA USIKU

Rudisheni pesa zetu, ndizo kauli za mashabiki baada ya kutangazwa kuahirishwa kwa mchezo wa Simba dhidi ya Yanga leo Mei 8, 2021.

Bodi ya Ligi imetangaza kuahirisha mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Simba na Yanga iliyokuwa ichezwe leo Jumamosi Mei 8, 2021 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa mkoani Dar es Salaam.

Mchezo wa Simba dhidi ya Yanga ulipangwa kupigwa leo saa 11:00 jioni na baadae kusogezwa mpaka saa 1:00 usiku kitendo ambacho Yanga walikigomea.

Uongozi wa Yanga umesema umepokea kwa masikitiko taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kuhusiana na kusogezwa kwa mechi kutoka saa 11:00 hadi 1:00 jioni.

Wamesema Mabadiliko hayo ni kinyume cha kanuni ya 15(10) za Ligi Kuu inayohusu taratibu za michezo ambayo unasema mabadiliko yoyote ya muda wa kuanza yatajulishwa ipasavyo kwa pande zote mbili husika za mchezo angalau masaa 24 kabla ya muda wa awali.

Uongozi wa Yanga umeitaka bodi ya Ligi na TFF kuendesha ligi kwa kuheshimu na kufuata kanuni zinazowekwa.

Basi la timu la Yanga limefika uwanjani saa 10:18, wakati Mwenyekiti wa klabu hiyo, Mshindo Msolla amefika saa 10:05.

Taarifa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) mchana huu imesema kwamba wamepokea agizo la Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuisogeza mbele mechi hiyo hadi Saa 1:00 usiku.

Dakika 15 pekee ziliwatosha Yanga kusubiri kuanza kwa mchezo wao dhidi ya Simba na baada ya kuona hakuna timu wala waamuzi wanaoingia uwanjani hapo waliondoka na kurudi katika vyumba vya kubadilishia nguo.

Wakati wanaondoka majukwaa yaliyokuwa ma mashabiki wa timu hiyo yaliinuka kwa shangwe na kuishangilia timu yao huku wengine wakiondoka uwanjani hapo.

Ilipofika saa 11:35 wachezaji wa Yanga walitoka vyumbani na kupanda gari lao na kisha waliondoka uwanjani.

Wakati gari likitoka uwanjani mashabiki walikuwa wakiswasindikiza huku wakiimba “TFF, TFF ”, na kulifuata gari kwa nyuma.

Baada ya Yanga kuondoka uwanjani hapo, mashabiki wa Simba walionekana kupoa huku wale wa Yanga wakiendelea kushangilia na kuondoka uwanjani hapo mdogo mdogo.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) lilisema mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Simba SC na Yanga SC iliyokuwa ianze saa 11 jioni sasa itaanza saa 1 usiku.

TFF ilisema imepokea maelekezo ya mabadiliko ya muda wa kuanza mchezo kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Mchezo huo marudiano wa msimu baada ya miamba hiyo kutoka sare ya 1-1 kwenye mechi ya kwanza Novemba 7, mwaka jana utaonyeshwa moja kwa moja na chaneli ya AzamSports1HD ya Azam TV.

Mechi ya kwanza hapo hapo Benjamin Mkapa, Yanga SC walitangulia kwa bao la penalti la mshambuliaji Mghana, Michael Sarpong kipindi cha kwanza, kabla ya beki Mkenya, Joash Onyango kuisawazishia Simba mwishoni kipindi cha pili.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger