Saturday, 1 May 2021

Serikali Yafunga mtambo wa kisasa JKCI wenye thamani ya shilingi bilioni 4.6


Serikali imefunga mtambo wa kisasa wenye thamani ya shilingi bilioni 4.6 wa uchunguzi na matibabu ya moyo (Catheterization Laboratory – Cathlab) uliounganishwa na mtambo wa  Carto 3 System 3D &  mapping electrophysiology System  ambao unauwezo wa kufanya uchunguzi na  kutibu hitilafu ya mfumo wa umeme  wa moyo.

Fedha za kununuliwa kwa mtambo huo ambao umefungwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) zilitolewa na Serikali mwanzoni mwa mwaka jana.

Akizungumza na waandishi wa habari jana  jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi alisema mtambo huo umeshaanza kutumika, licha ya kutibu mfumo wa  umeme wa moyo pia utafanya uchunguzi wa mishipa ya damu ya moyo, kuweka vifaa visaidizi vya moyo pamoja na kuzibua mishipa ya damu ya moyo iliyoziba.

“Tunaishukuru Serikali kwa kuiwezesha JKCI na kufunga mtambo huu wa kisasa   ambao unauwezo wa kufanya uchunguzi na  kutibu hitilafu ya mfumo wa umeme  wa moyo.Kufungwa kwa mashine hii yenye teknlologia ya hali ya juu kutaweza kuokoa maisha ya watu wengi wenye matatizo ya moyo ikiwemo mfumo wa umeme wa moyo hapa nchini ”,.

“Tuna wagonjwa wengi ambao mfumo wa umeme wa moyo umekuwa haufanyi kazi vizuri hii ikiwa ni pamoja na  hitilamu ya mfumo wa umeme wa moyo ambao mapigo yake ya  moyo yanakwenda haraka kuliko kawaida  ambao tulikuwa tunawasafirisha kwenda nje ya nchi kwa ajili ya kutibiwa huku wengine wachache wakipatiwa matibabu hapahapa nchini”, alisema Prof. Janabi.

Prof. Janabi alisema  mtu akiwa na tatizo katika mfumo wa umeme wa moyo ambalo anaweza kulipata kwa kuzaliwa nalo au athali ya ugonjwa linapelekea mfumo wa umeme wa moyo kubadili mapigo yake inaweza kuwa chini ya 60 kwa dakika  na hivyo kusababisha mapigo kuwa chini sana au kuwa juu ya 100 kwa dakika  na hivyo kuufanya moyo udunde kwa haraka. Kwa kawaida mapigo ya moyo huwa ni 60 hadi 100 kwa dakika.

Mkurugenzi huyo Mtendaji ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya moyo alisema kupitia utaalam wanaoendelea kuupata kutoka kwa wenzao wa nchi za nje ambao wamewatangulia  katika matibabu ya moyo pamoja na kusimikwa kwa mtambo huo wataweza kuwatibu wagonjwa hao hapa nchini  

“Kwa upande wa wataalamu tunao wa kutosha kwani kuna ambao tumewasomesha nchini China na Afrika ya Kusini pia kupitia kambi mbalimbali za matibabu ya moyo ambazo tunazifanya kwa kushirikiana na wenzetu  wa nje ya nchi ambao wanautaalamu mkubwa zaidi yetu kutatusaidia kupata utaalamu wa kutosha na wa kisasa”, alisema Prof. Janabi.

Kwa upande wake Hassan Ally kutoka kampuni ya Biosense webser ambao ndiyo wafungaji wa mtambo huo alisema katika nchi za Afrika ya Mashariki mtambo huo ni wa pili kufungwa hapa nchini ambapo mtambo wa kwanza ulifungwa katika Hospitali ya Aga Khan iliyopo Mombasa nchini Kenya.

Alisema mtambo huo una teknolojia mpya na ya kisasa ambayo hivi sasa inafanyika katika matibabu ya moyo Duniani na kuzitaja nchi zingine ambazo zimefunga mtambo huo katika bara la Afrika kuwa ni pamoja na  Afrika ya Kusini na Misri.

“Tumeshatoa na tutaendelea kutoa mafunzo kwa  wataalamu wa Taasisi hii ili wajue jinsi ya kuutumia mtambo huu na tutaendelea  kutoa mafunzo hayo kwa nchi zote za Afrika ambazo zimefunga mtambo huu wa kisasa ambao unateknolojia  mpya hapa Duniani”, alisema Ally .

Naye daktari mwanamke pekee hapa nchini ambaye ni mtaalamu mbobezi wa moyo na mzibuaji wa mishipa ya damu ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Honoratha Maucky alisema kufungwa kwa mtambo huo kutawasaidia kutoa huduma nyingi zaidi kwa wagonjwa na kuweza kuokoa maisha yao.

Dkt. Maucky alisema tatizo la mfumo wa umeme wa moyo ni moja ya magonjwa wanayokutana  nayo kila siku hivyo basi kuwepo kwa mtambo huo kutawasaidia kutoa huduma kwa wakati kwa wagonjwa wenye matatizo hayo.

“Teknolojia ya matibabu ya moyo inakuwa kila siku kama mnavyoona tumefungiwa mtambo ambao unateknolojia mpya na ya kisasa  hivyo basi ni muhimu kwa daktari kutenga muda wako ili uweze kujifunza kwa njia ya mtandao au kupitia kwa wenzetu ambao wameendelea kimatibabu kuliko sisi kwa kufanya hivyo hautakuwa nyuma ya teknolojia ya matibabu”, alisisitiza Dkt. Maucky.


Share:

Rais Samia atakuwa Mgeni Rasmi Mei Mosi leo Jijini Mwanza.



Share:

Katibu Mkuu CCM Daniel Chongolo aanza kazi, aongoza kikao cha utambulisho kwa Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM

 Katibu Mkuu mpya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo, jana jioni ameripoti ofisini na kuendesha kikao maalum cha utambulisho kwa Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa katika ofisi za makao makuu ya chama hicho jijini Dodoma.

Kikao hiko kimehudhuriwa na Wajumbe wapya akiwemo Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), -Christina Mndeme na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka.

Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Viongozi wastaafu wa CCM wakiongozwa na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), – Rodrick Mpogolo na aliyekuwa Katibu wa NEC, Oganaizesheni Pereira Silima.

Chongolo amechaguliwa na Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kuwa Katibu Mkuu mpya wa chama hicho, kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Bashiru Ally.

Kabla ya kuchaguliwa kushika wadhifa huo, Chongolo alikuwa mkuu wa wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es salaam.



Share:

RAIS SAMIA MGENI RASMI MEI MOSI ASUBUHI HII MWANZA..KULIHUTUBIA TAIFA


Rais Samia Suluhu Hassan
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI MEI 1,2021























Share:

Friday, 30 April 2021

Tazama Picha : MKUTANO MKUU MAALUMU WA CCM ...WAJUMBE WAMCHAGUA RAIS SAMIA KUWA MWENYEKITI WA CCM



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa ameshikilia Tuzo yake ya Heshima na Pongezi aliyopewa na Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi Tanzania (UWT) mara baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti Mpya wa CCM leo tarehe 30 Aprili, 2021 katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre Jijini Dodoma. PICHA NA IKULU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akipokea Tuzo ya Heshima kutoka kwa Mwenyekiti wa UWT Gaudensia Kabaka mara baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CCM leo tarehe 30 Aprili, 2021 katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre Jijini Dodoma.



Viongozi mbalimbali pamoja na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi wakifurahia ndani ya Ukumbi wa Mkutano wa Jakaya Kikwete Convention Centre mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CCM leo tarehe 30 Aprili, 2021 Jijini Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Mzee Ali Hassan Mwinyi pamoja na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mara baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CCM baada ya kupigiwa kura zote za Ndiyo na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM uliofanyika leo tarehe 30 Aprili, 2021 katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre Jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Samia Suluhu Hassan akiagana na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mara baada ya Mkutano Mkuu wa CCM uliofanyika leo tarehe 30 Aprili, 2021 katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre Jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Samia Suluhu Hassan akiwa katika Mkutano Mkuu wa CCM ambao Wajumbe wake Walimchagua kwa Kura zote za Ndiyo kuwa Mwenyekiti Mpya wa CCM leo tarehe 30 Aprili, 2021 katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre Jijini Dodoma.

Share:

SIMBA SC KUCHAPANA NA KAIZER CHIEFS YA AFRIKA KUSINI ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA AFRIKA


Timu ya Simba SC ya Tanzania itakutana na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini katika Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya droo iliyopangwa leo Jijini Cairo nchini Misri.

Mabingwa watetezi, Al Ahly ya Misri nao watamenyana na wapinzani kutoka Afrika Kusini, Mamelodi Sundowns.

Mshambuliaji Mtanzania, Simon Happygod Msuva yeye timu yake, Wydad Casablanca itamenyana na MC Alger ya Algeria. CR Belouizdad ya Algeria pia yenyewe itamenyana na vigogo wengine wa Afrika, Esperance ya Tunisia.

Mechi za kwanza zitachezwa kati ya Mei 14 na 15 na marudiano ni Mei 21 na 22, Simba SC wakianzia nyumbani Dar es Salaam.

ROBO FAINALI
Al Ahly vs Mamelodi Sundowns.
MC Alger vs Wydad Casablanca.
CR Belouizdad vs Esperance.
Kaizer Chiefs vs Simba SC.

NUSU FAINALI
MC Alger / Wydad Casablanca VS Kaizer Chiefs / Simba SC.
CR Belouizdad / Esperance VS Al Ahly / Mamelod Sundowns.
Share:

MWADUI FC YATINGA ROBO FAINALI KOMBE LA TFF BAADA YA KUICHARAZA COASTAL UNION 2-0


TIMU ya Mwadui FC imefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Coastal Union ya Tanga jioni ya leo Uwanja wa Mwadui Complex, Kishapu mkoani Shinyanga.

Mabao ya Mwadui FC yamefungwa na Roshwa Rashid dakika ya 14 na Wallace Kiango dakika ya 24.
Mwadui FC inakamilisha orodha ya timu tatu tupu za mikoa inayopakana kufuzu Robo Fainali hadi sasa, nyingine ni Biashara United ya Mara na Rhino Rangers ya Tabora.

Mchezo kati ta wenyeji, Tanzania Prisons na Yanga SC unafuatia hivi sasa Uwanja wa Mandela, Sumbawanga mkoani Rukwa.
 Via Binzubeiry
Share:

VIGOGO YANGA WATINGA ROBO FAINALI KOMBE LA TFF BAADA YA KUITWANGA TANZANIA PRISONS 1-0


Vigogo,Yanga SC wamefanikiwa kwenda Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Tanzania Prisons Uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga mkoani Rukwa.

Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, mshambuliaji Mburkinabe Yacouba Sogne dakika ya 54 akimalizia pasi ya kiungo Mrundi, Said Ntibanzokiza.

Yanga inaungana na Rhino Rangers ya Tabora, Biashara United ya Mara, Mwadui FC ya Shinyanga na Azam FC ya Dar es Salaam pia kuwa timu zilizotinga Nane Bora hadi sasa.

Michuano hiyo itaendelea kesho kwa mechi kati ya Dodoma Jiji FC na KMC Uwanja wa Jamhuri, Dodoma na Simba SC na Kagera Sugar Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam wakati keshokutwa JKT Tanzania watamenyana na Namungo FC Uwanja wa Jamhuri, Dodoma kukamilisha Hatua ya 16 Bora.

 Chanzo - Binzubeiry blog

Share:

MANISPAA YA SHINYANGA KUANZISHA MASHINDANO YA USAFI WA MAZINGIRA

 

Mkuu wa idara ya Usafi na Mazingira Manispaa ya Shinyanga Kuchibanda Snatus, akisoma taarifa ya mpango wa kuanzisha mashindano ya usafi wa mazingira kwenye Baraza la Madiwani kwa niaba ya Mkurugenzi. Picha zote na Marco Maduhu
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi akizungumza kwenye Baraza la Madiwani.
Meya wa Manispaa ya Shinyanga David Nkulila, akizungumza kwenye Baraza la Madiwani.

***
Na Marco Maduhu, Shinyanga.
Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, inatarajia kuanzisha mashindano ya usafi wa mazingira, kwa ajili ya kuuweka mji huo katika hali ya usafi, pamoja na kupambana na magonjwa yatokanayo na uchafu kikiwemo kipindupindu.

Akisoma taarifa ya mpango huo leo wa kuanzisha mashindano ya usafi wa mazingira, kwenye kikao cha Baraza la Madiwani Manispaa ya Shinyanga, Mkuu wa Idara ya Usafi na Mazingira Manispaa hiyo Kuchibanda Snatus, kwa niaba ya Mkurugenzi, alisema lengo la mashindano hayo ni kuhakikisha mji unakuwa safi muda wote.

Alisema mashindano hayo yatajumuisha kata zote 17 za Manispaa ya Shinyanga, Mitaa 55, vijiji 17, Taasisi zote za umma, na binafsi, zikiwamo Shule za Msingi na Sekondari, Masoko, viwanda, ambayo yanatarajiwa kuanza mwezi Julai mwaka huu.

“Maeneo yatakayokaguliwa kwenye mashindano hayo ni usafi wa Kaya, Shule, Masoko, Mitaro, Barabara, Viwanda, na Maeneo ya wazi na utekelezaji utasimamiwa na viongozi wa Serikali za vijiji, mitaa na Kata, kwa kufanya ukaguzi wa usafi wa mazingira kwenye maeneo yote,”alisema Snatus.

“Mshindi wa mashindano haya ngazi ya Kaya na Shule atapewa zawadi ya vifaa vya usafi, Kiwanda na Kata itakayo ongoza watapewa Ngao, Mtaa utapewa Cheti, na watakaofanya vibaya watapewa Kinyago,”aliongeza.

Aidha alisema faida za mashindano hayo ni kuboresha hali ya usafi wa mazingira kwenye maeneo mbalimbali ya Manispaa, kupunguza madharia ya Mbu, pamoja na kutokomeza magonjwa ya kuhara na kipindupindu.

Naye Meya wa Manispaa ya Shinyanga David Nkulila, alisema mpango huo ni mzuri na utasaidia kuondoa kero za uchafu mjini Shinyanga, ambapo mji utakuwa msafi pamoja na kuzolewa uchafu wa kwenye Maghuba kwa wakati, huku akitoa wito kwa madiwani wakatoe elimu ya usafi kwa wananchi.

Nao Madiwani wa Manispaa hiyo ya Shinyanga, walipongeza mpango huo wa mashindano ya usafi wa mazingira kuwa utaleta hamasa kubwa ya kuufanya mji huo kuwa msafi huku kila mmoja akijingamba kupata ushindi.

Pia Baraza hilo la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, limefanya kikao cha siku mbili kujadili ajenda mbalimbali, kwa ajili ya mstakabali wa maendeleo ya Manispaa hiyo.

Madiwani wakiwa kwenye kikao cha Baraza.
Madiwani wakiwa kwenye kikao cha Baraza.
Madiwani wakiwa kwenye kikao cha Baraza.
Madiwani wakiwa kwenye kikao cha Baraza
Madiwani wakiwa kwenye kikao cha Baraza
Madiwani wakiwa kwenye kikao cha Baraza

Na Marco Maduhu- Shinyanga.
Share:

VIJANA WA JKT WALIORUDISHWA NYUMBANI WATAKIWA KUREJEA KAMBINI MEI 7 - 14 , 2021

Kaimu Mkuu wa Tawi la Utawala Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kanali Hassan Mabena akitoa taarifa ya kurejeshwa kwa vijana wa kujitolea katika mafunzo ya JKT kuanzia Mei 7 hadi 14, 2021 baada ya kuwarejesha nyumbani hapo awali.
***
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limewataka vijana waliochaguliwa kujiunga na mafunzo ya kujitolea kuripoti katika makambi waliyopangiwa kati ya Mei 7 hadi 14, 2021 lakini utaratibu huo hautawahusu wenye elimu ya kidato cha sita, cheti, stashahada, shahada na taaluma ya uhandisi.

Kaimu mkuu wa utawala wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kanali Hassan Mabena, amewaambia wanahabari kuwa vijana hao wanatakiwa kuripoti kwenye makambi waliyopangiwa awali.
Kaimu Mkuu wa Tawi la Utawala (JKT), Kanali Hassan Mabena amesema, vijana hao wanatakiwa kuripoti katika kambi walizokuwa wamepangiwa awali kuanzia Mei 7 hadi Mei 14,2021.

“Vijana waliorejeshwa ni wale wenye elimu ya darasa la saba na kidato cha nne, wenye elimu ya kidato cha sita, ngazi ya cheti, stashahada, shahada na wale wenye Taaluma ya Uhandisi wataendelea kusubiri majumbani hadi hapo utaratibu mwingine utakapotangazwa"', amesema Kanali Mabena

Jeshi la Kujenga Taifa ( JKT) limekuwa likiendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo vijana kwa kuwapa stadi za maisha ikiwa ni pamoja na uzalishaji mali, uzalendo, kilimo, ufugaji na kushiriki katika ujenzi wa Taifa.

Mwezi Februari mwaka huu, Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) alitangaza kuwarejesha nyumbani zaidi ya vijana 12,000 hadi ambapo wangetangaziwa tena.
Share:

DANIEL CHONGOLO KATIBU MKUU WA CCM, SHAKA ACHUKUA NAFASI YA HUMPHREY POLEPOLE


Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimefanya mabadiliko ya viongozi wake wakuu kitaifa ikiwemo nafasi ya Katibu Mkuu iliyokuwa inashikiliwa na Bashiru Ally pamoja na nafasi ya Katibu wa Itikadi na Uenezi iliyokuwa inashikiliwa na Hamphrey Polepole.

Katika Mabadiliko hayo, CCM imempitisha Daniel Chongolo kuwa Katibu Mkuu Mpya wa chama hicho, huku nafasi ya Katibu wa Itikadi na Uenezi ikichukuliwa na Shaka Hamdu Shaka.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger