Thursday, 1 April 2021

DC MBONEKO APONGEZA WANANCHI NYALIGONGO KUANZISHA UJENZI ZAHANATI


Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nyaligongo Kata ya Mwakitolyo wilayani Shinyanga, na kuwapongeza kuanzisha ujenzi wa Zahanati.

Na Marco Maduhu, Shinyanga.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, amewapongeza wananchi wa kijiji cha Nyaligongo Kata ya Mwakitolyo wilayani Shinyanga, ambao wanajishughulisha na uchimbaji wa madini ya dhahabu, kwa kujitolea kuanza ujenzi wa Zahanati, ambayo itawaondolea adha ya kufuata matibabu umbali mrefu.

Mboneko ametoa pongezi hizo leo, alipofanya ziara ya kutembelea ujenzi huo wa Zahanati, akiwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Hoja Mahiba, na baadhi ya maofisa wa Polisi, ambapo Serikali ili ahidi kuwa unga mkono ili kukamilisha Zahanati hiyo.

Amesema ni jambo la pongezi kwa wananchi kujitoa wenyewe kuchangia shughuli za maendeleo, ili kutatua baadhi ya changamoto ambazo zinawakabili kuliko kuitegemea Serikali kwa kila kitu, ambapo Zahanati hiyo itakapokamilika, mbali na kuwaondolea adha ya kufuata matibabu umbali mrefu, pia watapunguza vifo vitokavyo na uzazi.

“Nawapongeza sana wananchi wa Nyaligongo kwa ujenzi huu wa Zahanati ambayo itawasaidia kupata huduma za matibabu karibu na kuimarisha afya zenu, ikiwamo kupunguza vifo vya uzaziwa wakati wa kujifungua, na mama akiwa na afya nzuri na nyumbani pana kuwa safi,”amesema Mboneko.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Hoja Mahiba, amewapongeza wananchi hao kwa kuanzisha ujenzi huo wa Zahanati, na kubainisha kuwa Sera ya afya inasema kuwepo na Zahanati kwa kila kijiji, ambapo miradi hiyo inafaa kuanza kuibuliwa na wananchi wenyewe na kisha Serikali inawaunga mkono kuikamilisha.

Mwenyekiti wa kijiji cha Nyaligongo Masumbuko Lushona, amesema walifanya mkutano wa hadhara na wananchi na kuhamasishana kuchanga pesa ili kuanza ujenzi wa Zahanati kwenye kijiji hicho, kutokana na kuteseka kufuata huduma ya afya umbari mrefu.

Kwa upande wake Mtendaji wa Kata ya Mwakitolyo Samson Lutonja, amesema ujenzi huo wa Zahanati upo kwenye hatua ya Msingi, ambapo unatarajiwa kukamilika mwaka huu kwa gharama ya Sh. Milioni 90.

Nao baadhi ya akina mama Mary Benjamini, wamesema ujenzi wa Zahanati hiyo utakuwa msaada kwao, na kueleze kuwa huduma ya matibabu inapokuwa mbali wanaoteseka hua ni wanawake pamoja na watoto.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nyaligongo Kata ya Mwakitolyo wilayani Shinyanga, na kuwapongeza kuanzisha ujenzi wa Zahanati.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Hoja Mahiba, akizungumza kwenye ujenzi wa Zahanati ya kijiji cha Nyaligongo ambayo imeanzishwa kujengwa na wanachi wenyewe.
Diwani wa Kata ya Mwakitolyo Masalu Nyese, akizungumzia ujenzi huo wa Zahanati namna walivyo hamasishana na Wananchi kuanza kuijenga.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Mwakitolyo Samson Lutonja, akizungumzia ujenzi huo wa Zahanati ya kijiji cha Nyaligongo.
Mary Benjamin mkazi wa kijiji cha Nyaligongo, akielezea umuhimu wa Zahanati hiyo kwenye kijiji hicho.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akikagua ujenzi wa Zahanati ya kijiji cha Nyaligongo.
ukaguzi wa ujenzi wa Zahanati hatua ya Msingi ukiendelea.
Muonekano wa Msingi ujenzi wa Zahanati kijiji cha Nyaligongo.

Picha na Marco Maduhu- Shinyanga.

Share:

Tazama Picha : KATIBU MKUU KIONGOZI, MAWAZIRI NA MANAIBU MAWAZIRI WAKILA KIAPO LEO IKULU


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimuapisha Balozi Hussein Othman Katanga kuwa Katibu Mkuu Kiongozi (CS) katika hafla iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 01 Aprili 2021. Picha na Ikulu
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Hussein Othman Katanga akila Kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi wa Umma Ikulu ya Chamwino.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimuapisha Ummy Ally Mwalimu kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI katika hafla iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 01 Aprili 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimuapisha Profesa Palamagamba Aidan Mwaluko Kabudi kuwa Waziri wa Katiba na Sheria katika hafla iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 01 Aprili 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimuapisha Selemani Saidi Jafo kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mwigulu Lameck Nchemba Madelu kuwa Waziri wa Fedha na Mipango katika hafla iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 01 Aprili 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimuapisha Profesa Kitila Alexander Mkumbo kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara katika hafla iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 01 Aprili 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimuapisha Geoffrey Idelphonce Mwambe kuwa Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu(Uwekezaji)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimuapisha Balozi Liberata Rutageruka Mulamula kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimuapisha William Tate Ole Nasha kuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimuapisha Abdallah Hamis Ulega kuwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi katika hafla iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 01 Aprili 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mwita Mwikwabe Waitara kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimuapisha Pauline Philipo Gekul kuwa Naibu Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mwanaidi Ally Hamis kuwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimuapisha Hamad Yussuf Masauni kuwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimuapisha Hamad Hassan Chande kuwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira katika hafla iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 01 Aprili 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mbarouk Nassoro Mbarouk kuwa Naibu Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Mawaziri pamoja na Manaibu Mawaziri wakila Kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi wa Umma Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali mara baada ya kuwaapisha Viongozi hao aliowateuwa katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu, Chamwino mkoani Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali mara baada ya kuwaapisha Viongozi hao aliowateuwa katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu, Chamwino mkoani Dodoma


PICHA NA IKULU


Share:

DC MBONEKO ARIDHISHWA KASI UJENZI KITUO CHA POLISI MACHIMBO YA DHAHABU MWAKITOLYO


Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko, akikagua ujenzi wa kituo cha Polisi kwenye machimbo ya madini ya dhahabu Mwakitolyo.

Na Marco Maduhu, Shinyanga.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, ameeleza kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa kituo cha Polisi kilichopo kwenye machimbo ya dhahabu Mwakitolyo wilayani Shinyanga, ambacho kitasaidia kuimarisha ulinzi na usalama.

Mboneko amebainisha hayo leo, alipofanya ziara kwenye machimbo hayo kukagua ujenzi wa kituo cha Polisi, ambacho kimejengwa kwa nguvu za umoja wa wachenjuaji wa madini ya dhahabu wa Mwakitolyo (UWADHAMWA) kwa kuchangishana pesa, kwa lengo la kuimarisha ulinzi na usalama kwenye eneo hilo.

Amesema anapongeza sana umoja huo wa wachenjuaji wa madini ya dhahabu kwa kuitikia agizo lake na kuamua kuanza ujenzi wa kituo cha Polisi kwenye machimbo hayo, ambacho ni muhimu sana kutokana na shughuli zao za uchimbaji wa madini, kwa kuwahakikishia amani inatawala kwenye maeneo hayo na hakuna uvunjifu wa amani tena.

“Kituo hiki cha Polisi kwenye maeneo hayo ya uchimbaji wa madini ya dhahabu, kitakuwa msaada mkubwa pamoja na wananchi kuwahakikishia ulinzi na usalama, ambapo zamani likitokea tukio la uharifu kupata huduma hadi salawe au Shinyanga mjini zaidi ya kilometa 100, lakini kwa sasa huduma mtaipata hapa hapa,”amesema Mboneko.

“Kutokana na kunifurahisha hatua hii mliyofikia ya ujenzi wa kituo hiki cha Polisi, na mimi nilitafuta wadau ili kuwaunga mkono kukamilisha ujenzi huu, ambapo nilipata wadau kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), na wamenipatia Sh. Milioni 10, na nimeshaikabidhi kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga,” ameongeza.

Aidha amesema kukamilika pia kwa ujenzi huo wa kituo cha Polisi, kutatoa fursa kwa wafanyabishara na wawekezaji kuwekeza kwenye mgodi huo wa Mwakitolyo, pamoja na Taasisi za kifedha kusogeza huduma kwenye maeneo hayo, wakiwamo TRA kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato.

Naye Mkuu wa Polisi Wilaya ya Shinyanga John Kafumu, amesema kituo hicho cha Polisi kitasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza matukio ya uharifu kwenye maeneo hayo yakiwamo ukatwaji wa mapanga, sababu Askari Polisi watakuwa doria masaa 24 ili kuhakikisha amani inatawala.

Aidha Mwenyekiti wa wachimbaji wa madini ya dhahabu Mwakitolyo Aphonce Paulo, amesema walikuwa na hamu sana ya kupatiwa kituo cha Polisi kwenye maeneo hayo kutokana na usalama kuwa hafifu, na ndio maana wakahamasishana kuanzisha ujenzi wa kituo hicho ili wawe salama na mali zao.

Kwa upande wake katibu msaidizi wa umoja wa wachenjuaji wa madini ya dhahabu Mwakitolyo Elisha Rugwisha, akisoma taarifa ya ujenzi huo wa kituo cha Polisi amesema ulianza Februari mwaka huu, na sasa upo katika hatua ya Renta, na unatarajiwa kukamilika mwezi huu kwa zaidi ya gharama ya Sh. Milioni 30.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza mara baada ya kumaliza kukagua ujenzi wa kituo cha Polisi kwenye machimbo ya madini ya dhahabu Mwakitolyo wilayani Shinyanga.
Mkuu wa Polisi Wilaya ya Shinyanga John Kafumu, akizungumza mara baada ya kumaliza ukaguzi ujenzi wa kituo cha Polisi Mwakitolyo wilayani Shinyanga.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Hoja Mahiba, akizungumza kwenye ukaguzi huo wa ujenzi wa kituo cha Polisi katika Machimbo ya dhahabu Mwakitolyo wilayani Shinyanga.
Afisa kutoka TRA Simon Mshofe, akizungumza kwa niaba ya Meneja wa TRA mkoani Shinyanga namna walivyoguswa na ujenzi wa kituo cha Polisi kwenye Machimbo hayo ya dhahabu Mwakitolyo, na kuamua kuunga mkono kwa kutoa Sh. Milioni 10.
Mwenyekiti wa wachimbaji wa madini ya dhahabu Mwakitolyo Aphonce Paulo, akizungumza namna waivyohamasika na kuanza ujenzi huo wa kituo cha Polisi.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, (katikati) mwenye viatu vya kaki, akikagua ujenzi wa kituo cha Polisi Mwakitolyo.
Ukaguzi ujenzi kituo cha Polisi Mwakitolyo ukiendelea.
Ukaguzi ujenzi kituo cha Polisi Mwakitolyo ukiendelea.
Ukaguzi ujenzi kituo cha Polisi Mwakitolyo ukiendelea.
Ukaguzi ujenzi kituo cha Polisi Mwakitolyo ukiendelea.
Muonekano ujenzi kituo cha Polisi Mwakitolyo.
Picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kukagua ujenzi kituo cha Polisi Mwakitolyo.

Na Marco Maduhu- Shinyanga.
Share:

RAIS SAMIA : NAFAHAMU MWAKA 2025 NI KARIBU...MWENYE HILI NA LILE AACHE MARA MOJA... TWENDENI TUKAFANYE KAZI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali mara baada ya kuwaapisha Viongozi hao aliowateuwa katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu, Chamwino mkoani Dodoma
**
Na Charles James, Michuzi TV

ACHENI hili na lile! Ni kauli ya Rais Mama Samia Suluhu Hassan kwa wanasiasa na viongozi wenye ndoto na uchaguzi wa mwaka 2025 kuacha fikra hizo na badala yake wajielekeze katika utendaji kazi wao na kuwatumikia watanzania.

Kauli hiyo ameitoa Ikulu Chamwino, Dodoma leo alipokuwa akimuapisha Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Hussein Katanga na Mawaziri Manaibu wapatao nane ambao aliwateua jana.

Rais Mama Samia amesema anafahamu ni desturi kwa nchi yetu na hata nchi nyingine Rais akiwa kwenye kipindi chake cha pili kunakua na hili na lile kwa baadhi ya viongozi hivyo amewaonya kuacha fikra hizo.

"Nafahamu mwaka 2025 ni karibu na mpo ambao mna hili na lile, niwaambie acheni twendeni tukafanye kazi, nawaambia kila mwenye hili na lile kwa mwaka 2025 aache mara moja," Amesema Rais Mama Samia.

Mama Samia amesema katika kufanya mabadiliko katika Wizara hizo amemteua mtu mtaalamu kwenye sekta anayoimudu lengo likiwa ni kwenda kuongeza ufanisi kwenye wizara na kuharakisha maendeleo.

" Kwa Mawaziri mlioapa leo nimechukua wale mabingwa wa sekta nikaona niwarudishe kwenye sekta zao, mfano Prof Palamagamba ni Bingwa wa Sheria nimemrudisha Wizara ya Sheria, Dk Mwigulu ananukianukia Fedha hivyo nimempeleka Wizara ya Fedha na Mipango na hapo umeambiwa na Makamu wa Rais kuwa tufikie lengo la Sh Trilioni 2 kweli tufikie lengo la mapato hayo kwa mwezi.

Sehemu tuliyopata shida na wenzangu wakati wa kuchagua ni kwenye Wizara ya Mambo ya Nje lakini tukatua kwa Balozi Liberata huyu amekua wizara hii anajua vichochoro vyote naamini atatusaidia kunyoosha mahusiano yetu kimataifa," Amesema Rais Samia.

Amesema anafahamu Pauline Gekul aliyekua Naibu Waziri wa Mifugo anaifahamu Mifugo vizuri ila ameona Ampeleke Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo ili akainue michezo.

" Gekul najua unafahamu Mifugo vizuri lakini nimekupeleka Michezo ukainue michezo kwa Wanawake maana Wanawake tunafanya vizuri sana ila hatusifiwi, wanaume wakifunga goli moja tu hata hawajafika nusu fainali na viwanja wanapewa, nenda kasimamie vizuri," Amesema Rais Samia.

Amewakumbusha mawaziri wote kuwa serikali ni moja wafanye kazi kwa ushirikiano na hatosita kumuondoa yeyote ambaye atainua mabega yake akiwataka kwenda kwa watanzania kutatua changamoto zao.

Mama Samia amesema upo uwezekano kuwaapisha viongozi wengine Jumanne wiki ijayo baada ya sikukuu ya Pasaka kumalizika.

Chanzo - Michuzi blog


Share:

RAIS SAMIA : TUMIENI AKILI NA MAARIFA KUKUSANYA KODI SIO NGUVU, MNAUA BIASHARA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali mara baada ya kuwaapisha Viongozi hao aliowateuwa katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu, Chamwino mkoani Dodoma
**
Na Said Mwishehe,Michuzi TV

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametoa maelekezo kwa Wizara ya Fedha kuhakikisha inaongeza makusanyo hadi kufikia Sh.Trilioni mbili kwa mwezi lakini ukusanyaji huo utumie akili na maarifa badala ya nguvu na kusababisha biashara kufungwa.

Amesema nguvu kubwa ambazo zinatumika kukusanya mapato ya Serikali zimekuwa zikisababisha wafanyabiashara kufunga biashara zao na kwenda kuzifungua katika nchi nyingine,hivyo Serikali inakosa mapato.

Amesema hayo leo Aprili 1, 2021 Ikulu Chamwino Mjini Dodoma baada ya kuapishwa kwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Hussein Katanga pamoja na mawaziri walioteuliwa jana ambao nao wameapa leo.

Rais Samia, amesema kwamba Makamu wa Rais wakati anazungumzia amesisitiza Serikali kuongeza ukusanyaji mapato kwa mwezi kufikia Sh.Trilioni mbili ambapo amesema hilo linawezekana lakini ametoa angalizo kwamba akili na maarifa ndio inatakiwa kutumika kuongeza ukusanyaji huo wa mapato ya Serikali.

Amemsisitiza Waziri wa Fedha Dk.Mwigulu Nchemba lazima wasimamie ukusanyaji mapato vizuri, hakuna sababu ya kutumia nguvu katika kukusanya kodi."Nguvu kubwa sana inatumika na badala ya kusaidia wafanyabiashara mnasababisha wafunge biashara zao na sio kufunga tu biashara za watu kwasababu sheria inaruhusu,hapana .tumieni weledi na maarifa katika ukusanyaji wa kodi."

Akimzumngumzia Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Hussein Katanga, Rais Samia amesema amemsikiliza wakati anazungumza na bahati nzuri amezungumzia kutokuwepo kwa mfumo wa ufanyaji kazi serikalini na huo ndio ugonjwa mkubwa."Katibu Mkuu Kiongozi najua wewe ndio daktari ambaye unakwenda kutibu huu ugonjwa, lazima Serikali ifanye kazi kwa pamoja."

Wakati huo amesema kwamba katika mazungumzo yake amekuwa akitaja Bunge la Katiba huenda ni kwasababu amepushiwa( msukumo) lakini ameweka wazi hilo la Katiba Mpya kwa sasa wasahau kwanza.

 Chanzo - Michuzi Blog
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger